Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015

with 12 comments

KABWE ZUBERI ZITTO, MP

KIGOMA KASKAZINI

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015

  1. Baadhi ya vyombo vya habari vimehusisha kauli yangu ya kutaka kupunguza umri wa kugombea urais na mimi ‘kuutaka urais’. Mimi nikiwa mwanachama na kiongozi wa chama chama changu cha CHADEMA naelewa na kuziheshimu taratibu na kanuni tulizojiwekea za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo nafasi ya urais. Nafasi ya uongozi ndani ya CHADEMA haiombwi kwenye warsha. Iwapo chama changu, wakati muafaka ukifika na kutokana na matakwa ya jamii, kikiona nipewe jukumu lolote sitasita kutekeleza wajibu huo niwe au nisiwe mgombea.
  2. Kwa hivyo, nilichozungumza jana ni kutoa maoni yangu kwamba muda umefika kwa Taifa letu kupunguza umri wa kugombea urais. Maoni yangu haya yanatokana na ukweli kwamba hakuna sababu zozote za kisayansi zinazomfanya mtu aliye chini ya umri wa miaka 40 akose sifa za kuwa Rais. Msimamo huu nimekuwa nao tangu zamani nikisoma shule na haujawahi kubadilika. Hakuna mahala popote katika maoni yangu niliyotoa jana niliposema kwamba nataka umri wa urais upunguzwe ili nipate fursa ya kugombea nafasi ya urais. Pia siwezi kutaka katiba iandikwe kwa ajili yangu. Vilevile kamwe isionekane kwamba matakwa ya muda mrefu ya vijana ya kutaka umri wa kugombea Urais kupunguzwa yanalenga kunipa fursa mimi kwani mimi ni binaadamu naweza nisiwe na sifa za kuwa Rais lakini kukawa na vijana wengine wengi wenye umri chini ya miaka 40 wenye Uwezo na Uzalendo wa kutosha kushika usukani wa nchi yetu. Ni maoni yangu kwamba tupate mabadiliko ya vizazi katika uongozi wa nchi yetu ili kukabili changamoto za sasa zinazokabili Taifa letu.
  3. Tunapojiandaa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya ni vizuri vyombo vya habari vikajikita kutoa taarifa bila kuweka tafsiri au kuwatafasiria maoni ambayo wananchi na viongozi watakuwa wanayatoa kuhusu maudhui ya Katiba Mpya.

Dar es Salaam

29 Februari 2012

Written by zittokabwe

February 29, 2012 at 1:25 PM

12 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. […] wa kampeni ya kupunguza umri wa urais na Zitto kutaka kugombea urais 2015 Source: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugom… TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka […]

  2. Uko sawa Mheshimiwa Zitto, binafsi sikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo maana ni dhahili zililenga kupotosha maudhui mazima na dhana ya hoja yenu na Mhe. Makamba, umejibu kwa wakati muafaka hongera kwa hili.
    Pia msiludi nyuma katika hili tupo pamoja kuwasapoti kaka.

    Shadrack Mbuki Feleshi

    February 29, 2012 at 1:39 PM

  3. Hakuna uhusiano wa miaka na urais….lakini busara, uchapakazi na umakini ndio chimbuko la mafanikio,
    kinachotusumbua wengi ni tafsiri ya lugha-kiswahili….lakini ni mtazamo mzuri, umri wa urais upunguzwe

    Frank Nkanda

    February 29, 2012 at 3:18 PM

  4. Kaka Zitto siyo wewe tu uliyekua na wazo hi nina imani ni wengi limekuwa likiwaumiza vichw ila muda na sehemu ya kulizungumzia ndo ulikua unakosekana kwa kuwa wewe kama mbunge kijana pia ukiwa na nafasi yakuliongelea swala hili na limetufikia tunashukuru na tunakupa support kwani lina hoja ya msingi, nipende kukushukuru kwa kuwa kijana mbunge unaetoa mawazo yaliyojaa hoja yakinifu.

    Exavery Rugina

    February 29, 2012 at 3:58 PM

  5. […] bado katika hili la urais wa Januari Maakamba na na Zitto Kabwe!!! By nice 2 Source: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugom… TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka […]

  6. Hapo kaka mimi binafsi nimekuelewa na kwa watanzania wote wenye uelewa wanapaswa kukuelewa na si kukubeza,kukuungia maneno ya uelewa wao wala kutafasiri mtazamo wako huo na mtazamo wa maoni ya mtu mwingine hasa katika wakati huu muhimu wa kutengeneza Nchi yaani Katiba,

    Kuna mambo mengin ambayo jamii imefumbwa na serikali iliyopo na zilizopita hasa kwa kuendelea kutumia maneno yale ya Kikoloni ya kutuona wanajamii kama nyani au tumbili wasioelewa au kujali angalau kiwango cha mnyama kama Sokwe mtu,Tatizo hili ndilo linafanya jamii na watendaji wengine kuendelea pia kujinyanyapaa kwa kujidharau sana na kuona haiwezekani kwa kuwa Viongozi waliopo madalakani leo hii kwa mtazamo wangu wanatuona sisi jamii ya Kitanzania ni mateka wao mithili ileile ya kikoloni.Ninayo mengi yakusema ila kwa hatua hii Kaka Zitto naomba usiache kutuchochoa kama jiko la kupikia moto wa kuni ili mmojammoja tuje tufikie hatua ya kuona angalau kilomete 2 kuliko mita mia moja tu inayoonwa na Watanzania walio wengi juu ya Mstakabali wa maisha bora na ustawi wa jamii wenye tija kwa Taifa.

  7. Mh. Zitto nadhani wengi wanafahamu kuwa mwaka 2015 utakuwa na umri wa miaka 39, pungufu ya mwaka mmoja tu kustahili kuwa mgombea uraisi. Hii ndiyo maana inazua maneno kwa sababu mabadiliko yoyote yatakayofanywa kupunguza umri wa mgombea yatakufaidisha.

    Ni kawaida kabisa katika mazingira hayo watu kudadisi nia yako wakiona umeshupalia hoja ya umri wa mgombea uraisi.

    Upande mwingine kuna hoja nzito zaidi ambayo nyie wenzetu wa kwenye vyama naona hamuishupalii. Nayo ni hoja ya Mgombea Binafsi. Naamini wananchi wengi tu wanahitaji katiba iruhusu wagombea binafsi kuanzia ngazi ya Serikali ya Mtaa mpaka Uraisi.

    Endapo ngazi ya uraisi itaonekana ni nyeti sana, basi si mbaya tukiwa na kipindi cha mpito cha miaka kadhaa ambapo wagombea binafsi wataruhusiwa kwa ngazi za Serikali ya Mtaa mpaka Ubunge.

    Fredrick Mboma

    March 1, 2012 at 2:21 PM

  8. Hakuna uhusiano ulioko kati ya raisi na umri wa miaka 40,jambo la msingi kinachotakiwa ni hekima,kujituma katika kazi na kuwa muangalifu.Kuna mifano mingi ya maraisi katika nchi zingine ambaoumri wao ni chini ya miaka 40.Watanzania ifikie hatua tulitambue hilo.Huu ni mtazamo mzuri na wa kujenga.
    Asante sana Mh.Zitto kwa mawazo kama hayo

    Juma

    March 1, 2012 at 8:17 PM

  9. Mheshimiwa Zitto,

    maoni yako ni mazuri kwa wakati tuliokuwa nao.
    Shida hata ya vyombo vya habari ni kufanya siasa kupitia taarifa wanazotoa huku wakijisahau kuwa wao si wanasiasa katika shughuli zao.

    Nakubaliana na wewe kwa maoni yako na pia, vyombo vya habari vingejitahidi kuepuka kuweka chumvi zaidi katika mboga iliyotengwa mezani tayari kwa kula.
    Uhuru wa kutoa maoni ni haki ya msingi.

    William J.

    March 2, 2012 at 2:34 AM

  10. Mhe Zitto wazo lako ni dira angavu kwa watanzania vijana. Watanzania wa leo na hasa vijana, wala hatuhitaji tafsiri ya kauli au maoni ya mtu yeyote kutoka kwa mhariri wa gazeti lolote. Binafsi natambua na kutumainia sana jitihada zako na mhe January kutetea wanyonge ambao wengi wao ni sisi vijana wenzenu.

    juma kiolobele

    March 2, 2012 at 6:56 PM

  11. […] bado katika hili la urais wa Januari Maakamba na na Zitto Kabwe!!! By nice 2 Source: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugom… TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka […]

  12. Haina shida,hata ukisema kwa nafsi yako,ni kwel hv genetic au meiosis gan,ambazo zinahusiana na umri ndio utendaj?mbona kuna wazee,wanavuta bang na vijana wengine hawavut?ya ngoswe wa muachie ngoswe,nakupa moyo kaka kaza uz had mwisho.

    Steang

    March 3, 2012 at 2:41 PM


Leave a reply to Shadrack Mbuki Feleshi Cancel reply