Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Nisihusishwe na Matamshi na Makanusho wa Wabunge walokuwa Kigoma

with 24 comments

Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka ‘Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015’. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kuyasema. Napenda kusema masuala yafuatayo.

Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi.

Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba. Wabunge hawa hawakualikwa na mimi bali nilisaidia ‘logistics’ tu. Lengo la kushauriana na Vijana wa Kigoma All Stars kuwaalika wabunge kutoka vyama mbalimbali lilikuwa ni kuonyesha umoja na mshikamano wa nchi bila kujali vyama vya siasa.

Wabunge wote walioalikwa waliambiwa hii ni shughuli ya muziki na wala sikufanya mazungumzo nao yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa. Ni bahati mbaya sana kuwa kuna matamshi ya kisiasa yalitamkwa katika shughuli ile.

Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.

Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.

Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu. Mimi kama mlezi wa KigomaAllStars na vijana wenyewe tulijikita katika ‘shukrani Kigoma’ kwa watu wa Kigoma.

Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma.

Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.

Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.

Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.

Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema ‘weka akiba’ sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote.

Advertisements

Written by zittokabwe

July 25, 2012 at 9:07 AM

Posted in Uncategorized

24 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Mhe. Zitto.

  Nashukuru kwa ufafanuzi wako mpana, lakini mm nina mawazo tofauti. Samahani kama nitakuudhi.

  Sioni tatizo lolote katika mtamshi ya wabunge waalikwa kwenye tamasha.

  Inaonekana wanakutabiria jambo la kheri mbele, na hii ni kawaida na ni desturi za binadamu wa mataifa yote duniani. Mgeni hutoa baraka na kheri kwa mwenyeji. Japo siyo wewe uliyewaalika lakin Kigoma ni nyumbani kwako. Sioni ubaya labda kwa wenzangu.

  Na mimi pia nikutakie KHERI. Iwapo tutajaliwa UWE RAIS WETU MWAKA 2015 in JESUS NAME.

  mwanawavitto

  July 25, 2012 at 9:27 AM

 2. Asante kaka Zitto najua umewaacha watu njiapanda kwa maneno yako lakin ukwel utajulikana tu nan msemakweli

  Hansen Nasli

  July 25, 2012 at 9:32 AM

 3. kweli katibu! Watanzania wengi tumekuwa tukishugulia na kuzungumzia mambo yasiyo kuwa ya kimsingi! Leka dutigite.

  fredrick rulagilije

  July 25, 2012 at 9:55 AM

 4. Unajua mheshimiwa Zitto, suala la siasa hapa nchini linavuruga kila kitu, huwezi kusimama leo ukazungumza jambo zito, utasikia katumwa na CHADEMA au ukifanya jambo lolote utasikia maandalizi ya Urais 2015, hii yote ni woga na wasiwasi uliokithiri walionao baadhi ya watanzania hasa waliopoteza uzalendo kwa kung’ang’ana klinda maslahi ya vyama vyao. mtu anapotosha hata jambo ambalo lipo wazi kabisa.

  KIEZERA ALFRED

  July 25, 2012 at 9:59 AM

 5. hofu zishaanza kuwajaa mioyoni mwao. watake wasitake wewe ndo Raisi wetu 1day Mungu akipenda na Tutaikomboa Tz
  .

  masanja Mathew

  July 25, 2012 at 10:00 AM

  • Mimi nadhani wanatabiri ukweli na chama chako kimesikia.. ukisimamishwa wewe hakuna mjadala hapo wewe ndo Rais wetu wanyonge!! na tuliopo nje wote tutarudi kuijenga nchi yetu Tanzania maana tumekimbia kutokana na NJAA!!

   Janeth

   July 25, 2012 at 10:22 AM

 6. Hii inatokana na wanasiasa kututaka wote tuingie ndani ya siasa kwa madai ya kwamba siasa ndiyo maisha yetu ya kila siku,
  hatuna weledi wa mambo mazito na jinsi ya kuyaandaa na kuyatatua, tumejengwa kwenye uoga, tumekosa maarifa kwa kukosa muda wa kusoma historia ya jinsi waliotutangulia walivyofanya mambo yao kwa weledi wa hali ya juu, leo hii wote tumekuwa washabiki kwa kila jambo, wenye fikra Mgando ndio wanaoshabikiwa, ukileta fikra zenye kuiondoa nchi yetu ilipofikia unakuwa Adui.

 7. Kaka Zito let them talk always mti wenye matunda ndio unatupiwa mawe waache wahanye mwishowe watajionea aibu

  heaven

  July 25, 2012 at 10:52 AM

 8. Umeongea maneno sahìhi kwa wakati sahihi na muktadha sahihi!
  Zidi kuwa makini wakati huu kaka mana ww ni ‘modal’ (mfano) kisiasa kwa sisi vijana wengi. Tafadhali usituangushe!

  Kamwela Abraham

  July 25, 2012 at 10:55 AM

 9. Kweli naungana na wewe kaka Zitto katika hili,hivi kuna mpango gani wa kukugombanisha wewe na viongozi wengine wa chama?Naomba uwe makini sana na harakati hizi.Tunakuombea kwa Mungu azidi kukupa ujasiri.

  Franael Joshua Issangya

  July 25, 2012 at 10:59 AM

 10. Good mwana harakati we2

  Edfredson

  July 25, 2012 at 11:25 AM

 11. tatizo waaandishi wetu wanapenda kukuza mamabo katika swala lisilo na maana ili mradi kuuza magazeti, lkn hata kama ni hivyo wewe unakubalika lkn hilo swala linabaki kuwa la chama kutoa msimamo wa mgobea watu wasikuze mambo katika swala hili, nakutakia harakaki njema katika ukombozi wa vijana nchini ww ndo tumaembakiza

  felician makubo

  July 25, 2012 at 11:31 AM

 12. Haya maneno yaliyotamkwa kwenye hafla ya muziki si chochote si kitu cha kuwafanya muanze kusutana kihivyo. Mdee, Nasari, Filikunjombe na wengine wote ni viongozi wetu tunaowaheshimu sana. Nawasihi wote mlinyamazie hili jambo kuendelea kujibizana kimtindo, kukana nk kunawafarakanisha wakati ambao mnatakiwa kuipigania nchi hii. Bunge linatukera sasa fanyani kitu ku-reverse mambo badala kushughulika na maneno tu. ‘Kuongea ni shaba kunyamaza ni dhahabu’. Kitu kitakachotegemeza nchi hii ni mfumo na wala siyo mtu. Tutumie nguvu nyingi kuweka mifumo baadaye hata ikatokea tukapata rais mwenye udhaifu au nguvu kupita kiasi mfumo utamcheck.

  kadulyu

  July 25, 2012 at 11:43 AM

 13. Unahitaji kuwa makini tu, focus on your dreams! Wakukupinga na kutaka kukugombanisha na viongozi wenzako watatokea tu, lakini itahitaji hekima yako kustay on truck!

  Mathias

  July 25, 2012 at 11:58 AM

 14. ALL THE BEST BROTHER PRESHA INAWAPANDA COZ WANAJUA WEWE NDIO MTU AMBAE UNAKUBALIKA NDANI NA NJE YA CHAMA CHETU.KAMA MUNGU AMEPANGA WEWE NDIO UWE RAIS WETU AJAE HAKUNA ATAKAEZIWIA HILO.

  HAMISI LANGA

  July 25, 2012 at 12:35 PM

  • Pole sana lakini jua fika kwamaba you re man of the People, binafsi wewe ni kati ya wanasiasa walau watatu wa taifa letu ninawakubali kwa dhati, is Good kwamba uko pantual kukanusha uzushi wowote unaoleta kukubomoa, tunajua fika kwamba” You can stop the rains if it has to be rain” kama wewe utakua rais wa taifa letu then no body will stop it raining, subira huvuta heri cheza na wabaya wako kwa umakini wa hali ya juu. I am sure you will make it: Thanks like you so much

   Yassin madiwa

   July 25, 2012 at 2:47 PM

  • Kwani hata wakisema kwani dhambi we kuwa rais mbona unafaaa jamani acha waendelee kukutabilia mema ungejua hongera president Zitto Kabwe!!!

   Ntiruteguza

   July 25, 2012 at 3:11 PM

 15. Suala hili limekuwa tete title ya habari ndiyo haswa imebeba maudhui lakini ukifuatilia habari hiyo na nukuu zake inakupa jibu sahihi walichozunguma wabunge vijana walizungumza vizuri lakini kukanusha mara nyingine ni uoga wangepaswa watetee kile walichokisema. Vijana wa taifa hili tunaelekea wapi.Muda mwingine turusu fikira na nafsi zetu zizungumze na kufikiri postive tusijengwe kwa makundi bali tujegenge utamaduni wa kuatembea na kusimamia fact mimi nafikiri hii ndiyo njia sahihi itakayotuongoza kwa siku sijazo tusikubali kufunikwa na miavuli bali tuwe miavuli inayofunika msimamo (fikra zetu) na mambo tunayoamini.

  tom usiri

  July 25, 2012 at 3:29 PM

 16. NAFIKIRI MHESHIMIWA ZITTO HAYO SI MAMBO YA KUUMIZA VICHWA WATU WENYE AKILI TIMAMU ILA KWA WALE WENYE NDOTO ZA KUKIMBILIA IKULU KWA AJILI YA KWENDA KULIPA MADENI YA WATU WAKISIKIA NENO TU LA FULANI ANAFANYA KAMPENI ZA URAIS ROHO JUU ILA NINACHO OMBA NI KWAMBA TUUNGANE PAMOJA KUPIGANA NA MAFISADI NA KUWAONDOA KWENYE MADARAKA PIA TUKUMBUKE NI JINSI GANI YA KUWAPATIA VIJANA ELIMU YA URAIA PAMOJA NA KUIELEWA KATIBA YA NCHI KWANI HAO NDO WATATUSAIDIA KUIFIKISHA NCHI MAHALI AMBAPO TUNATARAJIA .VILEVILE TUANGALIE JINSI YA KUONDOA HIYO MIKATABA YA WAZEE KUJIONGEZEA UMRI KATIKA AJIRA ILI HIZO NAFASI ZIWEZE KUCHUKULIWA NA HAO VIJANA WANAOHITIMU VYUO MBALI MBALI KWANI UZOEFU WATAUPATIA HUKO HUKO MAKAZINI KWANI MWL NYERERE ALIPATIA WAPI UZOEFU WA URAIS?

  OMBENI IKOLA

  July 25, 2012 at 3:37 PM

  • Mh. wanakutabiria mambo mema nawe sema Amen!

   Christina

   July 25, 2012 at 5:03 PM

 17. sawa mh. tumekuelewa vizuri,tumekuomba msaada kwa swala la fao la taifa jins mlivyobadilisha sheria ile bila kuwashilikisha wadau ambao ndio wanachama wa hii mifuko,pili kwani N.S.S.F ni bank?mbona mnaluhusu watu kwenda kukupa bila ruhusa kwa wenye haki zao jamani? tunakwenda wapi? mbona ni kama ubabe tu? ama kwa kuwa nyie wabunge mkimaliza miaka 5 tu mnapata haki zenu mara moja?hapana kaka zitto apo mnatukosea tena sana tu.

  joachim

  July 26, 2012 at 7:15 AM

 18. Endelea kuwa mtumishi wa Umma ..hilo ndio la msingi ! Urais ni dhamana tu kama ulionayo sasa kwa wapiga kura ….

  Ulijualo

  July 26, 2012 at 8:29 AM

 19. hivi hakuna jinsi kabisa kushitaki vyombo vya habari vinavyo potosha uma?

  Simon Philemon

  July 26, 2012 at 10:41 AM

 20. kuwa muwazi,kwani tatizo ni lipi kusema unagombea urais?kwani si ruksa kutanguliza akiba ya maneno uliyonayo leo ili usije sahau siku za usoni?Leke Dutigite

  Ally Hassan Mambo

  July 27, 2012 at 10:01 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: