Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

MSIMAMO WA NDUGU ZITTO KABWE KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA

with 7 comments

MSIMAMO WA NDUGU ZITTO KABWE KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA

Jana tarehe 29 Julai, 2014 nimefanya mahojiano katika kipindi cha PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM. Baadhi ya vyombo vya habari vimeandika mahojiano yale. Napenda nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu msimamo wangu kuhusu mchakato wa Katiba.

Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa Washirika wake.

Pili, Mimi niliunga mkono ‘protest’ ya baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mkutano ule. Vilevile niliunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni Rasimu iliyotokana na Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba. Nasisitiza umuhimu wa kupata Katiba BORA itakayoimarisha DOLA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tatu, kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba Bora. Mkwamo unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana. UKAWA hawataki mazungumzo na Viongozi wa Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza UKAWA jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka. Ushauri wangu ni kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache kama ifuatavyo;

i) Tume ya Uchaguzi ili iwe huru na ionekane kuwa huru, ikiwemo kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia uchaguzi

ii) Kuruhusu mgombea binafsi

iii) Kuondoa Mafuta na Gesi kama Jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa Mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano

Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa maridhiano utakuwa hauna maana yeyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua madawa vijijini. Mimi binafsi sitahudhuria mkutano wa Bunge Maalumu kama makundi hasimu hayatakuwa yamefikia maridhiano.

Kabwe Zitto, MB/MBMK

Written by zittokabwe

July 30, 2014 at 2:07 PM

7 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Pamoja na kwamba sikusikiliza mahojiano yako na PB; msimamo wako ni sahihi (kwa mtazamo wangu) na ninaamini kwa mtu yeyote anayetamani kuonda Tanzania yenye neema ana msimamo huo. Tangu hatua za awali za kutunga sharia ya mabadiliko ya katiba baadhi tulijua ni changa la moto tu na hakuna nia ya dhati ya kutaka kuwepo kwa katiba mpya. Wenye kaya walituambia na wanatuambia ” Katiba iliyopo inatosha”. Katiba mpya si msingi wa mabadiliko ya maendeleo ya TZ.

  Kwa nini mahojiano yako yamepata promo kubwa na hata magazeti mengine kuandika kinyume???? Fahamu kuwa tangu mgogoro wako na chama chako uwe dhahiri hivi sasa wewe ni silaha muhimu kwa wanasiasa wa siasa za maji taka. Kila kauli yako na tendo lako linatumika kutaka kuonesha kwa kiasi gani unachukia si UKAWA bali CHADEMA. Aidha unataka kuonesha ni kwa kiasi gani umetumiwa na CCM kuua upinzani. Kaka, tumia akili zangu sasa kuliko wakati mwingine wowote ule katika maisha yako. Kila hatua utakayochukua kwa neno au tendo litaamua hatuma yako.Mfano angalia msiba wa mama yako ulivyopata promo chanya na hasi. Wewe unajua kabisa uzito na tafsiri ya “pole na rambirambi” iliyotolewa kwako.

  Edna J. Lugano

  July 30, 2014 at 5:50 PM

 2. ni kweli hakuna mwenye dhamira ya dhati juu upatikanaji wa katiba mpya.

  ferouz kara

  July 30, 2014 at 9:22 PM

 3. Ndugu zitto upo sahihi kabisa kwani bila malidhiano wataenda kupoteza muda pamoja na pesa za walipa kodi. Kwani tunahitaji katiba bora sio bola katiba kwani huo ni mskabali wa nchi

  Mwimbwa rangimpya

  July 31, 2014 at 10:17 PM

 4. ni kweli bwana kabwe bunge la katiba linatakiwa livunjwe mpaka 2016 ili maridhiano yafanyike

  Mlelema

  August 26, 2014 at 1:20 PM

 5. wote wangekuwa na mawazo kama yako tusingekuwa na mambo kama haya yanayofanyika sasa….sasa toa semina kwa wanasiasa wengine.

  karia peter

  September 7, 2014 at 3:20 PM

 6. Serikali haijali umaskini wa Watanzania ila matumbo yao kunenepa na mifuko yao kujaa.

  Ntilongwa Ruhana

  September 7, 2014 at 5:20 PM

 7. Kwa maoni yangu Bunge maalumu la katiba, baada ya kukaa vikao vyake vya ilani ya chama chao badala ya rasimu ya katiba yenye matakwa ya wananchi, na watanzania lishitakiwe kwa ubadhilifu wa mali ya umma. maana hatukuwatuma kufanya hayo.

  Na wewe kaka, jitenge na movements za watu ambao watajaribu kutumia vipawa vyako kujificha na kudhuru maisha ya wengi ilhali wao wanaendelea na ulaji. Mwisho wa siku wakishafanikisha malengo yao utajikuta uko pekee yako maana mfumo wao hautaweza kukubeba. Waliotangulia, walipojichanganya na kuwatumikia wajanja kwa njia hiyo leo wamekuwa mithali na kichekesho ndani ya nchi yao. Ni jukumu ambalo halina kiinua mgongo, so take care!

  Fred Cyril Kibali.

  September 27, 2014 at 9:55 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: