Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Statement: Hali Yangu ya Afya

with 109 comments

Ndugu zangu,

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha muda huu kuwa na nguvu za kukaa katika kiti na kuweza kuandika haya machache kwenu. Nawashukuru sana Wanamabadiliko kwa salaam zenu nyingi za pole mara mliposikia ninaumwa na kulazwa hospitalini. Najua hamkuwa na taarifa kamili za kuumwa kwangu na kwa kweli suala la kuumwa ni suala la mtu binafsi (hata kwa mtu mwenye dhamana ya kiuongozi wa umma japo umma nao una haki ya kujua kinachomsibu kiongozi husika).

Mwanzo

Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa siku ya Ijumaa tarehe 20 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa Mamlaka za Maji nchini.

Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za Jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya kuinigilia ziara za Jimboni ikiwemo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika.

Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.

Siku ya Jumapili saa kumi na moja jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla. Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba Dereva wa Mhe. Mhonga anifuate ili anisadie kunifikisha nyumbani.

Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma.

Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40).

Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku. Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia Hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania.

Nilipita Agakhan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.

Hali kubadilika

Siku ya Jumanne niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini sio vya kutisha. Nikawajulisha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi.

Hata hivyo ilipofika saa sita kamili nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kichwa kikiniuma sana sana sana!

Dada zangu wakamwita Driver na kunikimbiza Hospitali ya Agakhan. Wakarejea vipimo vilevile na matokeo yakawa yaleyale. Joto lilifika degree 39.8 Hivyo wakanipa dawa za kupoza homa na maumivu ya kichwa kwa drips na sindano kadhaa.

Siku ya pili hospitalini nikafanya vipimo zaidi ikiwemo ultra sound na vyote kuonekana sina tatizo lolote. Niliendelea kuwepo Hospitali na kwa kweli hali ilikuwa inatia moyo sana kwani nilipata nguvu na hata kuweza kuzungumza, homa ilikuwa imepungua sana.

Pamoja na kwamba Mganga Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Waziri wa Masuala ya Bunge na Daktari wangu binafsi kuwataka waangalie upya vipimo vya malaria, madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa ‘a trigger’ ya homa kali niliyokuwa napata.

Hali kuwa Mbaya

Usiku wa siku ya Jumatano Hali ilikuwa mbaya sana. Joto lilipanda tena kufikia 40 na kichwa kuuma zaidi. Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa.

Wageni waliokuwa wamekuja kunijulia hali wakati hali inabadilika ilikuwa ni pamoja na Ndugu Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya POAC, walishauri mara moja nihamishwe Hospitali kupelekwa Muhimbili.

Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika Chumba wanachokiita Mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mama Blandina Nyoni alikuwepo Hospitalini tayari.

Usiku huo huo nilifanyiwa vipimo upya. Full Blood picture pamoja na BS. Vile vile kufuatia malalamiko kuhusu maumivu ya kichwa ikaamuliwa kuwa nifanyiwe CT Scan usiku ule.

Ikaonekana nina wadudu wa Malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana Daktari kijana Dkt. Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale Mini ICU.

Asubuhi ya siku ya pili nikapata majibu ya tatizo la maumivu ya kichwa. Nimekuwa nasumbuliwa na kichwa kwa miaka zaidi ya Kumi sasa na katika kipindi hicho mara nne nilipoteza fahamu na kuanguka (Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Jijini Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, Mara Pili Mjini Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001 lakini ilikuwa usiku, Mara ya tatu Nikiwa chumbani, Hall II mara baada ya kutoka *Prep, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge (Ndugu Katulanda anakumbuka siku hii kwani yeye ndiye niliyemkamata njiani kunikimbiza Zahanati ya Bunge).

Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni ‘surgery’ na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.

Baada ya kuwa Malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya ‘dozi’ nilopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza ‘dozi’ hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya ‘surgery’ hiyo.

Sijafa

Uvumi ulienezwa nimekufa. Kwa kupitia kwenu ndugu zangu Wanamabadiliko, napenda Watanzania wenzangu wajue mimi ni mzima wa Afya. Nimepata maradhi kama Binadamu mwingine yeyote anavyoweza kupata na namshukuru Mungu kwamba ninapata matibabu mazuri kabisa.

Shukran
Nawashukuru sana Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Prof, Mwafongo kwa juhudi kubwa walioonyesha katika kunihudumia. Naishukuru Ofisi ya Bunge kwa Kutimiza wajibu wao kwangu kama Mbunge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu na watumishi wote wa Wizara ya Afya, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kwa ufuatiliaji wa karibu wa Afya ya Naibu wake, Wabunge wajumbe wa Kamati ya POAC, Dkt. Alex Kitumo, ndugu, jamaa na marafiki zangu wote.

Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uvumilivu mkubwa hasa kufuatia uvumi mbalimbali ulioenezwa, pia Watanzania wengine kwa uzito huo huo.

Nitawajulisha kwa lolote Mungu akipenda. Ninaendelea na matibabu na hali yangu ni nzuri

Ndugu yenu

Zitto

Written by zittokabwe

October 31, 2011 at 11:57 AM

Posted in Uncategorized

109 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. Pole

    Philip Neville Mbega

    October 31, 2011 at 12:07 PM

    • pole sana

      manuel matteru jr

      October 31, 2011 at 1:00 PM

  2. Kaka, pole sana sana kwa kuumwa. Sala na maombi yetu ni kwamba upate nafuu. Ni matumaini yngu utapona haraka na kuendelea na majukumu yako ya kawaida. Alberto

    Albert

    October 31, 2011 at 12:10 PM

  3. Mh. Zitto, maumivu na masumbufu yote ni sehemu ya mapigano yako kwenye mabadiliko ya kweli. Hapawezi kutokea mabadiliko bila maumivu. Bila shaka historia ya maumivu yako ni sehemu ya struggle zako tangu Chuo Kikuu na sasa kwenye siasa hizi ngumu za Tanzania. Tunakuombea kwa Mola utapona na hakika utashuhudia mabadilko ya kweli kwa nchi yetu kama unavyoyatamani.

    James Marenga

    James Marenga

    October 31, 2011 at 12:13 PM

  4. Our prayers r with u.

    Aggie

    October 31, 2011 at 12:13 PM

    • mh. zito sisi raia wapenda mabadiliko tupo nyuma tunakuombea mwenyezi mungu akujalie upate afya njema. na hatimae urudi Tanzania kuendeleza mapambano MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI willy foya

      willy herieli foya

      November 6, 2011 at 4:00 PM

  5. Mungu yu pa1 nawe kila cku za uhai wako kwa hakika nilihuzunika sana after uvumi be strong mpiganaji wetu. you will never walk alone.

    Ngatale

    October 31, 2011 at 12:15 PM

  6. Mungu Akuponye haraka…

    Reuben

    October 31, 2011 at 12:19 PM

  7. Get well soon brother. Mungu ataendelea kukubariki

    sanguro

    October 31, 2011 at 12:20 PM

  8. Pole sana na Mungu atakusaidia zaidi.

    Iddi kaluse(Gombe N.P)

    October 31, 2011 at 12:20 PM

  9. Pole sana ndg Zitto tuko pamoja kwenye maombi..hakika utapona.

    Frank

    October 31, 2011 at 12:24 PM

  10. Tunashukuru kwa taarifa Mh. Zito..Mungu ni Mwema na hakika Fadhili zake ni za Milele. Mungu akutie nguvu upata kupona haraka na kurudi katika kuwatumikia Watz kwa Ari ya hali ya juu. Amen!

    Simon

    October 31, 2011 at 12:30 PM

  11. Pole kaka,tupo pamoja namungu atakujalia utapona

    Azizliwamba

    October 31, 2011 at 12:31 PM

  12. Mpendwa Mh. Zitto. Mungu yupo pamoja nawe. Tunaamini kwamba Mungu yu pamoja nawe. Ugua Pole.

    Godwin Muganyizi

    October 31, 2011 at 12:34 PM

    • Pole sana mkuu tuko pamoja na chadema tuko pamoja daima.

      fredy

      October 31, 2011 at 8:08 PM

  13. Mheshimiwa Zito Kabwe pole sana na kuugua! Kama ulivyosema ni sehemu ya maisha ya mwanadamu! Naungana na watanzania walio wengi kukuombea afueni ili urejee salama na kuendelea kushiriki ujenzi wa Taifa letu! Mungu na akutangulie

    Faustine Kimario

    October 31, 2011 at 12:34 PM

  14. Tunakuombea opone haraka ili ushiriki katika vikao vya bunge vinavyotarajiwa kuanza, daima mambano mbele.

    MOHAMED

    October 31, 2011 at 12:37 PM

  15. Inshallah get well soon

    Zulekha

    October 31, 2011 at 12:38 PM

  16. Hakika Mwenyezi Mungu ndio mfumbuzi wa kila kitu. Hali ya kuugua kwako imezua uvumi huo kwa sababu watu walitamani kuwe na chombo cha habari kinachofuatilia na kudadafua kila hatua ya matibabu yako, na si vinginevyo.

    Wananchi wengi wa Jimbo la Kigoma kaskazini wamekuwa wakikaa kwa vikundi vikundi kujadili tatizo, chanzo cha maradhi hayo, matibabu na muafaka wa hali bila ufumbuzi. Wamepiga simu mara kadhaa kwa wadau mbalimbali kuulizia hali na kuongeza dua kwa Mwenyezi Mungu ili kuwekewa wepesi.

    Uwezo na nguvu zilizokuwezesha kutoa kauli hii ya busara ni jibu tosha kwetu.

    Hatutachoka kukuombea asilani na kuongeza imani kwa kila hatua. Mwenyezi Mungu akulinde katika matibabu yako, akujalie afya njema na hekima ili urejee salama na uendelee na majukumu ya kulijenga taifa.

    Ugua pole kiongozi.

    Paulus

    October 31, 2011 at 12:42 PM

  17. Pole sana Mh.Zitto kwa ugonjwa uliokupata, watanzania wote tupo nyuma yako. InshaAllah mwenyezi mungu atakusaidia.

    Ally Kassim Abdallah

    October 31, 2011 at 12:49 PM

  18. pole sana kamanda wetu tupo pamoja daima

    zakaria

    October 31, 2011 at 12:50 PM

  19. Tunakuombea Mungu upate nafuu mapema

    David

    October 31, 2011 at 12:54 PM

  20. Mungu akufanyie wepesi ‘or your upcoming surgery’na upone haraka baada ya hapo Inshallah.

    Kuruthumu Mwamende

    October 31, 2011 at 12:55 PM

  21. Yote ni hali ya maisha ya mwanadam natumain mungu atakusaidia kwa hili.

    Zani

    October 31, 2011 at 12:59 PM

  22. pole sana kaka na ugua pole!…

    Denilicious

    October 31, 2011 at 1:07 PM

    • Get well soon camander urudi kwenye mapambano watanzania tuko nyuma yako kwa maombi na kufunga iliupone haraka kwa upasuaji unaoendea

      Joachim

      October 31, 2011 at 1:22 PM

  23. Pole sana kwa maradhi yaliyokusibu. Tuko nyuma yako tukikesha kwa sala na maombi, Mwenyezi Mungu akuponye na kukulinda.Amen

    Peter Msirikale

    October 31, 2011 at 1:13 PM

  24. Mwenyezi Mungu akujalie afya njema, urudi kuendelea na ujenzi wa taifa letu

    lyimo

    October 31, 2011 at 1:16 PM

  25. Kaka Zitto pole sana kwa maradhi niko na ww mbali lakini ninaamini Sara na Maombi ninayo kuombea kwa Mwenyezi Mungu yatakufikia na yatatenda kazi amini utapona kabisa Mungu akutie nguvu kaka pole kwa maradhi

    Baraka Daniel Kubuka

    October 31, 2011 at 1:22 PM

  26. I pray for your full and quick recovery, God be with you..

    Martha

    October 31, 2011 at 1:22 PM

  27. Kaka MUNGU yuko pamoja na wewe amini kua utapona muda na siku si nyingi coz hakuna jambo lisilo wezekana kwa MUNGU,

    Martin sostin

    October 31, 2011 at 1:31 PM

  28. Pole sana Mh. Zito. Tunashukuru kwa taarifa, tunakuombea as long as tatizo limejulikana. Get well soon

    Nicholaus

    Nicholaus

    October 31, 2011 at 1:31 PM

  29. Pole sana Bro.Zito tunakuombea kwa MUNGU na tunaamini utapona mapema na kurudi katika mapambano.

    Godfrey Mkumbo

    October 31, 2011 at 1:56 PM

  30. Mwenyezi Mungu wa Rehema akuponye na maradhi yote urudi Tanzania ukiwa na nguvu ya kupambana na ufisadi. Tutakumiss sana kwenye mchakato huu wa Katiba kwa kuanza ila naamini Mungu mawazo yako yataheshimika sana hapo baadaye. Huyu mwenye kukuumba akujalie hekima, afya na maisha marefu. Upole na utoke kitandani kwa nguvu za uweza wake. Hata hivyo tunamshukurU Mungu pamoja na uvumi wote kwa wale waliokuwa na nia mbaya na uhai wako hakika wameaibika maana yote hayo ni kwa kazi ya yule mwovu. Uwezo wako wa kutuhabarisha juu ya afya yako ni kwa kazi ya yule mwenye utukufu mbinguni na duniani. Get well soon our brother. God loves you than any human kind.

    Winner

    October 31, 2011 at 1:56 PM

  31. pole sana my future presidar mungu akupe unafuu inshallah utapona na kurejea homu ukiwa fit .. tuko pamoja na allah anasikia dua zetu

    Mummie Ksummer

    October 31, 2011 at 2:07 PM

  32. POLE SANA KAKA TUNAKUOMBEA MUNGU AKUPE NGUVU NA UIMARA KAMA MWANZO

    MSEMO RAMLA

    October 31, 2011 at 2:10 PM

  33. Get well soon brother, we miss you dearly. May the good Lord give you a quick recovery.

    Harry James

    October 31, 2011 at 2:23 PM

  34. alhamdulillah kwa maelezo yako mazur na tunaamin utapona haraka na kurudi nyumbani coz we need u kabwe

    salum mustapha

    October 31, 2011 at 2:32 PM

  35. Mungu ni Mkubwa
    pole sana utakuwa salama bado Taifa linakuhitaji sana.

    Cleophace

    October 31, 2011 at 2:35 PM

  36. Pole sana mungu atakusaidia utapona na utarudi kulitumikia taifa lako

    Kabange Hassan

    October 31, 2011 at 3:23 PM

  37. Mungu ndiye mponyaji na ndiye mwamuzi wa afya zetu…Naamini atakuponya na kukurejesha katika hali njema ili uendelee na majukumu yako ya ujenzi wa taifa! GET WELL SOON HON. ZITTO KABWE!

    JOSEPH LABIA

    October 31, 2011 at 3:28 PM

  38. Get well soon…

    jerry

    October 31, 2011 at 3:28 PM

  39. Hasta La Victoria Siempre, Comrade !

    Ezekiel Kamwaga

    October 31, 2011 at 3:34 PM

  40. Mungu atakusaidia utapona na hatimaye kurudi kuja kuendelea na ujenzi wa Taifa letu! get well soon.

    Chuchuba, Amatus

    October 31, 2011 at 3:37 PM

  41. Pole sana, God is with you, utapona.

    Fabian Ninga

    October 31, 2011 at 3:52 PM

  42. Ploe sana kaka yetu…Mungu akujalie upone haraka uweze kuwahi kikao cha Bunge maana mchango wako ni mkubwa sana….Tunazidi kukuombea!

    Christopher MJ

    October 31, 2011 at 3:54 PM

  43. tunakutakia afya njema kiongoz wetu na mzalendo wetu, mola akutangulie pia kwa tiba iliyobakia

    METHOD JOHN MBILINYI

    October 31, 2011 at 4:00 PM

  44. POLE SANA MKUU

    MAFWIMBOBARAKA

    October 31, 2011 at 4:14 PM

  45. Pole sana ndugu! U will recover in Jesus name,ndugu Mheshimiwa! Ubarikiwe!

    Remmy Mushi

    October 31, 2011 at 4:26 PM

  46. Get well soon brother, mungu wetu ni mwaminifu alisema nitapigana nao wale wanaopigana nawe!! nitashindana nao wale wanaoshindana nawe. so mwangalie mungu naamini watashindwa na mungu atazidi kukupigania daima paka atakapoamua mwenyewe na siyo aliyechini ya hili jua. mungu baba akupe wepesi kaka yetu mpendwa, najua kama unajua watz twakupenda sana.

    amina mchape

    October 31, 2011 at 4:54 PM

  47. Maradhi ni sehemu ya maisha ya mwanadamu, tunakuombea uzima na afya njema. mungu yu pa1 na wewe na bado tunahitaji juhudi zako za kupambana na uozo ndani ya serikali yetu.

    william Jotham

    October 31, 2011 at 5:02 PM

  48. Kaka pole hope utakuwa mzima soon na kuendelea na harakati za kuleta mabadiliko kuifikisha Tanzania pale tunapotarajia ifike. GET WELL SOON.

    Sadock Josephat

    October 31, 2011 at 5:11 PM

  49. Mh uwe na moyo mkuu hasa wakati huu wa changamoto za kiafya, hayo hayana budi kutokea, tuko pamoja, tunakuombea kwa Mungu azidi kuimarisha afya yako ili urudi kuwatumikia watanzania maskini wanaohitaji utumishi wako

    Jefta Chaulo

    October 31, 2011 at 5:53 PM

    • Pole sana kaka Zitto Kabwe, kaka yetu wa kujidai hapa KIGOMA, Tunakuombea Mungu yupo pamoja nawe utapona na utarudi kuendelea na kazi za Kulijenga Taifa.

      Mimi Dada yako Lilian – Kigoma

      Lilian Francis

      October 31, 2011 at 6:37 PM

  50. Pole sana kaka, tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu, kwa pamoja twakuombea kwa Mungu upone haraka kaka, emen

    Abbas matan

    October 31, 2011 at 6:27 PM

  51. pole sana kaka..utapona na pia nakuombea sana..

    fidi

    October 31, 2011 at 6:41 PM

  52. Pole sana mwanamabadiliko

    ahmes

    October 31, 2011 at 6:48 PM

  53. Pole sana kaka…GET WELL SOON!!

    Geofrey Tumaini

    October 31, 2011 at 7:03 PM

  54. Pole kaka,nakutakia afya njema.

    Peter

    October 31, 2011 at 7:17 PM

  55. Mungu mwingi wa rehema akuponye kabisa kwa jina la Yesu. hatutaki kupoteza wana harakati hata mmoja hadi nchi hii imepata ukombozi

    Willy Shehemba

    October 31, 2011 at 7:39 PM

  56. Chadema we are together up to the end of the game, nakutakia upone haraka ili uje uzidi kututetea wananchi wako…

    fredy Chokela.

    October 31, 2011 at 8:29 PM

  57. pole sana sana mwanamapinduzi halisi kijana shupavu,,mungu atakujaalia afya bora na nguvu haraka sana yaillah yarasul allah ndie mueza wa kila jambo hakuna awezae zaidi yake.
    kaka zitto usimsahau allah kwani yy ndie muokozi wako hakuna anaye weza kama mungu yy ndie aliye kupa hayo maumivu makali na akayapunguza vile atakavyo
    Hakuna mjuzi zaidi ya allah
    aman na afya bora
    vyote tumtegemee allah
    pole sana kk mungu atakujaalia na utarudi nyumbani ukiwa na afya bora kabisa

    shaabani k

    October 31, 2011 at 9:58 PM

  58. u ll be well soon. God will heal u.

    dorosella

    October 31, 2011 at 10:34 PM

  59. pole sana kaka tunakuombea upone na urudi salama uje upiganie haki za wanyonge walio wengi wasio jiweza mungu aendelee kulinda katika matibabu.

    rehema kiwelu

    October 31, 2011 at 10:37 PM

  60. imana ni ishimwe chane,twetwe abhaha bhi kigoma tulashimye chane kulonka amagambo yawe .ugize neza kamanda wachu hakili imitima yachu ilahoze.inshallah mwenyezi mungu akupe afya njema.

    farida

    October 31, 2011 at 11:12 PM

  61. mungu akuponye ili urudi kuendeleza mapambano na wezi wa mali ya uma

    mwasipu, HA

    October 31, 2011 at 11:55 PM

  62. Pole sana ndugu mungu atakuepusha na maradhi sote ni binaadam wala mungu hachagui sote tuliumbwa na sote lazima tuugue hakuna kiongozi wala asiekua kiongozi.maneno yako ya busara na afya yako kwetu ni faraja mungu atakujalia kwa uwezo wake AMINI.LEO KDGO NITAPATA USINGIZI MATIBABU MEMA USIKU MWEMA.

    Sungura hamza sungura

    November 1, 2011 at 12:21 AM

  63. Polee sana Kiongozi

    Ramadhan J. Chatta

    November 1, 2011 at 7:01 AM

  64. pole sana rafiki yangu Z.KABWE ZITTO,kwani tayari turijawa na hofu,baada ya uvumi wakila namna lakini tunakutegemea sana kama kioo cha uongozi nategemea kukuona tena Tz,mwanza.Mungu akujarie uredi salama.

    Simon Philemon

    November 1, 2011 at 8:39 AM

  65. Pole sana mkuu naamini kwa kuvu za Mwenyezi Mungu atakuponya na kuendelea na majukumu yako ya kutetea taifa letu ambalo baadhi ya watu wachache wanapora mali za walipa kodi bila hata huruma. Mungu akuwezeshe urudi salama amini.

    Eliaringa Macha

    November 1, 2011 at 9:00 AM

  66. Rafiki Zitto, pole sana kwa maumivu unayopitia.Ninaamini utakuwa salama punde na utarudi kupigania demokrasia,haki na maendeleo ya kweli ya nchi hii.Taifa bado linakuitaji sana kwa kipindi kirefu kijacho…Mungu awe nawe!

    Martin

    November 1, 2011 at 9:44 AM

  67. Pole sana muheshimiwa. I strongly believe that our God who is the healer of all human sickness will stand by your side and heal you for He knows how hard and tirelessly you have worked to make our country Tanzania a better place. I wish you a quick recovery and may your strength be renewed so that you can continue to fight the evil in Tanzania.

    Sekunda Lyamuya

    November 1, 2011 at 9:45 AM

  68. Hi my brother,Greetings from Kigoma,Things here Seems to be good.Pole sana,Tunamshukuru sa Mungu kwakuwa amekuponya ni mengi sana tumeyasikia juu yako ila sisi tuna kupenda,tunakujali na tunakuheshimu sana mbunge wa jimbo letu la Kgm Kaskazini.Tuko pamoja
    Juma Jocker

    Juma

    November 1, 2011 at 10:32 AM

  69. Kamanda pole sana

    Amedeus mallya

    November 1, 2011 at 11:07 AM

  70. Mungu akusaidie ili ufanyiwe upasuaji wenye mafanikio ili urudi kuendelea na vikao muhimu vya Bunge pamoja na ujenzi wa Taifa hili changa.

    ENOCK

    November 1, 2011 at 11:53 AM

  71. pole sana mungu yu pamoja na we unatupa inspiration ss ambao tuko vyuoni; get well soon!!!

    feruzi mbingo

    November 1, 2011 at 11:54 AM

  72. pole sana mwanamabadiriko tunakuombea kwa mungu utapona na kazi yako itaendelea watu watakombolewa mungu awe nawe

    charles nilla

    November 1, 2011 at 12:11 PM

  73. Pole Kaka, Mungu akijaze uzima,urejee katika afya njema iliuweze kuendelea na mapambano ya kutetea haki na lasrimali zetu watanzania.

    Allen Francis

    November 1, 2011 at 12:20 PM

  74. Pole sana. Pona na urudi salama tuendeleze mapambano. Hali ya nchi bado ni tete.

    Jimmy Kalugendo

    November 1, 2011 at 1:27 PM

  75. Aisee brother tunashukuru sana kusikia hivyo kutoka kwako mwenyewe, Maana katika hali ya ubinaadam kuzusha mambo ambayo mtu huna uhakika nao ni dhambi km kisemavyo kitabu kitukufu kuwa uongo ni dhambi. Sina mengi kwenye hili isipokuwa tu Mungu akufanyie wepesi na Inshaalwah Jazak la Kheri urudi katika hali yako ya kawaida katika Mabadiliko ya kweli ya Nchi yetu.

    Amina.

    Chapa S. Magotti

    November 1, 2011 at 2:00 PM

  76. pole saana thnx to God u made it

    justin

    November 1, 2011 at 2:38 PM

  77. Pole sana Mh Zito.

    Mungu atakujalia utarudi katika afya yako tena.

    Mungu akubariki.

    Victor Sungusia

    November 1, 2011 at 2:51 PM

  78. pole sana Bro.

    mruta julius

    November 1, 2011 at 3:09 PM

  79. Pole sana tutakuwa pamoja kwenye mabadilko

    Alex Kivuyo

    November 1, 2011 at 3:14 PM

  80. pole sana kaka dua zetu kwa Mungu za watanzania hasa wanamabadiliko zipo juu yako.Mungu atakuponya na atakuweka huru kutoka kwa maradhi yanayokusumbua.

    Mkomwa,Frank

    November 1, 2011 at 3:42 PM

  81. Mungu yupo pamoja na wewe utapona haraka tu

    Mwande

    November 1, 2011 at 4:04 PM

  82. Get well Sooon our Master…we were dilema abt yo health but now at least we are hope God may let U recover and reJoin us in our daily schedules….!
    Just trust in ALLAH who makes us Breath until this sec.
    SO SORRYY……y
    ZITTO!

    Wilson

    November 1, 2011 at 4:23 PM

  83. 2nakuombea Mungu akulinde urudi nyumbani salama.Amen

    Salome Magesse

    November 1, 2011 at 6:23 PM

  84. ,praying for you brother,upate nafuu na urejee nyumbani salama.Mungu akujalie operation iende salama na upone kabisaa tatizo linalokusumbua.U mean alot to us,especially to our region Kigoma.
    Much love to you brother,

    gabriel mayengo

    November 1, 2011 at 7:41 PM

  85. Mh. Zitto yote hayo ni matokeo ya mapambano dhidi ya mabadiliko, Mungu akutie nguvu na hakika kiu yako Mabadiliko itakatika siku moja

    Chris Ndibato Kabazu

    November 2, 2011 at 6:13 AM

  86. Pole sana… Mwenyenzi Mungu atakujalia upone haraka lakini this is very eye open thing.. Ukirudi please champion for our health system… Sasa surgery hiyo tu wakupeleke India? Inashindikana Tanzania? Imagine ni watu wangapi wanaweza kua wanakufa just for not having that simple surgery in Tanzania? Inasikitisha sana sana kwa nchi kutojali hizo hela

    Simon

    November 2, 2011 at 6:49 AM

  87. Pole sana Mheshimiwa. Tunakuombea na Mungu akuponye urudi katika Majukumu ya Ujenzi wa Tanzania yetu

    Maselle Maziku

    November 2, 2011 at 6:56 AM

  88. Pole sana ndugu ye2 mpendwa na me binafsi km mwana mabadiliko nime furahi sana kusikia kwamba unaendelea vizuri na mungu atazid kukusaidia na utapona mwana mabadiliko wangu.

    Dickson Naomi John

    November 2, 2011 at 7:39 AM

  89. Mwenyezi muumba mbingu na ulimwengu akujalie afya njema we love kwa niac ya vijana wa shnyanga.

    Robert kanumba

    November 2, 2011 at 1:05 PM

  90. Mwenyezi muumba mbingu na ulimwengu akujalie afya njema we love u kwa niac ya vijana wa shnyanga.

    Robert kanumba

    November 2, 2011 at 1:06 PM

  91. POLE SANA MUNGU NI MWEMA ATAKUSAIDIA HATA BAADA Y UPASUAJI HUO UTARUDI NYUMBANI SALAMA.

    johari

    November 2, 2011 at 2:27 PM

  92. Pole kwa yote kaka na tunakuombea kwa allah!

    Hamisi Matemelela

    November 3, 2011 at 12:43 AM

  93. mungu akujaalie upone haraka na akupe nguvu pamoja na ujasiri na tunamuomba sana inshaaalah

    Musa Amiri

    November 3, 2011 at 1:28 PM

  94. Vipi mhe unaendereaje?

    Ally lilangela hamis

    November 3, 2011 at 10:22 PM

  95. pole kamanda naamini maombi yetu yamepokelewa.mungu yu pamoja nawe ktk kila jambo.pona haraka tuje kuendeleza mapambano ya kudai uhuru wetu.

    safina

    November 5, 2011 at 8:02 PM

  96. Pole sana mhe. Zitto, think how many stopped breathing since the year started? Thanks to God b’cause he made you alive till today with hope of recovering. It is time to say thanks to God b’cause he’s still loves you, and has made you strong even to give us updates about your illness, we are praying for you. Karibu tena ktk utendaji wa majukum, Taifa la Tanzania bado linakuhitaji Kaka.

    *By ALFRED, Kiezera
    member of CHASO-UDSM

    Kie

    November 6, 2011 at 9:38 AM

  97. pole sana mheshimiwa zitto na ni dua yangu na yetu wanamaendeleo afya yako irejee na uwe na nguvu ya kupambana zaidi kwa maendeleo ya taifa letu. Mungu ibarikiki Tanzania!

    sam de joe

    November 7, 2011 at 5:08 PM

  98. pole sana mh. Mi nakuombea afya njema ili uendeleze gurudum ulipoishia pia bora ulivyotoa taarifa sahihi juu ya afya yako maana hawana jema wabaya kumzushia mtu kifo wanaona kawaida ni mitihan ya maisha na kuumwa ni jambo la kawaida istoshe kuna fungu lako ktk ugonjwa wako maana mgonjwa c sawa na mzima usihuzunike hata nabii ayub aliumwa sana lakin hakukufuru alimshukur mungu.get wel

    nusrat hanje

    November 9, 2011 at 11:09 AM

    • Pole sana mzalendo wa taifa,Mungu yu pamoja nawe daima,Maombi ya watanzania kwa Mungu juu ya afya yako naamini yanaendelea kujibiwa ”UTAPONA KABISA”na kurudi kuendelea na mapambano ya ukombozi wa taifa hili.
      ASANTE KWA TAARIFA YA AFYA YAKO.
      Tutazidi kukuombea.
      By: Rozzo Haji,FROM (Zanzibar Institute of Financial administration).

      rozzo haji

      November 10, 2011 at 4:51 PM

  99. Pole sana kiongozi wangu, Mungu azidi kuwa nawe. Unapewa pole sana na rafiki yako Moris Simbaza kutoka Kagunga.

    MIFORO ESSAU

    November 14, 2011 at 8:40 AM

  100. pole sana kaka yangu hayo ni maneno tu kwani hata wao walikuwa wakijiuliza nani ataleta changamoto katika ripoti ambayo ulimuomba spika wa bunge aiunde ili kumchunguza katibu mkuu wizara ya nishati na madini kiukweli tunakuombea upone salama na uje uendelee na kutetea maslahi ya watanzania
    MUMGU IBARIKI TANZANIA ,MUNGU MBARIKI Mh.Zitto Kabwe

    Innocent Minja

    November 29, 2011 at 4:34 PM

  101. Pole sana mwana mabadiliko.
    Kwa imani tutashinda maradhi

    Alphonce G Maseke

    November 29, 2011 at 8:09 PM

    • pole sana mpambanaji ila tujitahidi basi tutetee uchumi wetu na mwisho wa siku tutibiwe kwenye hospital zetu

      Herman Mremi

      February 6, 2012 at 3:35 PM


Leave a comment