Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

PRESS RELEASE: HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

with 11 comments

HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012

•       Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini
•       Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’

Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 ya wabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge isipokuwa tu kama;

(a)    “taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni; ”Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa “hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri”.

Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo Bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’ hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi. Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni.

…………………………….
Kabwe Zuberi Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.

Written by zittokabwe

April 22, 2012 at 7:17 PM

Posted in Uncategorized

Tagged with

11 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Kaka watanzania wenye uchungu na nchi tuko nyuma yako…may God give you strength maana vita hii sio ndogo,but we will win the battle.

  masabho

  April 22, 2012 at 7:32 PM

 2. Tunakushuru kijana wetu maana hiyo ndiyo kazi tuliyokupa uifanye,Rehema na Amani viwe na wewe hadi siku ya kujikomboa tutokane na ukoloni huu uliopo mamboleo,Ni wewe tunakutegemea usukume gurudumu hili la maendeleo kwa kupinga uovu na uzembe unaofanywa na baadhi ya viongozi wanaopewa madaraka ili kleta amani na mwelekeo wa maendeleo kwa Watanzania.Mimi niko pamoja na wewe naamini kuwa hata Dua zangu zitakutia nguvu,Mungu awe na wewe kwa ulinzi na ujsili maana ndiyo chanzo cha maarifa.

  Kutoka Kwa
  Baraka Peter Nzovu
  Kigoma mjini-Mtaa wa Lake Tanganyika.

  • Hii imeka sawa,uwajibikaji ni muhimu nahisi kila mtu alikula kiapo,sasa waelewe maana ya kiapo unaposema nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wasipoilinda na kuitetea waweza kufungwa,wasiishie kujiuzuru wafikishwe vyombo vya sheria.

   Joshua Mwakilasa

   April 23, 2012 at 9:28 AM

 3. mimi kwa upande wangu tusishabikie vyama kwa mtazamo wa udini na ukabila ambao sasa unashamiri lakini watu hawataki kukubali ukweli .tuunge hoja za msingi bila kujali itikadi za kidini au kisiaa tukifanya hivyo tutafika mahali pazuri .mungu ibariki tanzania

  abdallah j msaghaa

  April 22, 2012 at 9:12 PM

 4. safi sana zitto wewe na safu nzima ya CDM ni viongozi wa kuigwa nchi hii, lazima mamluki wapigwe chini!!!

  mahenge

  April 22, 2012 at 9:40 PM

 5. Kweli zitto unafaa kuwa ata rais kutokana na kutoa hoja za msingi bungeni na hata nje ya bunge umemzidi hata docta slaa kwa 79.9 mm ni mwana ccm lakin mm nachagua mwenye hoja za msingi kama za kwako kama vip upewe ww kiti cha urais 2015 utapata kula zangu

  Alex felician

  April 23, 2012 at 12:21 AM

 6. Kamanda hongera sana tunakukaribisha Arusha TOWN J5 maana huku arusha kumekucha kila mtu amekukubali mno so tutakuwa na mkutano mkubwa Arusha njoo uwaeleze wanaarusha jinsi hao wezi wanavyohujumu hili taifa ………….. big up kamanda

  Amos Isaac

  April 23, 2012 at 12:30 AM

 7. Kaka Zitto Mungu akutangulie katika hili na nikuhakikishie, watanzania lukuki tuko nyuma yako kwa sala na kusubiri chochote mtakachoamua sisi wananchi tufanye endapo wabunge wetu wazalendo mtaona njia hiyo imekwama.

  Wazee hawa tumewachoka. Wametafuna nchi bila huruma na wanapoambiwa wawajibike kisiasa bado wanagoma. Washenzi hawa. Wakati mwingine watanzania tunatamani viongozi wetu lingewatokea balaa kama lililoikumba nchi fulani ya magharibi ambapo ndege ilianguka na kuua asilimia kubwa ya viongozi wake wa juu. Hata hivyo hivyo bado tulio wengi tunaamin i Mungu atafanya jambo.

  Ila watanzania tunakuomba comrade Zitto mshupalie ile hoja ya kupunguza miaka ya kugombea uraisi ili mwaka 2015 vijana kama wewe na Mh. Makamba muweze kugombea tuachana na wazee hawa hawana jipya tena.
  Big up…

  Richard Alphonce

  April 23, 2012 at 12:48 AM

 8. Kaka hii safi sana ndo inayotakiwa! Hatuhitaji watu wengi sana kuleta uhamsho katika inchi watu wachache sana ambao wamemaanisha ! Tunahitaji watu kama Zitto !

  REUBEN MWANJA

  April 23, 2012 at 4:19 PM

 9. Kijana mungu kakupa akili na unauwezo wa kuitumia vilivyo,wakati unatoa hoja ccm hawakujua kama kuna mtego mdogo na wameshindwa kuutegua.Hoja ilipoingia walikuja juu na kuonekana yao na wanaweza,sasa tendeni wameingia mitini.
  Lengo lao kuwahadaa wananchi,tupo nyuma yako zitto, kamwe haturudi nyuma.uongozi ni kipawa na si umri.
  Big up……

  gilagiza

  April 23, 2012 at 4:50 PM

 10. Mhe Zitto mungu akutangilie kwa jitihada zako kwa niaba ya Watanzania wenzako. Tuko nyuma yako kwa maombi zaidi.

  juma kiolobele

  April 25, 2012 at 9:07 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: