Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Siku ya Pili: Mpanda ndogo, Kapalamsenga, Karema na Ikola-Mpanda Vijijini

with 3 comments

Jana nilikuwa Jimbo na Mpanda Vijijini ambapo nimetembelea kata za Mpanda ndogo, Kapalamsenga, Karema na Ikola. Nimefanya jumla ya mikutano 6.

Nimezungumza kuhusu Katiba kuwapa nguvu wananchi dhidi ya wanasiasa ikiwemo nguvu ya kuwang’oa wabunge (recall) wanaposhindwa kufanya kazi au kuwa na makosa makubwa ya kimaadili.

Katika mikutano yote nimeambiwa na wananchi kuwa mbolea ya ruzuku ni changamoto kubwa maana inafika baada ya wao kuwa wameshapanda mahindi na hivyo ikifika inakuwa ni upotevu tu. Nimewaambia kuwa mfumo mzima wa mbolea ni mfumo wa kifisadi na suluhisho ni kuachana na mfumo huo na badala yake Serikali iweke utaratibu wa mbolea kuuzwa kwa bei nafuu ikiwemo kujenga viwanda vya mbolea nchini na kupunguza gharama za uzalishaji.

Niliwaambia kila mwaka Bunge linatenga tshs 120 bilioni za mbolea ya ruzuku lakini sehemu kubwa ya fedha inaibwa katika mfumo wa kifisadi.

Kwa uchungu tumezungumza kuhusu hali ya maisha ya watu wa vijijini. Gharama za ujenzi vijijini ni kubwa sana kuliko mijini kutokana na miundombinu mibovu na kutokuwa na sera maalumu ya kusaidia waishio vijijini.

Nimewataka wananchi waungane mkono na CHADEMA ili kuleta mabadiliko nchini na kuhakikisha kilimo kinapewa mkazo na mwananchi wa kijijini anapata umuhimu unaostahili.

Leo tutakuwa Mpanda Mjini ambapo tutafungua matawi ya chama kwenye kata mbalimbali na mkutano mkubwa wa hadhara viwanja vya Kashaulili

PICHA

Advertisements

Written by zittokabwe

October 7, 2013 at 11:19 AM

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Hongera kwa kazi nzuri kaka Zitto na makamanda wote wanaoendelea na kazi za ujenzi wa chama. Nawaomba wananchi muiamini CHADEMA ili iwape utumishi uliotukuka.

  Mutta

  October 7, 2013 at 7:29 PM

 2. Hongera sana kaka kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya,tunaamini UKOMBOZI Juu yenu….nice day

  Tito Mwakipesile

  October 8, 2013 at 9:37 AM

 3. Jambo zuri kiongozi. BADO LINDI NA MTWARA. karibu Nachingwea.

  Mwl. Sande

  October 8, 2013 at 12:34 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: