Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Matokeo ya Kidato cha nne 2012: Mataifa mawili katika nchi moja

with 23 comments

Matokeo ya Kidato cha nne 2012: Mataifa mawili katika nchi moja

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako akionyesha karatasi ya majibu ya mmoja wa watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2012, Dar es Salaam jana. Picha hisani ya Mwananchi

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako akionyesha karatasi ya majibu ya mmoja wa watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2012, Dar es Salaam jana.
Picha hisani ya Mwananchi

Kila Mtanzania sasa anajadili matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2012 yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi mwanzoni mwa wiki hii. Matokeo hayo yanaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 90 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne walipata daraja la nne na daraja la sifuri. Dara la Sifuri limebeba asilimia 60 ya matokeo yote. Taifa limepata mtikisiko mkubwa kuona vijana wake wakiwa wamefeli kwa kiwango hiki.

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kupata matokeo ya namna hii. Ukiangalia matokeo ya kidato cha nne kuanzia mwaka 2009 utaona kuwa kila mwaka wanafunzi wanaofeli wanaongezeka. Mwaka 2011, wanafunzi 302,000 sawa na asilimia 89 ya wahitimu wote wa kidato cha nne walipata daraja la nne na sifuri. Mwaka 2010 wanafunzi 310,000 ambao ni asilimia 90 ya wahitimu walipata madaraja hayo ya chini kabisa na mwaka 2009 jumla ya wanafunzi 195,000 sawa na asilimia 78 ya wahitimu wote walipata madaraja ya sifuri na daraja la nne. Kila mwaka matokeo yakitangazwa kuna kuwa na mjadala wa wiki moja au mbili, wabunge tunapiga kelele kidogo kisha tunasahau kabisa suala hili mpaka matokeo mengine.

Hivi tumewahi kujiuliza hawa vijana wanaoishia kidato cha nne wanakwenda wapi? Wanafanya nini? Hii nguvu kazi kubwa ya Taifa inapotelea wapi?

Ni vema ifahamike kwamba Tanzania ni Taifa la vijana na watoto. Kwa mujibu wa taarifa za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, hivi Tanzania ina jumla ya vijana 38 milioni wa chini ya umri wa miaka 35 , hii ni sawa na idadi ya watu waliokuwepo Tanzania mwaka 2003. Asilimia 78 ya Watanzania wapo chini ya umri wa miaka 35 na nusu ya Watanzania wapo chini ya umri wa miaka 17. Kwa takwimu hizi ni dhahiri kwamba suala moja kubwa kuliko yote linalohusu Watanzania ni Elimu. Suala moja kubwa linaloweza kujenga au kubomoa Taifa hili ni Elimu. Suala moja kubwa linaloweza kuepuka matabaka katika nchi ni Elimu. Tena Elimu Bora, na BURE.

Kuna nadharia inaitwa ‘gawio la idadi ya watu’ na ‘bomu la idadi ya watu’. Nadharia hizi zatumika kuelezea namna mataifa yanaweza kufaidika au kupata hasara kutokana na kuwepo kwa nguvu kazi kubwa ambayo ama inatumika kwa faida ya nchi hiyo kwa kufanya kazi na kuongeza uzalishaji ama inatumika kwa kwa kukaa tu kwenye vijiwe na kupiga soga. Taifa ambalo linaandaa vijana wake kwa maarifa na stadi za kazi huvuna gawio (demograpich dividend). Mataifa yaliyofaidika na hali hii ni kama India, Uchina na Ujapani ambapo nyakati wana vijana wengi sana kuliko wazee vijana hawa walipewa ujuzi mkubwa na stadi za maisha na hivyo kuongeza uzalishaji mali kwa Taifa. Watu ndio mtaji mkuu wa Taifa lolote lile duniani. Taifa ambalo haliandai vijana wake kupata elimu huingia kwenye mgogoro mkubwa maana kundi la vijana wasio na kazi na wasio na maarifa yeyote ni sawa sawa na bomu.

Tanzania tuna chaguzi katika masuala haya mawili, ama tuvune gawio la kuwa na vijana wengi sana kwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika Elimu au tusubiri bomu lilipuke. Kwa matokeo haya ya kidato cha nne kwa miaka minne iliyopita, ni dhahiri tumeamua kulipikiwa na bomu.

Tunajua chanzo cha matokeo haya. Watoto hawasomi wala kujifunza shuleni. Hasa watoto wa vijijini ambapo hakuna walimu wala vitabu. Tumejenga mataifa mawili ndani ya nchi moja, Taifa la masikini na wana shule zao, wanapata masifuri kila siku. Taifa la walalaheri wana shule zao na wanapata madaraja ya juu. Hawa ndio watakaoenda vyuoni na wenye elimu wataendelea kutawala. Suluhisho ni moja tu, kuamua kwa dhati kabisa kuwekeza kwenye elimu kwa kuhakikisha kuna walimu wa kutosha, walimu wanalipwa vizuri na kuishi kwenye mazingira mazuri. Iwe na marufuku wenye kufeli ndio wafanye kazi ya ualimu.

Ni lazima kuhakikisha kuwa kunakuwa na vitabu vya kutosha kwenye mashule. Serikali ihakikishe kwamba inaingia makubaliano na wachapishaji wa vitabu wa ndani na kutoa vitabu vinavyojenga Taifa kwa kutoa maarifa ya uhakika kwa watoto. Ieleweke kwamba shughuli ya uchapishaji wa vitabu ni ajira tosha iwapo tutawezesha wachapishaji wa ndani kutoa vitabu vingi zaidi na vyenye ubora.

Matokeo ya mwaka huu ya kidato cha nne yanatuambia jambo moja kubwa sana, kwamba sisi ni Taifa linalokufa. Tuweke siasa pembeni na kahakikisha kwamba kunakuwa na uwajibikaji kwa viongozi kutokana na matokeo ya namna ya hii ya vijana wetu. Tusione tabu kubadilisha mawaziri wa Elimu kila mwaka kwa kuwafukuza kutokana na matokeo ya mitihani ya watoto wetu. Hii itafanya Waziri ajue umuhimu wa elimu anayoisimamia. Tukate mzizi wa fitina, elimu ni suala la uwajibikaji. Makala zijazo tutaona hatua za kuchukua ili kuhakikisha hawa watoto zaidi ya 300,000 waliofeli tunawafanya nini.

Advertisements

Written by zittokabwe

February 22, 2013 at 1:42 PM

23 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. datz true diz pippo wana rule us forever since we will have no education

  kamsay

  February 22, 2013 at 2:04 PM

 2. hali ya taifa ni tete hapo watatizo ni mengi ila la msingi ni ukosefu wa walimu bora na wakutosha na vitendea kaz hasa ktk shule za kata hili linasababisha ukosefu wa msingi mzur pindi mwanafunz anapoanza kidato cha kwanza hivyo hawez kujituwa wakati hana hamu au tamaa ya elimu maana ukikosa mwalimu ujue unakosa morali na mustakabal wakusoma, serikali imejitahidi kujenga madarasa bas iimarishe upatikanaji wa vitendea kaz

  shaban mhando

  February 22, 2013 at 2:18 PM

 3. i always wish all leaders and civilians could have the same thinking capacity as yours…its a shame that most of tanzanians are not consious of what is happening to their own country

  upendo magreth

  February 22, 2013 at 2:20 PM

 4. mheshimiwa zitto tunaomba serikali isikilize matatizo ya walimu na ifanyie mkazi matatizo yote ya walimu. ili tuweze kulinisuru taifa hili.

  Efrahim Japheth

  February 22, 2013 at 2:39 PM

 5. Necta mnachukua uamuz gan kuhusu wanafunz kubadilishiwa matokeo yao na wengine kuekewa division wakat wa hawakufanya mtihani hii ni dhahiri kuwa necta mmechemka mwaka huu.

  Icramovic de sauza

  February 22, 2013 at 2:43 PM

 6. Necta wapuuzi

  Icramovic de sauza

  February 22, 2013 at 2:43 PM

 7. Hili janga kubwa ktk nchi yetu vijana wa mitaani wanazidi kuongezeka kila siku yaani tumejitegea bomu sisi wenyewe ambalo ukifika muda wake wa kulipuka mazara yake yatakuwa makubwa sana.

  Jeremiah Msangule

  February 22, 2013 at 2:44 PM

 8. Mhesimiwa what you say is true, hao watu hawatakujiuzulu kwa kuwa wanajua yakuwa vijana wengi wakipewa elimu yakutosha hawatapata mhanya mkubwa wa kuwanunua kwenye chaguzi zilizopo mbeleni! Wanatumia ile kauli inayosomeka “UKITAKA KUMTAWALA MTU VIZURI NA KWA URAHISI, MNYIME MTU HUYO ELIMU” Sasa hawaju kuwa zama ambazo hiyo kauli imepita tayari na sasa inakua ni “BOMU” inayobiri muda wake wa kulipuka.

  Japhary Khatemo

  February 22, 2013 at 2:49 PM

 9. Yote ni sahh nyie wawakilishi wetu mkomboe taifa kwa kutunga sheria,taratbu na sera nzur ktk elimu.Vyuo vya ufund bora

  JOSEPH

  February 22, 2013 at 3:25 PM

 10. Watoto hawasomi wanalaumu Necta,
  Tatizo ni wanafunzi sio Necta wala baraza,

  Maxmillian

  February 22, 2013 at 3:38 PM

 11. Kufeli kwa wanafunzi mwaka 2012, kuna mgusa kila mtanzania kwa takwim za upes upes, kama si wewe basi ndugu yako n janga la kitaifa , yale masifur yanagusa mpaka ukoo wa rais, wazir, necta na wengine wote yanatuhusu tupende tuspende, soln wanafunz wajitambue waheshm shule wazaz wahmize

  Japhet kyando

  February 22, 2013 at 3:40 PM

 12. bunge linawajibu ktk elimu yetu

  daudi masayi

  February 22, 2013 at 4:23 PM

 13. so shame for our nation we need support on this be
  fore the bomb erupted

  owden

  February 22, 2013 at 4:54 PM

 14. Kiongozi unamtazamo chanya sana.

  Si tu kwa kuelezea na kusikitishwa na yanayotokea ila kwa kuanza na suruhisho la hali hii. Natamani kama magazeti yote ya udaku na katika kila vipindi vya tamthilia na mule WATANZANIA wengi wanagubikwa na kupotezewa muda kuna na snippets kama hizi ulizozielezea.

  Nina-post makala hii kwenye Google+ kuna baadhi ya watanzania wananifuata huko nako!

  Asante na kaza mwendo. Mi ninakuja kwa vitendo kabisa bila ya kuwa na ukiongozi wa jina!

  Pamoja!

  Jonius

  February 22, 2013 at 5:10 PM

 15. It is a tragedy, the country can not carry on in this manner. Highly academicians have become politician seeking high level position as the only way to survive. Even those who make have succeeded to be elected as member of parliament and become ministers or top level government officials are very busy designing how to get foreign investors to take over government assets or related companies, how to get Chinese contractors to buy tenders for infrastructure and other projects since their respected high bribe givers and can keep secret.Even education department is not spared, they are busy with procurement etc.During the late Mwalimu Nyerere professionals, Masters and PhD degree owners complained that Mwalimu was keeping old CCM and not well educated people in as ministers instead of appointing highly qualified personnel, and this was perceived as the reason for the country not achieving required development, since not well educated failed to initiate proper management planning. President Kikwete tried his best to ensure well educated PhD holders are managing almost every ministry and associated departments. You can the PhD officer holding Zombe picture drawn by student during exam, just to show to the public that she did not perform her duties. What went wrong? Can you blame the students? Do we need serious soul searching? Do we need foreign experts? or Do we need Chinese contractors to advise on education matters? Again I repeat, my statement 100 times, ” No country have been developed by foreign contractors, investors, etc, The every country is build by its people, through a learning process, stage by stage, until the poverty is eradicated, citizen are economically empowered. Corruption is the root causes of all the problems faced by the nation. We heard stories of people purchasing PhDs hopping to be elected or appointed to higher government positions. POAC led by Mr. Zitto Kabwe which used to cross check the performance of government own companies has been banded by the speaker of parliament. President Kikwete fired 8 ministers at a go, never happen before. All these tells you the state of the nation with its corruption cancer deeply embedded into entire nation. There is no quick fix, or had hock trial and error solution.

  Alex Kakala

  February 22, 2013 at 6:59 PM

 16. Hii matoke ni combination ya sababu nyingi mimi nazani hawa serikali wanaujua ukweli ila wanadanganya watanzania mf mheshimiwa waziri kasema sababu ni uhaba wa maabara ni kweli ila alipaswa afafanue kua iyo ni sababu kwa masomo ya sayansi na je kwa masomo ya sanaa tatizo ni maabara, wasitudangaje na haki ya mungu wasipowasikiliza walimu hali ndo itazidi kuwa mbaya nazani huu ni mwanzo tu……

  henry

  February 23, 2013 at 10:57 AM

 17. Nadhani serikali itajifunza namna bora ya kulea na kuzalisha walimu.vilevile nadhani itapata mbinu mkakati ya kutatua kero za walimu ‘ni vizuri wajifunze kwamba mara unapokorofishana na walimu tegemea taifa la wajinga haraka sana’wamejifunza amri ya mahakama iliwasaidia kwa muda tu lakini tatizo lipo palepale tusubiri na tuone ya wahitimu mwaka huu.TUNAELEKEA KUBAYA kama TAIFA.

  ango jotham mbossa

  February 24, 2013 at 4:25 PM

 18. Nadhani kama taifa ni lazima tujadili na kuamua kama kaka Zitto ulivyosemaNajua Zitto unapenda siasa za kucompromise,ni nzuri lakini wakati mwingine matokeo yake ndo haya>

  Deudedit Kivyiro

  February 24, 2013 at 9:39 PM

 19. ..mheshimiwa,,hao wameshafeli and tukizidi,,kuwaangalia hao,,tuangalie pia na wale wa mwaka jana na juzi,,coz wapo wanaendesha bodaboda na wanavuta mabangi na kufanya vituko,,then pia katika uboreshaji,,wahakikishe mitaala in boreshwa na mitihani ya darasa la saba + kidato cha pili,,isimamiwe vinzuri,,coz in normal sence wale waliopita bila kutokujua kusoma,,na kwenda darasa la nne,saba, form one, three na kisha form four,,we unaonaje ajabu akipata zero?????..jenga maslahi ya taifa kwa kutoa elimu bora na sio kujaza madarasa kisa shule ya kata,,bora ziondolewe na kubakia na shule chache na wanafunzi wenye sifa stahiki katika kila ngazi…haaaaa,,its simple,,Engineers make things,,bt for Industrial Engineering and Management,,we make things better!!

  Kajia Rogers

  February 25, 2013 at 10:57 PM

 20. …heeeeeiiiiiiiii,,wats up btn this two colour jamaniiiii,,,i hate ,,hate sanaaa,,weupe wako wanakula bata na mali zetu,,wanafanya kazi ya kusogeza nondo wlipwa vinzuri,,cheking vifaa,,store keeper,,wasafishaji and any where u go,,mweupe anathaminiwa zaidi ya wewe mweusi,,daaaa,,mnajua wanachofanyiwa weusi huko nje,,masokwe masokwe,,,,….duuuu serekali yetu mbumbumbu sana,,TUKUMBUKE KAMA WALE WEUPE WALIWATESA IN ACTION BABU NA BIBI ZETU,,,why do u still embrasing them jamaniiiiiiiii,,wanakaa nchini na kufanya uhalifu,,kubebana na kazi za watanzania wananyanyasikaaaaa…what is this!!!,,I know u can ready this,,please take it seriously,,its very upumbavu na ushenzi na ndipo tuataendelea kua nyuma zaidi…Please tukubaliane,,means apriciating sisi kwa sisi……!!duuuu ninahasiraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!

  Kajia Rogers

  February 25, 2013 at 11:09 PM

 21. I think the entire education system need to be revamped

  Mabusi, Jm

  February 26, 2013 at 4:30 PM

 22. Naomba mitihani irudiwe kusahiswa na siyo kurudia kufanya tena mitihani by rashidy ally

  Rashidy ally

  March 11, 2013 at 12:59 PM

 23. Blunder iliyofanyika ni kubwa mno. Wapo wanafunzi ambao huku kwetu wanashangaa hawakufanya mtihani lakini wamepata division two. Inaonekana kuna mkanganyiko mkubwa huko NECTA. Inawezekana pia marekebisho au upangaji mpya wa matokeo ukazua mgogoro badala ya kuwa suluhisho. Baraza halijatulia kwa nchi yenye demokrasia ya kweli watendaji wakuu wanastahili kuwajibika ili kuonyesha umma wa Watanzania kuwa kweli wanajali.

  Mawazo Dudu

  May 8, 2013 at 5:23 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: