Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

TAIFA LINA NYUFA

with 14 comments

TAIFA LINA NYUFA

NDUGU  KABWE Z. ZITTO, MB – BUNGENI TAREHE 6 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia leo katika mjadala huu muhimu sana.

Hapa Afrika kulikuwa  kuna nchi, na bado ipo, inaitwa Ivory Coast. Ilikuwa ni nchi ambayo inasifika sana kwa amani na utulivu;  na  ilikuwa ni nchi ya kupigiwa mfano.  Leo hii Ivory Coast imegawanyika vipande vipande. Ukienda leo Ivory Coast unakuta wanaoitwa Ivorite na wanaoitwa wageni ambao wazazi wao walienda Ivory Coast kufanya kazi miaka mingi sana.  Lakini pili katika mgawanyiko huo kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kidini kati ya watu wa Ivory Coast wanaotokea Kaskazini na watu wa Ivory Coast wanaotokea Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa tuna Sierra Leone nchi ambayo wageni walikuwa wanakirimiwa katika hali ambayo haijawahi kutokea hapa duniani.  Lakini leo Sierra Leone ina rekodi kubwa sana ya watu wenye ulemavu kwa sababu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Naomba nichukue nafasi hii kufuatia matukio ambayo yametokea hivi karibuni na hasa jana na siku zilizopita ninanukuu hotuba ambayo Rais wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa  Benjamin Mkapa aliitoa katika Bunge hili tarehe 4 Novemba, 1998.  Alisema:

Mr. Speaker, after three years of my presidency, I can dare to modify the words of famous Zanzibar maestro Siti Binti Saada by saying, Tanzania is a good country, let one who wishes to come do so.  God has showered blessings on our country.  It is a country of unity, peace, love, rejoicing and exciding generosity.  It is a country of people who love equality and justice.  Our national unity brings from our firm believe in equality of human beings before God and before the Law.  A Unity reinforced by correct policies of national building.  Policies based on the principles of social justice, peace, harmony and development for all.  A unity which is extra sensitive to policies, statements behavior and actions which may sore seeds discard hatred and suspicious among Tanzanians”

Mheshimiwa Mwenyekiti sitatafsiri.  Lakini naomba kila Mbunge ajiulize leo iwapo Rais Mkapa tukimpa fursa ya kuja kuhutubia Bunge hili anaweza akayatumia maneno haya tena?  Hakuna mtanzania yoyote anayeweza kuthubutu  leo kutumia maneno haya tena kwa sababu nchi yetu ina nyufa. Ina nyufa ambazo kwa kujua au kwa kutokujua sisi kama watu ambao tumepewa wajibi na wananchi wa kuitunza nchi hii na kuipeleka  pamoja tumejikuta tukiingia katika kutoa kauli, maneno na vitendo ambavyo ni “irresponsible” vinavyopelekea kugawanya nchi; na yanayotokea sasa ni matumizi ya nyufa hizo.

NDUGU  KABWE Z. ZITTO

Asubuhi hapa Mheshimiwa Lissu amesema, ametoa rekodi ya namna ambavyo  wanasiasa wa chama kinachoongoza (CCM) wamekuwa wakitoa kauli dhidi ya vyama vya upinzani kuhusiana na masuala haya ya kidini.  Wametoa mfano kuhusu chama cha CUF kilipoitwa chama cha waislam, wamekitolea mfano kuhusu CHADEMA kinavyoitwa mpaka sasa chama cha wakristo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana ikawa ni rahisi sana tuka-“point fingers” kwa wenzetu nyie, ni rahisi sana; lakini CUF wakati wanaitwa ni chama cha waislam ambao walikuwa hawaitwi ni   chama cha waislam hawakunyoosha mkono kupinga.  Wakati CHADEMA kinaitwa cha cha Kikristo ambao hawaitwi hivyo hawakunyoosha mkono.  Matokeo yakeni nini?  Tumejenga hofu kubwa sana katika Taifa na  hii ni lawama kwa wote.  Wote kama nchi ili tuseme kwamba hapa tumekosea na tuanze upya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, adui anapokuja kwenye nyumba anaangalia ni wapi ambapo ni rahisi kamba kukatika. Tumeji-“expose”, tumejiweka wazi.  Leo mtu anayetaka kuishughulikia Tanzania ata-deal na udini tu.  Kwa sababu anajua watanzania hivi sasa wamegawanyika katika misingi hiyo.  Jana limetokea tukio  Arusha, angalia kwenye mitandao  ya kijamii mara moja watanzania wenyewe kwa wenyewe na ukiangalia majina ya watu wanaojadiliana wanaanza kusemana kwa dini zao.  Ndiyo hatari ambayo tumeifikia;  na ndio  anachokitaka adui.  Ni hicho.  Atakuja, wanaitwa “Agent Provacateur”, watapiga, mtabaki mnagombana ninyi.  Tukiruhusu NYUFA hizi ziendelee hatutakuwa taifa.  Ni lazima sote kwa pamoja tusimame imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua wakristo.  Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii.  Waislam na wakristo wa nchi hii ni wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni “very irresponsible” tunawagawa watu wetu na ni lazima tukatae hali hii.  Tunafanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima twende mbele. Kwanza ni lazima sasa Serikali ijenge utamaduni wa kufuatilia “grievances” zote ambazo wananchi wanazo bila kujali dini zao.  Pili turuhusu watu kuwa huru kusema.  Nimesikia hapa watu wanasema kwamba maandamano ni tatizo nakadhalika.  Maandamano si tatizo, ukimzuia mtu kuandamana akiweka hasira zake kesho atafanya nini?  Atatoka na bomu.  Turuhusu “honest discussions” miongoni mwetu kama wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni lazima sasa tuseme ya kwamba ni marufuku kuwa  na kauli za chuki “hate speeches”.  Kama hatuna vipengele vya kisheria tutunge sheria kwa sababu kumekuwa na “hate speeches” nyingi sana katika hii nchi na hakuna hatua ambazo zinachukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za uendeshaji wa mambo ya kidini.  Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika.  Leo hii Serikali ikitaka kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita BAKWATA.   Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji wa shughuli  za kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namaliza kwa kusema nchi hii si ya waislam peke yake, nchi hii si ya wakristo peke yake. Nchi hii si ya CCM au ya CHADEMA, CUF au ya NCCR-Mageuzi au TLP na kadhalika.  Nchi hii ni moja, nchi hii ni ya Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania.  Lazima wote tusimame kuhakikisha tunailinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana asante.

Written by zittokabwe

May 7, 2013 at 8:04 PM

Posted in Tanzania, Zitto Kabwe

Tagged with

14 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. ilianza kama hoja katikta kampen kwamba hawa wana udini msiwachague matokeo yake ndo hayo………., kweli aliwazalo mjinga ndo litalomtokea…………… mungu tuepushe na majanga

  frank amedeus

  May 7, 2013 at 8:50 PM

 2. Reblogged this on Msafiri Kitumbo.

  msafirikitumbo

  May 7, 2013 at 9:18 PM

 3. Niliwahi kusoma article yako kwenye RAIA MWEMA regarding religion matters in Tanzania. This is the additional of what you said on RAIA Mwema. We should stand as Tanzanian and not as a Muslim or christian.

  Sultan Rajab

  May 7, 2013 at 9:27 PM

 4. Big up’ Mheshimiwa kwa hoja yenye mantiki!

  Francis Runyota

  May 7, 2013 at 9:38 PM

 5. Mr. Zitto, I closely read your speech which you just posted and I was impressed with the content of the arguments raised, and also a bit puzzled by the angle which you addressed this volatile issue.
  First, I was impressed in a way that you realized we do have a problem, and given the nature of the problem, you were actually courageous enough to come forward and address it despite the top leadership in our country being quite . With a topic of such nature, is unlikely for most people to find a balanced angle to reason from without stirring more chaos, but your speech seemed to a greater extent establish a well-reasoned argument.
  However, I was a bit puzzled that in a way you exploited this topic for some reasons I am only speculating. The blame for recent religious should not entirely lie upon leaders who you perceive as fueling the chaos by their “hate speeches”. This problem is mainly caused by certain extremist elements within our various religions. I by no means mean extreme in a sense of abiding to the strictest of their religious pillars, but rather extreme in myopic application of their views and will upon other people in a society which is supposed to be respectful of each other views. The role of curbing this issue should be entrusted to religious leader to lead their flocks into the correct interpretation of the scriptures and at the same time our government should do more to ensure the citizens fully comprehend the meaning of “religious-less” country. With 60% of our supposed “elite” citizens failing to make to the basics of a secondary education, how do we intend to have a population of people who comprehend the meaning of living in a “modern” society where personal freedom which is stipulated by the governing rules flourish? Although this linkage might sound as a leap in trying to explain the recent chaos, but with close analysis which I can not offer here, all this issues are linked in an intricate way.
  I can go further debunking the angle at which you attacked this issue but I would be naive not to acknowledge despite the few flaws in your speech(in my opinion), you are actually one of the few people who had the guts to come forward and speak it out.
  God bless Tanzania.
  Dennis John Salewi

  Dennis John

  May 7, 2013 at 9:39 PM

 6. Haya ndio yanayotakiwa kuzungumzwa katika kulinusuru taifa hili halali kwa Utanzania wetu. hoja na mantiki ya mchango wa wa mh Zitto unalenga kujenga utaifa, utanzania ambao utakuwepo siku zote hata kama watanzania wote waliopo sasa wata toweka. Leo kulikua na kongomano la namna ya kusuluhisha migogoro ya kidini mkoa wa Dar. haya yangesemwa pale ilingekua sawasawa pia. Walio itwa pale hawana kitu cha kushauri ni njia ipi inafaa kutatua migogoro hiyo. wenye kutoa ushauri mzuri na hoja za kuongea hawana uwakilishi, hawatakiwi, na hawapewi nafasi ya kusema wakasikilizwa. kwa kiwango kikubwa haya ndio yanayo changia nyufa kutokea kwani wasipopewa nafasi ya kusema sehemu rasmi watasema sehemu zisizo rasmi na hivyo kuzua tafsiri potofu. Wakristo kwa uwakilishi wao halali “legitimate representation” waseme yanayo wakera na waisalmu hali kadhalika na pia wasio na uwakilishi wapewe nafsi waseme yanyowakera. hapa tutapata suluhu endelevu yenye kujenga utanzania endelevu. kwenye makongamano kama hayo waitwe watu kwa uwakilishi halali hata kama hawatkiwi huenda wakasema maneno yanayo takiwa. Ushauri wangu kwako Zitto usiogope Padri, Askofu, Sheikh au mchungaji katika kusema ukweli. wapo Maaskofu na mashekh wanaongea mambo ya hovyo ambayo haya leti mustakbali mzuri wa Taifa letu. mafano wa maneno kama vile …….nchi hii haita tawalika, Tunatawaliwa na kanisa….na mengineyo mengi. Tafadhali wenzetu wenye sehemu za kusema , hebu yaemeni haya.

 7. Ni kweli kaka una akili ya kipekee mshukuru mungu kwa kipaji»wengi huwa wanacnzia 2 hapo mjengoni!bg up,

  amir amanyike

  May 7, 2013 at 11:13 PM

 8. Mwenye sikio amesikia maneno mazuri na ya busara cha muhimu ni kuyafanyia kazi kwa uzito wake la sivyo taifa litapasuka.

  Meshack Osiah

  May 7, 2013 at 11:40 PM

 9. umeliangalia kwa jicho la upekee kabisa na umenena jambo ambalo lina utata miongoni mwetu kama muumini wa dini ya kiislam watu wengi hawaamini kama una uthubutu wa kauli zenye mtazamo wa umoja na mshikamano.leo tujiulize bakwata ni nani?na kkt ni nani?kama bakwata ni mimi na wewe na hali kadhalika kkt vivyo hivyo basi hatuna budi si kutupa lawama bali kuangalia hayo yanayosemwa ni malalamiko na kuyafanyia kazi.kama mlivyo hapo bungeni,mpo kwa maslahi ya taifa na si chama

  Ally Mambo

  May 8, 2013 at 9:36 AM

 10. kaka unasema kweli sana ila baadhi ya viongozi huwa hawaoni haya kawasababu tu ya utashi wa vyama vyao na wakimaini yote yanosemwa ni propaganda za kisiasa. please kiongozi endelea kusema ukweli siku moja wataelewa siku ambayo hapatakuwa mheshimiwa bali wakimbizi.

  haruna

  May 8, 2013 at 12:49 PM

 11. realy he’s blessed

  sadock

  May 8, 2013 at 1:49 PM

  • Ulichosema ni kweli tupu. Kitendo cha wakati wa kampeni wanasiasa wengi hasa wa ccm kwenda makanisani na misikitini kuomba kura kwa kutoa michango ya ujenzi hakikubaliki. Kinawagawa sana watanzania iwe marufuku.

   abas

   May 9, 2013 at 12:21 PM

 12. mheshimiwa umeongea mambo ya busara sana. ningeshauri ninyi wabunge mngekwenda mafunzo kidogo ili baadhi yenu mjifunze kauli za kuongea kwenye public. inasikitisha sana kusikia kauli za baadhi yenu mnazozitoa kama za mitaani tu. jana nilimsikia mh. spika akitoa kauli alipotembelea majeruhi arusha ambayo kwa upande wangu naona nayo ni kichocheo vilevile. hajifunzi tu jamani?mbona kauli zake ni nyepesi mno? ana-hint kwamba mabomu yaliyopigwa ni kitendo cha wafuasi wa chama fulani… na ndio umekuwa msimamo wa wabunge wengi wa ccm. jamani, tuache politicalaffiliations tunaposhughulikia mambo ya kitaifa.

  angalia pia para fulani umesema mambo ya maandamano…. kwamba mtu ukinyimwa uhuru wa kutoa mawazo yako au kuandamana, basi unatengeneza vibomu. mara kwa mara ni CDM ndiyo wamekuwa wakinyimwa hiyo haki. je, ina maana ni wao ndiyo waliofanya vitendo hivi? SI KWELI! EBU TUWAZE NJE YA BOX…… kwa nini haya matukio yamezidi sasa? SABABU NI OMBWE LA UONGOZI

  Bebe

  May 9, 2013 at 12:15 PM

 13. Excellent speech ever heard before, muhimili wa umoja wete kama Taifa umechezewa sana na tusipoangalia kama taifa tutakuja kujuta sanaaa. Baba wa Taifa aliseme Kiongozi aliyefirisika kisera atajihalalisha kwa dini yake, kabila lake, ukanda anaotoka. Na hili tumeliona kama Taifa kwa baadhi ya watu kutafuta kura kwa kutumia dini zao which is extremely very bad.

  Vita au chuki za kidini hakuna mshindi.

  david

  May 10, 2013 at 5:44 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: