Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Kwanini Bei ya mafuta kwa walaji haishuki kwa kasi?

with 6 comments

Kwanini Bei ya mafuta kwa walaji haishuki kwa kasi?

EWURA

 

Kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 mpaka Desemba, bei ya mafuta ghafi imekuwa ikishuka kutoka $110 kwa pipa mpaka $56 kwa pipa. Mporomoko huu wa bei wa zaidi ya 40% haujaleta unafuu kwa mtumiaji wa kawaida wa mafuta ikiwemo wenye daladala na kupelekea nauli za usafiri wa umma kupungua. Leo bado bei ya mafuta kwenye vituo vya mafuta ni tshs 2029 kwa Petroli na 1909 kwa dizeli, bei ambayo ni karibia ile ile kwa miezi michache iliyopita.

EWURA,inasemekana, wamesema kuwa bei za hapa nchini hushuka baada ya miezi 2 kwa sababu waagizaji huagiza kwa ujumla mafuta mengi zaidi na hivyo kutofaidika na punguzo la bei. Hata hivyo bei zimeanza kushuka toka mwezi Julai na hatujashuhudia unafuu wowote kwa wananchi. Ingekuwa bei ya mafuta imepanda tungeona bei zimepanda mara moja na sababu za kununua ‘ bulky’ huwa hazitolewi.

Ni kweli kwamba Tanzania hununua mafuta yaliyosafishwa na hivyo bei inayoshuka sio hiyo. Lakini hao wasafishaji hununua mafuta ghafi yenye bei ndogo hivi sasa kwa hiyo ni dhahiri lazima bei za pampu zipungue. Vile vile ni kweli kwamba thamani ya shilingi ya Tanzania imeporomoka hivyo wananchi hawawezi kuona unafuu wa bei ya mafuta kwa sababu hununuliwa kwa fedha za kigeni na kuuzwa kwa Sarafu yetu. Hata hivyo kasi ya kushuka kwa bei ya mafuta ni 40% wakati shilingi imeshuka kwa chini ya 10%. Katika hali ya kawaida na kwa kutumia mfumo wa kukokotoa bei wa EWURA, angalau bei ya mafuta ingeshuka kwa kati ya 15% and 25%.

Ni dhahiri mamlaka za nchi na hasa EWURA wanapaswa kueleza kwa umma ni Kwanini bei za mafuta hazishuki kulingana na bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia. Wananchi wana haki ya kujua na kama hakuna Maelezo basi bei hizo zishuke na wananchi wafaidike na punguzo hilo.

Zitto Kabwe, Mb

 

Advertisements

Written by zittokabwe

January 4, 2015 at 2:12 PM

Posted in Uncategorized

Tagged with , ,

6 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Tanzania vitu hupanda kwa kasi sana,ila kushuku huwa vina shuka taratibu sana,na huwa havirudi kwen bei ya zamani.

  SUMA MZEE

  January 4, 2015 at 3:10 PM

 2. Hili tatizo bado linaikabili Wizara ya Nishati na Madini, Sijui kwanini Muhongo hang’olewi kama ilivyopendekeza kamati ya kudumu ya bunge unayoiongoza!. hapa kuna kubebana

  benedicto didas tembagala

  January 4, 2015 at 5:38 PM

 3. yeah! ni kweli kaka zitto, cjui ni kwanini ??, imefikia hatua sasa wananchi tumeshindwa hata cha kufanya!!

  Andrew nakolo

  January 5, 2015 at 8:06 AM

 4. Fanya kazi mh Zitto.hakika hii mamlaka ya EWURA km ipo kwa maslahi ya wachache hasa wao wenyewe na wafanyabiashara wakubwa,heri livunjwe tume ya bei irudi kiufanisi zaidi,hawa wanakula% ya walaji wanatetea wauzaji.Km wabunge wengine watashikirikiana nawe kupigania maslahi ya wadogo itakuwa faraja na kura zitakuwa zimelipa.Songa mbele mh

  Amani shoo

  January 5, 2015 at 2:13 PM

 5. Kiukweli watanzania tumekuwa tukinyonywa sana na hizi mamlaka… mi natoa pongez zangu kwa watanzania wachache kama mheshimiwa Zitto Kabwe kwa kuchukua mda wake kututetea wananchi wenye hali ya chini ya kimaisha…
  Keep on a good work bro tunateseka sana kwan wengne hata kupata tu ada ya tshs.600,000/= ni kazi lakin wao kwavile wanakula vizur na kusomesha watoto wao bac wanashindwa hata kusimamia mamlaka walizopewa kwajili ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla..

  sebastian bahati

  January 6, 2015 at 6:34 PM

 6. Reblogged this on MKWELI DAIMA.

  EMANUEL HINGI

  January 11, 2015 at 11:11 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: