Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Mhamiaji Haramu? #WahamiajiHaramu cc @hrw @refugees @amensty

with 5 comments

This old man lives in Kigoma with documents from UN as a refugee. The govt denies that it doesn’t deport such people. This is an evidence of a person dumped at DR Congo Embassy in Kigoma. Interestingly during elections CCM gives membership cards to refugees to vote for them as evidenced here.

For how long will Tanzania lives in state of denial?

 

Familia moja kwa wazazi wote 2 haiwezi kuwa na baadhi wahamiaji haramu na baadhi Watanzania. Lakini kutokana na kukamata watu hovyo kunakofanywa na Askari wa Polisi, Uhamiaji na JWTZ huko Kigoma inawezekana.

 

Mzee huyu alikamatwa akitoka porini kuchimba dawa. Amekamatwa na familia yake nzima. Alihukumiwa ni mhamiaji haramu hata kabla ya kuhojiwa. Kosa lake? Mmanyema. Askari wakikumata ukasema wewe ni Mmanyema au Mbembe unaitwa mkongo. Ukisema wewe Muha unaitwa Mrundi. Operesheni ya wahamiaji haramu itaacha mtu Kigoma?

 

Mama huyu kakamatwa kama mhamiaji haramu na kupelekwa Ubalozi mdogo wa DR Congo uliopo Manispaa ya Kigoma. Amezaliwa Tanzania, amesomea Tanzania, Baba yake Mtanzania, Babu yake Mtanzania na Ndugu zake wengine Watanzania na hawakukamatwa. Amekamatwa akitoka kuchota maji ziwani Tanganyika. Malalamiko yake nimeyafikisha kwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Written by zittokabwe

September 16, 2013 at 11:16 AM

5 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Ndo maana nasema kila siku kuwa watu wanatakiwa kubadilika.wajue kuwa upinzani si vita bali chama cha kuzaliwa kikiwepo kinakuwa kimekusoma ukasomeka na baadaye kinakubadili kama tarakimu kwenye computer.Tubadilike tuweke Nguvu ya Umma

  mortone

  September 16, 2013 at 6:02 PM

 2. Yanayojiri Kigoma nashindwa hata kusimulia na roho inauma sana, ni sawa na kisa cha mwanachui na mwanakondoo ambapo chui aliamua kumla mwanakondoo eti kwa vile kondoo mama alimtukana chui. Nimesikitishwa na kisa cha mtu kukamatwa eti kwa vile kaka yake anayesadikiwa kuoa murundi haonekani na huyo mkewe murundi, mpaka sasa jamaa bado yuko huko kisa tu kaka yake katoroka. Huyu aliyekamatwa kwa vile Kaka yake katoroka ni mtu mzima na ana watoto wakubwa sana.

  Baba yao na hawa vijana ni marehemu sasa tangu mwaka jana lakini nakumbuka Marehemu Baba yangu akinisimulia kuwa walikuwa wanapishana miaka miwili tu kuwa Baba yao na hawa alizaliwa mwaka 1922 na Baba yangu 1924 na wote wamezaliwa hapo Manyovu-Buhigwe(Kasulu)Kigoma, leo hii baada ya miaka 91 tangu Baba yao azaliwe watoto wanaambiwa wao ni wakimbizi na si raia, isitoshe Huyo Baba yao aliyezaliwa mwaka 1922 naye alikuwa na Baba ambaye ni Babu wa watoto hawa na walizaliwa kabla ya 1900 na walizaliwa na kukulia hapo leo vitukuu kama si wajukuu wanaambiwa si raia. Wanaoambiwa hivi ni wale walioajiliwa na jamhuri na kwa sababu wao wameajiliwa basi wao ni raia. Nahisi hata yule jamaa anaye sadikika kutoroka kutoka jeshini huenda naye kumbe ni raia kwa vile yeye aliajiliwa na Jamhuri.

  Mwingine kapigwa sana kisa tu kawaambia wenye nchi kuwa na wao hawawezi kuthibitisha uraia wao, kwa vile wao wameajiliwa na jamhuri basi wao ni raia eti jamani, visa ni vingi vingine ni vigumu kuvisema kwa vile havina ushahidi kama vile rushwa. Masai, mjaruo,mnyasa na mkurya ambao wote wanapatikana nchini jirani wao ni raia eti. Hivi Kigoma itapata uhuru lini?

  Silas

  September 17, 2013 at 7:56 AM

 3. Hii operation inafanyika sehemu za mipakani ambako ni kweli kuna whamiaji japo si wote ni haramu, bali wengine na walio wengi wanajikuta wanaitwa ni haramu kwa kuwa tu hawawezi kumudu rushwa inayotolewa kwa hao watekelezaji wa operation. Lakini pia inafanyika maeneo ambako CCM imekataliwa na wananchi, hapana shaka huu ni mkakati kuelekea 2015 kwenye uchaguzi, kwa hiyo inaweza kuwa ni namna ya kupunguza nguvu ya umma ulio ikataa CCM. Mbona Dar imejaa wahamiaji haramu na hatusikii lolote?. kuna wageni haramu wengi sana wa kutoka nchi za Uarabuni, Asia na mashariki ya mbali, wengi sana kuliko hata walioko katika sehemu za mipakani, na wengi ni waioletwa na matajiri ambao ni hao wafadhili wa CCM. Wako wengi sana wameweka makazi yao katika viwanda wanakofanyia kazi au mjaumbani mwa matajiri waliowaleta. Kuna haja ya kuangalia upya tafsiri ya hiyo operation.

  Zephaniah Nyambele

  September 17, 2013 at 11:01 AM

 4. Ki ukweli hakuna mtu anae pinga hii operation Kimbunga ya kuwabaini wahamiaji haramu isifanyike,
  Mimi nafikiri maafisa husika wa operation hii hawatumii njia nzuri ya kuwabaini wahamiaji haramu
  Ukisema mbembe,mmanyema,m`bwari wanasema hawa ndio tunawatafuta ili warudi kwao DR congo,Ukisema Muha wanadai mrundi na wao warejee kwao Burundi,swali kwa Raisi,Waziri wa mambo ya ndani na maafisa usalama kama makabila hayo ni wageni nani mwenyeji wa mkoa wa kigoma?
  Rushwa imetawala katika zoezi hili hivi TAKUKURU mkoa wa Kigoma wanafanya kazi gani?
  Haki lazima ifuatwe
  Watu wanakamatwa wakiwa njiani na kupelekwa sehemu wanapowahojiwa huku wakiwa wamevikwa mabango yaliyo andikwa MUHAMIAJI HARAMU,tayari kwa kupelekwa nchi husika.Inasikitisha sana baadhi ya watanzania kuvikwa mabango na baadae kuachiwa.

  Juma Songoro

  September 20, 2013 at 10:59 PM

 5. Poleni sana waTanzani wenzetu wa Kigoma mliosumbuliwa kwa namna moja ama nyingine kwa operesheni ya kukurupuka ya chama kilichopo madarakani poleni sana tena sana!

  Mussa

  September 23, 2013 at 5:53 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: