Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Archive for the ‘WILLIAM NGELEJA’ Category

Ripoti/Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge(“Ripoti ya Jairo”)

with 13 comments

TAARIFA YA KAMATI TEULE YA BUNGE ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA UHALALI WA UTARATIBU WA WIZARA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUPITISHA BAJETI BUNGENI

(Eng. Ramo Matala Makani, Mb.)
MWENYEKITI
KAMATI TEULE YA BUNGE
Novemba, 2011

View this document on Scribd

 

 

Mchango Kwenye Bajeti ya Nishati na Madini

with 3 comments

Bajeti ya Nishati na Madini

MHE. KABWE Z. ZITTO:

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nakushukuru sikutarajia kabisa kama nitachangia leo, lakini nakushukuru sana nadhani umeona mada yenyewe ni mada ambayo mimi ni mdau mkubwa sana wa muda mrefu. Lakini pili pamoja na kwamba Mheshimiwa Mwijage yeye miaka 27 ameitumia katika eneo la mafuta, mimi namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba baada ya kuteuliwa kwenye Kamati ya Jaji Bomani niliamua kwenda kujiongezea maarifa na kusoma Shahada yangu ya Uzamili katika eneo la Mineral Economics na nimeandika katika eneo laFiscal Regime Maeneo ya Kikodi katika Mikataba ya Madini na Mafuta.  Kwa hiyo nakushukuru sana kwa kupata fursa hii ambayo sikuitegemea kabisa kuweza kuchangia.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza nitaanza na eneo la madini.  Ripoti ya Jaji Bomani kuna mapendekezo ambayo iliyapendekeza yameshughulikiwa katika Sheria Mpya na kuna mapendekezo ambayo bado hayajashughulikiwa na hasa kwenye kanuni.  Utakumbuka kwamba katika Sheria Mpya ya Madini tulipitisha viwango vipya vya mirahaba.  Zamani tulikuwa tunatoza asilimia 3 na tukapitisha kwamba sasa tutoze asilimia 4, ingawa Ripoti ya Jaji Bomani ilipendekeza asilimia 5.   Lakini jambo kubwa kuliko yote ambayo tulipendekeza katika ripoti ile lilikuwa ni suala la kubadilisha mfumo wa kukokotoa mrahaba kutoka netbook value kwenda gross value.  Kwa maana ya kwamba sasa hivi Makampuni ya Madini yanapozalisha dhahabu kwa mfano yakiuza yanaondoa gharama za usafirishaji ambazo hatuna control nazo yanaondoa gharama za insurance ambazo hatuna control nazo na gharama nyinginezo ambazo zinaendana na ule usafirishaji katika kukokoto mrahaba.

Sasa ukiangalia tuna mirahaba kwa madini tofauti tofauti.  Nilipiga hesabu hapa mwaka jana tumeuza nje dhahabu ya thamani ya dola bilioni 1.6 ambazo ni sawa sawa na shilingi za Kitanzania takriban shilingi trilioni 2.6 kwa exchange rate ya sasa.  Katika hiyo tuliuza dhahabu peke yake ya thamani ya dola bilioni 1.4, lakini loyalty ambayo ilikusanywa mwaka jana ilikuwa ni shilingi bilioni 80 tu.  Royalty ambayo tunaitarajia kuikusanya mwaka huu wa fedha kwa mujibu wa kitabu volume 1 na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini amezungumza ni shilingi bilioni 99.5.  Hizi ni sawa sawa na asilimia 3.8 ya mauzo yote ya dhahabu ambayo tumefanya nje pamoja na madini mengine.  Iwapo tungetekeleza ripoti kwa kubadilisha mfumo wa kukokotoa mrahaba na kupandisha hiyo asilimia 1 tungekusanya royalty ya shilingi bilioni 198 ambayo ingekuwa sawa na asilimia 7.6 ya madini yote ambayo tunauza nje.

Katika hotuba ya Waziri amesema kwamba Serikali bado inazungumza na Makampuni ya Madini.  Serikali imeanza kuzungumza na Makampuni ya Madini mwaka 2006 ni lini itamaliza mazungumzo hayo na Makampuni ya Madini.  Lazima ifikie wakati kwamba tujione kwamba sisi ni dola iliyo huru, tuna mamlaka yetu katika ukusanyaji wa kodi na hao wenzetu wakubali kwamba na sisi tunapaswa kufaidika na rasilimali zetu za madini.  Nilikuwa naomba kwamba kuanzia tarehe 1 Julai, 2011 Makampuni ya Madini yapelekewe invoice ya royalty kutokana na Sheria Mpya ya Madini ili tuweze kupata mapato ya kutosha na kuweza kuiendesha nchi yetu.

La pili, tulitoa mapendekezo, Makampuni ya Madini yanapouza dhahabu yao nje, sheria yetu ya foreign exchange act inawaruhusu kuweka fedha zote nje.  Fedha ya mapato yote ambayo nimesoma hapa ya 1.6 billion dollars ambazo zinatokana na mauzo yetu ya madini nje yote inawekwa nje, hakuna hata senti inayorudi kwenye Benki za Ndani na ndiyo maana mnaona pamoja na mapato makubwa tunayoyapata kwenye madini na bei ya dhahabu kuongezeka shilingi yetu inatetereka kwa sababu hatuna dola za kutosha ndani ya economy ya ndani.  Sasa tulipendekeza kwamba asilimia 60 ya procurement ambayo Makampuni ya Madini yanafanya ni locally na sasa hivi wananunua vitu vya ndani asilimia 60.  Ripoti ya Jaji Bomani ikapendekeza asilimia 60 ya mauzo ya dhahabu kwa maana fedha za kigeni inayouzwa nje irudi iwekwe kwenye fedha za ndani na ikirudi sasa hivi dola haitakuwa shilingi 1,600 tena itashuka mpaka shilingi 1,200 kwa mujibu wa taarifa za watalaamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba katika regulations za Sheria Mpya ya Madini hili liangaliwe, tuweze kuhakikisha kwamba tunaweka kipengele hiki ili asilimia 60 ya mauzo yanayotokana na dhahabu nje irudi kwenye Benki za ndani.  Tuwe na dola ya kutosha kwenye economy yetu tuweze kudhibiti mabadiliko makubwa sana kuporomoka kwa shilingi yetu. Geological Survey, Mheshimiwa Hamad Rashid katika jambo ambalo nadhani ni trademark yake ni mapping ya nchi kwenye madini.  Amekuwa akizungumza sana nashangaa sijui kwa nini hatumsikilizi.  Sasa hivi hatujui ni kiwango gani mashapo ya madini kiasi gani tuliyonayo nchi nzima. Chombo pekee ambacho kinaweza kutusaidia kufahamu ni Geologocal Survey of Tanzania (GST).  Tembelea Geological Survey zote duniani ni Taasisi zenye nguvu sana.  Sisi Taasisi yetu tunaipa fedha kidogo sana kwa hiyo hatufanyi mapping.  Matokeo yake ni nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafanya mfumo wa kutoa leseni za utafutaji wa madini kwa anayekuja kwanza anapewa kwanza bila ya kujua kiwango cha mashapo ambacho tunacho. Wakati kama tukiitumia vizuri Geological Survey huko siku za usoni tunapokwenda inaweza ikawa inafanya tendering.  Inatangaza tenda kwa sababu itakuwa inajua wapi kuna dhahabu kiasi gani na matokeo yake ni kwamba tutapata fedha nyingi na tunatumia huu mfumo kwa TPDC sasa hivi.  TPDC vitalu vyote vya mafuta ambavyo vinatolewa vinafanywa kwa zabuni, kwa tenda kwa sababu tumewapa jukumu hilo, lakini kwa upande wa leseni za madini hatufanyi hivi. Kwa hiyo nilikuwa naomba voti 58 tuangalie vifungu vya ndani vya voti 58, tufanye reallocation nitapendekeza hili siku ya Jumatatu ili tuongeze fedha kidogo kwenye Geological Survey of Tanzania, tuipe kazi ya kufanya mapping ya nchi tujue rasilimali za madini ambazo tunazo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie gesi.  Waheshimiwa Wabunge waliotangulia kuzungumza na napenda nitoe shukrani zangu za dhati kabisa kwa vijana wenzangu wawili, nimewatangulia Bungeni kwa hiyo ni vijana wangu, Mheshimiwa Mnyika na Mheshimiwa Makamba kwa hotuba zao ambazo zinaonyesha dhahiri kwamba imefikia wakati sasa vijana wachukue utawala wa nchi hii.  Kwa sababu hotuba zao zimetoa mwelekeo wa namna gani ambapo tunaweza tukamiliki rasilimali zetu. Tuna tatizo kwenye mikataba ya gesi, tumeingia mikataba hii inawezekana hatukuwa tunajua ni nini ambacho tunafanya.  Mheshimiwa Mbowe amezungumza hapa Kampuni ya ORICA ambayo ndiyo Kampuni Mama ya Pan African Energy ndiyo yenye mkataba na Shirika la TPDC, (PSA) Products Sharing Agremeent). Pan African Energy ina-operate vile visima.  ORICA Mheshimiwa Mbowe amesema hapa katika taarifa yake ya mwaka na naomba kunukuu.  “Under the terms of the PSA with TPDC, the company liable for income tax in Tanzania at the corporate rate of 30%, however where income tax is payable this is recovered from TPDC by deducting an amount from TPDC’s profit share.  This is reflected in accounts by adjusting the company’s revenues by appropriate amount”

Leo tunavyozungumza Sweden kuna ripoti iliyotolewa na Action Aid zaidi ya dola milioni 13.3 zimekwepwa kama kodi kunatokana na mkataba wa ORICA na TPDC kwa PSA.  Kwa lugha nyepesi ni kwamba ORICA hawalipi kodi ya mapato, wakilipa kodi ya mapato wakati tunapofikia ku-share ile gesi ya ziada ambayo imekuwa imeuzwa wanaondoa fedha yao ambayo waliilipa kama kodi ya mapato, hili jambo sio jipya.  Mwaka 2009 mwezi Aprili, katika Taarifa ya Mwaka ya Kamati ya Mashirika ya Umma tulielezea hapa kwamba tulipoteza shilingi bilioni 2 kutokana na kodi ambayo Pan African Energy walipaswa wailipe kama kodi ya mapato lakini wakairejesha kinyume kupitia TPDC kufuatia mkataba huo wa Production Sharing Agreement.

Mheshimiwa Naibu Spika, ORICA inamiliki Pan African Energy.  Pan African Energy ndio mmiliki wa gesi.  Kimsingi gesi inamilikiwa na TPDC.  Lakini kwa sababu kwanza hatujapewa asilimia 20 yetu ambayo tunatakiwa tuichangie katika umiliki wa gesi.  Lakini pili kwa sababu Pan African Energy imesajiliwa option hayo ndiyo mambo ambayo niliyokuwa nayazungumza juzi wakati wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwamba ORICA imesajiliwa offshore, Pan African Energy  Corporation imesajiliwa offshore.  Halafu you have Pan African Energy Tanzania. Ukishaona tu mfumo wa namna hiyo ni mfumo mkubwa sana wa kupoteza kodi. Naungana na Kamati ya Nishati na Madini, naungana na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mheshimiwa Mnyika kwamba investigation ya kina ifanyike kuhusiana na Production Ssharing Agreement kati ya TPDC na ORICA na Pan African Energy.

Lakini pili, Mheshimiwa Waziri Mkuu aliunda timu ya kuchunguza Mkataba wa Umeme kati ya Songas na TANESCO mwaka 2008.  Tunaomba ripoti ambayo alikabidhiwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ionekane na tuweze kuona namna gani ambapo tunalitatua tatizo hili kwa sababu tunalipa fedha nyingi sana kama capacity charge kwa Songas zaidi ya shilingi bilioni 5 kila mwezi tunalipa na sasa hivi nasikia sijui imefika bilioni 6 hata kama hawajazalisha umeme. Lakini ikitokea matatizo ya uzalishaji wa umeme ni yao.  Kwa mfano juzi ilipotokea visima vikawa na kutu wakashindwa kuzalisha umeme wao hawatulipi, ila sisi tunaendelea kuwalipa capacity charges.  Mambo kama haya ni lazima tuyaangalie na tuyafanyie marekebisho makubwa. Kiongozi wa Upinzani Bungeni ametoa mapendekezo hapa kwamba Wizara ya Nishati na Madini iwe-sprit into two.  Tuwe na Wizara ya Energy and Petroleum Resources na Wizara ya Mine and Minerals Resources.  Mbunge mmoja akatoka akasema kwamba nyie ndio mnalilia Serikali mnasema kwamba ni kubwa, lazima wakati mwingine tujaribu kuangalia mazingira yanayotuzunguka.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna Wizara hapa ya Vitoweo, unaweza ukaivunja ikawa ni Idara tu, lakini uhakikisha kwamba una mtu mmoja akilala, akiamka anawaza umeme.  Akilala, akiamka anawaza gesi na mikataba, uwe na mwingine ashughulike na madini.  Hili sio pendekezo sababu amesema Kiongozi wa Upinzani ndio watu wakaanza kubeza, pendekezo hili Jaji Bomani alilitoa pia na kwenye Ripoti ya Bomani kuna pendekezo hili pia.  Sio kila jambo ambalo Kambi ya Upinzani inalitoa ni baya na sisi ndio tunaathirika na umeme.  Wapiga kura wetu wanakosa ajira, nchi inaumia.  Sasa hivi IMF wamesema kwamba forecast ya growth imeshuka mpaka 1.5% more than one trililion kwenye economic. Mtu mwingine wa kawaida ambaye hajui hizi economic za energy za mining mtu akadhani hilo ni jambo dogo sana.  1.5% ya growth maana yake ni kwamba unaondoa from the economy 1 billion dolar.  Kwa hiyo nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu hili ulisikie, ushauri huu ambao wameutoa Kiongozi wa Upinzani Bungeni uuzingatie na uufanyie kazi mara moja ili tuweze kutatua hili tatizo kubwa ambalo tunalo la umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeiambia Serikali mara kwa mara, kwanza sijui kama nitawahi kumaliza.  Sasa hivi tuna SYMBION inazalisha umeme sijui megawati ngapi kupitia mitambo iliyokuwa ya DOWANS, mitambo hii tuliambiwa ni mitambo chakavu na kelele zilipigwa sana na wengine tulipewa majina mengi sana.  Leo sisikii mtu kila mtu ameufyata, nobody is saying anything kwa sababu sijui ni Wamerikani.  Lakini mimi I am happy kwamba niliyoyasema mwaka 2009 mnayatekeleza mwaka 2011.  Tumeumia sana.  Lakini namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba kabla sijaondoka duniani limeonekana nililolisema na watu wote ambao walikuwa wanapinga wanaona aibu hawasemi sasa hivi.  Sijui kwa sababu Mmarekani amechukua, we don’t know.  Mheshimiwa Mrema alimwuliza Mheshimiwa Ngeleja, maana yake mimi na wewe Ngeleja ndio tulisema tununue, tutekeleze hili.

 

Written by zittokabwe

July 18, 2011 at 11:03 AM