Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Maandamano dhidi ya Bomba la Gesi: Kilio cha Uwajibikaji

with 24 comments

Maandamano dhidi ya Bomba la Gesi: Kilio cha Uwajibikaji

Maandamano dhidi ya Bomba la GesiPicha Hisani ya: Mtwara Kumekucha Blog by Baraka Mfunguo

Maandamano dhidi ya Bomba la Gesi
Picha Hisani ya: Mtwara Kumekucha Blog by Baraka Mfunguo

‘Dar inachangia asilimia 80 ya mapato. Kitovu cha Uchumi. Dar inachangia 90% ya ufisadi. Uti wa mgongo wa ufisadi nchini’

Malumbano kati ya wananchi wa Mtwara na Serikali kuhusu matumizi bora ya utajiri wa nchi yameendelea kwa takribani wiki moja sasa. Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Nishati na Madini kuwaita Watanzania wa Mtwara Wahaini, wapuuzi na watu hatari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naye aliingia kwenye mjadala huo kwa kuonya watu wanaowaunga mkono watu wa Mtwara na kuwaita watu wanaotafuta umaarufu wa kisiasa na wanaotaka kugawa nchi. Siku moja baada ya hotuba ya Rais, Waziri wa Nishati na Madini alifanya mkutano na waandishi wa habari kueleza suala lile lile ambalo bosi wake alilielezea usiku wa kuamkia mwaka mpya 2013. Hii ni dalili ya Serikali kuweweseka.

Katika kauli ya Serikali, ambayo haikuwa na jipya zaidi ya wimbo ule ule wa ‘kugawa nchi’ ‘umaarufu wa kisiasa’ nk, Serikali ilitaka kuonyesha umma kuwa watu wa Mtwara hawana shukurani. Kwamba miaka yote toka Uhuru watu wa Mtwara wamekuwa wakilishwa na Pamba, Kahawa, Chai, Tumbaku, Sukari, Kidatu nk. Kwamba watu wa Mtwara na Lindi hawakuchangia hata kidogo kwenye hazina ya Taifa. Hivyo wao kupigia kelele gesi yao ni uchoyo na roho mbaya na kukosa shukurani. Kauli ya Serikali ni kauli ya chombo kinachoendelea kukosa ‘legitimacy’ ya kuongoza taifa. Ni kauli ya kukata tamaa. Ni kauli hatari sana dhidi ya Watanzania waliojitolea damu kulinda uhuru wa nchi yetu.

Moja, Serikali katika kauli yake haitaji kabisa kwamba toka Uhuru watu wa Mtwara na Lindi wamekuwa wachangiaji wakubwa sana katika uchumi wa Taifa kupitia zao la Korosho. Takwimu za Uzalishaji wa Korosho zinaonyesha kwamba kuanzia mwaka 1965 mpaka 2011 Korosho imeliingizia Taifa fedha kigeni jumla ya dola za Kimarekani 4.58 bilioni ( Cashewnuts Sub-sector study 2003, Hali ya Uchumi 2012, Cashewnuts Tanzania Report 2010). Katika Mwaka wa Uchumi unaoishia Novemba 2012, Korosho imeliingizia Taifa jumla ya dola za Kimarekani 151 milioni. Katika mwaka 2011 zao hili liliingiza dola 130 milioni wakati Pamba iliingiza dola 53 milioni tu. Licha ya Zao la Korosho kuingiza fedha hizi za kigeni  (sawa ni shilingi trilioni 7.2) kwa nchi mikoa ya Lindi na Mtwara ipo miaka 50 nyuma kimaendeleo kulinganisha na mikoa mingine ya Tanzania. Serikali inataka kufuta historia ya mchango wa zao la Korosho kwenye uchumi wa nchi yetu kwa sababu ya uroho wa gesi asilia. Kwa nini kauli rasmi ya Serikali haijataja Korosho kabisa? Kauli hii ilipitishwa na ngazi zote za Serikali? Mawaziri wa Serikali wanaotoka mikoa ya Lindi na Mtwara walikubali kauli kama hii itoke dhidi ya wananchi wao wanaoteseka na zao la Korosho miaka nenda miaka rudi?

Pili, Serikali imesahau kabisa mchango wa watu wa Lindi na Mtwara katika ulinzi wa Taifa letu. Moja ya sababu ya mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa nyuma kimaendeleo ni juhudi za ukombozi wa kusini mwa Afrika. Kambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji ilikuwa Nachingwea. Kambi ya Frelimo iliwekwa kwenye Shamba la Mkonge kilometa 17 tu kutoka mjini Nachingwea ambapo ilikuwa makao makuu ya ukombozi wa Msumbiji. Rais Samora Machel, Rais Joaqim Chissano na Rais Guebuza waliendesha mapambano kutoka kusini mwa Tanzania. Makaburu wa Afrika Kusini na Wareno walikuwa wanashambulia nchi yetu na mikoa hii miwili ya Lindi na Mtwara ikawa ‘buffer zone’. Wakati Dar es Salaam inaendelea kwa kila aina ya maendeleo, mikoa ya Lindi na Mtwara ilikuwa inalinda ili wanaoishi Dar es Salaam na mikoa mingine waishi wa amani na starehe. Serikali inapimaje mchango huu wa mikoa hii? Tunaipima kwa fedha? Uroho wa gesi asilia kuzalisha umeme wa kufurahisha walalaheri asilimia 14 nchini ndio inaifanya Serikali kusahau kabisa ‘sacrifice’ ya watu wa Mtwara katika kulinda uhuru wa Taifa letu?

Tatu, Serikali inasema lazima bomba lije Dar es Salaam kwa sababu Dar ndio inazalisha asilimia 80 ya Mapato ya Serikali. Kwanza huu ni uwongo. Ni aibu Serikali kujitetea kwa uwongo. Dar es Salaam ni kituo tu cha kukusanyia mapato ya Serikali. Uzalishaji mkubwa wa nchi yetu wenye kuzalisha kodi unafanyika nje ya Dar es Salaam. Walipa kodi wakubwa wengi Ofisi zao Kuu zipo Dar es Salaam lakini uzalishaji wao unafanyika nje ya Dar es Salaam. Serikali itoe orodha ya walipa kodi wakubwa 100 tuone uzalishaji halisi wa mapato hayo unafanyika wapi. Hata hivyo inawezekana kuwa ikawa kweli Dar es Salaam inakusanya asilimia 80 ya mapato ya nchi. Basi na tuseme Dar es Salaam inachangia asilimia 90 ya ufisadi wote nchini. Kashfa zote kubwa za Ufisadi zinafanyika Dar es Salaam na fedha nyingi za ufisadi zinatumika Dar es Salaam.

Mwisho, maandamano ya watu wa Mtwara ni kielelezo tosha kwamba watu wa mikoa ya Lindi na Mtwara wamechoshwa na longolongo za Serikali. Wananchi wa Mtwara na Lindi wanataka Uwajibikaji wa Serikali kuhusu utajiri wa nchi. Mtanzania yeyote mwenye tahadhari ya nchi yetu kutokuwa na laana ya rasilimali ataungana mkono na watu wa Lindi na Mtwara kudai maendeleo. Nilitoa mfano wa Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu yote tani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega. Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza dola 370 milioni kuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June 1997). Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14,  Kampuni hii imeuza dhahabu ya thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni. Kabla Serikali haijawaita watu Mtwara wahaini, wapuuzi na watu hatari, iwaambie watu Watanzania kodi kiasi gani imekusanywa kutoka mgodi huu katika kipindi cha miaka 14. Mpaka mwaka 2008, kwa mujibu wa Taarifa ya Kamati ya Bomani, kampuni hii ilikuwa imelipa mrahaba wa dola 11 milioni na kodi nyingine dola 16 milioni. Serikali itwambie ilipofika Disemba 2012 kodi kiasi imekusanywa kutoka kampuni hii?

Pia watu wa Mtwara na Lindi wameona historia ya bomba la Songosongo. Hata kodi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (0.3%) ilikuwa inalipwa Halmashauri ya Manispaa Ilala na kampuni ya Pan Africa Energy. Ilichukua juhudi za mbunge wa Kilwa Kaskazini Murtaza Mangungu kuingilia kati ndio kodi ikaanza kulipwa Kilwa ambapo uzalishaji unafanyika. Watu wa Mtwara ni werevu, wanajua wafanyalo. Wanataka utajiri wa nchi unufaishe nchi kwa kuanzia kule utajiri ulipo. Kuna dhambi gani?

Uwajibikaji katika uvunaji wa Rasilimali ya Gesi ndio chanzo cha maandamano ya watu wa Mtwara. Serikali isikimbilie kulaumu wanasiasa kwamba ndio wamechochea maandamano haya. Haya ni maandamno ya wananchi wakitaka Serikali yao iwajibike kwao. Serikali ithubutu kufanya ubabe wa kujenga bomba la gesi bila ridhaa ya Wananchi wa Lindi na Mtwara. Wananchi wanapohitaji uwajibikaji ni wajibu wa Serikali kuwajibika kwao ni sio kuwaita wahaini, wachochezi, watu hatari, wapuuzi. Watu wa Mtwara wamechangia maendeleo ya Taifa letu kwa jasho na damu. Serikali ina wajibu wa kuwasikiliza, kuwaelimisha na kupata mwafaka. Kauli ya Serikali imewatukana watu wa Mtwara na Lindi. Hawatakubali kudhalilishwa. Hawatakubali historia yao kufutwa. Hawatakubali waendelee kubaki nyuma kimaendeleo. Serikali ifikirie tena.

Written by zittokabwe

January 3, 2013 at 2:10 PM

24 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. Ni kweli maandamano ya mtwara yanatija c kupuuzwa wasikilizeni hao wananchi wanadai haki yao ya msingi

    Mussa

    January 3, 2013 at 2:43 PM

    • Hoja ya wananchi wa Mtwara inamashiko makubwa,hawakatai umeme wa gesi kunufaisha taifa kwea ujumla,ila wanataka wao wawe wa kwanza kuonja keki!!!hivi ukichinja mbuzim nyumbani nani anakula maini kwanza??nani anapeleka maini kwa jirani au kisusio!!!
      Mbona wananchi wanaoishi karibu na Hifadhi zetu za wanyama H/mashauri zao hupata 25% ya mapato yatokanayo na hifadhi hizo!!bali na hayo makampuni zote yanayowinda hutoa 20% ya mapato kwa wanavijiji husika wa maeneo ya karibu.Iweje Mtwara na Lindi waonekane wabaya???
      Kwanini kila kitu lazima ianzie Dar??Kwani mtambo wa umeme ukijengwa Mtwara umeme haiendi Dar??Kwani unahitaji gravity kusafirisha umeme??Gharama ya bomba ya kusafirisha kilometa 1000 toka Mtara hadi Dar na gharama ya kuweka mtambo Mtwara ipi kubwa au ni 10%inawatoa roho viongozi??Waziri wa maliasili amewaita watu Mtwara eti wanaelimu ,eti hata walioandamana elimu yao ndogo,Kwanini kwanza waziri anakiri kuwa Mtwara elimu ndogo,basi tatizo si yao ni serikali kwanini haijawasomesha ???kudai haki inayokustahili inahitaji elimu kiasi gani??Kwanii maprofesa wengi hutoa maneno ya dharau hasa kutukana wanachi kuhusu elimu.Inamana kuwa Profesa ndio mwisho kila kitu??Ndio maana Profesa yeyeote hafai kuwa kwnye chombo cha maamuzi kama polisi ,mahakama au raisi angeua watu sana wabaki kufanya reseach sisi wenye elimu ndogo lakini tuna busara tutatumia hiyo resech yao kungoza nchi,tokeni maprogfesa kwenye serikali mtaleta balaa.Kamanda ZITTO elekea Mtwara wape hii data uliyotoa mandamano yaendelee,hii serikali siyo yakuzungumza nao tena tunahiji vitendo.Kamanda Bush-Arusha

      kalisti lazaro

      January 8, 2013 at 3:53 PM

      • *LATEST HOT NEWS: NEW ROADS TO BE CONSTRUCTED IN TABORA WORTH 380 BILLION SHILLINGS HAVE BEEN SOLD TO CHINESE CONTRACTORS: * *TODAY DAILY NEWS PAPER PUBLISHED NEWS OF TANZANIA PRESIDENT FLANKED BY MINISTER OF WORKS AND TANROADS OFFICIALS, PROUDLY ANNOUNCING ANNOUNCING THESE PROJECTS TO WANACHI.*

        AFTER 51 YEARS OF INDEPENDENCE, DO TANZANIA NEED TO DEPEND ON CHINESE COMPANIES FOR EACH AND EVERY INFRASTRUCTURE PROJECT?

        ARE TANZANIA LEADERS CONSPIRING WITH CHINESE GOVERNMENT TO KILL THE TANZANIA LOCAL PROFESSION, SO THAT FOR EVER WE HAVE TO DEPEND ON CHINESE?

        IS THE TANZANIA BUSINESS TO ENSURE THE SURVIVAL OF CHINESE COMPANIES BEFORE EVEN TAKING CARE OF OUR OWN PEOPLE?

        WHAT A SHAMELESS AND DISGUSTING ACTION BY TANZANIA GOVERNMENT TO CONTINUOUSLY AWARDING ALL THESE INFRASTRUCTURE PROJECTS TO CHINESE COMPANIES DESPITE OUTCRY BY TANZANIA PUBLIC TO STOP. SINCE THESE LEADERS CAN NOT LISTEN TO THE PUBLIC ANYMORE , IT IS TIME THEY BE REMOVED FROM POWER. WANANCHI CAN NOT CONTINUE WATCHING AND LISTENING TO PROPAGANDA, WHILE THEIR ECONOMIC SECURITY IS BEING PRONDERED BY THE SAME PEOPLE THEY ELECTED TO TAKE CARE NATIONAL ECONOMY AND ITS PEOPLE.

        *WE ARE DEMANDING THE FOLLOWING ACTION TO BE TAKEN:*

        * *

        1) ALL THESE TABORA ROAD PROJECTS SHOULD BE IMMEDIATELY SUSPENDED

        2) THE CONTRACTS SHOULD BE NULLIFIED

        3) PARLIAMENTARY COMMITTEEMEN LED BY ZITTO KABWE , ATTONERY GENERAL, AUDITOR GENERAL SHOULD TAKE OVER THESE PROJECTS AND RE-TENDER THEM TO LOCAL,CONTRACTORS AND INVESTIGATE THE CASE.

        4) CHINESE CONTRACTORS SHOULD BE IMMEDIATELY DEPORTED

        5) THE CASE MUST BE LOGGED TO WTO AGAINST UNFAIR PRACTICE BY CHINESE COMPANIES TO AFRICAN COUNTRIES , DEPRIVING LOCAL AFRICAN OPPORTUNITY BY BRIBING AFRICAN LEADERS.

        *ENOUGH IS ENOUGH, 51 YEARS OF INDEPENDENCE , LOCAL ENGINEERS CAN NOT BUILD THESE ROADS, AND WE SHOULD DEPEND ON CHINA FOR EACH AND EVERY THING?*

        * *

        *by Alex Kakala*

        Alex Kakala

        January 9, 2013 at 3:44 PM

  2. kusema kweli w2 wa mtwara wakomae hivyo hivyo kwani ikitoka 2 hawana chao tena ushauli wangu ni huo ila kama viongozi wao wakiwa kimya basi wananchi watakuwa sawa na hakuna kwani hata wapige kelele namna gani haitasaidia kwa sababu hawana nguvu viongozi 2saidiane hili swala na sio kuwaunga mkono hao serikali http://www.natafutanapata.com/nandule

    kassim nandule

    January 3, 2013 at 3:51 PM

  3. The main problem is not what Mtwara people are demonstrating, I think the main problem is the luck of a well organized and competent system to manage entire natural resources investments. From mining sector, to oil and gas, Watanzania have never seen or witnessed any beneficial program by the government put in place to run these investments. From Geita, Mara, Shyinyanga, Arusha, Mbeya were all minerals are situated people do not see any economic benefit impacted on them due to foreign investments conducted by the government. They see skewed contracts, based on corruption, each minister running to get Chinese contractors who are believed to give huge sum of bribes and keeping secret. The country has been loosing and continue to loose economic security form natural resources due to corruption. Therefore Mtwara people have no hope and do not trust whatever the government trying to tell them, hence they are demonstrating in act of desperation.

    Alex Kakala

    January 3, 2013 at 5:52 PM

  4. Rasilimali za mtwara kwanini zinufaishe kwanza watu wa dar? Umekuwa ni upuuzi unaofanywa kila siku katika nchi hii jambo linaloendelea kusababisha umikoa! Tofauti kubwa ya maendeleo ya nchi hii husababishwa na na baadhi ya watu wenye tamaaa! Kwani ni lazima kiwanda cha kusindika ges kijengwe dar kwa kusudi gani? Tunahitaji kupunguza watu dar na sio kuongeza watu dar! Wananchi wa mtwara wapewe haki yao!

    Melkior patrick

    January 3, 2013 at 6:32 PM

  5. Zitto,

    Good article. Kweli inaonekana kama serikali imeshindwa kuwajibika. Sidhani kama ni busara kwa viongozi wa serikali kuwaita wananchi wa Mtwara wahaini, wachochezi, hatari au wapuuzi. Serikali ina wajibu wa kuwasikiliza kwa makini.

    Umemalizia kwa kusema kuwa “Serikali ifikirie tena.” Lakini kusema tuu serikali ifikirie tena, sidhani kama umetoa alternative kwa wananchi wa Mtwara. Ukiwa kama kiongozi wa ngazi ya juu wa chama kikuu cha upinzania nchini, ingekuwa bora kama ungeenda mbele zaidi kwa kutoa alternative. Kusema tuu kuwa serikali ifikirie tena ni kama vile unaishauri serikali.

    Lakini wewe siyo mshauri wa serikali. Wewe ni mpinzani wa serikali na unatakiwa kukosoa na kutoa alternative ambayo ungefanya kama ungekuwa madarakani. As an apposition ni nini ambacho mngefanya ambacho serikali ya sasa imeshindwa kufanya? That is what people of Mtwara and others voters would like to hear.

    Tayari serikali imeshaonyesha msimamo wake na kujaribu kuishauri ni sawa na kupigia mbuzi gitaa. Lakini ukija na alternative ambayo chama chako kitafanya kama kikiingia madarakani na kuweza kuwashawishi watu wa kusini na wananchi wengine kwa ujumla, basi hapo wapiga kura watakuwa na options. Tena hiyo alternative ya chama chako inaweza kuishawishi serikali kufanya u-turn. Mfano mzuri ni suala zima la katiba mpya. Katiba mpya haikuwa kwenye ilani ya CCM lakini ilikuwa kwenye ilani ya chama chako. CCM imejikuta yenyewe ikitekeleza ilani ya chama chako. Iwe hivyo kwa mambo mengine pia.

    Kwa maoni yangu, kama mpiga kura wa Mtwara, nishawishi kama chama chako kikiingia madarakani mtalitatuaje hili tatizo? Kuishauri tuu serikali ambayo tayari imeshafunga mlango wake sidhani kama utakuwa umenipa options kama mpiga kura unless labda uniambie kuwa sera za chama tawala na zile za chama chako ni sawa, kwa hiyo hakuna jipya ambacho chama chako kingefanya.

    You want my vote? Tell me how you would address the problem if you were in power; not how you would advise those in power who have already failed to address the problem.

    Sungi

    January 3, 2013 at 7:31 PM

    • Bw/Bi Sungi.

      Nimeupenda mchango, lakini unafikiri kipi kifanyike ambacho Zitto anaweza kukitumia kama mbadala? Nikiwa na maana, unafikiri CHADEMA itoe ahadi gani kwa wapiga kura kuhusiana na utajiri wa gesi huko mtwara?

      Dotto Rangimoto

      January 4, 2013 at 12:29 PM

  6. KWANZA: Pamoja na kwamba najua ni wajibu wako kama mbunge na kiongozi wa kada ya juu ndani ya chama chako katika kuikosoa, kuishauri na hata kuilazimisha serikali kwa nguvu ya hoja katika kuhakikisha serikali inawatumikia wananchi ipasavyo, naomba nikupongeze kwa ufafanuzi wa kina juu ya suala hili,

    PILI: Naomba niungane na mchangiaji mwenzangu, Bw/Bi Sungi katika yale aliyoyasema. Mh. Zitto makala yako haijaja na mbadala, nafikiri wanachi wa Mtwara wanahitaji mbadala, mbadala ambao utazingatia maslahi ya wana Mtwara kwanza. Mfano wanahoji, barabara imechukua miaka zaidi ya arobaini na bado ukute haijakamilika, lakini bomba la mafuta litachukua miezi 18. Unafikiri kuna uwezekano miradi ya gesi kuwekezwa Mtwara badala ya Dar es salaam? Kama hakuna, kwanini Dar es salaam, na isiwe Mtwara?

    TATU; Kuna haja ya rasimali za mikoa zianze kuwanufaisha wazawa kwanza kabla hata ya watu wa mikoa mingine, ndio kusema sera ya majimbo ni muhimu sana. Kuna dhana kuwa wanasiasa wanaelekeza miradi ya maendeleo kwenye mikoa wanayotoka au maeneo wanayotoka. Nadhani serikali ya majimbo ni muhimu sana, na tutumie mwanya wa mchakato wa katiba mpya kufanya hayo.

    NNE: Naomba kwa kutumia wadhifa wako wa ubunge, uende na hoja binafsi katika bunge lijalo, hoja ambayo itakayokuja na mbadala wa matumizi wa rasilimali ya gesi, mbadala ambao utakuwa ndio dawa wa tatizo hili. Hata kama ujenzi utaendelea, lakini, je, wanamtwara watafaidika vipi? hapa tunataka faida za mojakwamoja.

    Mwisho nakutakia mwaka mpya wewe na familia yako.

    Njano5.

    Dotto Rangimoto

    January 4, 2013 at 12:25 PM

  7. Zitto we nakukubali,kwetu kigoma fanya juu chini mtwara na lindi wpate haki yao haiwezekan gas itumiwe mhl icpo zalshwa

    Issac

    January 4, 2013 at 5:09 PM

    • uko sahihi kaka.

      Dotto Rangimoto

      January 5, 2013 at 12:40 PM

      • Two main proposals: No.1) Natural resources(mining, oil and gas) should be placed under a special commission comprising all stake holders in the country: Presidential commission(state house), ministry of ( minerals, finance, trade and economy, labor, law) ngo, wananchi representative from each region and expert. the commission should be almost similar to Katiba commission led by Warrioba. The commission should be tasked with drawing a comprehensive policy on natural resources exploration, investments, 100% Tanzania ownership, in case of JV with foreign company majority share should be won by Tanzanian. Policy on local citizen empowerment with full participation, usage, distribution, priorities to national development projects, benefits to local -region where resources are based, licencing, local market and export market, re-investment of revenue to social and economic development. All must be put on the table, and Wananchi participation in debate must be pre-requisite.

        No.2) Combating corruption. It is useless to draw a comprehensive effective policy to manage the country natural resources, if not implemented accordingly, thrown out by leaders trusted to execute the programs in quest of seeking corruption. The system must be in place for check and balance, monitoring, transparent. ISO system, ICT, must be immediately adopted from day one. Strict laws must be put in place and stern actions taken for anyone violating the laws governing the implementation.

        No.3) Key Performance Index for monitoring targeted achievements must be in place, and reported to all stake holders. for example if we target Tanzanian to own 5 large mining operations in 5 years, planning and monitoring the progress monthly for 5 years.

        No 4.) Winner take all policies and mentality must be totally discarded. No more 100% foreign ownership of any natural resources investment. If Watanzania are not ready, then continue to build the base, I think they all ready, only bold, unwavering leadership is required, the commission will ensure the capable leaders are appointed to lead. Remember to avoid following a band wagon, just because a neighboring country has implemented 100% foreign owned natural resources, we need not follow the same policy if do not suit Tanzania national development requirements.

        No.5) Government not listening: It is true, the ministry of ministry of energy and natural resources have never listen to wananchi. Numerous suggestions to form a special commission have been put forward several years back, and almost every month till to date, but they pay deaf hear.They view citizen suggestions as waste of time, because they are in hurry to sell whatever to foreign investors in peruse of corruption, quick personal gains. They are dead wrong! They can measure what progress they have achieved in relation to economic development of the country and its people, local empowerment. Graduates are languishing in streets looking for jobs. You won’t be surprised a Chines construction company technician harassing local Tanzanian Phd holder at work. Because our own leaders we trusted and put in place manage the country economic security of natural resources, have deviated and surrendered to anyone who show up with bundles of money. Go to Germany, Holland , Scandinavia, USA, China, India, see who run the country’s economy? Their own citizen, then why Africa including Tanzania are to become spectators and rubber stamp so called foreign investors economic manipulative policies? To me Mtwara issue is just a conformation of long delayed economic policy revolution in the country. It is the issue of the whole country, Geita-Tabora, Shinyanga, Mara, Kagera, Arusha, Mbeya, where all mines are situated, show me what local people have benefited, do they own these mines? How many percent of mining profits by foreign owners goes into national and local regions social and economic development? Just building one school or providing school desks as show games are all insults to local communities. Tanzania under the late Mwalimu Nyerere established education policies tailored to produce engineers, technicians, ready to take control of natural resources since independence 1961. Today our ministers are running amok to China, India, Korea, etc to get engineers to build a simple road, mining, to construct a simple building or water supply scheme. What a shame and insult to intelligence of local professionals? If doctors at Muhimbili hospital can conduct operation to every Mtanzania in need of services, what is so difficult a mining engineer can not run the mines? Which is more life threatening? now you can remember all those words Mwalimu used to address the nation, sometimes we used to lough as jokes, but it is all true before our own eyes. Self reliance in any form is needed to build the nation and empower local people. Tanzania need Chinese army to keep the country safe? The answer is no! Why? Tanzania army is capable of doing the job, because was exposed to do job. Engineers are kept to sign documents and crap and hands to so called foreign investors while bosses pocketing millions of man and sell all the projects to foreigners. Who to blame? Guys think carefully, it is not a gas pipe or oil rig, it is entire system need to be overhauled, then each Mtanzania can see and feel the benefits of our natural resources through full participation.

        2013/1/5 Zitto na Demokrasia

        > ** > Dotto Rangimoto commented: “uko sahihi kaka.” >

        Alex Kakala

        January 5, 2013 at 10:59 PM

  8. Asante Doto Rangimoto kwa majibu,

    Kama ndiyo hivyo basi, ni bora tuu kurudi kwenye mfuno wa chama kimoja. Nini hasa maana ya kuwa na mfumo wa vyama vingi? Siyo kuwapa wapiga kura mbadala? Kama ni hivyo, watajuaje una alternatives kama hutawaambia? Chama za upinzani lazima kijue matatizo yanayowakabili wananchi na kije na alternatives za kuyatatua.

    Tatizo kubwa la upinzani Tanzania ni kwamba haujui kazi yake kama upinzani. Demokrasia inafanya kazi on the basis kuwa kuna alternatives mpaka kuchagua serikali. Hii inaenda mpaka bungeni ambapo kila upande unatakiwa kutoa alternatives zake kwa kipindi kizima cha bunge.

    Alternatives zinajumuisha siyo zile za serikali bali pia zile za upinzani ambao unatakiwa kupinga sera mbaya sa serikali kwa kuja na sera zao ambazo wanaamini ni bora zaidi. Kwa maana nyingine, wabunge hasa wale wa upinzani wanatakiwa kuja bungeni na kujadili alternative policies hata kama hawako ndani ya serikali.

    Ni-quote sehemu “The opposition has a duty to themselves and to their voters to play the role of an alternative government and indeed, the role of a government in waiting. The leader of the largest opposition party should be regarded as the President waiting. He has to be ready to perform the role of running the country at comparatively short notice.

    Sasa hebu niambie kwa suala zima la mgogoro uliotokea huko Mtwara did Chadema act as a government in waiting? Kwa mfano, unaweza kusema kuwa kwa Mh. Zitto kuishauri serikali iwasikilize Wana Mtwara ndiyo ku-act as a leader in waiting? Unless anataka kuendelea kubakia kwenye upinzania, a President in waiting huwa anamshauri the President in power jinsi ya kufanya kazi yake au ana step in na kuja na altenative ambayo angeifanya kama angekuwa au atakapokuwa madarakani?

    Niseme tuu kuwa kila Mtanzania na institutions mbalimbali zina majukumu ya kujenga taifa. Kwa maana hiyo basi, kama institution, hata chama kikuu cha upinzani kina majukumu yake pia ya kulijenga taifa. Lazima kije na alternatives ya jinsi watakavyoongoza taifa na jinsi ya watakavyotatua matatizo yanayotukabili. Badala ya kuishauri serikali iwasikilize Wana Mtwara, Mh Zitto anatakiwa awa-convince that Chademna, as a government in waiting (unlike CCM the government in power), they will not only listen to them, but they will also act differently (alternatives) when they take over the government.

    Kwa hiyo, kwenye suala la kujenga nchi, Mh. Zitto kama Zitto ana majukumu yake kwa taifa kama uliyonayo wewe na mimi. Lakini Mh. Zitto kama mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa chama kikuu cha upinzani nchini ana majukumu zaidi ya sii tuu kuisokoa serikali bali pia kutueleza wapiga kura wa Mtwara kuwa chama chake kina alternative ipi ya kutatua tatizo lao la gesi. Akiwa kama kiongozi wa upinzani (Chadema) siyo jukumu lake la kuishauri serikali. Vinginevyo wataendelea kubakia wapinzani milele na milele, AMINA.

    Sungi

    January 5, 2013 at 4:08 AM

  9. Maendeleo katika jiji laDar es salaam ni kutokana na uwepo wa mahitaji muhimu ambayo yanamfaa binadamu wa karne hii.Katika kukataa na kutowasikiliza wananchi kwa mahitaji yao wanayoyapigania ni kuendelea kutowasikiliza wananchi na kuwaita majina yasiyofaa.Hivi kweli mpiga kura aliye kupigia kura unaamua kumtusi eti utegemee akuchague tena hizo ni ndoto.

    Sera yenyewew ya utafutaji,uchimbaji na usambazaji walipaswa wananchi washirikishwe katika maamuzi.Mimi ni mkazi wa Geita lakini naona ni vema hata kusini wakasikilizwa ili napo paaendelee kama hawata wasikiliza gesi kupelekwa Dar ni ulaji wa mafisadi.

    Ndugu zangu wananchi inchi yetu imegubikwa na udikiteta au aimura wa mawazo unaofanya na serikali ya chama cha Mapinduzi na serikali yake.Wasifikiri sisi watanzania tumechoka sana na mfumo mzima wa kimaamuzi katika nchi yetu mnyonge hathaminiki wala mawazo yake.

    Furaha ya ufisadi ni kuona umaskini unakithiri (The pride of corruption is the famous absolute poverty indeed absolutely poverty) .

    nubi

    January 5, 2013 at 6:02 PM

    • Nubi uko sahihi, ushirikishwaji wa wananchi ni muhimu sana kabla hata ya utiaji saini mktaba na utekelezaji wa mkataba. yote haya yataisha endapo tu tukibadilisha serikali na kuweka serikali ya chama kingine, tushirikiane vijana wenzangu.

      Dotto Rangimoto

      January 5, 2013 at 8:13 PM

  10. Mh ZItto kabwe naomba ujue kwamba wewe ni zaidi ya mawaziri wote katika serikali ya dhaifu so issue ya gesi iko wazi haitaji uwe profesor kujua ukweki wa madai ya wananchi mtwara. so tutawaonyesha 2015.

    Chilindima

    January 6, 2013 at 10:47 PM

  11. Pamoja na kwamba madai ya wenyeji wa Mtwara kutaka matumizi ya gesi asilia ya Mtwara itumike kwa ajili ya shughuli za kiuchumi huko Mtwara badala ya Dar es Salaam ni yaliolenga kuwapatia watanzania wote kama taifa moja faida kubwa zaidi, ukweli ni kwamba sio wakati wote na mahali pote raslimmali kutumika palepale inapopatikana inakuwa njia pekee au bora zaidi katika kuhakikisha matumizi ya raslimali hiyo yanakuwa na faida kubwa zaidi kwa wenyeji wa eneo husika na kwetu sisi sote kama taifa moja. Pia, kusema ni lazima wenyeji wa Mtwara wanufaike zaidi kwa kuwa wako karibu zaidi na machimbo ya gesi asilia ya Mtwara kuliko watanzania wengine ni wazo ambalo halikubaliki na halina mfano wake mahali popote duniani kati ya mataifa huru na yenye dola zake kamili.
    Raslimali ya gesi asilia ya Mtwara ni mali ya watanzania wote kama taifa moja na itatumika kwa manufaa ya watanzania wote pale inapohitajika zaidi na itakapotuletea faida kubwa zaidi sisi sote kama taifa moja lililojumuisha wanamtwara. Kama Dar es Salaam ndiko gesi asilia ya Mtwara inakohitajika zaidi kuliko Mtwara kwenyewe na kutumika kwake kwa ajili ya uzalishaji wa umeme mkoani Dar es Salaam kutatuletea faida kubwa zaidi sisi sote kama taifa moja kuliko kutumika kwake huko Mtwara kwenyewe kwa ajili ya uzalishaji wa mbolea na umeme, basi itabidi gesi asilia ya Mtwara itumike kwa ajili ya uzalishaji wa umeme Dar es Salaam. Vinginevyo gesi asilia ya Mtwara itabidi itumike huko huko Mtwara kwa ajili ya uzalishaji wa mbolea na umeme.
    Swala la Mtwara kufaidi au kutofaidi kutokana na ni wapi gesi asilia ya Mtwara itakapotumika halipo kwani mgawo wa pato lote la taifa linalojumuisha mapato yote yatokanayo na uvunaji wa gesi kote nchini hutawanywa kwa maeneo yote ya Tanzania kwa kuzingatia mahitaji halisi ya maeneo yote ya Tanzania na ni mgao upi kwa maeneo hayo utakaotuletea faida kubwa zaidi sisi sote kama taifa moja lililojumuisha wanamtwara. Kwa hiyo, cha kujiuliza ni kama gesi asila ya Mtwara inahitajika zaidi Dar es Salaam kuliko Mtwara na kama ikitumika Dar es Salaam kwa ajili ya uzalishaji wa umeme itatuletea sisi sote kama taifa moja faida kubwa zaidi kuliko ingetumika Mtwara kwenyewe kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na mbolea na kama Mtwara itakuwa mojawopo ya maeneo yanayostahili na yatakayotengewa pato kubwa zaidi la taifa ukilinganisha na maeneo mengine ya Nchi kwa ajili ya maendeleo yake pindi mradi wa gesi utakapoanza kufanya kazi na kuliingizia taifa faida.
    Pamoja na kwamba soko kubwa zaidi la gesi asilia hapa Tanzania kwa sasa hivi liko Dar es Salaam, kusafirisha gesi ya Mtwara kuja Dar es Salaam kwa ajili ya uzalishaji mkubwa wa umeme ni ubadhirifu mkubwa mno wa raslimali ya taifa kwani gesi asilia hiyo ikitumika kwa ajili ya uzalishaji mkubwa wa mbolea na umeme huko Mtwara (ambako ndiko kulikosahaulika zaidi ukilinganisha na maeneo mengine kwenye ujenzi wa miundo mbinu na miradi ya uzalishaji mali kwa ajili ya kuleta uwiano wa maendeleo ya kiuchumi kwa maeneo yote ya taifa letu) itatuletea ziada kubwa zaidi ya faida ya mabilioni ya dola za kimarekani kwa kipindi chote cha uhai wa mradi ukilinganisha na faida tarajiwa kutokana na matummizi ya gesi hiyo asilia ya Mtwara kwa ajili ya uzalishaji wa umeme mkoani Dar es Salaam.
    Kwa hiyo ukosoaji wa mradi huu wa kusafirisha gesi ya Mtwara kuja Dar es Salaam kwa ajili ya uzalishaji wa umeme unatakiwa ulenge kudai kwamba matumizi ya gesi asilia ya Mtwara yatakuwa na manufaa makubwa zaidi kwetu sisi sote kama taifa moja lililojumuisha wanamtwara iwapo yatakuwa ni kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na mboleo huko Mtwara badala ya kusafirishwa kwa bomba kwa ajili ya uzalishaji umeme mkoani Dar es Salaam. Ukosoaji huu pia ulenge kuishauri Serikali kuangalia umuhimu na uwezekano wa kupunguza kiasi cha gesi ya ziada kilichokuwa kimepangwa kisafirishwe kwa bomba kutoka Mtwara kuja Da es Salaam kwa ajili ya uzalishaji wa umeme ambao itabidi pia upunguzwe na kujenga miundo mbinu ya ziada itakayowezesha kuongezeka kwa kiasi cha gesi inayosafirishwa kwa sasa kutoka Songosongo kuja Dar es Salaam kwa ajili ya uzalishaji wa umeme hadi kiwango cha gesi asilia ya ziada kilichokuwakimepangwa kitoke Mtwara na kilichopunguzwa kwa sasa hivi. Matokeo yake ni kwamba raslimali ya gesi huko Songosongo itakwisha mapema zaidi lakini hii haitakuwa na madhara makubwa kwetu sisi sote kama taifa moja kwani hadi hapo itakapokuwa hivyo, raslimali mpya za gesi asilia inawezekana sana zitakuwa zimepatikana karibu zaidi na Dar es Salaam na huenda pia ujenzi wa miradi mipya mikubwa ya umeme nafuu zaidi wa maji huko Stiglers Gorge na kwingineko ikawa imekamilika na mahitaji ya umeme wa gesi ulio wa gharama kubwa zaidi kwenye uzalishaji yakawa yamepungua.

    Dr A. Massawe

    January 7, 2013 at 6:03 PM

  12. ZITTO:
    wananchi wa mtwara tumechoshwa na siasa za unyonyaji unaofanywa na cha tawala.
    tupo nyuma kimaendeleo kwa zaidi ya miaka 50.
    na jimbo la mtwara vijiji gesi ilikogunduliwa ni vijiji 6 tu vyenye umeme.jimbo hili limekaa gizani miaka 51 tokea uhuru upatikane.
    leo viongozi wakubwa wa serikali wamepotosha dhamira ya maandamano ya watu wa kusini.
    tumetukanwa,tumedhalilishwa,tumebaguliwa kwa kiasi kikubwa.ni radhi tufe wote tuiache gesi au tupate manufaa ya gesi kwanza.

    LULANJE

    January 10, 2013 at 3:38 PM

  13. Zitto,

    Wewe ni msomi hebu soma the normal practise ya sekta ya gesi duniani:

    http://pipeliner.com.au/pipeline_map_of_australia/

    http://en.m.wikipedia.org/wiki/List_of_natural_gas_pipelines

    Kwa kifupi daima gesi inapelekwa sokoni na wawekezaji hawajengi mabomba bila kuandika mikataba na wateja anzilishi. Je hapo Mtwara wapo?

    Fikiria kwanza.

    Maj

    Maj

    January 11, 2013 at 6:36 PM

  14. […] wa Gesi Asilia: Tuwasikilize Watanzania wa Mtwara na Lindi. Nikaandika tena: Tusipuuze mandamano dhidi ya Bomba la Gesi: Kilio cha Uwajibikaji; Nikaandika tena: Mtwara : Serikali inavunja nchi kwa kutosikiliza Wananchi; ni baadhi ya makala […]

  15. NAOMBA SERIKALI IJIPANGE UPYA JUU YA SWALA LA GES MTWARA.

    flowin ngonyani

    May 18, 2013 at 1:03 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: