Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Tuhuma dhidi yangu zichunguzwe-Zitto Kabwe

with 4 comments

Tuhuma dhidi yangu zichunguzwe-Zitto Kabwe

Katika kujitetea mbele ya Baraza la Maadili kuhusu tuhuma dhidi yake za kugawiwa mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Escrow, mbunge wa Sengerema Bwana William Ngeleja alisema kuwa ni kawaida wabunge kupewa misaada na wafanyabiashara na taasisi za umma. Katika Maelezo yake alirudia tuhuma za kipuuzi dhidi yangu zilizokwisha tolewa huko nyuma kwamba
1) nilipewa fedha na kampuni ya PAP na
2) nilipewa fedha na shirika la NSSF.

Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema “Hatutetereki”
https://zittokabwe.wordpress.com/2014/11/09/nashambuliwa-tunashambuliwa-pac-tunasema-hatutetereki/

Maelezo yangu kuhusu kazi za Kigoma AllStars/LEKADUTIGITE kwa NSSF na TANAPA. https://www.facebook.com/zittokabwe/posts/755794044441295

MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI
https://zittokabwe.wordpress.com/2012/08/01/maelezo-binafsi-ya-mhe-zitto-zuberi-kabwe-dhidi-ya-tuhuma-za-rushwa-hususan-kuelekea-katika-kupitisha-bajeti-ya-wizara-ya-nishati-na-madini/

Tuhuma zote hizo nimewahi kuzitolea ufafanuzi na kukanusha kwani hazina msingi wowote na zilikuwa siasa za majitaka. Hata hivyo bado zimekuwa zikijirudia rudia kwa malengo maalumu wanayoyajua wanaotoa tuhuma hizo. Watuhumiwa wa ufisadi wa escrow hawajazoea kuona taasisi za maadili zikifanya kazi kwa namna ilivyo sasa na hivyo wanajaribu na watajaribu kubwabwaja na kuhangaika ikiwemo kutaka kila mtu aonekane ni mtuhumiwa kama wao. Ndio maana Bwana Ngeleja ametaja msururu wa watu wakiwemo wafanyabiashara kwamba huwapa fedha wabunge bila chembe ya ushahidi.

Hivyo narudia kutamka kwamba ninataka uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ufanyike mara moja, wenye ushahidi wapeleke kwenye vyombo vya uchunguzi na niitwe mbele ya Baraza la Maadili kujieleza. Nikiwa mbunge ambaye maisha yangu yote ya siasa nimeyatumia kupambana na ufisadi na kuchochea mabadiliko ili kujenga misingi madhubuti ya uwajibikaji na kuimarisha taasisi zake, nipo tayari kwa uchunguzi mahususi dhidi yangu dhidi ya tuhuma zilizotolewa na nyingine zozote ambazo mtanzania yeyote anazo dhidi yangu.

Naunga Mkono kwa nguvu kubwa kazi inayofanywa na Baraza la Maadili. Ni kazi ambayo ilipaswa kuwa imefanyika kwa muda mrefu sana kwa kashfa mbali mbali ambazo viongozi wa umma wamepata kama vile ile ya rada, rushwa katika manunuzi ya mafuta mazito kuendesha mitambo ya Umeme, kujipatia mikopo kwenye taasisi za umma bila kulipa, kujilimbikizia Mali tofauti na kipato nk. Hivyo naiomba Sekretariat ya maadili iyachukue kwa uzito maoni ya Bwana Ngeleja na kama yana uzito kwa mujibu wa sheria na kanuni yafanyiwe uchunguzi. Nipo tayari kufanyiwa uchunguzi.

Katika kujenga Misingi Madhubuti ya uwajibikaji nchini ni lazima kila kiongozi aheshimu taasisi kama Baraza la Maadili. Baraza likiendelea kufanya kazi kama inavyofanyika sasa, vita dhidi ya ufisadi itakuwa imepiga hatua na porojo za kuzushiana mitaani zitapungua.

Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC
Dar Es salaam, tarehe 4 Machi 2015.

Written by zittokabwe

March 4, 2015 at 1:59 PM

4 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Mheshimiwa Zitto!
  Naamini kuwa kazi unayofanya tunaitambua na hata mimi binafsi nikiwa mtanzania maskini na mpenda amani na maendeleo kwa vijana walio wengi na si wachache kama hao wasio adilika, nakuomba uendelee kupambana bila kutetemeka wala kurudi nyuma. Tumechoka kuibiwa na watu kujifanya Miungu watu wasioguswa wakikosea na wakiguswa wanataka kuzamisha Boat nzima hata wasiohusika wafe.
  Mimi si mshabiki wa chama chochote kile ila nina uchungu sana kuona tunarudishwa nyuma.
  Hii nchi si ya chama wala kiongozi yeyote ila ni ya watanzania wote. na watu wasiishi kwa migongo ya watu walio maskini.

  Leo

  March 4, 2015 at 2:09 PM

 2. Nakupa pongezi saana Zito,Daima HAKI hudai HAKI.Haki itaharamiwa kila mara ila hatima yake ni HAKI.A CHANGE IS HERE TO COME,Lets play with a bolded UNITY.

  Simon

  March 4, 2015 at 3:52 PM

 3. mheshimiwa!nakuomba usife moyo unajua mtu akikutwa na tuhuma lazima atafute njia z kujitetea.kwaiyo wewe kama kiongoz unaejali maslah ya nchi huwez fanya ufisadi kama huo.vijana tupo nyuma yako

  Regan mtuka

  March 4, 2015 at 5:06 PM

 4. Thank you for you clarification this will strength your credibility! Philemon

  Sent from my iPhone

  >

  Philemon Mtoi

  March 5, 2015 at 8:03 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: