Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Posts Tagged ‘#voteofNOconfidence

Press ya Mwisho ya hoja

with 5 comments

Photo from press conference.

Written by zittokabwe

April 22, 2012 at 8:09 PM

Posted in Uncategorized

Tagged with

PRESS RELEASE: HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

with 11 comments

HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012

•       Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini
•       Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’

Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 ya wabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge isipokuwa tu kama;

(a)    “taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni; ”Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa “hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri”.

Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo Bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’ hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi. Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni.

…………………………….
Kabwe Zuberi Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.

Written by zittokabwe

April 22, 2012 at 7:17 PM

Posted in Uncategorized

Tagged with

Wabunge wapiga sahihi kutokuwa na imani na Pinda #voteofNOconfidence

with 8 comments

Deo akitia sahihi
Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana. Kulia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefanya zoezi la kukusanya sahihi za wabunge ili aweze kuwasilisha bungeni hoja kutokuwa na imani na waziri mkuu, Jumatatu wiki ijayo.

Kangi Logola akiweka sahihi
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni mjini Dodoma jana. Kushoto ni Msaidizi katika ofisi ya kami hiyo, John Mrema.
Machali wa NCCR akiweka sahihi
Mbunge wa wa Kasulu Mjini, Moses Machali akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ndani ya ukumbi wa Bungeni mjini Dodoma jana. Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kusini, Zitto Kabwe anayetaka kuwasilisha bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Mbowe akiweka Sahihi
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ndani ya ukumbi wa Bungeni mjini Dodoma jana.
Mrema wa TLP akiweka sahihi
Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ndani ya ukumbi wa Bungeni mjini Dodoma jana.
Kahigi wa Chadema akiweka sahihi
Mbunge wa Bukombe, Prof Kulikoyela Kahigi akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Katikati ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.

Written by zittokabwe

April 21, 2012 at 9:15 PM

Posted in Uncategorized

Tagged with