Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Pembejeo za ruzuku: Bomba la ubadhirifu

with 6 comments

Mkulima wa mahindi anayelima hekta moja anahitaji mbegu na mbolea za kupandia na kukuzia zenye thamani ya tshs 220,000. Kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa chakula nchini Serikali iliamua kuanzisha mfumo wa kutoa ruzuku ya pembejeo kwa wakulima wa hali ya chini. Kwa mfumo huu serikali hulipia tshs 140,000 kupitia vocha anazopewa mkulima na kuziwasilisha kwa mawakala wa mbolea na mbegu. Hivyo mkulima hulipia tshs 80,000 tu.

Serikali kupitia wizara ya kilimo na chakula hutengeneza Vocha hizo na kuzigawa mikoani ambapo napo huzigawa wilayani kisha vijijini. Serikali ya Kijiji kupitia mkutano Mkuu wa kijiji huteua wafaidika wa mfumo huu na kuwapa Vocha. Wao hupeleka Vocha hizi kwa mawakala wa pembejeo, wanalipa fedha ya juu na kupewa mbolea na mbegu. Mawakala hupeleka fedha hizi Benki ya NMB ambayo huwalipa mawakala fedha ya thamani ya Vocha. Wizara ya Fedha nayo huilipa NMB ambayo hutoa huduma hii kwa riba ya 4%. Mwaka 2012/13 jumla ya wakulima   2m walifikiwa kwa mujibu wa taarifa ya Serikali. Kwa ujumla toka mwaka 2008/09 mpaka 2013/14 Serikali imetumia jumla ya tshs 574 bilioni katika mradi huu. Sehemu ya fedha hizi ni mkopo wa benki ya Dunia wa dola 160m.

Habari hii ikiishia hapa ni habari Njema sana na yenye malengo mazuri kabisa ya kujenga uwezo wa wananchi kwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na kuondoa umasikini nchini. Wastani wa tshs 93 bilioni kwenda kwa wananchi wa vijijini ni mfumo bora kabisa wa dola kujengea uwezo wananchi wake. Hata hivyo jambo jema limegeuka moja ya skandali kubwa sana katika historia ya nchi yetu.
Kwanza mradi umegubikwa na changamoto zisizokwisha za uteuzi mbovu wa mawakala wa pembejeo, uteuzi mbovu na wa upendeleo wa wafaidika wa mradi, ucheleweshaji mkubwa wa pembejeo kufika na wakati mwingine kufika wakati msimu wa kupanda umepita na mwisho wananchi kupewa mbolea bandia na hata mbegu zenye ubora hafifu.

Pili, mfumo mzima umegundulika ni wa kifisadi ambapo orodha ya wafaidika huchakachuliwa kiasi cha kuweka hata watu waliokufa kwamba wamepokea mbolea. Kamati ya Bunge ya PAC katika kikao chake na wizara ya kilimo na mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali tarehe 28 January 2014, iliambiwa kuwa baadhi ya maeneo nchini mawakala walikuwa wananunua Vocha kutoka kwa wakulima kwa tshs 10,000. Katika jimbo la uchaguzi la kigoma kaskazini mawakala walinunua Vocha hata kwa shs 2000 na wao kwenda kulipwa tshs 140,000 huko benki kana kwamba waliuza mbolea ile kwa wakulima.

Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia katika mkoa wa kilimanjaro mwaka 2012 uligundua kuwa asilimia 60 ya pembejeo zilichukuliwa na viongozi wa serikali za vijiji. Kiuhakika, nchi nzima viongozi wa vijiji wanatuhumiwa kuiba Vocha na kushirikiana na mawakala kujipatia fedha kwa njia za kifisadi. Inasemekana kuwa asilimia kati ya 60 na 70 ya Bajeti ya pembejeo ya ruzuku haikufikia walengwa na ilitafunwa na mtandao wa maafisa wa wizara ya kilimo, wakuu wa wilaya na makampuni ya mbolea na mawakala wa pembejeo
Kamati ya PAC imeagiza CAG kufanya uchunguzi wa kiforensiki (forensic investigation) ili kuweza kubaini wabadhirifu wa mradi huu wa mabilioni ya fedha na kuwachukulia hatua za kisheria.

Inawezekana hili nalo likapita tu……..

Advertisements

Written by zittokabwe

January 28, 2014 at 6:43 PM

Posted in Uncategorized

6 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Siamini kama uchunguzi huu utasaidia kuwafikisha pahala husika mafisadi wa mradi huu mkubwa wa kilimo kwanza.
  Nchi hii bwana ni ya wenye meno ambao wao wapo tu pale kuharibu mikakati na mipango ya kuwainua wanyonge.mpango wa kilimo kwanza kwa sasa ni wimbo tu tena ambao wanao ujua ni hao hao mafisadi.

  Zambery mome

  January 28, 2014 at 8:05 PM

 2. Hapo sawa kabisa My. Zitto. Unajua ifike mahali wananchi tuhoji mambo us msingi kama haya badala ya kushupalia matukio ya kipuuzi yanayogubika siasa ya nchi. Big up Mh Mbunge

  Albert ottaru

  January 29, 2014 at 11:43 AM

 3. kiukweli zitto ataendelea kuwa mtu mhm kwa watanzania wote.

  gasper misibo

  January 30, 2014 at 9:05 AM

 4. ..nice touch Dude!!

  Sayeed

  January 30, 2014 at 9:56 AM

 5. KAKA ZITTO NAOMBA UTUSAIDI KUCHUNGUZA HAWA WATU WALIOKUJA DAR WANAOITWA TELEX FREE, AMBAO INAONEKANA NI KAMPUNI YA UTAPELI KAMA ILIVYOKUA DECI. HAWA WATU WAMESHINDWA BRAZIL WAMEAMUA KUKIMBILIA KATIKA NCHI MASIKINI KAMA TANZANIA KUWAIBIA WATU.
  TUSAIDIE KAKA YETU.

  Ramona

  February 11, 2014 at 5:13 PM

 6. Moja ya hoja zako kuu ni kuwa hii nchi inahitaji mapInduzi.. we need to mAke reforms ambazo si kubadilisha chama.

  hussein kiyungi

  March 13, 2014 at 4:49 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: