Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

No Tax Revenue, No Mining Licence on Uranium – Zitto Kabwe

with one comment

 No Tax Revenue, No Mining Licence on Uranium – Zitto Kabwe

Leseni (Special Mining Licence) ya kuchimba Uranium (Mkuju River Project) isitolewe mpaka Kodi (capital gains tax) Tshs 290 bilioni ilipwe na Waustralia/Warusi.

(taarifa ya mbunge Zitto Kabwe Bungeni kama ilivyorekodiwa na Hansard)

=========

MHE. KABWE Z. ZITTO:

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa taarifa kwa mujibu wa Kanuni ya 68 (8). Sikupenda kusimama wakati maswali yanaendelea ili kutokuondoa flow ya maswali, Wakati swali Na. 353 linajibiwa la Mheshimiwa Ali Khamis Seif la Wizara ya Nishati na Madini, pamoja na swali la nyongeza kuhusiana na mradi wa Uranium wa Mkuju River Project, ambapo alitaka kufahamu kwamba Serikali imefaidika namna gani na mabadiliko ya umiliki.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasikitika kwamba swali hilo halikujibiwa inavyopaswa, kwa sababu mwaka jana kampuni ya Mantra Resources ya Australia iliuza mradi huu, kampuni nzima asilimia 100, kwenda kwa kampuni ya Russia ya (ARZM) kwa thamani ya dola za kimarekani milioni mia tisa na themanini (USD980m). Baada ya mauzo hayo, mamlaka ya mapato Tanzania TRA walihitaji walipwe Capital Gains Tax ya asilimia 20, ambayo ni sawa sawa na shilingi milioni mia moja themanini na sita (USD 186m).

Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa pesa hizi hazijalipwa, na Serikali inafanya mazungumzo na kampuni hii, na si kweli kwamba kampuni ya UraniumOne, ni tofauti na hiyo kampuni ya Urusi. Kampuni ya UraniumOne ni sehemu ya Subsidiary ya hiyo kampuni ya Urusi, inamilikiwa na hiyo kampuni ya Urusi. Kwa hiyo palitokea mabadiliko ya ownership katika mradi huu, Serikali inapaswa kuhakikisha kabla Special Mining License haijatolewa kwa ajili ya mradi wa Mkuju River Project wa Uranium, Serikali ipate dola milioni 186 za capital gains ambazo TRA mpaka sasa wanazidai. Tutasikitika sana iwapo Special Mining License itatolewa kabla ya tax compliance. Kwa sababu Tax Compliance ni lazima iwe ni sharti muhimu sana kwa miradi ambayo inaendelea.

[MHE. KABWE Z. ZITTO]

Mheshimiwa Naibu Spika, tusiridhike na mafanikio tutakayokuja kuyapata, kwa sababu kwenye dhahabu tuliambiwa hivyo hivyo kwamba tutapata ajira, tutapata mrahaba, tutapata FDI lakini matokeo yake ni kwamba mpaka leo wananchi bado wanalalamika.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe rai kwamba special mining licence Waziri wa Nishati na Madini, asiitoe mpaka fedha zetu dola milioni mia moja themanini na sita za capital gains tax ambazo TRA wanawadai hawa watu wa Uranium zimelipwa, vinginevyo Serikali itakuwa imeshindwa kutetea na kulinda rasilimali za nchi yetu inavyotakiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naomba kutoa taarifa hiyo na Waziri aweze kuifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.

 

Written by zittokabwe

August 11, 2012 at 12:49 PM

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Hongera Kabwe usiwaachie nafasi hata kidogo waziri anasema wako makini kuliko wewe lakini mbona maliasili zetu wazungu na watu wenye pesa zao wanatupola sisi walala hoi badala yake kufuatilia kwake ni kuongeza makali ya maisha kila kukicha mwambie waziri propaganda zake tumezichoka tunataka mikataba yenye tija si mikataba ya kutishia maisha ya wananchi na kuuwa watu hasa wasio kuwa nacho. Tuko pamoja natamani mwaka 2015 ufike mapema nahamu sana ya kupiga kula kwa sababu mawaziri sasa wanaongea wanachotaka ili mradi waonekane wanajibu hata kama wanacho kijibu kiko tofauti na swali lililo ulizwa. May God bless you and all who fight for Tanzanian rights.

    Fikiri

    August 11, 2012 at 2:41 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: