Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

PRESS RELEASE: Ndugu Zitto ziarani Ulaya

with 12 comments

PRESS RELEASE

 Ndugu Zitto ziarani Ulaya

Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini ndugu Zitto Zuberi Kabwe ameanza ziara ya kikazi nchini Ujerumani ambapo atahudhuria na kuhutubia Mkutano mkubwa wa masuala ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ujerumani na Africa. Mkutano huo “Economic Conference: Commitment to Africa Initiative” utafanyika Jijini Berlin kuanzia tarehe 9 – 11 Desemba 2012 na umeandaliwa na Wizara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo ya Serikali ya Ujerumani.

Katika ufunguzi wa Mkutano huo ndugu Zitto atatoa mada kuhusu mgongano wa maslahi kati ya Kampuni binafsi na Jamii ambapo ataongelea suala zima la makampuni makubwa ya kimataifa yanavyonyonya rasilimali za Afrika bila kuwajibika kulipa kodi na kuendeleza jamii zinazozunguka shughuli zao. Atazungumzia pia mitaji kiduchu inayokuja Afrika na fedha nyingi inayotoroshwa Afrika kupitia rushwa, ukwepaji kodi na wizi wa rasilimali. Afrika inapoteza zaidi ya dola za kimarekani 583 bilioni kila mwaka kutokana na utoroshaji wa fedha unaofanywa na makampuni ya kimataifa kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa Afrika. Hata hivyo Afrika inapokea takribani dola za Kimarekani 80 bilioni tu kwa mwaka kutokana na Uwekezaji (FDI) na Misaada (foreign Aid). Tanzania ni moja ya nchi inayopokea misaada mingi kutoka nje na moja ya nchi ambayo rasilimali zake zinatoroshwa na baadhi ya viongozi wake kutorosha fedha na kuzihifadhi kwenye mabenki ya Ulaya kama Uswiss.

Mnamo tarehe 11 Desemba ndugu Zitto atakuwa kwenye jukwaa moja na Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani kuzungumzia namna bora ya kushirikiana kati ya Ujerumani na nchi za Kiafrika. Miongoni mwa mapendekezo ya Zitto ni kuondokana na mfumo wa sasa wa ushirikiano wa misaada na badala yake kuwe na ushirikiano wa kujengeana uwezo ili kila nchi iweze kuhimili maendeleo yake yenyewe.

Katika ziara hii Zitto atakutana na Mawaziri Wakuu wa majimbo ya Nord Rhein Westphalen jimbo ambalo limefanikiwa sana katika vita dhidi ya ukwepaji kodi unaotokana na raia wa Ujerumani kuficha fedha kwenye mabenki ya Uswiss na wa jimbo la Lower Saxony kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ukarabati wa Meli ya Liemba na kujenga mahusiano kati ya Mkoa huu na Mkoa wa Kigoma pia kati ya mji wa PapenBurg na Manispaa ya Kigoma.

Zitto anatarajiwa kutembelea baadhi ya nchi nyingine za Ulaya na kukutana na watu mbalimbali katika kuimarisha mtandao wa kimataifa dhidi ya utoroshaji wa fedha kutoka Afrika (illicit money transfer). Pia atakutana na watu binafsi wenye ujuzi na weledi katika masuala haya ya kupambana na watoroshaji wa fedha. Zitto anataraji kurudi nchini mnamo tarehe 16 Desemba 2012. Kwa namna itaakavyowezekana umma utapewa taarifa kuhusu ziara hii kupitia akaunti ya twitter na facebook ya ndugu Zitto. Pia mada zote atakazowasilisha zitawekwa kwenye blogu ya zittokabwe.com kila itakapowezekana.

Waziri Kivuli wa Fedha na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni anawatakia Watanzania wote kila la kheri katika Sikukuu ya Uhuru wa Tanzania Bara. Utu, Uzalendo, Uadilifu na Uwajibikaji ni silaha muhimu sana za kujenga Taifa lenye heshima na jamii ya watu wenye fursa za kuendeleza maisha yao kwa haki na amani. Tutimize wajibu wetu katika kuijenga Tanzania tuitakayo kwa ajili yetu na kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini

8 Desemba 2012, Dar es Salaam

Written by zittokabwe

December 8, 2012 at 5:27 PM

Posted in Uncategorized

12 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. Mkuu kila la kheli, tunakuombea sana watanzania wenzio.

    Philimon Godfrey

    December 8, 2012 at 5:43 PM

  2. Reblogged this on A NEW ERA OF CHANGE IN TANZANIA.

    Philimon Godfrey

    December 8, 2012 at 5:45 PM

  3. I would like you to say much on that insue so that we can be benefited with foreign aid. All the best mkuu.

    Shaban mahwisa

    December 8, 2012 at 5:50 PM

  4. Nakutakia safari njema na yenye mafanikio!

    James Raphael Mdima

    December 8, 2012 at 6:09 PM

  5. plz dear lod give him backup ——————————

    Ramso Msongera

    December 8, 2012 at 6:58 PM

  6. kila la kheri kaka katika juhudi zako za kutukomboa tupo pamoja nawe

    idd mbaraka

    December 8, 2012 at 10:13 PM

  7. Safi sana Muheshimiwa

    Mussa

    December 8, 2012 at 10:19 PM

  8. Hongera sana kutuwakilisha kaka Zitto, nakutakia ziara njema. Hizi TNCs zinazojishughulisha na madini sio tu kwamba zinakwemba kulipa kodi, bali zinaharibu sana mazingira hasa vyanzo vya maji ambavyo vinatumika na local communities. Wawekezaji hawajali kabisa health & safety standard upande wa mining industry, hiyo uranium itayoanzwa kuchimbwa hapo SELOUS na warusi ambao wana sifa mbaya ya corruption na kutojali afya za watu na mazingira nchini kwao Russia, nina wasiwasi wengi tutakufa kama kuku kwani vumbi la uranium ni sumu kali na vumbi hilo litaathiri mto Ruaha na mto Rufiji. Mito hiyo ni muhimu sana kwa uvuvi & water supply na inakatisha mikoa mingi. Halafu kwao Russia kuna uranium wamekimbia regulations na environmental groups (Greenpeace, etc.) na kuja kuchimba barani Africa sababu tunawapa tu kama jungu au karanga.

    Eeh Mola tuangalie waja wako utuepushe na sumu ya uranium (silence killer).

    Rose Matiku

    December 9, 2012 at 11:41 AM

  9. Tuna kutakia safari njema. Uiwakilishe vyema nchi yetu na Bara letu kwa ujumla.

    David

    December 9, 2012 at 5:44 PM

  10. kila la kheri Mhe. Zitto, tunaamni katika juhudi ndipo mafanikio yanapatinka. safari yako iwe yenye kuzaa matunda mema
    kwa pamoja tunaweza.

    FERDIANA BRASTUS MUKAMA

    December 11, 2012 at 10:24 AM

  11. Thats what a true leader z all about, you are truly presidential figure, cheers:)

    aldo a. kamugisha

    December 13, 2012 at 5:46 AM


Leave a comment