Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Sera ya Gesi: Maoni ya awali #RasimuyaGesiAsilia #TanzaniaNaturalGasPolicy

with 6 comments

Jana wabunge tumegawiwa rasimu ya Sera ya Gesi Asilia. Leo Wizara ya Nishati na Madini itaendesha semina kwa wabunge kuhusu sera hiyo.

Draft 3- The Natural Gas Policy of Tanzania -2013

Draft 3- The Natural Gas Policy of Tanzania -2013(Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia)

Nimepata muda kidogo wa kuipitia hii rasimu ya 3 nikiwa safarini kwenda Tabora kwa shughuli za chama changu cha CHADEMA , nina maoni ya awali kama ifuatavyo;

1). Kwa ujumla kupata Sera mpya ya gesi asilia ni hatua muafaka japo imechelewa sana. Hata hivyo ni bora kuchelewa kuliko kutofika kabisa. Ni vema wananchi wachukue fursa hii kuisoma na kuijadili rasimu hii na kuiboresha ili iwezeshe wananchi wenyewe kufaidika na utajiri ambao nchi yetu imejaaliwa.

2). Sera ina jumla ya sura Sita. Sura ya kwanza ya inaweka sababu na masuala ya jumla na utangulizi . Sura ya pili inaweka sababu za kuwepo kwa sera mpya na madhumuni maalumu, Sura ya tatu ndio yenye matamko ya msingi ya kisera (fundamental policy issues) ikiwemo masuala ya miundombinu ya gesi kwa ajili ya soko la ndani, usimamizi wa mapato yatokanayo na gesi asilia na masuala ya ‘’ local content’’. Sura hii pia imezungumzia masuala ya uwazi na uwajibikaji. Sura ya nne ni masuala ya mfumo wa kisheria na udhibiti na sura ya tano ni taasisi za usimamizi wa sera ya gesi asilia. Sura ya sita ni hitimisho. Kila sura imeweka matamko ya kisera.

3). Rasimu ya sera imeshindwa kutofautisha suala la Mafuta na Gesi kuwa ni suala la Muungano au sio suala la muungano katika muktadha wa Katiba mpya inayojadiliwa sasa. Hii inadhihirisha umuhimu wa kuwianisha mchakato wa katiba na michakato mingine inayoendelea nchini. Hivi sasa Zanzibar inajiandaa kuwa na sera na sheria yao ya mafuta ya gesi, iweje sera hii itamke gesi asilia ni mali ya Jamhuri ya Muungano wakati upande mmoja wa Muungano utakuwa unafaidi utajiri wake peke yake? Rasimu ya sera imeshindwa kutambua kuwa kuna vitalu vya mafuta na gesi ya (vitalu namba 9-12) vimesimamisha shughuli kwa sababu Serikali ya Zanziabar haitambui mafuta na gesi kuwa suala la muungano. Rasimu inapaswa kuzingatia jambo hili kabla ya kupata sera yenyewe.

4). Rasimu imetamka katika ukurasa wa 9 kwamba sera hii haitambui shughuli za utafutaji (‘This policy document only covers mid-and downstream segments’ ndio nukuu ya neno kwa neon ya Sera hii). Hiki ni kichekesho cha milenia .

Taifa linawezaje kuandika sera ya gesi asilia kwa upande wa uchuuzi tu (biashara) na kuacha kazi yenyewe haswa ya utafutaji na uchimbaji (exploration and exploitation are upstream). Shughuli za utafutaji na uchimbaji ndio msingi haswa wa sera ya gesi asilia.

Mikataba yote huamuliwa kwa kuzingatia kwanza utafutaji, shughuli nyingine ni biashara tu ya kitakachogunduliwa . Rasimu kuacha kabisa eneo la utafutaji na uendelezaji (upstream) ni sawa na kutokuwa na sera kabisa.

Kwa namna eneo hili lilivyoachwa kuna harufu ya mkakati wa siri wa kuwanyima wananchi msimamo wa kisera kuhusu utajiri wao unavyonyonywa . Sentensi hii yenye maneno 10 katika uk. wa 9 wa kijitabu cha rasimu ya sera unaondoa kabisa umuhimu wa sera yenyewe wakati dhumuni kuu la sera linatamkwa uk.6 kwamba Gesi asilia ni mali ya wananchi wa ‘Jamhuri ya Muungano’ wa Tanzania’’ kurasa tatu baadaye zinaiondoa sera kwenye eneo hilo la umiliki wa mali hii ( Upstream). Tumeamua kuandika sera ya uchuuzi wa gesi asilia?

5). Rasimu katika 3.2.2(uk.24) imeweka matamko ya kisera kuhusu uwazi na uwajibikaji . Uwazi ndio eneo ambalo watanzania wengi walikuwa wanasubiri kwa hamu sana . Usiri wa mikataba katika sekta mbali mbali nchini ni chanzo cha ufisadi na uporaji wa utajiri wa mali yetu. Sera hii imeJibu swala hili? HAPANA. Sera haisemi ni namna gani mikataba itakuwa wazi kwa wananchi. Sera haisemi ni namna gani wananchi wataiwajibisha Serikali na vyombo vyake (Accountability) kwenye masuala ya mafuta na gesi. Sera imepiga porojo kuhusu uwazi na uwajibikaji. Bila misingi imara ya Uwazi na Uwajibikaji katika rasilimali ya gesi asilia, sera haina maana yoyote ile.

6). Serikali ni lazima ijue kwamba hivi sasa nchi yetu nchi tajiri yenye watu masikini.[i] sera ya gesi inapaswa kutuondoa kuwa nchi yenye laana ya rasilimali. Sera hii haina mwelekeo huo kabisa . Sera inapaswa kuwezesha wananchi kupata thamani ya maliasili yetu na kuwezesha matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na utajiri wa nchi.

Sera yetu lazima ioneshe dhahiri kwamba gesi asilia ni mali ya wananchi na uendelezaji na unyonyaji wa rasilimali hii utafaidisha wananchi kwanza na kwa ruhusa yao (Prior informed Consent Principle) sera ni lazima itamke hilo kinagaubaga.Sera ni lazima ionyeshe kuwa katika ushindani wa soko makampuni ya mafuta na gesi asilia yatapata faida ya halali ( normal retuns) ya uwekezaji wao na kwamba lolote linalozidi litabakia kuwa mali ya wananchi wa Tanzania.

Mkakati wa makampuni ya mafuta na gesi asilia ni kuhakikisha taifa linapata kiduchu na wanasaidia serikali kutoa majibu ya kipato hicho kiduchu. Watanzania hawatakubali tena.

7). Ni lazima tuseme kuwa tunataka utajiri wetu uwe neema kwa wananchi wetu, na siyo laana. Maendeleo yetu yatategemea ni namna gani tunafaidika na utajiri wetu wa maliasili kama gesi asilia. Sera ya Gesi Asilia itujengee imani hiyo. Hii Sera (Rasimu) inapaswa iangaliwe upya na hasa maeneo ya uwazi na uwajibikaji.

 

Kabwe Z. Zitto, Mb Kigoma Kaskazini

Tabora, tarehe 18 Mei 2013

6 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. i think kuna haja ya kila mtanzania kujua sheria, uchumi, na utaifa hata ikibidi kwa fimbo za matakoni

    Anthony Tukai

    May 18, 2013 at 4:34 PM

  2. Huu ni udhalilisha na upotefu wa taifa hili lililowekwa misingi na waasisi wetu, gesi nkitu gani kwa kuangalia manufaa na muktadha wa watanzania maskini wanaosubiri kesho yao itokayo kwa viongoz waliowachagua. Sioni haja ya kuletwa kwa hyo rasmu ya gesi kwa sasa kwan tayari wananchi hawajui chochote kinachohusu gesi yenyewe. Sioni hata haja ya waziri wa nishati na naibu wake kuendelea kukaa madarakan kwan ni ubabaishaji mtupu

    Elieza mwanyika

    May 18, 2013 at 4:38 PM

  3. Kuna haja ya kusitisha hili zoezi ili turudi kwenye katiba. Pamoja na kutizama swala la rasilimali hii (Mafuta/gesi) limekaaje ndani ya muungano kama Mh. Zitto anavyoshauri; lakini pia katiba itusaidie kuweka utaratibu wa adhabu ndani ya katiba kwa watu wanaotia aibu taifa letu kwa kuleta sera mbovu kama rasimu inavyoonesha kinachotarajiwa juu ya hili. Rasimu hii ni fedheha kwa kila mzalendo!

    Juma Ngeze

    May 18, 2013 at 7:48 PM

  4. WE THANK YOU MR. ZITTO FOR YOUR UNWAVERING STAND AND EXEMPLARY WORK.
    IN MY EARLIER COMMENTS I INDICATED 2 MAIN POINTS.

    NO.1), IS FOR THE PARLIAMENTARIAN TO DEMAND AN IMMEDIATE RESIGNATION OF THE MINISTER AND HIS DEPUTIES, NOT BECAUSE THEY DO NOT UNDERSTAND THEIR RESPONSIBILITIES, THEY HAVE LIED AND CONTINUE TO LIE TO THE PUBLIC FOR THEIR COVETED CORRUPTION ACTS OF SELLING OIL AND GAS BLOCKS TO FOREIGN COMPANIES IN SECRECY, KNOWING THAT THEY WERE NOT SUPPOSED TO UNTIL THE POLICY IS PRESENTED AND FULLY DELIBERATED BY MPS, CITIZEN, EXPERTS, AND ATTORNEY GENERAL CHAMBERS.

    NO.2), TO REMOVE OIL , GAS AND MINERALS FROM THE MINISTRY OF ENERGY, BE PLACED TO A SPECIAL COMMITTEE TO BE FORMED BY MEMBER OF PARLIAMENT, MINISTRY OF FINANCE, ATTORNEY GENERAL, EXPERTS. THE COMMITTEE TO DRAFT NEW POLICY WHICH WILL COVER ALL GRAY AREAS SIMILAR TO WHAT YOU MENTION, THE PRIORITY IS THE POLICY OF EXPLORATION, TANZANIA MUST BE FULLY PARTICIPATE IN EXPLORATION, UPSTREAM AND DOWNSTREAM, DISTRIBUTION AND MARKETING, HOW REVENUE COLLECTED SHOULD BE SPEND AND PART RESERVED. THIS IS A COMPLETE PACKAGE WHICH ENSURE TANZANIA FORMING NEW COMPANIES TO BE INVOLVED TECHNOLOGICALLY AND COMMERCIALLY. OWNERSHIP SHARE FOR JOINT VENTURES WITH FOREIGN COMPANIES, PERCENTAGE FOR TANZANIA , 60% MINIMUM FOR TANZANIA.

    NO.3), AFTER READING YOUR LATEST POSTING, SINCE THE MINISTRY HAS FAILED TO DRAFT THE POLICY, OPPOSITION CHADEMA SHOULD TAKE THE LEAD, DRAFT THE POLICY AS SUPPOSED TO BE AND PRESENT IT TO THE PARLIAMENT TO BE THE BASE FOR THE SPECIAL COMMITTEE TO BE FORMED.

    NO.4), FINALLY EVERY MTANZANIA MUST UNDERSTAND THAT, THE NEED TO BE STEADFAST TO COME FORWARD AND DEMAND THE FULL PARTICIPATION OF THE CITIZEN IN NATURAL RESOURCES, INCLUDING OWNERSHIP, EXPLORATION, PROCESSING, MARKETING, AND UTILIZATION OF REVENUE TO FUND DEVELOPMENT PROGRAMS SUCH AS INFRASTRUCTURE, EDUCATION, HEALTHCARE, AGRICULTURE ETC. NO MORE BORROWING MONEY TO FEED CORRUPT MINISTERS THROUGH FOREIGN COMPANIES, THEN ASK POOR PEOPLE TO PAY THE DEBTS. DEMAND TO USE THE COUNTRY NATURAL RESOURCES TO FUND DEVELOPMENT AND EXPENDITURE.

    NO5) A, ON GOING BUDGET DISCUSSION, MEMBER OF PARLIAMENT SHOULD FREEZE ALL PROPOSED NEW DEVELOPMENT IN EACH MINISTRY, UNTIL THE MINISTER OF FINANCE PRESENT A REPORT ON HOW THE EXISTING DEBT CREATED BY MOST OF INFRASTRUCTURE PROJECTS GOING TO BE PAID! WHICH ARE CONSTRUCTED BY MAJORITY CHINESE COMPANIES DELIBERATELY DENYING LOCAL CONTRACTORS AND ENGINEERS PARTICIPATION, DUE TO CORRUPT MINISTERS.

    NO5)B, THE TOTAL BUDGET OF PROPOSED NEW DEVELOPMENT FROM EACH MINISTRY, THAT MONEY SHOULD BE USED TO FINANCE NATURAL RESOURCES INVESTMENT BY TANZANIA COMPANIES. I) MINING, II) OIL AND GAS, II) YOUNG ENTREPRENEURS FUND FOR SMALL COMPANIES

    THIS IS TRANSFORMATION REQUIRED TO LIFT THE COUNTRY FROM POVERTY, AND PUT THE THE COUNTRY WEALTH IN HANDS OF TANZANIANS. NO MORE WASTING TIME FOR HANDOUTS AND BEGGING, INSTEAD WE USE OUR AVAILABLE RESOURCES TO UNLOCK THE GIANT WEALTH WE SITTING ON, WHICH IS HIGHLY HUNTED BY FOREIGNERS.
    SIMILAR TO HOW OUR PAST GENERATION USED THEIR COMMON SENSE TO CREATIVELY TO CULTIVATE COFFEE, COTTON, TEA, SISAL, PADDY, AND OTHER FOODS. THEY EVEN PLANTED TREES TO CREATE TIMBER FOR BUILDING INDUSTRY. THEY USED CHARCOAL TO CREATE COOKING ENERGY. MY FRIENDS, WHAT HAVE WE CONTRIBUTED DESPITE OF OUR HIGH ACADEMIC ACHIEVEMENTS? MINISTERS WITH PHDs ARE VERY BUSY RUNNING TO CHINA TO SELL THE LOCAL CONTRACTS TO THE CHINESE, BY DOING SO THEY ARE CREATING DEBTS WHICH THEIR PRESENTING TO THE PARLIAMENT FOR POOR TAX PAYERS TO FOOT THE BILL, WHERE IS THEIR SUBCONSCIOUS AND INTELLIGENCE? OUR MINISTERS ARE USING THE EDUCATION THEY HAVE PAID BY THE SAME POOR TAX PAYERS TO DRAFT CONFUSING OIL AND GAS POLICIES JUST TO DECEIVE THEIR SAME PEOPLE WHO VOTED THEM INTO OFFICE , JUST TO FIND THE WAY TO SELL THE EXPLORATION CONTRACTS TO FOREIGN COMPANIES WHO ARE PAYING THEM BRIBE, AND ASKING THEM FOREIGN COMPANIES TO PAY THE MONEY TO THEM INSTEAD OF ENFORCING THE POLICIES WHICH WILL BENEFIT THE WHOLE COUNTRY. THEY THINK THEY ARE VERY SMART, BUT WE TELL THEM THEY ARE VERY FOOLISH, BECAUSE THEY ARE EXCHANGING DIAMOND WITH WITH DECORATED PLASTIC BALLS. THEY DO NOT DESERVE TO REPRESENT WANACHI DEVELOPMENT, SO THEY MUST GO!

    Alex Kakala

    May 19, 2013 at 3:58 AM

  5. Asante sana Mheshimiwa. Sielewi ni namna gani juhudi hizi uzifanyazo zinaweza kuwafikia walengwa bila kupindishwa na wanaotakakuendelea kutawala bila kujali adhari ambazo watanzania walio wengi wataendelea kuzipata. Mungu akupe ujasiri wa kuyafanya haya uyafanyayo hata kama wewe binafsi au nduguyo wa kuzaliwa hatafaidika ila vizazi vijavyo. Amen

    Geremiah Mtweve

    May 20, 2013 at 3:05 PM

  6. Uwepo wako wewe hapo ni faida kwetu tusiokuwepo.Watanzania wanatambua na kuheshimu mchango wako ktk nafasi uliopo.Usikate tamaa ktk kusimamia ukweli na maslahi ya taifa hili.Viongozi wetu wamechoka kufikiri na hawajui walitendalo ndio maana kila wanalofanya wanaishia kujichanganya na kuudhihirisha udhaifu wao. Endelea kupigana kiume naamini siku moja utajua namaanisha nini pale utakapokuta Watanzania walio wengi wakiwa nyuma yako.

    John William

    May 24, 2013 at 9:23 PM


Leave a comment