Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Update: Yaliojiri Jana-Risasi za Moto na Mabomu ya Machozi

with 10 comments

Update:

Ganda la risasi ya moto limeokotwa ndani ya ofisi ya CHADEMA nilimokuwamo wakati polisi wanapiga mabomu. polisi walitumia risasi za moto!naenda polisi sasa hivi. uchunguzi wa kina unatakiwa

Mdogo wangu Bashiri ndiye aliyenikinga na bomu na hivyo yeye kujeruhiwa. alinivamia alipoona wamenilenga mimi na kurusha mabomu kule nilipo mie.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Written by zittokabwe

November 3, 2010 at 12:15 PM

10 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. Hawa jamaa mwisho wao unakaribia!

    Roger

    November 3, 2010 at 2:04 PM

  2. This is not fair at all. Nadhani Mh. Zitto sioni jinsi utakavyopata haki yako kwa kwenda Polisi walio piga hizo risasi na mabomu. Naomba uchukue njia mbadala yenye tija baada ya kujadiliana na Wanasheria. Polisi hawatatenda haki. Watapenda kuficha mambo. Upande wa pili ni kuweka hii kitu kama kumbukumbu ili 2015 tuwafikishe The Hegue wakajibu tuhuma zao!!!

    Eng. Magafu,F.F

    November 4, 2010 at 3:25 AM

  3. Mh zito pole sana.mungu ndiye mkuu wa yote.ubabe wa serikali za kafrika huwa una mwisho.nimekuwa najiuliza,kama mtu ataki kushindwa uchaguzi anaitisha wa nini?raslimali za nchi zinapotea kwa ajiri ya mtu kubaki madarakani.lengo letu mwaka 2010-05 iwe ni civic education kwa wananchi hasa vijijini,kudai tume huru ya uchaguzi.ya kivuitu naona yananukia tz na mwisho uwepo mpango mahususi wa kuunganisha vyama vya upinzani ingawa kuna vyama vibaraka.songa mbele na mabadiriko yanakuja.tuko pamoja

    Mwombeki

    November 4, 2010 at 11:03 AM

  4. Ndugu Zitto

    Poleni na hekaheka zilizowapata huko Kigoma. Uliyoeleza na vielelezo hivyo hapo juu ni dalili tosha ya kubadilika kwa mambo. Huu sasa si USHINDANI ni VITA. Hivi, huyo aliyefyatua risasi ya moto … lengo lake lilikuwa nini? Dhamira yake ilikuwa ipi? Je, alifyatua mwenyewe kwa utashi wake au alishinikizwa? Kama alishinikizwa, nani alimshinikiza? Je, kuna utaratibu gani – wa kisheria – unaomruhusu yeyote mwenye silaha ya moto kuitumia? Naona kuna maswali mengi sana yanayohitaji majibu. Na ili kutibu matatizo haya ambayo sasa yameanza kujitokeza, ni vema na haki kwamba tupate majibu sahihi kwa maswali haya na mengine mengi.

    Jamani … tudumishe amani Tanzania … tushindane kwa hoja na sera … tuache kutafuta kumwaga damu.

    kakasimba

    November 4, 2010 at 11:52 AM

  5. Hongera sana Zitto na pole sana kwa heka heka zote za mabomu,CCM ziku zao zinahesabika na ukweli umeshaonekana,hivyo basi kazi inayotakiwa ni kukaza buti kujiandaa na 2014 serikali za mitaa kuhakikisha kila mtaa na kila kijiji tanzania mnawafikia wananchi tayari kwa kuchukua nchi 2015.Wananchi walishachoka na CCM na sioni nani atakayekuwa mvuto kwa CCM mwaka 2015 zaidi ya hao mafisadi.
    Peooples power

    Dr.Mallaba

    November 5, 2010 at 8:26 PM

    • Zito au mtu yeyote tunaomba tujue uchaguzi wa raisi mmemaliza? and what is your stand at the moment.

      Ahasanteni wakuu
      yani wazee hii ni muhimu tunafuatiilia.

      Yasser Mziba

      November 6, 2010 at 4:23 AM

  6. Ebwana Zitto kwanza hongera kwa kushinda na pia hongera kwa upinzani wa kweli Kigoma maana kuchukua majimbo 5 kati ya 8 si mchezo. Haijalishi ni CHADEMA au NCCR upinzani ni muhimu na nawapa hongera zote.

    Ushauri wangu ndugu yangu hasa kwenu CHADEMA tafadhali, kama listi yenu ya wabunge wa kuteuliwa bado hamjai-submit hebu muwekeni Dr Slaa huko. Bunge bila huyu jamaa litapwaya mno. Maadamu wamemuibia kura za uraisi, mrudisheni bungeni. CCM wanataka waweke spika fisadi ili azuie mijadala muhimu bungeni kwaiyo inabidi muwe na wabunge makini mno safari hii.

    Jambo jingine naomba kama unafikiri CUF sio tawi la CCM, hebu ongeeni nao mtengeneze coalition nao. Kila mtu aendelee na itikadi na uongozi wake lakini muwe na coalition maana baada ya uchaguzi uliopita, ujao unakuja si muda mrefu. MWaka 2015 kuna nafasi kubwa ya kushinda.

    Pia hebu jaribuni kubadili katika safari hii. Nguvu ya raisi ni kubwa mno kiasi kwamba ufisadi haukwepeki. UNapoona mke wa raisi na watoto wake wanakuwa na nguvu kama raisi ujue hali ni mbaya. Nguvu ya nchi inatakiwa iwe bungeni sio ikulu jamani. Wakuu wa vitengo muhimu kama usalama wa taifa inatakiwa wafanyiwe vetting na bunge na kupitishwa au kuondolewa na bunge pia. Kila mfanyakazi wa serikali ikiwa ni pamoja na mkuu wa usalama wa taifa anapaswa kuwa chini ya supervision ya bunge na aitwe anytime kujieleza kuhusu mwenendo wa idara.

    Mwisho hebu pelekeni jimboni mada ya kuhoji utendaji wa NEC. Ni aibu na hasara kwa nchi yenye wapiga kura milioni ishirini kuwa na uchaguzi wenye watu chini ya milioni 9. Nchi nyingine uchaguzi ulitakiwa urudiwe kwa maana kwamba hata anaedaiwa kuwa mshindi, hajapata asilimia 50 ya wapiga kura. Alitakiwa apate at least kura milioni 10 ili awe mshindi lakini JK pamoja na kuchakachua, amepata kura milioni 5. Hii inaonyesha kuwa hakukuwa na mshindi wa jumla wa uchaguzi huu. Ila wanaotakiwa kuwajibika ni NEC na Kiravu aeleze kwanini hali imekuwa hivyo. BILA KLUBADILI KATIBA NCHI ITAZIDI KUDORORA. RUDESHENI NCHI KWA WANANCXHI JAMANI. ITOENI IKULU NA KWA MAFISADI.

    Abel

    November 6, 2010 at 3:10 PM

  7. Mzee Abel naona hapo umenifidisha. hata kabwe simuhitaji kwa sasa. sasa mkuu mimi nitaongea na mkigoma ambaye ni fundi kidogo wa politiki. kwa upande mungine ccm wameliwa hela na watu ikiwemo ccm elders wamewatosa. Kigoma wana Akili ya kidemokrasia. hakuna ukabila wala udini. Toka enzi za mkoloni ni watu wanaoamua kiukweli. Na huyu cufu kwanza ninani. @Abel yani kwa kweli umechambua. Naomba ruhusa nichangie barua yako na wengine maana hata NEC umeizungumzia. Anyway, lamuhimu ni amani Warundi wasitucheke! Wenyewe mbona wametulia zao kimya. sijasikia kokolo uko. Speaker wa Bunge ni mtu muhimu sana, tena shirikianeni.

    Yasser Mziba

    November 6, 2010 at 6:13 PM

  8. Bro, pole huu ni unyama wa wazi kabisa. Go to police but try to contact your lawyer i think there is something to to

    elvan stambuli

    November 7, 2010 at 3:31 PM


Leave a comment