Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI-TAMKO rasmi la Ndugu Zitto Z. KABWE (MB) kuhusiana na kinachoitwa “Taarifa ya Siri ya Chadema”

with 51 comments

                        TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO rasmi la Ndugu Zitto Z. KABWE (MB) kuhusiana na kinachoitwa “Taarifa ya Siri ya Chadema”

Ndugu Wanahabari,

NILIPOKUWA katika ziara ya bara la Ulaya kati ya Oktoba 21 mpaka Novemba 2 mwaka huu (2013), nilipokea kwa njia ya barua pepe ripoti inayoitwa “Taarifa ya Siri ya Chadema” ambayo pia ilikuwa imesambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

“Taarifa ya Chadema inasema kwamba chama hicho (chama changu) kilikuwa kimechunguza mwenendo wangu tangu mwaka 2008 hadi 2010 na kubaini kuwa mimi napokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuivuruga Chadema.

Ripoti hiyo ilinihusisha pia na mwananchi raia wa Ujerumani, Andrea Cordes ambaye, kwa mujibu wa ripoti hiyo, alinisaidia kupokea na kuhifadhi kiasi cha dola 250,000 za Marekani kupitia kwenye akaunti yake binafsi.

Taarifa hii ya kutunga na iliyojaa uongo wa kiwango cha kutisha, imenifadhaisha, kunisikitisha na kunikasirisha.

Taarifa hii iliibuliwa katika kipindi ambacho nilikuwa safarini kutetea haki za Watanzania na Waafrika ambao utajiri wao wa rasilimali unafaidiwa na watu wachache waliohifadhi mali katika nje za nje na pia kupigania makampuni ya mataifa tajiri yalipe kodi stahiki katika nchi zetu.

Pengine lengo la ripoti hiyo lilikuwa ni kutaka kunipoteza kutoka katika nia na dhamira yangu ya dhati ya kutaka Watanzania wafaidike na utajiri wao. Muda ambao watunzi wa ripoti hiyo waliamua kutoa taarifa yao unazua maswali mengi kuliko majibu.

Nafahamu kwamba mimi ni mwanasiasa ambaye nimekuwa mlengwa (target) wa mashambulizi kutoka kwa makundi mbalimbali ya wanasiasa na vikundi vyao. Kama mwanasiasa, niko tayari kupokea changamoto zozote zinazokuja na uanasiasa wangu.

Hata hivyo, ambacho sitakubali ni kwa watu kutumia jina langu na uanasiasa wangu kunichafua mimi binafsi na watu wengine wasiohusika kwa sababu ya kutaka kutimiza malengo yao ya kidhalimu.

Raia huyo wa Kijerumani tayari amekana kuhifadhi fedha zangu. Kwa maelezo yake kwa baadhi ya viongozi wa Chadema amekana kuwa na akaunti inayotajwa na amekana pia kuwepo nchini Ujerumani katika siku na wakati uliotajwa kwenye ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imemtaja pia mtu kama Dk. Charles Kimei, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ikidai kwamba nilikutana naye na alishiriki kwenye igizo hilo la kunipa fedha.

Niseme mapema kwamba tangu kuzaliwa kwangu sijawahi hata mara moja kukutana na Dk. Kimei popote pale ndani au nje ya nchi. Kumuingiza mtu ambaye amejenga jina lake kwenye taaluma ya kibenki kwa sababu tu ya lengo ovu la kumchafua Zitto Zuberi Kabwe si uungwana bali ni unyama.

Kutokana na uchafuzi huu wa wazi dhidi ya taswira yangu binafsi na watu wengine walioingizwa kwenye mkumbo huu, nimeandika rasmi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Wilbrod Slaa kumwomba athibitishe kwamba kinachoitwa Taarifa ya Siri ya Chadema ni kweli ni taarifa ya chama au kiikanushe ili niweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa hekaya hiyo.

Cha ajabu, nimepokea ujumbe wa kutishiwa maisha kutoka kwa mtu anayejiita Theo Mutahaba na kuahidiwa KUPOTEZWA endapo nitaendelea na jitihada zangu za kupambana na ufisadi na kutafuta haki kwa Watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kiitikadi, kikanda, kikabila na kidini.

Natarajia kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote ambao wamehusika na utungaji na uenezi wa taarifa hii. Nitahakikisha kwamba wahusika wanatafutwa na kufunguliwa mashitaka stahiki ya upotoshaji na kuchafuana.

Ni matarajio yangu kwamba wale wenye mapenzi mema na Tanzania, mimi binafsi na utawala wa sheria, wataelewa nia yangu ya kutafuta haki katika suala hili.

Nimeamua kujitolea maisha yangu kwa ajili ya Watanzania na kama alivyopata kusema Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela; “Struggle Is My Life.”

Forward Ever, Backward Never- Kwame Nkrumah

Zitto Kabwe (Mb)

10/11/2013

Advertisements

Written by zittokabwe

November 10, 2013 at 3:24 PM

51 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Something is very wrong…..

  Anthony Tukai

  November 10, 2013 at 3:36 PM

  • Hey, comm-red zitto, don’t get scared, for what is being written in new papers or any challenges you face we people with socialism ideology, we find the challenges you face is the victory to the mass of this land the problem you face is that you are not flying with birds of same feathers. Charity begins at Home keep up
   gery nyika

   gery nyika

   November 18, 2013 at 2:52 PM

 2. kwel kaka zito nadhan huu ndio wakati wa kuwapa watu ADABU, maana ni kashifa nzito

  shafii zubery

  November 10, 2013 at 3:49 PM

 3. Sorry for that Zito. Just take the actions basing on the facts and bring them to justice.
  You must continue with the struggle, even if for blood, for it will nourish the tree that will bare fruits of democracy.

  Godwin

  November 10, 2013 at 3:52 PM

 4. wasikutishe Kaka.Vijana tupo hatutakuangusha.Songa Mbele na hatua zichukuliwe zidi yao.Najua ni kijani kinachowasumbua.

  mortone

  November 10, 2013 at 3:58 PM

 5. Wanafanya njama ila Mwenyezi Mungu ni bingwa wa kuzifichua hizo njama. Songa mbele kwa uwezo wa Muumba tutafika tu.

  Kabamba

  November 10, 2013 at 4:20 PM

 6. binafs hili siwezi kulisemea,,nasubiri uongozi wa chadema uliweke wazi ili2one nani mchawi we2 au2jue kama ni prpaganda.
  ‘pamoja 2ijenge nchi e2’

  ambokile osward

  November 10, 2013 at 4:54 PM

 7. Tena ungempa huyo Dr slaa mda maalum wa kuithibitisha au kuikanusha hiyo taarifa

  David Fortunatus Sr

  November 10, 2013 at 4:58 PM

 8. Siasa

  david elias mabanza

  November 10, 2013 at 5:14 PM

 9. Zito Zuberi Kabwe, wewe ni mwanasiasa. Umechagua mwenyewe kuwa mwanasiasa. Siasa hasa za nchi za dunia ya tatu unazijua. Wanasiasa hawatafuti nafasi za kisiasa kwa kujinasibu jinsi walivyobora wa kutenda kazi, bali kwa kueleza ubaya wa wapinzani wao kisiasa. Mchezaji mzuri wa mpira wa miguu ni yule anayejua kucheza na kukaba adui asifunge goli. Ubaya wa wapinzani wao sio tu wenye ukweli bali hata wa kutunga. Wapo mabingwa wa kutunga uwongo hadi wamepewa cheo cha Master Mind.
  Katika kipindi cha kumtafuta mpeperusha bendera ya CCM ya nafasi ya uraisi (2005) mmoja wa wagombea aliambiwa alishiriki katika njama za kumuua Hayati Abed Karume. Mgombea huyu alifadhaika kuliko ulivyofadhaika wewe hadi akaishiwa nguvu za kuendelea kuutaka uraisi. Mpaka leo mwanasiasa huyu amenyong’onyea. Haamini kama watu wanaweza kutunga, kuaandaa na kuratibu uongo kiasi hiki. Kama tungalikuwa na wanasiasa wabunifu wa mbinu za kuleta maendeleo kama walivyo hodari kuzua uchafunzi wa majina ya watu Tanzania tung’ara kwa maeendeleo. Ni bahati mbaya fitina haijengi na wajenga fitina hawana lolote la maana kwenye kuleta maendeleo.
  Kwa bahati mbaya zaidi wazandiki hawa hufanikiwa kupitia njia hizi chafu na baadaye hugeuka kuwa mzigo kwa Taifa usiotulika kirahisi.
  Jambo la matumaini makubwa ni kuwa sasa Watanzania walio wengi wameanza kuzijua mbinu hizi chafu na wameanza kuzipuuza na kuwapuuza waanzilishi. Usifadhaike.
  CHADEMA ni chama. Ni taasisi inayoheshimika Tanzania na hata kimataifa. Kinao mfumo wake rasimi wa mawasiliano. Ili nyaraka itambulike kuwa ni ya CHADEMA ni lazima itakuwa na sifa yenye vitambulisho vya Chama ikiwa ni pamoja sahihi ya watendaji, bendera yake na nembo ya chama. Kama vitu hivyo havipo nyaraka hiyo inakosa sifa za kuwa mali ya Chama. CHADEMA haiwezi kuwajibika kwayo. Kama wewe ni mmoja wa viongozi wa CHADEMA hukupaswa kufadhaishwa nayo vinginevyo kwenye uongozi wenu hamwaminiani.Kama huwaamini viongozi wenzako unaweza kuamini propapaganda hizi, lakini kama munaaminiana unaweza kusimama kidete kuukataa upuuzi huu.
  Wanasema uchunguzi wa siri. Siamini taasisi yenye taaluma ya kiintelijesia inaweza baadaye kuandika taarifa zao kwenye mtandao wa kijamii. Uchunguzi wa siri hubaki kuwa siri isipokuwa kwa wahusika wenyewe. Kama uongozi wa juu wa CHADEMA baada kupata taarifa za mwenendo wako wa siri ilishindwa kuzifanyia kazi taarifa zao za siri badala yake wakaamua kuziweka kwenye mtandao, basi uongozi huo unapwaya. Jambo ambalo nasita kuliamini kirahisi.
  Mwisho kama mambo yanayosemwa dhidi yako ni ya uongo, huna sababu ya kufadhaika unapaswa kuimarika zaidi. Usije ukafanya kosa kama la mwanasiasa mmoja aliyesema, na mnukuu ‘Nimetafakari sana nakuona kwamba shida hapa ni UWAZIRI MKUU. Watu wameona tumchafue, tumseme vibaya kwa sababu ya uwaziri Mkuu. Nimeona kwa faida na heshima ya chama changu na serikali yangu najizulu uwaziri mkuu’
  Ukimuuliza leo hii ni faida gani chama chake kimepata baada yeye kuachia ngazi, hana majibu. Na tena leo anatamani nafasi a juu kuliko uwaziri wake mkuu alioutema kwa kukosa uvumilivu wa kisiasa. Dereva mzuri si tu yule anayejua kuendesha bali yule anayejua pia barabara anmopita. Mwanasiasa sio tu kujua kujenga hoja bali kujua mazingira ya siasa yalivyo.

  asungwile

  November 10, 2013 at 5:27 PM

  • 90% right.

   kanju hassani

   November 11, 2013 at 11:06 AM

  • Namuunga mkono Zitto kwa kila hali – kutafuta haki na kutetea hadhi na utu wake na kuheshimika. Nakubaliana sana na mawazo na hekima ya Asungwile na ushauri anaoutoa kwa Zitto. Lkn wakati mwingi sikubaliani na namna Zitto anavyoshughulikia mambo au matukio mengi yanayohusisha kutuhumiana au kutokuelewana na wenzako ndani ya CDM. Zitto anapenda vyombo vya habari, anapenda utoaji wa taarifa kwa umma, kwa vyombo vya habari. Anapenda sana publicity ya issues zilizo chini au ndani ya uwezo wake. Anapenda sana kulalamika kwa umma, may be wamuonee huruma au aonyeshe ujasiri kwa wengi. Fikra zangu zinanituma kuamini kuwa njia hii si nzuri, haimfai, haimsaidii, haimjengi. Zitto haitaji kuwasiliana na Dr Slaa kwa barua au vyombo vya habari ktk suala kama hili kabla hajakaa nae. Mambo hili haliitaji taarifa kwa umma au kiutawala waandishi wa habari, njia anayoitumia Mh Zitto ni ya ovyo, haionyeshi ukomavu. Zitto anastahili awe makini zaidi kuliko alivyo sasa. Vikao vya chama vipo, yeye kama Naibu Katibu Mkuu wa CDM, kwa haraka yeye ndo anastahili kujibu tuhuma hizo kwa niaba ya chama. Ili Dr Slaa aweze kujibu barua ya Zitto atahitaji msaada wa Naibu wake ambaye ni Zitto. Kwa akili ndogo kabisa hii inamaanisha kuwa Zitto amejiandikia barua akitaka ajijibu mwenyewe. Ni katika hili ndipo ukomavu wa CCM unapoonekana. CCM hawakurupuki kama wanavyofanya akina Zitto, ndo maana wanajiita ni watu makini. Zitto si makini. Kutoa pozi la ukimya na kujidai kuwa mwe fikra na kuongea kwa vituo hakutoshi ku kumfanya mtu awe makini. Ni kupitia ukurupukaji huu wabaya wa CDM humtega Zitto (na ndo walifanya kwa Kasusura pia) na kumnasa kwa urahisi na hivyo kutoisha ubishi kati ya Zitto na CDM. Mungu ibariki Tanzania.

   Majani Rwambali

   November 12, 2013 at 7:56 PM

 10. Safi sana kaka. Waache upumbavu. Napatwa sana na hasira na namna watu wanavyotumia vibaya watu

  Leopold Kimaro, The Managing Director, Babito Trading Co, Box 1688, Mbeya. +255 713 032222 +255 789 032222 Email;leopoldk2004@yahoo.com beacoresort@yahoo.com Babitotrading@yahoo.com

  Leopold

  November 10, 2013 at 6:07 PM

 11. Reblogged this on chescomatunda and commented:
  Taarifa ya zitto Hii utata

  chescomatunda

  November 10, 2013 at 6:18 PM

 12. kaka,mh,MB napenda kukuita kwa majina yote ili ujijue kwangu wewe ni nani ciasa za Tanzania ni chafu sana usikate tamaa Mm sisi na watanzania wap tenda haki tupo na wewe Mm nakupa pole na kumbuka mti mwema ndo hupigwa mawe

  msongamwanja

  November 10, 2013 at 6:44 PM

 13. Pole sana Mh. Zitto kwa misukosuko hii inayokupata.
  Kwanza nikutie moyo kuwa huna haja ya kufadhaika na kuvunjika moyo kuaacha kutumikia umma. KAMWE USIRUDI NYUMA na UKIRUDI nyuma utageuka ngozo ya chumvi! Tambua hizi ni njama si dhidi ya wewe bali dhidi ya CHADEMA.

  Baada ya hayo nina ushauri kwako binafsi na kwa viongozi wenzako wa CHADEMA juu ya hili na mambo mengine ambayo yamekuwa yakizungumzwa mara kwa mara:
  KWAKO WEWE:
  1. Usiishie kuzungumza na wana habari tu bali chukua hatua za kisheria kwenda mahakamani hata kama Katibu Mkuu Dr Slaa hatatoa tamko la kukanusha kwa vyombo vya habari. Kwa nini uende mahakamani? Zitto umekuwa mtuhumiwa wa mambo mengi sana lakini si kila mtanzania anao uwezo wa kupata taarifa sahihi/ za ukweli juu ya tuhuma hizo. Mara nyingi umeishia kuzungumza ktk vyombo vya habari (na kwa bahati mbaya sana vyombo vyeti vina tabia ya kutafsiri kauli za wasemaji vile waonavyo na kwa msimamo wao; sasa inategemea mwananchi anapata taarifa kupitia chanzo kipi). Wakati kesi ikiwa mahakamani acha kuizungumzia (kama unajitete) bali endelea na harakati za kututumikia

  2. Kulingana na hali ya kisiasa ya sasa, na kutokana na utendaji wako usitegemee kukosa maadui; na wengi si kwamba nia yako ni kukuchafua wewe la hasha bali kuchafua na kuangamiza chama chako. Tangu kuanza mfumo wa vyama vingi watanzania tunajua kuwa wanasiasa mnaweza kuhamia chama chovote lakini lengo la wanakuandama si kukuchafua wewe bali wewe utumike kuua CHADEMA na hata harakati za mabadiliko nchini.

  KWA VIONGOZI WA CHADEMA

  1. Iwe taarifa hii ni ya kweli au ya uongo ni wakati muafaka sasa mtoe tamko rasmi la Chama kwa umma. Kunyamaza kwenu kunajenga taswira mbovu juu yenu kwa umma. Kumekuwa na maneno mengi sana juu ya Mh. Zitto na viongozi wengine lakini mnanyamaza kana kwamba hamsikii na hamjali athari za taarifa hizo kwa umma. Ninyi mnajua kabisa kwa muda sasa kumekuwepo na taarifa za kutilia shaka mwenendo wa Mh. Zitto (mfano: kuwa Zitto anaanza harakati za kuwania uraisi wakati muda bado na ninyi mnaye mgombea; kwamba Zitto si mwenzenu kwa kuwa hashiriki/ haambatani nanyi katika mikutano ya M4C, nk. Kwamba kuna mgogoro wa viongozi, nk).
  Taarifa hizi ni ndogo sana lakini zina athari kwa Chama ambacho kimejijengea kuaminika kwa umma na hasa daima mfahamu kuwa huu ndio wakati sasa wa kujitofautisha baina ya ninyi na CCM.
  CCM wanatabia ya unafiki (hawaambiani ukweli wanabaki kuumana ndio maana leo baraza moja la mawaziri lakini kila waziri ana kauli yake juu ya suala moja).

  2. Fahamuni kuwa hata kama Zitto ana tatizo lakini mlengwa si Zitto. Mlengwa wa mashambulizi haya ni CHADEMA na Zitto anatumika kama chambo, kutokana na harakati zake. Ni rahisi kusema Zitto si CHADEMA lakini mnajua kabisa kuwa mnao wanachama na au viongozi ambao wanaathari kubwa kwa CHADEMA. Leo hii hakuna mtanzania asiyemjua Shibuda (huyu hata mlipomokea wengine tulijiuliza ni kwa sababu mnakata kuongeza viti vya ubunge? Shibuda hana thamani ya kisiasa kwa hiyo hata aongee vipi kuhusu CHADEMA hakuna wa kumwamini- hata akitoka au mkifukuza hana athari). Lakini Mh. Zitto; Mnyika, Mdee, Tundu, Wenje. Nyerere. Msigwa, Lema, hawa jambo lolote linalowahusu ni agenda kubwa. Hawa leo wakituhumiwa kwa lolote ni tuhuma ya Chama. Hawa wakitoka leo LAZIMA WATANG’OKA NA KUNDI!
  Kwa kuwa hawa (akina Zitto) sio Chama lakini wana athari kubwa katika Chama basi lazima jambo lolote linalowahusu (hasa tuhuma mbaya) zifanyiwe kazi na kutolewa taarifa sasa kwa umma

  3. Kama kuna tofauti zozote baina yenu viongozi huu ni wakati muafaka wa kuzishughulikia, na mmalize tofauti hizo kuanzia mioyoni mwenu. CHADEMA tudhihirishieni kuwa mnao uwezo wa kujenga chama na serkali yenye kuaminiana na kuaminika!

  HUWA MNASEMA CHADEMA NI CHAGUO LA MUNGU, HIVYO KAMA CHAGUO BASI MNAPASWA KUSIMAMA KAMA KUSUDI LA WITO WENU. Baada ya Kikwete kuvunja moyo watanzania tunapaswa kupata tiba (KUPITIA CHADEMA) na kama kuna kuvunjika moyo mara ya pili; basi anayeweza kutuvunja ni CHADEMA (kama atatenda kinyume)

  Lugano, E

  Edna J. Lugano

  November 10, 2013 at 7:54 PM

 14. Zitto we Songa Mbele,Mtu yeyote Makini Anajua Unachofanya ,we no Mwanasiasa Makini Kuliko wao , Achaea na Hekaya zao Za Abunuwasi we chapa kazi ,kwa Mtu yeyote Anayefikiri vizuri hizo ni Habari Za Kutunga Za Hao wanaowadanganya kina Slaa eti ni Usalama wa Taifa,Usalama Gani atakupa Fedha halafu tena Akiri kwenye Mtandao Ndio haya KONTENA LA KURA ZA WIZI TUNDUMA

  Joseph Lugakingira

  November 10, 2013 at 8:16 PM

 15. pole sana mh kwa magumu unayopambana nayo.

  LULONGA JOSHUA

  November 11, 2013 at 1:26 AM

 16. Ubarikiwe kaka kwa majib mazuri kwan taarifa ile imewakwaza na kuwakatisha tama watanzania waliowengi waliokuwa wakiamini kuwa CHADEMA ndo tumaini pekee ktk ukombozi wa pili wa taifa hili na miongoni mwa watu watakaokumbukwa na historia katika harakati hizi ni wewe Mh. zitto Kabwe Zuberi. USIKATE TAMAA KAMWE KIONGOZI NA HATIMAYE UFANIKIWE.

  *MAO ANDREW BERNARD (BENNY MAO)* *bennymmao@gmail.com/ bennymmao@yahoo.com * *0783-459190, 0655-459190,0765-340687* *S.L.P 42,MBULU-MANYARA TANZANIA*

  – M/KITI WA BAVICHA MKOA WA MANYARA – M/KITI WA BAVICHA WILAYA YA MBULU – MJUMBE WA KAMATI TENDAJI YA BAVICHA TAIFA

  Benny Mao

  November 11, 2013 at 2:48 AM

 17. Pole sana Mh. Zitto. kwa tuhuma hizo. Ushauri wangu ni kama waliokwisha uandika Ndg. E. Lugano na Asungwile katika thread zilizotangulia hivyo sioni kama ni busara kurudia kile ambacho wenzangu wameshakushauri. Labda tu niseme mh. Zitto, watanzania wengi (kama sio wote) wanakufahamu na wanajua mchango wako kwa taifa letu tulipendalo la Tanzania. Pia hakuna asiyejua kuwa nyota yako katika siasa inang’aa na ianzidi kung’aa kial siku kutonana na jinsi unavyowapigania wanyonge na maslahi ya taifa letu kwetu ujumla. Hata hivyo unajua (au unapaswa kujua) kwamba penye mafanikio hapakosi vikwazo. Inawezekana kabisa unafanyiwa mizengwe ili wanaokuchukia wakuharibie wewe mustakabali wako kisiasa. Pia inawezekana kinachofanyika ni propaganda za wanaokichukia chama chako cha CHADEMA-chama ambacho wewe umechangia na unazidi kuchangia pakubwa katika kufikia heshima na umaarufu kilichonao leo hii- ili wakiangamize. Yote hayo hayo yanawezekana. Kama ambavyo LUGANO na ASUNGWILE wamekushauri, hakuna sababu ya wewe kuwa na hofu au mfadhaiko endapo unafahamu shahiri dhahiri kuwa story hiyo ni ya kuundwa, ni dhahiri kwamba wanataka kukuchafulia wewe au chama chako.

  Mwanaharakati mkongwe Mzee Mahatma Gandhi aliwahi kusema, na hapa namnukuu katika lugha ya kiingereza kwamba, “Many people, especially ignorant people want to punish you for speaking the truth, for being correct, for being you. Never apologize for being correct, or for being years ahead of your time. If you are right and you know it, speak your mind. Even if you are a minority, of one, the truth is still the truth”
  Kwa hiyo mh. Zitto wala usifadhaishwe na tuhuma hizo. Wewe nenda mahakamani ili haki itendeke.

  Mwisho, Zingatia ushauri wa hao ndg wawili ili usijechukua uamzi kama uliowahi kuchukuliwa na mmoja wa viongozi wakubwa katika nchi hii alipoamua kuijiuzuru eti kwa maslahi ya chama au serikali yake.

  richard

  November 11, 2013 at 10:02 AM

 18. Mheshimiwa we simama kwenye haki na Mungu atakusimamia tu usiangalie mwanadamu anasema nini bali angalia mungu anasema au ufanye nini! UBARIKIWE.

  Frank E.Mahembo

  November 11, 2013 at 12:04 PM

 19. Good decision is to hold it and continue with journey. Remember that people are not the same, and simple solution to reach compromise is u should decide not to decide.

  Priscus Fulgence

  November 11, 2013 at 8:38 PM

 20. Good decision is to hold it and continue with journey. Remember that people are not the same, and simple solution to reach a compromise u should decide not to decide.

  Priscus Fulgence

  November 11, 2013 at 8:44 PM

 21. Pole sana kijana wetu tunaithamini kazi unayoifanya na pamoja kwamba wengine hawawezi kufurahia wewe usirudi nyuma. Mbele ya macho yao wewe ni mbaya lakini mbele za MUNGU (muumba wa vyote pamoja na hao) wewe ni wa thamani kubwa na anapendezwa na anayetetea wanyonge, yatima, wajane, maskini, N.k. Wakumbuke MUNGU amekalia kiti chake cha ENZI na.anaona haya yote na hawana uwezo wa kujificha na zaidi ya yote hapokei rushwa

  Brighton Kalinga

  November 11, 2013 at 9:40 PM

 22. kamanda nakukubali sana usirudi nyuma na harakati zako hakuna kama wewe kiongozi imara usihame chama the strongest man is the one who stand alone you are not alone buddy.

  nehemia

  November 11, 2013 at 10:06 PM

 23. vumilia.kama utaachia ngazi utakuwa wewe ni kiongozi dhaifu, sifa zako zote zitaishia kwenye makabati ya bunge.

  bakari

  November 12, 2013 at 8:33 AM

 24. Pole u have to wash ur self not to wait for Dr slaa,umechafuka, our friend

  beda

  November 12, 2013 at 8:05 PM

  • Mh, kwanini wewetu isiwe kwa wengine hizi lawama? mimi napenda sana hoja zako na naamini hata.wengine wanapenda lakini mpaka sasa wewe unaonekana cheo cha Ubunge kimekuchosha na unaonekana kutamani cheo cha juu is ok good vision lakini umri wako.bado dhamana ya Urais, l remember the.speech of Mh, Jannuari Makamba he said when the time is ok l wil do, which means he will use his time to convise the nec member of ccm as

   well as the societies .If you still like apolitics issues lam advise.you that you are suppose to be clean and
   politely items of challenges of
   politics matters just like Mh, Samuel
   Sita . upuka makundi, upuka
   vishawishi, upuka Fedha, la mwisho Heshimu Viongozi wa juu yako. huoni
   ccm wanavyoheshimiana na kupeana uongozi kwa utaratibu subira ya vuta heri l like u na natamani kuendelea kukuoma ukiperform zaidi katika ulingo wa Kisiasa

   paul Masunzu

   November 14, 2013 at 12:16 PM

 25. pole. sasa kaka,usirudi nyuma kuwatetea wanyonge. Hao ni mafisadi wanaotaka kukunyong’onyesha

  godfrey masilamba

  November 14, 2013 at 6:42 AM

 26. Mh.piga kazi tuko nyuma yako

  Felix Mwalitegete

  November 14, 2013 at 11:57 AM

 27. Taifa linajengwa na wenye moyo wa kujitolea maisha yao.(A GRAIN HAS TO DIE IN ORDER TO PRODUCE NEW GENERATION) Songa mbele kaka tuko nyuma yako!

  DEUS S

  November 14, 2013 at 4:43 PM

 28. Siasa! neno siasa kwa watu wengi wanadhani ni kupiga domo saaana hadi mate yakauke! hawadhani kabisa kama ni kitu cha kuikomboa jamii na kuiletea maendeleo na zaidi ya yote wanadhani mwanasiasa ni mtu wa kuganga njaa tu! na hii inatokana na wanasiasa wengi kupenda kumalizia matatizo yao
  kwenye nyadhifa za kisiasa. Mbayazaidi hata wananchi wa kawaida wanadhani
  mwanasiasa anaweza kumaliza matatizo yao kwa kumuomba vijisenti!
  na mwanasiasa nae anaona asipogawa vijisenti basi watamuona wa nini uchaguzi ukifika. TABIA MBAYA SANA
  HII. Na ni kusosa elimu tu ya uraia. Ndio maana maneno haya ya ZITO KUHONGWA yameanza kushika kasi.
  huu ni uroho tu wa madaraka wa baadhi ya wanasiasa wanaodhani siasa ni mbeleko ya kumaliza matatizo yao! Binafsi naichukia sana siasa chafu ya kumtia mtu maneno ya kichochezi awachukie wengine ili wewe upate.
  Tujifunze kutoka kwa wenzetu Misri na
  Libya watu walichochewa kwa maneno ya chuki wakajaa sumu wakawaondoa waliodhani ni wachafu na mwisho wa siku waliokuja wakaonekana sio tu ni wachafu bali ni takataka! tuache siasa za kichochezi tujenge hoja na mwenye kisu kikali atakula nyama!
  pole sana bwana zito mi ni mwana
  CCM ila siku ukigombea uraisi wa Tz au ukiwa mwenyekiti wa chadema nitahamia chadema maana nimekuwa nafuatilia na kubaini kuwa unaijua siasa hasa ya kumwaga sera na naamini wewe ni kiongozi makini huna jazba wala huoneshi dalili ya visasi

  MUNGU AKUTANGULIE TUKO PAMOJA DAIMA KWENDA MBELE KWENYE MAANA HALISI YA SIASA

  milambo

  November 14, 2013 at 10:46 PM

  • You know kaka zitto, people normally do not want the TRUTH,and therefore once they hear that somebody is speculating to get truth,they try to set some restrictions or obstacles to make sure that the one who is looking for the truth does not succeed. REMEMBER KAKA KABWE, IN ANY KIND OF STRUGGLE FEWER MUST SUFFER TO SERVE THE MAGNITUDE,IT IS RARELY THE MAGNITUDE TO BE ILL-TREATED FOR THE SA KE OF BRINGING HOPE TO FEWER. “IT CAN BE DONE PLAY YOUR PART”.MAY THE ALMIGHT PRECEED YOU IN YOUR STRUGGLE. WISHING YOU ALL THE GREAT.

   TOPEN TENZA

   November 15, 2013 at 4:00 PM

 29. Zitto,
  Je, hao walosambaza au kuandika huo waraka au hao unaofikiria kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa kusambaza au kuanika huo waraka, ni wanahusika katika mfumo wa mawasiliano ya chama chenu? umesema umemwandikia Katibu mkuu wa chama chako afafanue kama huo ndo msimamo wa chama chenu au la, Je, ndo aleandika au kusambaza huo waraka? kuna ugumu gani kuwalazimisha hao waloandika kukana walichoandika vinginevyo uwachukulie hatua za kisheria bila kuanza kulazimisha mtendaji wa chama chako(ambvaye kwa upande mwingine ni wewe mwenyewe) akubali au akanushe? Ki-utendaji wewe ni msaidizi wa Slaa (naibu katibu mkuu) ikimaanisha katibu mkuu anapokuwa hayupo ofisini wewe ndo mtendaji wa kazi zake, fafanua itakapotokea Slaa kasafiri halafu deadline ya hiyo barua uloandika inakaribia kufika nawe upo ofisini (kwa kuwa wewe ndiye mtendaji mkuu kwa wakti huo) utaandika nini kuijibu hiyo barua?
  Huoni kama barua ulomuandikia mtendaji wa chama chako inasambaratisha uwajibikaji wa pamoja katika chama chenu. Kama mmeshindwa kuendesha team work katika mazingira ambayo mu-watendaji wa taasisi yenu. Kama hiyo taasisi ndogo isiyofikia hata theluthi moja ya taasisi za Jamhuri ya muungano wa Tanzania inakushinda kuisimamia wewe kama mtendaji, utawezaje kusimamia taasisi zenye kusigana katika serikali hasa katika kipindi hiki cha mpito wa kutoka ujamaa kwenda upepari?
  THERE ARE TOO MUCH VOIDS IN ALL PUBLIC CORRESPONDENCES RELATED TO WHAT CLAIMED TO CONFIDENTIAL REPORT. Inatia wasiwasi juu ya weledi wetu (Watanzania)

  Roberto

  November 16, 2013 at 1:23 PM

 30. Ndugu achana na siasa za Bongo kuwa na kifua kipana.Kuwa mfano wa mtu aliye aliyemkumbatia nungunungu kwa uvumilivu kwa miaka minne.Wakati mwingine hizo taarifa zaweza kuwa zimeghushiwa na maadui zenu kisiasa.Kuweni makin kwan imeshaonekana 2015 suluhisho ni Chadema na chadema ndio ninyi.Msituchanganye

  Nyamhanga james

  November 16, 2013 at 10:00 PM

 31. my role modal in politics of tz is ZZK but the problem is………………………………………..

  qzedon

  November 18, 2013 at 1:51 AM

 32. Rais wa africa ya kusini mstaafu nelson mandela aliwahi kusema hii nchi yoyote ile itakapoamua kudai uhuru wake yenyewe au kutaka kujitawala itapitia mambo magumu ikiwemo unyanywasaji,kuonewa na kutishiwa maisha na kuteswa pia mimi naamini mh zitto kabwe ni mwanaharakati mpambanaji na mtetezi wa sisi wanyonge wa tanzania tunaoishi kwa kipato chini ya dola moja na hii yote ni kutaka kumchafua zittokatika harakati zake za kuwania urais 2015 kwani alitangaza nia na naamini ndio best contestant wa urais 2015 kupitia chadema,kaka tupo pamoja na wewe sisis vijana tunaotambua maana ya ukombozi ” Ni bora kufa kishujaa kuliko kuishi kwa fedheha” Viva mh zitto kabwe and hoe gaat het? Daima mbele nyuma mwiko

  deniswood

  November 19, 2013 at 9:02 AM

 33. pole kiongozi,hiyo ni safari ya kuiendea 2015,uwe na maamuzi magumu yenye busara, maana ukila na kipofu usimguse mkono,na mti wenye matunda matamu ndo unaopigwa mawe,AMUA SAHIHI.

  jumanne kulwa

  November 22, 2013 at 11:00 AM

 34. Zito waambie hao wanajishauwa tu, wanatafuta jina

  Doddi

  November 22, 2013 at 4:51 PM

  • CHADEMA majungu hayajengi chamsingi kuweni wakeli muueleweshe umma maana mtapoteza uaminifu wenu kwa umma.

   kapoli

   November 23, 2013 at 9:57 PM

 35. Kaka kaza buti tu, siasa ni kama maisha,yana milina na mabonde. So we be together

  Juma

  November 23, 2013 at 5:41 PM

 36. kwani zitto kafukuzwa uanachama? au kapewa muda kujieleza?na ikithibitika sio kweli anarudishiwa vyeo vyake.

  cedrick

  November 24, 2013 at 5:19 PM

 37. Tunataka demokrasia ya kweli katika upeo wake. Kanuni, taratibu na sheria viheshimiwe na kila kiongozi. Sitarajii Kamati Kuu iendelee kuukataa ukweli kuhusu Zito Kabwe; kama ni hivyo,yenyewe ndiyo mzigo kwa Chama.

  Bushishi

  November 25, 2013 at 10:13 AM

 38. mimi ni mwanachama wa Chadema tawi la shirati Rorya,nimehuzunika sana kwa mwanaharakati wa watu wanyonge mh ZITTO ZUBERI KABWE kuvuliwa madaraka ndan ya chama cha CHADEMA hili jambo limeniuma sana na ni sehemu ya kukipoteza chama chetu cha kutetea wananchi wanyonge ila si mbaya kama huo ni ukwel wa ripoti ya chama na imefanyanyiwa uchunguz wa kina basi sawa na iwe hivyo ila laah sivyo tutapambana na hao wakabaji na wanaotaka kumuangamiza mwanaharakati wetu ZITTO KABWE

  mathew

  November 25, 2013 at 12:10 PM

 39. Politics in Africa is nowdays a dirty game,it need time/creativity and patience.So lets play the LORD

  DANIEL NSULWA

  December 3, 2013 at 3:01 PM

 40. mimi nadhani tunahitaji muda wote kujiuliza tumekosea wapi.

  revokatus rweikiza

  January 10, 2014 at 3:57 AM

 41. pole zitto kabwe tupo nyuma yako.

  bishanga

  February 5, 2015 at 6:55 PM

 42. Reblogged this on rukajuu.

  rutarakajagi

  March 20, 2015 at 10:06 PM

 43. siku zote mti wenye matunda ndo unapigwa mawe mi naic mh.zitto kila mtanzania anatambua mchango wako na tupo tyr kukulinda

  yasin gahoile

  April 8, 2015 at 9:18 AM

 44. Zitto Una Moyo Wa Ajabu, Unaruka Faida Yako Binafsi Kupigania Faida Ya Wengi!

  ntakiluta

  July 30, 2015 at 3:30 PM

 45. Reblogged this on Ntakilutandato's Blog.

  ntakiluta

  July 31, 2015 at 5:38 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: