Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Download: RASIMU YA KATIBA MPYA -DRAFT CONSTITUTION OF URT

with 108 comments

View this document on Scribd

108 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. […] rasimu ya katiba inapatikana hapa: http://www.katiba.go.tz/attachments/…nal_%20(1).pdf Na hapa: Download: RASIMU YA KATIBA MPYA -DRAFT CONSTITUTION OF URT | Zitto na Demokrasia Creativity is the sudden cessation of stupidity. Edwin H. Land Reply With […]

  • haipatikani nimejaribu kufuata kiunganishi ila hakuna kitu!

   hassan kanju

   June 4, 2013 at 9:40 AM

  • kaka Zitto nashukuru nifanikiwa kui-download

   Samweli Andrea Kijigo

   June 6, 2013 at 3:06 PM

  • nimeipenda rasimu hii kwani watanzania wamenuia kuleta mabadiliko makubwa nchini lakin nimesikitika suala la rushwa halijaongelewa ambalo ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya taifa letu tukilisahau hili litatusumbua sana watanzania kwani ni mdudu mbaya sana

   albert fen

   June 9, 2013 at 4:26 PM

  • inshort serikali 3 hazifai kwa rasimu hii naomba waliangalie vizuri

   masabo amos

   January 4, 2014 at 10:07 AM

 2. […] Gwalihenzi Asante Mwali. Download: RASIMU YA KATIBA MPYA -DRAFT CONSTITUTION OF URT | Zitto na Demokrasia Creativity is the sudden cessation of stupidity. Edwin H. Land Reply With […]

 3. Nimependezwa na naunga mkono suala la kuondolewa kwa viti maalum bungeni, waziri asiwe mbunge na spika n naibu kutokua mbunge n kutotokana na chama chochote

  Evarest

  June 4, 2013 at 9:27 AM

 4. rasimu ya katiba

  duncan

  June 4, 2013 at 9:34 AM

 5. Why Presidential power is still the same as before? It’s better to reduce them little bit. The President shouldn’t choose Permanent Secretaries Of Mistiries, Chief Attorney or other top position.

  Trevor

  June 4, 2013 at 9:38 AM

 6. mii nimeipenda muheshimiwa japo nimeisoma kwa ufupi

  Jackson Mfungwa

  June 4, 2013 at 9:39 AM

  • Madaraka ya Rais yapunguzwe watendaji wakuu,kama makatibu wakuu,wakuu wa mikoa,mwanasheria mkuu n.k wasiteuliwe na Rais.

   Becker

   June 6, 2013 at 9:51 PM

 7. […] YA KATIBU MPYA HIYO WADAU KWA HISANI YA Download: RASIMU YA KATIBA MPYA -DRAFT CONSTITUTION OF URT | Zitto na Demokrasia Attached […]

  • nimefurahishwa sana na rasimu ya katiba, lakini nguvu ya rais hijapunguzw the power of president in Tanzania is too excessive compared to other states like USA where by the president power is limited every appointed of top offical leader must be approved by senator or upper chamber, we need electoral commission which is independence like the constitution of kenya 2010

   Amos Enock Masala

   June 4, 2013 at 10:08 AM

 8. Hakika hii imekaa sawa kwan imeweza kupunguza mlundikano wa madaraka kwa wabunge

  Julius b benson

  June 4, 2013 at 9:51 AM

 9. Eeheeee!!! Haya cc twapita2

  barahiyan tuwa

  June 4, 2013 at 10:19 AM

 10. thax kwa link

  Geofrey Fredrick

  June 4, 2013 at 10:29 AM

 11. Cyo mbaya

 12. Mwanzo mzuri na vitu vingi vya msingi ambavyo watanzania walivitaka vimeonyeshwa,Tume imeonyesha inaweza cha msingi hisiwasikilize sana wanasiasa kwani kufanya hivyo inaweza kuelekea pasipo,Ili nimelisema kimakusudi kwani wanasiasa wetu wanasamini vyama vyao kuliko taifa letu,Mungu Ibariki Tanzania.

  simula maregesi

  June 4, 2013 at 11:26 AM

 13. Vipi kuhusu haki za wanaume? Naona haki za watoto, wanawake walemavu na vikundi maalumu zinatajwa kwenye katib. Nadhani ni vizuri hata haki za wanume zitajwe kwenye katiba hata kama hazitatungiwa sheria.

  Prosper

  June 4, 2013 at 12:26 PM

  • ndugu haki ya mwanaume anayo siku nyingi toka kuumbwa kwa adam, hivyo haki ya mwanaume anayeikosa itapatikana kwenye vikundi maalum. kwani wewe huoni kuwa siku za wanawake, watoto na vikundi maalum zimetengwa? basi kaa ukijua siku nyingi ni za mwanamume na za wengine hao ni chache. wanaume tuache ubabe!!!!!!!!!

   GWAKISA

   June 14, 2013 at 5:36 AM

   • kaka gwakisa mbona wanawake unawashusha kiasi hicho leta thread nyingine kaka cha msingi unatakiwa uchangie maoni yako kwa rasimu kama ifuatavyo, rasimu bado mamlaka ya rais ni makubwa kwani hata hawa wakuu wa mikoa na wilaya bado wanamtegemea rais why?

    daniel chacha

    June 18, 2013 at 11:38 AM

 14. Thanx alot kwa tume kuiweka ktk rasimu ya katiba ishu ya mgombea binafsi, km mmoja wa waliopata nafasi na wachangiaji wa hili nimefarijika sn.
  Kwa mwongozi wa tume juu ya rasimu ya katiba hope hili litapitishwa.
  Thanx kwa kazi nzuri tume.

  Simtowe Placid Joseph

  June 4, 2013 at 1:49 PM

 15. asilimia 90 rasimu ni nzuri. Tunaelekea kuzuri. hii asilimia kumi tutarekebisha tu. good!

  ben ngalya

  June 4, 2013 at 9:56 PM

 16. Nimefurahia katika mgawanyo wa kazi,wabunge wahudumu kama wabunge,mawaziri kama mawaziri na si mawaziri watokane na ubunge hili ni jambo jema,..pia uwepo wa tume huru ya uchaguzi ni swala zuri sana.

  Jossy Jacky

  June 5, 2013 at 12:06 PM

 17. tuwe na serikali ya Jamuhuri ya Tanganyika na siyo Tanzania Bara kama ilivyo kwenye rasmu ya katiba mpya 2013

  Alfred Maira

  June 5, 2013 at 12:08 PM

 18. SWALA KA KUWA NA SERIKALI TATU NI UTOTO. KAMA TUNATAKA MAMBO YAWE SAWIA IPIGWE KURA YA MAONI JUU YA HATIMA YA MUUNGANO ILI WENGI WAKISEMA MUUNGANO UDUMU BASI TUWE NA SERIKALI MOJA KAMA KUVUNJA TUVUNJE ILI TUKUTANE NDANI YA AFRIKA MASHARIKI NA SADEC.

  IBRAHIM CHOTOLA

  June 5, 2013 at 1:46 PM

  • Kweli kabisa,Muungano wa serikali moja au kila nchi na lwake, tukutane EAC,SADC,AU na UN.
   Nje ya Muungano wa serikali moja ni kuendelea kuzungumzia kero za Muungano wa serkali 2,3 au mkataba.
   Serikali 3 MWL alikataa na akatunga kitabu Uongozi wetu na hatma ya Tanzania.Azimio la Bunge lilisema serikali moja muda muafaka utakapofika.Muda huo ni sasa,vinginevyo tuachane kwa usalama.

   KOMBA,G.O.P

   June 6, 2013 at 1:20 PM

   • kuhusu muungano kweli ni janga la kitaifa! inaonesha watu wengi wana dukuduku linalofukuta mioyoni mwao hasa watanganyika. tatizo la watanganyika wengi wanaogopa wosia wa nyerere kuuvunja muungano, uhalisia uko hivi ukimuuliza mmojammoja atakuambia bora kuuvunja ila wanaogopa wosia wa nyerere ili wasije wakaonekana wenyewe ndo waanzilishi wa kutaka kuuvunja. kuna wengine wamediriki kusema eti waende kwenye kaburi la nyerere kuliambia kuwa limpe taarifa ya ombi la kutaka kuuvunja muungano. maana wanakerwa nao

    GWAKISA

    June 14, 2013 at 5:54 AM

 19. SUALA LA KUWA NA SERIKALI TATU HAPANA. KAMA TUNATAKA MAMBO YAWE SAWIA IPIGWE KURA YA MAONI JUU YA HATIMA YA MUUNGANO ILI WENGI WAKISEMA MUUNGANO UDUMU BASI TUWE NA SERIKALI MOJA KAMA KUVUNJA TUVUNJE ILI TUKUTANE NDANI YA AFRIKA MASHARIKI NA SADEC.

  IBRAHIM CHOTOLA

  June 5, 2013 at 1:53 PM

 20. MAMBO MENGI NDANI YA RASIMU NI MAZURI. ILA RAIS ANAPEWA JUKUMU LA KUTEUWA ILI IWEJE? HILI JAMBO LINANIPA KICHEFUCHEFU NAOMBA MLIONDOE AMA MLIWEKE KWA MUUNDO MWINGINE. LABDA ATEUWE MAWAZIRI TU NASIO NAFASI KAMA YA JAJI MKUU.

  IBRAHIM CHOTOLA

  June 5, 2013 at 2:00 PM

 21. HONGERA TUME! ILA KAZI YENU ITAONEKANA HAINA MAANA KWAKUWA KILICHO NYUMA YA PAZIA LA MUUNGANO NINYI MNAJUA NA MMETUWEKEA SERIKALI TATU KWA KUTUTEGA WANANCHI. FANYENI KAZI ACHENI KUFICHA MAMBO MWISHO WA SIKU NAWAHAKIKISHIA MUUNGANO NI BOMU.

  IBRAHIM CHOTOLA

  June 5, 2013 at 2:05 PM

 22. MFANO CCM AKIONGOZA MUUNGANO, CHADEMA BARA NA CUF ZANZIBAR! KISHA CHADEMA NA CUF WAGOME KUFANYA KAZI BAINA YAO NA KATI YAO NA CCM JE, MUUNGANO UTADUMU? HATAKAMA MAWAZIRI WATAFANYA KAZI MAMBO YA MUUNGANO 7 YATALIFIKISHA TAIFA KAMA MUUNGANO?

  IBRAHIM CHOTOLA

  June 5, 2013 at 2:11 PM

 23. ZANZIBAR WANA KATIBA YAO. TANGANYIKA KATIBA ITAKAMILIKA LINI? WAKATI ILI MCHAKATO UANZE NI MPAKA REFERENDUM IKAMILIKE! AU MNATUMIA UBABE NA UZOEFU. MAZURI NI MENGI NDANI YA RASIMU NINGEPENDA YAFANYE KAZI CHINI YA SERIKALI MOJA.

  IBRAHIM CHOTOLA

  June 5, 2013 at 2:17 PM

 24. kuwepo na baraza la ushauri kwa ofisi ya raisi kutoka vyuo vikuu

  chilongani

  June 6, 2013 at 9:46 AM

  • Kwani kuna mapungufu gani ikulu hadi liundwe baraza la kumshauri raisi kutoka vyuovikuu?,nafikiri hii hoja ni nyepesi

   ISMAIL,NASSOR

   June 7, 2013 at 9:42 PM

 25. HIO SERIKALI YA TANGANGANYIKA ITAANZA NA RASILIMALI ZIPI? HIZO ZILIZOPO NI ZA MUUNGANO, HIVYO ZIGAWIWE KWANZA ZANZIBAR IPATE HAKI YAKE KWANI YEYE NI MMOJA YA WARITHI YA MALI ZA MUUNGANO NA TANGANYIKA IPATE CHA KWAKE

  ALI - ZANZIBAR

  June 6, 2013 at 11:44 AM

  • NDG ALI, NI RASILIMALI GANI HIZO UNAZOONGOLEA? HEBU WEKA SAWA HAPA ILI TWENDE SAWA. UNAONGELEA MAOFISI? AU JUMBA KAMA LA BUNGE LA DODOMA? AU MAJENGO MENGINE YA SERIKALI KAMA BOT N.K? KAMA HIVYO NDIVYO UNAVYOVIITA RASILIMALI AMBAZO UNATAKA VIGAWIWE KWANZA NASIKITIKA KUSEMA KUWA UELEWA WAKO NI MDOGO JUU YA RASILIMALI ZA MUUNGANO.

   KWA TAARIFA YAKO, NILIVYOVITAJA HAPO JUU HAKUNA CHOCHOTE TUNACHOWEZA KUKIITA RASILIMALI YA MUUNGANO. NA IKITOKEA MUUNGANO HUU UKAVUNJIKA, Z’BAR HAINA INACHODAI TANGANYIKA, VIVYO HIVYO TANGANYIKA HAKUNA INACHPIDAI Z’BAR. KILICHO Z’BAR KITABAKI KUWA MALI YA WA-Z’BAR, NA KILICHO TANGANYIKA KITABAKI KUWA MALI YA WATANGANYIKA. KAMA ILIVYO SASA KWA ARDHI YA Z’BAR ILIVYO MALI YA WAZANZIBAR NA WATANGANYIKA HAWANA HAKI KUMILIKI ARDHI Z’BAR. VIVYO HIVYO KWA MTINDO WA SERIKALI TATU WA Z’BAR ITAKUWA MARUFUKU KUMILIKI ARDHI TANGANYIKA, LABDA KWA NJIA YA UWEKEZAJI. SERIKALI TATU NDO UTAKUWA MWISHO WA KUI-BABY-SEAT Z’BAR.

   NIKUULIZE, Z’BAR ILICHANGIA NINI KTK UJENZI WA MAJENGO PACHA YA BOT DAR AU JENGO LA BUNGE DODOMA? KWA MAWAZO KAMA YAKO, NADHANI MUUNGANO UKO ICU………….. NA NITAKUBALIANA NA MAWAZO YA WENZANGU HAPO JUU, TUWE NA SERIKALI MOJA, AU KILA UPANDE UCHUKUE TANO ZAKE TUTAKUTANA EAC (Z’BAR IKITAKA), AU au UN. TAFAKARI VIZURI KAKA

   richard

   June 8, 2013 at 4:54 AM

 26. RASIMU YA KATIBA MPYA NI MAONI YETU WATANZANIA YALIYKUSANYWA NA TUME. WATANZANIA TUACHE CHOKOCHOKO. TUMEPEWA FURSA ADHIMU YA KUBADILI KATIBA,SASA TUMEPATA RASIMU BADO CHOKOCHOKO.ENYI MNAOPINGA SERIKALI TATU NI WAOGA WA MABADILIKO. TUSONGE MBELE, TUWE NA SERIKALI TATU KAMA WENGI TULIVYOPENDEKEZA. RASIM
  U HII SI YA CCM WALA WARIOBA, BALI NI YETU WATANZANIA. MCHAKATO UENDELEE HAKUNA KURUDI NYUMA.SERIKALI ZIWE TATU,MUUNGANO UDUMU DAIMA. MIMI KAMUGISHA,M.B-BUKOBA

  Kamugisha M. Bilal

  June 6, 2013 at 11:46 AM

  • safi sana kyoma watz waoga sana serikali tatu ndo muarobaini wa matatizo ya muungano MIMI ENG.ISMAIL,ISMAIL SUA MOROGORO

   ISMAIL,NASSOR

   June 7, 2013 at 9:35 PM

  • UKO SAHIHI KAKA KAMUGISHA. SERIKALI TATU NI MAONI YA WATANZANIA HASA KWA KUZINGATIA HALI YA MUUNGANO ILIVYO LEO KWA MTIZAMO WA WAKAZI WA PANDE MBILI ZA MUUNGANO. LABDA WATU HAWA WANAOPINGA SERIKALI TATU PENGINE HAWAIISHI HAPA TZ, YUMKINI WANAISHI NG’AMBO NA HAWAJUI KINACHOENDELEA TZ. KWA HALI ILIVYO SASA KTK MUUNGANO WETU, SERIKALI TATU NDIYO NJIA PEKEE YA KUULINDA MUUNGANO HUU. SERKALI MOJA HAIWEZEKANI (HASA KWA WENZETU WAZ’BAR HAWAKO TAYARI, NA SERIKALI MBILI YENYEWE NDIYO KABISAAA HAIKUBALIKI.

   KWA MAZINGIRA YA SHERIA ILITUNGWA KUONGOZA MCHAKATO WA KATIBA MPYA ILIYOSAINIWA NA RAISI, AMBAPO NI MARUFUKU KUZUNGUMZIA HABARI YA KUVUNJA MUUNGANO, SERIKALI TATU NDIYO SULUHISHO, JAPOKUWA NI LA MDA MFUPI (KWA MAWAZO YANGU). UTEKELEZAJII WA SERIKALI TATU UTAKUWA NA UFANISI KAMA PANDE ZOTE MBILI ZA MUUNGANO ZITAKUWA WAZI BILA KUWA NA “HIDDEN AGENDA BEHIND THE DOOR” NA KWA KUWEKA MISINGI YA KIKATIBA YA UTENDAJI AU UTEKELEZAJI WA SERIKALI TATU AMBAYO ITAZILAZIMISHA SERIKALI ZA TANGANYIKA NA ZANZIBAR KUWA “LOYAL” KWA SERIKALI YA MUUNGANO HATA PALE SERIKALI ZA Z’BAR NA T’KA ZITAKAPOKUWA CHINI YA VYAMA TOFAUTI NA SERIKALI YA MUUNGANO AU KINYUME CHAKE.

   MISINGI HII LAZIMA IWEKWE. KWA MWELEKEO WA KISIASA ULIVYO SASA, UPO UWEZEKANO MKUBWA UKAKUTA SERIKALI YA MUUNGANO IKAONGOZWA NA, SAY CCM, YA TANGANYIKA IKAONGOZWA NA CHADEMA, NA YA Z’BAR IKAWA CHINI YA CUF AU KINYUME CHAKE. KATIKA HALI KAMA HIYO, KAMA HAKUNA MISINGI YA KIKATIBA JUU YA NINI WAJIBU WA SERKALI ZA PANDE MBILI ZA MUUNGANO KWA SERIKALI KUU YA MUUNGANO, UNAWEZA UKAWA MWANZO WA KUVUNJIKA KWA MUUNGANO NATURALLY BILA KUWEPO REFERENDUM KWA PANDE MBILI JUU YA UWEPO AU KUTOKUWEPO KWA MUUNGANO KAMA AMBAVYO BAADHI YA WATU WANASHAURI.

   ILI MUUNGANO UZIDI KUWEPO, UWE WA SERIKALI TATU AU MOJA ITATEGEMEA NIA NA UWAZI WA VIONGOZI WETU. LAZIMA SUALA LA MUUNGANO LIWEKWE WAZI MBELE YA WATANGANYIKA NA WAZANZIBAR ILI UJADILIWE KWA UWAZI BILA WOGA, VITISHO WALA MIPAKA ILI MWISHO WA SIKU WANANCHI WA PANDE ZINAZOHUSIKA NDIO WAAMUE NINI KIFANYIKE JUU YA MUUNGANO. NIONAVYO MIMI, UBABE WA VIONGOZI AU WANASIASA JUU YA SUALA LA MUUNGANO UNAWEZA KULETA SHIDA KUBWA SIKU CHACHE ZIJAZO-NA WALA SIYO MBALI SANA.

   richard

   June 8, 2013 at 5:24 AM

 27. Rasimu hii ya Katiba tuisome kwa makini na wala tusikurupuke kwa kusoma kwa juu juu

  Deule, T.

  June 7, 2013 at 8:32 AM

 28. Ciipati nifanye nn?

  badru badrudeen

  June 7, 2013 at 11:26 AM

 29. kwa vile ni rasimu ya kwanza makosa hayaepukiki kama makofi polis bt ushulu bandalin haujakaa vizur kam kwel ni muungan

  Mike

  June 7, 2013 at 8:05 PM

 30. Kwanza naipongeza Tume kwa kazi nzuri mlioifanya. Pili natoa maoni yangu kuhusu serikali tatu. Napendekeza kuwe na makamu rais wawili ambao watapatikana katika uchaguzi wa serikali ya Muungano, yaani wa Tanzania bara na Zanzibar na ndiyo wawe wakuu wa serikali za Bara na Zanzibar. Hii itasaidia kutokuwa na marais wengi ndani ya nchi moja, na itamsaidia rais wa serikali ya Muungano kuwa na madaraka kamili ndani ya serikali tatu.

  Alfred Mwakitalu

  June 7, 2013 at 9:03 PM

 31. HII NI NJIA NZURI ILA INABIDI WANANCHI TUPATE MUDA WA KUANGALIA RASMU HUU KWA UANGALIFU SANA

  aloyce mwaana olodonjilao

  June 7, 2013 at 9:51 PM

 32. RASIMU SIOMBAYA SANA TUME IMEJARIBU KIZIMGATIA MAONI YA WATANZANIA HASA KWENYE KIPENGELE CHA MALAKA YA RAIS KUTEUWA BARAZA LA MAWAZIRI MIONGONI MW WABUNGE WALIOMO NDANI YA BUNBE, VIVYO HIVYO NAIPA BIGAPU TUME KATITA KIPENGELE CHA UTEUZI WA SPIKA UWE NJE YA MEMBER WA BUNGE INGAWAJE TUME BADO INACHANGAMOTO KATIKA SWALA LA KUMWACHIA RAIS MAJUKU KARIBU YOTE YA KUTEUA BAANDI YA VIONGOZI HII HAILETU MANANA YA SEPARATION OF POWER KAMA ILIVYO KWENYE IBARA ZIFUATAZO ZILIZO AINISHWA NA KATIBA YA JAMUHURI YA MUNGANO WA TANZANIA IBARA YA 35(1), 36(1), 55(4), 63(2), 97 NA IBARA YA 109.

  WILSON WILLIAM

  June 7, 2013 at 11:53 PM

 33. Nguvu ya rais bado ni kubwa sana inabd ipunguzwe coz ataendelea kuwa mungu mtu, swala la rais kupewa uwezo wa kuteua viongoz wa sekta muhmu kama mwanasheria mkuu wa serikari,wakuu wa mikoa iabd iwe kaz ya wabunge kuteua la sivo iundwe bod maalum ya kufanya kaz iyo,swala lingne akuna umuhmu wa kuwa na mkuu wa wilaya hii ni moja wapo ya matumzi mabaya ya pesa.

  Saviola savinus

  June 8, 2013 at 4:37 PM

 34. rasimu kwa maelezo ya awali njema ngoja tusubiri kuisoma juu ya rasilimali uwekezaji na mengineyo huku tukisubiri kudada vuliwa na wataalam walio zamia katika mambo hii kuhusu serikikali tatu kigugumizi

  Abdul hussein

  June 8, 2013 at 4:59 PM

 35. nadhani tudumishe muungano kwa kupeana free of movement kati ya watanganyika na wazanzibari, maana kwa mazingira ya muungano uliodumu mda wa miaka 50, ilikua ni kuinyanyasa zanzibar na bdo rasimu hii inaelekea kulekule….mana bdo hata nusu ya malengo ya wazanzibari hayafikia, yale mambo muhimu yote yanayofanya muhimili wa nchi wameyatia kwenye muungano ili kuendelea kuinyanyasa zanzibar!!

  abdul

  June 8, 2013 at 11:42 PM

  • Muungano kwel udumishwe ila sheria znazotubana tanganyka hko zanzbar ziondolewe kama haki ya kumiliki ardhi.pia marais watatu isiwepo chakufanya hawa wawili wapewe nguvu sawa katika maamuz ya kiuchumi,kijamii na kisiasa ndani na nje ya nchi.

   Richard mlata

   June 9, 2013 at 5:29 PM

 36. mheshimiwa pole na kazi, naweza nikapata soft copy ya draft ya marekebisho ya sheria ndogondogo? Alex Maketa NAO-SHINYANGA 0713708686

  Alex Maketa

  June 10, 2013 at 6:15 PM

 37. nimependa rasimu ya katiba mpya. lakini spika wa bunge asiwe mbunge kama rasimu inavyosema pia asiwe mfuasi wa chama chochote cha siasa. viongozi wa mihimili mingine kama vile mahakama na bunge wachaguliwe kusiwe na mkono wa Rais kabisa.

  Emanuel Geydan

  June 10, 2013 at 6:24 PM

 38. wadau nisaidiani sielewi hii rasimu sasa itakuwa ni ya katiba ya tanzaina au tanganyika? najua zanziabar wanakatibia yao tayari. sasa je tutakuja kukaa tena na kuunda tume itakayoanza mchakato wa kupata katiba ya tanganyika ???

  masambua

  June 11, 2013 at 9:22 AM

 39. ndugu zangu nimejaribu kuidownload rasimu ya katiba kupitia page hiii lakini nimwshindawa naomba mzarendo yoyoyte anisaidie mwenyenayo kama soft copy kuptia email ya ronaldmwandambo@gmail.com by ronald mwandambo

  ronald. j. mwandambo

  June 11, 2013 at 2:33 PM

 40. IKO POUWA SANA, TUTAJUA MENGI

  Tinno Sanga

  June 11, 2013 at 2:48 PM

 41. RASIMU ya katiba iko poa kabisa kwani imezingatia mambo mengi muhimu k.v.independent electral commission,speaker na naibu wake wasiwe wabunge au wanasiasa,mahakama huru,madaraka ya Raisi kupunguzwa n.k. Muundo wa serikali tatu unafaa kwa maslahi ya muungano ili udumu.

  Eng.Wansakya

  June 12, 2013 at 10:43 AM

  • Neno Tanzania bara lifutwe na badala yake lisomeke Tanganyika

   evans

   June 12, 2013 at 11:54 AM

 42. hao wezetu tumewaona jinsi gan walivyo pigana kwa
  mambo kama haya tuna miala 50 ya uhuru wote wana
  tuonea chuki kwa muungano wetu wa serikali mbili leo
  hii tumepata shetani gani juu ya hilo.

  abdalla

  June 12, 2013 at 12:15 PM

 43. Tz kumekua na vyama vingi sana ila tusiige
  idadi ya vyama kuwa serikali ni makosa makubwa
  kama kuna mambo ya kuangalia bc tuangalie na sio
  kusema serikali tatu pia tume ya mabadiliko imekuwa
  na mapungufu yake kwani mambo yametolewa mengi
  wameyaona ya serikali tatu tu why?

  abdalla

  June 12, 2013 at 12:26 PM

 44. RASIMU HII YA KATIBA NAONA KAMA IMEJIBU MAONI YETU ISIPOKUWA NINA WASIWASI WA UTEUZI WA TUME JUU YA VIONGOZI WA JUU KAMA JAJI MKUU NK . WASIWASI WANGU NI KUWA TUME HIZI ZINATEULIWA NA RAIS AND THEN WAPENDEKEZE MAJINA YA RAIS KUTEUWA MIMI NADHANI TUNARUDI KULEKULE
  JAMBO LINGINE RASIMU IMETAJA MWANASHERIA MKUU KUWA MMOJA WA WABUNGE JE MDHIBITI NA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI SI ZAIDI?
  MIMI NIGESHAURI WATU HAWA WALIOTJWA KUWA RAISI ATAWATEUWA WAOMBE KAZI HII NA CV ZAO ZITAJWE KWENYE MAGAZETI NA WANANCHI WATOE MAONI YAO

  NINA HOFU JUU YA CHAGUZI NDOGO KUWA KAMA CHAMA CHA SIASA KINA ORODHA YA WATU WAKE VIPI WAGOMBEA BINAFSI

  Msanii wa Kimasai

  June 12, 2013 at 12:53 PM

 45. Many of tz p’ple we are nt aware of this new constitution for havn mor than two gvnt

  Azaria

  June 12, 2013 at 8:07 PM

 46. kwanini rais anateua sana naona kama bado anaingilia mihimili mengine,powers zake zipunguzwe……..haswaaa kwenye judiciary

  christer

  June 13, 2013 at 11:55 AM

 47. safi sana mh. zitto, rasmu mpya nimeipata.

  mheshimiwa zitto kuna habari inimeipata kwenye mtandao, ninaomba unithibitishie. mimi ninaona bora wote tuwe wa bunge2.

  “””””””Here are the top highest best paying jobs in Tanzania in no particular order

  1. Member of Parliament (m.p)

  Tanzanian mps are among the best paid law makers in the world as far as I know. To them (I call them greedy fellows) the amount they earn isn’t enough and unfortunately they are always agitating for a salary increase. Here is what a Tanzanian member of parliament makes in a month (30 days to be exact)

  Basic salary sh.6,000,000
  Entertainment allowance sh.1,000,000
  House allowance sh.1,250, 000
  Car maintenance allowance sh.3,000,000
  Gym membership sh.60,000
  Vehicle fixed cost allowance. Sh.3,000,000
  Committee meeting allowance sh.100,000
  Constituency allowance sh.900,000
  A grand total amount of shillings 16,000,000 million which is equivalent to $14,118

  2. Commercial bank C.E.Os and Top managers

  The banking and financial sector in Tanzania is also home to some of the top highest paying jobs in Tanzania. Banks in Tanzania pay competitive salaries and bonuses to their employees. Economists and financial analysts are of the opinion that banks in Tanzania pay competitive salaries to employees due to the fact that they make billions of shillings in profits every financial year and hence no room for losses which may have reduced salary and remuneration budgets. It’s often very rare to see a bank in Tanzania making losses whatever the prevailing economic condition is. Currently loan customers are charged 19% interest rate on the money they borrow for whatever reasons. Tanzania banks also make a lot of money in forex
  Most major Banks in Tanzania banks don’t make losses and that is why you will see chief executive officers being paid salary in the range of $23,530 – $35,295. Word on the street is that C.E.O’s and top managers in Barclays, CRDB, Standard Chattered, NBC, Exim Bank and other co-operative bank are among the highest paid in the banking industry of Tanzania

  3. Constitutional / Government office holders

  Constitutional office holders are also one of the highest paid people in Tanzania.
  • The chief justice and his assistant
  • Governors,directors and deputy governors of The Central Bank
  • Chairman of the independent electoral and boundaries commission and the commissioners that come under him.
  • The attorney general
  • Chairpersons and commissioners of various commissions e.g commission on implementation of constitution, Tanzania national commission on human rights e.t.c.
  • All in all constitutional office holders in Tanzania are paid salaries and allowances in the range of $17,647 – $29,412)

  mwanamagauzi

  June 13, 2013 at 3:50 PM

  • Mheshimiwa Jaji Warioba na timu yako mimi binafsi nikupe pole kwa kazi hiyo ngumu lakini ninayo mawili yangu maoni,
   Kwanza ni kuhusu uwajibishwaji wa Rais naona hili halijajitokeza sana kiasi cha kutozungumzwa au andikwa katika rasimu yako. Kwa Afrika kwa sasa tunahitaji wapiga kura kumwajibisha Rais hata baada ya kumaliza muda wake kwa kumvua kinga. Umetamka matokea ya U-rais yajadiliwe endapo itaonekana yana utata hilo sina shaka. Shaka yangu ipo kwenye uwajibishwaji wa Rais baada ya kumaliza muda wake mimi sijaona ingawa nina uhakika watu watu wengi tulitoa maoni haya. Tunaomba hili lingizwe kwenye Rasimu hii

   Msomba

   June 17, 2013 at 7:03 PM

 48. napendekeza selikari kama ilivyo sasa tu.Pia itungwe sheria ya kunyongwa kwa mafisadi na wahujumu uchumi wa tz.

  KANYAMALA

  June 15, 2013 at 8:13 PM

 49. serikali 3 ni gharama tupu

  prims kimario

  June 16, 2013 at 4:31 PM

 50. spika asiwe mbunge wa chama chochote pia kuwe na tume huru ya uchaguzi na raisi apewe mamlaka ya kuteuwa mawaziri tu wakurugenzi wengine wateuriwe na mawaziri wa wizara husika ili kuwe na mfumo wa uwajibikaji.kiutendaji

  wazir mwenda

  June 17, 2013 at 12:46 PM

 51. muundo wa serikali 3 haufai,ni bora tujue tu kuwa kuna serikali moja au hakuna muungano,!! hata hivyo rasimu hii haijaanisha moja kwa moja ni mambo gani yapo chini ya muungano na yapi yatakuwa sio ya muungano!!!

  prosper juma

  June 17, 2013 at 3:59 PM

 52. zanzibar hatuna haja na serikali tatu bali tunataka zanzibar yetu yenye mamlaka kamili nationally and internationally sawasawa!!! however ndugu zetu wa damu walioko Tanganyika wataendelea kuwa ndugu zetu na hatutawaacha kamwe!i love Zanzibar

  mzanzibari

  June 18, 2013 at 2:32 AM

  • Mzanzibari uko sahihi saaana, unajua ukiamua kula nyama ya mbwa ukiulizwa uwe tayari kujibu kua unakula mbwa? Ikiwa Tanganyika na Zanzibar zitakua nchi mbili tofauti hata watanganyika waishio zanzibara na wazanzibar waishio tanganyika itawalazimu kurudi kwao ili watu watembeleane kwa pasport kama ilivyo kenya, uganda n.k, Na ikiwa watu wa upande wowote wataamua kubaki upande mwingine basi waombe kibali cha kuomba uraia….na wao kuishi miaka mingi Tanganyika au Zanzibar siyo tija ya wao kuomba uraia.

   Frank

   June 18, 2013 at 1:32 PM

  • Mzanzibari uko sahihi saaana, unajua ukiamua kula nyama ya mbwa ukiulizwa uwe tayari kujibu kua unakula mbwa? Ikiwa Tanganyika na Zanzibar zitakua nchi mbili tofauti hata watanganyika waishio zanzibara na wazanzibar waishio tanganyika itawalazimu kurudi kwao ili watu watembeleane kwa pasport kama ilivyo kenya, uganda n.k, Na ikiwa watu wa upande wowote wataamua kubaki upande mwingine basi waombe kibali cha kuomba uraia….na wao kuishi miaka mingi Tanganyika au Zanzibar siyo tija ya wao kuomba uraia.

   Frank

   June 19, 2013 at 1:27 PM

 53. Haionekani

  Godfrey Gerard

  June 18, 2013 at 7:49 PM

  • ardhi haijaguswa licha ya kuwa tatizo kubwa,

   Elias matunge

   June 19, 2013 at 8:57 PM

 54. Naona Rasimu imekidhi Matakwa ya wacahche, bado haijakithi baadhi ya wanachi wengine.

  Abdulrahman Omar

  June 22, 2013 at 1:00 PM

 55. Naomba mnsiaidie haya.
  1.Nini maana ya Muungano?
  2.Kwa nini Nchi Zinaungana?
  3.Faida ya nchi kuungana?
  4.Muungano huo una tija gani?
  Kwa hayo machache juu naomba kuongelea kidogo Kuhusu huu mchakato wa katiba.
  Nashangaa kuona watu wanakaa na kuzungumzia mchakato wa katiba wakati Wazanzibar wameisha sema kuwa wanataka mamlaka yao kamili,hii si ya kwangu bali namanukuu Bwana Sharif Hammad katika vikao vyake alivyo kuwa akifanya kipindi cha kwanza wakati mchakato ndo unaanza.
  Sasa wenzangu naomba hili tuliangalie kwa jicho la pili ili siku ikifika mambo yameenda ndivyo sivyo tusibaki daraja la Selander tukiwa hatuwezi kwenda mbele wala kurudi nyuma.
  Watanganyika nawaomba nawala si ubaguzi tusimame tuongelee Tanganyika yetu pasipo woga wala kutafuna maneno.
  Zanzibar wana Rais wao, Bunge lao, wana jeshi lao,kimoja tu hawana ni Mahakama, hiyo mifumo niliyo hitaja ya Zanzibar sisi ya Tanganyika iko wapi?
  Naomba majibu ya maswali yangu hayo hapo juu.
  Kwa leo naishia hapa.
  Potentine Protas wa Dar eS salaam.

  Potentine Protas

  June 22, 2013 at 6:27 PM

 56. Napata shida kidogo ninaposoma juu ya muungano wa serikali tatu ambao watu wameupendekeza, sidhani kama serikali 2 zikiungana zinatengeza ya tatu, mi nilifikiri serikali mbili zikiungana zinadisolve na kutengeneza moja yenye zote 2 na sio 2 au 3. Mi nadhani kuna haja ya kuliangalia vizuri suala la muundo wa serikali katika ibara ya 57(1). “MUNGU IBARIKI TANZANIA”

  Egid Mwakaponda Sanga

  June 28, 2013 at 10:09 PM

 57. Amna kinachopatikana mbona?
  Mie nadownload haipatikani, Hivi na nyinyi mambo haya mmeanzalini? Hivi mnazani wenzetu wanavyoeka na kudownload ni kitu rahisi eenh?
  Learn Back!

  bynder Mzawa

  June 29, 2013 at 5:06 PM

 58. MUUNGANO UMETUPELEKA SHULE WAZANZIBAR,TUNA KHOFU MARAHII KUPELEKWA CHUO KIKUU.
  MUUNGANO WA MKATABA,
  NDIO,WA MKATABA
  WA MKATABA BWANA.

  KWA SABABU TULIAMBIWA MUUNGANO NI SAWA NA KOTI,UKIHISI LINAKUBANA,UNAVUA,LAKINI MBANO WENYEWE SI WA KOTI!!! NI WA SURUALI ILIOKAMATANA VYEME NA MWILI.HALIVUKIIIII.
  HATA UKITUMIA NGUVU LITAKUSHINDA KULIVUA.NAAM
  WA MKATABA TUUUUUUUUU….

  KIM

  July 3, 2013 at 5:49 PM

 59. Muungano wa serikali mbili: sahani moja ni yetu sote; sahani ya pili ni yangu mwenyewe. Serikali moja: sahani moja tupiganie wote, usiposhiba shauri yako. Muungano wa serikali tatu:. Kila mmojawetu ana sahani yake lakini akiba. yetu sote iko salama kwenye jungu la pamoja. Serikali. Tatu si lazima ziwe na maraisi watatu ila inaweza kuwa na rais mmoja wa muungano mwenye makamu wawili. Asemaye serikali tatu ni ghali anafumbia macho jinsi serikali mbili zilivyo ghali kwa upande wa bara.

  dr mkangare medard minja

  July 5, 2013 at 1:00 AM

 60. great great Zitto! I support you indeed

  Raphael Mbogo

  July 7, 2013 at 3:44 PM

 61. nisaidien jins yakudownlod rasm ya katba mpya najarib inashindikana

  muhoja

  July 18, 2013 at 1:51 PM

 62. MVUNGI WE SHALL MISS YOU THEN,OUR LEARNED BROTHER.

  LIBE RUGIGA

  November 19, 2013 at 8:34 AM

 63. mwanzo mzuri,hongera Tume ya Jaji warioba…

  Emmy Nyuma

  December 31, 2013 at 1:50 PM

 64. kwanza naomba swala la serikali tatu lifutwe kabisa hata kama mnasema watanzania wanataka serikali tatu. naomba tujue ni asilimia ngapi ya watanzania wanataka hizo serikali tatu kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume kwa kweli wale watu laki tatu walio toa maoni ni asilimia sitini tu waliongelea muungano kwa watu wanaojua hesabu wakikokotoa vizuri kwa bara na visiwani ni watu 38000 wameongelea mambo ya muungano sasa jamani hawa wengine laki tatu na ushee hawajaongelea mambo ya muungano kabisa sasa iweje mseme wengi wanataka serikali tatu lazima tutumie akili jamani
  mimi ni Apoly Temu

  apoly

  January 5, 2014 at 11:43 AM

 65. kama mtanzania , mimi maoni yangu ni kuwa na serikali moja.kwa nini tunaogopa ?tunahitaji kusonga mbele na ndipotutakuwa tumemuenzi Baba wa Taifa.taifa linalokuwa kiuchumi ,kijamiii ni lazima pia likue kifkra na serikali moja ndio muda wake rejea wenzetu USA,GERMAN,USSR kwa uchache tu,wabogo ni waoga wa mabadiliko kwa nini? silas manyonyi mauna (the radical)

  silas manyonyi

  February 11, 2014 at 8:09 AM

 66. rasim ni nzuri suala la rushwa nalo liwekwe waz na mafisadi nao tujue hatima yao sawa selkar inaandaa wazawa wa kumiliki uchum lakini tunaumia sana.

  john malale

  February 28, 2014 at 9:30 PM

 67. serekali iwe makini na elimu ya tanzania

  junior naga

  March 1, 2014 at 12:49 AM

 68. Nahitaji copy ya katiba mpya

  kassim juma

  March 8, 2014 at 4:18 PM

 69. serikali tatu hapana tunapmba sdrikali ziwepo mbili kama ilivyo hivi sasa kuendelea na fursa zilizopo hivi sasa

  dr julius eliabu

  March 21, 2014 at 5:13 PM

 70. Sijaona haki ya mwanaume,pia swala la rushwa halijazungumziwa kinagaubaga.

  Festo Benjamin

  April 1, 2014 at 10:52 PM

 71. good plan

  mayai shedy

  April 7, 2014 at 11:16 PM

 72. if our words and plans about 3gvnt are heard and examined by outsiders{states} may be considered as loosing direction of Tzns bye creating negtv perspectives sp let’s be smart!and stop kidding..

  mayai shedy

  April 7, 2014 at 11:52 PM

 73. Jaman ee hebu jaribun kuangalia katika sekta ya elimu maana tanzania elimu ipo kisiasa zaidi ilituweze kuboresha hii sekta.

  Lackson wiliam

  April 15, 2014 at 12:36 PM

 74. KWA KWELI KULINGANA NA MAELEZO YA MWENYEKITI WALIOBA MIMI NAUNGA MKONO SERIKALI TATU.KWA UKWELI NDO ZINAWEZA KUMALIZA MIGOGOLO IYOPO

  GIDEON MUGISHA KILYANGA

  May 1, 2014 at 6:55 PM

 75. Jamani viongozi wetu mezani kwanza!ila mipango yote inayohusu maendeleo ya nchi yazingatiwe tena sana,Tunawaombea viongozi wetu wawe na umoja na hata hayo maendeleo yatakuja.

  RIGHTMAN MASONDOLE

  May 25, 2014 at 8:41 PM

 76. Swala la ziwe ngapi serikari nijambo ambalolingeachwa kwa wananchi, mie ninachotaka tuyatazame matatizo sugu yanayotutesa. Yako bayana, Umaskini uliokithiri, unyang’anyi wa rasilimali unaofanywa na wazungu kwakushirikiana na viongozi wetu, uterekezwaji wa sekta ya Afya na Elimu, kuporomoka kulikozidi kipimo kwa sekta ya kilimo, dharau inayooneshwa na serikari kupitia viongozi wake kwa wakulima na wafanyakazi in mbaya saana, na hili likomeshwe kwenye katiba ijayo. Upande wawalimu wetu, kuwe na wizara ianyojitegemea kwa ajira, na uongozi, na idara ya Fya pia. Raisi asipunguziwe madaraka, ila tunamtaka mew he maamuzi haswaa.

  Mpemba Suleiman.

  July 4, 2014 at 8:25 AM

 77. Swala la ziwe ngapi serikari nijambo ambalolingeachwa kwa wananchi, mie ninachotaka tuyatazame matatizo sugu yanayotutesa. Yako bayana, Umaskini uliokithiri, unyang’anyi wa rasilimali unaofanywa na wazungu kwakushirikiana na viongozi wetu, uterekezwaji wa sekta ya Afya na Elimu, kuporomoka kulikozidi kipimo kwa sekta ya kilimo, dharau inayooneshwa na serikari kupitia viongozi wake kwa wakulima na wafanyakazi in mbaya saana, na hili likomeshwe kwenye katiba ijayo. Upande wawalimu wetu, kuwe na wizara ianyojitegemea kwa ajira, na uongozi, na idara ya Fya pia. Raisi asipunguziwe madaraka, ila tunamtaka mwenye maamuzi haswaa.

  Mpemba Suleiman.

  July 4, 2014 at 8:31 AM

 78. Katiba ni ya nchi kwa ajili ya wananchi wake wote. Kosa lililofanyika mpaka sasa ni kutaka kuhodhi katiba iwe ya chama, hususan CCM. Tulifanya kosa kubwa kuwaamini wanasiasa watutengenezee kaiba bora!? Bunge lililopo sasa si la katiba, ni la siasa. Kinachotakiwa ni kulivunja na kuunda jopo la wataalam wenye weledi ili waiangalie rasimu hiyo, hata kama tutaipata baada ya uchaguzi ujao. Tusipoziba ufa sasa tutajenga ukuta….

  Joseph Mwandambo

  July 19, 2014 at 8:54 PM

 79. Bado kabisa. Katiba haijaeleweka

  gilbert

  September 20, 2014 at 1:31 PM

 80. mchakato wenyewe mzuri lakini watanzania waeilimishwe vizuri kuhusu rasimu hii na faida zake kwa wananchi

  buluba mayenga

  November 1, 2014 at 1:47 PM

 81. Kama Katiba Ya Nchi Inasema Mtoto wakike mwenye umri chini ya miaka 18 akiingiliwa kimapenzi na mvulana inasema amebakwa,je ni kwanini katiba yetu inamzungumzia mtoto wakike pekee bila yakumzungumzia mtoto wakiume?na kwa hali ya sasa mtoto wakike kuanzia umri wamiaka 13 hadi 17 huwa teyali anakuwa na mtoto au kashakubuu kimapenzi..serikali naomba itazame nakuwasaidia watoto wakiume maana tabia hii yaukandamizaji ishakuwa endelevu pia imekuwa kama chanzo chakupato kwawale wenye watoto wakike

  fadhili ngabuja

  November 3, 2014 at 1:41 PM

 82. Tanzania Siasa tunaziingiza hata mahali panapohitaji umakini wa hali ya juu sana. Suala la katiba ni suala nyeti sana inatakiwa kila mtanzania kuwa na nia moja kwa maana hiyo haya makundi sidhani kama tutafika mahali inatakiwa kuwa kitum kimoja. Hata kama kunakukinzana ktk hoja zetu ila umoja unahitajika sana kwa kujenga Taifa lenye mwongozo mpya.

  Abson Mhanje

  November 4, 2014 at 10:17 AM

 83. Reblogged this on massungoo.

  massungoo

  February 6, 2015 at 1:04 PM

 84. katiba haijazingatia maadili ya viongozi,inatakiwa kabla ya kura ya maoni maadili ya viongozi yaingizwe ili kukwepa mambo ya escrow,epa n.k

  John mwacha

  February 28, 2015 at 8:45 PM

 85. Hii katiba mimi ninavyo iona ni nzuri sana, kwani inamjali kila Mtanzania,.

  Ezra Protas

  June 16, 2015 at 4:44 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: