Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Archive for the ‘TANZANIA BUDGET’ Category

Video: Michango yangu Bungeni-Biashara ya Ringtone, Shirika la Posta, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

with one comment

Michango yangu BUNGENI-Kazi na haki za wasanii, biashara ya ringtone, shirika la Posta-Wizara ya Sayansi na Teknologia na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika,
*Sayansi na Teknologia-25.07.2012
*Kuchangia Kilimo-20.07.2012
*Maswali 2 ya Nyongeza-20.07.2012

Benki Kuu: Hazina ya Taifa imekauka?

with 35 comments

 Zitto Kabwe, Mb.

Benki Kuu ya Taifa lolote ndio taasisi pekee yenye takwimu zote nyeti na za uhakika zinazohusu uchumi wa Taifa hilo. Katika tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania eneo la Machapisho kuna Taarifa nyeti sana mbili, Mapitio ya Uchumi ya Mwezi (Monthly Economic Review) inayotoka kila Mwezi katika Mwaka na Mapitio ya Uchumi ya Robo Mwaka (Quarterly Economic Bulletin). Taarifa hizi hutoa taarifa kuhusu masuala yote muhimu yanayohusu Uchumi wa Jamhuri ya Muungano na Uchumi wa Zanzibar ikiwemo taarifa za Mfumuko wa Bei, Mapato na Matumizi ya Serikali, Mwenendo wa Biashara ya Kimataifa na Deni la Taifa.

Ukienda kwenye tovuti ya Benki Kuu leo utakuta Taarifa hizi. Lakini Taarifa hizi zimeishia Desemba mwaka 2011 zikitaarifu masuala ya Uchumi ya Mwezi Novemba na robo ya mwaka inayoishia Desemba. Ukitaka kujua Bajeti ya Serikali na mwenendo wake hutapata taarifa za sasa bali za Mwezi Novemba mwaka 2011, miezi sita nyuma. Huu sio utendaji uliotukuka. Hii ni kuficha taarifa kwa wananchi. Taarifa zinafichwa ili iwe nini? Nani anafaidika na kufichwa kwa taarifa muhimu kama hizi?

Kuna tetesi kwamba Hazina ya Taifa (Hifadhi ya Fedha za kigeni – foreign reserve) inakauka, kwamba tuna hifadhi ya kuagiza bidhaa nje kwa mwezi mmoja tu. Niliposikia tetesi hizi sikuamini. Nilipoenda katika tovuti ya Benki Kuu ili kuweza kuwa na habari rasmi (authoritative) nimekuta takwimu za Novemba 2011.

Takwimu ya Mfumuko wa Bei iliyoko kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania ni ya mwezi Novemba mwaka 2011!

Ukitaka kujua mwenendo wa Bajeti ya Serikali kama makusanyo ya Kodi na Matumizi utapata Taarifa ya Mwezi Novemba mwaka 2011.

Ukitaka kujua manunuzi ya Mafuta (fuel imports) kwa miezi 3 ya mwanzo ya mwaka 2012 ili kuweza kuona namna Umeme wa dharura umeathiri urari wetu wa Biashara ya Nje hupati taarifa hiyo katika tovuti ya Benki Kuu.

Taarifa zinafichwa.

Ndio. Zinafichwa tena makusudi maana taarifa hizi zipo Benki Kuu. Huu ni uzembe maana Nchi inawalipa wafanyakazi wa Benki Kuu mishahara minono ili wafanye kazi hizi. Benki Kuu pia imetoa zabuni kwa Kampuni Binafsi kuchapisha Taarifa hizi. Kama Taarifa hazitoki kwa wakati ni wizi. Wizi ambao haupaswi kufumbiwa macho.

Benki Kuu ya Tanzania ipo miezi Sita nyuma. Aibu kubwa sana.

Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano akihakikishia mataifa duniani kuhusu uwazi Serikalini (#OGP), Taasisi kubwa kama Benki Kuu inaficha Taarifa ambazo ni nyeti kwa wananchi na muhimu kwa wafuatiliaji wa sera za Serikali. Rais wa nchi anaongea Buluu, Gavana wa Benki Kuu anasimamia Kijani!

Inaudhi na kukera sana kwenda kwenye tovuti ya Benki Kuu na kukuta taarifa za miezi Sita iliyopita. Benki Kuu hamstahili kuitwa Benki Kuu, labda benki kuu kuu. Rekebisheni jambo hili haraka sana maana kuficha taarifa kwa Umma ni ufisadi. Haki ya kupata taarifa ni haki ya msingi katika Katiba yetu.  Hatutaki kushtukizwa na kuambiwa Hazina ya Taifa imekauka.

Prof. Ndulu hakikisha Taarifa ya Mapitio ya Uchumi wa kila Mwezi imewekwa kwenye tovuti kwa muda mwafaka. Ifikapo mwisho wa Wiki inayoanzia Jumatatu Mei 14, tovuti ya Benki Kuu iwe na Taarifa za miezi yote (Desemba, Januari, Februari, Machi na Aprili). Taarifa hizi ni muhimu ili nasi tutekeleze majukumu yetu ya Kikatiba kama Wabunge, Mawaziri vivuli na Wananchi wa Tanzania.

PRESS RELEASE: On Government Austerity Measures-Cut Re-current Expenditure Not Development Expenditure

with 15 comments

PRESS RELEASE

MPANGO WA SERIKALI KUPUNGUZA MATUMIZI

Punguza Matumizi ya Posho SIYO Matumizi ya Reli, Barabara, Elimu na Afya

Mwezi Disemba mwaka 2011 Waziri wa Fedha na Uchumi alimwandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) kumwahidi mambo yepi Serikali ya Tanzania itafanya ili kurekebisha Bajeti yake. Utaratibu huu hufanyika kila mwaka kupitia mpango unaoitwa ‘Policy Support Instrument (PSI). Katika barua hiyo Waziri wa Fedha wa Tanzania ameahidi kwamba Serikali itafanya juhudi kupunguza matumizi ili kuweza kupunguza uwiano wa nakisi ya Bajeti na Pato la Taifa (fiscal deficit to GDP ratio) kutoka asilimia 7.2 mpaka asilimia 6.6 ya Pato la Taifa.

Waziri wa Fedha na Uchumi ameiambia IMF kwamba ifikapo mwisho wa Mwezi Disemba mwaka 2011 (wiki mbili zilizopita) Baraza la Mawaziri la Tanzania limefikia maamuzi ya kupunguza nakisi ya Bajeti kwa kiwango kilichotajwa. Maeneo yanayotajwa ni Pamoja na Miradi ya Maendeleo ambapo jumla ya miradi yenye thamani ya Tshs 157bn itakatwa. Waziri
wa Fedha ametaja miradi hiyo katika Ukarabati na Ujenzi wa Miundombinu.

Kambi ya Upinzani Bungeni inapinga kuondolewa kwa miradi ya maendeleo ili kupunguza matumizi ya Serikali. Kimsingi wakati kama huu ambapo hali ya uchumi ni mbaya na vijana wengi vijijini na mijini hawana ajira tunasisitiza umuhimu wa kutumia zaidi kwenye miradi ya maendeleo.

Punguza matumizi ya kawaida

Kambi ya Upinzani Bungeni inarejea wito wake kwa Serikali kupunguza matumizi ya kawaida ili kupata fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo. Haiwezekani kamwe tukawa Taifa huru iwapo miradi yetu yote ya maendeleo inafadhiliwa na wahisani. Kiwango kidogo tulichokiweka katika Bajeti ya mwaka huu ndicho hicho sasa kinakatwa na hivyo miradi yote ya maendeleo kubakia kwa wahisani ama kwa mikopo au misaada. Kiwango cha Tshs 203bn sawa na 0.5% ya Pato la Taifa ambacho Serikali imeahidi kupunguza ni kidogo mno na kinalenga kuumiza watumishi wa kada ya chini ya Serikali na sio viongozi wakubwa. Bajeti ya Mafunzo inayoenda kukatwa itaumiza Manesi na Walimu au watumishi wanaoongeza ujuzi ili kuboresha kazi zao. Serikali ikate matumizi yote yasiyo ya lazima na hasa posho (360bn), ipunguze matumizi ya magari na yale yasiyo na uhitaji yapigwe mnada na viongozi wote isipokuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika na Jaji Mkuu washushwe madaraja ya kusafiria kwenye ndege. Safari zote ambazo hazina mahusiano na miradi ya maendeleo zipigwe marufuku kwa muda wote wa miezi sita ya Bajeti iliyobakia.

Serikali ihakikishe matumizi katika Sekta ya Elimu na Afya hayakatwi kabisa ili kuhakikisha tunalinda mafanikio kiduchu ya upanuzi wa sekta hizi na kuongeza uwezo wa Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi hasa wa vijijini.

Matumizi ya Maendeleo yasiguswe, yaongezwe

Tayari imeonekana kwamba katika kipindi chote cha nusu ya Bajeti Halmashauri za Wilaya hazijapata fedha za maendeleo. Mfano Halmashauri ya Wilaya Kigoma imepata asilimia 0.3 tu ya Bajeti ya Maendeleo ilhali Halmashauri ya Mji wa Mpanda imepata asilimia 4 tu. Ni dhahiri miradi ya maendeleo kwa maeneo mengi ya vijijini itakwama kwani ni wazi kabisa kwamba Halmashauri hazipati fedha zote za Bajeti ya Maendeleo. Serikali itambue kwamba miradi ya maendeleo sio anasa bali ndio vyanzo vya baadaye vya mapato ya serikali. Miradi ya maendeleo hutoa ajira kwa wananchi na hivyo kuwapunguzia umasikini wa kipato. Jumla ya Tshs 157bn zinazotakiwa kukatwa zisikatwe bali ziongezwe ili kupata fedha za kurekebisha miundombinu kama Reli ya Kati.Kwa mfano Reli ya Kati inahitaji Tshs 200bn katika kipindi cha miaka 3 ili iweze kusafirisha mizigo tani 1.5m kwa mwaka kila siku na kuzalisha faida.

Ongeza Mapato ya Ndani

Inashangaza kwamba katika mpango wa Serikali kupunguza nakisi ya Bajeti mkazo umewekwa kwenye kuondoa miradi ya maendeleo badala ya kuongeza mapato. Nakisi hupunguzwa ama kwa kupunguza matumizi au kwa kuongeza Mapato. Serikali katika Taarifa yake kwa IMF imeibua njia moja tu ya kuongeza mapato, kodi ya mapato kutoka Kampuni ya Geita Goldmine. Huu ni uvivu wa kufikiri.

Serikali imeambiwa mara kadhaa suala la kuanza kutumika kwa sheria mpya ya madini kwa Kampuni za Madini zilizokuwapo. Makusanyo ya Mrahaba peke yake kwa sheria mpya, kiwango kipya na kanuni mpya ya kukokotoa ingeongeza mrahaba mpaka Tshs 203bn kutoka Tshs 99bn za sasa. Kwanini Serikali ianvuta miguu katika kutekeleza hili? Waziri wa Nishati na Madini aliahidi Bungeni kwamba mazungumzo na Kampuni za Madini yanaisha Mwezi Septemba. Mbona Serikali imekuwa BUBU katika hili?

Serikali iliahidi kuangalia suala la mauzo ya mali za makampuni zilizoko Tanzania na kodi ambayo tunapaswa kukusanya, Serikali imekuwa kimya kabisa katika suala hili. Marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kuondoa msamaha kwenye ‘deemed capital goods yangeongeza mapato ya Serikali kwa kiwango kikubwa na kupunguza mzigo wa
misamaha ya Kodi.

Uwajibikaji kwa Bunge

Inashangaza zaidi kwamba sasa imekuwa ni mtindo kwa Serikali kutoa ‘commitments’ muhimu za kibajeti kwa Shirika la IMF badala ya wananchi kupitia Bunge. Bunge limepitisha Bajeti, mapitio yeyote ya Bajeti yanapaswa kuidhinishwa na Bunge. Bila kufanya hivyo maana ya Bunge kupitisha Bajeti inakuwa haina mantiki na uhuru wa Taifa letu unakuwa haupo kwetu.

Umuhimu wa Bunge kutunga haraka Sheria ya Ofisi ya Bajeti ya Bunge (Parliamentary Budget Act) sasa unaonekana waziwazi. Muswada umewasilishwa Bungeni na Wabunge binafsi kutaka kuundwa kwa mfumo wa kuisimamia Serikali katika Bajeti. Ofisi ya Spika wa Bunge ihakikishe muswada huu unachapishwa katika Gazeti la Serikali mara moja ili usomwe kwa mara ya kwanza katika mkutano wa Sita wa Bunge na kutungwa kuwa sheria katika mkutano wa Saba.

Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali ilete mpango wa kupunguza matumizi Bungeni ili ujadiliwe na kuidhinishwa na Bunge kabla ya kuanza kutumika. Vinginevyo Mpango wa Serikali kwa IMF utakuwa ni kudharau wananchi na kuuza uhuru wetu kwa Shirika la Fedha la Kimataifa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mwishoni mwa miaka ya Sabini ‘toka lini Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limekuwa Wizara ya Fedha ya Kimataifa (International Ministry of Finance)?’

Kabwe Zuberi Zitto, Mb

Waziri Kivuli Fedha na Uchumi

Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni (NKUB)

Dar es Salaam, 10 Januari 2012.

Mkulo, Zitto lock horns on inflation(via The Citizen)

with 2 comments

 

By Alawi Masare
The Citizen Reporter

Dar es Salaam. Finance and Economic Affairs minister Mustafa Mkulo has countered the recent assertion by his parliamentary shadow counterpart, Mr Zitto Kabwe, that the spiralling inflation that had persisted over the past six months had caused a six per cent budget deficit.Mr Mkulo argues that there is no significant relationship between the two variables, but in a quick rejoinder, Mr Kabwe (Chadema-Kigoma North) expressed amazement at the minister’s reaction.Speaking to this paper yesterday from Kigoma where he is on end-of-the-year holidays, he remarked that “the ministry is out of touch with the basics of the economy”.

Mr Mkulo’s reaction was in response to comments made by Mr Kabwe last week, against the backdrop of the inflation rate chalking 19.2 per cent in November.Mr Kabwe, who also doubles as deputy leader of the official opposition in the Parliament, said the government’s  capacity to pay for goods and services had been diminished by six per cent by the growing inflation.He warned that the deficit (equivalent to Sh780 billion) would affect the economy seriously if it was not contained immediately.

However, Mr Mkulo told The Citizen on Monday that the said deficit didn’t feature in the budget which he tabled in the Parliament in June this year.Brushing aside Mr Kabwe’s comments, he was emphatic that the government would proceed with implementation of its budget as planned.He accused Mr Kabwe of misleading the public on the issue, characterising his sentiments as political gimmickry associated with his being in the opposition camp.

Mr Mkulo remarked in a telephone interview: “I am the minister who supervises the data body (National Bureau of Statistics-NBS) and the central bank, but so far, no such information has been brought to my notice.  Where did he get it?”

Generally, the government may run a budget deficit when its expenditure exceeds total tax revenue in a given year. And one of the factors which might diminish the government’s purchasing power is spiralling inflation, according to economists.

As part of a verbal ping-pong, Mr Kabwe wondered who, between him and Mr Mkulo, was politicising the matter.
“Any economist you would talk to would tell you that increasing inflation is not healthy for the budget.”
“He has demoted our country from a stable economy to the current situation in which  even macro economy fundamentals are starting to become unstable; it is  high time he vacated the office,”  Mr Kabwe furiously remarked.

Mr Kabwe said if Mr Mkulo could not fathom the impact of increasing inflation on the national budget, then “he is out of touch with economic fundamentals and is not supposed to handle such a high portfolio in the government.”
When the budget was endorsed in July, the inflation rate was recorded at 13 per cent and by last month it had jumped to 19.2 per cent.

According to Mr Kabwe, the trend means  that the government’s capacity to pay for goods and services has been reduced by about six per cent, equivalent to Sh780 billion evaporating from the budget within four months of its implementation.According to the Bank of Tanzania (BoT)’s September monthly economic review, during August 2011,  government budgetary operations on cheques issued, registered a deficit of Sh112.1 billion after adjustment to cash.

Economists fear that the government would either jump into borrowing or cutting expenditure,  hence increasing debts or sometimes denying  the public of vital services.

“If the government is running a budget deficit, it has to borrow this money through the issue of government debt such as Treasury Bills and long-term government bonds,” commented Dr Honest Ngowi of the Mzumbe University Business School.He added: “Sometimes it may decide to cut expenditure, which I think is a bad option because by so doing it will not implement some important projects planned earlier.”

He also warned that the second half of the financial year may require more expenditure following the increase in allowances for MPs and widen the deficit.“The recent floods in Dar es Salaam and some other parts of the country are also increasing government spending,” he noted.

Source: The Citizen Newspaper

 

Written by zittokabwe

December 28, 2011 at 12:07 PM

HOTUBA YA WAZIRI KIVULI WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012

with 12 comments

View this document on Scribd

Dondoo/Highlights

Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma

Mashirika ya Umma mia tatu sitini (360) yalibainishwa (specified) kwa ajili ya ubinafsishaji mpaka Disemba 2009

Kati ya Mashirika hayo, Mia Tatu Thelathini na Moja (331) yamebinafsishwa na ishirini na tisa (29) yalikuwa katika hatua
mbalimbali za kubinafsishwa

Mapato la serikali kutokana na ubinafsishaji huo yalikuwa Shilingi billion 482. Hii maana yake ni wastani wa shilingi 1.5 bilioni kwa kila Shirika lililouzwa

Huu ni wakati mwafaka wa kufanya tathmini ya kina juu ya sera utekelezaji wa Sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma (Public Inquiry on Privatisation)

Ubinafsishaji pamoja na uwekezaji kwa ujumla haujaweza kutanzua tatizo la ajira ambalo linawakumba vijana wengi

Mashirika mengi ya umma yaliyobinafsishwa wawekezaji wameshindwa kutekeleza mambo/masharti waliyokubaliana na serikali hii ikiwa ni pamoja na wao kufanya mambo mengine kinyume na makubaliano kwa mfano Kiwanda cha Urafiki Dar es Salaam ambapo mwekezaji kutoka China amekuwa akiuza baadhi ya mashine kama vyuma chakavu

Usimamizi wa Mashirika ya Umma

Serikali imetenga shilingi bilioni 35.7 zikiwa fedha za kulipia madeni na mahitaji ya dharura kwa Mashirika ya Umma

Serikali imetenga shilingi bilioni 26.4 kwa ajili ya kulipa fidia kwa mikataba mbalimbali ambayo serikali imeingia

Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR-Treasury Registrar) imekuwa dhaifu mno katika kusimamia mali za serikali Katika Mashirika. *Mifano miwili ya namna hisa za Serikali zilivyouzwa itasaidia kuonyesha hali hii. Kampuni ya Oryx ilikuwa inamilikiwa na Serikali kwa asilimia hamsini mpaka mwaka 2004. Mwaka 2004, kupitia ofisi ya TR serikali iliuza hisa zake ambazo ni asilimia 50% kwa bei ya kutupa kwa thamani ya dola 2.5 milioni. Hivi sasa Oryx ni moja ya Kampuni inayofanya vizuri sana katika sekta ya Mafuta lakini hatuna umiliki tena na pesa kiduchu tulizopata zimekwishatumika!

*pia serikali ilikuwa na hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Mobitel ambayo kwa sasa inajulikana kama “tigo”. Katika hatua ya kushangaza na haina maelezo kabisa Serikali imeuza hisa zake asilimia kumi na sita (16%) kwa thamani ya dola 1.3 milioni mwaka 2006 na kwa sasa kampuni hiyo ni ya kigeni kwa asilimia mia moja jambo ambalo ni kunyume na sheria. Kampuni za Simu zatakiwa kumilikiwa na Watanzania kwa sio chini ya Asilimia 35. Asilimia 16 ya hisa Tigo leo thamani yake ni zaidi yakumi ya bei tuliyouza mwaka 2006.

Ofisi ya Msajili wa hazina (TR) ifumuliwe na ianzishwe ofisi ya Mashirika ya Umma ambayo itakuwa ni kama Wakala wa
Serikali chini ya Wizara ya Fedha ikiwa ni chombo huru chenye kusimamia Mashirika yote ya Umma (Office of Public Enterprises– OPE))

Mashirika yaliyo katika Sekta nyeti kwa umma yasibinafsishwe tena na badala yake yaendelee kumilikiwa na Serikali kwa
kuweka Menejimenti mahiri na kuwa na lengo la kuorodhesha hisa zao katika Soko la Hisa la Dar es Salaam ili kumilikisha
wananchi na kuweka uwazi katika uendeshaji.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania/National Bureau of Statistics-NBS

Mapendekezo ya kuboresha utendaji wa Ofisi ya Takwimu

Taarifa mbali mbali za takwimu zitolewe kwa uwazi ikiwahusisha wanahabari na wataalamu wa kada mbalimbali kama vile wachumi na kuwepo mjadala wa wazi kuhusiana na taarifa hiyo

Kuwa na uhisiano wa moja kwa moja wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa na ngazi za mikoa, halmashauri za wilaya, kata na vijiji
kurahisha upatikanaji wa takwimu ili zisaidie katika kupanga mipango ya maendeleo.

Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA

Kambi ya upinzani tunaitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania kuanza mara moja kufanya utafiti wa namna bora ya kutoza kodi ya faida kwenye dhahabu (windfall tax) ili kuongeza mapato ya serikali kwa sababu wawekezaji wanapata faida mara dufu kwa sasa kwa sababu ya ongezeko hilo la bei.

Deni La Taifa

Deni la taifa liliongezeka kwa asilimia 38% kutoka trilioni 7.6 mwaka 2008 mpaka Tshs 10.5 trilioni mwaka 2009/2010,
hadi kufikia mwisho wa mwezi Aprili 2011 kwa mujibu wa tamko la hali ya kifedha la Benki Kuu ya Tanzania la Juni 2011, deni la taifa lilikuwa dola za kimarekani milioni 11,455.4 sawa na shilingi trilioni 17.1 ambapo asilimia 80 ya deni hilo ni deni la nje

Wakati wenzetu wanakopa ili kuongeza uzalishaji (capital investments), sisi tunakopa kwa matumizi ya kawaida

Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

Kuna kuna mifuko mitano ya hifadhi ya jamii nchini yenye jumla ya wanachama 1,073,441

Kati ya hao Shirika la NSSF lina wanachama 506,218 (47%), Shirika la PSPF lina wanachama 289,046 (27%), Shirika la PPF lina wanachama 160,068 (15%), Shirika la LAPF lina wanachama 73,833 (7%) na Shirika la GEPF ambalo lina wanachama 35,279 (4%)

Idadi hii ya wanachama katika Mifuko yote ni sawa na asilimia 2.5 ya idadi ya watu waliopo nchini na ni asilimia 4.7 ya nguvu kazi yote iliyo katika sekta rasmi ya ajira

Mifuko hii imewekeza katika vitega uchumi vyenye thamani ya shilingi trilioni 2.8, ambayo ni takribani asilimia 8.7 ya Pato la Taifa kwa bei za sasa. NSSF inaongoza kwa kuwa na uwekezaji wenye thamani ya
shilingi trilioni 1.03 (38%), PSPF inafuatiwa kwa kufanya uwekezaji wenye thamani ya shilingi bilioni 751 (27%), PPF uwekezaji wenye thamani ya shilingi bilioni 670 (24%), LAPF shilingi bilioni 206 (7%) na GEPF shilingi bilioni 82 (3%)

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni bado inasisitiza ushauri wake kuwa Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii ihamishiwe Wizara ya Kazi na Ajira kama Wizara inayohusika na ‘social security’. Hata Mdhibiti wa Mifuko (SSRA) yupo chini ya Wizara ya Kazi.

Hakuna sababu ya kuwa na utitiri wa mifuko mingi kama ilivyo sasa. Ipunguzwe na kubakia na mifuko miwili tu, mmoja wa wafanyakazi walio aktika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi na mwingine kwa wafanyakazi wa sekta ya umma.

NSSF na PPF iunganishwe kuwa mfuko mmoja kwa ajili ya sekta binafsi na isiyo rasmi na PSPF, LAPF na GEPF iunganishwe na kushughulika na wafanyakazi wa Sekta ya Umma

Huduma Kwa Wastaafu kwa Ujumla

Madeni ya PSPF ya michango ya kabla ya Julai 1999

watumishi wa umma wanaolipwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanapostaafu hulipwa mafao yao tangu kipindi walipoanza kazi, japo wao wameanza kuchangia kuanzia Julai 1999. Kipindi cha Julai 1999 kurudi nyuma ni deni ambalo serikali inapaswa kuulipa Mfuko huu wa PSPF. Kwa bahati mbaya deni hili lilikuwa halilipwi kwa kipindi chote tangu Mfuko uanzishwe hiyo Julai 1999, na limeendelea kukua na kuwa deni kubwa sana sasa; takriban Shs 3,380 Billioni.

Nyongeza ya kiwango cha Pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu

Masuala ya Jumla

Miundo Kandamizi kwa Watumishi wa kada ya Uhasibu Serikalini

Uwajibikaji ndio suluhisho kubwa kwa matatizo ya rushwa, hongo, ubadhirifu na ufisadi

Kambi ya Upinzani tutaendelea kuwa jicho la watanzania dhidi ya watawala, ninawataka Mawaziri Vivuli wote wafuatilie kwa karibu sana utendaji wa Mawziri katika maeneo yao ili kuhakikisha kuwa bajeti hii inatekelezwa kwa faida ya mwananchi wa kawaida.

Video Clip: Zitto na Bajeti Mbadala ya Upinzani (Courtesy of Mwanakijiji)

with one comment

Written by zittokabwe

June 16, 2011 at 12:10 AM

Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/2012 ina upotoshaji mkubwa

with 4 comments

Private Member’s Bill: Notice to Establish a Parliamentary Budget Office

with 4 comments

Update:

Following  wide consultation and a meeting between several members of the house and Policy Forum i have decided to withdraw the bill. After improvement the bill will be presented by group of MPs together. Hon. Ndugulile will coordinate the group

Zitto Kabwe

 

OBJECTIVES/ REASONS FOR THIS BILL

The objective of this Bill is to enact a law establishing a Budget Office under Parliamentary Service; to provide for a budgetary procedure and oversight of the National Budget.

The Bill is divided into Five Parts as follows:-.

Part 1 contains  preliminary provisions which  include a short title, commencement date and interpretation clause.  Part II deals with provisions establishing the Budget Office and its functions.

Part III  contains provisions that set out the budgetary process; the  National Budget Plan, annual estimates and preparation of budget by public corporations. Part IV makes proposals for oversight  monthly publication of  revenues of the National Budget and  compliance report .

Part V provides for miscellaneous issues such as authority to obtain information and regulations.

MADHUMUNI NA SABABU

Muswada huu unakusudia kutunga Sheria itakayoanzisha Ofisi ya Bajeti itakayokuwa chini ya Ofisi ya Bunge, kuainisha mchakato wa kushughulikia Bajeti ya Serikali na usimamizi wake.

Muswada umegawanyika katika Sehemu Kuu Tano:-

Sehemu ya Kwanza inahusu mambo ya utangulizi ambayo ni jina la Sheria , tarehe ya Sheria kuanza kutumika na tafsiri ya maneno mbalimbali yaliyotumika katika Sheria hii. Sehemu ya Pili inaanzisha Ofisi ya Bajeti, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Bajeti pamoja na kuainisha majukumu yao.

Sehemu ya Tatu inahusu mchakato wa kutengeneza Bajeti, makisio ya mwaka na utaratibu wa taasisi za umma kuwasilisha Makisio ya Bajeti zao kwenye Wizara Mama.

Sehemu ya Nne inahusu utaratibu wa usimamizi wa fedha za Serikali na Sehemu ya Tano inahusu masuala ya jumla ambapo inatoa utaratibu wa kutoa taarifa na mamlaka ya kuandaa Kanuni chini ya Sheria hii.

Dar-es-Salaam

03 Juni, 2011

Zitto Zuberi Kabwe

Mbunge wa Kigoma Kaskazini

View this document on Scribd

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA KABWE ZUBERI ZITTO(MB) WIZARA YA MIUNDOMBINU KUHUSU MPANGO NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA BAJETI,KWA MWAKA WA FEDHA 2010/2011

with one comment

___________________

UTANGULIZI:

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Kambi ya Upinzani naomba nitoe maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu hotuba ya bajeti ya Wizara ya Miundombinu kwa mwaka wa fedha 2010/2011 kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Kanuni ya 99(7) toleo la Mwaka 2007.

Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Hamad Rashid Mohamed kwa kuniteua kuwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Miundombinu kwa kipindi cha takribani miaka mitatu sasa. Namshukuru kwa miongozo yake na kuiweka kambi katika uongozi dhabiti akishirikiana na Naibu wake Dkt. Willibrod Slaa. Namshukuru pia Naibu Waziri Kivuli Mhe. Shamis Bakar Faki kwa kazi yake nzuri katika kamati ya miundombinu na vilevile kwa ushirikiano wake mkubwa name katika kuisimamia serikali kupitia Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni katika Bunge la Tisa imefanya kazi kubwa sana ya kuwasemea Watanzania na hasa Watanzania wasio na sauti na hivyo kuleta mabadiliko makubwa katika uongozi wa Taifa letu. Kambi ya upinzani Bungeni bila ya woga wala upendeleo imekuwa ikisema ukweli kuhusiana na jinsi Taifa letu linavyoongozwa na kuibua maovu yote kwa lengo la kuhakikisha kuwa mlipa kodi wa Tanzania anapata thamani ya kodi anayolipa. Kambi ya upinzani Bungeni imetimiza wajibu wake wa Kikatiba wa kuwa Serikali mbadala kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita na sasa tunatoa rai kwa Watanzania kutukabidhi serikali ili tuweze kuiongoza tofauti na ufanisi zaidi kwa kuondoa ufisadi uliokithiri, kupambana na umasikini kwa kukuza uzalishaji mali viwandani na mashambani na kujenga miundombinu imara.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kuwashukuru wananchi wa jimbo langu la Kigoma Kaskazini kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa katika kazi zangu. Katika kipindi cha miaka mitano tumefanya kazi kubwa sana ya kuleta maendeleo katika Mkoa wetu wa Kigoma na Jimbo letu la Kigoma Kaskazini. Mwaka 2005 kulikuwa kuna mtandao wa barabara za lami wenye kilomita 8 tu mkoa mzima wa Kigoma, leo kuna mtandao wenye kilomita 80 na ifikapo Oktoba mwaka 2010 kutakuwa na Mtandao wenye kilomita zaidi ya 100 baada ya kukamilika kwa barabara ya Mwandiga Manyovu (Asilimia 90 ya Mtanadao huu wa barabara upo katika Jimbo la Kigoma Kaskazini). Mwaka 2005, kulikuwa na uwezo wa kuzalisha 4MW za umeme pekee, leo tuna uwezo wa kuzalisha 11MW. Mwaka 2005 hapakuwa na Gati hata moja katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, leo magati mawili yanajengwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania – moja Kigoma kusini na linguine katika Kijiji cha Kagunga jimboni Kigoma Kaskazini. Mwaka 2005 hatukuwa na Bweni hata moja la Wanafunzi wa kike katika Shule za Sekondari, leo Kigoma Kaskazini peke yake inajenga mabweni 3 katika shule tatu tofauti ili kuhakikishe mabinti wa Kigoma Kaskazini wanasoma bila matatizo. Wakati Rais Jakaya Kikwete ametembelea Mkoa wa Kigoma, ukiachana na miradi ya kimkoa aliyozindua miradi mingine yote ilizinduliwa ni ya Kigoma Kaskazini peke yake. Watu wa Kigoma Kaskazini wanajivunia sana mafanikio haya ambayo yametokea ndani ya miaka mitano tu.

Mheshimiwa Spika, Napenda kurejea kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa niaba ya wakazi wote wa Kigoma, kwa kutusikiliza watu wa Kigoma na hususani kwa kunisikiliza mimi binafsi nikiwa Mbunge pekee wa Upinzani wa majimbo kutoka Mkoa wa Kigoma. Maneno aliyoyasema Rais kuwa Serikali haibagui maeneo kulingana na itikadi za vyama, alipokuwa akizindua Mitambo ya Umeme Kigoma ndio maneno ya kiungwana katika demokrasia yeyote duniani. Bado kuna changamoto nyingi sana Kigoma na tutaendelea kuzisemea ili nasi watu wa Kigoma tujione kuwa tupo sehemu ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, Natambua kuwa Mkandarasi wa kujenga kipande cha Kidahwe Uvinza katika barabara ya Kigoma Tabora tayari amepatikana. Nawashukuru sana watendaji wa TANROADS na hasa Mkurugenzi Mkuu na Meneja wa Mkoa wa Kigoma kwa kuwa wepesi katika kuhakikisha miradi ya Kigoma inakwenda haraka. Natambua kuwa Fedha zimetengwa katika Bajeti kwa ajili ya kipande cha Kidahwe Kasulu katika Barabara kuu ya Kigoma Nyakanazi. Nawashukuru sana Wizara ya Miundombinu kwa kutenga fedha hizi katika Bajeti na kuwapongeza sana wabunge wote kabisa wa Mkoa wa Kigoma bila kujali itikadi za vyama kwa ushirikiano mkubwa uliopo kuhusu miradi ya miundombinu katika Mkoa wa Kigoma. Ninaiomba Serikali na hasa Wizara ya Miundombinu iharakishe mchakato wa kumalizia malipo ya fidia kwa wananchi waliobomolewa nyumba zao kupisha ujenzi wa barabara hizi.

Mheshimiwa Spika, Kwa Wabunge wa Kigoma tofauti na mimi na kwa michango yao ya kuchochea maendeleo ya mkoa wetu wa Kigoma, mungu atawalipa lakini siwaombei mrudi Bungeni kwani ni lazima kuimarisha demokrasia ya vyama vingi kwa kuchagua wabunge wengi zaidi wa Upinzani na mkoa wa Kigoma ni muhimu na lazima kupata wabunge wengi kutoka kambi ya upinzani ili kupaza sauti ya Kigoma zaidi, jambo ambalo wabunge kutoka CCM wanakwazwa. Hata hivyo tutawakumbuka katika historia kama wabunge mliokuwepo katika miaka muhimu ya mabadiliko katika mkoa wa Kigoma na Mungu awajaalie huko mwendako!

MASUALA YA JUMLA

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Usafirishaji (Transport services) ndio sekta inayoonekana ya kimkakati katika uchumi wa Tanzania. Nafasi ya kijiografia ya Tanzania inatoa upendelea wa pekee wa sekta hii kuwa sekta chocheo kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa letu. Sekta hii ina mahusiano mazuri na chanya (positive strong linkages) na shughuli nyingine za kiuchumi pia inagawa vizuri faida za ukuaji uchumi (strongly supportive of broad based enabling environment) na inaweza kutengeneza ajira nyingi sana. Sekta hii inajumuisha usafiri wa Reli, Barabara, Anga na usafiri wa Majini. Sekta hii kwa Tanzania ni moja ya sekta zinazokua kwa kasi na mchango wake katika pato la Taifa ni takribani asilimia 7, hii ni zaidi ya mara mbili ya mchango wa sekta ya madini katika GDP na zaidi ya mara sita ya mchango wa sekta ya umeme na gesi katika uchumi.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo sekta ya Usafirishaji imegubikwa na changamoto nyingi sana na ni moja ya sekta ambazo licha ya umuhimu wake haipewi kipaumbele kabisa katika maamuzi ya Serikali. Iliichukua serikali zaidi ya miaka 3 kupata suluhisho kuhusu kitengo cha Makontena katika Bandari ya Dar es Salaam na kusababisha usumbufu mkubwa sana kwa wateja wa bandari yetu na hivyo kupoteza biashara kwa kiwango kikubwa sana. Imeichukua serikali zaidi ya miaka 4 kushughulikia suala la Ubinafsishaji wa Uwanja wa ndege wa KIA na kuinunua kampuni ya KADCO na mpaka sasa bado menejimenti haijawa ya Shirika la Serikali. Imeichukua serikali miaka mitano bila kupata suluhisho kuhusu ubinafsishaji wa Shirika la Reli Tanzania na hata kuweza kumaliza ubinafsishaji huo na kuua kabisa usafiri wa Reli nchini. Inaendelea kuichukua serikali miaka kadhaa kumaliza tatizo la Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na kuhatarisha sana biashara ya utalii nchini.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Miundombinu imekuwa ni Wizara yenye matatizo kuliko wizara zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati gazeti la Sunday Citizen, liliita Wizara ya Nishati na Madini ‘the most corrupt ministry of the year 2007’, Wizara ya Miundombinu imekuwa ‘the most incompetent Ministry’ katika kipindi chote cha utawala wa miaka mitano ya Awamu ya nne. Hii ni kutokana na hoja kuwa katika wizara hii hakuna maamuzi yanayochukuliwa katika masuala mengi sana na hivyo kusabibisha hasara kubwa kwa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inamtaka  Waziri wa Miundombinu alieleze Bunge na Taifa kwa Ujumla juu ya utekelezaji wa Program ya Maendeleo ya Sekta ya Usafirishaji (TSIP). Huu ni mwaka wa tatu wa TSIP, Serikali haisemi hatua za utekelezaji ili tuweze kuipima. Kama rasilimali hazielekezwi katika ‘blue prints’ ambazo tumezipanga wenyewe, ni kwa nini tunatumia muda na fedha kuweka mipango hii?

Mheshimiwa Spika, nchi yetu imejaaliwa na Mungu kwa kuzungukwa na Bahari ya Hindi na Maziwa makuu matatu ambayo ni Ziwa Nyasa, Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria. Mungu angeweza kutunyima rasilimali nyingine zote na akatuacha na rasilimali hizi tu na tungeweza kukua kama Taifa kutokana na utajiri unaoweza kuzalishwa na Rasilimali hizi. Hata hivyo Mungu ametujaalia mengine mengi sana kama Madini, Mito yenye kuzalisha Umeme na Watu wapenda amani na wakarimu. Hata hivyo bado hatujaweza kutumia rasilimali hizi kujiendeleza inavyopaswa.

Mheshimiwa Spika, Usafiri wa Reli ni usafiri muhimu sana kwa nchi na hasa kuhusiana na usafiri wa mizigo yenye uzito mkubwa. Hatuwezi kuendelea kamwe kwa kutegemea usafiri wa barabara kusafirisha mizigo yenye uzito mkubwa kama Madini na bidhaa nyingine. Tanzania tuna reli mbili yaani ya TAZARA na ile ya Kati. Wabunge wamezugumza humu Bungeni kwa miaka mitano kuhusiana na adha ya usafiri wa Reli. Kimsingi hatujapata jibu kuhusu Reli ya kati. Wananchi wanaotumia reli kwa usafiri wanapata taabu kubwa. Usafirishaji wa mizigo umeporomoka kwa kiasi kikubwa sana kutoka tani 954 mpaka tani 570 ndani ya mwaka mmoja.

Mheshimiwa Spika, Reli zetu zote zinazosimamiwa na TRL na TAZARA bado zipo katika utaratibu ambao si wa kisasa.  Ukiondoa uwezo mdogo wa kuhimili mizigo yenye uzito mkubwa zaidi, bado upishanaji wa treni unategemea kufika stesheni (single track), Ni muhimu kuwa na treni zinazoweza kupishana bila kufika stesheni kwa kuongeza njia ili angalau ziwe mbili. Lazima pia uwepo mkakati wa makusudi wa kuzifanya reli zote ziwe katika mfumo wa kutumia umeme (electrified railway system) ili kuongeza ufanisi wa usafiri wa reli kwa kuongeza sana kasi, usalama na hata raha (comfortability) ndani ya mabehewa ya abiria.

Mheshimiwa Spika, Kukosekana kwa mfumo wa reli za umeme kumezuia ujio wa wawekezaji walio makini zaidi kwenye sekta ya reli.  Mifumo ya kizamani mno ya reli haivutii kuwekeza kwa faida na ni lazima kuachana nayo haraka. Treni zetu karibu zote zinatumia mifumo ya kizamani ya mawasiliano na ukiondoa simu za mikononi za abiria, wahudumu na madereva wa treni hizo, si rahisi kuona treni yenye mawasiliano bora ya redio au teknolojia.

Mheshimiwa Spika, kama ilivyo viwanja vya ndege kwa usafiri wa anga, Stesheni za Reli zina umuhimu mkubwa sana kwa usafiri wa Reli. Kwa muda mrefu sana Stesheni za Reli zimekuwa ndio maofisi ya Shirika la Reli na pia zimekuwa zinamilikiwa kwa pamoja na Reli. Stesheni za Reli, hasa zile stesheni kubwa kama vile Tabora, Kigoma, Urambo, Mpanda, Kilosa, Dodoma, Morogoro, Tanga, Mwanza na Dar es Salaam zimekuwa hazitumiki kwa asilimia 100 na kwa kweli stesheni nyingine zimekuwa chafu na hazihudumiwi ipasavyo. Nilizungumza suala hili katika hotuba zangu zote mbili zilizopita. Wizara imeweka mkakati gani wa kutumia Stesheni hizi kama vituo vya biashara na mahoteli?

Mheshimiwa Spika, nafasi ya Tanzania kijiografia inatoa fursa kubwa kwa usafiri wa anga kuwa na manufaa kwa Taifa. Hivi sasa Taifa letu lina viwanja vya ndege viwili vya kimataifa yaani Julius Nyerere International Airport na Kilimanjaro International Airport. Kiwanja cha Songwe kinamaliziwa kujengwa. Viwanja vya ndege vya Mwanza, Kigoma, Tanga, Mtwara na Mafia ni viwanja muhimu sana kwa ukuaji wa sekta na uchumi kwa ujumla. Juzi alipokuwa Kigoma Rais wa Jamhuri ya Muungano alisema hadharani na mbele ya wananchi wa Manispaa ya Kigoma kuwa Kiwanja cha ndege cha Kigoma kinajengwa kama kiwanja cha Kimataifa ili kuhudumia nchi za Kongo – Kinshasa na Burundi katika eneo la Maziwa Makuu. Natumaini kuwa watendaji wa Wizara watakumbuka kauli hii ya Rais katika mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma.

Mheshimiwa Spika, TCAA waliweka ushindani katika viwanja vyote vya ndege isipokuwa KIA katika suala la ‘ground handling’ ambapo ni Kampuni moja tu ya Swissport inaruhusiwa kutoa huduma. Kwa sababu ya ukiritimba ni rahisi kwa kampuni hii kukataa kutoa huduma kwa makampuni mengine yenye wateja na hata kufanya huduma hizo kuwa ghali sana. Wizara iseme ni lini itaondoa ukiritimba huu ili kuongeza ufanisi katika huduma za usafiri wa anga.

Mheshimiwa Spika, kuna hili suala la hanga pale KIA ambalo linaweza kutumika kwa ajili ya ‘hub’ ya ndege binafsi katika eneo hili la Afrika Mashariki kwa ajili ya kuweka mafuta au kwa ajili ya kuhifadhi ndege kipindi ambacho wenyewe wapo katika mapumziko. Mamlaka ya Viwanja vya ndege TAA imekodisha hanga hili kwa kampuni binafsi. Hata hivyo kampuni hii haiwezi kupeleka ndege katika eneo hili na hivyo kupunguza matumizi ambayo yangeweza kuingiza mapato zaidi kwa nchi. Wizara iondoe vikwazo hivi ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inafaidika na uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa Hanga hii.

Mheshimiwa Spika, Kampuni yetu ya Umma ya Air Tanzania (ATCL) ambayo ilianzishwa baada ya kuvunjwa kwa mkataba na Kampuni ya South Africa Airways iliendelea kusuasua katika mwaka uliopita. ATCL ilisafirisha abiria wapatao 60,018 tu mwaka 2009 ikilinganishwa na abiria 207,305 mwaka 2008. Abiria waliosafirishwa na Kampuni binafsi ya Precision Air mwaka 2009 walikuwa 583,000 ambao ni zaidi ya nusu ya abiria wote waliosafirishwa nchini mwaka husika. ATCL haikuweza kufikia hata idadi ya abiria waliosafirshwa na Kampuni ya Coastal Travel 9141,995). Ni mategemeo ya Watanzania kuiona ATCL kama fahari ya Taifa (The National Pride). Hata hivyo hali ya ATCL inatia simanzi sana kwa sisi wapenzi wa sekta ya umma katika maeneo nyeti kama usafiri wa anga.

Mheshimiwa Spika, shirika letu la ndege limekuwa katika wakati mgumu sana kwa kipindi kirefu kutokana na ukata na ukosefu wa fedha kutokana na hali ngumu ya kiuchumi ambayo inalikumba shirika hilo , na hii inatokana na serikali kutenga kiasi kidogo sana cha fedha ili liweze kujiendesha. kitendo cha ATCL kusafirisha nusu ya abiria waliosafirishwa na kampuni moja binafsi kama Coastal Travel na moja ya Ishirini ya abiria waliosafiri kwa ndege nchi nzima ni aibu kwa shirika letu la ndege kwani kama abiria wanaongezeka ilitegemewa kuwa ni shirika letu la ndege lingeweza kujiongezea faida na mapato zaidi kutokana na ongezeko hili la wateja, ila badala yake shirika letu limekuwa na wakati mgumu zaidi kifedha. Waziri wa Miundombinu aliunda kikosi kazi cha kutazama jinsi ya kuokoa ATCL na taarifa yake tayari imekabidhiwa kwa Waziri. Hata hivyo taarifa hii imefanywa siri kubwa na utawala bora unataka taarifa hii kutolewa kwa umma ili kuweza kujua hali ya Shirika lao la umma. Kambi ya Upinzani Bungeni inatamtaka Waziri wa Miundombinu kutoa taarifa hii hapa Bungeni ili wawakilishi wa wananchi waweze kujua.

Mheshimiwa Spika, kwa ,mujibu wa Taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji wa mitaji ya Umma ya Juni 2009, Shirika la Ndege ATCL linadaiwa na kampuni ya Celtic Capital ya Miami USA kiasi cha shilingi 1.1bn kutokana na mkopo ambao haujulikani ulikuwa wa kiasi gani uliochukuliwa 15/12/2006 ili kukodisha ndege 2 Boeing 737-200. Dhamana ya serikali imekwisha na deni halijalipwa . Shirika  la ATCL pia linadaiwa na Wallis Trading Company ya Liberia USD 60,000,000 kwa kukodisha Air bus A320. Deni kwa mpaka sasa limefikia Tshs 13.3bn. Ndege hii ya Airbus ilipelekwa nchini Ufaransa kwa matengenezo na mpaka sasa haijarudi. Wakati serikali inalipa gharama za matengenezo kwa ndege hii, vile vile inatakiwa kulipa gharama za kukodisha ndege hii. Shirika limekufa na madeni yanazidi kuongezeka siku hadi siku. Naitaka Wizara ieleze kwa kina kuhusu madeni haya ya Shirika la ATCL na ni namna gani yatalipwa? Waziri wa miundombinu aeleze pia kwa nini ndege hii ya Airbus haijarudi nchini baada ya matengenezo, gharama za matenegenezo zilikuwa kiasi gani na Serikali imelipa au inadaiwa kiasi gani?

Mheshimiwa Spika, tafiti za masuala ya utalii zinaonesha kuwa kwa nchi zenye Shirika la ndege la kitaifa, asilimia 70 ya mapato yanayotokana na utalii hubakia ndani ya nchi husika ilhali kwa nchi ambazo hazina National Carriers, ni asilimia 30 tu ya mapato yanayotokana na Utalii hubakia katika nchi zao. Ndio maana nchi kama Kenya inapata watalii zaidi na mapato ya Utalii kubakia nchini humo kwa kiwango kikubwa. Hapa nchini kwa kuwa Shirika la Ndege la Taifa limekufa, ni theluthi moja tu ya mapato yanayotokana na Utalii hubakia nchini.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeshindwa kabisa kuona mahusiano haya na ndio maana imeshindwa kupata ufumbuzi kwa miaka 5 iliyopita. Kimsingi Shirika hili Serikali imeliua kwa miaka kumi sasa na kila mwaka linatokea katika ilani ya uchaguzi ya CCM kwamba litaokolewa. Mwaka 2000, ilani ya uchaguzi ya CCM ilisema ATC itabinafsishwa ili kuongeza ufanisi. Ilani ya mwaka 2005 ikasema Serikali italiondoa Shirika katika ubinafsishaji na kuliunda upya. Mwaka 2010, ilani ya CCM itasema Serikali imeamua kulifuta Shirika hili iwapo kauli ya Waziri itazingatiwa kwamba Shirika litafutwa!

Mheshimiwa Spika, ninatoa ushauri kwa Serikali kwamba iwe na mwono tofauti katika suala la Shirika la Ndege la Taifa. Kwa kuwa Utalii unategemea sana usafiri wa ndege na kwamba sekta ya utalii itafaidisha zaidi nchi iwapo kutakuwa na Shirika la Ndege la Umma lenye nguvu.

Mheshimiwa Spika, tunaitaka Serikali ihusishe mashirika ya Umma yenye kuendesha shughuli za uhifadhi katika umiliki wa Shirika la Ndege. Serikali isitoze kodi kwa TANAPA na NCA na badala yake mashirika haya yaruhusiwe kununua hisa za ATCL na kuwekeza mtaji. Sehemu ya mtaji ishikwe na Serikali na itakapofika Shirika kuanza kupata faida wananchi wauziwe sehemu ya hisa za Shirika. Uwekezaji kutoka nje sio mwarobaini wa matatizo yetu yote. Tunaweza kutumia mitaji ya ndani kimkakati ili kuimarisha Shirika la Ndege. Jambo la msingi ni serikali kusafisha vitabu vya Shirika kwa kuchukua madeni yote na kuingiza uwekezaji kutoka mashirika ya umma ya ndani ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Ndege ya TGF aina ya Gulfstream imezungumzwa sana hapa Bungeni. Kama wote tunavyofahamu, ununuzi wa ndege hii ambayo pia inayo hadhi ya kutumiwa na Rais wa Jamhuri, ulizua malalamiko mengi mno, hasa bei yake kubwa sana ikilinganishwa na umaskini mkubwa wa Tanzania, pamoja pia na gharama zake kubwa za kimatunzo na kiuendeshaji. Ni mara chache sana Rais wa Jamhuri yetu ameitumia ndege hiyo kwa safari zake nyingi sana za kimataifa, ukiondoa zile za ndani ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inataka kujua ni nini kinachoendelea kuhusu uwepo mzima wa ndege hiyo na mchanganuo sahihi na wa kina wa faida zake za kiuchumi.  Je, ni faida zipi za kiuchumi nchi yetu imezipata tangu ndege hiyo inunuliwe karibu miaka sita iliyopita.  Ni kwa kiasi gani uwepo wa ndege hiyo umechangia kupungua kwa umaskini wa kupindukia wa wananchi wetu?

BARABARA

Mheshimiwa Spika, Taarifa ya hali ya uchumi inaonyesha kuwa Tanzania ina mtandao wa barabara wenye jumla  km. 85,000 ambapo asilimia 53 zipo katika hali nzuri, asilimia 33 wastani na asilimia 14 katika hali mbaya sana.  Mwaka 2008 KM. 5900 zilikuwa na hali nzuri, 2009 jumla ya KM 7400 ziko katika hali nzuri. Ongezeko hili limetokana na ukarabati wa barabara za zamani na ujenzi wa barabara mpya. Hata hivyo, licha ya juhudi za wakala wa barabara nchini kujenga barabara zaidi, mtandao wa barabara za lami nchini ni KM 5800 tu ambazo ni chini ya asilimia 10 ya mtandao wote wa barabara.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na marumbano yasiyokwisha kati ya wizara ya miundombinu na wakala wa barabara nchini kuhusu muda wa mkurugenzi mkuu. Marumbano hayo yamekuwa yakiendeshwa kupitia vyombo vya habari na masikitiko ni kwamba marumbano hayo hayahusiann na ubora wa barabara zetu. Kwa mfano kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya wakandarasi kuchelewa kulipwa hali inayopelekea gharama za ujenzi kuongezeka kutokana na riba au hata wakandarasi kuchelewa kuanza kazi.

Mheshimiwa Spika, taarifa ya mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu ukaguzi wa barabara (value for money audit 2009), inaonyesha kwamba zaidi ya shs. 36 billioni zimelipwa kama ziada kwa mkandarasi kutokana na hali niliyoieleza hapo juu. Kumekuwa na  kurushiana mpira kati ya hazina, wizara  ya miundombinu  na TANROADS kuhusiana na malipo ya wakandarasi. Lakini ni ukweli kuwa Tanroads hawazalishi fedha bali wao ni watumiaji tu. Wenye fedha ni hazina na wizara, hivyo basi wanaosababisha hasara kwa ucheleweshaji huo ni Serikali na sote ni mashahidi wa amri za viongozi wa Serikali kuhusu kujenga barabara ambazo hazimo katika mpango wa bajeti. Kambi ya Upinzani inamtaka Waziri atoe maelezo ni kwanini malumbano hayo yanaendeleo kati ya wizara na idara zilizo chini ya wizara yake? Na lini wataacha kulumbana na kufanya kazi za wananchi?

Mheshimiwa Spika, la mwisho ni kuhusu mjadala unaoendelea sasa  wa kupitisha barabara (kama 60km hivi) katikati ya Hifadhi ya Serengeti. Kumekuwa na majadiliano makali kuhusu suala hili, ambayo wakati mwingine yamezaa hali ya uzalendo na pia uzalendo upofu (blind nationalism). Napenda kunukuu maneno ya Mwalimu Nyerere kuhusu uhifadhi kama alivyoyatamka katika Arusha Manifesto mnamo Septemba mwaka 1961 “….In accepting the trusteeship of our wildlife we solemnly declare that we will do everthing in  our power  to make sure that our children’s  grandchildren will be  able to enjoy this rich and  precious hertage”. Maneno haya ya Mwalimu imekuwa ni dira ya wahifadhi wote nchini na suala la Barabara ya kupita hifadhi ya Serengeti lipimwe kutokana lengo hili la kutunza uhifadhi. Suala muhimu la kujiuliza wakati tunafikia kujenga ama kutokujenga barabara hii na hata kuweza kuhatarisha uhifadhi ni je, kama nchi tutafaidika au hatutafaidika?, na je, kuna mbadala au hakuna mbadala wa barabara hii? Tusikimbilie kupeleka lawama kwa wenzetu wa nchi jirani kwamba wanatupiga vita. Au kusema ni chaguo kati ya maendeleo ya mwananchi au wanyama, bali tuamue tukijua tunawajibu wa kiulimwengu wa kutunza utajiri uliopo Serengeti.

HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, napenda kurejea hitimisho langu la mwezi Julai mwaka 2007. Kambi ya upinzani inatekeleza wajibu wake wa kidemokrasia wa kutoa maoni na hojaji ili Kambi ya chama kinachotawala ifanyie kazi kwa maslahi ya Taifa. Ninawatahadharisha wenzetu kuwa hali ya kisiasa ya nchi imebadilika sana na kwa kasi. Iwapo walio na serikali watashindwa kutekeleza mabadiliko muhimu ya kisera ili kuendena na upepo wa mabadiliko ya kiuchumi wananchi watawapumzisha. Sisi tunasubiri tupewe ridhaa na wananchi ili tutekeleze mipango hii ambayo wenzetu mmeshindwa kutekeleza. Mawazo mbadala tunayo, nguvu ya kutekeleza mawazo haya tunayo, nia tunayao na tunaweza!

Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa nafasi hii uliyonipa na naomba kuwasilisha.

…………………………………….

Kabwe Zuberi Zitto (Mb)

MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI-

WIZARA YA MIUNDOMBINU

29Juni, 2010

Written by zittokabwe

June 30, 2010 at 1:38 PM

Mchango wa Zitto Kabwe katika Bajeti ya Serikali 2010/2011

with one comment

Dodoma, 11/6/2010.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotuba hii ya Bajeti, hotuba ya mwisho ya bajeti kwa Serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi katika kipindi chake cha miaka 5 toka wameingia madarakani.  Toka Serikali hii imeingia madarakani kwa miaka 4 iliyopita Bunge limeidhinisha zaidi ya shilingi trilioni 26 kama bajeti, [2006/2007 Tshs 4tr, 2007/2008 Tshs 6tr, 2008/2009 Tshs 7tr na 2009/2010 Tshs 9tr] toka mwaka 2006/2007 mpaka mwaka 2009/2010.  Leo na mpaka Jumatatu tunajadili na kwa wingi wa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi humu kwa vyotevyote vile watatoa hundi nyingine ya shilingi trilioni 11.  Kwa hiyo jumla katika miaka 5 tutakuwa tumewapa [serikali] jumla ya shilingi trilioni 37 kwa ajili ya kuweza kuleta maendeleo katika Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini katika kipindi cha miaka 4 iliyopita jumla ya Watanzania milioni 1.9 wamekuwa maskini zaidi na kuongeza idadi ya watu maskini mpaka kufikia watu milioni 13. Kwa hiyo tunapojadili bajeti hii tunazungumza bajeti ambayo tuna Watanzania zaidi ya milioni 13 ambao wanaishi chini ya Dola moja kwa siku na bajeti hii haijibu matarajio yao.  Bajeti hii haielezi ni jinsi gani Watanzania hawa wataweza kushiriki katika uchumi na kukua na kuondoka katika wimbi la umaskini.

Bajeti hii ni the longest suicide letter ambayo Chama cha Mapinduzi imejiandikia mbele ya wananchi.  Kwa sababu ni bajeti ambayo inatoa faida zaidi kwa watu ambao tayari wana uwezo [rich people] na haielezi jinsi ya kuondoa changamoto kwa watu ambao ni maskini [impoverished people] zaidi ya milioni 13.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa aliyetoka kuzungumza hivi sasa [mheshimiwa Mzindakaya] alizungumza kuhusiana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi.

Mwaka 2005 Chama cha Mapinduzi kiliwaahidi Watanzania kwamba watahakikisha kwenye ilani yao sekta ya kilimo inakua kwa asilimia 20 [!].  Kwa mujibu wa MKUKUTA wa kwanza ambao tunaumaliza sasa ilitakiwa sekta ya kilimo ikue kwa asilimia kati ya 8 mpaka 10 ili kuweza kuwaondoa nusu ya Watanzania kwenye umaskini [wa kutupwa].

Kwa masikitiko makubwa kwa taarifa ya hali ya uchumi ambayo Waziri wa Fedha ameisoma jana sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 3.2 tu mwaka 2009 [ukiweka na wastani wa ukuaji wa idadi ya watu pamoja na madhara ya mfumuko wa bei ukuaji huu ni hasi (negative growth)].

Katika kipindi cha miaka 5 toka Serikali ya awamu ya 4 iingie madarakani sekta ya kilimo imekua kwa wastani wa asilimia 4 peke yake.  Mmeshindwa hata kufikia nusu ya malengo yenu ya ilani ya Chama cha Mapinduzi.  Mmeshindwa hata kufikia nusu ya ahadi kwa mujibu wa MKUKUTA.  Hii ni aibu kubwa sana na tumewapa jumla ya shilingi trilioni 26 kwa miaka 4 iliyopita na mmeshidwa kukuza kilimo angalau kufikia nusu ya mambo ambayo nyinyi mlikuwa mmeyatarajia.

Faida kama za Dodoma University, nilikuwa naomba nitoe challenge.  Kwa Mbunge yoyote wa Chama cha Mapinduzi asimame na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi aonyeshe ni wapi Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi imesema itajenga Chuo Kikuu Dodoma?

Yeyote miongoni mwenu asimame nam-challenge, hakuna.  Mtu yeyote asimame na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi aseme Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi iliahidi University of Dodoma, hakuna. Kwa hiyo hamuwezi kufaidika na kutaka kujisifu kwa vitu ambavyo wala hamkuwaambia wananchi. UDOM wazo la ujenzi na kugeuza Dodoma kuwa University City ni wazo ambalo lilitolewa na CHADEMA toka mwaka 1992.  Huo ndio ukweli.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri wa Fedha ametusomea bajeti ya mapato ya ndani kuongezeka kwa zaidi ya shilingi trilioni moja  (Domestic Revenue).  Tofauti kati ya Recurrent Budget [Bajeti ya kawaida] peke yake kwa mujibu wa takwimu ambazo amezisoma Waziri wa Fedha zinaonyesha kwamba asilimia 23 ya Recurrent Budget ita-financi-wa [itagharamiwa] kutokana na mikopo na misaada kutoka nje.  Recurrent yaani Mishahara, Mafuta jumla ya shilingi trilioni 1.8 ni a black hole kwenye Recurrent Budget.

Huko nyuma tulifikia wakati ambapo (Domestic Revenue) au fedha za ndani ziliweza kuendesha matumizi ya kawaida.  Sasa hivi tunakwenda katika hali ambayo fedha za ndani hazitoshi kuendesha matumizi ya kawaida.  Hii ni hali mbaya sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, yaani katika kila shilingi 100 tunaitumia katika matumizi ya kawaida shilingi 23 inabidi twende tukakope, tunakopa kulipa mishahara, tunakopa kulipa posho, tunakopa kununua mafuta ya magari yetu, hii ni nchi ya namna gani?

Kama alivyosema Waziri Kivuli wa Fedha na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Fedha na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni [Hamad Rashid Mohammed] bajeti hii ni moja ya bajeti mbaya kuliko zote katika historia ya nchi yetu.  Kwa sababu ni bajeti ya kuchumia tumbo, ni bajeti ya chote tunachokikusanya tunakila hatuendelei na bado tunabakia na gap ya kwenda kutafuta na kwenda kukopa na misaada kwa ajili ya kula na sio kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa sababu asilimia 65 ya bajeti ya maendeleo bado inategemea wafadhili na ukichukua recurrent na development budget asilimia 44 ya bajeti yetu na sio 33 kama Waziri alivyosema bajeti bado tunategemea wafadhili.

[Bajeti ya matumizi ya kawaida ina nakisi ya Tshs 1.8tr ambayo itazibwa na misaada ya wafadhili na mikopo kutoka ndani na nje. Inasemekana mwaka huu Serikali itafanya Deficit Financing (PRINTING MONEY!!!) ya thamani ya takribani 350bn. Katika Bajeti ya Maendeleo kuna nakisi ya Tsh 2.4tr ambayo ni sawa na asilimia 65 ya Bajeti ya Maendeleo na itazibwa na misaada na mikopo kutoka ndani na nje ya nchi].

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima Serikali ikubali sio sifa kuwa na bajeti kubwa sana.  Kwa sababu bajeti hii inapelekea kwa mfano kodi ambazo zitaongezeka kwa ajili ya kuziba kuongeza mwanya wa makusanyo shilingi bilioni 300 zinatoka Large Tax Payers Department. [ Kodi mpya zinazopendekezwa kukusanywa za jumla ya shilingi 1tr, 300bn zitatoka kwa walipa kodi wakubwa, 300bn kodi za biashara ya kimtaifa ie trade taxes na 110bn kutokana na PAYE. Shilingi 300bn nyingine zitatoka ‘non-tax revenue ambapo 153bn ni mrahaba wa Madini]. Kwa Shilingi biloni 300 zitakazotoka trade taxes na hali ya uchumi sio nzuri kiasi hicho [itabidi tutegemee importation].  Maana yake ni kwamba tunategemea watu wa import zaidi ili tuweze kukusanya zaidi.  Ni hali ambayo sio nzuri ni hali ambayo inaweza kuleta matatizo zaidi katika uchumi wa Taifa letu. [kwa kodi kutoka walipaji wakubwa na PAYE makadirio yanaweza yasifikiwe maana zitategmea mazingira ya biashara na hasa ukizingatia kuwa Serikali itaenda kukopa katika mabenki na crowding out effect itakosesha private sector mikopo na hata kupunguza uzalishaji na kupunguza ajira].

[mapendekezo ya kutatua changamoto hizi ni pamoja na kupunguza matumizi ya kawaida kwa kiasi kikubwa ikiwemo kupunguza sana posho zikiwemo posho kwa Wabunge na viongozi wa Serikali na matumizi makubwa ya mafuta ya magari (fuel bill). Pili, badala ya kukopa katika Benki za Biashara Serikali itoe Infrastructure Bond kwa ajili ya kupata fedha za kutengeneza mfumo wa usafirishaji umeme, kuimarisha gridi ya Taifa na kujenga Gridi mpya ya Kaskazini Magharibi. Tatu, Uzalishaji wa Umeme (power generation) ufanywe na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kama ambavyo wameelekezwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma. Nne, Serikali iuze 25% ya hisa zake katika Kampuni ya simu ya Zain Tanzania kupitia IPO. Uuzwaji wa sehemu ya hisa za serikali katika Benki ya NBC bado haupo wazi kwani mapato ambayo serikali inasema itapata ni kidogo mno kulingana thamani ya Benki hiyo (serikali ina hisa 30% na wanasema watapata Tshs 30bn. Serikali ikiuza asilimia 20 ya hisa NBC kwa njia ya IPO itapata zaidi ya Tshs 100bn). Tano, EuroBond ilete mapato yatakayotumika kujenga Barabara na Reli peke yake ili kupata manufaa ya mkopo huu ambao utakuwa ghali sana].

Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri wa Fedha amezungumza kuhusu kuuzwa kwa hisa za NBC na Serikali kupata zaidi ya shilingi bilioni 30.  Lakini nimeangalia kitabu namba moja Revenue Book hiyo source of revenue haimo.  Kwa hiyo nilikuwa naomba Waziri wa Fedha aweze kutoa ufafanuzi ? [Kila shilingi inayotarajiwa kukusanywa na Serikali ni lazima ionyeshwe katika Kitabu Na 1 cha Mapato ya Serikali. Tshs 30bn zimetajwa katika Hotuba ya Bajeti lakini haimo katika kitabu hicho…..!!!!].

Mheshimiwa Naibu Spika, la tatu na la mwisho kwa sababu ya muda.  Waziri wa Fedha jana alizungumza kurejesha misamaha ya kodi ya mafuta kwa Kampuni za Madini.  Madhara ya uamuzi ambao umeufanya ambao ni kwamba tunarudi nyuma, ile goodwill ambayo tumeitengeneza kwenye Sheria Mpya ya Madini tunaiua.  Naelewa kwamba  Serikali inaogopa kushtakiwa kwa sababu watu wamesaini zile MDA[mineral development agreements]. Lakini kuna namna za kuhakikisha kwamba sekta ya madini inafungamanishwa na sekta nyingine za uchumi.

Ukiruhusu Makampuni ya Madini yaagize mafuta kuzalisha umeme wao bila kulipa kodi maana yake ni kwamba hawatanunua umeme kutoka TANESCO. Sasa hivi kuna kazi ambayo imefanyika tayari Wizara ya Nishati na Madini.  Migodi yote isipokuwa mmoja sasa unaweza kupata umeme kutoka TANESCO. Lakini kwa kuwaruhusu kuagiza mafuta ya kuzalisha umeme wao wenyewe tunaingia kwenye tatizo la fungamanisho kati ya sekta ya madini na sekta ya umeme. [Migodi hutumia takribani asilimia 13 ya gharama zake za uzalishaji katika Umeme]

[Vile vile, Kwa kuwa msamaha huu hautahusisha wakandarasi wa ndani wanaofanya biashara na Kampuni za Madini (local contractors), hivyo hapatakuwa na vivutio kwa kampuni za madini kutumia wakandarasi wa ndani. Kampuni za madini zitaona ni rahisi zaidi (less costly)  kufanya shughuli ya kuchimba wenyewe (owner mining). Hii inaua (kills) dhana ya fungamanisho kati ya sekta ya madini na sekta ya ujenzi (construction sector) ambayo ilikuwa ni dhumuni mojawapo la Sheria mpya ya madini ili kujibu changamoto ya fungamanisho dogo la sekta ya Madini na sekta nyingine za Uchumi (low integration of the mining sector to other sectors of the economy). Katika muundo wa gharama za uzalishaji kwa Kampuni za madini, takribani asilimia 30 ni gharama za kuchimba].

[Napendekeza kama ifuatavyo]

Kuhusu Umeme; Sheria ya fedha iseme wazi kuwa mara baada ya migodi yote kupata Umeme kutoka TANESCO, msamaha wa mafuta utakwisha.

Kuhusu Makandarasi wa ndani;

Ama   (a)      Msamaha huu uendelezwe mpaka kwa kampuni za ujenzi katika migodi (local contractors [worst case scenario].

Au      (b) Katika Finance Bill, kuanzishwe (introduce) 15% withholding tax on technical services kwa kampuni za madini zitakazofanya “owner mining” (second best case scenario).

Kwa kuwa local contractors wamatozwa 5% withholding tax on technical services, itakuwa ni rahisi (cheap) kwa kampuni za madini kutoa zabuni (tender) kwa kampuni za ndani. Hata hivyo pendekezo hili litaathiriwa na MDAs zilizopo.

Kwa hiyo kuna haja ya kuwa na measures maalum ya ku-mitigate huo uamuzi ambao Serikali imeufanya [kurejesha msamaha wa kodi ya mafuta kwa kampuni za madini] na kwa vyovyote vile si uamuzi sahihi na uamuzi ambao haukufikiriwa vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, siungi Bajeti mkono.

Written by zittokabwe

June 12, 2010 at 5:47 PM