Posts Tagged ‘PAC’
Tamko la Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe kuhusu Ripoti ya CAG mwaka 2013/2014
Tamko la Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe kuhusu Ripoti ya CAG mwaka 2013/2014
1) Taarifa nyingine ya CAG imetoka, kwa mujibu wa Katiba ya JMT na kwa mujibu wa sheria za nchi. Taarifa hii imechelewa kutolewa kulingana na mabadiliko ya Ratiba za Bunge ambapo hapo awali taarifa ilikuwa ikitoka mwezi Aprili na kuwezesha kuchangia katika mchakato wa Bajeti ya nchi. Taarifa ya mwaka huu na ile ya mwaka Jana imetoka wakati wa Bunge la Bajeti na hivyo Bajeti ya Serikali haijazingatia hoja za ukaguzi ili kuboresha mfumo wa matumizi ya fedha za umma. Ni vema utaratibu wa zamani wa ripoti kutolewa mwezi Aprili urejewe ili wabunge waweze kutumia ripoti hizo wakati wa kamati katika kujadili makadirio ya Bajeti za Wizara mbalimbali.
2) Taarifa kama miaka iliyopita bado sio nzuri. Mapato mengi ya Serikali bado yanapotea. Uk. 53 wa Taarifa unaonyesha kuwa mizigo inayoingizwa nchini kupita kwenda nchi jirani zinazotumia bandari zetu hubakia nchini na kuingizwa sokoni hivyo kukwepa kodi. Mwaka 2013/2014 mizigo ya transit iliyobaki nchini kiudanganyifu ilikuwa zaidi ya bidhaa 6000 kwa mujibu wa Taarifa ya CAG. Hivyo kodi ya tshs 836 bilioni haikulipwa kwa mizigo hiyo sawa sawa na 10% ya makusanyo yote ya kodi za ndani. Tshs 836 bilioni ilipotea mwaka 2013/14 peke yake. Wakati hili linatokea Serikali ipo ukata mkubwa na kushindwa kuendesha miradi yake mbalimbali. Fedha iliyokwepwa idara ya forodha peke yake inalipa Madeni yote ya wakandarasi wa barabara wanaoidai TANROADS na riba kulimbikizwa kila mwaka. Fedha hii ingelipa Madeni yote ya mfuko wa PSPF wanayoidai Serikali. Fedha hizi zingeweza kulipia miradi 2 mikubwa nchini ya BVR na vitambulisho vya Taifa ambayo inasuasua kutokana na ukata.
Natoa wito kwa CAG kwanza kuweka wazi orodha ya bidhaa hizo zilizobakia nchini na kuingizwa nchini bila kulipa kodi. Vile vile CAG aweke wazi wafanyabiashara wote walioagiza bidhaa hizi na vyombo vya kiuchunguzi vichukue hatua za kuwashtaki wafanya biashara hawa mara moja.
Natoa wito kwa Kamati ya Bunge ya PAC kuwaita mara moja maafisa wa TRA kujieleza mbele ya kamati kuhusu suala hili na kuandaa taarifa maalumu bungeni ili kuanika uoza huu unaopoteza mapato mengi sana ya Serikali.
3) CAG kaonyesha kuwa kuna ubadhirifu mkubwa sana kitengo cha maafa cha ofisi ya Waziri Mkuu ambapo tshs 163 billioni za chakula cha maafa hazikukusanywa katika kipindi cha miaka 5 iliyopita. Huu ni kama mrija wenye wastani wa tshs 32 bilioni kuchotwa kwa kisingizio cha chakula cha maafa kwa wananchi. Kwa malezo ya CAG ni kwamba Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wamekula fedha za chakula cha misaada. Maana hakuna uthibitisho wa kuwa mahindi yaliyogawanywa na taarifa kutolewa na Wakala wa Akiba ya Chakula (NFRA). Kitengo cha maafa ofisi ya PM kimekuwa mrija wa wizi wa fedha za umma, wizi ambao umekuwa ukifanyika bila ya kugunduliwa kwa miaka 5 sasa. ACT Wazalendo inaisihi Kamati ya Bunge ya PAC kufanya uchunguzi maalumu kwenye kashfa hii ya tshs 163 bilioni katika Ofisi ya Waziri Mkuu na Wakala wa Hifadhi ya Chakula ( NFRA).
4) ACT Wazalendo inalitaka Bunge kuchukua stahiki dhidi ya Wizara ya Ujenzi kufuatia ripoti ya CAG kuonyesha kuwa Wizara ilidanganya Bunge katika kupitisha Bajeti ya tshs 252 bilioni ambapo kati yake tshs 87 bilioni ziliibiwa au matumizi yake kutoeleweka.
5) ACT Wazalendo inampongeza CAG kwa kuendelea na zoezi la kisheria la kukagua mahesabu ya vyama vya siasa. Hii inaweka misingi ya uwajibikaji kuanzia kwenye vyama vya siasa, taasisi muhimu sana katika ujenzi wa demokrasia. Vyama vya siasa vichukulie ripoti ya CAG kama changamoto ya kutoa kwanza kibanzi kwenye macho yao ili kuwa na ‘ moral standing’ ya kupambana dhidi ya ubadhirifu wa fedha za umma nchini.
Zitto Kabwe
Kiongozi wa Chama ACT Wazalendo
Uwajibikaji, Changamoto na Uweledi wa Kamati ya PAC
Uwajibikaji, Changamoto na Uweledi wa Kamati ya PAC
Mfumo thabiti wa Uwajibikaji ni moja ya jawabu muhimu sana katika kuhakikisha Taifa linaondokana na ufisadi na masuala mengine yanayorudisha nyuma maendeleo ya Tanzania. Kazi za mwisho za Kamati ya PAC katika Bunge la Kumi zilisheheni mambo mengi muhimu katika mchakato endelevu wa ujenzi wa mfumo thabiti wa uwajibikaji nchini kwetu.
Taarifa ya Mwaka iliyojadiliwa na kupitishwa na Bunge wiki iliyopita ndio ilikuwa taarifa yetu ya mwisho katika Bunge hili. Kama kawaida mwaka 2015 ulianza kwa ziara za kukagua miradi na hatimaye kukutana na maafisa masuuli wa Wizara na Mashirika ya Umma ili kukagua mahesabu yao na kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya wakaguzi na Kamati.
Kipindi hiki ni muhimu sana kwangu kwani kwa vyovyote vile ni kazi yangu ya mwisho kufanya kama Mwenyekiti wa PAC, nafasi niliyoichukua mwezi Machi mwaka 2013. Kabla ya hapo nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) kuanzia Februari mwaka 2008 mpaka Februari mwaka 2013. Katika Maisha yangu ya miaka 10 Bungeni, nimetumikia uongozi wa kamati hizi kwa miaka Saba na Nusu. Hata hivyo leo natafakari kazi ya wiki nne tu na nilichojifunza katika siku hizo.
Wiki ya Kwanza, tulitembelea miradi ya njia za Reli na Mashamba ya Miwa ili kuongeza uzalishaji wa Sukari nchini. Tulikwenda mkoani Morogoro katika Wilaya za Kilosa na Kilombero. Tulijulishwa kuhusu mahitaji ya fedha nyingi katika ujenzi wa Reli ya Kati ambapo ili kukarabati mtandao Reli iliyopo zinahitajika jumla ya shilingi 500 bilioni kwa miaka mitatu mfululizo ($800m). Vilevile zinahitajika dola za Kimarekani $6 bilioni kujenga reli mpya ya kisasa (standard gauge). Wiki mbili baada ya kumaliza ziara hiyo, niliona picha ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akikagua ujenzi wa Reli ya kisasa nchini humo. Nilipoangalia picha yangu na wajumbe wenzangu katika kijireli chetu, nilicheka kicheko cha huzuni sana. Nimejifunza kwamba nchi yetu inaweza kusonga mbele iwapo tu tutaamua kujinyima baadhi ya maeneo ili kuendelea kwenye maeneo mengine. Fedha inayopotea katika kutoa misamaha ya kodi (tshs 1.9 trilioni ) peke yake, kwa mwaka mmoja inamaliza ukarabati wa Reli yote ( Kigoma – Tabora – Dar es Salaam na Tabora – Mwanza ).
Wiki hiyo pia tulitembelea kiwanda cha Sukari cha Kilombero na kukutana na Wakulima wa Miwa. Tanzania ina nakisi ya Sukari ya takribani tani 120,000 – 200,000 kwa mwaka. Uzalishaji wa ndani wa tani 300,000 hautoshelezi mahitaji ya wananchi na hivyo twalazimika kuagiza Sukari kutoka nje ya nchi ambayo husamehewa kodi. Kwa mwaka Tanzania husamehe kodi ya zaidi ya shilingi 200 bilioni katika Sukari peke yake. Fedha hii ingeweza kujenga viwanda kadhaa vya Sukari na hivyo kuachana kabisa na uagizaji na badala yake kuuza nje. Nimejifunza mengi sana katika kushughulikia suala la Sukari nchini. Nimeona namna ambavyo mfumo mzima wa Serikali ulivyo na ganzi katika kupata suluhisho la kudumu. Hivi sasa Serikali inataka uagizaji wa Sukari ufanywe na wazalishaji wa Sukari, majawabu ya namna hii ni majawabu ya kugawana pato nyemelezi (rent seeking). Jawabu la kudumu la sekta ya Sukari ni kuongeza uzalishaji wa ndani kwa kufungua viwanda vipya maeneo yenye miwa ya ziada hivi sasa, kutoa ruzuku kwa viwanda ili kupunguza gharama za uzalishaji na hatimaye kuwa na bei nafuu kwa walaji na kufungua mashamba mapya ili kuzalisha ziada na kuuza nje kwa ajili ya kupata fedha za kigeni.
Tulijadili kwa kina sana changamoto zinazoikabili sekta ndogo ya kilimo cha Korosho. Ukaguzi Maalumu ulionyesha kuwa kuna unyonyaji mkubwa wa wakulima ikiwemo kupewa pembejeo zilizoisha muda na kutofikishiwa pembejeo kabisa. Pia upotevu mkubwa sana wa Korosho na suala zima la kuuza korosho ghafi nje ya nchi. Utafiti uliofanywa na African Cashew Alliance unaonyesha kuwa Tanzania hupoteza zaidi ya dola za kimarekani 110 milioni kila mwaka kwa kuuza korosho ambazo hazijabanguliwa. Ikumbukwe kuwa Tanzania ilikuwa na viwanda 12 vya kubangua Korosho na vyote viliuzwa katika zoezi la ubinafsishaji na sasa vimekuwa ni maghala ya kuhifadhia Korosho. Tulielekeza kuwa mapato yanayotokana na tozo ya mauzo ya Korosho nje (export levy) yatumike kujenga viwanda vipya vya korosho kwa kutumia teknolojia mpya kutoka Vietnam ambapo viwanda vidogo vidogo vitajengwa kuanzia vijijini na kuzalisha ajira nyingi na kuondoa umasikini. Nimejifunza kwamba Korosho peke yake inaweza kuingiza fedha za kigeni katika nchi yetu kwa thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 500 milioni kwa mwaka. Mwaka 2014 Tanzania imezalisha tani 200,000 za Korosho, rekodi ambayo haijawahi kufikiwa tangu tupate Uhuru. Korosho inaweza kuondoa umasikini kwa watu wa mikoa ya Kusini iwapo Viongozi wakiamua iwe hivyo.
Ilituchukua siku 2 kujadiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhusu mahesabu yao ya mwaka wa fedha ulioishia Juni, 2013. Sababu kubwa ilikuwa ni mjadala kuhusu misamaha ya Kodi. Kama nilivyoeleza hapo juu, tulijulishwa kuhusu misamaha mingi ya kodi kuendelea kutolewa mpaka kufikia jumla ya shilingi 1.9 trilioni katika mwaka wa fedha ulioishia Juni, 2014. Kamati pia ilijadili Taarifa ya ukaguzi maalumu kuhusu misamaha ya kodi na kugundua kuwa misamaha mingi inatumika ndivyo sivyo. Nimejifunza kuwa tukiendelea kusisitiza uwazi na uwajibikaji tunaweza kupunguza tatizo hili la misamaha holela ya kodi. Tuliagiza kuwa kuanzia sasa, katika kila Taarifa ya makusanyo ya TRA kila mwezi, pia taarifa ya misamaha ya mwezi huo itolewe kwa umma. Hii itasaidia kuonyesha ni mapato kiasi gani yangeweza kukusanywa bila ya misamaha na kama misamaha hiyo ni muhimu na inatumika ipasavyo.
Mifano hii michache ya Reli, Sukari, Korosho na Misamaha ya Kodi imenikumbusha changamoto nyingi ambazo nchi yetu inazo na namna bora ya kukabiliana na Changamoto hizo. Mfumo thabiti wa Uwajibikaji ni suluhisho endelevu dhidi ya changamoto hizi. Kamati ya PAC imeshiriki kikamilifu kujenga mfumo huo. Kazi bado kubwa lakini inaendelea.
Zitto Zuberi Kabwe
Tunaweza kujitosheleza kwa Sukari
Tunaweza kujitosheleza kwa Sukari
Leo siku nzima kamati ya PAC ilikuwa inazungumza na Bodi ya Sukari, Wizara ya Kilimo na Wakulima wa Miwa Wilayani Kilombero. Tanzania huzalisha wastani wa tani 300,000 za Sukari kwa mwaka ilhali mahitaji ni tani 420,000 kwa mwaka. Hii hupelekea uagizaji wa Sukari kutoka nje ambao umekumbwa na malalamiko makubwa sana kutoka kwa wadau mbalimbali.
Masuala kadhaa yameibuliwa katika kikao cha leo
- Wakulima wamelalamikia sana uingizaji holela wa Sukari nchini. Bei ya Miwa imeshuka kutoka tshs 69,000 kwa tani mpaka tshs 55,000 sababu ya Sukari ya ndani kukosa soko.
- Wakulima wamelalamikia viwanda kwa kujipangia bei bila kuwashirikisha wao na pia viwanda ndio vinapima Miwa na ubora wa mua wa mkulima hivyo kuleta mgongano mkubwa wa MASLAHI kwa mwekezaji
- Wakulima wametaka hisa 25% za Serikali katika viwanda vya Sukari wapewe wao ili waweze kushiriki katika Uchumi wa nchi
- Bodi ya Sukari imeshindwa kuendeleza mradi wa RUIPA kwa sababu ya kutokuwa na Fedha tshs 11 bilioni za kulipa fidia ya Wananchi katika eneo la mradi. Mradi huu ungeweza kuzalisha tani 244,000 za Sukari kwa mwaka
- Wakulima wamelalamikia sana tabia ya viwanda kushindwa kununua Miwa yote ya Wakulima na hivyo kupelekea takribani nusu tu ya Miwa kutumika na nusu nyingine kubaki mashambani na kuharibika. Wastani wa tani 400,000 za Miwa huharibika Wilayani Kilombero peke yake. Hii ni sawa na tani 50,000 za Sukari
PAC imetoa ufafanuzi wa masuala yafuatayo
- Kamati ilikwishaiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania kufanya uchunguzi wa kikodi katika Sekta nzima ya Sukari nchini. TRA wameijulisha kamati kwamba wanafanyia kazi suala hilo na wameomba muda zaidi ili kukamilisha kazi hiyo. PAC imekubaliana na ombi hilo na pia kwamba inasubiri Taarifa ya kikosi kazi kilichoundwa na Katibu Mkuu Kiongozi ili kupata suluhisho la kudumu la Changamoto zinazokabili Sekta ya Sukari. Kamati ikishapata taarifa zote hizo itazifanyia kazi na kuziwasilisha Bungeni.
- Kamati imeielekeza Bodi ya Sukari kuhakikisha inaendeleza mradi wa RUIPA kwa kutangaza zabuni ya kumpata mwekezaji ambaye atalima sehemu ya shamba na kumilikisha kwa hati Wakulima ( outgrowers) sehemu nyingine ya shamba. Mradi wa RUIPA uwe mfano wa ushiriki wa wananchi katika Kilimo cha kisasa. Wakulima wamilikishwe Ardhi ya kulima Miwa na kuuza kwenye kiwanda, wasikodishiwe Ardhi hiyo. Bodi ya Sukari ipate FEDHA tshs 11 bilioni za fidia ya wananchi kutokana na zabuni ya kupata mwekezaji na malipo tangulizi ya mwekezaji.
- Modeli ya Malaysia yaweza kutumika katika mradi wa RUIPA, kwa kuwagawia wananchi ( households ) 1500 wanaoathiriwa na mradi kila mmoja hekta 5 ( 4 za kulima Miwa na 1 ya makazi yake ) na hekta zinazobakia katika jumla ya hekta 14700 ziwe nucleus. Ushiriki wa wananchi katika uzalishaji wa Ndio njia endelevu ya kutokomeza umasikini nchini.
- Kamati imeelekeza kuwa Bodi ya Sukari iwe na mamlaka ya kuwa mdhibiti ( regulator ) kwa kutoa bei elekezi za mauzo ya Miwa na Sukari nchini ili kulinda Wakulima dhidi ya unyonyaji wa wawekezaji. Bodi pia ihusike na udhibiti katika upimaji wa Miwa na kiwango cha Sukari katika Miwa ( sucrose ) ili kujibu Changamoto ya Wakulima kupunjwa.
- Kamati imeelekeza kuwa vianzishwe viwanda vya ngazi ya kati vya Sukari ili kutumia Miwa ya ziada na kuzalisha Sukari na hivyo kuongeza uzalishaji. Vyama vya Wakulima wa Sukari vimehamasishwa kuanzisha viwanda vidogo hivyo na Bodi ya Sukari imeelekezwa kulegeza masharti ya uanzishaji wa viwanda vya ngazi ya kati.
- PAC imepingana na Wakulima kwamba hisa za Kampuni 25% wapewe wao na badala yake PAC imeelekeza Msajili wa Hazina aangalie uwezekano wa kuorodhesha hisa za Serikali katika soko la hisa la Dar Es Salaam na vyama vya Wakulima vipewe fursa kununua sehemu ya hisa hizo ( angalau 5%).
- Wakulima wa Miwa wamehamasishwa kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili wafaidike na mafao ya muda mrefu na muda mfupi ikiwemo Bima ya Afya, mikopo katika SACCOS zao na pensheni uzeeni. Tanzania ina jumla ya Wakulima wa Miwa ( out-growers ) 19,000 wenye kuzalisha nusu ya Sukari inayozalishwa nchini.
Tukipunguza upotevu wa Miwa ya Sukari ( wastage ) nchi nzima kwa kuanzisha viwanda vya Kati vya kusindika Miwa, tunaweza kuongeza uzalishaji kwa zaidi ya tani 80,000 za Sukari na kupunguza Sukari inayoagizwa kutoka nje. Tukitekeleza mradi wa RUIPA, tutakuwa na Sukari ya ziada tani 200,000 ambazo tunaweza kuuza nje na kupata fedha za kigeni.
Hii iwe mikakati ya muda mfupi. Tunaweza tukiamua na kashfa za Sukari zitakuwa Historia. Tufanye sasa
Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema “Hatutetereki”
Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema “Hatutetereki”
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Kamati ninayoongoza ya PAC kuwasilisha Bungeni Taarifa Maalumu kuhusu ukaguzi maalumu wa akaunti ya Tegeta Escrow, kumekuwa na kampeni za chini chini zinazoendeshwa kwenye korido za Bunge na kwenye mitandao dhidi yangu binafsi na baadhi ya wabunge waliosimama kidete dhidi ya wizi wa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania akaunti ya Escrow.
Baadhi ya tuhuma nimezipeleka kwenye vyombo vya dola ili zichunguzwe kwani zina vielelezo vya mahala pa kuanzia (kama leseni ya udereva ya mwanamke anajulikana kama Vivian Emmanuel Sirikwa na muhuri wa kampuni ya uwakili inayomilikiwa na Bwana Joseph Mkandege).
Baadhi ya tuhuma nitazijibu moja baada ya moja.
Waziri mmoja ambaye ni mtuhumiwa wa wizi wa fedha za Tegeta Escrow anazunguka kwa wabunge akisema tuhuma hizi kupikwa kama njia yake ya kuhamisha mjadala kutoka uporaji wa Tshs 200 bilioni kwenda kwenye masuala binafsi.
Tuhuma hizi zenye kichwa cha habari “Zitto na Filikunjombe wanatumiwa na Kenya na Uingereza kuvuruga na kudhoofisha Uwekezaji nchini mwetu” zinajibiwa hapa chini. Utaona ndugu Filikunjombe ametajwa kwa kichwa cha habari ili kumtaja tu bila sababu yeyote ile.
Tuhuma #1:
Zitto anaye rafiki yake Mkenya aitwae Rapahel Ongangi ambao kwa pamoja wameanzisha Gombe Advisors Co. Ltd (registered on 24 November 2011, Certificate No 87387) kwa ajili ya kufanya biashara na Makampuni ya Gesi na Mafuta yanayofanya kazi nchini hapa.
Majibu:
Gombe Advisors ni kampuni binafsi isiyofanya faida yaani ‘Company Limited by Guarantee’. Haina kazi na kampuni yoyote ya Gesi na Mafuta na wala yenyewe haijuhusishi na biashara hiyo. Gombe advisors haijafanya kazi yoyote ile na kampuni nyingine zaidi ya kusaidia wasanii wa kundi la Kigoma All stars. Upotoshaji hapa unalenga kupindisha mjadala.
Tuhuma #2:
Zitto amemsaidia Ongangi kupata uraia wa Tanzania na kwa sasa ni raia wa pasipoti. Zitto na Ongangi walimtafutia CEO wa Shell aitwae Axel Knospe nyumba na gari ya kukodi.
Majibu:
Raphael ni mtu binafsi ambaye anafanya shughuli zake hapa nchini, amesoma hapa nchini na ameoa na ana mtoto. Tuhuma hizi hazina msingi wowote ule maana ni uwongo. Wanaotoa tuhuma hizi waonyeshe hiyo pasipoti ya Bwana Ongangi kuthibitisha madai yao.
Tuhuma #3:
Mikataba ya STATOIL iliyokuwa inarushwa kwenye mitandao ya jamii na kuchapishwa kwenye magazeti ya Kenya ya hapa nchini (The Citizen na Mwananchi) mwandishi mkuu alikuwa huyo CEO wa Shell.
Majibu:
Mkataba uliovujishwa wa StatOil ulivujishwa na waandishi wa habari wa Norway. Uchambuzi wa mkataba huo nimeufanya mwenyewe kwa kutumia utaalamu wangu niliosomea wa kuchambua mifumo ya kodi kwenye sekta ya mafuta na gesi. Kwa namna yoyote ile, huyo anayetajwa kuwa CEO wa kampuni ya Shell hahusiki. Tuhuma hii wanaoitoa watoe ushahidi usio na chembe ya mashaka.
Ikumbukwe kuwa mkataba wa StatOil utaipotezea Tanzania mapato ya dola za Marekani bilioni 12 (takribani Tshs 20,400,000,000,000/=) katika kipindi cha miaka 15 baada ya gesi kuanza kuchimbwa.
Uamuzi wa Kamati ya PAC kutaka mikataba yote ya Gesi kuwa wazi una lengo la kuchambua kuona kama mikataba yote nchini haipotezi mapato kwa nchi. Uamuzi huo umewakasirisha sana baadhi ya waliohusika kuingia mikataba Serikalini maana wanajua kuna madudu kwenye mikataba na wanataka umma wa watanzania usijue!
Tuhuma #4:
Kampuni ya SHELL imechukizwa sana kucheleweshwa kwa kupata kibali cha kutafuta gesi na mafuta kule Pemba. Vilevile SHELL haina uwekezaji mkubwa Tanzania Bara kwani ilishindwa kwenye tenda zenye vitalu vyenye gesi nyingi upande wa Bara.
Majibu:
Ukweli ni kuwa Kampuni ya Shell ina vitalu 4 huko Zanzibar na tayari ina makubaliano na Serikali ya Zanzibar kuhusu utafutaji mafuta huko katika vitalu namba 9,10,11 na 12. Shell inafanya kazi na kampuni ya Petrobras ya Brazil kwenye kitalu namba 6 na namba 8. Taarifa hizi zipo wazi kwenye tovuti ya TPDC. Tuhuma nyepesi namna hii dhidi ya kampuni kubwa kama Shell zinaonyesha dharau na kiburi kinachotokana na uelewa mdogo wa mambo wa watu wanaotuhumu.
Tuhuma 5:
Ongangi anapokea maelekezo kutoka Serikali ya Kenya kuhujumu uwekezaji nchini mwetu.
Majibu:
Nazifahamu mbinu nyingi zinazotumika kufanya propaganda, lakini mbinu hii imeshindwa ikiwa mapema sana. Ni vema wanaotoa tuhuma hizi wazithibitishe vinginevyo ni mwendelezo wa propaganda zisozingatia diplomasia ndani yake dhidi ya jirani zetu wa Kenya. Hizi ni propaganda hatari ambazo hata hao wanaotuhumiwa wakisikia watatudharau sana.
Tuhuma #6 (juu ya Uingereza):
Uingereza imekuwa inamfadhili Zitto kwa miaka mingi kwa mambo yake ya kisiasa kwa hiyo sasa hivi Ubalozi wa Uingereza unamlipa Zitto na Kafulila kuhakikisha kwamba Standard Chartered ya Uingereza inalipwa deni lake lisilotambulika kisheria nchini mwetu.
Majibu:
Nimetangulia kusema hapo awali kuwa kuna propaganda ambazo haziangalii hata diplomasia; nyingine ni hii. Pamoja na kukanusha uzushi huu, ni vizuri wanaotoa tuhuma za namna hii kuthibitisha. Mimi binafsi sijawahi kufadhiliwa kisiasa na Taifa lolote lile. Inaelekea kuna wanasiasa wanaofadhiliwa na mataifa mengine ambao kwakuwa kwao ndiyo maisha wanaamini na wengine tupo kama walivyo.
Kwangu itikadi yangu ni ‘Uzalendo kwa nchi yangu’, ni jambo ambalo halina mbadala wake. Siku zote nasema “Right or wrong, my country first”.
Kurudia kurusha tuhuma kwa Ubalozi wa Uingereza nchini ni kudhihirisha kwa mara nyingine kiburi cha kuwa na mamlaka (arrogance of power) walicho nacho wanaotuma tuhuma hizi.
Aidha, wanatuhumu kuwa “Kafulila na Zitto wamehaidiwa 15% ya USD 150 million kama deni likilipwa”
Mtanzania anayeweza propaganda dhaifu kama hizi basi anatakiwa ajitafakari. Hata hivyo ni vema wanaotoa tuhuma hizi wathibitishe bila chembe ya mashaka.
Tuhuma #7:
Mbunge Mkono nae ameshikwa hasira kupoteza kazi ya uwakili pale TANESCO. Kafulila na Zitto wanalipwa na Mkono kuvuruga Serikali kwa hasira za kukosa fedha za kitapeli za TANESCO.
Majibu:
Hizi ni tuhuma ambazo sasa tumezizoea kutolewa. Mambo mepesi hayawezi kujibu mambo ya msingi kama tuhuma za wizi wa fedha zaidi ya Tshs bilioni 200 kutoka Benki kuu ya Tanzania. Kukusanya kila propaganda ili kuuhamisha umma ni kupungukiwa hekima na busara.
Aidha, wanaotuhumu wanadokeza kuwa “Naomba tuwe macho na Wabunge wetu achananeni na madai ya Zitto ya wizi. Huyu mtu anafanya biashara na Kampuni ya SHELL na inasemekana analipwa na Ubalozi wa Uingereza. Serikali ya Kenya na tapeli mkubwa Mbunge Mkono nae anawalipa Zitto na Kafulila”.
Watanzania, haya ni maneno ya hasira ya watu wanaokaribia kukamatwa kwa kushiriki wizi wa fedha katika Benki kuu ya Tanzania. Kamwe tuhuma kama hizi haziwezi kutukatisha tamaa katika kupambana ili ukweli ujulikane. Sisi tutapigana kwa ajili ya Taifa, kwa ajili ya mtanzania na tunachotaka ni umma uujue ukweli wa mambo.
Hasira hizi zinatokana na mambo mawili:
Moja ni uamuzi wa kamati ya PAC kuwasweka ndani baadhi ya watendaji wa TPDC kwa kushindwa kutekeleza maamuzi ya Kamati yanayohusu uwazi wa mikataba ya Gesi na Mafuta.
Pili, ni uamuzi wa PAC kuagiza ukaguzi maalumu wa mchakato mzima wa kuanzishwa na kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 200 ziliporwa na zaidi ya shilingi bilioni 12 zinalipwa na TANESCO kila mwezi kwenda kampuni ya PAP inayomilikiwa na Harbinder Singh Seth (50%) na watu wasiojulikana kupitia kampuni ya Simba Trust iliyosajiliwa na kufichwa nchini Australia (50%).
Ieleweke kuwa PAP inalipwa shilingi milioni 400 kila siku kutoka TANESCO izalishe au isizalishe Umeme! Watanzania, PAP itaendelea kulipwa namna hiyo kwa miaka 20 ijayo. Kwa namna ambayo Seth analindwa na baadhi ya watendaji Serikalini na hasa ndani ya Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, kuna fununu kuwa kuna maofisa serikalini wanaomiliki hizo 50% za kampuni ya PAP. Seth pia anamiliki kitalu cha gesi Mnazi bay Kaskazini kupitia kampuni ya HydroTanz.
Hasira hizi walizo nazo wanaonituhumu na Kamati yangu zimewapelekea kugushi nyaraka mbalimbali zinazonituhumu mimi na wenzangu ili kutuogopesha na kutukatisha tamaa katika kutafuta ukweli juu ya suala la uporaji wa fedha kutoka Benki kuu. Lengo lao ni kututoa kwenye mstari. Mimi na wenzangu hatutatoka kwenye mstari, tutashirikiana na wabunge wenzetu kuhakikisha ukweli unajulikana na wezi kuchukuliwa hatua kali.
Harbinder Singh Seth aliiangusha Serikali ya KANU nchini Kenya, sasa anachotaka kukifanya kinaweza kuiangusha Serikali ya CCM wakiendelea kumkumbatia.
Watanzania sio mabwege!
Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC
Dodoma, 9 Novemba 2014
Corruption stinks, We must end it now
Corruption stinks, We must end it now
Also reported by The Citizen Newspaper
Remarks by Zitto Kabwe, MP at the launch of nationwide survey on people’s perceptions of corruption in Tanzania by Sauti za Wananchi, TWAWEZA on the 5th August, 2014 Dar es Salaam.
In 1999 when I was a first year student at the university and a student activist, the student body invited Judge Joseph Warioba to speak about corruption. At the Council Chamber he narrated a story about a woman whose child was sick at Mbeya Referral hospital and died because she did not have tshs 500 bribe to give to a nurse in order for the nurse to admit a drip on the child. I always remember this story and results of this survey confirm it. This survey shows that 7 out of 10 individuals consider a patient giving money or other materials to a public health facility doctor for the help they gave to them as corruption. Our people are confronted with this reality in their daily lives. We must fight everyday corruption as much as grand corruption. It is the poorest that pays the highest price of corruption. As endemic as corruption in Tanzania is, we need new approach to combat it, Thomas Sankara once said “You cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness”.
Everyday corruption isn’t reported in our media outlets as much as mega scams, but it is real and so pervasive in our society. Daily life in Tanzania is governed by the ‘petty’ corruption of public officials in services such as health, education, agriculture and judicial system. It takes various forms including commission for illicit service, string-pulling, favours, nepotism, rent seeking and misappropriation.
The survey once again confirms the pervasive nature of corruption in Tanzania and the hopelessness the population has on cutting down corruption. It is argued that corruption in Africa generally and in Tanzania in particular is qualitatively different from corruption in other parts of the world in its pervasiveness, its legitimations and its significant impact on the nature of the state.[1] Formal definitions of corruption range from decay of society to single act of bribery. It involves the acquisition of money, assets or power in a way which escapes public view.[2]
The survey we are presented with today shows all signs of a rotten society with sustained bad habit of putting things under the carpets. 8 out of 10 people believe corruption has increased over the last decade and majority believe that we can not end corruption. What is shocking is the fact that 7 out of 10 people believe that even if we change the governing party corruption wont be fought. With the revelations of the audited report of the accounts of political parties coming soon, the people are stating the obvious. There is a moral decay. It stinks.
Public Accounts Committee’s (PAC) duty is to hold public officials accountable. Through reports of the Comptroller and Auditor General, PAC and previously POAC has produced reports and reports about mismanagement of public funds. We were very successful in 2012 whereby through a threat to impeach the Prime minister, the President sacked 6 senior ministers and 2 deputies. 1 prosecution has been done (TBS) but the hunter became hunted. POAC was disbanded, annual reports by committees pushed to November sessions of parliament (so during election year in 2015 the PAC report won’t be submitted in April!) and Public Audit Act of 2008 amended to reduce the powers of oversight committees vis a vis auditor general reports. Obviously these are steps backward. It is comparable to the famous Tehelka scandal in India where journalists showed a secret video footage of senior politicians accepting bribes. Journalists became victims instead of the corrupt.[3] But these negative actions against anti corruption campaigners shall not deter us from fighting graft in Tanzania.
I am not shocked at all with the revelations that many Tanzanians know little about scams like IPTL (8 out of 10 Tanzanians had not heard of the scandal). I knew about withdrawal of Tegeta escrow money for the first time through The Citizen newspaper and immediately I acted upon and summoned central bank governor before PAC (https://zittokabwe.wordpress.com/2014/03/04/mapya-iptl-270million-zimetokaje-bot/). We issued statements on every single step we were taking including a directive to CAG and PCCB to carry a special audit. PAC directed special audit on Tegeta Escrow Account on the 20th March, 2014. Media houses with exception of Mwananchi, The Citizen and Mtanzania were not covering the scam at all regardless of number of statements we issued. May be they did not understand it. The day ndugu David Kafulila spoke about it in parliament, handful of papers reported and majority ignored the story but carried a clarification about it. (https://www.facebook.com/zittokabwe/posts/746280225392677). I posted on my Facebook wall ‘wahariri na miwani za mbao’. Now coverage about the scam has increased with the newest revelations from RaiaMwema weekly and daily TanzaniaDaima that the scam involve a tax fraud and a fraudulent transfer of ownership involving tax havens. Therefore, there is a significant need for media coverage in order for the public to hear about these scams. In addition, it is about how the scam is communicated for the people to understand.- therefore, I believe there is a need for adequate and rational media coverage of these scams so that people can be informed about them.
In Tanzania, we have metamorphosed into a situation whereby somebody is corrupt if he or she is your political enemy. And sometimes politics drive media coverage in order to confuse the public. Today IPTL scam is one of the most misunderstood because politicians, bureaucrats and some media have collaborated for it to be so. However when PAC submits its report to the house based on the findings from special audit, the country will be stunned to see how public officials participated in sanctioning a fraudulent transaction in the name of national interest. Will PCCB go ahead with prosecutions? Yes and No.
I have full trust in the ability and capacity of PCCB. But the system is set in such a way that the latter has no powers to bite. A number of cases are with Director of Public Prosecutions (DPP). As a nation we must decide now to grant PCCB the power to prosecute. I strongly advocate the establishment of Serious Fraud Office within PCCB that will have legislative powers to investigate and prosecute all major scams done by public officials. Granting PCCB powers to prosecute may be included in the draft constitution through establishment of the Public Integrity Office.
Civil Society Organisations may as well engage in addressing everyday corruption through surveys and providing an opportunity for the people to report incidences of corruption. What about ranking regions based on corruption persecution index? Or even district authorities?
PAC is going to introduce a bill in parliament to amend proceeds of crime act so that an individual with assets not commensurate with his or her income levels has a burden of proof on the legality of the assets. Councils’ officials, central government bureaucrats and politicians with wealth not in line with their incomes must be subjected to prove origin of their wealth in court. This will help the war against corruption.
I strongly propose that pressure to enact a freedom of information act be increased. This was promised by President Kikwete under OGP and the deadline set has already passed. Powered with information, the citizens can be mobilized to end public corruption.
We have to ACT now.
[1] From Everyday Corruption and the State by Blundo G, et al.
[2] Global Corruption by Cockcroft L.
[3] Curbing Corruption in Asian Countries: An Impossible Dream? By Quah J.S
Ukaguzi Maalumu akaunti ya Tegeta Escrow-Hadidu Rejea-PAC
Ukaguzi Maalumu akaunti ya Tegeta Escrow
Hadidu rejea
1) Kuchunguza uendeshaji wa mkataba wa kuzalisha Umeme kati ya kampuni ya IPTL na TANESCO
2) Kuchunguza kama wakati escrow inafunguliwa kampuni ya mechmar ilikuwa inamiliki IPTL, kama ilikuwa imefilisiwa na kama ilikuwa imehamisha umiliki wake kwa kampuni ya PAP.
3) Kuchunguza na kuthibitisha ushahidi wa kampuni ya PAP kununua kampuni ya mechmar na kumiliki IPTL
4) Kuchunguza chanzo cha mgogoro kuhusu tozo kati ya TANESCO na IPTL na kuthibitisha ushahidi wowote kuwa mgogoro uliamuliwa kwa faida ya IPTL
5) Kuchunguza kama ilikuwa sahihi kwa mwanasheria mkuu wa Serikali kusamehe kodi ya VAT ya jumla ya tshs 26 bilioni kutokana na tozo ya capacity charges na TRA wachukue hatua gani kuhakikisha kodi hiyo inakusanywa
6) Kuchunguza kiwango cha fedha kilichopaswa kuwemo katika akaunti ya escrow, kiwango gani kilikuwepo wakati IPTL wanalipwa na kiwango gani kitapaswa kulipwa zaidi kutoka tanesco
7) Kuchunguza madai ya benki ya standard chartered kwa tanesco na madai mengine yeyote yanayohusiana na mkataba wa kuzalisha Umeme wa IPTL na iwapo Serikali imejihadhari na uwezekano wa madai yanayoweza kufunguliwa, nafasi na heshima ya nchi katika kuheshimu mikataba ya kimataifa na ya uwekezaji.
8) Kuchunguza iwapo Wizara ya Nishati na madini ambayo ni mhusika Mkuu wa akaunti ya tegeta escrow ilifanya ‘due diligence’ ya kutosha kabla ya kuingia makubaliano ya kutoa fedha zilizopo akaunti ya tegeta escrow. Kupata Maelezo ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na madini ni kwa nini aliagiza ukaguzi maalum wakati yeye ni mhusika Mkuu kwenye mchakato mzima na ilhali akijua PAC tayari imeanza mchakato wa ukaguzi.
9) Kutoa mapendekezo ya njia bora za kisheria kulinda Taifa kutoingia hasara zaidi katika mkataba wa IPTL chini ya wamiliki wapya
10) Kutoa ushauri kwa kamati ya PAC juu ya mapendekezo ya hatua ambazo Bunge linapaswa kuchukua kuhusu matokeo ya ukaguzi huu maalumu
Imetolewa na;
KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)
Deni la Taifa: Wafaidi wachache, twalipa wote #DeniLaTaifa
Deni la Taifa: wafaidi wachache, twalipa wote
Leo nimeandika kuhusu Deni la Taifa kukua kwa kasi na kufikia tshs 27 trilioni mpaka Desemba 2013 kutoka tshs 10 trilioni mwaka 2005. Baadhi ya Watalaamu wanajenga hoja kuwa kukopa sio shida, bali kukopa kwa ajili ya nini. Nikakumbuka mzigo wa madeni ambao Taifa lilibeba miaka ya sabini na themanini kiasi cha Tanzania kukoswa koswa kuwa nchi ya Kwanza duniani kushindwa kuhudumia madeni yake. ‘heshima’ hiyo ilikwenda kwa nchi ya Nicaragua mwaka 1982. Mikopo ya nini?
Mwishoni mwa miaka ya sabini Tanzania ilikopa dola za kimarekani milioni sitini (USD 60m) kwa ajili ya mradi wa Kiwanda cha viatu Morogoro. Lengo la kiwanda kiwanda kile ilikuwa ni kuuza viatu nchini Italia. Mwaka mmoja baada ya kiwanda kuzinduliwa kilikuwa na uwezo wa kuzalisha kwa ufanisi wa asilimia 4 tu ya uwezo wake na hakikuweza kuuza hata jozi moja ya kiatu nje ya nchi. Miaka ya tisini kiwanda kile kiliuzwa katika mpango wa ubinafsishaji na hivi sasa kimegeuzwa kuwa ghala. Hata hivyo Deni hili lilipwa na kila Mtanzania kupitia kodi.
Kesho Jumanne tarehe 28 Januari, 2014 Kamati ya Bunge ninayoongoza ya Hesabu za Serikali (PAC) inapokea taarifa ya ukaguzi maalumu uliofanywa kuhusu Mfumo na Mchakato wa kusambaza pembejeo za ruzuku kwa wakulima. Ukaguzi huu umefanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali (CAG). Nimeipitia Taarifa hii na kukumbuka habari ya ‘Morogoro Shoe Factory’.
Bajeti ya pembejeo za ruzuku ya mwaka 2011/12 ilikuwa tshs 122.4 bilioni, kati ya hizo tshs 88.9 bilioni ni mkopo kutoka Benki ya Dunia. Taarifa ya CAG inaonyesha uvundo wa ufisadi katika mfumo mzima wa pembejeo za ruzuku. Katika kijiji cha Lunyala wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa asilimia 70 ya wananchi waliorodheshwa kupata mbolea walikuwa bandia, hata hao waliopata mbolea walidai mbolea ilikuwa haina ubora stahili na matokeo yake uzalishaji wa mazao ulikuwa mdogo. Hata hivyo wasambaji wa mbolea walilipwa fedha zao zote. Afisa mmoja mwandamizi wa Benki ya Dunia alipata nukuliwa kusema kuwa asilimia 60 ya Bajeti ya pembejeo za ruzuku iliporwa na wajanja wachache.
Deni hili nalo litalipwa na Watanzania wote japo waliofadika ni wezi wachache. Kinachosikitisha ni kwamba masuala haya yanayohusu wananchi hayapati msukumo kwenye mijadala ya kitaifa. Tusipobadilika tutajikuta tuna madeni mpaka kwenye kope za macho yetu.
“…mikopo haisaidii, hata tukiitumia kujenga shule au hospitali au viwanda lazima ilipwe. Mlipaji ni mkulima wa vijijini…” Azimio la Arusha, 1967.