Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Lumumba: Miaka 52 ya kifo chake, Afrika ipo vile vile

with 23 comments

Lumumba: Miaka 52 ya kifo chake, Afrika ipo vile vile

Zitto Kabwe

Patrice Lumumba

Patrice Lumumba

Msinililie, wazalendo wenzangu, najua kuwa nchi yangu, inayoumia sana hivi sasa, itaweza kulinda Uhuru wake. Idumu Kongo! Idumu Afrika’.

…. hakuna mateso wala vitendo vyovyote vya kinyama vitakavyonifanya kuomba huruma, ni bora kufa kwa heshima, nikiamini kabisa na kujiamini kuhusu hatma ya nchi yangu kuliko kuishi kwenye utumwa na kuvunja misingi yangu. Ipo siku historia itasema;sio historia iliyoandikwa Umoja wa Mataifa, Washington, Paris au Brussels, lakini historia itakayofundishwa katika nchi zilizoondoa ukoloni na vibaraka wake. Afrika itaandika historia yake iliyojaa utuna heshima

Haya ni maneno kutoka kwenye barua ya Patrice Lumumba kwenda kwa mkewe Pauline aliyoandika akiwa kwenye selo yake gerezani siku chache sana kabla hajauwawa. Leo tarehe 17 January, ndio siku ambayo Lumumba aliuwawa kwa kupigwa risasi na mwili wake kuzikwa mahala kusikojulikana katika Jimbo la Katanga huko Kongo. Lumumba alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Kongo aliyeleta uhuru kwa Taifa hilo na Mwanamapinduzi wa kweli ambaye Afrika ilinyanganywa mapema sana ikiwa anahitajika sana.

Patrice Emery Lumumba alikuwa Waziri Mkuu wa Kongo akiwa na umri wa miaka 37 tu na kwa kweli mabeberu hawakumruhusu kuongoza nchi yake kwa uhuru kuanzia siku ya kwanza ya Uhuru wa Taifa hilo. Akiwa kijana wa miaka 27 alianza mapambano ya kupigania Uhuru wa nchi yake, alifungwa, alipigwa, aliteswa na kudhalilishwa kwa kila namna na maafisa wa Kibeligiji lakini hakukata tamaa na alihakikisha Taifa lake linapata ukombozi wa kweli. Mabeberu, kwa tamaa ya utajiri wa Kongo kamwe hawakutaka nchi hiyo ipate uhuru wa kweli. Kwa kutumia vibaraka wao kama Tshombe, Kasavubu na Mobutu,  Wabeligiji na rafiki zao Wamerekani walihakikisha wanammaliza mkombozi huyu. Leo ndio siku ambayo Lumumba aliuwawa. Siku ambayo ni ya majonzi makubwa kwa Afrika nzima. Lumumba alipewa adhabu ya juu kabisa binaadamu kupewa kwa kosa moja tu – kutaka uhuru wa kweli kwa Waafrika wa Kongo.

Lumumba alijipa hukumu ya kifo siku ya kwanza kabisa ya Uhuru wa Kongo. Katika sherehe za Uhuru tarehe 30 Juni 1960, Mfalme wa Ubeligiji Baudouin alitoa hotuba katika Jumba la Taifa (Palais de le Nation – Kinshasa) ambayo ilimsifia sana babu yake Mfalme Leopold II kwa kuijenga Kongo. Alisema ‘ Uhuru wa Kongo ni mwendelezo wa kazi iliyotukuka iliyopangwa na mtu mwenye akili sana Mfalme Leopold kwa ujasiri wa hali yajuu na uvumilivu mkubwa wa Taifa la Ubeligiji. Msiharibu maisha yenu ya baadaye kwa kufanya mageuzi ya haraka haraka na msiondoe muundo ambao Ubeligiji umewajengea mpaka hapo mtakapoweza kufanya vema zaidi’. Wakati Mfalme huyu anatoa maneno haya ya kifedhuli kwa wananchi wa Kongo, Lumumba ambaye hakuwa kwenye orodha ya wazungumzaji siku hiyo alikuwa anaandika hotuba yake kwa mkono na kwa haraka haraka. Hakutaka ufedhuli ule wa Mfalme wa Ubeligiji upite bila kujibiwa. Akajibu kwenye Hotuba ambayo haikuwa kwenye ratiba kabisa.

Tumezoea dhihaka na matusi, tumepigwa asubuhi mchana na usiku, kwa sababu sisi ni watu weusi. Tumeona ardhi yetu ikinajisiwa. Tumeona sheria zikitambua wenye nguvu na sheria tofauti kati ya watu weusi na watu weupe. Hatutasahau mamlaka zikijaza watu kwenye jela, watu ambao hawakukubali kwamba haki ni ukandamizaji na unyonyaji” Maneno haya yalifurahiwa sana na wananchi wa Kongo lakini yalikuwa ndio hukumu ya kifo ya Lumumba maana baada ya hotuba hii Wabeligiji waliamua kuwa ni lazima auwawe. Kweli siku kama ya leo mwaka 1961 Lumumba aliuwawa. Hakuna kaburi lake wala nguzo zake za mwisho. Alichomwa yeye na wenzake wawili. Mauaji yaliyoratibiwa kwakaribu sana na Serikali ya Marekani chini ya Shirika lake la Ujasusi.

Patrice Emery Lumumba aliuwawa wakati Kongo ipo chini ya majeshi ya Umoja wa Mataifa. Askari wa kulinda amani wa Ghana walipoona Lumumba amekamatwa na askari wa Mobutu walitaka kumwokoa na kumweka chini ya ulinzi wa Umoja wa Mataifa lakini wakuu wa Umoja wa Mataifa wakasema hiyo sio kazi yao, sio ‘mandate’ yao. Wakuu wa Umoja wa Mataifa walisahau kabisa kwamba Lumumba alikuwa ni Mbunge na hivyo alikuwa na Kinga na hadhi ya Kulindwa kwa mujibu wa sheria. Lakini kwa kuwa umoja wa Mataifa wenyewe walikuwa wanafanya kazi ya Ubeligiji na Marekani, waliacha Lumumba, adui yao mkubwa, auwawe. Hivi sasa Bunge la Ubeligiji limeruhusu uchunguzi maalumu kuhusu Kifo cha Lumumba, miaka kadhaa baada ya Serikali ya Ubeligiji kuomba radhi kwa kuhusika na kifo hicho. Serikali ya Marekani, pamoja na nyaraka kuonyesha kuhusika kwake na mauaji ya mwanamapinduzi huyu, bado haijaomba radhi. Pamoja na Rais Barack Obama kuwa na asili ya bara la Afrika, hatutaraji kama ataomba radhi kwa mauaji haya ya kinyama dhidi ya Mzalendo namba moja barani Afrika.

Wakati Waafrika tunamkumbuka hayati Lumumba katika siku yake hii, masuala tunayopaswa kuyatafakari ni kama tunasimamia yale ambayo Mwanapanduzi huyu aliyasimamia. Lumumba alitaka uhuru kamili wa bara la Afrika, sio uhuru wa bandia. Alitaka utajiri wa Afrika utumike kwa ajili ya kuendeleza waafrika. Leo tunaona Afrika inaendelea kunyonywa na mataifa makubwa. Uchumi wa Afrika umemezwa kabisa kabisa na nchi nyingine. Utajiri wa Afrika unaendeleza mataifa yale yale ya magharibi. Kama alivyosema afisa mmoja wa jeshi la Ubeligiji mara baada ya uhuru wa Kongo ‘Kabla ya Uhuru sawasawana Baada ya Uhuru’.Afrika yenye utu na heshima yake bado. Nchi yenyewe ya Kongo bado imegubikwa mauaji. Mamilioni ya wananchi wa Kongo wameuwawa toka mwaka 1996. Mataifa jirani ya Kongo yanashiriki kabisa katika kuleta machafuko nchini humo. Umoja wa Mataifa bado upo Kongo na wala hawawezi kuzuia uvamizi. Waafrika wenyewe kwa wenyewe tunatumika dhidi yetu. Lumumba alishirikiana na wenzake kama Nyerere, Nkrumah, Kenyatta nk katika kupigania uhuru. Viongozi wa sasa wa Afrika wanashirikiana na mabeberu kuinyonya Afrika.

Nitamalizia kumbukumbu yangu ya hayati Lumumba kwa hadithi niliyohadithiwa na marehemu Kanyama Chiume, Waziri wa kwanza wa Mambo ya Nje wa Malawi. Mmoja wa wanamapinduzi ambaye alibahatika kuonana na kufanya kazi na Lumumba. Nilimwuliza, nikiwa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alimjuaje Lumbumba? Akanijibu ‘walimvumbua wapi Lumumba?’ Yeye na wenzake. Ni hadithi ya kukumbukwa na vizazi na vizazi.

Ujumbe wa Chama cha kupigania Uhuru Afrika Mashariki Kati na Kusini (PAFMECSA) ulikuwa umetua jijini Kinshasa wakielekea Accra kwenye Mkutano wa nchi za Africa ulioitishwa na Rais Kwame Nkrumah wa Ghana mwaka 1958 (All Africa Conference). Ujumbe huu ulimjumuisha Julius Nyerere wa Tanzania, Abdurahman Babu wa Zanzibar, Tom Mboya wa Kenya na Kanyama Chiume wa NyasaLand. Wakiwa jijini humo, Kanyama Chiume na Babu wakawa wanatembea tembea mjini kusubiri ndege ya kuwabeba kuwapeleka Accra, walikuwa pale kwa siku 5 hivi. Katika kuuliza uliza kuhusu harakati za ukombozi katika Kongo, ndio wakaambiwa kuna kijana anapigapiga kelele mjini pale anaitwa Lumumba, wakaomba kumwona. Wakashangaa namna ambavyo habari za kupigania Uhuru Kongo hazijulikani kabisa nje ya Kongo. Walivutiwa sana na Lumumba. Wakamkatia tiketi ya ndege (Tom Mboya ndio alitumia fedha za wapigania uhuru wa Kenya kununua tiketi ya Lumumba). Wakaenda naye Accra. Afrika ikamjua Lumumba. Mapambano ya Kongo ya Kongo yakapata nguvu kubwa na hatimaye Uhuru ukapatikana.

Katika kikao cha Mwalimu Nyerere wa Tanganyika na Rais Ahmed Sekou Toure wa Guinea, Lumumba ndiye alikuwa mfasiri maana yeye alijua Kiswahili na Kifaransa, Mwalimu alijua Kiingereza na Kiswahili na Sekou Toure alijua Kifaransa tu. Namna ambavyo wapigania uhuru walivyokuwa wanashirikiana inasisimua mwili. Kizazi hiki cha viongozi wa Uhuru kimekwisha. Viongozi wa sasa wamejaa tamaa ya mali na sifa za kusifiwa na Mataifa ya magharibi.

Lumumba mpaka anakufa alikuwa jasiri. Wazungu waligopa hata maiti yake ndio maana walimwunguza kwa tindikali. Hata barua yake ya mwisho kwa mke wake ilionyesha ni mtu wa namna gani. Badala ya kuanza kusema ameacha akiba yake wapi yeye alisema ‘historia ya kweli ya Afrika itaandikwa na Waafrika wenyewe’. Mwanaume wa shoka. Tutakukumbuka daima. Hata kama waliokufuata wameshindwa kuandika historia ya kweli ya mapambano ya Afrika, maneno yako yatabaki daima kama kishawishi kwa Waafrika. Afrika itakombolewa tu. Pumzika kwa amani Patrice Emery Lumumba, Mwafrika kindakindaki.

Advertisements

23 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Why him? Because he was the first to understand that the only force capable of achieving full independence was that of the great mass of the exploited and oppressed…
  ‘historia ya kweli ya Afrika itaandikwa na Waafrika wenyewe’.
  In agreement…

  Santa

  January 17, 2013 at 11:29 AM

 2. Among other things,in his speech at Accra Ghana in 1958 he said,”We wish to see a modern Democratic State established in our country,which will grant its citizens freedoom,justice,social peace,tolerance,wellbeing ang equality with no discriminatio whatsoever.”

  I mostly like this part of that speech.

  R.I.P Patrice Lumumba.Your name will always be immortal.

  Erick Machua

  January 17, 2013 at 12:42 PM

 3. Among other things,in his speech at Accra Ghana in 1958 he said,”We wish to see a modern Democratic State established in our country,which will grant its citizens freedoom,justice,social peace,tolerance,wellbeing ang equality with no discrimination whatsoever.”

  I mostly like this part of that speech.

  R.I.P Patrice Lumumba.Your name will always be immortal.

  Erick Machua

  January 17, 2013 at 12:47 PM

 4. Asante sana Ndugu yangu Zitto kwa kumbukizi hii adhimu na muhimu katika kupigania haki na usawa kwa Mwafrika.

  Nafahamu kuwa jitihada za miamba ya Afrika kama akina Patrice E. Lumumba zilikuwa na leongo la ukombozi wa Afrika na watu wake, na zaidi sana kuunganisha nguvu za Waafrika popote pale dhidi ya udhalimu na unyonyaji. Ukombozi huu ulimaanisha umoja ni muhimu sana katika jitihada za kuinua utu wa Mwafrika na kumpatia ukombozi wa kweli kiuchumi, kisiasa na kijamii, kitu ambacho ni nadra sana katika zama tulizomo.

  Ni mtazamo wangu kuwa jitihada za wapigania uhuru wa Afrika zilikuwa ni za kuunganisha Afrika pia. NB: Mwl. Nyerere katika ‘Ahadi 10 za MwanaTANU; “Binadamu wote ndugu zangu, na Afrika ni moja”! Viongozi wa sasa ni wabinafsi, wasiojali wala kuheshimu utu wa binadamu mwingine. Ubinafsi ndo umetufikisha hapa tulipo; angalia jinsi rasilimali za taifa zinavyofujwa bila ya mtu kuona uchungu! Inauma sana! Wako wapi wazalendo kama hawa?

  Rodrick Maro

  January 17, 2013 at 2:47 PM

 5. Thank you @Zitto for reminding us of one of the greatest heroes in Africa. We all need to remember how much these people sacrificed for us. Yet we keep betraying them by embracing what they fought so hard by their soul, blood, and even life. I personally challenged.

  Aikande

  January 17, 2013 at 6:11 PM

 6. When a Chinese contract walk in to Tanzania minister’s office and ask for infrastructure development project such as road construction, he is received with two hands, and automatically he will get the construction project if he pays the highest bribe. The tender process which follows is just a formality, the project is pre-sold. This practice have resulted into 95% of infrastructure projects being awarded to foreign contractors, mostly to Chinese contractors.

  Now if a local contractor try to make an appointment with the same minister, he will be given a running around, even if he meets the minister he will never get the project , he will be asked to tender, but he never be awarded the project. The reason as stated Tanzania ministers and their officers prefer foreign contractors due to chronic corruption disease.

  Where is a policy for local citizen economic empowerment being talked by the government as propaganda?

  This a a missed opportunity, by any means the tax payers have to pay for these development projects running into billion of money. Ministers fail to understand that , if they award these projects to local contractors, there will be a chain reaction of benefits to local citizen, through employment, improved skills of doing business, re-investment of profit gained by local contractors into business expansion within the country, thus fulfilling economic empowerment of local citizen.

  The question is foreign contractors are not investors and they will never be, they utilize the country available funds to make profits , and repatriate the profits back to their own countries. leaving our local contractors and engineers to fend for themselves. In short they become spectators in their own country.

  We must remember the strength of the country is in its people capability to develop their own country.
  The late Mwalimu Nyerere policies of self reliance still apply, may in different fashion.
  Any country which aspire to develop economically depending on foreigners, will fail. It is like sitting on clay soil. Nyerere was smart enough to know this facts more than 59 years back. Arusha declaration, education programs he initiated ” kufuta ujinga ” all points to such long term development plan.

  Each one can ask the ministers prone to awarding these contracts to Chinese contractors, what tangible benefits in terms of local citizen empowerment have they achieved?

  You can see clearly, Chinese contractor can not force our ministers to award them the projects, it is the stupidity of our own leaders coupled with greed, naivety, short slightness and lack of vision for the country development. You ask any most of leaders, how to solve this problem., they will tell you, ” wait we are looking for foreign investors”. How do you expect such leaders to escape economic colonization which Rumumba and Nyerere talked about?

  Alex Kakala

  January 17, 2013 at 7:02 PM

 7. Ni bahati mbaya alikufa mapema mno. Matokeo yake ni vigumu kujua angekuwa kiongozi wa aina gani zaidi ya kuguess tuu. Lakini ipo mifano hai ya wapigania uhuru wengi tuu wa Kiafrika ambao walikuwa kama Lumumba wakati wa kupigania uhuru. Lakini walipopewa nchi baada ya uhuru, walitokea kuwa viongozi wabaya sana, wengi wao wakawa hawataki hata kuondoka madarakani baada ya kunogewa na madaraka, wengine wakawa madikteta, wengine wapo madarakani kwa raha zao mpaka leo. Inawezekana kabisa Lumumba angekuwa kama wao na leo hii tungekuwa tunamchukia kama kama tunavyowachukia hao wengine.

  Inawezekana pia angeweza kuwa kiongozi mzuri. In that case, then angekuwa mpigania uhuru wa kipekee Afrika kutokea kuwa kiongozi bora baade ambaye ukitaja jina lake tuu kila mtu anamkubali. Kwa sasa tunaye Nelson Mandela tuu. Lumumba angeweza kuwa wa pili? Kwa nini?

  Lakini hata kama angetokea kuwa kiongozi mzuri, sidhani kama angeweza kuibadilisha Afrika yeye mwenyewe ikizingatiwa wapigania uhuru wenzake walianza kuponda raha za uongozi na kusahahu walichokuwa wanapigania. Mandela mwenyewe hakuweza.

  Matatizo tuliyonayo tumeyaleta sisi wenyewe. Tufike mahali tujilaumu sisi wenyewe badala ya wazungu. Mchawi tunaye humu humu barani Afrika. Tena ni mweusi tii! Wezi wakubwa wa mali za Afrika ni Wafrika wenyewe tena na wamo humu humu barani Afrika. Tunapishana nao barabarani kila mara. Wengine ni ndugu zetu tena wa karibu sana, tunajua jinsi wanavyoiba, lakini wala hatuwakemei wala kuwachukulia hatua. Tunaishia kulalama labda kwa sababu hatukubahatika kuwa kwenye hizo nafasi walizonazo. Kwa hiyo, Afrika itakombolewa tuu kama tutaacha kuoneana haya humu Afrika. Vinginevyo, baada ya miaka 100 bado tutakuwa kama tulivyo sasa.

  Probably, Lumumba akifufuka leo atashangaa kukuta Kongo na Afrika bado ipo kama alivyoiacha . RIP Lumumba.

  Andrea

  January 17, 2013 at 8:03 PM

 8. mkuu zito hongera kwa kutumegea japo kwa uchache historia ya huyu mwanamapinduzi kijana wa africa

  john mabagala

  January 18, 2013 at 7:39 AM

 9. africa na dunia itamkumbuka lumumba kwa mambo mengi hata aina yake ya kifo ni ya kipekee ambayo inapaswa kukumbukwa na itakumbukwa japo watu wabaya hawapo tayari kukubali. naamini ni suala la muda tu waliofanya ukatili huu watakiri na kutubu.Mungu mlaze pema mwanamapinduzi huyu.Zitto kabwe nakushukuru kwa kutupa profile ya lumumba ambayo iko very silent to the public naamini huu ni mwanzo mzuri wa kufichua wabaya wake na mazuri yake aliyofanya kwetu na kuyaendeleza.

  pazi kitabu

  January 19, 2013 at 8:40 AM

 10. Nakumbuka sana shule nilivyo msoma Patrice lumumba nimwana mapinduzi wakweli ambae kamwe waafrika wenye uchungu bara lao hawata kusahau daima viongozi wa sasa Hawajali watu wapi wanaendekeza tamaa ya mali na madaraka.mungu akulaze Pemba peponi comred

  othumani kihedu

  January 19, 2013 at 10:49 AM

 11. Zitto vaa viatu vya Lumumba.kwa namna ambayo hawatakudhuru hao majangili yanayo chafua na kunyonya Afrika.

  leia

  January 19, 2013 at 3:49 PM

 12. Viongozi wenye nyoyo hizo wapo japo kuwa ni wachache na nadra kuona wakijitangaza ila matendo yao yanadhihirisha dhamira njema kwa Taifa. Tatizo ni mfumo wa Tawala za Maeneo mengi katika Africa wametoka katika dhamira ya Viongozi wetu wa awali kwa walichokipigania na kuingia katika matamanio ya nafsi zao.

  Tunapo wakumbuka viongozi kama ndugu yetu Patrice Lumumba, tunataraji viongozi wetu japo wangetufahamisha machache juu ya walichokipigani ili kizazi kinachokuja na kilichopo kitambuwe nini hasa waliotangulia walikipigania na kwa ajili ya faida ya nani?, tofauti na sasa hasa Tanzania vijana wengi wanachoiga ni matendo wanayoyaona kwa Viongozi wabinafsi na kuamini kuwa labda tuko huru tayali na kilichobaki ni kutumia matunda ya Nchi,kama wafanyavyo Viongozi wetu wa sasa wanaojilimbikia Fedha nje ya Nchi kama vile tumesha jikombowa na tuna UHURU KAMILI ili wakoloni ndio kwanza wamerudi upya na kasi mbaya zaidi kutokana na Tekinolojia ilivyo ya kisasa ndio wanakomba raslimali zetu kwa mda mfupi kwa kiwango cha kutisha kutokana na Viongozi wetu wabinafsi wanaojali Familia zao na matumbo yao.

  Nacho weza kusema ili tushinde na tufikie malengo kitu cha kwanza katika TANZANIA YANGU;-

  1. Udini – Kuna viongozi wanaoona ni ufahali wa dhehebu flani ni bora na linafaa kutawala watu wa
  wanaoamini madhehebu mengine na kufikia kutowa ajira za watendaji hata wasio kuwa na
  ili mradi ni waumini wa dhehebu flani na kuwaacha watu wenye sifa na nafasi hizo au kwa
  sababu atakuwa na mchango wa pato katika dhehebu lake bila kujali hayo mapato yatasa
  idia Taifa au kule dhehebu lilikotokea matokeo yake, tunajikuta tunaishi katika misingi ya
  kubaguwana kielimu,kiajira na hata mijadala ya pamoja juu ya hatma ya Taifa letu kwa ku
  kidhi matakwa ya madhehebu na kusahau matakwa ya wanchi kwa ujumla.

  2. Ukanda – Hili na lenyewe limekuwa ni tatizo linalo tafuna maendeleo na ustawi wa Taifa letu hasa
  athali zake hazina tofauti kubwa sana na matatizo yatokanayo na Udini japo kuwa hili lin
  apelekea maendeleo yasio ya viwango vinavyowiana kati ya kanda na kanda inapelekea
  kupunguza morali katika utendaji wa kazi za kitaifa hasa miradi inapokuwa ya upande
  wa viongozi wanapotokea na kujali majimbo yao ili hali mapato yanatokea majimbo meng
  ine.

  3.Mfumo – Utawala wa mapato yote kupelekwa Dar es Salaam ndio yarudi kwenye vyanzo ni tatizo ten
  a kubwa na ndio mwanzo wa Ufisadi.

  Ushauri kwa Viongozi wetu wanapaswa kujali watu wote kwa usawa na kwa dhamira ya waasisi wa Uhuru wa Taifa letu, wapo waliouuawa kama Patrice Lumumba tuwaenzi kwa kukumbuka nasaha, matendo yao yalio kuwa na dhati ya ukombozi wa kweli na si kuishia kuweka majina ya mitaa na mabarabara kama tunavyo ona katika Tanzania yetu. Madhehebu yawe ni vyuo vya matendo mema na isiwe ni sehemu ya kupandikiza chuki katika jamii. Makabili iwe ni utambulisho tu kwa kuenzi mila na desturi njema na si iwe kigezo cha kutugawa na kusahau nini wananchi wa Taifa hili wanategemea kutoka kwa viongozi wao kwa kukumbuka ahadi walizo nadi na viapo wakati wanakabidhiwa majukumu waliyonayo na hili la mfumo ni vyema vIONGOZI WA TAIFA letu watambuwe kwa idadi tuliyo fikia na utendaji usio na uaminifu suala la utawala ili mapato na matumizi yaweze kudhibitiwa warudishe MAJIMBO ili tuweze kudhibitiana, TUWAENZI WATU NA VIONGOZI KWA KUTENDA MAZURI WALIYAPIGANIA KWA USTAWI WA NCHI YETU NA AFRIKA KWA UJUMLA. Asante kiongozi wetu ZITTO kwa kutukumbusha watu wema endelea na moyo huo. Mungu amuepushe na moto na amujalie rehema na Amani ndugu yetu Patrice LUMUMBA daima atakumbukwa na wote walipigania Uhuru wa kweli katika NCHI ZAO.

  Haji Harun Luge

  January 19, 2013 at 3:52 PM

  • Yaani mie hata naogopa kabisa. Mie sioni kabisa kiongozi anayeweza kutetea nchi yake. Hata kwa upande wa dini tunazoabudu, hapo ndiyo usiseme kabisa. Wachungaji, mapadri, maaskofu, mashehe na makasisi pamoja na wainjilisti ni sawa na wakoloni tuu. Nao pia kwa sababu dini zilianzia nchi za magharibi, wanafuata kile kinachosemwa kutoka huko magharibi. Mie naona hakuna haja tena ya kumtumainia kiongozi yeyote awe wa dini au wa serikali. Wakoloni walimuua Edward Moringe Sokoine, nchi ikakaa kimya tuu na kulete habari zisizofaa. Nadriki kusema hivyo kwani hainiingii akilini msafara wa waziri mkuu ulivyo na magari mengi na ulinzi wa kutosha upate ajali na afe waziri mkuu peke yake bila hata mmoja kuumia. Nasema walimuua! Africa kabla ya uhuru ni sawa tu na baada ya uhuru. Anahitajika kiongozi! Kiongozi asiyekufa! Kiongozi anayeweza kusoma mawazo ya mtu yeyote kabla hajayawaza! Kiongozi awezaye kujua hitaji la kila mtu kabla mtu yule hajahitaji! Kiongozi aonaye kila mahali na kwa wakati mmoja! Kiongozi asiyefichwa na jambo lolote lile. Kiongozi ajuaye kuliko wote anaowaongoza! Anahitajiwa kiongozi! Hatimaye tutampata!

   David Moses

   May 1, 2014 at 4:11 PM

 13. Mungu amlaze mahali peponi,Amina.
  Ila Zitto hao mapebari na nchi unazoziongelea kweli hazijawahi kukusaidia wewe binafsi kwa hali na mali (I.e. scholarships au nauli kwenda kwenye makongamano nje?).

  Lazima tubadili world view yetu maana wengi kizazi hiki tupo huku na huku. Singapore imeendelea kwa kujijua na kuelewa kwamba uzalendo sio kulaumu wakoloni bali kuwapiku kwa kukufanya kazi kwa bidii. Pia kwa kuwaengage kama wadau maslahi yakigongana.

  Majaliwa

  January 20, 2013 at 5:34 PM

  • On Lee Kuan Yew, first PM of Singapore:

   He shared with his guests how Singapore had overcome its challenges.

   It was thanks to globalisation and the presence of transnational corporations like Total that Singapore survived, after it was thrust into independence following separation from Malaysia, and had no resources to call its own, he said.

   “We had no reason to believe we could go from a per capita GDP of just over a thousand, to now around $54,000. What was the miracle? Globalisation,” he said.

   Singapore benefited by being a port of call for ocean trade, but more than that, he said, “we learned how to create conditions that gave confidence to investors, made living in Singapore safe for foreigners and their families”.

   Majaliwa

   January 20, 2013 at 5:58 PM

 14. […] After reading Mr.Kabwe’s blog entry- ‘Lumumba, Miaka 52 ya kifo chake, Afrika ipo vile vile’ (https://zittokabwe.wordpress.com/2013/01/17/lumumba-miaka-52-ya-kifo-chake-afrika-ipo-vile-vile/), my interests to learn more about DRC was rejuvenated.  I knew that to grasp the urgency of […]

  • Yani kaka Zitto hakika umenikumbusha taabu niliyoipata ndani ya nafsi yangu ktk kpnd kile niliposimuliwa na mkongo mmoja mpenda amani na mwanamapinduzi kama mimi habari hizi za LUMUMBA na jamani nchi za Afrika, Waafrika wenzangu naombeni tuungane tuwe kitu kimoja tuupiganie uhuru wa kweli ktk kila sector kwani hadi sasa tumekuwa bdo jamii yakufanya yale wenzetu wanayotaka tufanye ni wakati wa kufanya wenyewe kwani tunajitosheleza karibia kila kitu nchi yetu sio makapi ina kila utajiri tunao

   Fau

   June 2, 2013 at 11:40 PM

 15. hapa katika orodha ya wagombania uhuru wa kweli, nyerere muondoweni kwani alikuwa miongoni mwa remote of neocolonilism..

  JUMA ISSA

  January 1, 2014 at 7:42 AM

 16. Hapo humenikuna vya kutosha sana, ndo maana siku zote mimi namchukia mtu anayeitwa mzungu. Afrika itakombolewa na vichaa na siyo mashalobalo. Kikubwa hapa ni kujitambuwa tu, mbona Mugabe anaweza?

  Henri Malumalu

  April 14, 2015 at 12:35 PM

 17. kweli Lumumba hataki kuwa mwamba wa afrika

  zacharia mussa

  September 5, 2015 at 3:35 PM

 18. kwanza na toa shukurani zangu za zati kwa kunipa story ya nyumbani kwangu, mungu hakubariki Mzee.

  Tuta zidikua kuwa kumbuka viongozi wetu waliotupigania uhuru wetu was Africa

  suleima Amani

  October 22, 2015 at 6:12 PM

 19. Mungu aiweke roho yake mahali pema AMINA.wako wapi viongozi wa kiafrika wa naofuata misimamamo kama hii kwa sasa Afrika ?waliokuwepo wanajali matumbo yao ubinafsi

  mgoa saidi

  January 17, 2016 at 11:17 AM

 20. asante sana mh. nzito kabwe kwa kutupahistoria nzuri inayofundisha na kutupa mwanga nini cha kufanya wakati haki na uhuru unaminywa na watu wachache

  paulo lulandala

  August 15, 2016 at 6:16 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: