Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Obama: Uwazi wa Mikataba, Lumumba

with 5 comments

Rais Barack Obama

Rais Barack Obama

Hatimaye Barack Obama, Rais wa Marekani anatembelea tena bara la Afrika. Hii itakuwa ni mara ya pili Obama kutembelea Bara hili alikotoka baba yake baada ya ziara yake ya kwanza mwaka 2009. Mwaka huo alitembelea Ghana na Misri ilhali mwaka huu anatembelea Senegali, Afrika Kusini na Tanzania. Ziara hiyo itakayoanza tarehe 26 mwezi Juni, itamfikisha Tanzania tarehe 1 Julai na kuondoka siku ya pili yake.

Uchaguzi wa Obama kuwa Rais wa Marekani ulipokolewa kwa shangwe Afrika nzima. Wakati Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria alilia kwa furaha, nchi ya Kenya ilitangaza siku ya mapumziko na Rais wa zamani wa Afrika Kusini ndugu Nelson ‘Madiba’ Mandela alisema ‘ushindi wa Obama unawafanya Waafrika wathubutu kuota ndoto (Jarida la The Economist). Hapa Tanzania kulikuwa kuna shamra shamra za kila namna na magazeti yaliweka vichwa vya habari kana kwamba ni Rais wa Tanzania aliyechaguliwa. Waafrika walikuwa na matumaini makubwa sana na bwana Obama. Yamefikiwa?

Ni vema ifahamike kuwa Barack Obama ni Rais wa Marekani na siku zote atalinda maslahi ya Marekani tu. Kuwa na matumaini makubwa kwamba labda yeye angeliweza kuiweka Afrika mbele sana ilikuwa ni kujifurahisha tu nafsi. Maslahi ya Marekani ni ya kipaumbele kuliko kitu kingine chochote kwa Rais Obama. Kwa wengi Obama amekuwa kama amewavunja moyo.

Tanzania inapokea kiongozi wa Taifa kubwa duniani wa pili sasa ndani ya kipindi cha miezi 3 tu. Kwanza alikuja Rais wa China na sasa wiki hii anakuja Rais wa Marekani. Maneno ya mtaani na kwenye mabaraza ya majadiliano ni kwamba viongozi hawa wanakuja kugombea maliasili tulizo nazo kama gesi asilia na madini. Nadhani haya ni maneno ya kusema katika kupiga soga maana kunyonywa kwa rasilimali hakuhitaji Rais wa Marekani aje Tanzania. Makampuni yote makubwa yanayochimba dhahabu hapa nchini ni makampuni ya nje na marais wao hawakuja ili waweze kupata mikataba minono ya kuvuna utajiri wetu.  Katika kitalu namba 2 cha utafutaji wa mafuta na gesi huko Bahari Kuu kampuni ya kimarekani ya ExxonMobil ina ubia na kampuni ya Norway ya StatOil. Kampuni hiyo haikusubiri Rais wa Marekani aje ili wapate mikataba.

Kuna makampuni mengi sana ya kichina yanajenga barabara zetu hapa nchini yakiwa na mikataba minono sana. Kule Mchuchuma na Liganga kuna kampuni ya kichina inajiandaa na uchimbaji wa chuma na makaa ya mawe. Makampuni yote haya hayakusubiri Rais wao aje.

Hoja inayojengwa hapa ni kwamba ujio wa Marais mbalimbali nchini ni ujio wa kujijenga kidiplomasia na wakati mwingine kama sehemu ya kutuma ujumbe Fulani kwa dunia. Nchi inayotembelewa pia inaweza kuona kuwa diplomasia yake inaheshimiwa na mataifa yanayoitembelea.

Hata hivyo hii haiondoi ukweli kwamba Obama anakuja kwa ajili ya maslahi ya nchi yake kama ilivyo kwa wachina walivyokuja. Tumesikia Rais Obama ataambatana na mamia ya wafanyabishara kutoka Marekani kwa ajili ya kupata fursa za kuwekeza nchini. Pia tutasikia matangazo kuhusu msaada wa pili wa Millenium Challenge ambapo Wamarekani wanaendelea kumwaga pesa nchini kusaidia miundombinu lakini pia kushawishi kuungwa mkono na nchi zetu kwenye maamuzi Fulani Fulani jumuiya za kimataifa.

Tumesikia Obama atakwenda kutembelea mitambo ya kampuni ya Symbion. Hii ni mitambo ambayo miaka 4 iliyopita ilipigiwa kelele kuwa ni mitumba na hivyo TANESCO wasiinunue. Hawakununua na badala yake kampuni hiyo ya kimarekani ikainunua, wakaingia  mkataba na TANESCO kuwauzia umeme unaozalishwa na mitambo hiyo hiyo chakavu. Wakati tunasuburi kulipa takribani tshs 105 bilioni kwa Dowans baada ya kutubwaga kwenye kesi, tunasubiri kuona wanasiasa watakaokwenda kumsindikiza Obama kwenye matembezi hayo ya kutembelea mitambo chakavu.

Kampuni kubwa ya kutengeneza mitambo ya kuzalisha umeme ya GE imetangaza kuingia ubia na kampuni ya Symbion kuzalisha umeme nchini. Takribani 400MW zitazalishwa kutoka Mtwara na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa. Pia sehemu kubwa ya umeme utakaozalishwa Mtwara tayari umepata soko kwenye kiwanda cha kuzalisha udongo ulaya (simenti) cha bwana Dangote kule Mtwara. Mtendaji Mkuu wa GE bwana Jeff Immelt ametangaza kuwa kampuni yake itauza mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi mingi zaidi Afrika Mashariki kuliko Marekani katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Ni biashara tu!

Nishati naona ni kipaumbele kikubwa sana kwa ziara ya Rais Obama. Kwa nchi kama yetu yenye watu asilimia 21 tu wenye umeme, ni dhahiri kipaumbele hiki watu wengi watakiiunga mkono. Hata hivyo Obama ni lazima asimame kidete kuhakikisha kuwa kampuni za nchini mwake zinazopata miakataba hapa nchini ziweke wazi mikataba hiyo na kulipa kodi inavyostahili. Makampuni ya mafuta kutoka Marekani hayana historia nzuri duniani na hivyo ni lazima tulisisitize mapema kabisa. Uwazi wa mikataba na uwezo wa kupambana na ukwepaji kodi ni muhimu sana katika vita dhidi ya Ufisadi na ubadhirifu.

Rais Obama atambue kuwa iwapo Tanzania ingekuwa inakusanya nusu ya kodi zinazokwepwa na makampuni makubwa yanayotumia mbinu kali, basi tungehitaji misaada ya Marekani na hapa nchini angekuja kama mbia wa kweli na sawa katika dunia. Hivyo ni vema aungane na Waziri Mkuu wa Uingereza kuhakikisha kuwa makampuni makubwa hayatumii ‘tax havens’ kukwepa kodi katika nchi kama Tanzania. Uwazi wa mapato yao na kilicholipwa kwa Serikali ni vema usisitizwe sana na Obama mwenyewe ili makampuni yao yasikie na yaache kupora utajiri wa Afrika kiujanja ujanja.

Patrice Lumumba

Mwisho ni vema kama Rais Obama ataomba radhi kwa ushiriki wa Marekani kwenye mauaji wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo Patrice Lumumba. Hivi Tanzania inahangaika zaidi ya uwezo wake kupeleka majeshi huko mashariki ya Kongo kulinda amani. Waafrika wengi tunaamini kuwa mauaji ya Lumumba ilikuwa ni kama laana kwa Taifa lile na hivyo limekuwa ni taifa la vurugu na vita licha ya utajiri mkubwa ulioko nchini humo. Nyaraka za CIA zinaonyesha dhahiri kuwa Rais wa Marekani wa wakati huo Lyndon Johnson aliagiza kuuwawa kwa mwanamapinduzi Patrice Lumumba. Kuwaomba radhi Waafrika na hasa Wakongo kuhusu mauaji ya Lumumba ni jambo litakaloweza kusaidia sana kurejesha amani Kongo.

Karibu Afrika, Karibu Tanzania ndugu Barack Hussein Obama.

Written by zittokabwe

July 1, 2013 at 8:56 AM

5 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Monday
  On Monday afternoon, President Obama
  takes part in a formal arrival ceremony in
  Dar es Salaam, Tanzania.
  President Obama participates in a bilateral
  meeting and joint press conference with
  President Jakaya Kikwete of Tanzania.
  In the evening, President Obama
  participates in a CEO roundtable and
  business leaders forum.
  President Obama and President Jakaya
  Kikwete of Tanzania participate in an
  official dinner.
  Tuesday
  In the morning, President Obama takes
  place in a Consulate meet and greet.
  President Obama visits the Ubungo Power
  Plant.

  john

  July 1, 2013 at 9:37 AM

 2. Brother, i am shocked to read Oil and Gas exploration advertisement by the ministry of Energy and Natural Resources, how they are advertisement is like selling tomatoes in wet market as if not sold immediately they will get rotten.
  Is this how the government intend to eradicate poverty? All expectation and excitement they giving to Tanzania citizen boasting of discovery of 35trillion cubic feet of gas etc, in which way a low participation of 20% share can generate reasonable to finance development programs, to create reserve funds for future use? I am very very disappointing by Professor Muhongo, is acting like he know nothing about business! What is the position of the cabinet on parentage share in investment? Why the minister is taking so lightly this matter? This is national economic security, should not be touched unless there is proper policy on each and every item by all stake holders. The ministry job is to implement what is agreed by all stake holders not to override and do whatever fits their pocket in form of bribes.I believe he does not tell the president the truth, is very manipulative. Should resign immediately, is selling out the country resources for his personal gains. By the time the citizen confront him will be too late. The best is to suspend all contracts untill the proper policy is in place.
  ————————————————————————

  The Government of the United Republic of Tanzania
  and the
  Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC)
  TPDC logo

  are pleased to invite the international petroleum industry and other specialized investors to participate in the exploration of hydrocarbons in Tanzania. Companies may wish to negotiate a Production Sharing Agreement (PSA) for a number of available blocks in the sedimentary basins both onshore and offshore. Currently, open acreage include the Rufiji basin, inland rift basins of L. Rukwa, L. Tanganyika, L. Nyasa, and the Ruhuhu Karoo Basin.
  KEY TERMS AND INCENTIVES

  Data on previous exploration available
  Negotiable work programme
  No ring-fencing for the recovery of exploration costs
  Favorable profit sharing
  Low TPDC’s participation, capped at 20% *****************
  Duty exemption on exploration equipment
  VAT exemption on locally purchased goods and services for use in Petroleum exploration
  No foreign exchange restrictions
  No initial payments such as signature or production bonuses
  Negotiable training fund
  Fast track negotiations for concluding a Production Sharing Agreement

  Model (PSA) and Petroleum (Exploration and Production) Act 1980:.

  A model PSA, the Petroleum (Exploration and Production) Act 1980, The Income Tax 2004, and also a brochure on petroleum exploration potential are available free of charge. Following the first round, Petrobras have been awarded exploration rights for Block # 5 in year 2004. Following the closure of the Second round in July 2002, Shell were awarded exploration rights over Blocks 9-12. The agreement awaits the endorsement of the Government. The third licensing round was closed in May 2005 and three companies namely OPHIR ENERGY, STATOIL and PETROBRAS were invited for PSA negotiations. OPHIR ENERGY signed their PSA agreement over Block #1 end of October 2005. Negotiations with PETROBRAS and STATOIL are continuing. For details on the deep sea project companies that may wish to apply for open acreages onshore or to buy deep sea data may contact us using the following contacts:
  Contacts

  Permanent Secretary
  Ministry of Energy and Minerals
  P.O. Box 2000
  Tel: 255-22-117153/9
  Fax: 255-22-116719
  E-mail:mem@mem.go.tz

  Managing Director
  Tanzania Petroleum Development Corporation
  P.O. Box 2774
  Tel: +255 222200103/4
  Fax: +255 222200113
  E-mail:tpdcmd@tpdc-tz.com.com

  Directorates

  Exploration, Production & Tech

  Copyright © 2013 Tanzania Petroleum

  Alex Kakala

  July 1, 2013 at 12:07 PM

 3. Katika tanzania ya leo, mapinduzi inawezekana kwa kuanzia ngazi za familia kwa kuwalea watoto wawe na uzalendo, ukweli ni kwamba ujio wa baraka oboma hauna tija ila tumefurahi tu ya kwamba tumethubuti kwa rangi nyeusi kuongoza marekani taifa kama hilo lenye mchanganyiko wa watu aina mbalimbali! kweli baraka alikuwa na malezi ya maadili! Pia naipenda demokrasia yao, Watanzania twendeni shule kwa nyanja mbalimbali !

  emmanuel laizer

  July 2, 2013 at 6:37 PM

 4. Baada ya mauaji ya Lumumba, Marekani ilitumia gharama kubwa kuhakikisha dikteta Mabutu anabakia madarakani kwa hali yoyote. Wananchi wa Kiwilu(1963) na Kivu (1964) walipoanzisha vuguvugu la kutaka kumn’goa madarakani Marekani kupitia CIA waliunda genge la askari mamluki ili kuzima la kuzuia vuguvugu hilo la mabadiliko. Genge hilo mamluki wa Marekani lilivamia vijiji,kupora mali,kunyonga kikatili na kutenda vitendo vyengine vya ukatili usio na kifani.

  Naungana na wewe,ni vema kama Rais Obama angeomba radhi kwa ushiriki wa
  Marekani kwenye mauaji wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo
  Patrice Lumumba.

  Erick Machua

  July 19, 2013 at 11:34 AM

 5. Maisha marefu twakuombea Obama.

  Daudi Wa Iramba

  August 15, 2013 at 1:32 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: