Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Vitabu 53 nilivyosoma mwaka 2016

with 7 comments

Vitabu 53 nilivyosoma mwaka 2016

Zitto Kabwe

The Strongman: Vladimir Putin and struggle for Russia – Augus Roxburgh

The Strongman: Vladimir Putin and struggle for Russia – Augus Roxburgh

Mwaka 2016 nimesoma vitabu 53. Nimeongeza vitabu nilivyosoma tofauti na mwaka 2015 lakini sikuweza kufikia idadi ya mwaka 2014 ambapo nilisoma vitabu 56. Hiyo ndio rekodi ya juu zaidi tangu nilipoanza kuorodhesha vitabu nilivyosoma mnamo mwaka 2012. Mwaka 2013 niliorodhesha vitabu vichache zaidi nilivyosoma.

Mafanikio makubwa ya mwaka huu ni kuongeza vitabu vya Riwaya (fiction), ingawa mtaona mwandishi mmoja, Jeffrey Archer amejitokeza sana kuliko wengine. Hiyo ni kutokana na kusoma kazi yake moja nzuri na yenye mafunzo mengi sana kwa wanasiasa iitwayo First Among Equals. Kazi hiyo ilinifungua macho na kuanza kusoma Clifton Chronicles (vitabu 7) na kufuatia mapendekezo ya wanaonifuata kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram niliweza kupata vitabu vingine vya mwandishi huyu. Kwangu mimi Bwana Jeffrey Archer ni Mwandishi wa Riwaya Bora wa Mwaka 2016.

Licha kutaka kuanza na Gavana Ben Bernanke, nilijikuta naanza na vitabu kuhusu Russia na Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin. Msukumo huo ulitokana na namna nilivyomsoma Mtawala mpya wa Tanzania Rais John Magufuli kulinganisha na Kiongozi wa zamani wa nchi yetu Rais Jakaya Kikwete. Kitabu nilichoanza nacho mwaka 2016 ni The Strongman: Vladimir Putin and the Struggle for Russia kilichoandikwa na Angus Roxburgh. Baada ya kusoma kitabu hiki nilijikuta ninanunua vitabu vingi kuhusu Urusi, Putin, Udikteta, Demokrasia na Maendeleo ili kuweza kuelewa mwelekeo wa Siasa za Tanzania za sasa. Vitabu hivyo vimenisaidia sana kujua namna ya kutafsiri watawala wapya kiasi cha kuunda neno Dikteta Mamboleo (neo-dictatorship) na kuipa tafsiri yake mnamo tarehe 29 Septemba 2016; kwamba Dikteta Mamboleo ni mtawala ambaye ana uzalendo usio tiliwa shaka na anahangaika kuleta maendeleo ya nchi yake lakini hataki kuhojiwa kwa namna yeyote ile.

Mwaka 2016 pia ulinifunua kuhusu uwezo mkubwa na umahiri wa wachapishaji wa Vitabu wa ndani. Nilipata fursa adhimu ya kuzungumza na Mzee Walter Bgoya wa Mkuki na Nyota Publishers. Vitabu kadhaa nilivyosoma katika orodha ya mwaka huu vimechapishwa na Mkuki na Nyota. Nilijifunza mengi mapya ya historia ya nchi yetu na Afrika nzima. Juzuu za masimulizi ya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika nilizipata kutoka Mkuki na Nyota na humo nilipata mambo mapya mengi sana. Kisa kimoja kinachonichekesha kila nikumbukapo ni hadithi ya Rais Khama (baba) wa Botswana alivyobeba machungwa kwenye ndege kumletea zawadi Mwalimu Nyerere akimtania kuwa sera zake za Ujamaa zilileta njaa nchini.

Mwaka huu ninawawekea mapema vitabu nilivyosoma tofauti na miaka iliyopita kwa sababu kwa uwezo wake Manani sitaweza kusoma vitabu vingine baada ya leo kwani nitakuwa na majukumu ya malezi. Karibu kwenye orodha ya vitabu vyangu mwaka 2016.

  1. The Strongman: Vladimir Putin and struggle for Russia – Augus Roxburgh
  2. Putin’s Progress – Peter Truscott
  3. The Putin Mystique: Inside Russia’s Power Cult – Anna Arutunyan
  4. The Invention of Russia: The Journey from Gorbachev’s Freedom to Putin’s War – Arkady Ostrovsky
  5. I am going to Ruin Their Lives: Inside Putin’s War on Russian Opposition – Marc Bennet
  6. Red Notice: How I became Putin’s no 1 enemy: Bill Browell
  7. Ruling Russia: Authoritarianism from the Revolution to Putin – William Zimmerman
  8. Dictator’s Learning Curve: Inside the global debate for Democracy – William Dobson
  9. Dictator’s Handbook: Why bad behavior is almost good politics – Bruce Buener de Mesquita and Alastair Smith
  10. Dictator – Tom Cain
  11. The Warlord- James Steel
  12. Tanzania: A Political Economy ( 2nd Ed ) – Andrew Coulson
  13. Thieves of the State: Why corruption threatens global security – Sarah Chayes
  14. How to Run A Country – Marcus Tullius Cicero
  15. The End of Karma: Hope and fury among India’s young – Somini Sengupta
  16. The Hidden Wealth of Nations: The scourge of tax havens – Gabriel Zucman
  17. Mystery of Capital – Hernando De Soto
  18. So long a letter – Mariama Ba ( Special thanks to January Makamba for recommending this to Bunge Readers’ Club )
  19. The Fifth Mountain – Paulo Coelho
  20. First Among Equals – J. Archer
  21. Kane and Abel – J. Archer
  22. Best Kept Secret – J. Archer
  23. The Sins of the Father – J. Archer
  24. Only Time Will Tell – J. Archer
  25. Shall we Tell the President – J. Archer
  26. Mightier Than The Sword – J. Archer
  27. The Fourth Estate – J. Archer
  28. Honour Among Thieves – J. Archer
  29. Cometh The Hour – J. Archer
  30. This was a Man – J. Archer
  31. The New Collected Short Stories – J. Archer
  32. Building a Peaceful Nation – Bjerk
  33. Burundi Peace Dialogue- Pierre Buyoya
  34. Burundi: The Biography of a small African Nation – Nigel Weltt
  35. The Thabo Mbeki I know – ed. Sifiso Mxolisi and Miranda Staydom (Special Thanks to Amb. Ami Mpungwe, a contributor to the very book)
  36. Clinton Cash – Peter Schweizer
  37. Connectography: Mapping the Global Network Revolution – Parag Khanna
  38. The Rohingyas: Inside Myanmar’s Hidden Genocide – Azeem Ibrahim
  39. Stringer: A Reporter’s Journey in the Congo – Anjan Sundaram
  40. Uchambuzi wa Sera, Uongozi na Maslahi ya Watanzania – CSL Chachage
  41. Haki, Amani na Maendeleo: Nafasi na Wajibu wa Mahakama Tanzania – S J Bwana
  42. Wanawake wa TANU – Susan Geiger (a special thanks to my wife for bringing this home)
  43. African Socialism or Socialist Africa – A M Babu ( Special Thanks to Dr. Khamis Kigwangalla for suggesting it to Bunge Readers Club and Ezekiel Kamwaga who lent it to me )
  44. The Courage to Act – Ben Bernanke
  45. The Litigators – John Grisham
  46. White Lioness – Henning Mankell
  47. The Dogs of Riga – H. Mankell
  48. Fifth Woman – H. Mankell
  49. Kennedy’s Brain – H. Mankell
  50. Treachorous Paradise – H. Mankell
  51. Harusi ya Dogoli – Athumani Mauya
  52. Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere – Peter Bwimbo
  53. The Hashim Mbita Project: Southern African Liberation Struggles Contemporaneous documents ( 1960 – 1994 Volumes 1, 3, 5, 6 & 7 ) – Ed. A J Temu and J N Tembe

Written by zittokabwe

December 20, 2016 at 6:01 PM

7 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. habar yako mheshimiwa??? tafadhali naomba unitumie hvo vitabu na mimi niweze kuvisoma…hongera sana kwa kusoma vitabu vyote hvo.

    Mseco Kidee

    December 20, 2016 at 6:43 PM

  2. Hivi havipatikani online ndugu Ruyagwa ?

    Burhani Khaled

    December 21, 2016 at 6:02 AM

  3. Vitabu vizuri sana vimenivutia

    Sent from my Samsung Galaxy smartphone.

    amanmwamlima

    December 21, 2016 at 7:44 AM

  4. Pia hongera sana…big up

    Sent from my Samsung Galaxy smartphone.

    amanmwamlima

    December 21, 2016 at 7:44 AM

  5. Hongera sana mheshimiwa.
    nisaidie nami nivipitie tafadhali.

    Ally Malumalu

    January 26, 2017 at 11:46 AM

  6. Hongera Sana broo, natamani niwe karibu nawe kwan utanifunza mengi kwa ustawi wa uongozi wa nchi yetu. Ntakupataje sasa ndg?? Nmejarb kukutafta manually for long time but…

    Tumain S Mabala

    January 27, 2017 at 9:08 PM

  7. nina appreciate sana uzallendo wako mkuu.. mara nyingi umekua ukitanguliza maslahi ya ncchi mbele before mihemko ya uchama..nnakuheshimu sana kwa hilo… Tafadhari endelea na kazi hiyo nzuri.. ntasoma vitabu hivi juu chini on this 2017..ume ni inspire sana..
    ndimi mtanzania wa kwanza.. mzalendo halisi

    mvungi kunjumu sebastian

    April 12, 2017 at 1:07 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: