Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Mchango wangu Bungeni-Hotuba ya Waziri Mkuu: Haki za Uraia, Mafuta/Gesi Asilia na Uwajibikaji

with 18 comments

MHE. ZITTO Z. KABWE:

Haki za Uraia, Mafuta/Gesi Asilia na Uwajibikaji

Unyanyasi wa Watu wa Kigoma

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia Hotuba hii ya Waziri Mkuu. Jana Mheshimiwa Waziri amekuja kuomba Bunge limuidhinishie jumla ya shilingi trilioni 3.8 kwa ajili ya Ofisi yake na taasisi zote zilizo chini ya Ofisi yake pamoja na takribani shilingi bilioni 113 kwa ajili ya Bunge. Fedha zote hizi takribani shillingi trilioni 3.2 zinakwenda Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla hatujaweza kumuidhinishia Mheshimiwa Waziri Mkuu fedha hizi na yeye kama Mkuu wa Shughuli za Serikali, msimamizi wa kazi za Serikali za kila siku na ambaye anaangalia utendaji wa takribani Mawaziri, wote ni vizuri aweze kutoa majibu kwa baadhi ya masuala ambayo mengine ameyaainisha kwenye hotuba yake, lakini mengine hakuyaainisha katika hotuba yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza na Kigoma. Mheshimiwa Waziri Mkuu katika ukurasa wa 51 wa Hotuba yake amezungumzia masuala ya ulinzi na usalama lakini hakugusia kabisa operesheni ambazo zinaendelea hivi sasa katika Mkoa wa Kigoma nadhani na Mkoa wa Kagera kuhusiana na masuala ya wahamiaji haramu. Hivi tunavyozungumza ni kwamba mamia ya watu wa Kigoma wameonyeshwa kwamba siyo raia wa Tanzania. Utaratibu huu umekuwa ukiendelea mwaka hadi mwaka. Napenda Mheshimiwa Waziri Mkuu akumbuke historia baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia kati ya mwaka 1918 na mwaka 1924 Kigoma haikuwa sehemu ya Tanganyika. Kigoma ilikuwa inatawala kama inavyotawaliwa tofauti sasa hivi Burundi kama inavyotawaliwa sasa tofauti Rwanda. Kwa muda mrefu sana Mkoa wa Kigoma umeachwa nyuma katika kila kitu eneo la maendeleo.

Mimi nimeona lami ya kwanza ya highway mwaka 2008. Miaka zaidi ya 40 baada ya uhuru. Leo hii watu wa Kigoma wa maeneo ya Kusini mwa Kigoma wa maeneo ya Kaskazini mwa Kigoma wanasombwa kwenye maboti, wanasomwa kwenye magari wakiambiwa kwamba siyo raia wa Tanzania. Hatuwaoni Wamakonde wakiambiwa kwamba siyo raia wa Tanzania na wanapakana na Msumbiji. Hatuwaoni Wamasai wanaambiwa siyo raia wa Tanzania na wanapakana na Kenya. Hatuwaoni Wachaga wanaambiwa siyo raia wa Tanzania wanapakana na Kenya. Hatuwaoni Wanyakyusa wanaambiwa siyo raia wa Tanzania wanapakana na Zambia na vile vile wanapakana na Malawi.

Kwa nini suala hili liwe ni kwa watu wa Kigoma na watu wa Katavi peke yake? Kwa nini tunatumia fedha za nchi, polisi wa nchi kwenda kusumbua watu wa Kigoma. Nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu operesheni inaendelea sasa hivi katika Mkoa wa Kigoma kuwanyanyasa Raia wa Kigoma waonekane ni Raia wa Tanzania wa daraja B ikome mara moja na viongozi wa Kisiasa, Wabunge wote  wa Mkoa wa Kigoma na Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa tukae tuweze kuangalia kwa sababu kuna uonevu wa hali ya juu sana katika operesheni ambayo inaendelea hivi sasa.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa naomba niyaseme hayo vizuri na ninarejea kwamba tumefundishwa na wazee wetu kwamba sisi kati ya mwaka 1918 na mwaka 1924 hatukuwa sehemu ya Tanganyika iliyokuwa inatawaliwa na Mwingereza. Ninaomba nirejee sisi ni watu wa Kigoma kwanza kabla hatujawa wa Tanganyika, kabla hatujawa Watanzania. Ninaomba nilisisitize hili na watu wa Kigoma wananisikia kwa sababu tumenyanyaswa sana. Ninaomba masuala ya uraia yaangaliwe kwa karibu sana. Huu ni ujumbe ambao nimepewa na watu wa Kigoma nimeombwa niueleze na naomba Ofisi ya Waziri Mkuu, Mkuu wa Kigoma yupo hapa, Wakuu wa Wilaya, Kamanda Mkuu wa Mkoa wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma na IGP waweze kuliangalia jambo hili kuweza kuhakikisha kwamba tunawalinda raia wa Kigoma.

Wenye Mabilioni Uswisi(Switzerland)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Mheshimiwa Waziri Mkuu kumekuwa na taarifa ambazo zimeandikwa katika vyombo vya habari toka wiki iliyopita. Lilianza Gazeti la The East African baadaye wakaja Gazeti la The Citizen na leo nimesikia kwamba Gazeti la Mwananchi limezungumza kwamba kuna Watanzania 6 wana fedha katika akaunti kule Uswisi zaidi ya shilingi bilioni 303. India walipopata taarifa hizi kutoka Benki ya Uswisi waliwataja majina watu wote wana siasa na wafanyabiashara wenye fedha nje na fedh zile zikachunguzwa zile ambazo zimepatikana kwa haramu zikarejeshwa India. Nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu uagize TAKUKURU na vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama kwanza tutambue ni Watanzania gani hawa na fedha hizi zimepatikana kwa njia zipi na zile ambazo zimepatikana kwa njia ya wizi na ufisadi zirejeshwe nchini mara moja. Kwa sababu hatujaanza kunyonya utajiri huu wa gesi tayari kuna watu ambao wameshaanza kutajirika nao.

Tutakapoanza kunyonya hali itakuwaje? Kwa hiyo, nilikuwa naomba suala hili Serikali ilichukulie kwa uzito mkubwa ili itume salaam kwa mtu yeyote ambaye anatarajia kwamba atafaidika na utajiri wa rasilimali ya nchi kama gesi na madini na kadhalika ajue kwamba kokote atakapoficha fedha zake tutazifuata na zitarudi katika nchi hii. Nilikuwa naomba Waziri Mkuu aweze kuliangalia jambo hili kwa ukaribu sana.

Zuia Makampuni ya Kigeni kwenye Ulinzi

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu hivi sasa Kiongozi wa Upinzania amezungumza jana kuna meli ziko Pwani ya Mkoa wa Pwani, Lindi na Mtwara zinatafuta mafuta. Mheshimiwa Waziri Mkuu hakuna kampuni hata moja ya mafuta inayonunua hata mchicha kutoka Tanzania. Meli zote ambazo ziko Bandari Mtwara zinakwenda kupeleka huduma kwenye maeneo ambayo yanatafuta mafuta yanapata mchele, nyanya, vitunguu, mchicha, mafuta ya kula na kadhalika kutokea Kenya kwa sababu hatujaweka utaratibu wa kufanya nchi yetu iweze kufaidika na utaraji huu mwanzoni. Kwa sababu hatua hizi za mwanzoni hakuna kodi ambayo tunapata kwa sababu mafuta bado yanatafutwa.

Hatua hizi za mwanzoni tunatakiwa tufaidike na fedha inayokuja, watu waweze kutumia fedha za kutoka ndani. Lakini hali ilivyo hivi sasa ni kwamba makampuni ya mafuta yanatumia zaidi ya dola milioni 161 kwa ajili ya shughuli za ulinzi na makampuni yanayolinda, ni makampuni ya nje. Yanabeba silaha kubwa kubwa, siku yakiamua kutugeuka na Navy yetu ilivyo tutapata shida. Nilikuwa naomba tutenge resources za kutosha na hata kama hatujaziweka kwenye bajeti sasa hivi, tuangalie, tuimarishe Navy na tupige marufuku, tuandike sheria kabisa kwamba itakuwa ni marufuku kwa raia yeyote wa kigeni kubeba silaha zozote kubwa ili kuweza kuhakikisha kwamba ulinzi ama unafanywa na watu wa ndani au unafanywa na Navy yetu tuweze kulinda mipaka yetu vizuri.

Utafutaji Mafuta Zanzibar Uendelee

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili kuna suala ambalo halijaisha na Kiongozi wa Upinzani Bungeni jana amelizungumzia la mafuta na gesi katika masuala ya muungano. Nilikuwa naomba jambo hili tulimalize kwa haraka. tulimalize kwa haraka na mimi sioni ubaya kwa kweli, sioni ubaya hata kidogo kama tukiamua kwamba shughuli zote commercial not upstream, sio masuala ya regulation, sio masuala ya vibali, sio masuala ya kutoa leseni, masuala yote commercial yanayohusiana na mafuta na gesi, kila upande wa muungano ushughulike na masuala yake.

Hakuna sababu ya kunga’gania jambo hili kama sisi tuna dhahabu, tuna tanzanite, tuna madini hayapo sehemu ya muungano, kwa nini mafuta na gesi yawe sehemu ya muungano? Hili ni jambo ambalo tulimalize, liishe tuimalize hii kero, vikao na vikao havitasaidia, tuimalize hii kero, tu-move forward watu wa Zanzibar waanze utaratibu wao wa kufanya utafutaji wao, waangalie kama watayapata hayo mafuta au hawatayapata, sisi tayari huku Bara tumeshapata, tuna matrilioni ya gesi, basin a wenyewe tuwaache waendelee na utaratibu wao. Hakuna sababu ya kuchelewesha jambo hili tuweze kulimaliza mapema.

TZS 40 Bilioni kwa Kiwira

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni suala la Kiwira na baadae nitakuwa na mazungumzo na baadhi ya Mawaziri kuhusiana na suala hili tuliangalie kwa makini. Tumetenga shilingi bilioni 40 kwenye fedha ya maendeleo Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya nini? Kuna fedha ambayo tunaenda kuwalipa watu ambao wameuharibu mgodi. Kwa nini tulipe watu ambao wameuharibu mgodi?

Lakini tunaenda kulipa bilioni 40 sio kwa Kiwira nzima..

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

******

Related Story in THE Citizen(Wednesday, 27 June 2012):  Zitto wants Swiss bank accounts investigated probed

18 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. hoja zote zina mashiko.issue ni utendaji wa kazi.

  todo

  June 27, 2012 at 10:31 AM

 2. YES KAKA, BIG UP, MAONI YAKO BUNGENI YALIKUWA DSAFI,MM MKAZ WA ARUSHA NILIYASIKILIZA LIVE, BIG UP KAKA TUNAKUTEGEMEA UKUZE CHAMA HIKI.

  Elineema

  June 27, 2012 at 10:37 AM

 3. Nimependa maoni yako mheshimiwa Zitto, unaongea ukweli mtupu.

  Aloys Makunja

  June 27, 2012 at 10:53 AM

 4. At least hilo linaongelewa bungeni sasa. Mh. Zitto, Kigoma inakutegemea. Tumeonewa vya kutosha. Mimi nina marafiki wanyakyusa ambao shangazi zao na baba zao wadogo ni wamalawi 100% lakini wao ni watanzania. Wengine ni wazambia kabisa. Mbona hatusikii wakikamatwa? Uonevu Kigoma ukomeshwe mara moja!

  Eresh

  June 27, 2012 at 11:11 AM

 5. Kaka nashukuru kwa kuonyesha angalau mwanga wa kutaka kutoka hapa tulipo japo nikusisitizie tu kuwa si njia rahisi kutoka hapa kutokana na baadhi ya watendajoi wetu kw maana ya viongozi kutokuwa tayari kutoka hapa na hii inatokana na mazoea waliyokwisha jiwekea kwa maana ya kutokuwa tayari kuwajibika,
  lkn pili naungana na ww kuhusiana na isue ya mafuta zanzibar,binafsi sioni haja ya kung’ang’ania yawe shm ya muungano hili hali haya yaliyopo dar si shm ya muungano
  mwisho nikutie moyo tu na kukumbusha kuwa mara chache sana mpigania haki hufaidi matunda ya kile alichokipigania ila thaman yake haitahaulika kwa vizazi vijavyo kamwe.so fanya hivyo kwa ajili yua kizazi kijacho.

  Sam senior

  June 27, 2012 at 11:19 AM

 6. Ikumbukwe miaka michache iliyopita wanachi wa kigoma kwa sababu ya manyanyaso kama haya, kutopewa huduma muhimu ambazo ni stahili yao, kudharauliwa na mambo mengine yenye maudhi. WALIFIKA HATUA YA KUOMBA KUWA JAMHURI HURU NA NAKUMBUKA VIONGOZI WA VYAMA VINGI WALISHIRIKI KTK MAANDAMANO HAYO AKIWEMO WA CCM MR MAYONGA ALIYEWAHI KUWA MBUNGE WA JIMBO ANALOONGOZA KABWE. TATIZO HILI LA WANA KIGOMA KUNYANYASWA NI KUBWA SANA. WATU WOTE WALIOJITENGA WALIANZA TARATIBU NA KWA MANYANYASO KAMA HAYO, SOUTH SUDAN WAMENYANYASWA NA WAKAOMBA KUJITENGA. SERIKALI KAMA HAITALIVALIA NJUGA BAADAYE INAWEZA KUJIKUTA INATUMIA NGUVU NYINGI SANA KULINDA MUUNGANO ULIODUMU KWA MUDA MUREFU SASA. leo tunao wamasai ambao wamewahi kuwa mawaziri wakuu lakini masai yupo kenya na tz, wakurya na wajaruo wapo kenya na Tz lakini wao eti ni raia ila mtu wa kigoma si raia. Seriklali ispuuze maandamano yale ambayo watu waliwahi kuomba kujitenga, iwape haki yao wanakigoma, isiwanyanyase, na wapewe huduma za jamii sawa na mikoa mingine.

  silas

  June 27, 2012 at 11:21 AM

  • Kaka nimefurahi sana. Naomba tuungane mkono ili Kigoma iendelee. Mimi nilikataa kuishi Kigoma kutokana na utovu wa nidhamu na elimu ndogo ya maafisa wa Idara ya Uhamiaji na leo niko Mwanza. Shida ilikuwa kuongea lugha ya Kifaransa. Nikawaelewesha kwamba Babangu ni Mfipa na Mamangu ni Mmanyema(Mbembe). Lakini at the age of of 3 years, wazazi wangu walitengana. Mimi nikarudi na Mama Kigoma na kwa vile ni Mwanamke baada ya miezi mitatu akaolewa Burundi. Nikaishi huko na kusoma hadi nikafadhiliwa na Father white kwenda chuo kikuu Lubumbashi/DRC. Wakati Mama alipofariki nikiwa Mwaka wangu wa Mwisho chuo kikuu kule DRC nikakosa mwelekeo na pia nafasi ya kufahamiana na watu wa ukoo wangu. Bad was my mother hakupendelea sana niwe karibu na Baba.
   Sasa Ndugu yangu, Form IV ambaye hata akihojiwa na yeye anakigugumizi kujieleza, lakini akivaa uniform za Migration na kutumwa Kigoma kazi yake ni kutengeneza hela kwa kigezo cha kudai kila mtu ni Mkongomani au Mrundi au Mnyarwanda. Hivi Mwanza sio Tanzania? I have investment in Mwanza my friend lakini nalia kila siku ndugu zetu wanavyoteseka kwenye umachinga. Kigoma imekuwa kana kwamba si Tanzania wala haina wazawa? Let us pray for Zitto please!

   William

   June 28, 2012 at 12:41 AM

 7. Bip up bro!TZ ni ye2 sote!!!

  Emmanuel moshi

  June 27, 2012 at 11:26 AM

  • ASANTE ZITTO GOOD COMMENT TATIZO LA SERIKALI HII NI DHARAU NO ACTION WILL BE TAKEN.LAZIMA TUTAFUTE SURUHU KWA MAMBO YA MSINGI AMBAYO SERIKALI HAITAKI KUSIKILIZA USHAURI NA KUCHUKUA HATUA.VIVA ZITTO TOGETHER WE ARE.WE WONT LET YOU DOWN

   John Ntungumburane

   June 27, 2012 at 12:49 PM

 8. Watanzania bado hawana elimu ya uraia, naomba nieleze kwamba kabila, utaifa navitu vyanamna hiyo (social construct) mtu ana vikuta dunian. Lakini pindi vikichukuliwa kama utambulisho wa ubaguzi ni tishio la maisha kwa mtenda na mtendewa na mifano iko wazi dunia nzima. Sasa kwa nini KIGOMA, KAGERA yanakuwa meneo ya mistrust of citizenship in Tanzania. Basi kama hizo wizara hazijui psyco-social dangers they are creating today let them contact us. Tunaufahamu kuhusu hayo mambo nakama wanaufahamu pia basi watende kuzingatia maadali muhimu.

  AUDAX MUPERASOKA

  June 27, 2012 at 1:01 PM

  • LET US LIVE AS REFUGEES IN OUR COUNTRY. NDUGU ZANGU WAMANYEMA(WABEMBE)NA WAHA, NARUDIA KUSEMA KWAMBA TUMUOMBEE MHESHIMIWA ZITTO. MACHOZI YANANITOKA NINAPOANDIKA COMMENTS HII. PROJECTS NYINGI ZIPO MFUKONI ZA KUINUA KIGOMA LAKINI WENZETU AMBAO LABDA WALIKUWA NA MUNGU PAMOJA NA AKAWAAMBIA WAO NDIO WATANZANIA DARAJA LA KWANZA WANUFAIKE KATIKA KIGEZO HICHO. MUNGU AWABARIKI. NAWAKUMBUSHA WAJOMBA ZANGU WANAKIGOMA MAMANGU NI MTOTO WENU. ENZI BUKOBA ILINIACHA YATIMA, SIFAHAMU NDUGU ZANGU NA SINA WAZAZI LAKINI KILA MWENYE UCHUNGU NA KIGOMA NI BABANGU, MAMANGU, DADANGU, KAKANGU AU MDOGO WANGU.
   NAOMBA MESIMWA ZITTO AJARIB HATA KUJA MWANZA SPECIALLY KUSHUHUDIA UHURU TULIONAO NA HESHIMA TUNAYOPEWA KAMA WANAKIGOMA.
   MHESHIMIWA ZITTO, SI WEWE ILA NI MUNGU ALIYEKUPA UJASIRI WA KUWEKA WAZI HALI YA MANYANYASO MKOA WA KIGOMA. TUONANE KATIKA MAOMBI. NINACHUKIA SIASA ILIAKWA HOJA ZAKO ULIZOTOA, NAOMBA MUNGU AKUBARIKI.

   William ILEMBO Johnson

   June 28, 2012 at 1:06 AM

 9. big up hon.

  david

  June 27, 2012 at 3:18 PM

 10. safi sana mh zitto tutanyanyaswa hadi lini?

  lucas y gwivaha

  June 28, 2012 at 3:18 AM

 11. Yaani hata sielewi kwa nini ni KIGOMA tu,,kila sehemu unayokwenda Oh ,,we sio mTZ…Mbona wengine walioko mipakani hawaitwi hivyoo,,,halafu hawashituka sasa hivi Kg kila ki2 tunacho km book sana tu hadi secta zote,,,KAMANDA tuko sambamba…

  SADOCK

  June 28, 2012 at 5:38 PM

 12. unajua nini mh.kabwe, hii nchi ni ya watu watu wachache, na kama ni ya wachache basi wanajiamulia wenyewe wanavyotaka, wanafaidika na resources zetu za nchi hii, inasikitisha sana muheshimiwa, naongea kama mtanzania ambaye ninauchungu wa nchi hii, ajira kwa vijana iko wapi! Yaani ni uzembe mtupu unaofanywa na viongozi wetu, sisi wenyewe tunateseka wao wakikaa bungeni tu bila kuchangia mada wanaingiza pesa, huu ni upumbavu kabisa, 2015 CHADEMA ni ushindi 100%,nakupongeza sana Mh. Kabwe kwa kutopokea posho yao. Mungu akuwezeshe muheshimiwa uweze kuongoza vizuri wananchi wa KIGOMA asante sana.

  Andrew Agrey

  July 5, 2012 at 1:24 PM

 13. Kaka mimi ninakukubali mimi ni mzanzibar mzee unatisha tatizo la muungano ni mgawanyo wa rasilimali nihilo ndio mgumzo kubwa kaka

  Ommy

  July 5, 2012 at 10:03 PM

 14. God Bless you Hon:Zitto Kabwe!

  Henry Robert

  April 2, 2013 at 6:25 PM

 15. Kuna mtu kama zito kabwe huyu ni mtu wa kulindwa sana kwani uhai wake una faida kwa kila mwana kigoma na watanzania wote kigoma tunaitaji watu kama hao wa kutetea na kuweka wazi mipango ya kutenga wengine na kama vp basi watupe uhuru tujitawale wenyewe uwezo wa kujiendesha tunao sana tu kaka zito

  mm kimanga

  January 12, 2014 at 2:14 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: