Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Highlights za Hotuba: Sakata la rada Bado Bichi-Zitto

with 2 comments

2.5 MKOPO WA KUNUNUA RADA ILIYOGUBIKWA NA UFISADI

Mheshimiwa Spika, sehemu ya Malipo ya Deni la Taifa ni Mkopo ambao Serikali ilichukua ili kununua Rada kutoka kampuni ya BAE ya Uingereza. Suala hili la rada limejadiliwa sana nchini kwa upande mmoja tu wa ufisadi wa kupandisha bei ya Rada na hatimaye kurejeshwa kwa iliyoitwa chenji ya Rada. Hiyo ilikuwa ni nusu tu ya ukweli kuhusu suala la Rada kwani Serikali ilikopa kiasi cha dola za kimarekani 40 milioni kutoka Benki ya Barclays ya Uingereza kwa ajili ya kununulia Rada. Mkopo huo ulikuwa na Riba ya asilimia 4.9 juu ya kiwango cha riba zinazotolewa na Benki ya Dunia au IMF.

Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kujua kama mkopo huu umeshalipwa wote na jumla tulilipa kiasi gani cha fedha. Ukilinganisha fedha iliyorejeshwa kama chenji ya Rada na Fedha ambayo Tanzania iliilipa Benki ya Barclays (Principal amount na Interest), je chenji ya Rada ilikuwa na thamani yoyote kifedha?  Mjadala wa ununuzi wa Rada hauwezi kuisha kwa kufurahia kurejeshewa chenji tu. Mjadala huu bado mbichi kabisa kwani tunataka ukweli na ukweli mtupu uelezwe kwa umma na kuona Taifa lilipata hasara kiasi gani kwa ufisadi huu wa kimataifa na hatua stahiki za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wote walioingiza hasara kwa Taifa letu.

Advertisements

Written by zittokabwe

August 15, 2012 at 11:27 AM

Posted in Uncategorized

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. mbona waziri anasema hakuna mtanzania yeyote anayehusika na ufisadi huu wa rada?na hakuna hatua yeyote itakayochukuliwa dhidi ya ile kampuni?mara mafisadi wapo mara hawapo,mbona mnatuchanganya?membe alishawahi kusema nitawataja wote kwa majina,juzi anakanusha vp tena,tuweke sawa kamanda

  nickson medrd

  August 15, 2012 at 11:47 AM

 2. Pamoja na kwamba serikali, kwa sababu za wazi kabisa, imejitahidi sana kukana ufisadi ulitawala ununuzi huu kwa kujikita kwenye swala la rushwa tu, kuna vipengele vya sheria nyingine za taifa hili ambavyo hatusikii serikali ikivizunguimzia. Kwa mfano:

  (a) mahitaji ya kisheria ya wale walioainishwa kama viongozi kuorodhesha mali zao (na madeni) kila mwaka kwa Tume ya Maadili. Watu wawili ambao wametajwa kwenye kadhia ya rada ni viongozi au walikuwa viongozi kwa muda mrefu wa sheria hiyo. Je, waliorodhesha pesa hizi kwenye mali zao, au la; na kama hawakufanya hivyo wasimamizi wa sheria wamechukua hatua gani?

  (b) sheria ya kodi ya mapato inaruhusu kuchunguza mtu na kukadiria kodi pale ambapo inaonekana mali/ matumizi yake (lifestyle) haviendani na kipato chake alicholipia kodi. Je, kuna hatua imechukuliwa?

  (c) taratibu za kifedha za benki kuu ya Tanzania (BoT) zinazuia Mtanzania kuwa na akaunti nje ya nchi bila kibali cha BOT. Je, hawa wawili wanaotajwa kwenye vyombo vya habari walikuwa na vibali hivyo au la; na kama walikuwa/ wana vyo, vilipatikana kihalali?

  Ngemera Ndibalema

  August 18, 2012 at 11:24 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: