Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Posts Tagged ‘Swiss Govt

PRESS RELEASE: ZITTO ZIARANI ULAYA

with 7 comments

PRESS RELEASE

Zitto aenda Uswiss na Uingereza kuhusu utoroshaji wa fedha

Shirika la Kimataifa la Mtandao wa Ulaya wa Madeni na Maendeleo, European Network on Debt and Development (Eurodad)  watafanya ziara ya kiuchunguzi kuhusu masuala ya uwazi katika kodi katika nchi za Ulaya kuanzia tarehe 20 Oktoba mpaka tarehe 5 Novemba mwaka 2013. Uchunguzi huo utaendeshwa na wataalamu waliobobea wa masuala ya kodi na maendeleo. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wa Bunge la Tanzania Zitto Zuberi Kabwe ameteuliwa kuongoza Jopo la uchunguzi huo.

Eurodad ni Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yapatayo 48 kutoka nchi 19 za Ulaya ambayo yanajihusisha na masuala ya kufutia madeni nchi zilizoendelea, misaada yenye maana na kodi za haki. Mashirika haya yamekuwa kwenye kampeni ya kupinga utoroshwaji wa fedha kupitia ukwepaji kodi unaofanywa na mashirika ya kimataifa kwa nchi zinazoendelea. Zitto amekuwa mmoja wa wabunge wanaosimamia hoja ya kutaka Watanzania waliotorosha fedha kwenda nje warejeshe na kufunguliwa mashtaka. Mwaka 2012 aliwasilisha hoja binafsi Bungeni na kupitishwa kuwa Azimio la Bunge ya kutaka uchunguzi kuhusu utoroshwaji wa fedha na kufichwa nje kama Uswiss. Kikosi Kazi cha Serikali kutekeleza Azimio hilo la Bunge kinatarajia kuwasilisha taarifa yake katika Mkutano wa Kumi na Sita wa Bunge. Siku ya Jumatatu tarehe 21 Oktoba Zitto atakutana na Waziri wa Fedha wa Uswiss na maafisa wa mabenki na asasi zisizo za kiserikali zilizopo jijini Geneva. Pia Zitto atahudhuria mkutano wa Kamati ya Kodi ya Umoja wa Mataifa katika kampeni ya kubadili mfumo wa kodi za kimataifa ili kuzuia unyonyaji wa nchi za Kiafrika unaofanywa na Makampuni makubwa ya Kimataifa.

Baada ya Geneva Zitto atatembelea nchi za Luxembourg na Brussels kabla ya kwenda Norway ambapo atamalizia ziara yake kwa Jopo la Wataalamu wa masuala ya kodi na Maendeleo kuandika taarifa maalumu yenye mapendekezo kuhusu kuzuia utoroshaji wa fedha kutoka Afrika.

Zitto atakwenda jijini London kutoa mada kuhusu masuala ya kodi za kimataifa katika mkutano wa Uwazi (Open Government Partnership). Mwenyekiti wa PAC Tanzania atafanya mazungumzo na Mwenyekiti wa PAC Uingereza Bi Margaret Eve Hodge, Lady Hodge MBE, PC, MP  kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa mabunge mawili na kuendeleza wito wake kwa makampuni ya kimataifa kulipa kodi zao barani Afrika na kuacha tabia ya kutumia ‘Tax Havens’ kukwepa kodi na kufukarisha nchi za Kiafrika.

Zitto invited to annual OGP Summit

The Kigoma North Member of Parliament and Chairman of the Public Accounts Committee (PAC), Hon Zitto Kabwe has been invited for the annual Open Government Partnership (OGP) Forum which kicks off in London at the end of the month.

The OGP Summit is a chance to promote tax and illicit issues to new audiences, to encourage new commitments in country action plans.

Hon Zitto, who also serves as Deputy Leader of Official Opposition in the Parliament, will serve in the panel which will discuss tax and illicit flows, which is among themes to be deliberated during the summit.

The OGP is a global platform for domestic reformers committed to making their governments more open, accountable, and responsive to citizens. Tanzania is among countries which have signed its membership to the OGP.

Hon Zitto has great interest on tax avoidance through illicit transfers and last year he tabled private motions which lead to the adoption of a Parliament Resolution compelling the government to investigate a number of individuals who have illicitly stashed billions of dollars abroad.

The fact finding mission will see its members interact with UN Tax Committee, OECD, EU as well as key European governments. They will visit a number of European cities namely Geneva, Paris, Luxembourg, Brussels and Oslo.

Ends

Issued by;

Parliamentary Office of Hon. Zitto Kabwe MP

Dar es Salaam

October 19, 2013

 

Mabilioni ya Uswisi – Tusigeuzwe Mazezeta

with 32 comments

Mabilioni ya Uswisi – Tusigeuzwe Mazezeta

Jumanne tarehe 20 Novemba 2012, baadhi ya vyombo vya habari vimebeba habari zinazohusu matamshi ya Waziri wa Utawala Bora ndugu George Mkuchika kuhusu sakata ya mabilioni ya Uswisi. Waziri amesema kwamba Serikali ya Uswisi inataka majina ya Watanzania walioficha fedha huko ndio waweze kusaidia uchunguzi. Habari kama Hiyo, yenye maudhui na malengo hayo hayo iliandikwa na Gazeti la The Guardian on Sunday la tarehe 18 Novemba 2012.

Nimeona ni vema nitoe kauli yangu rasmi kuhusu suala hili. Lengo ni kuweka rekodi sawa juu ya Azimio la Bunge na kwamba Serikali inapaswa kutekeleza Azimio na sio kutoa kauli tata za kukata tamaa.

Moja, Suala hili japo sio jipya lakini limeandikwa kama ni jambo jipya. Suala la Serikali ya Uswisi kutaka majina lilisemwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati akichangia hoja binafsi niliyowasilisha Bungeni na pia wakati akileta maombi yake ya kuiondoa hoja ambayo yalikataliwa na Bunge. Kama sio sababu mpya ni kwanini imeibuka upya na kwa kasi? Ni wazi Serikali inajihami kwa kuona kuwa itashindwa kutekeleza azimio la Bunge. Watanzania wasikubali propaganda hii ya Serikali. Bunge limeagiza Serikali kufanya uchunguzi kwa kutumia njia za kiserikali au wachunguzi binafsi wa kimataifa. Kwa nini Serikali inaanza kubwabwaja ilhali wala haijaanza kazi hiyo? Serikali inajaribu kuficha nini? Kwa nini baada ya wiki iliyopita Benki Kuu kufanya uchunguzi kwenye Mabenki ya Biashara jijini Dar es Salaam na namna fedha zimekuwa zikipelekwa nje (international transfers), leo Serikali inakuja na kauli za kukakata tamaa? Kunani?

Pili, Watanzania wajue kwamba Taifa la Swiss limejengwa na linajengwa kwa fedha hizi za wizi ambazo watu mbalimbali duniani wanaiba au kukwepa kodi kwenye nchi zao na kuzificha huko. Serikali ya Swiss hata siku moja haiwezi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika suala kama hili. Ndio maana Azimio la Bunge linataka wachunguzi binafsi ambao hawatahitaji ushirikiano wa Serikali ya Swiss. Nawakumbusha kwamba mwaka 1997 mara baada ya Joseph Desire Mobutu kuangushwa na Rais Joseph Kabila kule Kongo – Kinshasa, Serikali ya Swiss iliitaka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuonyesha ushahidi kuwa hela hizo za Mobutu zilikuwa zimepatikana kwa njia haramu! Waswiss walitaka Kabila awakakikishie kuwa fedha zile zaidi ya dola bilioni nane za Kimarekani Mobutu hakuzipata kihalali ndio waweze kuzirejesha. Zaire ilikadiriwa kuwa na zaidi ya dola za Kimarekani bilioni thelathini katika Mabenki ya nje ya nchi hiyo. Majibu ya aina aina hii ni majibu ‘standard’ ambayo kila nchi inapewa. Hata Marekani ilipokuwa inafuatilia wakwepa kodi wao walijibiwa hivi hivi. Hatimaye Serikali ya Marekani ikaamua kununua taarifa hizo na kuwakamata wakwepaji kodi wao walioficha fedha Uswisi. Hao ndio Waswiss ambao Serikali ya Tanzania inashabikia majibu yao. Bila Aibu Mawaziri wetu wanayanukuu majibu ya Waswiss kama kasuku. Tunasahau historia haraka sana. Tunakuwa kama mazezeta.

Tusiwe Taifa la mazezeta. Mabwege na mazezeta huimba kila wanachoambiwa kuimba. Sasa Serikali ya Tanzania imekuwa msemaji wa Serikali ya Swiss badala ya kuchunguza utoroshaji wa fedha haramu na kisha kutoa taarifa Bungeni. Naitaka Serikali ianze uchunguzi mara moja kama namna ilivyoelekezwa na Bunge. Suala hili sio suala la kisiasa, sasa ni Azimio la Bunge ambalo linahitaji kutekelezwa kikamilifu. Suala hili sio suala la Zitto Kabwe tena, ni suala la Bunge, ni suala la Wananchi. Wananchi hawataki uzezeta wa watu waliopewa dhamana ya kutekeleza Azimio lao. Kama hawawezi wapishe watu wenye uwezo wa kusimamia maslahi ya Watanzania kwa kuchukua hatua stahili za kuchunguza utoroshaji mkubwa wa fedha za kigeni, ukwepaji mkubwa wa kodi na ufisadi uliopelekea Watanzania kuficha mabilioni kwenye mabenki nje ya Tanzania. Hatutakaa kimya mpaka tuone mwisho kamilifu wa suala hili. Utekelezaji wa Azimio la Bunge itakuwa ni salamu tosha mafisadi na watoroshaji wa fedha haramu kwamba hawana pa kujificha na Tanzania sio Taifa la kuchezeachezea. Lazima tushinde vita hii. Anayeona hawezi kutuongoza kuishinda atupishe mapema. Hatupaswi kuwa Taifa la Mazezeta. Watanzania sio mabwege tena, Mwakyembe alipata kusema.

 

Kabwe Zuberi Zitto, Mb

Kigoma Kaskazini.

Written by zittokabwe

November 20, 2012 at 6:13 PM