Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Kufutwa kwa #POAC: #AnnaMakinda adhibitiwe au tusahau Uwajibikaji nchini

with 33 comments

Katika mkutano wa Kumi wa Bunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Spika wa Bunge ndugu Anna Makinda alitangaza mabadiliko kadhaa ya muundo wa Bunge katika Kamati mbalimbali za Bunge. Moja ya maamuzi ya Spika yalikuwa ni kufutwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ambayo inajulikana kifupi kama POAC. Maamuzi haya yameleta sintofahamu kwa wananchi wengi na wafuatiliaji wa masuala ya Bunge na Uwajibikaji katika nchi yetu. Ni muhimu tufahamu uundwaji wa POAC ulitokana na misingi gani na kwamba Uamuzi wa Spika unarudisha nyuma maendeleo makubwa ya kujenga Bunge imara na lenye meno. Maamuzi ya Spika ni kinyume cha kanuni za Bunge, sheria ya Ukaguzi na Katiba ya nchi. Maamuzi ya Spika yanavuruga Bunge,ni ya hovyo na yanapaswa kupingwa na kila mdau wa Uwajibikaji nchini.

Baada ya Tanzania kuingia kwenye zoezi la Ubinafsishaji, mashirika mengi ya Umma yaliuzwa na mengine kufa kabisa. Wakati huo kulikuwa na chombo kinaitwa SCOPO (Standing Committee on Parastatal Organisations) kwa madhumuni ya kusimamia uendeshaji wa Mashirika ya Umma. Bunge lilikuwa na Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma na kamati hiyo ilifutwa mwaka 1997 kufuatia hatua za ubanifsishaji na ukweli kwamba Mashirika ya Umma hayatakuwapo na hivyo hapakuwa na haja ya kuwapo kwa kamati hiyo. Mwenyekiti wa mwisho wa Kamati hiyo alikuwa ni Mzee William Shelukindo wakati huo akiwa Mbunge wa Jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Mwaka 2007, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alifanya mkutano wa Uwajibikaji na kueleza Taifa kuwa kimsingi Mashirika ya Umma bado yapo na mahesabu yao, kwa kuwa hayaangaliwi, ni mabaya sana nafedha za umma zinapotea. Pia alieleza kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 143(5) inamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoa taarifa za Ukaguzi za Mashirika ya Umma (Public Authorities and Other Bodies). Hivyo aliomba Bunge liunde Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma ili liweze kupokea, kujadili na kutoa maelekezo kuhusu mahesabu ya Mashirika ya Umma na kusimamia ufanisi wa Mashirika ya Umma. Vile vile alishauri Kamati hiyo isimamie sera ya  Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma. Spika wa Bunge wa wakati huo, kupitia Kamati aliyoiunda chini ya Job Ndugai (wajumbe wengine walikuwa dkt Willibrod Slaa, Beatrice Shelukindo, Hamad Rashid Mohammed na Nimrod Mkono) wakaunda Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma kwa mujibu wa Kanuni za Bunge za Mwaka 2007. Kamati ya POAC iliundwa rasmi mwaka 2008 mwezi Februari. Nilipewa dhamana ya kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kamati hii. Sababu za kuanzishwa kwa kamati ya POAC bado zipo na kimsingi sababu hizo ni za maana sana sasa kuliko ilivyokuwa kabla.

Majukumu ya POAC yaliainishwa na sehemu ya tatu ya nyongeza ya nane ya Kanuni za Bunge toleo la mwaka 2007, kanuni ya 115 (13)(a-e). Majukumu hayo ni pamoja na kushughulikia mahesabu yaliyokaguliwa ya Mashirika ya Umma, kuainisha maeneo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za Umma, kutathmini ufanisi wa Mashirika ya Umma na kufuatilia utekelezwaji wa sera ya ubinafsishaji wa mashirika ya Umma. Kuanzia mwaka 2008 Mdhibiti na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali amekuwa akitoa taarifa za mahesabu ya mashirika kama Katiba ya nchi inavyomtaka na sheria ya ukaguzi ya mwaka 2008. Sheria hii imeitaja kamati ya POAC kama moja ya kamati zenye majukumu ya kuwasilisha Bungeni taarifa ya mwaka ya mahesabu ya Mashirika ya Umma.

Katika kipindi cha miaka mitano POAC imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa umahiri na kwa kweli kwa uwazi sana kuliko kamati nyingine zote za Bunge. Taarifa ya mwisho ya POAC katika Bunge iliyowasilishwa katika mkutano wa saba wa Bunge, mwezi Aprili mwaka 2012 ulipelekea kutolewa kwa hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ambayo ilisababisha mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri. Hatua hii ilikuwa ni hatua muhimu sana katika kuweka mizizi ya utamaduni wa uwajibikaji nchini kwetu. Wakati Kamati inajiandaa na Taarifa yake ya Mwaka 2012 kwenye Mkutano wa Kumi na Moja, Spika ameivunja. Ikumbukwe maagizo ya mwisho ya Kamati ya POAC yalikuwa ni kuzuia mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa mikopo kwa Serikali bila ya kuwapo kwa mikataba. Hivi sasa Serikali imekopa zaidi ya shilingi 1.2 trilioni kutoka mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa ajili ya miradi mbalimbali, mikopo hiyo ya fedha za wafanyakazi haina mikataba yeyote na POAC iliona hatari ya fedha za wafanyakazi kupotea na kuleta madhara makubwa kwa wastaafu nchini.

Katika maelezo yake Spika amesema nchi nyingine duniani hazina kamati kama ya POAC. Nadhani waliomshauri Spika waliamua kumdanganya na yeye akadanganyika. Nchi zote za Afrika Mashariki zina Kamati ya kusimamia Mashirika ya Umma. Kenya inaitwa Public Investments Committee, Uganda inaitwa State Corporations Committee na hata nchi nyingine kama India ambazo zinafuata utamaduni wa kibunge kama wetu wanayo na wanaita Public undertakings Committee. Nchini Afrika Kusini sio tu kuna Kamati ya Mashirika ya Umma bali pia kuna Wizara inayosimamia Mashirika ya Umma (Ministry of Public Entreprises). Kimsingi Kamati ya POAC ilipaswa kuongezewa nguvu zaidi ili kufikia uwezekaji wa Serikali kwenye makampuni binafsi badala ya kuifuta. Uwezekaji wa Serikali kwenye makampuni kama BP, AirTel, Kilombero Sugar, SonGas nk hauna uangalizi wowote.

Uamuzi wa Spika wa Bunge kuifuta Kamati ya POAC ni uamuzi unaorudisha nyuma juhudi za nchi kujenga asasi za uwajibikaji, ni kinyume cha sheria ya ukaguzi wa umma inayotaja Kamati tatu za Bunge za kusimamia fedha za Umma na ni kinyume cha Katiba ya nchi. Spika wa Bunge anasema kazi za Kamati ya POAC zitafanywa na Kamati ya PAC; Tanzania ina jumla ya Mashirika ya Umma 258 yenye thamani ya shilingi trilioni 10.2 mpaka mwezi Juni mwaka 2012, hata kamati ya POAC ilikuwa haiwezi kushughulikia Mashirika yote ya Umma katika mwaka mmoja, PAC itawezaje kusimamia Wizara za Serikali, Mikoa na wakala za Serikali na wakati huo huo Mashirika ya Umma 258? Kwa vyovyote vile Taifa linarudi miaka ya kabla ya 2008 ambapo Mashirika ya Umma yalikuwa kichaka cha kuiba fedha za Umma. Hivi karibuni Kamati ya POAC iligundua mtindo wa Wizara za Serikali kupeleka fedha Serikali kwenye Mashirika na kutumia kifisadi ili kukwepa ukaguzi kwenye Wizara (Wizara ya Utalii ilipeleka zaidi ya shilingi 600 milioni Bodi ya Utalii mwaka 2010/2011). Ikumbukwe pia wizi wa EPA, MEREMETA na hata uuzaji holela wa baadhi ya mali za Serikali kupitia ubinafsishaji ulifanyika nyakati ambazo Bunge halina kamati inayosimamia Mashirika ya Umma.

Kwa vyovyote vile Spika wa Bunge amedhihirisha namna ambavyo anafanya maamuzi bila kuzingatia maslahi ya nchi wala kuzingatia historia ya uwajibikaji katika nchi. Namna mijadala ya Bunge inavyoendeshwa, namna anavyobeba ajenda za Serikali katika kujenga Bunge kibogoyo na namna anavyofanya maamuzi kwa kukurupuka, inahitaji hatua za kuokoa misingi ya uwajibikaji wa nchi. Ni lazima Spika wa Bunge adhibitiwe kwa kuondolewa katika nafasi hiyo haraka iwezekanavyo. Spika lazima ajue kwamba Mamlaka yapo kwa wananchi na yeye ni msimamizi tu wa vikao vya Baraza la wananchi liitwalo Bunge. Anna Makinda lazima adhibitiwe, vinginevyo nchi yetu itaumia.

Written by zittokabwe

February 10, 2013 at 11:24 AM

33 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Glad to hear that 4rm you.

  Lutufyo Benedict

  February 10, 2013 at 11:36 AM

 2. Mh,Anna Makinda toka awali ammekuwa ni mtu wa kuwalinda mafisadi kama walivyompa Uspika naye pia analipa fadhila kwa kuwalinda na kuzilinda njama zao ovu za kifisadi.Ingekuwa heri kama angeachia ngazi.

  paschal nyabatende

  February 10, 2013 at 11:41 AM

 3. kweli kabisa huyo spika anafanya maamuzi kwa maslai ya chama chake kilichoko ni wabunge wote kuungana na kupiga kura ya kutokua na iman na spika ndio maana tulikataa viongozi wanawake bcz wala akili kama za kuku.

  andrew massae PJ

  February 10, 2013 at 11:47 AM

 4. Nimeshangazwa na maamuzi hayo ya spika na sifahamu kama huwa anayafanya peke yake au angalau kuna consultation anafanya ne wengine.POAC ni muhimu kwenye swala zima la kuhakikisha uwajibikaji unakuwepo sijui maamuzi kama hayo yanafanywa kwa maslahi ya nani.Kiti cha spika ndo kingekuwa cha kwanza kuhakikisha bunge linakuwa na meno.Sifahamu kwa nini kiti hicho ndo kinakuwa cha kwanza kujiondolea meno.Katika hali ya kawaida mtu angependa taasisi anayoiongoza inakuwa na nguvu na si vinginevyo.Ni ngumu sana nchi hii kusonga mbele

  Ramadhani Msoma

  February 10, 2013 at 11:51 AM

 5. 2015 imekaribia sana. Kwa hali ilivyo sasa ili mbinu chafu za siasa za ccm ziweze kuwabakisha angalau kidogo bungeni lazima watafute mipenyo ya kuanza kuiba hela za kuhonga waiba kura zetu. Uwepo wa kamati hii ilikuwa inampunguzia nini MAKINDA? Anadhani maisha ya wabena yatakombolewa na fikra za kitumwa kama hizo kweli? Tusiache kuwazomea mpaka watapogundua wao ni mazuzu kabisa!

  JOSEPH MIGUNDA

  February 10, 2013 at 11:53 AM

 6. Tangia awali cc kama wanannchi tulio wengi ha2kuwa na imani na spika makinda zaidi ya hapo 2tahamcshana kufanya maandamano ya amani ili kushinikiza spika kujiuzulu nafac yake kwn ameshindwa kuliongoza bunge kwa kanuni na sheria zilizo wekwa acongoze bunge atakavyo bali aliongoze bunge kwa misingi thabiti iliyowekwa

  ZE Bosco Rufatiye

  February 10, 2013 at 12:00 PM

 7. Hivi huyu mama huwa anafikiria nini anapofanya maamuzi mazito kama haya ambayo yanavunja katiba ya nchi? Duniani kote sasa hivi wimbo ni corporate governance corporate governance yeye anaturudisha nyuma miaka ishirini. Anapata wapi ujasiri wa kufanya hivyo hasa katika Tanzania ya leo? Anataka kuacha legacy gani atakapoacha uspika? Atataka tumkumbuke kwa kukumbatia serikali isiyowajibika?

  Harry

  February 10, 2013 at 12:09 PM

 8. nashukuru mungu sikuipigia kura ccm coz nw ningekuwa najutia

  hosea joseph

  February 10, 2013 at 1:06 PM

 9. Zito,ndugu yangu nchi hii ipo cku tu.Hayo maamuzi kayatoa kwenu je,wananchi wamelizia?

  Godfrey Musiba

  February 10, 2013 at 1:07 PM

 10. Ni taarifa inayotia uchungu kwa kila mtanzania mzalendo na mpenda maendeleo kwa nchi yetu. Mh.Zitto naomba taarifa hii iwafikie wananchi wengi kadiri inavyowezekana lakini ikamilishwe na muono mbele yaani watanzania wafanye nini ili kuharibu mawazo haya mabaya ya Spika na hatimaye kuinusuru nchi. Napendekeza njia ya ujumbe mfupi wa maandishi utumike kufikisha ujumbe na kuwajengea hisia za kizalendo wtanzania waamke kutoka kizani. Pamoja tunaweza!

  Deo

  February 10, 2013 at 1:08 PM

 11. Hili ni janga kwa Taifa.

  Nahisi kuwa nchi itateketea muda mfupi ujao.

  Tunahitaji kufanya maamuzi magumu kama Taifa

  mwanawavitto kiraro

  February 10, 2013 at 1:14 PM

 12. Bila shaka uamuzi wa kupunguza uwajibikaji na usimamizi wa matumizi ye fedha za umma zinazozidi trilioni 10 ni uamuzi unaoashiria mkakati maalumu wa kunyima upinzani silaha ya kuwashtaki kwa wananchi kati ya sasa na 2015. Ripoti za POAC na mijadala itokanayo ingeendelea kuonyesha ufisadi mkubwa kwenye mashirika yetu jambo ambalo lingeendelea kuchangia hoja mhimili ya kuing’oa CCM na serikali yake madarakani kwa sababu ni waasisi na waendekezaji ufisadi na matumizi mabaya ya mali za umma.

  Vile vile inapunguza mwanga kwenye vichaka vya CCM kujipatia fedha za Uchaguzi kuelekea 2015. Si vyema kutazama uamuzi huu wa Anna Makinda kama ni ukurupukaji. Tangu amevunja kamati ya madini na nishati karibu mwaka mzima serikali inaendesha sekta hii bila chombo teule cha kusimamia sekta mama wakati maamuzi makubwa kuhusu madini, mafuta, gesi na nishati yanafanyika. Bila kamati ya kumulika sekta hii kwa nini tusifikiri kuwa ufisadi uliodhihirika serikalini unapewa nafasi ya kushamiri na kufaidisha walioko madarakani wakati huu kabla ya 2015? Fedha zilizoko benki za Uswiss nyingi zinasemekana zimetokana na mikataba ya gesi na mafuta.

  Waliomtoa Sitta walichukizwa na yeye kutoa wasaa kwa kurunzi la upinzani na wapenda nchi kumulika na kujadili ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Waliyemuweka Makinda kwa kisingizio kuwa ni wakati wa kina mama bila shaka walijua yuko hafifu na atatekeleza matakwa yao ya kutofichuliwa udhalimu walioutenda na haswa kuhusu chama kuendelea kuhodhi dola. Kwa hili inaelekea atafanikiwa kama wananchi wa nia nzuri hawakusimama na kusema the hell no. We will not be dragged back to the pigsty of dastardly open corruption by those in power at a time when we are poised for economic take off. Like in aviation, there is no more dangerous event than a mismanaged takeoff. We the people must stand firm and make it clear that we want our representatives to continue having oversight over our public enterprises. We can do without Anna Makinda, we can not do without POAC.

  Makundi W R (@MakundiW)

  February 10, 2013 at 1:55 PM

 13. Ndio maana nasema tukitaka mabadiliko ya kweli njia ni kuitoa ccm madarakani bila hivyo tutaendelea kuwekwa rehani mpaka mwisho wa dunia.

  Tanzania Nchi Yetu Sote

  February 10, 2013 at 3:37 PM

 14. Hakuna jambo lisilo na sababu, lakini azima uangalie uzito wa jambo lenyewe na sababu ya kufanya hivyo, sijui kama makinda kaamua yeye bila kushauriwa au kuamriwa afanye hivyo.
  alilofanya makinda ni kutaka kuficha uozo unaoendelea ndani ya serijali na cvinginevyo, si mtu mwenye fikra njema kwa taifa letu na maendeleo yake. wakae na kujua kuwa hakuna kitu kisicho na mwisho. maamuzi yasiyo na busara na hekima ndiyo yatakayo fikisha mwisho wa uhai wa chama chao.
  Hakuna mtu anayependezwa na unduli wanaofanya ndani ya bunde eti kukataa kujadili mambo ya msingi na kujadili yasiyo ya msingi. Huu ndiyo mwisho wao.

  Musa Mtenzi

  February 10, 2013 at 3:53 PM

 15. nimesikitika sana kwa maamuzi ya mama spika kwangu me kamati hii ilikuwa muhimu kwa mustakabari wa mashirika ya umma na upatikanaji wa ajira kupitia mashirika haya.

  uswege

  February 10, 2013 at 8:10 PM

 16. Kama mnavofikiri mlionitangulia ni sawa kabisa anajenga mazingira mazuri kwa wao yaani wanaccm kuweza kufanya ufisadi bila hofu na kwa ukweli bila woga napenda kinacho tafutwa ni pesa ya kampeni 2015.Kwani njia waliokuwa wakiitumia ni ya ujangili kwa kuuwa Tembo kwa wingi sasa imeshajili kana ndiyo sababu ya msingi ya kuuwa hii kamati.Ndugu zangu Tanzania imeshaza sasa ni kuing’oa CCM tuaweke CHADEMA madarakani.

  Kijana Mpiganaji

  February 11, 2013 at 7:44 AM

 17. ikifutwa POAC mafisadi wataendelea kuiba pesa za wananchi milele daima wananchi ni lazima tumuwajibishe spika kwani si bunge la CCM ni lawatanzania wote.

  janeth mrema

  February 11, 2013 at 10:12 AM

 18. ikifutwa POAC mafisadi wataendelea kuiba pesa za wananchi milele daima wananchi ni lazima tumuwajibishe spika kwani si bunge la CCM ni lawatanzania wote.

  janeth mrema

  February 11, 2013 at 10:12 AM
  Reply

  Ramso Msongera

  February 11, 2013 at 10:16 AM

 19. Kaka hii hali si njema kabisa; lakini ndivyo ndugu zetu walivyo. Wakati mahali pote uwajibikaji kwa umma unahimizwa kwa Serikali ya CCM hawataki hata kusikia.
  Kwa hili nadhani ni wakati muafaka sasa kwa wananchi wote bila kujadili itikadi zetu kuungana si tu kulaani bali kupinga/ kutaa mabadiliko haya. Hebu fikiria serikali hii ya kishkaji, ufisadi uliokithiri halafu ukaua kamati za bunge na kumnyima mamlaka ya CGA na fursa ya wabunge kupitia na kujadili taarifa za CAG ni maafa gani yatalipata taifa?

  Ninakubali hisia zangu kwa haya ni maandalizi ya kujenga mazingira ya kuwezesha kuiba fedha za umma kwa ajili ya chaguzi za 2014 na 2015!

  Hivi wataalam wa sheria hakuna sheria inayotupa nguvu wananchi kupinga maamuzi haya? Au mnaonaje tuunge nguvu na twende mahakamani kupinga?

  Lugano

  Edna J. Lugano

  February 11, 2013 at 2:08 PM

 20. ndugu zangu sasa spika Anne Makinda kwa hili la kuivunja POAC ni kuitengenezea CCM mazingira ya kufanya ufisadi kwa ajili ya uchaguzi 2014 na 2015. Kwa hili hatuna budi kuandamana mpaka kieleweke na ikiwezekana huyu Anne Makinda aonolewe uspika.

  Eng.Wansakya

  February 11, 2013 at 5:07 PM

 21. Hiyo mama ni msenge sana mtu hana hata
  Mume unategemea atakua na akili kweli?
  Mi naona kilichobaki tuchapane tu tutakao kufa tufe tu watakdobaki waishi kwa adabu.

  Wizard

  February 11, 2013 at 5:15 PM

 22. sijajua vizuri,maelezo ni mazuri lakini nina wasiwasi kidogo.
  Unajua kaka Zito awali alisema hapo awali kamati kama hii walikuwemo akina mr.mkono na wakati tunajua fika mkono na kampuni yake ya uwakili ndio walikuwa washauri wakuu wa serikali kwenye ubinafishaji wa yaliyokuwa mashirika ya umma.Na pia umegusia meremeta ambayo waziri mkuu wetu amesikika akikemea watu wasiiongelee mara kwa mara bungeni ya kwamba inagusa usalama wa nchi.Hadi sasa hatujajua huo usalama wa nchi unaoguswa mnatuacha njia panda.Na ilikuwaje Mkono,jimboni kwake ndiko meremeta ilikuwa inafanya kazi kule Buhemba.Na kampuni yake ilihusika kwenye ubinafishaji yaani mkono & Co.Advocate (sio wa Buhemba hapa namaanisha wa yaliyokuwa mashirika ya umma) alijipenyezaje kuingia kwenye kamati hii.kulikuwa na Transparence ya ukweli hapa au kunakitu kilikuwa kinawekewa uzio?
  Nimebakia na maswali mengi?
  Nimezungukazunguka kwenye maelezo yangu ili watu watafakali.

  thomas

  February 11, 2013 at 5:16 PM

 23. Kimsingi najisikia vibaya sana pindi nixungumziapo utawala wa uwajibikaji, nakutolea mifano Kenya ijapokuwa hawakuweza kumshutumu yeyote kwa uvunjifu wa maadili ya utumishi wa umma, nilitegemea nchi yetu Tanzania ingeongeza nguvu kwa vyombo hivi PAC, POAC kutimiza kile tutegemeacho kukiona, mnanafasi nzuri kuleta mabadiliko, ili kila mmoja ajivunie kubaki Tanzania, ila mnabaki na tatizo la kila mwafrika minong’ono, gossip. Inachosha ubinafsi umekithiri

  Raphael kibindo

  February 11, 2013 at 7:06 PM

 24. toka huyo mama anchaguliwa nilijisikia vibaya sana coz madem hawakatai kutingozwa sasa mafisadi wananfaidi tu yani hana mcmamo kazi yake ni kutetea chama chake na kuboronga mipango ya wapinzani ya kuliletea taifa maendeleo.

  sunday pama

  February 12, 2013 at 6:38 AM

 25. Tanzania nakupenda kwa moyo nusu, nilalapo sikuoti wewe…

  Abdallah

  February 12, 2013 at 10:54 AM

 26. Adhibitiwe huyo Mama!

  Tito Mwakipesile

  February 12, 2013 at 12:20 PM

 27. Remove that women immediately. demonstrate to her that the times have changed, Watanzania can no longer tolerate unscrupulous leaders who have destroyed the country economy for decades through corruption. The leadership positions change hands among themselves through dubious ways of protecting each other against public scrutiny. Can you remember that lady has been in public office for decades? The country should be creating more POAC type of management to protect the nation investments and create accountability. She is acting with impunity. It is time for her to go. The country need young , energetic leaders with clear vision towards economic revolution of all Tanzania. Is it true, in the country need such very old leaders without clear vision for the country?

  Alex Kakala

  February 12, 2013 at 11:08 PM

 28. To show that we are serious, we request Mr. Zitto Kabwe to send a signature collection form support form, demanding for speaker removal with immediate effect. she has abused her position by trying to protect the blood suckers. Every one on this website will sign the form and send back to Mr. Zitto. Time to put a stop of Richmond type of stories, UK fake military equipment stories, you can go on and on. Why should the poor people continue to suffer at the hands of liars and lobbers? We will continue to beg for survival from other countries for ever, while we watch the country resources and assets are being squandered by the very same people we trusted to look after the business.These are criminals, who are smiling tigers. Any trustable leader who can come to power, must prosecute all the cases even things happened 20 years back. That will be a true revolution to send a clear signal, that they will can not still from public and hide!

  Alex Kakala

  February 12, 2013 at 11:29 PM

 29. […] ni baadhi ya mambo nyeti yaliyoibuliwa na kamati hii,kamwe hatuwezi kuyasahau kirahisi! Kufutwa kwa #POAC: #AnnaMakinda adhibitiwe au tusahau Uwajibikaji nchiniby zittokabweKatika mkutano wa Kumi wa Bunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Spika wa […]

 30. Naungana na muheshimiwa Zitto kuhusu POAC, spika sifahamu katumia kigezo gani kuifuta,labda tumkumbushe muheshimiwa spika kuwa wakati umefika wa kuweka masilahi ya nchi na wananchi wake mbele kisha masilahi binafsi au ya chama yakafuata ili kujenga imani kwa wananchi mnaotuongoza.

  Zakia Salum

  February 13, 2013 at 10:14 PM

 31. NIMEIPENDA KAULI YAKO

  Kwa vyovyote vile Spika wa Bunge amedhihirisha namna ambavyo anafanya maamuzi bila kuzingatia maslahi ya nchi wala kuzingatia historia ya uwajibikaji katika nchi. Namna mijadala ya Bunge inavyoendeshwa, namna anavyobeba ajenda za Serikali katika kujenga Bunge kibogoyo na namna anavyofanya maamuzi kwa kukurupuka, inahitaji hatua za kuokoa misingi ya uwajibikaji wa nchi. Ni lazima Spika wa Bunge adhibitiwe kwa kuondolewa katika nafasi hiyo haraka iwezekanavyo. Spika lazima ajue kwamba Mamlaka yapo kwa wananchi na yeye ni msimamizi tu wa vikao vya Baraza la wananchi liitwalo Bunge. Anna Makinda lazima adhibitiwe, vinginevyo nchi yetu itaumia.

  yuaja

  February 14, 2013 at 10:57 AM

 32. MABADILIKO MABADILIKO MABADILIKO,2015 sio mbali ccm endeleeni kuvurunda sana,hayo maamuzi sio ya huyo mama,yeye ni kama mbuzi wa kafara,lakn cha moto watakiona 2015,POAC ilikuwa inawaumbua mafisadi.

  HERBERT ELIYA

  February 19, 2013 at 8:15 PM

 33. bunge ndokila kitu katika nchi wawakilishi wetu mnatakiwa kuwa makini kututetea wananchi wenu ahadi feki zisikuwepo ili tuzidi kuwaamini

  omar hassan

  November 2, 2013 at 9:44 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: