Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Hotuba Niliyotaka Kuitoa Bungeni Jana

with 46 comments

Mheshimiwa Spika, nilijiunga na Bunge lako tukufu mwaka 2005 nikiwa kijana mdogo mwenye malengo ya kupaza sauti ya vijana kwenye masuala yanayohusu nchi yetu na pia kutetea maslahi ya wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Mkoa wa Kigoma.

Katika kudumu kwangu kama mbunge nililelewa na kukuzwa na chama cha siasa cha CHADEMA ambacho kupitia chama hiki niliingia Bungeni. Chama hiki kilinilea na kunikuza tangu nikiwa na umri wa miaka 16 na kupitia chama hiki nimejifunza mambo mengi sana. Nimeijua nchi yangu, nimejua siasa na nimejulikana ndani na nje ya nchi. Nitakuwa mwizi wa fadhila nisipotoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa CHADEMA na viongozi ambao nimefanya nao kazi muda wote nikiwa mwanachama na kiongozi.

Mheshimiwa Spika, Chama kilinikuza kama mwanasiasa lakini watu wa Kigoma Kaskazini ndio walionipa kiti hiki ninachokalia kama Mbunge. Juzi nilipokuwa nyumbani nilipata fursa ya kuwashukuru rasmi wananchi kwa imani waliyonipa kuwatumikia kwa vipindi viwili mfululizo. Wengi wenu ndugu zangu wabunge mnafahamu, mihula miwili sio jambo la mchezo, sio lelemama. Mola atawalipa wananchi wa Kigoma kwa imani kubwa walioionyesha kwangu na kuniwezesha kulitumikia Taifa langu kwa namna nilivyolitumikia.

Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii leo kuzungumzia suala la muda mrefu sasa la kutoelewana kati yangu na chama changu na hivyo kuleta msuguano kati ya wananchi walionichagua kuwawakilisha na chama nilichopitia na kupeperusha bendera yake wakati wa uchaguzi mkuu. Licha ya msimamo wangu wa siku zote kwamba wananchi pekee waliomchagua mwakilishi wao ndio wawe na mamlaka ya kumwondoa kwenye uwakilishi mchaguliwa huyo, mfumo wetu wa kikatiba na mfumo wetu wa kisiasa haupo hivyo na umeamua vinginevyo.

Mheshimiwa Spika, kwamba chama cha siasa kinaweza kumvua uanachama mwanachama wake na hivyo kupoteza kiti chake cha uwakilishi wa wananchi wake ni moja ya makosa makubwa ya kikatiba ambayo tumeendelea kuyakumbatia, nimekuwa nikipinga na nitaendelea kupinga udikteta wa vyama dhidi ya utashi wa wananchi.

Mheshimiwa Spika, licha ya upinzani wangu mkali wa vifungu kandamizi vya kikatiba, kama mzalendo ninaiheshimu Katiba yetu na mfumo wetu wa sasa na ninaheshimu uamuzi wa mahakama dhidi ya kesi yangu na sitakata rufaa. Hatua itakayofuata ni uamuzi wa chama changu na baadhi ya viongozi wameshatangaza kwa umma kupitia vyombo vya habari kunivua uanachama ingawa sijapewa taarifa rasmi.

Mheshimiwa Spika, ningeweza kukata rufaa kuhusu maamuzi ya mahakama kwani kuna sababu lukuki ya kushinda rufaa hiyo. Lakini ninadhani nimepigania haki zangu kwa muda mrefu sasa. Nimepigania kupanua wigo wa demokrasia ndani ya chama changu kwa muda mrefu sasa. Lakini ugomvi huu hauna manufaa kwa pande zote husika, kwa hakika unatuumiza wote. Mimi ni mwanademokrasia. Naamini katika siasa za ushindani ndani ya chama na katika mfumo mzima wa siasa kitaifa. Lakini sitakuwa tayari kudhoofisha harakati na kazi kubwa walizofanya wanamageuzi waliotutangulia kwa kuendeleza ugomvi unaotuumiza. Hivyo niko tayari kukubali kukaa pembeni. Ninaamini kuwa mapambano ya kuleta mabadiliko ya kweli na demokrasia katika nchi yetu Tanzania ni makubwa kuliko mimi, kuliko kiongozi yoyote wa Chadema na kuliko wanachama wa Chadema. Mapambano haya ya mabadiliko si kwa ajili ya kizazi hiki tu bali kwa vizazi vijavyo. Ndiyo maana siku zote nimesema Nchi kwanza, vyama baadae. Kuona makundi yanajitokeza ndani ya harakati hizi, na kuwa na uhasama mkubwa uliopindukia, unawakatisha tamaa wananchi wanaotutumaini kuleta siasa iliyo tofauti na siasa za sasa. Muda umefika wa kupiga mstari na kuanza upya. Hivyo nimeamua kuwa nitatii maamuzi ya chama ya kunivua uanachama na kung’atuka ubunge.

Mheshimiwa Spika, naomba niweke wazi kuwa nimefikia uamuzi huu kwa utashi wangu mwenyewe na nimepewa Baraka zote na wananchi wangu na wazee wa Jimbo la Kigoma Kaskazini. Najua Watanzania wengi ambao nimewatumikia kwa moyo wangu wote katika kipindi cha miaka hii 10 wanaweza wasikubaliane na uamuzi huu. Hata hivyo Watanzania wajue kuwa mfumo wetu wa siasa na katiba unatoa nguvu kwa vyama vya siasa kudhibiti wabunge wake. Naamua hivi kwa sababu wenzangu ndani ya chama ambao nimehangaika nao usiku na mchana kujenga chama na kukifisha hapa kilipo hawapo tayari kufanya kazi tena na mimi. Nimesoma na kusikia kauli nyingi zinazoweka wazi kuwa hawanitaki ndani ya chama. Nimejitahidi kwa njia zangu zote kuona kama tunaweza kuendelea kufanya kazi pamoja ya kujenga mfumo madhubuti wa vyama vingi nchini lakini imekuwa ngumu kama mwanachama mwenzao. Ninaheshimu uamuzi wao huo.

Mheshimiwa Spika, kwa miaka kumi hii si yote niliyafanya sahihi, yapo ambayo niliyakosea kama mwanadamu katika kufanya kazi kwangu, kwa namna yeyote ile naomba radhi Watanzania wote kwa yote ambayo sikuyafanya kwa usahihi. Mimi ni binadamu, kiumbe dhaifu, sijakamilika. Ni Mola peke yake amekamilika.

Mheshimiwa Spika, siwezi kuanza maisha yangu mapya bila ya kulishukuru Bunge lako tukufu, Bunge la Tisa chini ya Mzee Samwel Sitta na Bunge la Kumi chini yako Mama Anna Simamba Makinda. Bunge limekuwa ni nyumbani kwangu kwa takribani muongo mmoja. Nimekuzwa, nimejifunza, nimepambana, nimefurahi na nimelia ndani ya Bunge hili. Kwa pamoja tumepigania maslahi ya wananchi wetu na kupingana na kufanya mambo kwa mazoea na hivyo kuleta mabadiliko kadhaa. Ni kipindi hiki ambapo wabunge tumekuwa na sauti, Bunge la Tisa lilijenga ‘Bunge lenye Meno’ katika kupambana na ufisadi. Bunge la Kumi limejenga ‘Bunge lenye nguvu’ katika mfumo wa Bajeti ya nchi yetu. Kupitia Bunge hili tumeweka misingi ya kujenga mfumo madhubuti wa uwajibikaji katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, wakati Bunge la Tisa litakumbukwa kwa hoja ya Buzwagi iliyopelekea nchi yetu kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa uendeshaji wa sekta ya madini (Sera mpya ya Madini na Sheria mpya ya Madini ) na hivyo mapato ya sekta ya madini kuongezeka kutoka Tshs 32 bilioni kwa mwaka mpaka Tshs 450 bilioni kwa mwaka hivi sasa; Bunge la Kumi litakumbukwa kwa hoja maalumu ya Tegeta Escrow iliyopelekea mfumo wetu wa maadili ya Viongozi kupitia Baraza la Maadili kuanza kufanya kazi kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa katika miaka iliyopita. Mimi kuwa sehemu ya mabunge yaliyotekeleza hatua hizo za mabadiliko ni jambo la kujivunia sana.

Mheshimiwa Spika, kwa familia yangu, wajumbe wa PAC, tumekuwa nguzo kubwa ya kujenga uwajibikaji wa Serikali kwa Bunge na wananchi. Napenda kuwashukuru kwa dhati kabisa kwa kuniunga mkono na kwa kunipa ushirikiano kama Mwenyekiti wao. Changamoto na malezi mliyonipa kwa miaka yote hii yamejenga Mtanzania mmoja mwenye dhati ya kuitumikia nchi yake, muda wowote, wakati wowote na kwa namna yeyote ile bila woga wala upendeleo. Nawashukuru kwa kujitoa kwenu kwa nchi yetu na dhamira isiyo na mawaa ya kujenga Taifa imara zaidi.

Nitaendelea kuwatumikia wananchi wa Kigoma Kaskazini na Taifa langu hata kama nimelazimika kuachia nafasi yangu ya ubunge kwa kipindi hiki kilichosalia kwa kusimamia ukweli, kutetea demokrasia ya kweli na kupigania maendeleo ya kweli kwa mwananchi wa kawaida bila ubaguzi wowote.

Mheshimiwa Spika, Kwa CHADEMA, licha ya tofauti zetu ambazo zimekua kiwango cha kutosameheka, najivunia kwa fursa mliyonipa kuwa sehemu ya Baraza hili la Taifa ambalo leo ninalihutubia kwa mara ya mwisho kama mbunge wa Kigoma Kaskazini. Fursa iliyonifanya niweze kuitumikia nchi yangu na mkoa wangu wa Kigoma. Inawezekana tusiweze kuelewana katika masuala ya uongozi, misingi na itikadi, lakini ninaamini tunapaswa kuelewana na kukubaliana katika kubwa ya kuijenga nchi yetu kuwa Taifa linalojitegemea na lisilo na aina yeyote ya ubaguzi. Taifa lenye uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira na kuondoa umasikini, ujinga na maradhi, Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na ni matumaini yangu kuwa tutakuwa bega kwa bega katika harakati hizi katika siku zijazo. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo, nafasi hii ya kihistoria tuliyopewa haihitaji siasa za ubinafsi na unafsi! Uzalendo wetu utapimwa kwa uwezo wetu wa kuweka tofauti zetu binafsi pembeni kwa lengo lililo kubwa zaidi yetu.

Mheshimiwa Spika, Mwisho kwa wananchi wa Jimbo langu, wana Kigoma na raia wote wa Tanzania ambao kwa ridhaa yao nimekaa katika viti hivi kwa miaka takribani kumi, nawahakikishia kuwa dhamira yangu kuwatumikia, nia yangu na sababu za kutoa utumishi wangu kwenu vimekuwa na nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule. Huu ni mwanzo mpya. Ngugi aliandika ‘a grain of wheat’ kwa maana ya kwamba ‘Ili Mbegu iweze kumea lazima ife kwanza’.
Asanteni sana.

Advertisements

Written by TeamZitto

March 20, 2015 at 3:49 PM

Posted in Uncategorized

46 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. I always appreciate you for whatever you do. Tanzanians will remember you for your struggling fighting for their rights. really many people are behind you and don’t regret for what has happened.

  Juma Singitu

  March 20, 2015 at 4:21 PM

 2. Nahisi baba yako ni Hayati Kambarage Nyerere kwani misimamo yako na utashi wako na maamuzi yako hayotafautiani sana na dira na Tanzania ya Mwalimu Nyerere. Natambua mchango wako kisiasa na kiuchumi pia. Hongera sana kwa maneno yaliyojaaa hekima naamini kabisa kuacha ubunge si kuacha uongozi na nnakuona Ikulu ya Tanzania kama raisi wa Tanzania pambana usikate tamaa boti ikizama chukua life jacket subiri meli nyingine panda na endelea na safari Taifa bado linahitaji mchango wako hasa sisi vijana

  Emmanuel Mariki

  March 20, 2015 at 4:31 PM

 3. Hongera kaka, you have to fallbefore you fly but every thing will be alright.

  balthazar faustine

  March 20, 2015 at 4:34 PM

  • pole sana kabwe migongano huwa inaweza kuwa maisha ya kila mtu kutokana na hulka zetu binadamu,ila kwa uamuzi uliouchukua ni mzuri kwani unapo anguka usiangalie ulipoangukia bali unaangalia nini kimekuangusha,kwahivyo ni vizuri ukubali kurudi nyuma na kutafakari vizuri yaliyo kutokea, kwani wanasema kukiri upungufu sio dalili ya kushindwa bali ni ishara ya ya kujiimarisha.

   lepapa lomnyaki

   March 20, 2015 at 11:04 PM

 4. This country shall remember you forever. I personally, have written your name in my Mind & Heart.. Alongside with you, I will be.

  Mimi

  March 20, 2015 at 4:35 PM

 5. Reblogged this on madoler.

  madoler

  March 20, 2015 at 4:43 PM

  • pole sana kabwe migongano huwa inaweza kuwa maisha ya kila mtu kutokana na hulka zetu binadamu,ila kwa uamuzi uliouchukua ni mzuri kwani unapo anguka usiangalie ulipoangukia bali unaangalia nini kimekuangusha,kwahivyo ni vizuri ukubali kurudi nyuma na kutafakari vizuri yaliyo kutokea, kwani wanasema kukiri upungufu sio dalili ya kushindwa bali ni ishara ya ya kujiimarisha.

   lepapa lomnyaki

   March 20, 2015 at 11:02 PM

 6. nice speech binafsi naumia saana kuona kiongozi kab zitto unaachia na wasiokuwa na maana wanabaki..mti wenye matunda ndio upigwao mawe upo pamoja nasi tutaendelea kukuuunga mkono popote utapokuwa…namuomba allah akuongoze kwa kila jema inshallah

  Hassani Mohamedi

  March 20, 2015 at 4:51 PM

 7. Kiukweli tumesikia mengi kwenye vyombo mbalimbali vyq habar ila kwa hotuba hii ZZK ni mwanasiasa uliyekomaa naamini popote utakapoenda utaendelea na utamaduni huu wa uzalendo na upendo kwa taifa na mwisho wa siku tutakuwa na taifa ambalo ni sehemu bora ya kuishi duniani. IPO siku tutapata katiba bora ya nchi ambayo inawapa watanzania mamlaka huu ya viongozi waliowachagua, na wakati huo ukifika Mh. Zitto utakumbukwa. Wewe ni kamanda bado. ALL THE BEST THE HERO.

  Isaac Felix

  March 20, 2015 at 4:55 PM

 8. Mheshimiwa ,Zitto Kabwe.Mimi nimesikitishwa sana na uamuzi wako kutogombea tena ubunge.Ni imani yangu na hofu yangu kuwa tumepoteza mtu mahili katika mabadiliko.Hususani mabadiliko ya kimtazamo katika siasa.Mambo mengi ulihakikisha yanakuwa OPEN kwetu sisi raia wa kawaida na nikweli ilikuwa hivyo.Mchango wako bungeni ulikuwa sio wa manufaa kwa wananchi wa kigoma tu ila hata huku mikoani.
  Mheshimiwa,naamini kukiachia kiti cha ubunge ni mwanzo wa hutua nyingine iliyo bora zaidi.

  EDSON .M.MGOMAPAYO

  March 20, 2015 at 5:01 PM

 9. i have always seen you as open minded. but the problem with Tanzanian politics is the failure to understand and practice what they actually preach in the podium. as for CHADEMA they have always praised democracy but they have not lived to it. thats hypocrisy of the highest order. they always say and life goes on. carry on comrade this is Tanzanian politics. kufa IMAMU siyo mwisho wa IBADA

  emmanuel msina

  March 20, 2015 at 5:04 PM

 10. Sajjo L.M.

  March 20, 2015 at 5:08 PM

 11. Dah..,hutuba yako kaka inamguso wa kila aina,
  kweli nimekubali,
  “mbegu ili ipande,lazima ife..!”

  SUMA MZEE

  March 20, 2015 at 5:12 PM

 12. Hotuba safi sana, ina maono.

  Kichwa chawa

  March 20, 2015 at 5:28 PM

 13. Mh. Mbunge Zitto Zuberi Kabwe,

  Kwanza hongera kwa hotuba yako ndefu ambayo kwa kweli imenipa simanzi.
  kama mwananchi na mtu ambaye wazazi wangu wamekulia Manyovu napenda nikuambie kuwa, harakati zako niliziunga mkono kwa asilimia 100.

  Hakuna aliyeweza kunishawishi hasa pale nilipokuwa ninasimamia hoja katika kutetea hoja zako na pia kusimamia kile ulichosimamia kama mbunge na katika majukwa ulipokuwa ukihutubia.
  Awali ya yote napenda nikupe pole kwa kile kilichokupata katika chama ulichokulia na pia naomba nisikupe pole kwa kuwa ninahakika kuwa unaweza kulitumiakia Taifa kwa namna yoyotew ile na bado tukasonga mbele. Huwa siamini katika malumbano na hoja zisizo na msingi zinazotumika kukuondoa wewe katika chama.
  Lakini ukweli ni kuwa, Jiwe alilokataa muashi linakuwa jiwe la pembeni.
  Leo hii umuhimu wako umefunikwa kwenye ndoo, kesho mteka maji akifunua ndoo utaonekana umuhimu wako.

  wengi wamekukosoa pasipokujua ukweli uliofichwa nyuma ya pazia, lakini mimi ninahakika kuwa ipo siku pazia litafunuka kwa upepo na watu wakijua ukweli itakuwa too late.

  Kwa sasa ninasoma Japan masters in International business Baada ya kutambua kuwa kuna haja ya kufanya makubwa kupitia elimu na hakika ulikuwa kama mwongozo kwangu na nitashirikiana nawe popote katika kazi za maendeleo na kujenga Taifa.
  nahitaji kuendeleza Manyovu na kigoma kwa Ujumla na taifa zima.

  Ninakupa namba yangu hii +818070643924.

  tuwasiliane namna ya kuweka mikakati ya kuendelea kutumikia wananchi kwa kuanzisha miradi mbalimbali na hatimaye tutafika tu.

  sitaweka email yangu hapa nitakupa email yangu baada ya kupata namba yako.

  Leo

  March 20, 2015 at 5:28 PM

 14. hotuba yako kaka daaaah inagusa moyo was mtanzania mzalendo.”ili mbegu iweze kuota lazima ife kwanza”

  Regan mtuka

  March 20, 2015 at 5:37 PM

 15. Ni maisha ya siasa ya mbovu za Tanzania tulizozizoea leo wananchi tumebaki njia panda kwamba hatujui kiongozi yupi akiingia madarakani ataangalia maslahi ya watanzania kwa ujumla
  Pole braza Zitto kwa kazi ngumu japo una nafasi ya kuendelea kutetea haki za watanzania sio lazima uwe bungeni hata uraian unaweza watetea watanzania wenzako kwani bunge la bongo kama uwanja wa vijembe .

  Frank massawe

  March 20, 2015 at 6:43 PM

 16. Brother Zitto, jamii inakuelewa, umekuwa mhanga wa wasaka tonge, uwezo wako wakuchambua mambo nakuyaeleza hauwezi kuzibwa na yeyote, nikuhakikishie kila kijana ambaye anaelewa mambo kwa kuyafuatilia yuko nyuma yako, understand this brother, there is a huge number of youth who are not allied with any of the sides but are all on your back, tafadhari zidisha idadi ya vitabu ulivyosoma mwaka jana uendelee kukomaa, tuko tayari kukupokea nakupanga mikakati bora yakulijenga taifa. Relax and focus beyond politics, you are my hero#YOU WILL NEVER WALK ALONE#

  VICTOR NDAMGOBA

  March 20, 2015 at 7:13 PM

 17. zitto uko vizuri sana ktk siasa,uelewa wako ni mkubwa sana…na nina imani kupitia chama chochote cha siasa unaweza kurudi bungeni bila shaka yoyote…Tafuta chama unachotaka kwa sasa ili uendelee na gurudumu la maendeleo ya taifa kwa ustawi wa jamii ya watanzania.

  karim issa

  March 20, 2015 at 7:22 PM

 18. Hata sisi tulitambua uwepo wako uliokaa bungen miaka kumi sasa kazi uliyoifanya ni kubwa sana zaid ya umri wako umepigana sana juu ya nchi yako hii,naamin wanakigoma wamekuelewa juu ya mahamuz yako na vile vile umekuwa mbunge wa kwanza mwenye mahamuz ya kushangaza nchi nzima toka nilijue bunge,Mi binafs nakuunga mkono tuko pamoja kuilinda nchi yetu.Hongera zitto Mungu akulinde juu ya maandui wako!

  Alphonce rutashobya

  March 20, 2015 at 7:49 PM

 19. hongera kwa hotuba bro kwakweli nimeshindwa kuzuia machozi yangu.tungoje muda utatuambia ukweli(time will tell the thruth)

  yusufu makandilo

  March 20, 2015 at 8:02 PM

 20. You dont strike me like a quitter sir. Something big is in the works, I am sure. GOODLUCK.

  Bertie

  March 20, 2015 at 8:07 PM

 21. Kaka Zitto pigana hao usihangaike mai hawajui maana hawajui maana ha uzalendo hivo. hawakuanzisha chama bali ni kampuni.

  Kobell Sillah

  March 20, 2015 at 8:08 PM

 22. Kila ulichokifanya kwa Taifa hili kimeonekana wazi lakini nimependa sana hekima yako kwamba katika kipindi chote hicho pia yapo ambayo uliyafanya yanaweza kuwa hayakuwa sahihi lakini uliamini katika kusameheana na kuendelea kulitumikia Taifa. Pamoja na hayo kama Kiongozi na ukiwa mdogo wangu pia nadhani ipo haja kuthibitisha ukweli wa unachokipigania kwa vitendo kwa kuendelea na siasa kupitia jukwaa jingine badala ya kutogombea Ubunge kama ulivyotangaza jimboni kwako. Nakumbuka Mtanzania gazeti la Kiswahili la kila siku liliwahi kuandika katika ukurasa wake wa mbele mara baada ya maamuzi ya Msajili kwamba “MSAJILI AWARUDISHIA AKINA ZITO ACT YAO”. Endeleza mapambano ya kupatikana kwa demokrasia ya kweli ndani ya vyama vya siasa na Tiafa kwa ujumla kupitia jukwaa jingine la ACT. Nakubaliana na harakati zako na nakuunga mkono lakini wakati wote kumbuka kuepuka malumbano hasa kupitia vyombo vya habari kwani wao wanaandika kwa interest zao na kwa bahati mbaya wengine wameweka kando kabisa maadili ya Uandshi wa Habari na wamekuwa “money hunters”. Kila la kheri ndani ya chama kipya ACT habari ya mjini.

  Ipyana Mwakamela

  March 20, 2015 at 8:52 PM

 23. ni muda kidogo sana hatutokuwa na wewe najua utarudi kwa njia nyingine ambayo hatukuizoea ila wewe ni mpambanaji wa taifa hili

  Nzagamba Victor

  March 20, 2015 at 9:29 PM

 24. no longer at easy

  juma chitende

  March 20, 2015 at 9:44 PM

 25. binafsi mimi kama mwanasiasa mpya najifunza kitu hapa, nimesikiliza hotuba ya Mwal. Jk Nyerere hapa anaelezea umuhimu wa mgombea binafsi na ni vizuri nikuombe kaka mkubwa Ujiamini kwa utakayo yafanya na hivyo vijana tupo nyuma yako bado. Mimi binafsi nakuelewa mkuu

  Tumbu Ladislaus

  March 20, 2015 at 9:47 PM

  • Braza wewe kaza buti,tulikuwa tumeshaona uozo ulioko ndani ya chadema. Tuko nyuma yako kukuunga mkono kwa namna yoyote utakayokuja nayo. Hatupendi uishie hapo bali uendelee. Lakini usisahau kumwomba MUNGU Afya, Uhai na Uzima, na ktk mambo yako yooooooote MUNGU kwanza mbele sawa braza?

   Ashery

   March 21, 2015 at 1:45 AM

 26. kaka pole sana ila tuko nyuma yako kwa lolote lile

  philemon

  March 21, 2015 at 6:18 AM

 27. Mara nyingi tukigombana kwenye vyama hutupiana maneno,hutupiana lawama,lakini hutuba hii ni miongoni mwa hutuba za kuandikwa katika historia ya mabadiliko ya siasa za kistaarabu duniani,haionekani kumchafua mtu kukilaumu chama cha Chadema,na hii inatokana na hekima yako na busara zako za kuijenga demokrasia .Ni wazi unadhamira safi juu ya Watanzania.

  Abdalah Kileo

  March 21, 2015 at 6:25 AM

 28. This is a magnificent speech. I real love your last statement kutoka kwa kitabu cha grain of wheat.Wee brilliancy!!!!

  jey

  March 21, 2015 at 7:10 AM

 29. Herotic ideas never die,heroes will always be remembered and will be remembered more after their death.

  Salum

  March 21, 2015 at 9:29 AM

 30. Hongera Kaka Zitto Kwa Kazi Za Ujenz Wa Taifa Ulizozifanya,maisha Mema

  MATONYINGA ALEX MAKARO

  March 21, 2015 at 9:44 AM

 31. hongera kwA moyo wa kishupavu uliouonyesha kwa kupinga ufisadi ktk serekali yetu..Ww Ni jembe..usikate tamaa.,kutoka chadema si mwisho wa jitihada zako.,vyama viko vingi.,ingia kimojawapo uendeleze mapambano.,tuko pamoja nawe.,nakutakia kila la kheri..

  Anatoli massanja

  March 21, 2015 at 9:47 AM

 32. Kuna wakati ili kuleta maendeleo popote pale inabidi “kukubaliana kutokubaliana” iwe ni sehemu ya chaguo! Zitto umefanya hivyo! Umetoa somo kwa wengine kujifunza! Nafurahia jambo moja, kuwa ktk katiba pendekezwa ambayo kiukweli siipendi kwan wananchi tumevuliwa uwezo tuliouomba wa kuwavua vyeo tuliowachagua, angalau mgombea binafsi imesalia! Iwapo hiyo katiba itapita kwan ccm ni wengi kimazoea, basi gombea popote pale ili uwe mgombea binafsi.. Urais najua muda wako bado kwan muda haukuruhusu

  mnyanga

  March 21, 2015 at 9:56 AM

  • Muda haukuruhusu nikimaanisha umri kikatiba hivyo basi endelea kutoa mchango wako ktk nchi kupitia jukwaa lolote sahihi ambalo utaona linaweza kutukwamua hapa tulipofikia! You are the Great Philosophically..

   mnyanga

   March 21, 2015 at 10:04 AM

 33. Kaka Zitto, nimeumia sn kuona kwamba imefikia hatua ya ww ktokuwa mwañachama wa CHADEMA na kubwa zaidi wewe kuachia nafasi ya ubunge. Ulikuwa msaada mkubwa sn kwa taifa letu, hasa ktk kutetea maslahi ya wananchi wa taifa hili. Kamwe hautasaulika kwa ushujaa wako na uzalendo wsko. Nakutakia maisha mapya na yenye mafanikio zaidi popote uendapo. I believe a man can reshape himselves from what he does.

  A. Wama

  March 21, 2015 at 10:34 AM

 34. yap bab zitto kwa hotuma yenye hekma, kweli dunia ni mti mkavu inahitaji uweledi na wala si ukakamavu kwa mwenye kuelewa, you are the great in struggle, kwani anayetaka mafaninikio hachoki wala hachoshwi na vitimbi vidogo vya binadamu, umefuata protocal nzuri ambayo ni subra, naamini katika subira unayofanya utaibuka the great hero for another time.dont hasitate subra subra

  gimapc

  March 21, 2015 at 10:36 AM

 35. KUBALI NA UWE TYR KUISHI KIZALENDO KM ULIVOSEMA, JIPANGE KUWA TYR KUFANYA KAZI HATA NA USIOWAPENDA IKIWA WANA NIA THABITI KWA TAIFA. UKIJIWEKA MBALI NA KUSHAMBULIANA STAND WITH TANZANIANS HUKU UKITAMBUA HUWEZI KULIKOMBOA TAIFA UKIWA PEKE YAKO, WE NEED YOU YOU NEED US TOO. THEN BE FAITHFUL TO YOURSELF THE NEXT TO YOU WILL BE PROSPERITY

  Damian Dniel

  March 21, 2015 at 12:28 PM

 36. Hekima na busara ndio zimekupa mwongozo mzuri wa kulitumikia taifa letu la Tanzania na hekima hizohizo ndio zimesababisha ung’atuke kwenye marumbano yasiyokuwa na faida, binafsi nimekuona ww ni shujaa wa kuigwa katika hiki kizazi za ss. Tupo nyuma yako katika kulijenga hili Taifa letu.

  somboja

  March 21, 2015 at 1:00 PM

 37. Hongera sana kwa maamuzi magumu na kutoleta ushindani usio na nani bingwa. Nimesoma hotuba nzima sijaona sehemu inayosema madhaifu ya opponents wako, wee ni shujaa umekomaa kisiasa. Watanzania walio wengi wanakujua, hata mtu asiye enda shule anajua Zito ni nani, anatoka jimbo gani, anafanya nini Bungeni na kwa ajili ya nani? Huku uswahilini tunakukubali sana. You are my Hero.

  Mwakalonge, Daniel.

  March 21, 2015 at 2:52 PM

 38. Well,said Zitto,siku zote katika jamii,wale wanaonekana wanapigania haki huonekana maadui.Umefanya mengi kwa ajili ya chama na kwa taifa hilo halina ubishi.Remember: ‘A man of the People always be An Enemy of the People’ .Kwakuwa dhamira yako ni ya dhati kwa ajili ya maslahi ya taifa Mwenyezi Mungu atakujaalia Inshallah.Keep on going Komredi…

  Mohamed Mkangara

  March 21, 2015 at 6:58 PM

 39. Kaka Zito, Mwenyezi Mungu akutie nguvu mpya katika kipindi hiki kigumu kwako. Umepigana kadri ya uwezo wako ukiwa ndani na nje ya bunge, Watanzania tumeiona kazi yako na nia yako njema kwa Taifa la Tanzania. Mwl. Nyerere alisema ukishatenda dhambi ya chuki na ubaguzi, itendelea kukutafuna tu. Sasa nadhani na nataka kuamini kuwa Siasa za nchi hii ni za kubana demokrasia, na tukitaka kupanua demokrasia lazima tuanzie majumbani kwetu. Chama ni kama kanisa, unaweza kuanzisha au kujiunga na kanisa lolote unalodhani linaamini unachoamini. God Bless you Zito Kabwe Zuberi.

  Sanga, E.

  March 21, 2015 at 9:44 PM

 40. Hongera kwa hotuba nzuri. Safari huanza na hatua na huo ndo mwanzo

  Dominick James Kahungu

  March 22, 2015 at 3:09 AM

 41. Salute kaka, I believe in your capacity. It’s my hope that Aluta continua!!

  Yustino

  March 22, 2015 at 12:15 PM

 42. Ndugu yangu kwanza viongozi wote uliwafunika ,walikuhofu sana ,pili ,Uislam wako umekuponza ungekua Askof ungependwa ,tatu ,ww sio mhaga , NNE katika chama kipya weka usawa ,wote ni ndugu ,Tano nchi Wataisikia tu. sita ,usiofu Tumejipanga.

  mohamed h mohamed

  March 30, 2015 at 12:52 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: