Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Vitabu Nilivyosoma 2014 – Books I have read in 2014 #BooksRead2014 #letsread

with 20 comments

Mwaka 2014 nimesoma vitabu 53 na nimefanya uchambuzi wa vitabu 21 kupitia safu ya Kitabu na Kalamu ya gazeti la Raia Tanzania kila Jumatatu.

Tangu nimeanza utaratibu kuchapisha idadi ya vitabu nilivyosoma huu ni mwaka wa tatu sasa. Mwaka 2012 nilisoma vitabu 31, mwaka 2013 vitabu 13 na 2014 vitabu 53.

Mwaka 2014 niliuanza kwa changamoto nyingi sana katika maisha yangu ya kisiasa; kuvuliwa nyadhifa katika chama na kuwa hatarini kuvuliwa uanachama kilichopelekea kwenda mahakamani kutetea uanachama wangu. Vile vile kuanzia mwezi Machi nilianza kumwuguza mama yangu mzazi mpaka mungu alipomchukua hapo mwezi Juni. Muda mwingi niliutumia kusoma vitabu kama matibabu ya msongo ( therapy ). Mchakato wa Katiba ( ambao sikushiriki kwa sababu ya kuona dhahiri hautaleta katiba bora ) pia ulinipa muda mzuri wa kufanya jambo ninalolipenda kuliko yote – Kusoma.

Kitabu kimoja (ADAPT) kimenifanya kubadili kabisa mtazamo wangu wa maisha.

Vitabu 2 ( Exposure na Munyakei story ) vilinitia faraja kubwa katika kazi niliyokuwa nafanya tangu mwezi Machi ( uchunguzi wa akaunti ya #TegetaEscrow ).

Kitabu kimoja ( The myth of the strong leader ) kimepanua sana uwezo wangu katika kuchambua viongozi na mafanikio yao. Vyote nilifanikiwa kuvifanyia uchambuzi katika RaiaTanzania.

Bado India imechomoza sana katika orodha yangu. Miezi 2 niliyokaa Madras kumtibu mama imechangia sana kuongeza vitabu kutoka waandishi wa India. Vingi ni fiction. India Calling kilinivutia zaidi kuliko vyote. Mwaka 2014 nimeanza kusoma kazi za ushairi za zamani (Classics) ili kupata maarifa mengi yaliyojaa kwenye ushairi na kuendeleza ujuzi wa kuandika mashairi.

Kitabu kimoja nilikianza nikashindwa kukimaliza, The Capital. Mungu akipenda nitakimaliza mwaka 2015. Karibu katika orodha yangu ya vitabu mwaka 2014.

Zitto Kabwe, MB

BOOKS THAT I HAVE READ IN 2014

View this document on Scribd

Written by zittokabwe

December 27, 2014 at 12:16 PM

20 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. This is encouraging!Hongera sana, tukiweza kuiweka culture ya usomaji vitabu itapanua mafikirio yetu na kuwa na taifa bora zaidi!

    Noberto Makonda

    December 27, 2014 at 3:49 PM

  2. Mh, Ndugu lakini pia naweza kukuita Dr. Zitto Kabwe !

    Binafsi napenda kukupongeza kwa mapambano na mifumo dhalimu , hongera saaaana ! Wewe ni mmoja au wakwanza uliye, unaye na utakayefungua akili na macho ya Watanzania. Mchango wako mkubwa na huonekan
    a pale Bungeni .
    Kiukweli akili unayo na inatumika ” umeelimika” .

    Nangependa kusema pia kwa vyovyote vile itakavyoelezwa au kusemwa hatuwezi kuainisha mafanikio, ukuaji na uelekeo wa leo wa ” CHADEMA” bila kutaja nafasi yako “COMRADE ZITTO ” . Ni muhimu saaaana, hivyo nakuomba kaka fanyeni mashauriano ya maridhiano na Uongozi wa CHADEMA uendelee kuwa mwanachadema ! Vinginevyo mtaua ukuaji wa vyama pinzani hapa TANZANIA .

    Nikupongeze kwa kazi ngumu , kubwa na kujitoa mhanga # TEAS TEGETA ESCROW ACOUNT SCRAMBLE . Kwa ushirikiano na akina Kafulia, Kunjonbe, Kigwangala, Tundu , Mdee, n.k mlifanyakazi inayotakiwa ! Hongereni saana tuko nanyi na Mungu awalinde kwa yote mabaya.

    Mwisho nikupongeze kwa tabia tunduizi ya kupiga shule kila uchao # knowledge is power !!! Power hii ikodhahiri ktk hoja zako!
    U mfano wa kuigwa ! Mola akuongoze kwa kila jambo

    mutagayara

    December 27, 2014 at 4:07 PM

  3. Hakika unatisha mtetez wa wanyonge.mungu akujalie afya njema ktk kukamilsha michakato yote kwa kuonesha bidii zaid mwaka ujao.be blessed hourable.

    Apolinary nsindagi

    December 27, 2014 at 4:46 PM

  4. Reblogged this on mwanaapolonews.

    mwanaapolonews

    December 27, 2014 at 5:08 PM

  5. i have inspired bro

    ramadhan kilowoko

    December 28, 2014 at 3:51 AM

  6. Zitto Unafaa kuitwa kiongozi bora…! nafurahishwa sana na kazi zako,na napigania nifike pale ulipo. Mim binafsi nimesoma The myth of Strong leader..ni kitabu kizuri sana,kwa watu wenye future. Mungu akubariki sana, uendelee kuwa mtu wa kufanya vitu vizuri na vyenye ushahidi ktk masuala yanayoligusa taifa letu (TZ), Kwani mwanafalsafa mmoja alishasema”Without research, knowledge is died”

    Rajab Shamy.

    December 28, 2014 at 9:05 AM

  7. uko vyema mjomba..!

    Ezzy Jeckiah Swema

    December 28, 2014 at 10:25 AM

  8. Your legacy shall inspire generations Hon. Zitto. Keep it up man…

    Alby

    December 28, 2014 at 12:20 PM

  9. Kaka Zitto unafaa kuigwa kwa kila kitu, nimeipenda sana hii post yako na ujumbe wake maana umenifanya nijifanyie self audit matokeo yake ni kwamba sijasoma kitabu chochote kwa 2014. Nitauanza mwaka 2015 kwa kufuata nyayo zako kiongozi wangu. Big up brother!

    Pascal

    December 28, 2014 at 1:38 PM

  10. Mheshimiwa nakupongeza!
    Wewe ni kati ya masalia machache ya vijana orijino waliokuwa wanaona fahari katika hobby ya kusoma vitabu. Waliokuwa wanashindana kuonyesha nani kasoma vitabu vingi katika mwaka. Enzi hizo sasa tunazikumbuka tunapoona vijana mmoja mmoja kama wewe wakituorodheshea idadi ya vitabu walivyosoma.

    Vijana wetu wengi sasa wanasoma vitabu ili kufaulu mitihani tu. Tena hawavimalizi, maana wanasoma kwa kufuata topic zilizo kwenye mitaala ya masomo yao. Mkamate kijana yeyote aliyemaliza chuo kikuu chochote hapa nchini, halafu muulize tangu azaliwe amesoma vitabu vingapi kwa umakini hadi akavimaliza. Utashangaa kuona jinsi anavyojiumauma kukupa jibu la uhakika. Vijana wetu nawaasa waige mfano wa kijana mwenzao, Mheshimiwa Zitto ili wapanue ufahamu wao wa masuala mbalimbali.

    Bundala

    December 30, 2014 at 7:17 PM

  11. vizuri sana mkuu, inatia moyo wa kusoma

    Kamala J Lutatinisibwa

    January 2, 2015 at 2:33 PM

  12. Hakyamungu Wew Ni Mfano Wa Kuigwa Xan Mh.Zitto. Mungu Akupe Elimu Na Umri Mrefu Zaidi Uzidi Kufanya Mamb Mengi Mazuri Zaidi Ya Haya
    #big Up%

    Prince Kajeze

    January 4, 2015 at 4:26 PM

  13. […] Kupande wa Z nyingine ni Mh ZITTO Kabwe ambaye yeye amefikisha vitabu 100 kwa kipindi cha miaka mitatu https://zittokabwe.wordpress.com/2014/12/27/vitabu-nilivyosoma-2014-books-i-have-read-in-2014-booksr…. […]

  14. Napenda kuchukua nafasi hii kukupa pole kwa kuondekewa na mama yako mzazi mungu ailaze roho yake mahal pema pepon amin.
    Dunia hii ina watu wengi makini wanaopambania haki za wengine ili kuleta usawa katika maisha yetu ya kila siku na wewe pia ni mmoja wa watu makin katika nyanja ya kisiasa nakupongeza mheshimiwa zitto kabwe .Pia usichoke kusoma vitabu maana ndio msingi wa kiongozi bora.

    ustadh maduhu

    January 10, 2015 at 10:49 AM

  15. Hongera sana kaka Zitto kwa kuamua kusoma vitabu. Nadhani ndiyo maana katika maisha yangu tangu nimeanza kukufuatilia kama mwanasiasa kijana, mwenye ujasiri na unayevutia, kwa Mara ya kwanza nimesikia ukiongea angalau maneno ya unyenyekevu kuhusu utayari wako kuzungumza ili urejee Chadema.
    Utajiri wa hekima na maarifa uko ndani ya vitabu. Ushauri wangu kwako, soma vitabu vilivyoandikwa na watumishi wa Mungu vinavyohusu uongozi na uzoefu WS maisha. Hao ndiyo vitabu vyao vimezalisha viongozi wachache waliowahi kuacha alama ya uongozi wa mfano. Huo ushauri tu

    David Kumbuka

    January 11, 2015 at 3:37 PM

  16. Reblogged this on MKWELI DAIMA.

    EMANUEL HINGI

    January 11, 2015 at 11:09 PM

  17. Vizuri sana Kaka Zitto kusoma vitabu ndio kila kitu katika maisha

    Benjamine kataga

    December 31, 2015 at 11:50 AM

  18. your good comrade zitto

    maganga dashina

    June 19, 2016 at 7:28 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: