Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Zitto- Karatu Mjini Leo: Taarifa ya Ngwilizi, Mabilioni ya Uswisi na ulazima wa CHADEMA kuongoza nchi

with 23 comments

Nasubiri kwa hamu kubwa mkutano wetu wa leo hapa Karatu. Jimbo ambalo CHADEMA imeliongoza vipindi 4 mfululizo. Ngome yetu haswa.

Nitazungumzia;

 • Taarifa ya Kamati ya Ngwilizi(Kutaka taarifa iwekwe Wazi)
 • Hoja ya mabilioni yaliyofichwa Uswisi na
 • Ulazima wa kuindoa CCM madarakani mwaka 2015 ili CHADEMA iongoze nchi na ktutokomeza umaskini kwa kupambana na ufisai na kukuza uchumi wa vijijini.

ZZK

Karatu Mjini

 

Advertisements

Written by zittokabwe

September 30, 2012 at 11:29 AM

23 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Kila la kheri kamanda,ila hoja ya urais kwa sasa achana nayo.utaharibu upepo.

  Alphonce

  September 30, 2012 at 11:39 AM

 2. waiting for updates

  Castro Asel Kajula

  September 30, 2012 at 11:39 AM

 3. sana tu m2wetu,pamoja sana urais 2015 kama kawa ukiona vp ingia ulingon 2po nyuma yako,afu nipe mchakato nataka nijipange 2chukue jimbo la handen m2 wangu.

  waziri

  September 30, 2012 at 11:49 AM

 4. hakika mimi binafsi ningependa kuona chama changu CHADEMA kikishinda Uchaguzi mwaka 2015

  BULA SADI NUMBE

  September 30, 2012 at 12:00 PM

 5. hakika mimi binafsi ningependa kuona chama changu CHADEMA kikishinda Uchaguzi mwaka 2015, I LOVE U CHADEMA Forever

  BULA SADI NUMBE

  September 30, 2012 at 12:00 PM

 6. i’m waiting for your speech, real we need a change for the development of our country,

  THADEUS

  September 30, 2012 at 12:29 PM

 7. Kila laheri, najua we ni mpambanaji, kaza buti. Tuko pamoja wape hi wakwe zangu hapo karatu.

  Nakale nkwabi

  September 30, 2012 at 5:20 PM

 8. mchango wako bado unahitajika bungeni.

  khamis

  September 30, 2012 at 8:54 PM

 9. gd,,,uko!!!!

  KAJIA

  September 30, 2012 at 10:47 PM

  • Historia daima hujirudia,uhuru mwalimu miaka 39 kuwa rais na chama tawala kitaondolewa na kijana miaka 39.Kaza buti hakuna kulala.

   baraka gilagiza

   October 1, 2012 at 6:30 PM

 10. asante mh kwaku2juza habari nzuri na zenye faida kwa sisi wanachama wana Chadema

  BULA SADI NUMBE

  October 1, 2012 at 8:11 PM

 11. piga kazi kamanda..tanzania inahitaji ukombozi wa kweli si mabishano ya kisiasa,,,i believe in ur capability

  Frank Robert

  October 2, 2012 at 8:44 AM

 12. kama ukifuata utaratibu na mchakato wa chama chetu hamna shida na sisi wananchi tunataka kiongozi mzuri kama KAGAME WA RWANDA utaweza?na siyo vibaya kueleza nia yako ya urais mapema na kuanza mikakati yako dhambi iko wapi maana wote waliofanikiwa walifanya maandalizi mapema.Wakati wote mshikamano ktk chama udumu mtembee kila kona ya nchi ili muone ushindi mtapata,

  jasson taifa

  October 2, 2012 at 10:55 AM

 13. Hilo neno,lazima ripoti iwekwe bayana ili tujue mbivu na mbichi siyo kulindana kama walivyozoea.na leo utupe ukweli juu ya nia yako ya kuomba ridhaa ya kuongoza nchi kupitia chama chetu pendwa chadema.keep it up bro….

  Ally Mambo

  October 2, 2012 at 11:43 AM

 14. safi sana

  Ernest

  October 2, 2012 at 7:28 PM

 15. that is good bro. but we have a lot of victim in the country, they don’t see how our government manipulate our resouces, making all tanzanian as foolish. we need changes bwana and not otherwise

  HubE

  October 3, 2012 at 7:55 AM

 16. Naunga mkono nia yako ya kugombea u-president lakini kwa sasa naona muda bado kidogo na inaweza kuchafua hali ya hewa ndani ya chama na kutoa mwanya kwa ccm kuchukua urais kwa ulaini sana.

  Emily Juma

  October 3, 2012 at 1:47 PM

  • The way I know Zitto Kabwe.
   Sijawahi kutana naye uso kwa uso japo wote ni wenyeji wa mkoa wa kigoma. Lakini, nafurahishwa sana na jinsi anavyobeba mawazo ya vijana wengi wa kitanzania ambao wamesahauliwa na serikali yao kwa miaka nenda rudi. Somewhere something went wrong na viongozi wetu hawajaliona hili. Na hili ndilo limeifanya vijana kuichukia CCM na ari ya kuingiza viongozi vijana katika nyadhifa mbalimbali za uongozi limewadia. Leo sizungumzii hili bali nataka nijikite kwa yale ambayo yanasomeka magazetini juu yam h. Zitto.
   Ndoto ya viongozi wengi ni kuwa rais japo wote hawawezi kuupata urais huo. Hivyo basi, ni lazima mtu mmoja aaminiwe na kutumainiwa na wananchi ili abebe jukumu hili kuu. Viongozi wetu ni wale wanaouwaza urais na ni wale wanaoutaka urais. Na viongozi wetu wanautaka urais kisiri siri na wengine wakisingizia kuwa wametumwa na wazee. Usiutake uongozi kisiri siri kama unataka kuwa kiongozi kweli. Tangaza hadharani harafu uje tukuulize kwa nini unataka kuwa rais au kiongozi wetu? Maneno haya si yangu kwa kuwa mwalimu Nyerere aliwahi kuyatamka. Nayarudia tena kwa mara nyingine. Kwa nini?
   Hivi karibuni mh. Zitto Kabwe kwa kulifahamu hili aliamua kutangaza nia yake ya kugombea urais kwa tiketi ya chama chake. Ni haki yake ya msingi na kikatiba. Maana katika maisha yapo mawili, kuongoza au kuongozwa. Anadai, ipo siku atatoa sababu kwa nini ataka kupeperusha bendera ya chama chake katika wadhifa huu mkuu katika utumishi wa umma. Hivyo basi, badala ya kuwa wavumilivu, wengi wameamua kumshambulia eti ni mapema mno kutangaza wakati angejikita katika siasa za kukijenga chama na hivyo kusababisha misuguano ndani ya chama chake.
   Mimi sioni misuguano ndani ya chama ambayo imekuja baada ya zitto kutangaza nia yake ya kuwania urais. Kama ipo, ikifuatilia kwa undani zaidi utakuta ni misuguano ambayo ilikuwepo hata kabla ya yeye kutangaza nia hii. Si kwamba nampiagia upatu au kumtetea? La hasha, siwezi kufanya hivyo kwa kuwa mimi si swahiba wake. Mbali na hilo hajawahi na sijawahi kukutana naye, na hivyo hanifahamu japo wote tunatoka mkoa wa kigoma. Nalazimika kutoa maoni haya kwa kuwa vyombo vya habari nchini vimeacha kuandika mambo yanayohusu matatizo ya taifa na watanzania, badala yake kujikita kuamwandika Zitto. Zitto amekuwa gumzo nchini kuliko hata rais wa nchi. Najiuliza mwingine vipi kesho asipopita kwenye mchujo ndani ya chama au akatokea mtu mwingine ambaye chama kinamwona kuwa ni bora kuliko zitto. Mtasemaje?
   Mimi nadhani zitto ametangaza nia hiyo kwa lengo moja. Kwanza, anataka wanachama wa chama chake wampime na kumchunguza kama anafaa kupewa jukumu la kupeperusha bendera ya chama mwaka 2015. Lengo lake ni watanzania wampime. Mtampimaje? Wanachama wa Chadema jielekezeni katika utendaji kazi wake. Je anajituma ipasavyo ndani ya chama na nje ya chama? . Lingine, tumpime katika kuyatambua matatizo yanayolikabili taifa na umma wa wananchi, na hapa yapo mengi rukuki. Je anatoa masuluhisho ya matatizo hayo? Masuluhisho hayo yanajibu hoja za wengi hasa asilimia 80 ya watanzania maskini waishio vijijini na ambao wamesahaurika? Muhimu ni kwamba, je kuna tuhuma zozote zinamkabili hasa katika hasa katika utendaji kazi wake, vipi rushwa, matumizi mabaya ya madaraka, ufujaji wa mali za umma katika nafasi zake za uongozi na mengine mengi. Tuhuma ziwe zimethibitishwa na vyombo husika.
   Kuna watu wengine wamediriki hata kusema eti hajishughulishi na shughuli za kukijenga chama, sijui kama kweli wanamfahamu Zitto Kabwe? Japo sipo nyumbani kwa kipindi kirefu na ninavyoandika maoni haya naishi nje ya nchi, lakini nimeshuhudia kupitia mitandao ya kijamii akishiriki kikamilifu kukijenga chama; kama vile kufanya mikutano ya hadhara hasa katika kutangaza sera za chama, zipo video nyingi na hotuba nyingi tu zinazomhusisha yeye na viongozi wengine wa chama. Ameshirika barabara katika kampeni mbalimbali za uchaguzi kuanzia udiwani na ubunge katika maeneo yetu ya nchi. Labda nyie mnaona kuwa haitoshi lakini lazima mseme ni nani kafanya zaidi yake na wapi? Au ni ile methali kwamba akutukanaye hakuchagulii tusi…
   Suala lingine la kujadili ni mapungufu ya katiba yetu ya chama, ambayo haiko wazi katika kutoa muda mwafaka wa wanachama wa kutangaza (mimi sijui ni lini mtu anatakiwa atangaze). Katiba ya nchi nayo ipo kimya ingawaje haihusiki kwa lolote katika hili, wanachama wa vyama vya siasa na vyama vyao wameachwa waamue wenyewe. Sasa basi, inakuwaje mtu amwandame Zitto badala ya katiba ya chama ambayo ipo bubu. Ndugu zangu wana-Chadema na watanzania kwa ujumla tujikite katika kujadili masuala ni si majina au watu binafsi. Mbona John Shibuda alitangaza na hakuandamwa kama anavyoandamwa Zitto? Mbona, Deogratius Kisangu katibu Bavicha-Tanga ametangaza na haandamwi? Iweje Zitto Kabwe?
   Mimi naona aibu sana kwa mwasisi wetu wa chama Edwin Mtei kujikita katika kujadili jina la mtu badala ya kujikita katika kujadili masuala. Mh. Mtei amekwazika sana baada ya Zitto kutangaza, ni kama alikuwa hategemei mtu kama Zitto angefanya hivyo. Hoja yake anadai wakati wake bado, sijui alitaka afanye hivyo lini wakati katiba nayo ya chama ipo kimya. Mimi naonelea kabla ya kumtuhumu mtu, tutuhumu kwanza katiba yetu ya chama na vilevile pia tutuhumu vyombo vya habari kwa vile navyo vinachochea migogoro ndani ya vyama vya siasa kwa lengo tu la kutaka kuuza gmagazeti.
   Wengine wamesema zitto ni mbaguzi eti asingesema kuwa mapinduzi ya kiuchumi Tanzania yataletwa na mtu wa kizazi cha baada ya uhuru. Hili tusingelijadili leo, tungesubiri siku ya kuchuja wagombea harafu tukamwuliza; ulikuwa na maana gani kutoa kauli ya kibaguzi kama hiyo. Huenda anazo sababu za msingi na akipewa muda anaweza kutufafanulia na tukamwelewa.
   Mwisho, ningependa kusema kuwa tuziangalie upya sifa za kumpata mgombea wetu kwa nafasi yoyote ya uongozi. Tuhakikishe tunaingiza sifa hizi ndani ya katiba yetu kwamba “yeyote ambaye anatuhumiwa katika matumizi mabaya ya fedha za chama na serikali (lakini tuhuma hizi ziwe zimethibitishwa na mahakama au kamati teule za bunge au tume za uchunguzi na vyombo vya dola), ubadhilifu wa mali za umma, rushwa na ufisadi” asilogwe kuchukua fomu yetu. Lazima tujifunze kutoka chama cha CCM ambapo wao hayo yamekuwa ni vigezo vya kuwapata viongozi. Hili likifanikiwa, hakuna mtu atakayethubutu kutangaza au kujigamba kugombea kupitia chama chetu.
   Suala la kumpata mgombea kwa kiti cha urais, tusiwaachie viongozi wetu wa chama na kufanya hivyo ni kujitakia matatizo. Mkutano mkuu au halmashauri kuu ya chama washiriki tu katika kuyachuja majina ya wagombea ili mwisho watuletee majina matatu au mawili ambayo yatapigiwa kura na wanachama nchi nzima. Atakayeshinda, ndiye awe mgombea wetu. Suala hili si lao, ni letu. Na kama ni letu basi, tuwaache wanachama wenyewe wafanye maamuzi ya mwisho. Hawa watatu wazunguke nchi kwa kampeni kushawishi wanachama wetu na kuwe na public endorsement kutoka kwenye party leaders kumwunga mkono mgombea anayeona anafaa.
   Zipo hoja hapa zitajitokeza kuwa gharama za kuendesha kampeni hizi zitatoka wapi? Tuwe wakweli na tueleze umaskini wa chama chetu, wao wajigharimie kwa gharama zao wenyewe. Hapa tutakuwa tumeepuka suala la viongozi kupatika kwa njia za rushwa, tusiiandame CCM pekee katika hili, kwani laweza kutokea kwetu. Madhara ya viongozi wanaopatika kwa njia za rushwa ni makubwa na watanzania tumeyaona, rais baada ya kutumikia watu… Anatumikia wenye noti. Never again…
   Nimalizie tu kwa kutoa wito kwamba tuwaache watu wetu na yeyote mwenye nia ya kutangaza atangaze hata kesho. Tutawahukumu kwa matendo yao na si kwa kauli zao. Yeyote anayetanguliza maslahi ya chama mbele, anaye poteza muda wake mwingi katika kukijenga chama usiku na mchana, anatufaa kutuongoza katika kinyanganyiro cha kuisaka IKULU.
   Ikulu ni yetu hapo 2015. Peeeeooooppppplllllleeeeee’s Pooooowwwwweeeeeeeer!!!!
   Joshua Bukuru
   Belgium.

   Joshua Bukuru

   October 12, 2012 at 9:37 PM

 17. kwa hali ilivyo sasa tunawategemea sana kulikwamua hili taifa katika wimbi la umaskini,ufisadi uliokithiri nadhani unayo nafasi nzuri kitaifa na kimataifa,hebu jaribu kupiga picha je ni watu wangapi wanokuangali kwa sasa,ni wangapi wanaotegemea litokalo kinywani mwako kama ndiyo kauli yao!msituangushe watanzania tuko nyuma yenu.endeleeni kusonga mbele kwa umakini bila ya woga wowote,kwani bila ya kufanya hivyo hii nchi haina kitu mbeleni.watoto na wajukuu watawalilia nyinyi mliopata nafasi lakini mkahairisha kuitumia vizuri.God bless you.

  thobias

  October 4, 2012 at 4:14 PM

 18. kamanda zitto kabwe zipo taarifa kwamba CHADEMA huenda ikagawanyika na kuwa ktk makundi mawili chadema asilia na chadema unalizungumziaje hili ., Na hii ni kutokana na kutokukubaliana ktk uchaguzi wa 2015

  JULIUS MDOPE

  October 5, 2012 at 3:51 PM

 19. Hey. TZZK I’m among of vthose members who voted u twice as long as u leading North Kigoma.
  I hope the way God blessed you at first time will do it for more more times .
  Never give up

  Katandala Mlinzi

  October 8, 2012 at 3:58 AM

 20. Binafsi nilmpigia kura zitto kuliongoza jmbo la kg kas.mabdiliko ya kweli aliyoonesha jmbon na taifa yfaa k2mika kumpma.

  Tunguhole

  October 30, 2012 at 9:58 AM

 21. Zuberi zitto, nakuomba usimamie ukwel na usisalit wezako kwan siku hiz umepoa sana bungen why so? Kaza but mchukue madaraka na komaa mafisad warudishe pesa na wafungwe.

  Godfrey Gilala

  November 6, 2012 at 9:05 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: