Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Siku ya 5 ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi-Jimbo la Igalula, Wilaya ya Uyui

with one comment

Siku ya 5 ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetufikisha Jimbo la Igalula, wilaya ya Uyui. Tumekutana na wananchi katika vijiji vya Goweko, Loya, Miswaki, Miyenze na Kigwa.

Tumezungumza kuhusu changamoto ya usafiri wa Reli, wafugaji kunyanyaswa na watendaji wa kata na askari kwa kunyanganywa mifugo, zao la Tumbaku, maji safi na salama na suala la jumla la Katiba na mchakato wa kuandika katiba.

Kimsingi shughuli za kiuchumi za wananchi ni kubwa na hasa Kilimo na mifugo. Hata hivyo ukosefu wa miundombinu unafanya wananchi wasipate thamani ya mazao yao na jasho la kazi zao.

Nilipofika Kijiji cha Loya nimeona eneo kubwa lina miti ya mihama. Wananchi wanatumia tu mihama wakati wa njaa na mara nyingi matunda haya yanaharibika tu. Lazima matunda haya yana matumizi yake ya kiviwanda maana ‘kernel’ yake ina mafuta. Nani anajua matumizi ya Mihama?

This slideshow requires JavaScript.

Written by zittokabwe

October 10, 2013 at 9:37 AM

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Mh Zito kwanza kabisa nakupongeza kwa kufika UYUI kwani maeneo ya GOWEKO,LOYA nimaeneo yenye neema ambayo yamesaulika sana, nami ni mzaliwa wa KIJIJI CHA MALONGWE MALONGWE kijiji cha kina ASALI nyingi sana, pia mbao ambazo ndiyo utajili wa hapo sasa nani atasimamia hapo,TUSAIDIYE KUTAGAZA HIZO FRUSA

    GERALD MANENO MWANZIA

    October 10, 2013 at 11:50 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: