Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Vitabu 23 nilivyosoma mwaka 2015(The 23 Books I read in 2015) #letsread

with 3 comments

Vitabu 23 nilivyosoma mwaka 2015

Zitto Kabwe

Nimesoma vitabu 23 tu mwaka huu unaoisha leo.

Mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa uchaguzi, nimesoma zaidi kidogo ya nusu ya https://zittokabwe.wordpress.com/2014/12/27/vitabu-nilivyosoma-2014-books-i-have-read-in-2014-booksread2014-letsread/ .

Katika mwaka 2015 niliweza kufanya uchambuzi wa vitabu 4 tu kwani ilipofika mwishoni mwa mwezi Machi, 2015 nilianza kazi mpya kabisa ya kujenga Chama kipya cha Siasa chenye kufuata mrengo wa kushoto – ACT Wazalendo.

Niliweza kuchambua 1. The Establishment, Owen Jones 2. The Alchemist, Paulo Coelho 3. The Last Banana, Shelby Tucker na 4. Act of Treason, Vince Flynn. Natumai nitarejesha safu yangu ya Kitabu na Kalamu ya gazeti la #RaiaTanzania kuanzia Januari, 2016.

Baadhi ya vitabu nilivyosoma mwaka huu ni marudio ya vitabu nilivyosoma zamani ili kujikumbusha mambo Fulani Fulani. Mfano hivi sasa najitahidi sana kusoma vitabu nilivyosoma shule ya sekondari katika ‘literature’ ili kuelewa zaidi na kulinganisha na hali ya sasa. Ndio maana mwaka huu nilirudia kitabu cha A Man of the People cha Chinua Achebe mara tu baada ya uchaguzi. Kiukweli huwa narudia rudia sana vitabu vya Achebe kutafuta ulinganisho wa hali ya siasa ya miaka ya sitini na miaka hii ya sasa. Vile vile najaribu kuelewa suala la #Biafra kutoka katika jicho la mwandishi.

Mwaka huu nimejitahidi sana kusoma ‘fiction’ na nimefurahia sana juhudi hizo japo niliuweka kando ushairi na sikuweza kabisa kumaliza The Capital, Thomas Piketty. Kwa kuwa nimedhamiria kujikita tena kwenye taalumu yangu ya Uchumi na kutumia taaluma hiyo kwenye siasa za Bunge, nitamaliza The Capital In’Sha Allah. Ninataraji kufungua mwaka na The Courage to Act: A Memoir of a crisis and its aftermath, Ben S. Bernanke. Kitabu hiki nililetewa kama zawadi na @Ritaupara, mmoja wa rafiki zangu wanaopenda kusoma vitabu pia. Kitabu changu bora cha mwaka kilikuwa Ujamaa, Ralph Ibbot. Napendekeza kila Mtanzania anayethamini historia ya nchi yetu miaka ya mwanzo ya Uhuru asome kitabu hiki.

Karibu kuona orodha ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2015;

 1. The Alchemist – Paulo Coelho
 2. Deng Xiaoping: The Man who Made Modern China – Michael Dillon
 3. Ujamaa: The hidden story of Tanzania’s socialist villages – Ralph Ibbot
 4. Race, Revolution, and the Struggle for Human Rights in Zanzibar: The Memoirs of Ali Sultan Issa and Seif Sharif Hamad – G. Thomas Burgess
 5. Home and Exile – Chinua Achebe
 6. My Watch – Olesegun Obasanjo
 7. How Much Land Does A Man Need? – Leo Tolstoy
 8. Facing Mount Kenya – Jomo Kenyatta
 9. The Tipping Point – Malcolm Gladwell
 10. Chinua Achebe: Tributes and Reflections – Ed. Nana Ayebia Clarke & James Currey
 11. A Man of The People – Chinua Achebe
 12. Believer: My 40 Years in Politics – David Axelrod
 13. Politics – David Runciman
 14. The Man from Beijing – Henning Mankell
 15. The Establishment – Owen Jones
 16. 50 Years of Development Partnership – The World Bank
 17. Adultery – Paulo Coelho
 18. The Zahir – Paulo Coelho
 19. Growing Up With Tanzania – Karim Hirji
 20. The Governance of China – Xi Jinping
 21. The Last Banana – Shelby Tucker
 22. Act of Treason – Vince Flynn
 23. In the Footsteps of the Prophet – Tariq Ramadhan

 

 

Written by TeamZitto

December 31, 2015 at 5:09 PM

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. CONGRATS MY ROLE MODEL

  IDRISA

  January 1, 2016 at 10:50 AM

 2. 👏👏👏 allah akupe umri mrefu we ndo kilakitu kwa vijana wanaojitambua hongera sana kk

  Mwanahamisi

  January 15, 2016 at 9:28 AM

 3. […] 2016 nimesoma vitabu 53. Nimeongeza vitabu nilivyosoma tofauti na mwaka 2015 lakini sikuweza kufikia idadi ya mwaka 2014 ambapo nilisoma vitabu 56. Hiyo ndio rekodi ya juu […]


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: