Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

with 46 comments

MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Ndugu Waandishi,

Nalazimika kukutana nanyi kutoa maelezo juu ya tuhuma zenye shinikizo la kisiasa zinazoelekezwa kwangu binafsi kwamba hata mimi nimeshiriki katika vitendo vya rushwa, kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma. Taarifa hizo, kama kawaida ya uzushi mwingine wowote  zimesambazwa kimkakati na kwa kasi kubwa kiasi cha kuukanganya umma.

Nafahamu nabeba dhamana kubwa ya uongozi, taswira yangu ya uongozi daima imeakisi njozi na matumaini ya wananchi wa Kigoma Kaskazini, wananchi wanyonge na vijana kote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa, jinsia zao, makabila yao na rika zao. Hivyo, nawajibika kupitia kwenu kuwatoa hofu juu ya hisia potofu zinazopandikizwa kwao na wale wasiopenda kuona baadhi yetu tukiwaunganisha na kuwasemea watanzania wasio na sauti, dhidi ya vitendo vya hujuma na vyenye dhamira ovu kwa taifa.

Mkakati huo wa kuniunganisha na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wanaotuhumiwa kwa kupokea Rushwa unatekelezwa kwa njia zifuatazo:

 1.   Kumekuwa na kauli za watendaji wa serikali ambao wamekuwa wakizieneza na hususan kutoa taswira kwamba baadhi ya kauli zangu zinatokana na ushawishi wa rushwa;
 2.   Kuna taarifa ambazo zimeandikwa tena katika kurasa za mbele za baadhi ya vyombo vya habari  zikidai ’’Zitto kitanzini’’ ama ’’Zitto sawa na popo nundu’’  zikiashiria kwamba na mimi ni mla rushwa; na
 3.   Waandishi wa habari na jamii kwa ujumla wamefikia kuaminishwa habari hizi kiasi cha wengine kuuliza kwa nini Mhe. Zitto Kabwe hakutajwa katika orodha iliyotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani.

Ndugu Waandishi,

Naomba kutoa ufafanuzi wa hicho kinachoelezwa kwamba nina ushiriki katika masuala ya rushwa hususan kwenye masuala yanayohusu sekta ya Nishati na Madini:-

 1. Mara baada ya bodi ya Wakurugenzi ya  Shirika la Usambazaji wa Umeme Tanzania (TANESCO) chini ya Uenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Robert Mboma kutangaza kwamba imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Nd. William Mhando ili kupisha uchunguzi wa baadhi ya vitendo/mwenendo wake, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ambayo mimi ni Mwenyekiti wake ilimuandikia Mhe. Spika kumuomba aridhie ili Kamati iweze kuwaita Bodi ya TANESCO, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali  (CAG) na pia Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kujiridhisha na tuhuma zote zinazotajwa zinafanyiwa uchunguzi wa kina na hatua kuchukuliwa;
 2. Kamati ya POAC ninayoiongoza ilimuomba Mhe. Spika kuwaita wahusika tajwa kwa kuwa zilikuwapo tetesi kuwa kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi huyo siku chache kabla ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kulikuwa na lengo la kufunika ’madudu’ makubwa zaidi kwa kulichagiza Bunge na tukio hilo dogo, mkakati ambao naona umefanikiwa sana. Isitoshe, Kamati kutaka kujiridhisha na hatua za Bodi ni sehemu ya msingi ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati yaliyowekwa kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge na pia Shirika la TANESCO ni moja kati ya mashirika ambayo yanawajibika kwetu kwa hesabu zake na pia ufanisi wake kwa ujumla. Tumefanya hivyo pia katika mashirika mengine, hili la TANESCO sio tukio la kipekee;
 3. Kitendo hiki cha halali na kwa mujibu wa Kanuni kilichofanywa na Kamati yangu  kimetafsiriwa kwa makusudi na baadhi ya watu kwamba ni ishara ya kuwa sisi au zaidi kwamba mimi nina maslahi binafsi na TANESCO na hususan Mkurugenzi wake Injinia Mhando, ndio maana tumetaka maelezo ya Bodi. Ukweli kwamba Kamati ya POAC tumewaita pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu (CAG) na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa jambo hilo hilo umefichwa kwa makusudi!
 4. Baada ya  tukio hilo, nikiwa hapa Dodoma, mwandishi wa habari wa gazeti moja alinifuata akiniambia kuwa wamekutana na Mhe. Waziri Mhongo na Katibu Mkuu wake, Nd. Eliachim Maswi hapa hapa Bungeni na wamewaambia kuwa mimi nimepewa rushwa. Hakutaja nimepewa rushwa na nani, kiasi gani na wala kwa lengo gani!
 5. Nimejaribu kumtafuta kwa simu Mhe. Waziri Mhongo na Katibu Mkuu wake ili wanipe ufafanuzi juu ya mimi na Kamati ya POAC kuhusishwa na tuhuma hizi bila mafanikio, hali ambayo inaniondolea mashaka juu ya ushiriki wao katika kueneza au kuthibitisha uvumi huo. Najaribu sana kujizuia kutokuwa na mashaka na ushiriki wao huo ikizingatiwa uzito na taswira ya nafasi zao katika jamii, lakini wameshindwa kunidhihirishia tofauti.

Sasa naomba kutoa ufafanuzi rasmi kuhusu mlolongo wa matukio hayo tajwa ambayo yanatumiwa na baadhi ya wanasiasa kuonesha kwamba eti nimehusika na vitendo vya rushwa.

 1. Binafsi sijawahi kuwa na mawasiliano ya aina yeyote na uongozi wa TANESCO kushawishiwa juu ya hatua ambazo POAC ndio imezichukua za kutaka kujiridhisha juu ya utaratibu uliotumika. Ieleweke wazi kabisa kuwa, hakuna wakati wowote, popote ambapo mimi binafsi au Kamati yetu imekataa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO kuchunguzwa kwa tuhuma zozote. Ambacho tumesisitiza wakati wote ni ufuatwaji wa taratibu, kanuni na sheria, hili nitalisimamia iwe masika au kiangazi;
 1. Ni kwa sababu hiyo, na kwa kujiamini kabisa nimeunga mkono suala la tuhuma za rushwa zinazotajwa zichunguzwe na Kamati ya Haki, Maadili na  Madaraka  ya  Bunge kwa kina;
 1. Nimekwenda mbali zaidi kukiomba chama changu CHADEMA kifanye pia uchunguzi na tathmini yake kwa kina kujiridhisha na tuhuma hizo;
 1. Natumia fursa hii pia kuomba vyombo vya Dola vichunguze tuhuma hizo kwa nafasi yake ili kuweza kupata ukweli;
 1. Ninaahidi kushiriki kikamilifu iwapo nitatakiwa katika uchunguzi wowote utakaofanywa na niko tayari kuwajibika iwapo nitakutwa na hatia yeyote.

Napenda niwatoe hofu wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini walionituma kuja kuwawakilisha hapa Bungeni na Watanzania wote kwa ujumla kwamba:-

 1. Mimi Zitto Zuberi Kabwe sina bei, sijawahi kuwa nayo na sitarajii kuwa nayo huko mbeleni. Daima nimesimamia kidete maadili ya uongozi bora katika maisha yangu yote ya siasa, na nawaahidi sitarudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa katika nchi hii pamoja na mikakati ya aina hii ya kunidhoofisha na kunivunja moyo;
 1. Nafarijika na salam mbali mbali zinazotolewa kunifariji na kusisitiza kuwa nisilegeze kamba katika mapambano haya, nimepokea ujumbe mwingi kwa simu, sms, tweeter na hata facebook na niko pamoja nanyi Watanzania wenzangu kamwe sitarudi nyuma hadi kieleweke. Naamini katika nchi yetu tunazo rasilimali za kutosha mahitaji/haja ya kila mmoja wetu lakini si ‘tamaa/ulafi’ wa baadhi ya watanzania wenzetu;
 1. Napenda kuweka rekodi sawa kwa Watanzania kwamba nimekuwa Mbunge hiki ni kipindi cha pili, Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) huu ni takriban mwaka wa saba sasa, Kamati yangu inasimamia mashirika 259 ya Umma na si TANESCO peke yake. Mchango wa Kamati hii katika Bunge na kwa ustawi wa Mashirika ya Umma ni bayana na haujawahi kutiliwa shaka. Kamati yetu imeokoa upotevu mkubwa wa mali za umma na kuokoa fedha za umma kutokana na umakini wake. Tumefanya hivyo CHC hivi karibuni, Kiwira na kwenye mashirika mengine mengi. Kote huko uadilifu na uzalendo wa Kamati hii haujawahi kuhojiwa. Inatuwia vigumu kuona kuwa tunahojiwa katika suala hili la TANESCO. Hapa pana kitendawili.
 1. Zipo hoja pandikizi za kutaka Kamati ya POAC ivunjwe na haswa zikinilenga mimi binafsi. Nafahamu kiu ya wasioitakia mema nchi yetu kuiona POAC ikivunjwa au sura zikibadilishwa kwa kuwa Kamati hii imekuwa mwiba kwa mikakati yao ya kifisadi. Kwa maoni yangu, Kamati ya POAC isihusishwe na tuhuma hizi kwa vyovyote vile. Niko tayari nihukumiwe mimi kama mimi na sio kuhusisha wajumbe wengine ambao hawatajwi mahala popote katika tuhuma hizi mbaya sana katika historia ya Bunge letu. Nitakuwa tayari kunusuru Kamati ya POAC na maslahi ya taifa letu kwa kujiuzulu Uenyekiti iwapo itathibitika pasipo shaka kuwa nimehongwa. Kamati ya POAC ni muhimu zaidi kuliko mimi.
 1. Nafahamu pia kuwa kuna wanasiasa hasa wa Upinzani ambao wanautaka sana Uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha. Lakini hawajui kuwa anaepanga wajumbe wa Kamati ni Spika wa Bunge.
 1. Msishangae pia kuja baadae kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa wenye midomo mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa.
 1. Ni lazima tufike mahali kama viongozi kwamba utaratibu unapokiukwa na yeyote yule, au uongo unapotolewa hadharani tuseme bila kuogopa. Hili ndio jukumu letu kama wabunge na viongozi. Kusimamia ufuatiliaji wa utaratibu ni jukumu letu kama Kamati ya POAC na ndio sababu ya msingi ya kuanzishwa kwa mamlaka kama CAG na PPRA. Haiwezekani, tuwe na set ya kanuni kwa kundi fulani na nyingine kwa makundi mengine, au kuhukumu ufuataji wa taratibu kwa kuangalia sura ya mtu usoni

Mwisho

Kumejengeka tabia hivi sasa ya kuwamaliza wanasiasa wenye kudai uwajibikaji na uzalendo. Kumeanzishwa kiwanda kwenye medani ya siasa cha kuzalisha majungu na fitna zenye lengo la kuwachonganisha wanasiasa wa aina hiyo na wananchi kwa kutumia vyombo vya habari na nguvu ya fedha. Naamini mbinu hizi chafu, kama nyingine nyingi zilizojaribiwa kwangu huko nyuma nazo zitashindwa.

Naamini katika kweli na kweli daima huniweka huru. Naamini kuwa mwale mdogo wa mwanga wa mshumaa hufukuza kiza. Kwa imani hiyo, sitasalimu amri mbele ya dhamira zao ovu hata nitakapobaki peke yangu katika mapambano hayo ya kulinda na kutetea rasilimali za taifa zinufaishe watanzania wote.

Daima nitaongozwa na busara ya Hayati Shabaan Robert isemayo, ‘Msema kweli huchukiwa na marafiki zake, nitakapofikwa na ajali hiyo, sitaona wivu juu ya wale wawezao kudumu na marafiki zao siku zote, siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo, nikajitenga na furaha ya kweli itakayotokea pale uwongo utakapojitenga”.

Ahsanteni sana.

Written by zittokabwe

August 1, 2012 at 11:55 AM

46 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. MH; ZITTO naamini wewe ni shujaa siku zote na ukweli huwa haufichiki cha msingi endeleza mapambano mpaka mwisho usirudi nyuma sisi watanzania tunaotafakari na kuchunguza mambo kwa kina hatutayumbishwa na vyombo vya habari.
  Mungu ibariki Tz, Mungu walaani wote wenye majungu na fitna

  Lamu Pascal Elizayo

  August 1, 2012 at 12:13 PM

 2. Reblogged this on Yote yanayonihusu – Lusajo L.M. and commented:
  Add your thoughts Nafahamu nabeba dhamana kubwa ya uongozi, taswira yangu ya uongozi daima imeakisi njozi na matumaini ya wananchi wa Kigoma Kaskazini, wananchi wanyonge na vijana kote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa, jinsia zao, makabila yao na rika zao. Hivyo, nawajibika kupitia kwenu kuwatoa hofu juu ya hisia potofu zinazopandikizwa kwao na wale wasiopenda kuona baadhi yetu tukiwaunganisha na kuwasemea watanzania wasio na sauti, dhidi ya vitendo vya hujuma na vyenye dhamira ovu kwa taifa. – Zitto Kabwe

  Sajjo L.M.

  August 1, 2012 at 12:25 PM

 3. Mh.Zitto,
  siongei kwa kuwa nimeolea kigoma lakini naongea kamamtanzania yeyote yule mpenda haki na mchukia rushwa.umekuwa mtu wa kutiliwa mfano kwa watanzania wote kwa juhudi zako za kutetea wanyonge.pamoja na hayo usitegemee kuwa kuna watu walafi,wabinafsi,wachawi,wendawazimu,wasiokuwa na huruma na rasilimali za Taifa letu watakaa wavumilie ukiwazibia mianya yao ya rushwa na wizi dhahiri.usiwajali hao,piga moyo konde na songa mbele.

  Mortone Leo

  August 1, 2012 at 12:30 PM

 4. Mh. Zitto Binafsi nimefarijika na ufafanuzi wako juu ya tuuma hizi nzito zenye lengo la kupotosha umma. Pia napenda kutumia fulsa hii kuvilaumu vyombo vya habari kwa kubatilisha tuhuma kuwa ukweli. Nivyema vyombo hivi viwe vinatoa habari za uhakika baada ya uchunguzi kukamilika na siyo kuandika/kutangaza habari kana kwamba wameshafanya uchunguzi nakubaini muhusika ni fulani.
  Tunajua upo katika kipindi kigumu lakini tunakutia moyo katika kuendeleza mampambano yako kwa uwazi na ukweli katika kututetea tulio wanyonge.

  “Who the cap fit, let them wear it” ……….Some will eat and drink with you,Then behind them su-su ‘pon you. Only your friend know your secrets, So only he could reveal it. And who the cap fit, let them wear it! Who the cap fit, let them wear it!

  Tupo pamoja daima!

  Mkumbo

  August 1, 2012 at 12:33 PM

 5. Tupo pamoja nawe brother. ALUTA CONTINUA

  JUMA KAMBAJECK

  August 1, 2012 at 12:51 PM

 6. Hata nilivyosikia sikukutilia mashaka hata kidogo na nilikuwa sijaruhusu akili yangu kukubali kile kilichoandikwa nuikijua umebeba dhamana kubwa. Ukweli utajulikana tu. WEWE NI JEMBE LA UKWELI

  Silas

  August 1, 2012 at 12:54 PM

 7. Alwyz kwnye ukwl uongo hauna nafasi. Kuna watu wenye nia binafsi ktk hii issue ndo maana walitaka fnya kwa njia yyte kuwaaminisha watz uzushi huu na kwa kukulengo mh. Hakika watz wa leo si wale wajinga wa miaka ya nyuma tunapima kuanzia kauli inayotolewa 1st time na tunajua lengo lake ni lipi. Hakuna kurudi nyuma hakuna kusuasua daima mbele. Tupo pamoja mh. Kaka yetu kiongozi wetu. B blessed nadhan ukwl umeonekana

  Chriss

  August 1, 2012 at 12:54 PM

 8. safi sana ..tupo pamoja………..

  REUBEN MWANJA

  August 1, 2012 at 12:55 PM

 9. tupo pamoja

  Noel Ernest

  August 1, 2012 at 12:56 PM

  • I support you Zitto. Endelea kupambana, lazima uzushiwe ili ukomaee

   cc

   August 1, 2012 at 1:11 PM

 10. Kaka pole sana kwa yaliyokukuta lakini tunakuomba usiteteleke upo pamoja na watu wote wapenda haki na wazalendo wenye uchungu wa nchi. Ninaloliona ktk nchi hii kwa sasa ni kuibuka/kuibuliwa kwa makundi ya watu yanayofanya kazi mchana na usiku kufanya hila ya kudidimiza mipango na harakaki ya watetea haki na ukweli kama wewe, kitu ambacho kinatupeleka pabaya kama taifa. Kaka Zitto mimi binafsi nakukubali sana sababu mambo mengi huwa unayasema kwa kuyafanyia utafiti wa kina na wala huwa hukurupuki.

  Osiah, M.

  August 1, 2012 at 1:05 PM

 11. naamini sana maelezo yako kaka zitto, tuko pamoja na usirudi nyuma, nilichojifunza ktk hiki ni kwamba hata wenzako ndani ya kambi ya upinzani wanaweza kuwa maadui wako, take care na usonge mbele

  Bogias Mwamgunda

  August 1, 2012 at 1:22 PM

 12. Mh. Zitto wewe ni mpiganaji tena sana na mzalendo, katika usimamiaji wako juu ya uwajibikikaji umekuwa mara kazaa ukishindikiza baadhi ya mawiziri kuwajibika kwa tuuma tu za ki-wizara ili kuonyesha usafi wa mtu na uwajibikaji. nimependa na naikubali hoja yako ya kamati ya POAC kuto-hukumiwa kwa ujumla wake, nafikiri kwakuwa wewe ni msafi katika hili ni wakati muafaka kwa wewe kujitoa katika wadhifa wa mwenyekiti wa hiyo kamati ili kudhihirisha kwa watanzania kuwa wewe si tuu muongeaji bali pia ni mtekelezaji kwa kusimamia na kutetea rasilimali za taifa hili, utakuwa umetunza heshima yako ndani na nje ya nchi hii.

  George S.

  August 1, 2012 at 1:24 PM

 13. Mh. Zito, mimi naamini katika kweli. Taifa lililokumbatia rushwa kama sehemu ya maisha ni vigumu sana mtu mwenye msimamo kama wako kupendwa! usikate tamaa ndg yangu. Kama nafsi yako ipo safi hutataabika.

  maulaga

  August 1, 2012 at 1:38 PM

 14. Mungu yu pamoja nawe

  Tindigwe

  August 1, 2012 at 1:40 PM

 15. Pamoja na hayo mtu anaependa kujikweza si nzuri kabisa. Chadema tunapenda watu wastaarabu

  Mr Lugash

  August 1, 2012 at 1:42 PM

 16. Tupo pamoja sana Mh Zitto Kabwe Zuberi,uelewa wa Watanzania katika mambo haya ya kisiasa umeongezeka sana,hatudanganywi kirahisi hivyo,nasikitika pale Wenzio katika CHADEMA wanapofunga ndoa na wenye hila.

  Lusekelo Adam Mssika

  August 1, 2012 at 1:44 PM

 17. Pole sana Mhe. Zitto….Lakini hii isije ikawapasua ndani ya chama……Ila pia kuna maneno mengine mtaani kwamba umekuwa tajiri kwa muda mfupi…unatembelea gari za kifahari, majumba n.k…hili unaliongeleaje mheshimiwa

  Hans

  August 1, 2012 at 1:58 PM

  • huo ughafla unakujaje wakati ni mbunge wa miaka zaida ya 15 na mshahara wa wabunge unajulikana anajituma,anavyeo,mkopo wa gari kama munge,lakini sijui kama kuna mbunge mwenye maisha mabovu labda awe muhongaji aidha wanawake au wapiga kura kama badueli wa bahi,niniwasiwasi na elimu yako.

   carol paul

   August 1, 2012 at 8:24 PM

 18. Siku zote nimekuwa na Imani sana na Mh. ZITTO! Natamani na kusubiria sana Taarifa za uchunguzi wote ili kujiridhisha kama Imani yangu kwako ni sahihi. Sina wasiwasi na wewe JEMBE LA MABADILIKO NA SITAKI KUAMINI kama Unahusika. Nakuombea kwa mungu siku zote upate baraka na nguvu za kuendelea kuwatumikia Watanzania.

  TAWI G. KILUMILE

  August 1, 2012 at 2:41 PM

 19. tunashukuru sana mbunge wetu kwa kututoa hofu na hata hivyo tulikuwa hatukuwazii hivyo maan hata 2009 hayo yalikufika usife moyo daima songa mbele

  George marawa

  August 1, 2012 at 2:41 PM

 20. mungu akujaalie najua watashindwa tu!

  shaffi h.bakari

  August 1, 2012 at 2:49 PM

 21. Kamwe sijawahi na sidhani kama itakuja tokea nikawa na mashaka na wewe mheshimiwa, hakuna mtanzania mwenye akili timamu asiyetumia akili ya kuazima katika kufikiri eti asitambue kuwa hawa wenzetu mchezo wa haki umeshawashinda na wameona namna pekee ya kutimiza azma yao ni kuwekeza na kujiweka imara na thabiti katika fitina na majungu. Kaka tuko pamoja na kamwe usidiriki kurudi nyuma mana utalipeleka taifa katika mikono ya waasi milele yote. Big up bro

  IMANI ISAYA

  August 1, 2012 at 3:28 PM

 22. ukimya hauwezi kuleta ukombozi hata siku moja, SPEAK OUT so that we can have the reality of what goes on behind the curtain, tupo pamoja kaka, maisha ni mapambano na wewe ndiyo umeyaanzisha na unayaendeleza tupo pamoja nawe daima.

  deosanctus

  August 1, 2012 at 7:14 PM

 23. mungu yuko nawe na lazima utashinda tu, kamwe mafisadi wasijidanganye wala kujifariji kuwa utashindwa, watz tunakupenda sana na tuko nyuma yako broo.

  David

  August 1, 2012 at 7:38 PM

 24. jogoo hata siku moja hafi kwa utitiri,kaka zitto tupo wengi nyuma yako wasikutishe hao vikalagosi.

  carol paul

  August 1, 2012 at 8:10 PM

 25. Kaka nakusihi usivunike moyo. Amka usiku na fanya visimamo vya usiku sana, pray during breaking ur fast dua ya wakati wa kufuturu hairudi. Toa sadaka sana coz sadaka husafisha dhambi. My point is: don’t stress sana, dunia tunapita, no matter how difficult ur trials are, continue to do good as an obligation to your lord coz ultimately ‘inna lillahi wa inna illaihi rajiun’. The r a lot of people who genuinly care abt u and ur success, continue to fight and focus ur energy on the positive. Mwenyezi Mungu yupo nawe, he has never left u, he never will. Yatapita tu

  farhat

  August 1, 2012 at 9:47 PM

 26. mh. Zito usiwe na wasiwasi kwani mbinu zao umezijua chamsingi kuwa makini sana maana hawa mafisadi ni creative sana katika kumdestroy mtu bt tunazidi kukuombea kwa mungu kwani hii vita bado mbichi

  james

  August 1, 2012 at 9:51 PM

 27. asante sana kwa ufafanuzi kwani mie binafsi silisikitishwa sana na taarifa ya wewe kuhusishwa na pia wapinzani wangu walipata mwanya wa kunishambulia eti hata kaka yako kala rushwa. Nashukuru kwa ufafanuzi huo

  Rogers Andrew

  August 1, 2012 at 11:57 PM

 28. I ws not think,,that romours is true bcz i understand u well,God be with u allways,,dont untie ua rope,,,u will let us drop down!!!!
  God blease Tanzania my country….
  God blease Tanga – Lushoto my regional wise…..
  God blease CHADEMA…CZ we are truely agent of change………..
  God blease also those fire fighter(CCM),,,,to understand that is better to be fire preventer CHADEMA and to beleve on them always…………
  God be with us to all stepping steps……..
  I hope God has here our pray,,so dont wory kaka ZITO…no one clever for him!!!

  LUKI=-JEMBE!!!

  August 2, 2012 at 12:07 AM

 29. Nakushauri Mheshimiwa Zito upinzani siku zote ndio tunautegemea katika nchi hii kama Mapinduzi ya kweli ya haki na nina Amini bado unajua madudu Mengi ya Nchi hii sasa ukikaa kimya Bungeni uchafu huo watakupaka wewe kwa kigezo kuwa mwanzoni ulikuwa mchangiaji mzuri sana lakini umenyamazishwa na mafisadi ivyo endelea kuwa mstari wa Mbele bungeni kutetea haki

  NAMKANDA

  August 2, 2012 at 7:10 AM

 30. Nilijua tu lazma watakupakazia lolote ili mradi mambo yao yaende sawa c umeona bajet yao imepita BINAFSI NAKUAMINIA SANA JEMBE USIKATE TAMAA ENDELEA KUKAZA MPAKA KIELEWEKE

  Massoud Moshi

  August 2, 2012 at 10:21 AM

 31. tupo pamoja kaka

  NZOGELA

  August 2, 2012 at 12:36 PM

 32. Maneno ni hazina uwe unabakisha na ya kesho wewe si msemaji wa serikali kulisemea kila linalotokea, wakati mwingine dhamira chanya hutiwa doa na kurupu kurupu ambazo mara nyingi mwenye busara huziweka nyuma na kutafakari kwanza kabla ya kujihusisha na kitu, yaonekana wazi kwamba huu ulikuwa ni mtego-umenasa-mpaka ujinasue-utajikuta mda umekutupa mkono-huwezi fanya jipya-nakuishia kuendelea na mwenendo wa zamani bila kupata wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu mwenyewe. Bunge haliendeshi serikali bali linaisimamia serikali kupitia nyaraka na maelezo yanayoletwa Bungeni na si nje ya Bunge.
  God bless you MPIGANAJI…!!

  Denis

  August 2, 2012 at 1:22 PM

  • wewe ndio wale wanao tuhumiwa au vipi? Na wew ujue Mungu alipoumba dunia hii akaijaria na mali zote zilizomo hamkuwa pamoja wala hakuacha ameandika baraua kwamba ni kwa ajili ya kundi fulani la watu sawa? watanzania wengi sana hivi sasa wana elimu ya kutosha sasa hukuna haja ya kuendele kuwa na mafisadi, wala rushwa na wasiojali masilai ya watanzania

   Emmanuel William

   August 2, 2012 at 2:33 PM

 33. Hata hivyo Mheshimiwa nilijua mimi kabla kwamba huo ni mchezo wa baadhi ya wanasiasa ili kukuchafua jina. Ila kwa sasa wanagonga mwamba maana watanzania wa leo sio sawa na wa zamani kwamba utamdanganya kwa maneno tu akubali. Endelea kukukaa kidete tunakuchukulia kama baba yetu aliyembinguni, maana watanzania tokea huko nyuma walizoea kujua kwamba nchi yao ni maskini haikujaliwa na kuwa na rasilimali yoyote ile hapa duniani. Sasa hicho ni kijicho na ndio maana wameanzisha hii kansa ya kutaka kuwadhoofisha viongozi wetu wa juu (Chadema) kwa kuwa weka jela na mambo mengine. Sisi tuko huku Misri pia tunatarajia kujitolea kwa hali yoyote ile ili kuelimisha vijana juu ya elimu bora ya urai na sera nzuri zinzzotolea na CHADEMA kwa watu wote. Jamani watanzania tusidanganyike chadema ndicho chama pekee chenye kujari masrahi na kutetea haki za wanyonge.People’s power!!! Twende 2015

  Emmanuel William

  August 2, 2012 at 2:27 PM

 34. Mh Zitto usimlaumu yeyote,jilaumu mwenyewe. Unavuna ulichopanda!

  nkwabi masele

  August 2, 2012 at 10:08 PM

 35. Usivunjike moyo shujaa wetu tunajua ni jinsi gani unavyopigwa vita ila wengi wao tupo pamoja nawe hakika huwezi kutimiza lengo bila ya vikwazo ila tupo nyuma yako rais wetu mtarajiwa.

  Habibu hamisi

  August 3, 2012 at 5:57 PM

 36. Bro!kwanza pole ila sikukumbushi kuamini uongozi si mchezo hasa kwenye siasa.Nimekusoma vema na kukuelewa uliyoyazungumza pia nakushukuru kwa kujisogeza kwenye mwamba wa msalaba iwapo utabainika kuhusika sasa tunawataka walioyaleta hadharani watusaidie umma kufahamu kwa uthibitisho.KWENYE UKWELI UONGO HUJITENGA.Kama ndiyo wale tutawafahamu muda mfupi ujao.Pia magazeti wanamiliki wao,wanasema watakalo tunasubili ukweli mjengoni coz kamati iliyoundwa ni mchanganyiko wa itikadi.NITASEMA MUDA UKIFIKA

  Jackson sindoma

  August 3, 2012 at 6:51 PM

 37. Mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni daima watanzania tunapotoshwa na mafisadi kupitia magazeti yao,plse dont afraid we together man.

  adili hassan

  August 6, 2012 at 6:03 PM

 38. Goo d explanations.Politics is like riding a bicycle 2 maintan balance, you need 2 keep riding.To stay in politics you must do politics. Gather courage, show them CHADEMAthru you is for ppl for real and forever. Amen!

  Yohana

  August 29, 2012 at 1:06 AM

 39. pole sana mh.ZITTO KABWE pamoja na kuchafuliwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa pamoja na wabunge lakini bado unakazi kubwa ya kueleza kile walichokutuma watanzania wa k.kaskazini.Watanzania wanyonge km wa MTWARA tusiokuwa na wabunge wa kututetea na kueleza kero zetu huko bungeni 2nategemea wabunge makini kama ww mutukumbuke angalau kwa uchache.wana mtwara 2liobadilika,2naolitakia kheri taifa letu tutakuwa bega nawe na kamwe hatutakusaliti.kumbuka watanzania tunahitaji viongozi makini wanaojitambua na kujipambanua kama wewe.Endeleza juhudi zako.

  Ramadhan silimu

  August 21, 2013 at 9:06 AM

 40. Hii ndiyo Tanzania kakaangu wapo watakao kubeza na watakao kuunga mkono.hakika allah atakujalia uwezo wa juu kuwatete wengi walio wanyonge ktk taifa hili la walarushwa na mafisadi.kumbuka kujiepusha na kuwa ktk kundi viongozi mafisadi.

  Ramadhan silimu

  August 21, 2013 at 11:42 AM

 41. […] DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI https://zittokabwe.wordpress.com/2012/08/01/maelezo-binafsi-ya-mhe-… Tuhuma zote hizo nimewahi kuzitolea ufafanuzi na kukanusha kwani hazina msingi wowote na zilikuwa […]


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: