Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

TAMKO LA NDUGU BENJAMIN WILLIAM MKAPA

with 18 comments

TAMKO LA NDUGU BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Katika wiki za hapa karibuni kumekuwa na mijadala na mazungumzo mengi kuhusu mikakati ya maendeleo ya mikoa ya Kusini hususan Mkoa wa Mtwara.  Mazungumzo hayo yamekuwa na lugha kali na yameambatana, hatimaye, na maandamano na mikutano ya hadhara.  Kiini chake ni matumizi ya gesi iliyogunduliwa mkoani kwa ajili ya miradi au mipango ya maendeleo ya mkoa huo, mipango iliyopo mbioni kutekelezwa au inayotarajia kutekelezwa.  Mwenendo wa mazungumzo, maandamano na mikutano ya hadhara imeelekea kuashiria shari na kuvunjika kwa amani.

Aidha vituko na kauli hizo zimekaribia kujenga kutokuelewana kati ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Serikali, kati ya wanachama wa vyama vya siasa na viongozi wao, kati ya wananchi na viongozi wa Serikali.  Mtafaruku huu haufai kuachwa uendeleee na kutishia usalama.  Mipango ya maendeleo siyo Siri.  Mikakati na mbinu za Utekelezaji wake siyo Siri.  Maelezo yake mazuri yanaweza kutolewa yakadhihirisha namna na kasi ambayo raslimali zitawanufaisha wananchi wa eneo zilizomo na Taifa zima.  Utekelezaji wa miradi unategemea masharti kadhaa, k.m. Uwapo wa mitaji na teknolojia.  Lakini pia mwekezaji, awe Serikali au Sekta binafsi, atataka iwepo hali ya utulivu na usalama wa watu, hali na mali.  Hayo yatadaiwa na wawekezaji wa ndani na wa nje.  Vurugu, fujo, vitisho havivutii uwekezaji.

Nikiwa Mwana Mtwara na raia mwema mpenda nchi, nimefadhaishwa sana na matukio haya ya siku za karibuni Mtwara.  Kwa sababu hiyo natoa wito kwa wadau wote wa maendeleo ya Mtwara kusitisha harakati hizi na maandamano na mihadhara na badala yake wajipange KUKAA PAMOJA katika meza moja, kupitia historia, kutathmini mipango, kuchambua kwa kina mikakati ya utekelezaji wake, na hatimaye kufikia muafaka wa Ujia wa maendeleo. Fujo, vitisho, kupimana nguvu na malumbano kamwe si masharti ya maendeleo.  Mazungumzo yataboresha sera, ya uwekezaji ya mkoa na nchi.

Linalowezekana leo lisingoje kesho.

Benjamin William Mkapa

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Advertisements

Written by zittokabwe

January 22, 2013 at 3:06 PM

Posted in Uncategorized

18 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Busara si kila mtu anayo,waliyonayo huitoa na wasionayo kupata mawazo ya kuichambua..kuifata na kuitumia kutekeleza yalo mema toka kwayo. Mstaafu ametumia kauli nzuri kweli sitaki kuamini imetokana na kuwa na chembe ya asili ya mkoa husika naamini uzalendo pia umechangia..hebu kaeni na wenye mali muwasikie wanataka nini,sio muda wa kuchukua na kwenda enzi hizo ni za zamani kweli,serikali na vibaraka wako chukueni ujumbe.

  Patrick buluda

  January 22, 2013 at 3:55 PM

 2. Ni tamko muhimu kwa wakati muafaka haswa litokalo kwa mstaafu Rais mwana wa Mtwara. Lakini tunahitaji kulitizama kwa kina na mapana zaidi. Serikali ikae meza moja na wananchi wa Mtwara (milioni 1.4) kama wadau waliolingana au serikali ikiwa mdau muwakilishi wa wananchi milioni 43.6? Udau huu utakuwa na uzito gani kwenye maamuzi? Je wadau hawa wana bargaining chips zipi? Kila mmoja ana turufu? Kwa misingi ipi?

  Pili, tujiulize je wakati huo huo serikali ifungue mazungumzo na wakazi wa kila mkoa wenye madini, mafuta na gesi? Jee mikoa iliyo ni chanzo cha maji kama nyanda za kaskazini na za kusini? Vile vile mikoa yote yenye vivutio vya utalii kama fukwe za bahari na maziwa, mbuga za wanyama, milima, nk? Je mikoa inayozalisha mazao mengi ya chakula na biashara kama mahindi, ngano, pamba, korosho, kahawa? Hata mikoa inayozalisha madaktari, wahandisi, wakemia, wanajeshi, nk wengi kuliko mingine ikae chini na serikali kuangalia mikoa hiyo inavyofaidika na mchango wao kitaifa?

  Ninapoelekea ni kuonyesha futility ya approach hii leo hii wakati tuko taifa moja kwa miaka 50. Tunataka kuvunja hili taifa? Je iweje serikali isipoafikiana na WaMtwara (I hate this term for its divisive connotation). Kabla ya kuanza mazungumzo lazma uwe na uelewa wa exit strategy. Tusipoafikiana na wadau toka Mtwara ndio kuwa wana veto ya uchimbaji na uuzaji wa gesi? Tutegemee turrufu ya wanaharakati wanaosema wataosema bomba halitajengwa watapigana vita? Hii kweli ni political discourse tunayotaka kuendekeza this day and age? Je serikali ikitumia turufu zake nyingi si tumejiingiza kwenye vita na waasi?

  Wazo mbadala linalokumbatia hili la mzee Mkapa ni kuwa na national dialogue ambayo inahusu mgawo wa pato litokanalo na maliasili zetu kati ya wananchi waishio karibu na raslimali hizi na Watanzania wengine. Hii inaweza kujadiliwa kama sera, na wananchi wote wajue hatma ya pato litokanalo na raslimali zetu. Pendekezo langu kwa kuanzia ni mrabaha wote kubaki mkoa husika na angalau robo ya salio hilo libaki wilaya husika. Hii iamuliwe kitaifa sio baina ya WaMtwara au WaNzega au WaArusha na serikali. Ni kweli mawazo na mapendekezo toka sehemu hizi ni lazma yasikizwe na yafanyiwe kazi, lakini mwisho wa siku maamuzi haya yafanyike kwa manufaa ya taifa kitaifa bila kujali nguvu au wingi wa wadau wa maliasili fulani.

  Maandamano na mihadhara kwenye kila raslimali yakilazimisha mazungumzo kati ya serikali na wadau wa sehemu moja, ni sawa na kuanza kikao cha kwanza cha kuvunja taifa hili. Kila Mtanzania awe na haki ya kudai wasaa wa kiuchumi, elimu, maendeleo na amani toka kwa taifa letu hata kama chini ya ardhi yao hakuna madini wala gesi. Wale ambao wamebaki nyuma kwa miaka hamsini wawe na haki ya kutuuliza kulikoni hata bila ya ugunduzi wa gesi asilia. A conversation on rational regional development is a worthy cause for the country, but we have to be wary of overemphasis on regionalism while we are still trying to build a viable state. Once you wallow in regionalism for a while, tribalism is not very far away!

  makundi w.

  Makundi W R (@MakundiW)

  January 22, 2013 at 4:06 PM

 3. Mi nauliza kwani kujengea hiyo mitambo Mtwara halafu wasafirishe umeme kuna shida gani mpaka serikali inaona shida?hamuoni mlundikano wa viwanda vitakua kwenye mkoa mmoja halafu mnasema watu wanakimbilia dar waachsje na kila kitu mnapeleka huko.

  Elias.R.Mdee

  January 22, 2013 at 4:55 PM

  • NAELEKEA KUKUBALIANA NA MAWAZO YAKO. JUZI NILIKUWA DAR. NILISIKIA VIJANA WA DAR WAKISEMA ‘HUKO BARA KWENYE WATU WENYE MATONGOTONGO MACHONI WATAWEZA KUMUDU UZALISHAJI WA GESI?’

   HIYO NDIYO TANZANIA TUNAYOIITA NCHI YENYE UMOJA! WAJARIBU WANA MTWARA/LINDI. MTAONA MAAJABU

   DOMINICO KABYEMERA

   February 1, 2013 at 6:29 PM

 4. Ni kweli mazungumzo ni ya msingi na serikali iache kufanya uficho wa uwekezaje kwenye rasilimali za taifa, haya yote yanatokana na ubadhirifu wa viongoz, ila suluhu katiba mpya ielekeze uwazi na makubaliano ya jamii nzima katika rasilimali za nchi ili jamii itambue namna inavyonufaika kwa pamoja, ndipo uwekezaji ufanyike.

  Ivan Ishengoma

  January 22, 2013 at 5:17 PM

 5. Nadhani hii itatoa somo pia kwa mikoa mingine ,kama raslimali ikipatikana kila mkoa uweke vikao na kujadili jinsi ya kutumia raslimali zake kwa faida ya wenyeji wake.

  Mohamed Sleyim

  January 22, 2013 at 5:44 PM

 6. ninamwamini mkapa kwa hili ameweka utaifa mbele, iundwe timu ya kuratibu jambo hili na iongozwe na mkapa

  komu

  January 22, 2013 at 5:50 PM

 7. Mgogoro kama huu wa wanamtwara kutoridhika na gesi ya Mtwara kusafirishwa kwa ajili ya uzalishaji wa umeme huko Dar es Salaam badala ya Mtwara kabla ya kusambazwa Mikoa mingine haujawahi kutokea kwenye vipindi vya utawala chini serikali ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu. Mgogoro kama huu haujawahi kutokea kwa sababu maamuzi ya Serikali za awamu hizo kuhusu matumizi ya raslimali za Taifa au mapato yatokanayo na raslimali hizo yalizingatia kujenga fursa sawa na faida kubwa zaidi kwa watanzania wote bila upendeleo. Hivyo ndivyo ilivyokuwa na wananchi wote walielewa hivyo, mambo yanapangwa na kutekelezwa bila upendeleo wowote kwa eneo fulani na Rais alikuwa ni Rais wa Nchi nzima na sio wa Mkoa au wilaya alikotoka.
  Mikoa iliyokuwa imebaki nyuma kuwekewa miundo mbinu ya maendeleo kama vile gridi za umeme, reli, BaraBara nzuri, mashule, hospitali na kadhalika ilielewa wazi kwamba Mikoa yote haiwezi kupata kwa wakati mmoja na fursa zitakapotokea itakuwa ni zamu na wao kupatiwa hiyo miundo mbinu muhimu kwenye kujitafutia maendeleo yake na Taifa kwa ujumla.
  Kwa mfano, wananchi wa Mikoa ya Mtwara na Lindi wamevumilia kuishi kwa muda mrefu bila kunungunika kwa kutokuwa sehemu ya gridi ya umeme ya Taifa kwa sababu walielewa vianzio vyenye umeme wa kutosha havikuwepo ili kuwezesha na wao kuunganishwa na gridi ya Taifa wakiamini fika kwamba fursa itakapotokea wao ndio wangepewa kipaumbele kuunganishwa na gridi ya Taifa.
  Pia, wananchi hawa wamevumilia kuishi kwa muda mrefu bila kuwa na kiungo cha reli au BaraBara nzuri kati ya bandari yake na masoko ya nchi nyingine kusini mwa Bara la Afrika ambayo yako karibu zaidi na Mtwara kuliko Dar es Salaam wakielewa fika kwamba fursa itakapotokea kipaumbele kitakuwa ni wao kujengewa reli na barabara nzuri kuunganisha bandari yake na masoko ya nchi nyingine kusini mwa Bara la Afrika ili na na ukanda wa Mtwara uweze kufaidi kama ukanda wa Dar es Salaam unavyofaidi
  Kwa hiyo ni matarajio ya watanzania wengi wanaojuimuisha wanamtwara kwamba matumizi ya gesi nyingi iliyopatikana huko Mtwara na Lindi na maeneo ya karibu yangelenga kwanza kuunganisha Mikoa hii ya Mtwara na Lindi kwenye gridi ya Taifa kwa kuhakikisha mitambo ya uzalishaji umeme wa gesi inajengwa Mtwara na gridi mpya ya kusafirisha umeme uliozalishwa inajengwa kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
  Pia ni matarajio ya wengi kwamba viwanda vinavyotumia gesi ya Mtwara na Lindi kama mali ghafi vingejengwa kwanza Mtwara na Lindi ili kupunguza gharama za uzalishaji na kukuza ajira ndani ya Mikoa hii iliyobaki nyuma katika sekta ya viwanda kwa muda mrefu.
  Pia ni matarajio ya wengi kwamba kipaumbele kwenye matumizi ya pato la Taifa litakalotokana na uchimbaji wa gesi asilia huko Mtwara na Lindi yatakuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa reli na barabara nzuri kuunganisha bandari ya Mtwara na masoko ya nchi nyingine kusini mwa Bara la Afrika yaliyo karibu zaidi na Mtwara kuliko Dar es Salaam ili na ukanda wa Mtwara uweze kufaidi kama ukanda wa Dar es Salaam unavyofaidi. Naamini kabisa vipaumbele kama hivyo vingekuwa ni kwa faida zaidi kwa watanzania wote na sio wanamtwara peke yao na wa kulalamika kutokana na vipaumbele hivyo hategemewi kuwepo.
  Uamuzi wa kujenga bomba la kusafirishia gesi asilia ya Mtwara kwenda Dar es Salaam kuzalisha umeme haukulenga kuunganisha Mikoa iliyosubiri kwa muda mrefu ya Lindi na Mtwara kuunganishwa na gridi ya Taifa na badala yake umelenga kuboresha ufanisi wa miundo mbinu ya umeme ndani ya Mikoa ambayo tayari imeunganishwa na gridi ya umeme ya Taifa.
  Kwa mradi huu wa kuendeleza gesi asilia ya Mtwara, nahisi Serikali imeonyesha kuwa na tabia ya upendeleo hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam dhidi ya mikoa ya Mtwara na Lindi iliyostahili kupewa kipaumbele na inawezekana upembuzi yakinifu haukufanyika kikamilifu ili kubaini matumizi yatakayokuwa na faida kubwa zaidi kwa watanzania na wanamtwara kati ya matumizi yote mbadala ya gesi ya Mtwara yanayojumuisha uzalishaji wa umeme wa gesi asilia Mtwara na ujenzi wa gridi mpya ya kusafirisha umeme huo kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam(1) na ujenzi wa bomba la usafirishaji wa gesi aslia ya Mtwara kwa ajili ya uzalishaji wa umeme mkoani Dar es Salaam (2).
  Mradi huu wa kuendeleza gesi asilia ya Mtwara ni mradi mkubwa sana unaogharimu fedha nyingi na kama upembuzi yakinifu haukufanyika kikamilifu na matokeo yake ikawa ni kosa uamuzi wa kujenga bomba kwa ajili ya kusafirisha gesi ya Mtwara kuja kuzalisha umeme Dar es Salaam basi itatugharimu mabilioni ya dola za marekani kwa kipindi chote cha uhai wa mradi na kama upendeleo kwa Mkoa wa Dar es Salaam dhidi ya Mikoa ya Mtwara na Lindi (iliyobaki nyuma sana kwenye kuwekewa miundo mbinu ya maendeleo) basi hii itakuwa ni kuhatarisha umoja na kuaminiana kati ya watanzania wa maeneo tofauti hapa Nchini.
  Ni matumaini Mh Zitto Kabwe ataendeleza mapambano ya kutafuta haki ndani ya mradi huu wa kuendeleza gesi asilia ya Mtwara kwa kuhakikisha upembuzi yakinifu ulifanyika kwa kuhusisha matumizi yote mbadala ya gesi ya Mtwara na vipengele vyote vinavyojumuisha faida kwa kipindi chote cha uhai wa mradi na kwamba upendeleo kwa Dar es Salaam dhidi ya Mtwara haukuwepo.
  Mungu Ibariki Tanzania na Umoja wa Watu Wake.

 8. Amenena Mkapa ila tamko hili lilibidi litoke kwa rais aliye madarakani.

  Kisongo

  January 22, 2013 at 9:50 PM

 9. Imefikia wakati raslimali ziwasaidie wakazi mahali zinapopatikana kwanza kutokana na kusahaulika katika mgawo wa Kitaifa, hasa upande wa dhahabu kwa ndugu zangu Wasukuma inasikitisha sana kwani uwiano wa rasirimali na maendeleo yao havifanani wakati ndio waathilika wakubwa wa milipuko na sumu inayotumika kwenye uchimbaji.

  haji harun luge

  January 23, 2013 at 8:00 AM

 10. Tamko la Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa ni la busara laikini sio kwa ges tu na madini ila kila inapotokea kutofautiana kwa hoja baina ya pande mbili zenye maoni na mitazamo tofauti ni vizuri kukaa pamoja kujadiliana bila kutanguliza ubabe, madaraka, migomo, mandamano na ubinafsi. Ubinafsi wa matumizi ya rasilimali ndiyo kiini cha mifarakano mahali pengi. Serikali igawe sawa kwa wananchi wote sio pale tu panapopatikana madini kwa kuwa ni za watanzania wote.

  asungwile

  January 23, 2013 at 10:52 AM

 11. mimi naomba kumpongeza rais mstaafu ben, kama ningepata nafasi ya kuuliza swali ningemuuliza hivi: ”je anaizungumziaje ile gesi kutoka songo songo – lindi iliyokwenda dar ili kuzalisha gesi kwenye mitambo ya songas je hau wananchi wa lindi hawakuwa na haki kama hii inayodaiwa na watu wa mtwara sasa?” mwisho wa swali langu naomba majibu mheshimiwa rais!

  bariki

  January 23, 2013 at 12:32 PM

 12. Uwezo wa wananchi kufikiri unatofautiana ndio maana wengi wnakurupuka na kuongea wasio yajua wapi viongozi wa dini kuandamana kupinga kusafilishwa kwa gesi?yangu maoni ni viongozi wote waewe pamoja ili kuwaelewesha raia kuhusu ni busala gani itumike kutatua tatizo hili,pia selikali kuweni wazi kwani hatujawaelewa gesi dar inafata nini hamuoni ni kupoteza fedha za umma.

  francis shayo

  January 23, 2013 at 5:01 PM

 13. Mpenda amani siku zote hutafuta njia sahihi ili kutatua kero anazokumbana nazo na hata wakati furani hukubari yaishe kwa kuoteza haki yake ya msingi ili kutawalisha amani na utulivu
  Mchochezi ni yule anayechochea ama upande mmoja kati ya pande zinazo kinzana ama pande zote iwe ni kwa ama ili kuleta haki upande ulio kosa haki ama kuleta vurugu ili yeye anufaike na vurugu hiyo.
  Vurugu za Mtwara ni matokeo ya sera mbovu za maendeleo zisizo shirikisha wananchi pamoja na wadau wa maendeleo kikamilifu…….

  Rajab Nassor

  January 23, 2013 at 6:10 PM

 14. Maneno ya hekma.

  shadyfeleshi

  January 23, 2013 at 8:58 PM

 15. Mr. William Mkapa must not ignore the current situation of citizen exploding into demonstration, its is due to long vivid corruption entrenched in the government leaders. People have reached a boiling point.If a common man can understand the frustration of citizen due to mismanagement of the country natural resources, gold, diamond, oil and gas. The government failure to initiate long term plan to invest directly into natural resources , and get Watanzania to be fully involved in exploration, processing, marketing and managing the revenue obtained has prolonged the people to remain in poverty.Graduate as well as non graduate are massively unemployed, those working have seen their purchasing power diminishing, can not afford to purchase even a small apartment of three bedroom, can not afford sky rocketing daily expenses for transport, food,healthcare, education, basic amenities. Framers can not afford simple life, expand their farming through modern technology. Gas pipeline has been awarded to Chinese contractor costing billions of money, of which Tax payers have to settle the loan. Why the government can not award the contract on Jv with 60% to Tanzania local company and 40% to Chinese? That could have been a starting point to develop local expertise and construction profit of 60% would have remain in the country, for future re-investment. This is how you empower local citizen. The government officers practice is to sell any project to Chines in return for bribes .The they tell the citizen that they can benefit once the project is completed.

  That is not smart leadership, they are just following what China and others are telling them, but they can’t ask China the question, ” how did Chinese acquire such expertise? Obvious they started at home, participating in their country development, taking construction projects, and improving time after time. Tanzania is doing the opposite, it is grounding its well educated workforce, engineers, contractors. They are becoming spectators in their own country, while the government implement international tender system which benefits foreigners and get them bribe money. If a farmer in Mtrwara, has a relative or son , daughter involved in construction company as shareholder, he could see the improvement in the family, he will be very proud due to economic development in the family. The government can not employ all graduates, it should prepare a conducive environment for entrepreneurship, and empower local graduate through direct participation though ownership, of companies, or JVs , etc. Why people are fed up? The government is not sincere to its people, people have waited so long for economic revolution, but what they see, is projects being sold to Chinese, in fact in some areas citizen are evicted to allow a Chinese whole sale market in Kurasini. All are sad stories which will lead to explosion like “Arab Spring”. 690 million USD MCA millennium fund by American during George Bush to Tanzania, all the money were used to pay Chinese contractors at most for infrastructure projects, roads , water etc. Our leaders will show American that they have completed all these projects, well done job. Because they are not concerned who got the contract, but as a leader aspiring to economically empower your people, you should start with the direct benefit of construction profit money to your people, that will make you proud and American will be more proud. will tremendously improve the lives of local contractors, sub-contractors and employees. Domino economic effect to the whole society will be realized by majority,and will lessen the employment burden to the government. But current government leaders they do not see wide economic benefit, they want quick gain scheme, institute international tenders, a ploy to sell the projects to Chinese contractors and get some bribe money, job well done, they Chinese will complete the job without even much supervision.
  Now they want to sell Kigamboni projects to the same Chinese. I can tell you Soon or later Tanzania will become south Africa, holding political power, but economic power, the country economy will be in the ends of foreigners, Watanzania will be just begging foreigners, for jobs, for place to live in soon Kigamboni, Kurasini, Osterbay police station sold to build a super market. You do not build supermarket to low density matured township were people can enjoy living after day of hard work. You build a new supermarket in less developed outskirt of the city to distribute the development, create new township and office area so you can reduce traffic congestion in the city. I think they do not have time to think, once money is shown to them , that is it, job done. Therefore Mtwara gas development case, is not isolated is just explosion of what the government fail to acknowledge and change the course for long time. Mr. Mkapa also not excluded he left the government with so many corruption candles following him. How can he advise the current government to do the write thing?

  Alex Kakala

  January 24, 2013 at 11:43 AM

 16. My quick comment kwa mh. huyu would be “Good Statement But Too Late Mr. Ex-President”. Kama tayari mwekezaji yuko mbioni kuanza kuchimba bomba la kusafirisha gesi kwenda Dar, maana yake ni kwamba mikakati ya uwekezaji ktk rasilimali hiyo imekamilika. Na kama wananchi wanaonesha manunguniko, maana yake ni kwamba hawakushirikishwa vya kutosha katika mchakato mzima wa hatua za uwekezaji katika maeneo na rasilimali hiyo.

  Mawazo ya Rais wetu mstaafu ni mazuri lakini yanaibua maswali mengi kuliko majibu. Kwanza, yeye kama mdau mkubwa wa Mtwara (mzawa) na kwa nafasi yake kama Rais mstaafu, alikuwa wapi mpaka suala hili linafikia hatua hiyo bila yeye kushauri wahusika kuwashirikisha wananchi toka mwanzo na kwa uwazi kadiri iwezekanavyo? Suala la manunguniko ya raia wanaoishi katika maeneo ambayo rasilimali hizi za nchi zinagunduliwa na kutumika kwa uwekezaji huku wazawa wakiambulia patupu ni la mda mrefu (Mf. Machimbo ya madini) kwa nini mh. huyu hakuliona hili mapema na kutumia nafasi yake kuishauri mamlaka iliyohusika kupamga uwekezaji huu kuwashirikisha wananchi na kuwaelimisha vizuri juu ya namna watakavyofaidika na uwekezaji huu?

  Katika hili wanasiasa wasipotoshe hoja nzuri ya wana-mtwara kwamba “watafaidikaje na uwekezaji huo?” Wanachotaka wala sio kufaidika peke yao kutokana na rasilimali hii (ubaguzi) bila watanzania wengine kama baadhi ya watanzania (hasa wanasiasa) walivyokuwa wanajaribu kupotosha. Ni haki ya wana-mtwara kuhakikisha wanafaidika kutokana na rasilimali hiyo kwa namna mbalimbali kama ajira, miundombinu, huduma n.k. Serikali iliangalie vizuri hili na wasipotoshe umma na kuwaita wanamtwara kuwa ni wabaguzi au wabinafsi. Si kweli. Kama ilivyo kwa wana-kilimanjaro wanavyofaidika na mlima kilimanjaro na mbuga iliyo kandokando yake ndivyo hivyo na wana-mtwara wanavyopaswa kufaidika kutokana na miradi ya Gesi.

  Nakubaliana na hoja ya mh. ya kukaa kwenye meza na kuzungumza ili kulipatia suala hili ufumbuzi. Ila kinachonikera ni huu mtindo wa serikali yetu kusubiri wananchi waanze kufanya migomo na maandamano ili kuweza kuwasikiliza hata ktk mabo yaliyo wazi kama hili. Tubadilike

  Richard Alphonce

  January 24, 2013 at 1:13 PM

 17. Where does Mr. Mkapa get the Moral authority to speak about the Gas case, the prevailing government is just following the pace he set. I am sure if it would have been him in power to date it could be debaco fiasco he was never a listener!! I remember him scorning Watanzania while in UK eti ni wavivu wa kufikiri. For his information he did extremely the same when it comes to mines every where with his lower royalties leaving natives poor, it is said he even buried people alive in Bulyanhulu……….. He does not deserve neither to advise nor the honor he is enjoying but to wrote in jail. Please – Leave us in Peace.

  Lourance Njopilai David Mapunda

  January 27, 2013 at 10:24 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: