Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

PRESS RELEASE: Shilingi Bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO, Gridi ya Taifa hatarini

with 36 comments

Shilingi bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO, Gridi ya Taifa hatarini

Gazeti la The East African la Novemba 24 – 30, 2012 limetoa taarifa kwamba jumla ya dola za kimarekani milioni 54 zimegundulika kuibwa na watumishi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la TANESCO kupitia manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mtambo wa Umeme wa IPTL. Gazeti hili limenukuu taarifa ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Tanzania (Controller and Auditor General). Taarifa hiyo inasema kuna kikundi (racket) ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia manunuzi ya Mafuta mazito ya IPTL.

Itakumbukwa kwamba toka mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo lililotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za ununuzi wa mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato mzima wa manunuzi ya mafuta haya ufanyiwe uchunguzi wa kina (forensic audit).

Katika mkutano wa 3 wa Bunge la Kumi (April 2011) niliuliza swali Bungeni kuhusu kashfa hii ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mtambo wa IPTL na baadaye tarehe 16 Aprili 2011 nilimwomba Spika airuhusu Kamati ya Nishati na Madini kufanya uchunguzi kuhusu kashfa hii. Kamati ya Nishati na Madini chini ya aliyekuwa Mwenyekiti ndugu January Makamba ililitaka Bunge kuazimia kufanyika kwa uchunguzi kuhusu suala hili kwenye Taarifa yake ya mwaka 2011 iliyowasilishwa Bungeni mwezi Aprili mwaka 2012. Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ndugu John Mnyika katika Hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2011 alipendekeza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kashfa hii pia. Juhudi zote hizo hazikuzaa matunda.

Kipindi hicho kiwango kilichokuwa kinahojiwa kuibwa ni shilingi bilioni 15 tu. Taarifa ya The East African kama walivyonukuu kutoka kwenye taarifa ya CAG inaonyesha fedha zilizoibwa ni shilingi bilioni 86.

Zabuni za kununua mafuta ya kuendesha umeme wa dharura zimekuwa zikitolewa bila kufuata utaratibu wa zabuni kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi. Hivi sasa kila mwezi Tanzania inatumia dola milioni 70 kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme. Fedha hizi zinatoka Hazina na sehemu ndogo kutoka TANESCO. Wakati fedha hizi bilioni 112 zinachomwa kila mwezi kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendesha mitambo ya umeme, Taarifa za kitaalamu zinaonyesha kwamba Bwawa la Mtera hivi lina kina cha maji chini ya kiwango kinachotakiwa na uzalishaji wa umeme ni asilimia 20 tu ya uwezo (installed capacity). Iwapo TANESCO wataendelea kutumia zaidi maji yaliyopo Mtera, Mitambo itashindwa kazi na Gridi nzima itasimama maana Mtera ndio nguzo kuu ya Gridi ya Taifa. Hali hii ni hatari sana kwa uchumi na ulinzi na usalama wa Taifa. Kimsingi Gridi ya Taifa ipo hatarini kutokana na kiwango cha Maji kilichopo Mtera hivi sasa na kuendelea kupungua kwa kina hicho cha maji.

Wananchi wanapaswa kuelezwa kinaga ubaga nini kinaendelea katika sekta ndogo ya umeme hapa nchini;

1.      Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kuhusu zabuni za manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura iwekwe wazi na ‘racket’ inayosemekana kuiba jumla ya shilingi bilioni 86 ionyeshwe na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na bila kuchelewa.

2.      Waziri wa Nishati na Maadini auleze umma hali yalisi ya sekta ya umeme nchini, uzalishaji wa umeme upoje, hali ya maji katika bwawa mkakati la Mtera na nini hatma ya mitambo ya IPTL, kesi zake na utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii zimalizwe nje ya mahakama. Pia Taifa lielezwe Mpango wa Dharura wa umeme unakwisha lini maana muda uliotolewa na Bunge mwezi Agosti mwaka 2011 tayari umekamilika. Waziri aeleze hatua agni amechukua baada ya kukabidhiwa taarifa na CAG kuhusu maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi wa shilingi bilioni 86 za kununua mafuta ya IPTL.

3.      Waziri wa Fedha na Uchumi aueleze umma ni kiwango gani cha fedha Hazina imetoa kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Mwezi Novemba mwaka 2011 na Oktoba mwaka 2012 na kama taratibu zote za zabuni zilifuatwa na pale ambapo hazikufuatwa ni hatua gani PPRA wamechukua dhidi ya waliokiuka sheria ya manunuzi na kuleta hasara ya mabilioni ya fedha kwa Serikali.

 

Kabwe Zuberi Zitto, Mb

Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha

Dar es Salaam. Novemba 25, 2012

36 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Aisee hii ni Serikali inayolea mafisadi. Public sector productivity is so low, their policy making is ineffective, they are negligent in enforcing and executing directives and regulations but they are extremely efficient in embezzling public funds.

  Stephen Seyayi

  November 25, 2012 at 4:38 PM

 2. Watanzania pamoja na matatizo waliyo nayo watumishi wa umma hawaöni haya kupora mabilioni ambayo yangesaidia katika kuboresha miundo mbinu ya umeme nchini hata maeneo yasiyo na umeme hasa mjini ambapo network ya umeme haipo na hivyo kusababisha maendeleo kuwa duni ilhali mtu mmoja anafilisi nchi, Naomba wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo na kufirisiwa mali walizo nazo ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia chafu kama hizo!!

  Raymond R.Choma

  November 25, 2012 at 4:57 PM

 3. Ufisadi umekomaa kwenye hii serikali dhaifu

  Mathias Lyamunda

  November 25, 2012 at 5:04 PM

 4. Hiyo nayo kali. Mh zitto kaza buti mpaka kieleweke.

  Katambi james

  November 25, 2012 at 5:08 PM

 5. serikali ya ccm imetengenezwa na mafisadi waliokubuhu 2wapige chini faster

  BRUNO KIMS

  November 25, 2012 at 5:12 PM

 6. Jamani hiv hawa jamaa mbona hawatuonei huruma?Do they think that,we are unable to overthrough the existing GOVERNMENT?

  Ally Amiri

  November 25, 2012 at 5:57 PM

 7. Kaka hili ni balaa..Lakini ulitahadharisha kwenye matamko yako mbali mbali…go Zitto,go Zitto…

  kijana wa Manyovu

  November 25, 2012 at 6:18 PM

 8. Tanzania inakeraaa acha tu 😦 kaeni na li nchi lenu harudi mtu huko,pumbaav

  King

  November 25, 2012 at 6:42 PM

 9. Kaka komaa mwisho wao wakuiba maliza zaumma unakaribia, sasahivi wanalindana kwa sababu hakuna aliye msafi katiyao,wakumkemea mwenzake. Endelea kufichua uozo msimamie hatua za kisheria zichukuliwe zidi yao.

  Evarist kimaro

  November 25, 2012 at 6:47 PM

 10. Kaka kama huo ni ukweli ww waumbue hao wahujumu uchumi ni hayo tu

  Innocent minja

  November 25, 2012 at 6:57 PM

 11. Ni hatari taifa lenye nusu karne sasa kuendelea kuishi kwa mpango wa umeme wa dharura!
  Ni wazi hakuna jitihada za makusudi kwa upande wa serikali kuondokana na tatizo hili kwani limegeuzwa mradi wa “wakubwa”
  Tanzania tuamke…

  Lugiko Lugiko

  November 26, 2012 at 12:01 AM

  • sio siri kabwe wewe ni jembe,kwa msimamo huu hata uraisi unaweza

   Mandago

   December 9, 2012 at 12:46 PM

 12. Ununuzi wa umma umegeuzwa sehemu ambayo ufisadi wa kitaasisi, ufisadi wa kimfumo na wa ndani ya mfumo unaliingiza taifa kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Ujambazi wa kiserikali wa IPTL na yatokanayo na IPTL ni kielelezo tosha cha mfumo wa uongozi wa wizara na TANESCO kushinda kwenye usimamizi na menejimenti ya fedha za umma. Tanzania imekuwa “shamba la bibi” na watu wasiokuwa waadilifu wanafisidi mali ya umma!

  Bakari M. Mohamed

  November 26, 2012 at 6:10 AM

 13. Wanaoiba waibe saana ila siku itafika ambayo watazirudisha kwa RIBA na kifungo juu..

  George john

  November 26, 2012 at 9:29 AM

 14. Upotevu huu wa fedha za wananchi ni huruma sana kwa kweli ila tangu maneno kuanza kusemwa na hata baadhi ya wabunge wa kambi za upinzani walishawahi kujumuishwa kwenye ukaguzi wa baadhi ya tuhuma zilizowahi kutolewa na wao wenyewe wapinzani siku za mbele, cha kushangaza hoja imeletwa nao mwenyewe akawekwa kwenye kamati ya uchunguzi cha ajabu jamani hatujaletewa mwizi wetu na mpaka leo sijaona tume iliyomuwajibisha mtu kurudisha pesa za wananchi zilizodaiwa kuibwa au kutoroshwa nje ya nchi , hizi niulize tu jamani ina maana mwanachi wa kawaida hana uwezo wa kumshitaki mbunge au waziri ambaye amekutwa na tuhuma na kama ushaidi upo? siasa jamani ni game ngumu sana kuilewa hizi unashindwaje kuleta mwizi ambaye tuhuma zake ni wewe mwenyewe umezileta?

  Bally

  November 26, 2012 at 2:12 PM

 15. HAPO SASA.HII NCHI INATIA KICHEFUCHEFU.NA KWA BAHATI MBAYA HAKUNA ANAYEJALI! INASIKITISHA NA INAUMA.SI RAISI SI WAZIRI MKUU NA KINACHOSHANGAZA NI UKIMYA WAO KAMA VIONGOZI WAKUU.WAKIBANWA WANASEMA LETE USHAIDI WAKATI SERIKALI INA VYOMBO LUKUKI JE WANAFANYA KAZI GANI AU NI KUCHOTA NA KUPELEKA UGHAIBUNI!

  Charles Tongora

  November 26, 2012 at 5:55 PM

 16. nchi hii imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi sana ila wachache wenye uchu wa utajiri ndio wanaofaidi zaidi kuliko watanzania wa hali ya chini mhe zitto pambana cc tuko na wewe,na mwishowao ni karibu,manake kila mtz sasa wanajua kila kitu,keep it up zitto

  fred msakyi

  November 26, 2012 at 10:07 PM

 17. usiwape nafasi mafisadi kupumua wabane hasa

  Daudi Masayi

  November 27, 2012 at 7:58 AM

 18. Habari za ufisadi zinachosha kuzisikia kila siku. Je hakuna mamlaka inayoshugulikia tuhuma hizi? Tunahitaji kuona ufuatiliaji wa mambo hayo vinginevyo ufisadi ni wimbo uliozoeleka hauna maana kwetu.

  George Mkumbe (@georgemkumbe)

  November 27, 2012 at 1:00 PM

 19. I dont think hii secretariet mpya ya Chama Cha Mafisadi itatusaidia chochote, ni vizuri watanzania waamuke sasa na kufanya mapinduzi ya kuwapiga chini hawa jamaa, hii nchi watu hawako serious mpaka inaboa. wizara ya Nishati na Madini ndio shamba la bibi kila anayekuja anapiga mawe anatambaa, Sijui tufanyeje na hii serikali yetu? Mi am tired aisee………………..

  Eng. Leonard Mwambene

  November 27, 2012 at 1:52 PM

 20. you know what,even the time Baba wa taifa,Nelson mandela and other real revolutioneers when they were tried to overthrow those colonial government they were young men at the age of 20yrs and 39yrs ,they were not older so i want to advice my brothers and sisters these old people they must stop think that we dont understand their stupid game of stealing governments resources and cover each from the law and reason why they said during their young they suffered alot no shoes, no electricity,no infrastructures at all so they think that they made great development to compare with their life in past.So what in their poor mind is they are time to handle great positions,favour each other in the best post,exproit resources,miss use government properties just because they are older and their close die ,nothing they will understand for them rather we get in civil war than leave position, they even forget the moment they took power from colonial power they were young too now they we young we dont understand why,african leaders,why lord,pray for these ignorants change their stacked mind lord for the peace and development of africa,why whites people they are not selfish are cursed ohh lord change the mind of these old people who couldn’t sacrifice for the benefits of younger ones,they say politics mean old people talk young ones fighty,is that true lord if is true thank you because one day they will get what they want,we are not cowards,Aluta continua young men and women’s.AMEN OR AMINA

  Ilunga Kasongo

  November 27, 2012 at 7:18 PM

 21. Hii inatupa picha halisi ya kwanini vitisho vinaongezeka kila kukicha. Mara kama huna uthibitisho utatukoma, yaani mtoa taarifa badala ya kupongezwa na vyombo vya dola vinavyodai kusimamia maslahi ta taifa, vinamtishia mtu anayerahisisha shughuli zao. Natambua ideological hegemony ndo kitu kunachoendelea na pengine kuwafanya watu waelewa wawe na ahsira hata ya kuishi kwa kuona haya mambo yakiendelea ila naamini KUTAMBUA TATIZO NI NJIA YA KUANZA KULIKABILIBILI. Hakuna uchanga wowote kwenye taifa lenye umri zaidi ya nusu karne. Tutachukua hatua mda si mreeefu kama hawataki kujiwajibisha.
  Hii dhana ya watawala (wanasiasa na watendaji) kujifanya viongozi ni uizi mtupu. watu wanongoza matumbo yao na nyumba ndogo zao na si watu waliowapa zamana. Usiombe wananchi wakatambua BILA kuambiwa kuwa wao ndo wanawapa hayo madaraka ya kuwa mtendaji au kiongozi wa kisiasa, patachimbika.

  Maty.

  November 28, 2012 at 9:02 AM

 22. TUMECHOKA KUJADILIANA KUHUSU UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA! NA MIJADALA KATIKA MITANDAO KUHUSU WATU WANAOTUHUMIWA IMEANZA KITAMBO PIA, CHA KUSHANGAZA NI LINAISHA SAKATA HILI (kijuu juu) NA LINAANZISHWA LINGINE, SASA VIPORO TUMEMUACHIA NANI? NA KWA KWELI NASHINDWA KUELEWA KUWA YUPI WA KUMUAMINI, NASEMA HIVYO SABABU KUNA ANAYEKEMEA UFISADI SABABU HAJAPATA NAFASI NA LABDA KAMA ANGEIPATA ANGEFISADI KULIKO YULE ANAYEMTUHUMU, NA SIMAANISHI KUWA HATUPASWI KUIBUA MACHAFU TUNAYOYAONA BALI ONYESHA UZALENDO UNAPOAMINIWA KUCHUNGUZA SHUTMA DHIDI YA ALIYESHUTUMIWA. KWA KIFUPI NAPENDA KUHITIMISHA KWAMBA WAPO WATU WENYE UZALENDO KAMA ALIOKUWA NAO BABA WA TAIFA ILA HAWAJAPATA NAFASI KAMA ALIOKUWA NAYO MWALIMU, WATANZANIA TUFUNGUKE NA TUJIWAJIBISHE SOTE KWA KUTUMIA HAKI YAKO YA KUPIGA KURA KUWACHAGUA VIONGOZI BORA NA SI BORA VIONGOZI (wezi wa hizo bil 86 wawajibishwe)

  KIMOSO

  November 28, 2012 at 9:08 AM

 23. Mh! Inatisha. Tufanye nini kieleweke? Hivi hatua gani zichukuliwe pesa hizo zirejeshwe?

  Jamal

  November 28, 2012 at 7:30 PM

 24. Hivi jamani lini serikali ya CCM,itaheshimu jasho la Watanzania walalahoi.?

  Pavu Juma

  November 28, 2012 at 10:37 PM

 25. NAJIULIZA NI LINI TUTAACHA KUSIKIA MANENO YA WIZI WIZI KILA KUKICHA, TAIFA LIMEANGAMIA..

 26. Kaka, Mkuu wa nchi hivi haya mambo wewe huwa unayachukuliaje? Yanakuuma? mbona majanga makubwa kama haya huwa sikusikii kabisa, kaka kuwa unafunguka sometimes

  Emmer

  November 29, 2012 at 9:46 AM

 27. da!kweli watanzania tunaishi kwa neema tu ya Mungu.ama sivyo tungeshamalizwa kitambo na mafisadi.

  gil guy

  November 29, 2012 at 12:09 PM

 28. Hii ndiyo Tanzania bana!

  Samuel Mulumba

  November 29, 2012 at 12:23 PM

 29. hawa viongozi badala ya kufuatilia mambo ya msingi wanakaa kuwaza uchaguzi mwaka 2015 nani atakuwa rais. kama nchi imewashinda sas hivi mnafkiri kuna atakayeweza kuwa rais kati yao…..

  Patrick Simon

  November 29, 2012 at 12:41 PM

 30. Wananchi wapenda amani na maendeleo, hali hii haiwezi kwisha mpaka yawepo mabadiriko ya utawala huu ulioko madarakani na tusitegemee kuwa kuna kiongozi ndani ya serikali hii ataweza kufichua ufisadi huu mkubwa maana wakubwa wapo nyuma yao. Kelele zitapigwa na hakuna atakaye thubutu kufunua uchafu huu. iliyopo ni kufunguka watanzania wote tukabadili utawala huu vinginevyo watatukaanga na pesa zatu za walipa kodi walalahoi
  Hizi taarifa zisiishie mitandaoni tu zifike kila mahali nchi nzima watanzania waelewe kinachofanyika katika nchi yao.
  Asante Zitto Kabwe. Hakuna kulala mpaka kieleweke.

  P M Leonard

  November 29, 2012 at 12:53 PM

 31. Tatizo la nchi hii ipo kisiasa zaidi ndio maana wezi wamekua wengi,na wanalindana wakati masikimi tunakufa na njaa wahadizabe hawajui kama kuna mashine za kusaga hapa Tanzania na wengine wanakura mabilioni ya mapesa.hivi ni kwa nini?,mbele ya mungu mtajibu nini?,siku nchi hii ikiongozwa kisayansi itakua ya maana sana maana mwana sayansi anafanya uchunguzi sio maneno tu nchi zote zilizo weka sayansi kipaumbele hazina mafisadi ,Siasa ya Tanzania ni biashara sio democrasia ndio maana vijana wengi sas hivi wanakimbikia kwenye siasa,madactari wanaacha kazi yao wanakimbilia siasa hivi kweli tutafika,mimi hua natamani makatibu wakuu wote wa wizara zote wawe na huruma wajue kua kuna watu hapa Tanzania wanalala bila kura wanakura tu matunda ya porini,na pia wajue siku moja watakufa na hizo pesa hawazikwi nazo wataziacha hapa duniani kwahiyo nawaomba tu wajitahidi kila mtanzania apate haki yake.

  Mwita John

  November 30, 2012 at 12:59 AM

 32. Wakati wananchi wanapata shida kwa kukosa haduma za msingi,wengine wanachota fedha, TAKUKURU WAKO WAPI?,TISS, ok, Hv gharama halis ya hiyo mitambo ni Tshs ngap,kwanin serikali isitaifishe au kununua mipya ili kuondoa tatizo la wizi?

  James

  November 30, 2012 at 11:14 AM

 33. Hali ya umeme nchini kwa stahili hiyo ni tete nakumbuka waziri wa nishati aliwahi kutamka bungeni kua hakuta kua tena na mgawo wa umeme tukafarijika hata hivyo hilo halikutekelezwa. Hivi huu wizi utaisha lini? Hivi kwa nini watanzania wanakua na roho ya ulafi kiasi hicho? Hivi kizazi kinachokuja kitakuaje nadhani watagawana kila kitu ambacho ni mali ya tafaifa. Tumwamini nani sasa coz serikali ndio hiyo iko hoi bin taaban, ukija bungeni nako hakuna jibya kila mtu anavutia kweka mahakama nayo inaangalia upepo

  Karosi Mmari

  December 4, 2012 at 5:34 PM

 34. We people of tanzania we should alway thnk bfr doing any thng supid i gv a big hand to hon.Zito kabwe all leader should be like him and act like him

  Babbu

  December 29, 2012 at 8:19 PM

 35. hv hawa watu viatu why Tanzania everyday?no longer at easy .and this is a product of chama cha mapinduzi their end is coming soon.we will be together in 2015.END OF ALL MAFISADI PUMBAVU.

  ABDALAH MASUDI

  November 27, 2014 at 12:15 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: