Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Archive for the ‘MASWALI NA MAJIBU’ Category

Swali la Tarehe Aprili 5,2011 na Mwongozo wa Spika

leave a comment »

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, wakati Serikali imeleta hoja ya kuwa na stimulus package yenye thamani ya trilioni moja na milioni mia saba, aliYekuwa Waziri Kivuli wa Fedha ndani ya BuNge hili aliitaka Serikali imtake Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali akague jinsi gani ambavyo matumizi ya fedha hizo yalifanywa. Je, Serikali tayari ina taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusiana na fedha za stimulus package?

WAZIRI WA NCHI,OFISI YA WAZIRI MKUU – UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI:

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kabwe Zitto kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kawaida kwa fedha zozote za Serikali zinapotumika kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kuzifuatilia na kuzikagua na kwa vile Waziri Kivuli ndiye aliyetaka hivyo basi Serikali itakuwa imefanya na zaidi ya hivyo sisi wenyewe Ofisi ya Waziri Mkuu na Serikali kwa ujumla tunafuatilia matumizi ya fedha hizo ili zilete manufaa yaliyokuwa yamekusudiwa na kwa vyovyote vile bila shaka wengi mtakuwa mmeona jinsi stimulus package ilivyosaidia wakulima waliokusudiwa wa pamba na wale ambao walikuwa kwenye eneo la kahawa. Kwa hiyo, Serikali inajua hivyo.

************************************

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. KABWE Z. ZITTO:

Mheshimiwa Spika, mwongozo kwa mujibu wa Kanuni ya 68(7).  Kufuatia maelezo ya awali ambayo umeyatoa kwamba Muswada umesomwa kwa mara ya kwanza na tutausoma kwa hatua zake zote tatu ndani ya Bunge hili.  Ni kweli kabisa kwamba Muswada huu unaweka mchakato kwa ajili ya kuja kufikia kuandika Katiba. Lakini ni ukweli uliodhahiri kwamba mchakato usipokuwa unajenga muafaka wa Kitaifa kwa vyovyote vile Katiba haitakuwa inajenga muafaka wa Kitaifa.

Waheshimiwa Wabunge ndio kwanza wamepata Muswada na unataka tuupitishe kwenye Mkutano huu. Wabunge hatujaenda majimboni kwetu kupata opinion ya wapiga kura wetu wa namna gani ambavyo Muswada huu utajadiliwa.

Mheshimiwa Spika, huoni kwamba ni busara kuishauri Serikali to extend debate ya Muswada huu na hati ya dharura Mheshimiwa Rais aombwe aiondoe ili Wabunge tupate fursa ya kwenda majimboni kushauriana na wananchi wetu ili baadae tuje kuandika Muswada ambao una consensus ya Kitaifa?

Mheshimiwa Spika, naomba mwongozo wako?

SPIKA: Mwongozo wangu ni kwamba Mheshimiwa Kabwe Zitto ni Mjumbe wa Kamati ya Uongozi.  Kama kuna mtu aliyeanzisha kwamba huu Muswada uje kwa certificate of urgency ni Mheshimiwa Zitto. Sababu zilizotolewa ilikuwa kwamba tusipoanza mchakato huu tukifika wakati wa Bajeti fedha hazijaandaliwa kwa mujibu wa utaratibu wetu wa kubajeti hapa tutashindwa kuendesha mazungumzo haya anayoyasema Mheshimiwa Zitto kwamba kwa ada ya Muswada huu ndio mtakwenda Wabunge vijijini mpaka wapi na mtakaa na watu wenu na mtazungumza.  Hii ni hatua ya kufungua mlango. 

Sasa naona contradiction basi tunaendelea hoja za Serikali.

Mwongozo wa Spika, sasa unatosha. Mheshimiwa Msigwa huwezi kupewa nafasi kwa sababu umeshapewa nafasi ya kutoa mwongozo na huwezi kuzungumzia miongozo kumi kwa wakati mmoja.  Eeh Mheshimiwa.

 

Written by zittokabwe

April 6, 2011 at 4:19 PM