Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Posts Tagged ‘Mpanda Mjini

Siku ya Tatu: Mpanda Mjini-Ziara Kanda ya Magharibi

with one comment

Siku ya Tatu: Mpanda Mjini-Ziara Kanda ya Magharibi

Asanteni wananchi wa Mpanda Mjini. Nawashukuru wananchi wa Mkoa wa Katavi. Mapokezi yenu na heshima kubwa mliyonipa mimi na ujumbe wangu imenipa nguvu sana ya kuendelea kufanya siasa za masuala (issues) na majawabu (solutions). Changamoto za maisha magumu vijijini, ardhi, mbolea ya ruzuku, zao la tumbaku na miundombinu tunazibeba na kuwasemea.

Nawapenda sana watu wa Mpanda.

Mungu awabariki.

PICHA

This slideshow requires JavaScript.

Siku ya Pili: Mpanda ndogo, Kapalamsenga, Karema na Ikola-Mpanda Vijijini

with 3 comments

Jana nilikuwa Jimbo na Mpanda Vijijini ambapo nimetembelea kata za Mpanda ndogo, Kapalamsenga, Karema na Ikola. Nimefanya jumla ya mikutano 6.

Nimezungumza kuhusu Katiba kuwapa nguvu wananchi dhidi ya wanasiasa ikiwemo nguvu ya kuwang’oa wabunge (recall) wanaposhindwa kufanya kazi au kuwa na makosa makubwa ya kimaadili.

Katika mikutano yote nimeambiwa na wananchi kuwa mbolea ya ruzuku ni changamoto kubwa maana inafika baada ya wao kuwa wameshapanda mahindi na hivyo ikifika inakuwa ni upotevu tu. Nimewaambia kuwa mfumo mzima wa mbolea ni mfumo wa kifisadi na suluhisho ni kuachana na mfumo huo na badala yake Serikali iweke utaratibu wa mbolea kuuzwa kwa bei nafuu ikiwemo kujenga viwanda vya mbolea nchini na kupunguza gharama za uzalishaji.

Niliwaambia kila mwaka Bunge linatenga tshs 120 bilioni za mbolea ya ruzuku lakini sehemu kubwa ya fedha inaibwa katika mfumo wa kifisadi.

Kwa uchungu tumezungumza kuhusu hali ya maisha ya watu wa vijijini. Gharama za ujenzi vijijini ni kubwa sana kuliko mijini kutokana na miundombinu mibovu na kutokuwa na sera maalumu ya kusaidia waishio vijijini.

Nimewataka wananchi waungane mkono na CHADEMA ili kuleta mabadiliko nchini na kuhakikisha kilimo kinapewa mkazo na mwananchi wa kijijini anapata umuhimu unaostahili.

Leo tutakuwa Mpanda Mjini ambapo tutafungua matawi ya chama kwenye kata mbalimbali na mkutano mkubwa wa hadhara viwanja vya Kashaulili

PICHA

Written by zittokabwe

October 7, 2013 at 11:19 AM