Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

PRESS RELEASE: ‘SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’-SIO KWELI

with 74 comments

‘SIRI YA KUUAWA ZITTO’

Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘ SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.

Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

Nne, Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.

Kabwe Zuberi Zitto, Mb

Dar-es-Salaam

Jumatano, Machi 27, 2013

Advertisements

Written by zittokabwe

March 27, 2013 at 3:21 PM

74 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Asante kwa ufafanuzi kamanda.

  Felix.

  Felix Mpozemenya

  March 27, 2013 at 3:25 PM

 2. “Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu.”
  Well sais, nafikiri apo message ime pita sawa sawa…

  Santa

  March 27, 2013 at 3:29 PM

  • i real admire you Zitto,keep it up brother……

   frank jasper lyimo

   March 27, 2013 at 3:58 PM

   • i appreciate you Zitto,Tunajua huyo Shonza nam wenzie huko CCM ndio wanatunga hizi propoganda ila za Miwizi 40,2015 watakiona cha mtema kuni!Gog Bless u Brother

    Jimmy

    March 29, 2013 at 7:40 AM

 3. asante kiongzi kwa kutuhabarisha vyema

  richard makoi

  March 27, 2013 at 3:45 PM

 4. Umoja ndio nguvu

  Mwasumbi Sekela

  March 27, 2013 at 3:46 PM

 5. Thanks kijana, simamia ukweli , achana na siasa Za kuchafuana

  Ugomvi mwiko

  March 27, 2013 at 3:51 PM

 6. mipango ya kuyumbisha chama lakini hawawezi

  simon duhia

  March 27, 2013 at 3:52 PM

 7. We believe in People’s power and Solidarity! Mungu 2saidie!

  Frank

  March 27, 2013 at 3:52 PM

 8. umenifurahisha ulivyosema “Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama.”,,,,PAMOJA KAMANDA

  Frank Robert

  March 27, 2013 at 3:52 PM

 9. Ahsante sana mkuu, nimekuelewa, na ninaomba ni-share kwa fb friends ili ujumbe huu muhimu umfikie kila mtu, if possible. Hongera kamanda kwa kuwa muwazi, na ninahisi hili gazeti hatua zichukuliwe dhidi yake!

  Sylvester

  March 27, 2013 at 3:55 PM

 10. A luta Continue

  Ibrahim Peter

  March 27, 2013 at 4:08 PM

 11. Asante sana kaka.kwa maelezo stahiki kabisa!tunashukuru sana! Mungu akubariki sana na kukuongoza daima!

  sanze kibugwa

  March 27, 2013 at 4:11 PM

 12. mkubwa huo ndio uweneume na mweneume kamili uwa habandili msimamo,wake mungu ndio kali kitu hata kama watafanya wanavyo taka bali mungu anaweza kukuepusha

  juama

  March 27, 2013 at 4:16 PM

 13. Tunashukuru kwa kusema ukweli maana hili lingeweza kuanzisha mwanya wa wanafiki na wanzandiki wasio ipenda CHADEMA kuzidi kuweka mpasuko usio na maana katika chama kisicho wahusu…. CHADEMA oyeee

  gabriel michael

  March 27, 2013 at 4:17 PM

 14. Zitto,nakupendea hapo tu!una msimamo sana.yani bila kutangazwa mtu mwenye akili anaweza kujua wewe unaijua siasa and how to control people and uaself.Zitto hizo ni propaganda za kutaka wewe usielewane na wenzio ktk chama ila nachokuomba,na ninawaomb viongoz wa chadema,haya maneno maneno ya pemben yasiwatenganishe hata siku moja.ukiona kiongoz kahamia chama kingne ujue huyo hajui lolote ANAJARIBU KAMA ATAWEZA!ukweli chadema nawapenda sana!ila msiwasikilize wa pembeni.

  Sarah William

  March 27, 2013 at 4:17 PM

 15. Kamanda umesawazisha vilivyo…nawale wenye kuwashwa na midomo yao sasa waham,ie kwenye taarabu kwan hili ndio hitimisho la kamanda wetu Naibu katibu mkuu na naibu wa kambi ya upinzani..
  Peopleeees power never turn back..!!

  John JK......Phnx Ars Branch

  March 27, 2013 at 4:25 PM

 16. Congratulationr mr mp!

  denice bongole

  March 27, 2013 at 4:25 PM

 17. Unachosema ni kweli. Siku hizi wanahabari wanatuchangaya sana, propoganda ni nyingi kuliko ukweli

  ANDREW MASSAWE

  March 27, 2013 at 4:27 PM

 18. “Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti.”
  “Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa
  anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu.
  Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho.”
  “Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.”
  “Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama.
  Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama.”

  warda

  March 27, 2013 at 4:31 PM

 19. Mtu,anafikiria,kuwa,kumuua,zitto,ndio,furaha,ya,maisha,yake,atakua,anajidanganya,tu,maana,zitto,anaweza,kufa,kimwili,lakini,MAWAZO,FIKRA,na,MAONO,ya,zitto,yataishi,tu.Siogopi,kufa.”ASANTE,KAMANDA,KWA,WENYE,AKILI,WATAKUELEWA,SISI,SOTE,NIWAJA,WA,MUNGU,NA.MALEJEO,NI,KWAKE,HAKUNA,ATAKAEBAKIA,ANALINDA.DUNIA.mwenyezi,mungu,akupe,afya,njema,akuepushe,na,mabalaa,ya,hii,dunia,akuwekee,wepesi,kwa,kila,jema,unalolifikiria.

  Ami kabwe

  March 27, 2013 at 4:31 PM

 20. Naam kiongozi bora anachukua hatua haraka wananchi wa kawaida wasichanganyikiwe ila tunaopitia mitandao niwachache. So wengi hasa kule kwetu same masharik watachelewa kuupata ukweli

  mbike.j.mashauri

  March 27, 2013 at 4:35 PM

 21. Watashindana lakini hawatashinda.LAKINI MH.YAFAA KAJIULIZA NIKWANINI MASHAMBULIZI MENGI YANAPITISHWA UPANDE WAKO?

  God Shuma

  March 27, 2013 at 4:36 PM

 22. Pole sana muheshimiwa ZITTO ZUBERY KABWE kwa yote yaliyojiri.
  Ila kwanini vyombo vya habari vinakuwa na uwongo kiasi hiki?.
  Mimi kwa ushauri wangu inabidi visafishwe nihayo tu asanteni sana wachangiaji wenzangu.!

  Mubarak Lusonzo

  March 27, 2013 at 4:45 PM

 23. Kaka naomba usiwe na wacwac kabsa hy ni imeandaliwa na wapinzani we2 wa kisiasa wakijaribu ku2gawanya ila ninachomshkuru mungu umeitambua hl na umekua na maamuzi ya busara na yenye kulenga shabaha ya kujenga chama che2 badala ya kuharibu . Mungu ata2ongoza 2tende kaz kwa matakwa ya mungu 2 na 2simamie ukweli na haki sku zote.from kara2

  Leonard Diyay

  March 27, 2013 at 4:48 PM

 24. Yes hapo umelonga ndugu yangu,ufafanuzi mzuri ila chukua hatua zaidi ya hapo. Usipuuze tahadhari ingawaje umesema huogopi kufa kwakuwa “umechagua kazi hiyo na maisha haya”

  bethuel nyudike

  March 27, 2013 at 4:49 PM

 25. Wambie ukweli kamanda nakukubali ile mbaayaa

  Nestory kawimbe

  March 27, 2013 at 5:08 PM

 26. Pole sana kamanda wetu, zote ni hila! wanacho taka mfarakane nyie wakuu wetu, kwani tumesha litambua hilo, wanachama CHADEMA tushikamane kwa pamoja vita ni kali na tutawashinda tu 2015.

  Cherishi Mlambo

  March 27, 2013 at 5:21 PM

 27. Asante kwa maoni yako lakni kumbaka kwenye jopo la watu wengi apakosi kasoro, kujiamini ndio silaha ya mwanasiasa
  Mungu atakusimamia

  saimon gasper

  March 27, 2013 at 5:22 PM

 28. UMOJA NI NGUVU PAMOJA SAAAAAAAAAAAAAAANA MKUU.

  OPHOLO

  March 27, 2013 at 5:24 PM

 29. Umejibu kwa wakati muafaka na ninashukuru kwa kutuambia ukweli..lakini nashauri usiishie hapo, mwandishi wa habari hii ifikishwe kwenye vyombo vya usalama ili aseme taarifa hii aliipata wapi na alikuwa na dhamira gani kutoa habari hii…maana huu na ni uchochezi!!

  chris

  March 27, 2013 at 5:49 PM

 30. Hongera Sana kamanda Zitto kwa kutoa ufafanuzi maana wapo baadhi ya watu wasiopenda kuona taifa hili linakombolewa na watu walioonyesha nia ya kufanya hivyo. Chadema na Viongozi wake tuko imara dhidi ya propaganda chafu.

  Mutta Anselimi Adrian

  March 27, 2013 at 6:20 PM

 31. Weredi wa taaluma ya habari sasa unakwenda pabaya Tz !! umetoa jibu muda mwafaka so proud of you!!

  shabani

  March 27, 2013 at 6:34 PM

 32. kiongizi mapambano bado yansendelea uwe na moyo

  wa kiuongizi na kiushupavu tuko pamoja kiongozi

  haji mussa

  March 27, 2013 at 6:42 PM

 33. They are bankrupt of ideas that is the reason of employing intimidation to suppress your voice. You know, championing democracy, human rights and fighting corruption it is always accompanied with all sorts of threats. I think the time has come for opposition parties to unite and speak with one voice. Otherwise it will be difficult to achieve your aspirations. I agree with you, you have to continue with the good work your have been doing, to expose corruption and mismanaging of public resources by those in power. Unity is the main weapon for success. Today a read the news the government is signing 17 contracts with China worth of more than 14 billion USD. It worries me, this is being done without citizen input or dialog. How can this happen, because the future of the nation lies with new generation, creating huge debts to the nation without consensus by the public is wrong. Now I can understand why the government abolished POAC of which you was a chairman. Because you insisted every thing to be on the table, transparency, but they won’t let you do that. They prefer impunity with nobody questioning what they are doing. I read the news, someone is charged with TERRORISM for voicing different opinion. This is unbecoming of the government to start using threat in order to silence their critics. Tanzania is moving backwards. Democracy is valid only on the papers, in reality it is another story. Stay calm Mr. Zitto, the world is changing for the better and Tanzania won’t be excluded.

  Alex Kakala

  March 27, 2013 at 6:53 PM

 34. Kuna watu wanaotumia nguvu nyiingi kuhakikisha viongozi wetu wakuu mnakosana! Ila kwa msimamo wako wanapauka zzk bigup!

  Mbukaka kesi

  March 27, 2013 at 7:55 PM

 35. Well said , be blessed

  Mkuu Hanje

  March 27, 2013 at 7:57 PM

 36. Umeonesha uanasiasa kwanza nakupongeza kwa kutokukurupuka kujibu hili.

  Emmanuel asenga

  March 27, 2013 at 7:59 PM

 37. Nakupongeza kwa ufafanuzi mh.

  Emmanuel asenga

  March 27, 2013 at 8:01 PM

 38. Big up zitto simamia ukweli cha msingi achana na propaganda za watu!

  evarist

  March 27, 2013 at 8:23 PM

 39. Kabwe is one of the best politicians in TZ. Hii ni kwa kusimamia kitu anachokiona ni ukweli!! God bless you ufanye mabadiliko

  Abrahama

  March 27, 2013 at 8:23 PM

 40. siogopi kufa! Kwasababu maisha niliyochagua ndiyo haya yaliyojaa vitisho!!!
  (Kumbe vipo?? Usidharau ushauri wa watu Mungu akituma Malaika hajina mbawa zake, nikupitia kwa watu kama inavyotokea sasa!)
  Tanzania yetu imekuwa nchi ya ajabu sana tunaelekea kuwa kama Colombia na Mexico! Mwenye uwezo anafanya anachotaka, tuiombee nchi yetu!
  Wanasiasa muwe wakweli! Acha kutufanya watoto wadogo, Mh Kabwe siamini na sielewi kwanini unasema hayo!!! Eti haujui Lunch time Hotel ilipo?? Unaweza usiwe umewahi kuingia lakini unajua ilipo. Amani ya Bwana iwe pamoja nawe!

  edmond

  March 27, 2013 at 8:49 PM

 41. Mheshimiwa hongera kwa ufafanuzi wako makini.Watu waliopewa dhamana ya kuhabarisha watu wengine kuweni makini sana kuhusiana na habari mnazowalisha watu.Kabala ya kutoa habari tafakari uzuri na madhara ya habari hiyo.Tuelewe kwamba sio kila habari ni habari.

  Habari hii kuhusu njama za kuuawa kwa mh.Zitto hazina tofauti na baadhi ya video ambazo zimepostiwa kwenye mitandao na sasa zinagharimu watu.Swali la kujiuliza ni kwamba kama kweli hawa walioandika habari hizi walikuwa na uhakika wa habari hizo na wana uzalendo na upendo wa kweli kwa nini taarifa hizo hawakuzipeleka kwenye vyombo vya usalama?

  Tuwe makini sana na huu ulimbukeni wa sayansi na teknolojia.Sayansi na teknolojia ni mojawapo kati ya vitu vinavyochochea kasi ya maendeleo katika jamii zetu hivi sasa LAKINI tusipojua manufaa ya teknolojia basi tunayo hatari kuangamizana maana kila mtu atakuwa anatengeneza jambo lolote analofikiria hata kama si la kweli ili mradi kupotosha watu wengine.

  Napendekeza wizara inayohusika na masuala ya sayansi na teknolojia kuja na mikakati mipya kufanya udhibiti wa mitandao hii kama ilivyofanyika kwenye simu ili kutoruhusu matumizi mabaya ya teknolojia na watu wanaotumia mitandao wadhibitiwe kutumia majina yao ili waache kuandika mambo yasiyofaa na yenye kuwakwaza watu wengine.

  Mheshimiwa Zitto twakutegemea sana hasa baadaa ya kushinda uenyekiti wa kamati ya Bunge na tunayo matumaini makubwa na tuko wote, chapa kazi MWENYEZI MUNGU YU PAMOJA NAWE HAO WANAOZUSHA HABARI WATALIPWA KULINGANA NA KAZI ZAO.

  Jospide Majaba

  March 27, 2013 at 9:14 PM

  • hizi fitna wanazozipanga wanajulikana, ila ni wakati sasa viongozi, wanachama na wapenzi wote wa chadema kuwa pamoja kuliko wakati wote, wanajua ni hatari kwao mpaka 2015 chadema kuwa kama kilivyo sasa na wanalijua hilo ndio mana wanatumia hila na mbinu nyingi kukivuruga ili kionekane hakifai.

   Maxwell kweli

   March 28, 2013 at 10:29 AM

 42. pamoja na hivyo bado tuna hofu coz baadhi ya viongozi wenzako walishaanza vita na viongozi wa chadema toka Kigoma,walianza na Kabourou,Kafulila sasa nadhani zamu yako Zito. take care men!

  Hassan wa kgm

  March 27, 2013 at 11:05 PM

 43. Nakushukuru sana maana hao wazandiki na wanafiki wanatafuta njia ya kukufanya usielewane Katibu wako ili mambo yakwame.Maana kumbuka kila siku adui yako anakuombea njaa siku zote ili unyongonyee ili akutake over haraka.Simama imara jembe letu.I like you

  KANINGO GOLDIAN

  March 28, 2013 at 12:59 AM

 44. Ili kupima uwezo wa kiongozi bora ni lazima kuandaliwe mbinu mbalimbali za kumkatisha tamaa, kumchafua sana, kumchonganixha na marafiki zake wa karibu, na mengine mengi kama haya hivi ni vigezo muhimu xana katika kupima viwango vya uelewa wake. Huu ndo wakati muafaka wa zitto kuwaonesha watanzania namna anavyoweza kukabiliana na changamoto kama hizi hasa busara zake kama kiongozi makini.

  peter vitalis ojode

  March 28, 2013 at 4:52 AM

 45. Kweli mkuu,simamia haki mwanzo mwisho,kifo hupagwa na Mungu co bnadam,binadam yeye nimuwakilishi tu.

  Faraja

  March 28, 2013 at 8:16 AM

 46. Kauli zako mheshimiwa zimenigusa sana hasa juu ya suala la kutishiwa kuuwa najua kwa mtu mwingine ingekuwa shida.lakini umezungumzia suala gumu kwa njia ya amani.kila nafsi itaonja mauti na hakuna anaeelewa ni namna gani atakufa.hvy basi usiogope vitisho vya mtu zaidi sana ungeza ufanisi na juhudi zaidi.MUNGU ATAKULIPA Usipozimia kata tamaa.

  David msigallah

  March 28, 2013 at 8:39 AM

 47. BIG UP brother ZZK,napenda siasa za nchi hii,napenda misimamo uliyonayo,napenda namna unavyoendesha mambo yako,napenda na ni mwanachama wa CDM!you are my role model brother keep it up

  Tumaini

  March 28, 2013 at 9:16 AM

 48. Jamani watanzania tujiadhari na watu wanaotukaririsha ujinga.

  Jumahassan

  March 28, 2013 at 9:35 AM

 49. Great communications! Well done!

  Serge

  March 28, 2013 at 9:40 AM

 50. Hakika hutadhurika kwa namna yeyote mpiganaji wetu,Dua na Sala zetu zipo juu yako,Mungu ni mlinzi wako kamwe hatakuacha peke yako,mapambano bado yanaendelea.

  Fredie Mayeye

  March 28, 2013 at 10:17 AM

  • Hongera Brother Kabwe kwa kuwa siku zote daima hakurupukii mambo,na huo ndio uwanamume wa kweli,na unatuwakilisha vema sisi nduguzo wa lwama,kikubwa kaka jitahidi kuwa makini na mwangalifu kwani mafanikio yako kisiasa si kila mtu anayekuonyesha uso wa bashasha ni kweli anayafurahia.

   Binafsi post yako kutokana na kadhia hii imesheheni ukomavu na umakini uliyonao katika mambo yako…go ahead comrade! unatisha na unajua kucheza na fitna za kisiasa hasa katika ulimwengu huu ulojaa propaganda.

   Kapona

   March 28, 2013 at 2:43 PM

 51. Hao wanaozusha tuwaambie hiyo ndio mwisho wa akili yao na chama chao so wanapoteza muda kujadili chadema ila wajue tu chadema ni mipango ya mungu na hakuna wakukizuia kwenda ikulu 2015.mungu ibariki tz,wanachadema na chadema

  Donatus swai

  March 28, 2013 at 10:17 AM

 52. Mh.nimefurahishwa na kitendo cha wewe kuweka mambo makubwa kama hayo hadharan kwa tunaiamin CHADEMA sasa hizo taarifa zilitusononesha sana had kutaka kuamin CHADEMA imekuwa kichaka cha wahuni tu. MUNGU akuzidishie uelewa zaid

  Lumea Luis

  March 28, 2013 at 10:26 AM

 53. Kamanda Zito hayo ni maneno ya mkoswaji. Tunaamini ktk fikra na utendaji wako na ushirikiano mlionao nyie vongozi wa CHADEMA. Wala usiteteleke na kupata shida, siku hizi siasa zetu zimekuwa za Propaganda na kuzushiana mambo ya kiovu.

  Mkumbo

  March 28, 2013 at 11:52 AM

 54. Big up Mh Zitto

  Sweetbert Kalikawe

  March 28, 2013 at 12:31 PM

 55. ukishajitambua hutapata shida na walimwengu

  julius (@jubest2000)

  March 28, 2013 at 1:50 PM

 56. Nakushukuru sana juu ya kuliweka hili hadharani pengine watanzania twaitaji tambua ni mtaji wa nani kuhusu haya yanayovumishwa maana mwenye mtaji anaitaji vuna faida kutoka kati yetu tusiitaji kuwa mtaji wa mtu yeyote bali mtaji wa haki na usawa utakao liletea taifa letu maendeleo

  wanazuoni

  March 28, 2013 at 6:01 PM

 57. tunaelekea pabaya sana,mana itafika kipindi kila mwenye gazeti anakaa na kuandika chochote anachoona kila maslahi upande wake.

  malik

  March 29, 2013 at 10:02 AM

 58. It is believed that the one stands on the truth, often stands alone. courage and The Almight is with you.

  John Mitumba

  March 29, 2013 at 12:44 PM

 59. kwamujibu wa habari hii mh. zitto napenda kukushauri kuwa mwandishi wa habari hii afikishwe kwenye vyombo vya usalama ili authibitishie uma wa watanzania kuwa alicho andika ni kweli ili kukomesha watu wenye tabia kama hii kwani pamoja na ufafanuz ulioutoa uende mbali zaidi ya hapo ili kama ameandika kwa kuwanufaisha watu flani ijulikane maana inaleta ukakasi katika vichwa vya watu inawezekanaje mtu mwenye weledi na kazi yake afanye hivo? nadhani hii itasaidia kuto ruhusu watu wenye agenda kama hizo kutopata fursa ya kuzifikiria tena

  ABDULAZIZI SELEMANI

  March 29, 2013 at 2:20 PM

 60. Wanaodhani zitto msaliti wamepotea

  Elisante

  March 30, 2013 at 11:51 AM

 61. Mh. Zitto
  Ninakupongeza kwa kujibu na kutoa ufafanuzi kwa kitu ambacho umekiona si cha kweli. Hakika taarifa hizi zinashtua wengi (hasa wanaotamani kuona mabadiliko chanya kwa Tz). Ninaamini Mungu atakulinda na hila za maadui hawa; kwa kufuatilia kwangu kwa miaka 2 sasa; ninachokiona kuna mtu/ watu au kikundi ambacho kinachotafuta ni kumuua ZITTO si kKIMWILI bali KISIASA. Na niseme si Zitto tu anayetafutwa au viongozi wengine bali CHADEMA. Na hii ni mkakati maalum wakidhani kuwa kama wataiua CHADEMA basi fikra na kiu ya watanzania juu ya mabadiliko itakuwa imekufa. WAMEPOTEA SANA! NA WANAJIDANGANYA. Naishi na kufanya kazi vijijini; kila mkoa ninakopita nakutana na wazee na vijana, wanaume kwa wanawake ambao wamekata tamaa kabisa na wanatamani kitu fulani kifanyike. NA KAMA KITU HICHO (MABADILIKO) KISIPOTOKEA HAWANA HOFU YA KUAMUA VINGINEVYO.
  Bro Zitto mara nyingi nimeandika na kutahadharisha viongozi wa CHADEMA kuwa hizi taarifa zinazotolewa kila mara zina lengo la kuwatoa kwenye mstari wa kujadili. kuelimisha umma juu ya haki zao za msingi, kusukuma serikali ya CCM itekeleze wajibu wake, nk. Niliandika kupitia Bidii Forum mwaka 2008/09, nikaandika tena 2010!
  Maadui wa Tz wanataka CHADEMA (kwa kuwa ndio sauti ya umma wa Tz) mtoke katika mambo ya msingi muanze kunyukana ninyi kwa ninyi au mtumie muda kujibu hoja zao zisizo na msingi badala ya kujadili mambo ya msingi kwa mabadiliko ya TAIFA LETU!
  Kwa hili nina mtazamo wa aina mbili

  1. HUU NI MPANGO WA MUNGU ili muweze kuwabaini waliojiingiza kwa siri ili kuwafitini na kisha muwatoe au wajitoe nje.
  -Kusingetokea kilichotokea leo Shonza, Mataka (Meya wa Ilemela), Shibuda na wengine msingejulikana. Naamini sasa kwa kupitia Meya wa Ilemela mmejua ni aina gani ya viongozi CHADEMA iliwaweka katika uongozi na endapo mngechukua dola wangeendeleza ufisadi ule ule

  2. ADUI ZETU WAMEFANIKIWA:
  -Wamewatoa (CHADEMA na watanzania wote) kwenye agenda ya msingi -Fedha zilizoko USWISI, TATIZO LA MAJI, KUSHUKA KWA KIWANGO CHA ELIMU, nk na kuwaelekeza kujibu na kufuatilia haya:
  Dr Slaa na kadi ya CCM
  Zitto ana ukaribu na JK na anataka kujitoa
  Elimu ya Mh. Mnyika
  Dr Lwakatare na video ya ugaidi, nk

  Hasara ya haya ndio kama tulivyoona leo tumepoteza umeya wa jiji na manispaa zote mbili Mwanza. Leo tumeacha kujadili na kudai uchunguzi na taarifa juu ya mabilioni Uswisi na chenji ya rada!

  MSIFE MOYO, MUNGU BADO ANAMPANGO WA KUTENDA KITU KUPITIA CHADEMA

  Lugano E.J

  Edna J. Lugano

  April 2, 2013 at 8:55 AM

  • Isiku yakwanza hontegeleje izonkuru,ndalakanguse chane,Ila kwiko we nyene wiyandise ngaho
   Ntanoma braza kaza umusuli wi shavu ameneke mana bhagomba bhagukosanishe ni chama chawe,twetwe abhapiga kura nabhapenzi bhahambavu.BHAHINKONKO BHIJOLE.
   Nayo bhraza wibeleho

   Godwin Ndomoye

   April 3, 2013 at 8:04 PM

 62. NAPONGEZA KAULI YAKO NA MAELEKEZO YAKO MHE,ZITTO KABWE MBUNGE WETU, MAANA TOFAUTI ZILIZO KATIKA CHAMA CHETU IKIWA ZITAONDOLEWA CHADEMA ITAKUWA NA NAFASI KUBWA YA KUTUFIKISHA MAHALA TUNAPOPATAKA  NA CHAMA KITAKUWA KATIKA NAFASI YA KUONGOZA NCHI KWA SERA ZAKE.

  KAKA YETU  NA MHESHIMIWA WETU SISI WANA KIGOMA TUNAKUPENDA LAKINI PIA KUENDELEA KUONYESHA USHIRIKIANO NA UKARIBU KWA WANACHAMA NA WAPIGA KURA WAKO HUKU KIGOMA NI MOJA YA MAARIFA NA HEKIMA MUNGU ATAKAYOKUWA AMEKUJALIA NA TUNAKUOMBEA KUWA JUU ZAIDI YA HAPO ULIPO  KIMAAMZI NA KIUTENDAJI KATIKA TAIFA LETU.

  NINA IMANI KUWA  UELEWA WAKO NA UJASIRI ULIONAO HIYO NDO ASILI YETU YA WATU WA KIGOMA  NA  SISI NDO WATANGANYIKA  TUNAKUTAKIA KUTANGAZA SANA UTANGANYIKA WETU KATIKA TANZANIA.MWENYEZI  MUNGU AKUNUSURU NA HIRA  NA UPOTOVU WA SHETANI NA MAAJENTI WAKE TUFANYE KAZI KWA PAMOJA NA NCHI HII TUINUSURU.

  KWA MTAZAMO WANGU KWA SASA KULINGANA NA HALI  ILIVYO NCHI YETU YA TANZANIA NI BORA  ILIPOKUWA  CHINI YA UTAWALA WA WAKOLONI KULIKO SASA HIVI,MAANA KWA SASA NCHI INAONEKANA KUWA KOLONI LA WATU WASIOJULIKANA WAZI  KWA WANANCHI,HAKUNA HATA ASILIMIA 30%KWA  MWANANCHI WA TANZANIA ANAYEWEZA KUSEMA KUWA ANA FURSA  ASILIA MUHIMU  ZA KIMAENDELEO KATIKA NCHI YETU .MAANA MAKABURU WALIOFANYA VIBAYA AFRICA KUSINI KWA KUJUA  NA KUWA UWEZO WA KIUTESAJI NA UUAJI NDIO WATENDAJI NA WALINZI WA MIGODI NA UHALISIA UKO WAZI KWA WAKAZI WA NZEGA ,RUNZEWE,USHIROMBO N.K/SIYO HAPO TU MIKATABA YA USHIRIKIANO WA AFRICA MASHARIKI,CHINA N.K  YOYE HIYO KWA TANZANIA SISI WANANCHI WA CHINI BADO TUMEUZWA BEI NYANYA KWANI WATANZANIA WENGI HATUKUANDALIWA KUWA NA USHINDANI KATIKA NYANYA YOYOTE YA KIMAENDELEO KATIKA BIASHARA,KILIMO,UWEKEZAJI N,K.NDIYO MAANA HATA  MADAMPO YA TAKA TAKA TENDA WANAPEWA WACHINA MFANO HUO NI HAPA KIGOMA IKO INAFANYIKA HIVYO,BIASHARA  YA AINA YOTE NDOGO NDO NA KUBWA WACHINA WANAFANYA HIYO IKO WAZI DAR NA KWINGINEKO MNADHANI MWISHO WA SIKU  NI NINI?

  ZAMANI TULIJUA KUWA WAJERUMANI WAMETUTAWALA NA WAKATUWEKEZA KWA WAINGEREZA  LAKINI HATUJUI  HASA MIMI NATAWALIWA NA NANI,HII NI KWA VILE NAONA  MADINI TUMEMILIKISHA WA WEUPE YOTE NA KILA TUNAPOYAGUNDUA KWA BAHATI NA SIBU MAANA HATUNA VIPIMO WAWEKEZAJI  WANAITWA HARAKA NA KUKABIDHIWA,MWISHO WA SIKU TUNALETEWA VYANDARUA TU TENA VINGI VILIVYOCHOAKA MADINI YA DHAHABU,TANZANAITI,ULENIAMU,ALIMASI,PATNAMU NA MENGINE MENGI SANA.KIGOMA HIII YA KWAKO MHE,TANGU MWAKA 1930 KWA HISTORIA NILIYONAYO WAZUNGU WANACHIMA MADINI  KATIKA KATA YA IGALULA  NA INASEMEKANA KUWA WANATAFITI TU SIKU WAKIJUA   KIASI CHA MADINI YALIYOPO WAFUNGUA MGODI JE TOKA MWAKA WA 1930 HADI 2013 HII HUO UTAFITI NI WA NAMNA GANI NA UWANJA WA NDEGE WALISHA JENGA ILI KUBEBA MALI ZETU?KWA KUFICHA UBAYA WAO WANAOUFANYA NA HAO WANAOCHIMBA NAO KATIKA WAHUSIKA NDANI YA NCHI YETU BARA BARA HAWAZIJENGI KWA NAMNA YOYOTE WACHIMAJI HAO HUFANYA KAZI MUDA  ULE MVUA ZINAPOANZA KUPUNGUA NA KIANGAZI TU.MVUA ZIKINYESHA NA KUKOLEA WAO HUONDOKA NA KUWAACHA WATU WALINZI NA BAADHI YA SHUGHULI  NDOGOGO ZA KAMBINI KWAO HASA USAFI NA UJENZI.

  kWAKUWA HUONDOKA SIZON BAADA YA MVUA KUONGEZEKA MASIKA HUTOA FEDHA KWA VIBARUA WAO NA KUKATA MITI YETU NA KUIJAZA KATIKA MITO YETU ILI WAWEZE KUPITISHA MITAMBO YAO NA MAGARI MAKUBWA KANA NDIYO MADARAJA. VIVYO HIVYO NDIVYO HUFANYA WAKIWA WANARUDI  KUCHIMBA JAMANI HALI HII TUNAKWENDA WAPI?

   MIMI KAMA MTANZANIA BABA YANGU ALIKUFA KATIKA VITA VYA UGANDA  KWA UVAMIZI WA IDD AMIN DADA NA KABURI LAKE LIKO KATIKA MAKABURI YA MASHUJAA WA VITA VYA KAGERA  NA NILIKUWA MDOGO SANA MIEZI 2,LAKINI KWA JANGA HILO MIMI MWANAE WA PEKEEE SERIKALI HAIJANISAIDIA CHOCHOTE ILA MIMI NDIYE NAISAIDIA SERIKALI KWA MAMBO MENGI NA BADO UELEWA WETU  WA KUZALIWA NAO NDIO TUNAOUTUMIA ZAIDI MAANA HATA FURSA ZA KIELIMU TULINYIMWA  KUTOKANA NA SERIKALI  KUTOJALI NA KUNITELEKEZA  SIJUI KWA HATUA YA UELEWA NILIONAO UNAWEZA KUNISHAULIJE?

  NAIPENDA NCHI YETU NAWAPENDA WATANZANIA NA NAPENDA WACHAPA KAZI NA HODARI WENYE UWAZI NA UKWELI KAMA WEWE.MIMI NI MMOJA WA WATU JASIRI NA KWA SASA NIKIPATA KUSHIKWA MKONO NAAMINI NAWEZA KUFIKA POPOTE KATIKA KULETA MABADILIKO YA JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA KATIKA KULETA MAENDELEO.mUNGU AKUBALIKI NA AKULINDE MR.ZITTO TUKO PAMOJA WEKA NGUVU PANAPOSTAHILI NGUVU KWA MAFANIKIO ZAIDI HIYO NDO KAULI YANGU.

  FROM: BARAKA PETER NZOVU KIGOMA-TANZANIA.

  ________________________________

  Baraka Peter

  April 7, 2013 at 9:32 PM

 63. Ubarikiwe mh Zitto. Wanaotoa habari ni bora wafuate mising ya kazi yao kwani hauwezi ukapewa taarifa ukaziamini kwa 100% bila uchunguzi. Waandishi njaa wanakera xana, wawe wanashitakiwa na kuadhibiwa ili @ taarifa itolewayo iwe ya kuaminika. Kila la kheri mhe Zitto.

  Dotto Mungo

  April 8, 2013 at 12:29 PM

 64. sielewi inakuaje mtu-mwandish anakua na ujasiri wa kutoa taarifa zisizo za kweli …

  Simba Willie ScopeJeff

  April 8, 2013 at 5:26 PM

 65. saluti yako mh shimiwa

  mmtingala

  April 28, 2013 at 4:08 PM

 66. oh very delicate issues. hatari!

  emmanuel mbati

  April 29, 2013 at 8:12 PM

 67. Pole Kamanda ndiyo njia uliyoichagua ya kuitumikia jamii yako jipe moyo Mungu yuko upande wa haki.

  Pendael H.Mbuga

  May 17, 2013 at 8:53 PM

 68. Asante sana kamanda ZITTO! We always believe in you! Hao madogo waliopew hongo ndo wachochez na wanalenga kùleta migogoro ndan ya chama chetu cha ukomboz dhid ya utawala wa dhuluma na kifisad wa CCM! Hao kina Shonza na Mwampamba siwakalale??

  Laurean Rugambwa

  July 28, 2013 at 10:23 AM

 69. Nakuomba piga kazi kama waida hizo kelele zao mwisho watachoka tu

  Dotto mabula

  November 19, 2013 at 10:21 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: