Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Posts Tagged ‘vitabu

Vitabu Nilivyosoma 2014 – Books I have read in 2014 #BooksRead2014 #letsread

with 20 comments

Mwaka 2014 nimesoma vitabu 53 na nimefanya uchambuzi wa vitabu 21 kupitia safu ya Kitabu na Kalamu ya gazeti la Raia Tanzania kila Jumatatu.

Tangu nimeanza utaratibu kuchapisha idadi ya vitabu nilivyosoma huu ni mwaka wa tatu sasa. Mwaka 2012 nilisoma vitabu 31, mwaka 2013 vitabu 13 na 2014 vitabu 53.

Mwaka 2014 niliuanza kwa changamoto nyingi sana katika maisha yangu ya kisiasa; kuvuliwa nyadhifa katika chama na kuwa hatarini kuvuliwa uanachama kilichopelekea kwenda mahakamani kutetea uanachama wangu. Vile vile kuanzia mwezi Machi nilianza kumwuguza mama yangu mzazi mpaka mungu alipomchukua hapo mwezi Juni. Muda mwingi niliutumia kusoma vitabu kama matibabu ya msongo ( therapy ). Mchakato wa Katiba ( ambao sikushiriki kwa sababu ya kuona dhahiri hautaleta katiba bora ) pia ulinipa muda mzuri wa kufanya jambo ninalolipenda kuliko yote – Kusoma.

Kitabu kimoja (ADAPT) kimenifanya kubadili kabisa mtazamo wangu wa maisha.

Vitabu 2 ( Exposure na Munyakei story ) vilinitia faraja kubwa katika kazi niliyokuwa nafanya tangu mwezi Machi ( uchunguzi wa akaunti ya #TegetaEscrow ).

Kitabu kimoja ( The myth of the strong leader ) kimepanua sana uwezo wangu katika kuchambua viongozi na mafanikio yao. Vyote nilifanikiwa kuvifanyia uchambuzi katika RaiaTanzania.

Bado India imechomoza sana katika orodha yangu. Miezi 2 niliyokaa Madras kumtibu mama imechangia sana kuongeza vitabu kutoka waandishi wa India. Vingi ni fiction. India Calling kilinivutia zaidi kuliko vyote. Mwaka 2014 nimeanza kusoma kazi za ushairi za zamani (Classics) ili kupata maarifa mengi yaliyojaa kwenye ushairi na kuendeleza ujuzi wa kuandika mashairi.

Kitabu kimoja nilikianza nikashindwa kukimaliza, The Capital. Mungu akipenda nitakimaliza mwaka 2015. Karibu katika orodha yangu ya vitabu mwaka 2014.

Zitto Kabwe, MB

BOOKS THAT I HAVE READ IN 2014

View this document on Scribd

Written by zittokabwe

December 27, 2014 at 12:16 PM