Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Mabilioni ya Uswisi – Tusigeuzwe Mazezeta

with 32 comments

Mabilioni ya Uswisi – Tusigeuzwe Mazezeta

Jumanne tarehe 20 Novemba 2012, baadhi ya vyombo vya habari vimebeba habari zinazohusu matamshi ya Waziri wa Utawala Bora ndugu George Mkuchika kuhusu sakata ya mabilioni ya Uswisi. Waziri amesema kwamba Serikali ya Uswisi inataka majina ya Watanzania walioficha fedha huko ndio waweze kusaidia uchunguzi. Habari kama Hiyo, yenye maudhui na malengo hayo hayo iliandikwa na Gazeti la The Guardian on Sunday la tarehe 18 Novemba 2012.

Nimeona ni vema nitoe kauli yangu rasmi kuhusu suala hili. Lengo ni kuweka rekodi sawa juu ya Azimio la Bunge na kwamba Serikali inapaswa kutekeleza Azimio na sio kutoa kauli tata za kukata tamaa.

Moja, Suala hili japo sio jipya lakini limeandikwa kama ni jambo jipya. Suala la Serikali ya Uswisi kutaka majina lilisemwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati akichangia hoja binafsi niliyowasilisha Bungeni na pia wakati akileta maombi yake ya kuiondoa hoja ambayo yalikataliwa na Bunge. Kama sio sababu mpya ni kwanini imeibuka upya na kwa kasi? Ni wazi Serikali inajihami kwa kuona kuwa itashindwa kutekeleza azimio la Bunge. Watanzania wasikubali propaganda hii ya Serikali. Bunge limeagiza Serikali kufanya uchunguzi kwa kutumia njia za kiserikali au wachunguzi binafsi wa kimataifa. Kwa nini Serikali inaanza kubwabwaja ilhali wala haijaanza kazi hiyo? Serikali inajaribu kuficha nini? Kwa nini baada ya wiki iliyopita Benki Kuu kufanya uchunguzi kwenye Mabenki ya Biashara jijini Dar es Salaam na namna fedha zimekuwa zikipelekwa nje (international transfers), leo Serikali inakuja na kauli za kukakata tamaa? Kunani?

Pili, Watanzania wajue kwamba Taifa la Swiss limejengwa na linajengwa kwa fedha hizi za wizi ambazo watu mbalimbali duniani wanaiba au kukwepa kodi kwenye nchi zao na kuzificha huko. Serikali ya Swiss hata siku moja haiwezi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika suala kama hili. Ndio maana Azimio la Bunge linataka wachunguzi binafsi ambao hawatahitaji ushirikiano wa Serikali ya Swiss. Nawakumbusha kwamba mwaka 1997 mara baada ya Joseph Desire Mobutu kuangushwa na Rais Joseph Kabila kule Kongo – Kinshasa, Serikali ya Swiss iliitaka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuonyesha ushahidi kuwa hela hizo za Mobutu zilikuwa zimepatikana kwa njia haramu! Waswiss walitaka Kabila awakakikishie kuwa fedha zile zaidi ya dola bilioni nane za Kimarekani Mobutu hakuzipata kihalali ndio waweze kuzirejesha. Zaire ilikadiriwa kuwa na zaidi ya dola za Kimarekani bilioni thelathini katika Mabenki ya nje ya nchi hiyo. Majibu ya aina aina hii ni majibu ‘standard’ ambayo kila nchi inapewa. Hata Marekani ilipokuwa inafuatilia wakwepa kodi wao walijibiwa hivi hivi. Hatimaye Serikali ya Marekani ikaamua kununua taarifa hizo na kuwakamata wakwepaji kodi wao walioficha fedha Uswisi. Hao ndio Waswiss ambao Serikali ya Tanzania inashabikia majibu yao. Bila Aibu Mawaziri wetu wanayanukuu majibu ya Waswiss kama kasuku. Tunasahau historia haraka sana. Tunakuwa kama mazezeta.

Tusiwe Taifa la mazezeta. Mabwege na mazezeta huimba kila wanachoambiwa kuimba. Sasa Serikali ya Tanzania imekuwa msemaji wa Serikali ya Swiss badala ya kuchunguza utoroshaji wa fedha haramu na kisha kutoa taarifa Bungeni. Naitaka Serikali ianze uchunguzi mara moja kama namna ilivyoelekezwa na Bunge. Suala hili sio suala la kisiasa, sasa ni Azimio la Bunge ambalo linahitaji kutekelezwa kikamilifu. Suala hili sio suala la Zitto Kabwe tena, ni suala la Bunge, ni suala la Wananchi. Wananchi hawataki uzezeta wa watu waliopewa dhamana ya kutekeleza Azimio lao. Kama hawawezi wapishe watu wenye uwezo wa kusimamia maslahi ya Watanzania kwa kuchukua hatua stahili za kuchunguza utoroshaji mkubwa wa fedha za kigeni, ukwepaji mkubwa wa kodi na ufisadi uliopelekea Watanzania kuficha mabilioni kwenye mabenki nje ya Tanzania. Hatutakaa kimya mpaka tuone mwisho kamilifu wa suala hili. Utekelezaji wa Azimio la Bunge itakuwa ni salamu tosha mafisadi na watoroshaji wa fedha haramu kwamba hawana pa kujificha na Tanzania sio Taifa la kuchezeachezea. Lazima tushinde vita hii. Anayeona hawezi kutuongoza kuishinda atupishe mapema. Hatupaswi kuwa Taifa la Mazezeta. Watanzania sio mabwege tena, Mwakyembe alipata kusema.

 

Kabwe Zuberi Zitto, Mb

Kigoma Kaskazini.

Written by zittokabwe

November 20, 2012 at 6:13 PM

32 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Mheshimiwa Kabwe, hongera sana kwa ujasiri wako katika kupeleka swala hili mbele. Tunakuunga mkono na kukuombea kwa Mwenyezi Mungu. Swali la msingi ni: je, majina ya wahusika yako wapi? Kwa nini hawatajwi?

  James Mlali

  November 20, 2012 at 6:33 PM

  • Katika Waraka huu nimeng’amua uchungu wa kweli uliopo kwa mwandishi, lakini nachelea kusema hawa ndugu zetu watachukulia kauli hii kama kelele za mlango na kamwe hazimnyimi mwenye nyumba kulala. Taifa letu ni meli ambayo imeanza kujaa maji na wasafiri na manahodha wote wameliwa na mtoto mchanga analia wakati mama mtu yupo anaumba mtoto mwingine chumba cha pili (kumradhi) hakika dharau hiihuleta mauti makubwa sana.

   Nelson Mmari

   November 20, 2012 at 6:52 PM

   • kabwe wewe ni jembe kweli ,mpaka umekuwa na ujasiri wa kutaja mabilioni yaliyoko uswiswi,Isalute on you and I respect yuou in politics

    mandago from Saut Mwanza

    December 4, 2012 at 4:03 PM

  • Hii documentary by Aljazeera inaonyesha jinsi wanavyoufanya huu mchezo —-> http://www.aljazeera.com/programmes/peopleandpower/2012/11/201211714649852604.html

   gwamakatm

   November 20, 2012 at 6:57 PM

  • mheshimiwa zito mimi binafsi nakukubali sana lakini bado kuna utata hapa wa jambo hili kama kweli majina unayo kwani kuna ugumu gani kuyasoma ili watanzania wawajue wezi wa fedha zao ili wasibaki katika wimbi la mawazo?toa ukweli muheshimiwa ili uwaondoe watanzania katika mtihani huu

   peter mwakajumba

   November 20, 2012 at 6:58 PM

   • Cha msingi hapa ni fedha kurudishwa. unajua suala la majina linaweza kuleta kasoro ndogondogo ambazo zitatumiwa na watu waovu kujenga propaganda. Je! una habari hao watu wanaweza wakawa wametumia majina ambayo sio yao mf. marafiki n.k. Mh. zito ni mtu Makini sana inahitaji umakini mkubwakuhoji umakini wake.

    Gibson E.

    November 21, 2012 at 9:48 AM

   • Hivi una maana hujui CCM ndiyo mwasisi wa huu Wizi? Ukizungumzia CCM unazungumzia JK and family, Lowasa and Familyt Chenge and family, the Balalis, the Rostams, the Megjis. Wasomali na matajiri wafadhili wa CCM orodha yote ni CCM

    Msafiri

    November 30, 2012 at 11:58 AM

 2. tupo pamoja mkuu,
  but ila unanishangaza why unaendelea kuwa na urafiki mkubwa na kiongozi mkuu wa nchi,ambae kwa mamlaka aliyonayo walau angelisemea jambo hili

  aziz bakari

  November 20, 2012 at 6:49 PM

  • Peter Mwakajumba, wewe ukishajua majina ya watu waliotorosha fedha, utachukua hatua gani?

   Stephen Seyayi

   November 20, 2012 at 7:06 PM

 3. Big up Zitto. Tunakuunga mkono Mh. wetu. Watanzania sio mazezeta,sio mabwege na tumechoshwa na usanii wa serikali hii iliyoko madarakani. Ambao hawawezi basi waondoke maana wako vijana wenye uwezo wa kulinda maslahi ya Taifa. Mungu akulinde na kukuongezea ujasiri wa kupambana mafisadi.

  Erasto

  November 20, 2012 at 7:02 PM

 4. Kwakweli kitendo cha Makinda kutokubaliana na mapendekezo yako ya kuunda kamati huru ya kufuatilia haya mabilioni hapo ndipo hoja yako ama watanzania tulipigwa chanagalamacho. Haingiii akilini kabisa kwamba Maazimio ya bunge kupitia makinda kwamba yatafanyiwa kazi.Yaani waliohusika kwenye hayo mabilioni wako kwenye serikali na viongozi kwenye serikali hivi itaiingia akili wajichunguze??? Hapo ni sawa na ile sentensi isemayo NANI ATAMFUNGA PAKA KENGELE?? hivyo kwakweli tusitegemee jipya kufanywa na Serikali hii.Mapendekezo yako ya kuunda kamati yangepitishwa hakika wangebainika tu.Kilichobaki hapa serikali hii kupitia waziri wa fedha ama G.Mkuchika mwenyewe watabaki watatekeleza hoja ya Mwanasheria mkuu aliyekuwa anaua hoja yako.Mwisho hatua ya mwisho andaa orodha yako na kiasi kilichokwapuliwa ikiwezekana hata akaunti zao zilizotumika tuwapeleke kwenye mahakama ya umma Nyumba kwa nyumba tunawambia wananchi mjini na Vijijini nchi nzima.Na hii itawezekana kupitia M4C yaani hakuna lingine.Tusitegemee Serikali itawaumbua hata siku moja.M4C itawaumbua na kuwaanika wazi tukipita Nyumba kwa nyumba,mtaa kwa mtaa,na kijiji kwa kijiji nchi nzima.Mungu ibariki CDM.na Mungu ibariki Tanzania.

  Abel Dendwa

  November 20, 2012 at 7:28 PM

 5. Ndugu Zitto wewe ni JEMBE na jembe lenyewe mpini chuma!! Nakupongeza sn kwa UJASIRI unaouonyesha mbele ya watanzania waliokupa DHAMANA ya uwakilishi bungeni! Mh.Mkuchika hana jipya na ni AIBU kwake kubwabwaja kiasi hicho na inaonyesha ni jinsi gani anajaribu KULIPA FADHILA za kunusurika na PANGA la kujiuzulu wakati mawaziri wenzie walipojiuzulu kwani yeye alikuwa waziri wa TAMISEMI wizara ambayo iliboronga na wizi mkubwa wa UFISADI ktk halmashauri mbalimbali nchini kulingana na ukaguzi wa CAG.Tulishangaa sana kunani kati yake na rais kwa kuachwa na kupewa wizara nyingine na leo anaanza KUBWABWAJA TENA! Ndugu Zitto tuko nyuma yako na hata wakikumaliza wataibuka akina Zitto wengi!! Kwn mfano tunao,wako wapi akina Sokoine? Uliona wapi msafara wa kiongozi km waziri mkuu ambao mbele kuna mapikipiki na magari ya trafics lakini inatokea gari mbele inagongana na gari ya waziri mkuu! Mpaka leo watanzania tunaona kifo kile ni kiini macho! Wako wapi akina Stan Katabalo? Kolimba? Leo wameibuka wengi zaidi ya hao! Keep on brother.Mwisho wa safari si mbali.

  MICHAEL JULIUS MACOKO

  November 20, 2012 at 8:09 PM

 6. kimsingi hatuwezi kuwaachia viongozi nchi wanene wanayoyataka ni lazima kuchukua hatua sie wenyewe mimi kila ninapo pata furusa ya kusema huwa sisiti kuzungumza kuwa Ufisadi katika nchi hii ni mfumo ambao kimsingi ili kuutokomeza ni lazima kufanya mabadiliko makubwa ya Uongozi ,kwa mfano Mkuchika anaweza kusaidia nn katika taifa hili wakati akiwa Tamisemi alishindwa hata kuzuia mishahara hewa na halimashauri zimekuwa na wizi wa kupindukia yy akiwapo haoni wala kusikia nani kamtuma kuwa tetea mafisadi mie naamini 2015 sio mbali wataondoka tu na kubebana kwao .

  mrimi zablon

  November 20, 2012 at 9:28 PM

 7. Tusikatishwe tamaa kupigania haki zetu watanzania na hao kina mkuchika. Yote haya yana mwisho. As we know we shall, as we are confident in the victory of good over evil… Aluta continua.

  Anderson

  November 20, 2012 at 11:03 PM

 8. tumshukuru mungu kwa kngia kuleta dunian wewe zitto,,umetufumbua mengi tangu ulipo ingia bungeni ukiwa kijana mdogo,wanzania wanatambua kazi unayoifanya kitaifa sio faida ya jimboni kwako au kwa mkoa wa kgm tu,tambua wewe ni dhahabu iliyotoka kgm.Usikate tamaa watanzania wapo pamoja nawe

  diwani mtarajiwa 2015

  November 20, 2012 at 11:19 PM

 9. Ni dhaili kabisa selikali inataka kuwalinda watu hawa. Na inadhiilisha inausika au ina Maslai binafsi na watu hao. Kwanza Raisi mwenyewe yuko kimya, hata kutoa kauli yoyote hakuna. Safari hii hatukubali, tumechoka kufanywa wajinga na tumechoka kuongea. Hapa Selikali inachezea koki, na italoa,

  Augustine Alexander

  November 21, 2012 at 5:40 AM

 10. Binafsi sina la kuongea kwa kazi unayo fanya nataman wote wangekuwa hvyo basi taifa letu lingepiga hatua co muda wote wawakilish wetu wanawaza kuiba iba tu.Mbunge kaz iliyompeleka bungeni hatekelez badala yake anataka kuiba tu.Ubarikiwe sana kaka na uendlee hvyo hivyo

  Joshua hongoli

  November 21, 2012 at 6:39 AM

 11. Zito tushanini kifanyike ,maana hatuelwi hata tuanzie wapi,kama mazezeta tushakuwa

  chris mushendwa

  November 21, 2012 at 11:03 AM

 12. muda umefika wa serikali kutafakali na kujipima kwa watanzania kama inafaa kuwa madalakani au itoke maana kama zitto aliweza kupata taarifa hizo serikali inayojiita sikivu iliziba masikio

  mwitatoye

  November 21, 2012 at 11:40 AM

 13. Huyu Mkuchika tunawasiwasi nae.
  (1) Nimuhusika
  (2) Si msomi mzuri
  Sababu ninazo ambazo ni hizi.
  Ninamuomba arejee hutuba ya hoja binafsi ya Muheshimiwa Zitto ukurasa wa 13, juu ya mapendekezo aliyoyato ya nani wafanyiwe uchunguzi, ninaomba ninukuu:-
  Mheshimiwa aliomba uchunguzi wa kina ufanyike wa mali za awtanzania wote waliowahi kushika nyadhifa zifuatazo:-
  (1)Waziri mkuu tz kati ya 2003-2010.
  (2)Waziri wa nishati na madini 2003-2010
  (3)Waziri wa ulinzi 2003-2010.
  (4)Mkuu wa majeshi 2003-2010.
  (5)Katibu mkuu nishati/madini 2003-2010.
  (6)Mwanasheria mkuu 2003-2010
  (7)Kamishna wa nishati 2003-2010.
  (8)Mkurugenzi mkuu TPDC 2003-2010 na
  (9)M/kiti na wajumbe wa bodi ya TPDC.
  Jamani hayo si majina ya watu? kwani hawajulikani. Huyo mganga wa kienyeji tunae mtafuta atupe majina wanini wakati majina yapo wazi? Hatasisi walalahoi tunaona pa kuanzia na twaweza kujaribu.
  Serikali isituchanganye sasa watanzania wengi wanaelewa.

  baraka gilagiza

  November 21, 2012 at 5:49 PM

 14. kila jambo lina mwanzo na mwisho wake, serikari haitaweza kamwe kukwepa juu ya mambo haya, ni lazima iwajibike yenyewe na kama haitaki sisi wananchi tutaiwajibisha maana tunaweza.tunaitaka serikari isikwepe katika hili,hizi pesa za watanzania wote ni lazima watanzania wote wanufaike nazo.

  Longino Masanja.

  November 21, 2012 at 7:20 PM

 15. mh wewe tutajie hao walioficha!

  winston

  November 22, 2012 at 1:52 PM

 16. Si walishazoea tulipokuwa mazezeta kutupelekesha wanavyotaka lakini sasa wajue wale Watanzania wajinga wa miaka hiyo sasa tumeelevuka na usiombe mjinga akielevuka ni balaa na ndiomana kila wanapokwenda na wanachoifanya vyote vyamoto. La msingi mheshimiwa Zito kama kawaida kaza mkanda wa Gwanda tusonge mbele.

  irnenensemwa

  November 22, 2012 at 4:16 PM

 17. Kwa nini watanzania mnalazimisha Mheshimiwa Zitto ataje majina? Nini kazi ya vyombo mbalimbali vya uchunguzi vilivyopo ndani ya nchi hii? Hili swala limejadiliwa na wabunge wengi kwa uchungu mkubwa tena wa vyama vyote,hii inadhihirisha wanajua hili jambo lipo na wahusika wanafahamika isipokuwa wanaotakiwa kuhakiki na kutuambia wananchi ni vyombo husika sio mtirirko wa kihayawani kila mtu aseme kila kitu,Watanzania tuamini hilo kwa huu mfano mdogo tuu uliopo…..Jamaa mmoja aliulizwa kuhusu mabilioni aliyoficha nje ya nchi hakukana ila aliviita vijisenti sasa hadi hapo kuna wasiwasi gani? Ila namsapoti mheshimiwa kuviacha vyombo husika kufanya uchunguzi na kuja na majibu sahihi kwa sababu kama watatutania hapo utakuwa ni wakati muafaka wa mh kuweka mambo hadharani.

  Reginald petro

  November 22, 2012 at 7:00 PM

 18. Mbunge wangu wa ukweri, please ,nakuomba uwataje ili sisi watanzania wapiga kula ,sisi ambao tumeibiwa ili tuchukue hatua ,tena kwa hasila sana sana. basi walivyo wahuni hawaoni hata aibu ,maana hata wabunge wengne wa ccm wenye akili tayali walishanza kuwaponda .NA HATUWAACHI MAANA UCHAGUZI UJAO NILAZIMA TUWAPIGE CHINI ,.CHADEMA TUTAWAWEKA IKULU CHAKWANZA KAMATENI WOTE WAWEKENI GEREZANI NA KUFLISI MALI WALIZONAZO ZOTE..mwananchi wako KIGOMA NIKOPAMAJA NAWE KTK MAENDEREO YA MKOWA NA TAIFA KWA UJUMLA .

  sixto modesit

  November 22, 2012 at 7:31 PM

 19. CCM TUMEWACHOKA heeh! CHADEMA under Kamanda ZITTO wabaneni mpaka wajikunyie

  nelson marwa

  November 23, 2012 at 10:31 AM

 20. majina ya nini? ndo maana ya kufanya uchunguzi, hapa ana maana kwamba anataka aone ushiriki wa serikali katika jambo hili. tuache siasa kwenye mambo ya msingi kwa taifa. big up zitto!!!!1………

  malaki stephano

  November 24, 2012 at 7:16 AM

 21. Hali ya siasa na demokrasia, kudorora kwa uchumi na ongezeko la umaskini nchini Tanzania Survey
  “‎”http://www.surveymonkey.com/s/KTRXRMW””

  William Elibariki Ngowi

  November 26, 2012 at 7:36 PM

 22. Ndugu! Zitto! Ujinga wa Watanzania walio wachache unaonekana hapa! Tunakutegemea kwa haya ulio yaona na kuyafahamu na kuanza kuyasemea kwenye eneo husika japo kwenye eneo lenyewe limekuwa ni la kwao kwa mipango mipango ya kwao na si kwa WATANZANIA. Kwa wale watanzania wajinga kama kina Mkuchika kwa maneno wanayo weza kusema juu ya mambo yaliyoweza kubainishwa Sio watanzania na wala hawafai kuwa viongozi ktk nchi hii.

  Zitto! napenda nikuite hivyo kwakua najua ww ni Zitto. najua kunakundi dogo la watu wanaojiita nchi hii ndiyo ya kwao na wanamamuzi yasio sahihi kwa Watanzania. Sasa tunasema watanzania kuibiwa basi! na kile ambacho kimeibiwa! kirudishwe Tanzania kwa Watanzania wenyewe. Napenda Watanzania wote watambue hizi ni fedha zetu na wala si za CHAMA CHOTE CHOTE cha SIASA. na si maslahi ya chama chochote! ni hoja kwa WATANZANIA. Kudahi haki zetu kwa kutowaonea haya hawa viongozi wetu mchwala wasio jielewa kujua kuwa cheo ni Dhamana. Kama kweli hili litapita hivi hivi! inanama hii Inchi yaina Wanaichi. BIg UP ZITTO! Tupo pamoja.

  Lyimo

  November 28, 2012 at 1:19 PM

 23. Big Up, Hon. ZZ Kabwe!

  2015 is all yours for Presidency!

  Mayenga Mabula Mbuzah

  November 30, 2012 at 8:00 AM

 24. Hon. Nakupongeza kwa kusimamia kidete na kuongea bila kusita wala kukatishwa tamaa. Sina shaka na ujasiri ulionao na chachu ya kutetea haki ya mvuja jasho toka siku ya kwanza unaingia bungeni. Usirudi nyuma na umma wa watz utafaidika na msimamo wako, membe, ole sendeka na wengineo waliochagiza na kuonyesha hisia zao kwa hoja yako @ALUTA CONTINUA DE ZITO ,KILA LAKHERI

  Leonard simeone

  December 1, 2012 at 5:41 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: