Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Mkataba wa Gesi umevuja: #Tanzania kupoteza shs 1.6 trilioni kwa mwaka – #Norway kujirudishia misaada yake yote nchini kupitia mkataba huu

with 20 comments

Mkataba wa Gesi umevuja: Tanzania kupoteza shs 1.6 trilioni kwa mwaka

–       Norway kujirudishia misaada yake yote nchini kupitia mkataba huu

 Zitto Kabwe, Mb

Mkataba wa mgawanyo wa mapato yanayotokana na uzalishaji wa Gesi Asilia (PSA) kati ya Shirika la Mafuta na Gesi Tanzania na Kampuni ya Mafuta ya Norway umevujishwa (https://onedrive.live.com/view.aspx?cid=0EC42B180C06D0B8&resid=EC42B180C06D0B8%21107&app=WordPdf). Toka Mkataba huo uvuje na kuanza mijadala kwenye mitandao ya kijamii, habari zake zimekuwa zinazimwa na hivyo kukosa kabisa mjadala mpana kitaifa na hasa kwa wananchi wenye rasilimali zao. Mwanzoni wengi wetu tulidhani (kwa makosa) kuwa tatizo la mkataba huu ni eneo la umiliki wa kampuni tu (shareholding) kulingana na namna ulivyowasilishwa, kumbe mgawanyo mzima wa mapato unakwenda kinyume na maelezo ya Serikali na TPDC kwa umma.

Mkataba uliovuja unaonyesha kwamba makubaliano ambayo Serikali imeingia na Wawekezaji hawa kutoka Norway yanaenda kinyume kabisa na mfano wa mkataba unaotakiwa kusainiwa (Model PSA). Kwa mujibu wa makala iliyoandikwa na jarida la mtandaoni ( http://africanarguments.org/2014/07/04/leaked-agreement-shows-tanzania-may-not-get-a-good-deal-for-gas-by-ben-taylor/ ) Tanzania itapoteza zaidi ya shilingi 1.6 trilioni kila mwaka kulingana na viwango vya uzalishaji wa gesi asilia katika Kitalu namba 2. Kitalu hiki kinamilikiwa na Kampuni ya StatOil ya Norway na kampuni ya ExxonMobil ya Marekani. Norway ni nchi inayosifika duniani kwa kupambana na rushwa na kwa kutumia vizuri rasilimali yake ya mafuta.

Uchambuzi nilioufanya kulingana na viwango vya mgawo wa mapato kati ya ‘model’ PSA na mkataba huu unaonyesha kwamba Tanzania itapata mgawo kiduchu sana na kinyume na mgawo unavyopaswa kuwa. Mgawanyo ni  kama ifuatavyo katika majedwali hapa chini; Ikumbukwe kuwa mgawanyo huu hupatikana baada ya mwekezaji kuondoa gharama zake za uzalishaji, kinachobakia ndio hugawanywa kati ya mwekezaji na Tanzania.

Jedwali 1 Mkataba wa mgawanyo wa Mapato unaopaswa kutumiwa na TPDC (Model PSA) katika Mikataba na Wawekezaji

Viwango vya uzalishaji kila siku (MMscf per Day) Mgawo wa TPDC (Profit Gas)  Mgawo wa Mwekezaji (Profit Gas)
0 249.999 50 50
250 499.999 55 45
500 749.999 60 40
750 999.999 65 35
1000 1249.999 70 30
1250 1499.999 75 25
1500 Above 1500 80 20

 

Jedwali 2 Mkataba wa mgawanyo wa Mapato kati ya TPDC na Statoil/ExxonMobil.

Viwango vya uzalishaji kila siku (MMscf per Day) Mgawo wa TPDC (Profit Gas)  Mgawo wa Mwekezaji (Share of Profit Gas)
0 299.999 30 70
300 599.999 35 65
600 899.999 37.5 62.5
900 119.999 40 60
1200 1499.999 45 55
1500 Above 1500 50 50

 

Ukilinganisha majdwali haya utaona kwamba mgawanyo wa mapato utafaidisha zaidi kampuni ya StatOil na ni kinyume kabisa na mkataba unavyopaswa kuwa.

Wakati mgawo wa nusu kwa nusu upo katika uzalishaji wa chini kabisa kwenye ‘model PSA’, kwenye mkataba wa StatOil mgawo huo upo kwenye uzalishaji wa juu kabisa. Ukilinganisha mgawanyo huu wa mapato, iwapo kiwango cha ‘model PSA’ kingetumika Tanzania ingepata shilingi 1.6 trilioni zaidi ya kiwango itakachopata kwenye mkataba wa sasa uliovujishwa. Hii ni kutokana na Bei ambazo Shirika la Fedha la Kimataifa limeweka katika uchambuzi wake (https://www.imf.org/external/pubs/ft/scr/2014/cr14121.pdf ) kuhusu Gesi asilia ya Tanzania.

Kwa mujibu wa Mwandishi Ben Taylor katika makala iliyotajwa hapo juu, kiwango cha mapato ambacho Kampuni ya StatOil ya Norway itajipatia kutokana na mkataba huu wa kinyonyaji, katika kipindi cha miaka 15 ya kuzalisha Gesi Asilia nchini itakuwa ni sawa sawa na misaada yote ambayo Tanzania imepata kutoka Norway toka Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961. Tangu Tanzania ipate Uhuru Norway imetoa misaada ya thamani ya $2.5 bilioni, wakati kwa mkataba huu na Kampuni ya StatOil ambayo inamilikiwa na Serikali ya Norway, kwa miaka 15 watapata $5.6 bilioni. Kwa hiyo kwa miaka 7 tu Norway itakuwa imerudisha misaada yote yake mara mbili zaidi!

Kuvuja kwa Mkataba huu kumesaidia sana kuona ukweli wa matamko ya viongozi wetu kuhusu ni namna gani Tanzania itafaidika na utajiri wake wa gesi. Kama kwa mkataba huu mmoja tu Taifa litapoteza matrilioni ya fedha kiasi hiki, ipoje hiyo mikataba mingine 29? Hivi sasa ugunduzi wa Gesi Asilia nchini ni lita za ujazo trilioni 51 ambayo ni sawa na mapipa bilioni 10 ya Mafuta. Katika Gesi Asilia yote iliyopatikana nchini, StatOil peke yao wana jumla ya lita za uzajo trilioni 20, sawa sawa na mapipa ya mafuta bilioni 4 (zaidi ya mafuta yaliyogunduliwa nchini Uganda na Ghana kwa pamoja). Hata hivyo utajiri wote huu utainufaisha zaidi Norway na Marekani kupitia makampuni yao kuliko watu wa Tanzania. Watanzania watabakia wanapewa misaada ya vyandarua na mataifa haya ilhali wanafaidi Gesi Asilia yetu.

Natoa wito kwa Wizara ya Nishati na Madini kutoa tamko kuhusu mkataba huu kati ya Shirika la TPDC na StatOil. Vile vile Kampuni hii ya StatOil kutoka nchi rafiki mkubwa wa Tanzania ina wajibu wa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na mkataba huu. Serikali ieleze ni hatua gani inachukua kurekebisha Mkataba huu. StatOil nao waeleze watachukua hatua gani kuhakikisha wanaacha unyonyaji huu mkubwa na wa aibu kwa Taifa la Norway.

Sasa ni wakati mwafaka Watanzania kuweza kuona mikataba yote ya Gesi na Mafuta ambayo Serikali imeingia na Wawekezaji. Uwazi wa Mikataba sasa. Nimewahi kuandika huko nyuma (https://zittokabwe.wordpress.com/2012/09/17/press-release-contracts-review-is-a-publicity-stunt-and-creation-of-unnecessary-uncertainty-in-the-sector/ ) kwamba njia pekee ya Watanzania kufaidika na utajiri wa rasilimali zao ni kuhimiza uwazi wa Mikataba. Mkataba huu wa StatOil uliovujishwa uwe ni chachu ya kulazimisha Serikali na Makampuni kuweka mikataba yao wazi. Tuanze mashinikizo haya sasa kwa faida ya vizazi vijavyo.

Written by zittokabwe

July 6, 2014 at 11:02 AM

Posted in Uncategorized

Tagged with , ,

20 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Inasikitisha sana kuona viongozi wetu wanakuwa sio wasikivu sisi watanzania hatutaki kusikia misaada kutoka nje tunataka kusikia ubunifu na uwajibikaji wa sisi wenyewe watanzania ili tuweze kupiga hatua wakumbuke kuna mamilioni ya watanzania ambao hatuna hata mahitaji muhimu lakini wenzetu kila kitu wanacho hivi kweli hawaoni wakija huku ulaya kwamba wenzetu ni wanyonyaji ? mimi sidhani kuna mtu ambae haoni hili je swali kwako Mh #Zitto unadhani viongozi hawana uchungu na umakini katika kusimamia maliasili na mambo mengine kiumakini ? na je nini kinachosababisha hili

  Amosi Peter Rwangarya

  July 6, 2014 at 11:25 AM

 2. Sidhani kwamba wanaorway ni waaminifu, hapa wanafanya biashara

  kambi

  July 6, 2014 at 2:15 PM

  • The point is this we are not responsible for our own countries even for ourselves in life. Take this vivid example then you will see why we are not responsible.A village has no even water and the village has revenue which they correct form different shops and markets and no one thinks about providing important service LIKE WATER …..me i believe if leaders want Africa for African first then others follow like the way its in America and Europe too then we shall be solving many African problems but our leaders are so blind with abruptly life change which they get after being corrupt so at the end of the day no one things about being strict in putting everything in the right way.I am really very sad to see how much resources we have and no one tried to use this in the right way and another thing so important we should not talk to much rather than doing Benjamin Franklin once said (Well done is better than well said) so Mh Zitto well said but we are waiting for well done as said by Mr Kambi mabillion ya uswis yako wapi,hela za EPA ziko wapi ?

   Amosi Peter Rwangarya

   July 6, 2014 at 4:08 PM

  • Rushwa kwa nchi zilizoendelea ipo tena sana, tusibweteke.

   jones igembe

   July 9, 2014 at 2:52 PM

 3. Mh Zitto Unafaa kuwa Rais wa Tanzania, yenye utajiri mkubwa….Tatizo ni pale ulipojiingiza kwenye ile vurugu, na chama chako, na baadhi wa Tanzania kukosa imani ingawa wangependa waongozwen mtu anaesema ukweli,

  SWALA NA MABILIONI YA USWISI LIKO WAPI, HELA ZA EPA ZIKO WAPI.

  hawa wahusika wako wapi…

  kwa nn watanzania tunaachwa katika giza nene? mpaka lini? Nikup habari moja huku mtaani, watanzania wanakufa sana kwawa magongwa mbali mbali. Inaonyeshwa wanatafuta tu upenyo wote wapenye, wamechoka wanaogopa, wanatishwa na hali ilivyo, kila kukicha afadhai jana.

  magonjwa yanayoongoza kuwaua watanania ni kisukali, presha, nk
  wanaona kila kinachoendelea, tunawashukuru wanasiasa kama wewe vyombo vya habari huru walau tunapata taarifa ingawa sio kwa ubora unaostahili,

  lakin watannzania ttunajilia tu kila kitu hapa ndo tatizo lilipo, kwa kwa kuwa ujinga, umasikini, kutojua nini chakula bora, sumu na wanga, kutengeneza mazingira bora ya kuishi ili kujikinga na magonjwa hatari.

  TATIZO NI MAZINGIRA MAGUMU YA KUISHI.

  iweje nchi kama norway tajiri, yenye idadi ndogo ya watu, mil 5 kwa noway mil 50 kwa tanzania) data sio rasmi. watunyanganye mapipa kiasi hiki cha gesi? tena wale wanagesi, na mafuta, na reserve yao ya mfuko wa pesa za mafuta hatajatumika, hii dhambi gani hii? wanataka waishi sis tufe. ?

  kambi

  July 6, 2014 at 2:34 PM

 4. Ziwekwe sheria kali, viongozi wetu wanaotuingiza kwenye mikataba mibovu wanyongwe au wafungwe maisha jela

  Honery

  July 6, 2014 at 3:50 PM

 5. Kiukweli Mh. Zitto unajitahidi sana kutupulizia tarumbeta masikioni mwetu ili tuamke lakini ndo kwanza tunavuta blanket ili tuendelee kulala. Taarifa hizi na nyingine nyingi ulizozitoa hakuna hata moja ambayo cc kama wananchi wa tanzania tumezifanyia kazi. Ndo maana uozo huu unaendelea na utaendelea kwa miaka zaidi ya 10 kama watz hatutaamka. Nasema haya kwa sababu watz tunapenda kusiki nani kafanya nini na nani kasema nini lakina hatuchukui hatua madhubuti dhidi ya watuhumiwa hata kama ushahidi kamili tunao. Kwa mantiki hiyo kuna watu wako mitandaoni kuponda kila unachoposti mh. Zitto. Hii inatokana na ahadi zako ulizozitoa ambazo hukuzitimiza. Kwa upande wangu sikulaumu kwa sababu najua hata ungetaja kusingekuwa na hatua zozote dhidi ya hao walioficha mabilion uswiz. Sana sana tungekuwa bizy kujadili mwisho wa siku watu wanapanda vitandani wanalala. Pia tungekuwa tumekufanya kuwa target ya hao uliowataja ambapo tusingekusaidia kwa lolote zaidi ya kukusifu tu kama watz wanavyofanya kwa DAVID KAFULILA.

  Sembe A.

  July 6, 2014 at 3:57 PM

 6. Swali ni je, hawa viongozi wanaotia saini mikataba hii wanajua wanachokifanya au hawajui? Ikiwa wanajua, wanaona wenzao wa upande wa pili wanachuma pesa hizo na kuzipeleka kwao wakati wao wanabakia omba omba wanaona fahari gani? Kama wanaosimamia ni watu waliobobea kama Prof. Muhongo, elimu yao inatusaidia nini? Kuna tofauti gani gati a Stephen Ngonyani (Prof. Maji marefu na Prof. Muhongo)

  asungwile

  July 6, 2014 at 5:55 PM

 7. Kawaida na hii haitakwisha kuchukuliwa uchumi wetu huku tuna toa macho…mikataba mibovu tangu nizaliwe na nina wajukuu still mikataba inawanufaisha investors, no wonder Baba Nyerere alijaribu kuepuka. Tena tuangalie umuhimu wa amani yetu, tusije geuka landa of blood like other countries who are fighting for their own natural resources, Libya, Iraq, Ukraine, Nigeria, Angola, Sierra Leone, Liberia, Syiria….its all about mad ini na nishati…be careful bongo……

  E Lambo

  July 6, 2014 at 7:09 PM

 8. Inauma sana KIONGOZI.. Sasa mhe. Mbunge peleka hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mamuu bungeni au hoja binafsi huu ya mikataba inayoingiwa na serkali na kielelezo hiki unacho tumfunge tu yule profesa Muongo anayetumia taaluma yke vibaya, hta hvyo vyuo alivyoptia bora wamnyanganye utaalamu waliompatia… INAUDHI NA INAUMIZAAA

  Jackson

  July 7, 2014 at 1:57 AM

 9. […] More from Zitto: Mkataba wa Gesi umevuja: #Tanzania kupoteza shs 1.6 trilioni kwa mwaka – #Norway kujirudishia misa…. […]

 10. Hiv kwnn viongoz wetu nawao wamegeuka kuwa wa nyonyaji kupitia wawekezaji? wafike sehemu watuone huruma,watakuja kuuza hdi kucha zetu,mh,zitto mubunge wangu wa ukweli,pambana na hao walafi. asante

  jackson kibabi

  July 7, 2014 at 4:16 PM

 11. Mpaka nimechoka! Nasubiri majibu ya dharau na kejeli kwa viongozi wetu wasio na uchungu na nchi yao! MUNGU IBARHKI TZ!

  Masunga Martine

  July 7, 2014 at 4:31 PM

 12. kwakweli mm na amini viongozi wa inchi hii hawana akili mm nikajua sasa tanzania umasikini tunauaga kumbe tuna ukalibisha jamani kweli kabisa viongozi wanashindwa kuona jicho la masiki hawa alio jawa na matatizo lukuki njaa elim magonjwa nk ilavwana jali kushibisha matumbo yaoo kwakweli mm naumia na nina lia kuona utajili wetu.una wafaidisha wengine watanzania wenzangu tuu ngane kuondoa huu ujinga na upumbavu uliopo kwa hawa viongozi wasiona uluma na inchi yao daa eeemalo najuta kwa nn nili zaliwa katika inchi hii ya watu wasio na huluma wala msaaada

  paul ndasi

  July 7, 2014 at 10:59 PM

 13. ni us***** tokea rais mpaka mawazir na wabunge vilaza. ku****** zenu

  victor mahela

  July 8, 2014 at 12:09 PM

 14. Suala la ukosefu wa uadilifu wa viongozi wengi wa Tanzania haliitaji hata elimu ya elementary school kutambua.Lakini pia sisi watanzania uwezo wetu wa kufikiri umekuwa ni mdogo sana kiasi kwamba kiongozi mbadhilifu anavua shati la rangi fulani na kuvaa la rangi nyingine tunasahau ubadhilifu wake na kuendelea kumchagua.
  Cha muhimu ni kwamba “binadamu yoyote atakae acha ajiongoze lazima ataenda upogo”. Kama kweli watanzania tunaona ubadhilifu wa mali ya umma ni tatizo kwa ustawi wa nchi yetu basi tuwe na sheria ya kuwaua wanaohusika kila watakapobainika kisheria.
  Jambo hili mara nyingi limekuwa na kigugumizi kwa watu wengi wakiwemo wanaharakati ambao akili zimejifunga bila kuangalia cost-benefit ya tatizo.Hivi mmewahi kufikiri ni watanzania wangapi huku majita,ileje au kamara usifikirie kupata huduma za maji,matibabu,barabara hata hizo za vumbi,elimu nk lakini hata chakula hawana wanakufa kwa njaa.
  Bila kujali kwa makusudi kabisa, watu ambao bado uchumi wao ni mzuri watoto wao wanasoma ulaya,chakula,maji safi na salama,magari yenye AC ambavyo kama haitoshi vinatokana na kodi ya mwanachi huyo ambae hata chakula kwake ni mtihani lakini watu wanaendelea kuwanyonya?.
  Brothers what should we tanzania suffering from axtreme povert pay this kind of a person if not death?Come on if you are actually serious brothers

  Bakari Mugini

  July 8, 2014 at 3:29 PM

 15. Mh zitto unajua uozo wa viongoz wa nchi hii.,sasa unachukua hatua gani kuuelimisha umma kuhusu haya masuala mazito kabisa yenye maslahi kwa nchi watu ambao hawana hats redio ya kusikiliza na wanaoishi kwenye umaskini wa kutupwa

  mazengo

  July 9, 2014 at 3:11 PM

 16. kipindi cha nyuma wakati wa buzwagi ulitusaidia sana kupiga kelele,japo hatujui sana nini kiliendelea katika mikaba ya madini ikiwapo buzwagi na tume uliyochaguliwa kuwa ndani yake,ni vipi basi ukitusaidia kuwasilisha hoja binafsi bungeni kutunusutu kama taifa

  Disney

  August 6, 2014 at 6:13 PM

 17. ukoloni mamboleo ndo kikwazo kikubwa sana katika kutokomeza umaskini.

  ALPHA MPUMILWA

  September 6, 2014 at 8:57 AM

 18. Hey Zitto we ndo mzalendo wa kweli panda majukwaani elimisha jamii juu ya mikataba hii ili tupambane na huu unyonyaji.

  ALPHA MPUMILWA

  September 6, 2014 at 9:03 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: