Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Dr. Ulimboka kutekwa, kupigwa na kuumizwa: Serikali inawajibika kutueleza

with 195 comments

Dr. Steven Ulimboka

Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI

‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous’

Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.

Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.

Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa ‘agente provocateure‘ kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.

Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.

Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all’

Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.

Written by zittokabwe

June 27, 2012 at 12:12 PM

195 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. This is unacceptable…is Tanzania another Syria??

  mawazo

  June 27, 2012 at 12:27 PM

  • Sio sahihi kuilaumu Serikali katika suala hili, najiuliza hivi kweli wale ndugu wa wagonjwa waliolazwa hospitali bila huduma yeyote, wakimkuta Ulimboka ambaye ndie kiongozi wa mgomo huo hawawezi kumshughulikia? tusiupotoshe umma naamini Mhe. hata wewe angeingia kwenye 18 zako usingemwacha, WATU WANA HASIRA KALI KWA KUPOTEZA NDUGU ZAO TOKA ULE MGOMO WA MWANZO

   Evod Kigosi

   June 27, 2012 at 1:27 PM

   • Achana na ushabiki wa kisaisa ndugu sasa hapo wa kulaumiwa nani kama si serikali? nani mwenye vyombo vya usalama wa raia? umepotoka kwa siasa zako za kiyunani..kwa hiyo kitendo alichofanyiwa Dr Ulimboka unataka kimtokee na Mh Zitto ndo ujue uzito ukowapi? Hoja nyepesi sana..labda ikutokee wewe

    evancekomu

    June 27, 2012 at 4:24 PM

   • Siku zote hawaishi watu wanjinga katika nchi yetu….SASA WEWE UNATAKA TUMLAUMU NANI WAKATI SERIKALI NDIO INATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUHAKIKISHA USALAMA WA WANANCHI WAKE SANA SANA HAO WANAHARAKATI!! PUMBAVU SANA WEWE!!

    Osama wa Kitanzania

    June 27, 2012 at 5:58 PM

   • Wewe kama umetumwa na mfumo uweke hicho unachotaka kutueleza umekwama

    Danstan

    June 27, 2012 at 6:49 PM

   • Subiri mahakama ya kadhi iundwe ndio mfanye mambo ya jino kwa jino…!! Hapa tunazungumzia haki ya kufanya kazi kwenye mazingira mazuri… madaktari watakuwa watu wa kupigwa ‘kalenda’ hadi lini?!?

    fademark

    June 27, 2012 at 7:30 PM

   • naona kama ntakutukana we mpumbavu!!wacha nikuache coz u aint a doctor afta all,mpuuzi!1

    abassi

    June 27, 2012 at 8:14 PM

   • Huu ni mgogoro wa Serikali na Madaktari ktk kudai haki zao. Anae takiwa ku Solve this situation ni Serikali na sio Mwingine. Kama unatumika ubabe kumtuliza mtu ana waongoza wenzake ktk kudai haki zao tena kumtuliza kibabe, Hii sio Demokrasia bali nji Demogasia. Kama Serikali wange Rescue situation mapema hili swala lisingefika hapa. Serikali lazima icheze sehemu yake, LAKINI KWA MANENO YA WAZIRI MKUU YA BUNGENI TAREHE 27/06/2012 , nanukuu “KAMA LIWALO NA LIWE” sasa najiuliza Huu ndio utawala bora????, “KAMA LIWALO NA LIWE” sasa najiuliza “haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania???, “KAMA LIWALO NA LIWE” sasa najiuliza Huu ndio utaratibu wa kidemokrasia wa kusolve matatizo na Madaktari???

    Ramadhan Mchatta

    June 28, 2012 at 1:45 AM

   • Sasa unataka nani alaumiwe, na nani anamakosa hapa, hapa ni uzembe mkubwa wa utawala tulionao madarakani, na kilichotokea ni matokeo ya upuuzi mkubwa wa hii serlkali, acha mambo ya siasa, Huyu daktari kaonewa sana hiyo ndio hali halisi tulionayo sasa, tena na hisi huu ni mwanzo tuu, tusipoungana kama raia wema maisha ya wasomi wengi hayatathaminiwa na hii serikali inayokumbatia wageni na kuwapa maisha bora! Lazima serilkali itoe tamko kuhusu ukweli wa hili jambo, wasisingizie raia wema kuwa ndio waliohusika!

    James

    June 28, 2012 at 1:54 AM

   • Nadhani wewe unapaswa ukapimwe akili.huo ni ushabiki wa kisiasa na inaonekana umejawa na hisia zaidi kuliko ukweli.kwa hiyo unadai ulimboka ndiye aliwaua hao nduguzo?unadhani ulimboka angewatibu bila vifaa vya kufanyia kazi?ni ulimboka ndiye anayepaswa kununua vifaa hivyo au serikali yako?kama huna point kaa kimya au kahadithie hadithi za cartoon.

    katyega

    June 28, 2012 at 10:40 AM

   • Napata taabu sana kuelewa juu ya uwezo wa kufikili wa watanzania.siamini kama elimu ni lazima iwe darasani tu.kumbe kuna watu hata leo wanadhani doctor ulimboka angewatibu raia hata bila vifaa anavyodai serikali impe ili afanye kazi yake kwa ufasaha?si kazi ya ulimboka kununua vifaa hivyo bali serikali.wagonjwa tunawaua sisi wenyewe kwa kuendelea kufumbia macho madai halali na ya kimsingi ya madaktari.mbona madiwani wameongezewa posho toka laki moja na zaidi hadi laki 2 na zaidi.kuna madiwani wngapi nchini?serikali inakila sababu ya kulaumiwa kwa uzembe huu.
    huna point za kuchangia bora utulie.

    mortone

    June 28, 2012 at 11:04 AM

   • wewe hasa ndio hoja yako nyepesi saaana hivi kuna wangapi yamewatokea mambo ya kisasi na kwa sababu ya kukosekana umaarufu yanaishia chini chini,huyu amepigwa na watu na nakueleza bado mengi yatatokea kwani watu wana hasira na kupotelewa ndugu zao,yaani wao waue sawa na yeye kupewa kichapo imekuwa nongwa hapana jipya uloliongea wewe ndio has umeandika kisiasa

    augustino

    June 28, 2012 at 1:24 PM

   • Tunajua katikai ya Mgomo wa Madaktari Watu wanafariki, hata bila mgomo watu wataendelea kufa, hata mie naweza kufa na wewe pia. Watu wanakufa hata kama Madaktari wapo kazini kwa jaili ya kukosekana madawa, madawa na vifaa feki, kwa udharimu uliokisiri wa serikali za ccm. Tuwe wepesi wa kufikiri, kweli inasikitisha kuhalalisha uhuni huu kwani kwa sababu za kipuuzi kama hizi. Ni watu wangapi wanakufa kwa sababu serikali inafuja pesa na kuwafanya wakose huduma za jamii? Madaktari wanafanya mgomo wa wazi na wanahukumiwa kwayo japo na wajinga wachache. Lakini uhuni huu, mauwaji, kutishana, na serikali kama hivi sio vitu vya kutolea majibu mepesi kiasi cha fikra za huyu bwana. Wananchi kama waliona wafwa walipaswa kuungana na Madaktari sio kuwalaumu kwani hawaoni kuwa madaktari wanaonewa na katika hili wanawapigania wananchi? wakubwa wanatibiwa nje hata kwa mafua we mjinga huoni hili? Tunalo janga la kitaifa kwa jinsi na namna watanzania wanavyoona mambo! Yupo mwanafalsafa mmoja ambae aliwahi kusema jamii itaendelea kuuana wenyewe kwa wenyewe…. mpaka pale watapopata ufahamu wa kumtambua adui wao wakamgeukia na kumuangamiza!!! Evod elimika!!!!!! Unasikitisha

    Lourance Njopilai David Mapunda

    June 28, 2012 at 2:20 PM

   • Uko sawa Kigosi, waache hao na siasa zao za kuuona utu wa Dr Ulimboka tu, ila wale wanaotaabika kwa kukosa matibabu bila hatia wanawaona si lolote!!

    Moh'd

    June 28, 2012 at 6:31 PM

   • Nafikiri wewe si mwanaharakati hata kidogo kwani usingedhubutu kusema maneno kama hayo.Je ulishawahi kusikia mtu akikuletea haki yako bila ya wewe kuitafuta wewe mwenyewe?Nafikiri huna historia ya kutosha ndo maana ukakurupuka kusema hizo pumba

    OMBENI IKOLA

    June 29, 2012 at 9:40 AM

   • Wewe kaka umejitakia2, ujue unavotoa comments kwenye issue senstivitve km hiz u need to be a multidimensinal thinker kama hukujaliwa kuwa critical thinker.. hata mim nilijua hawa mabwana wanachodai ni posho tu kumbe its a chain of problems ndomana hata yule anayejiita mtoto wa mkulima, alisema baadhi ya mambo tumeyaweka sawa.. just imagine hapa alikuwa anafichaficha nini..! ujue mficha maradhi kifo lazma kimtendee haki..! haya, je ile kauli ya LIWALO NA LIWE yeye kama kiongoz wa serikali bungen ilimaanisha nin.? ni mtu mzima yule ile kauli sidhan kama alikurupuka tu na kuiropoka kwa bahat mbaya.. inaonekana tayar kama kamati (wthn a system) ilishakaaa.. sema yey tu alijisahau akaropka..(nafikir hivyo..) kwa nin soo after yanatokea haya.. kwa mtu anayetumia LOGIC sio lazime ziwe zile za Pure Maths.. ni lazima tu ataconclude hivyo.. ukumbuke Mbunge wa Vunjo anayajua sana haya mambo.. aliwah kugomea mic bungeni..alafu ujue wanaoathirika hasa ni wale low income earners ambao sanasana watasema tu “Bwana alitoa na Bwana ametwaa” wakifiwa na wapendwa wao.. wakifika mbali zaid ya hapo nikuilaum serikali.. wakufanya tukio kama hili sio makabwela kama wewe mnaotegemea panadol za govnment hospital.. sory km ntakukwaza.. NI UHURU TU WA MAONI KAMA MIMI.! ila lakn maDR. kale kafigure ka Posho naona kama hamkuwa realistic vile.! anyway GET WELL SOON DR. ULIMBOKA.!

    Mtoto wa Mwalim

    July 1, 2012 at 5:28 AM

   • We kigosi unaonekana hujielewi kabisa,au ndo nyie?wanachodai madaktar n sahihi..mbona wabunge wanajptshia mahela yao bila hata kpngamiz,wao wamesomea nin hasa na miaka mingap na kwa ugumu gan had wajilipe millions???wamekaa tu pale hata hayaumiz kichwa,yanacnzia hovyo tu..MUNGU YUPO NA ATATENDA,WOTE WALIOSHIRIKI KUTENGENEZA MPANGO MZMA WATAUMBUKA.

    C

    July 3, 2012 at 10:11 AM

  • Najiuliza: Kila anayekerwa na Mafisadi akiamua kuchukua sheria mkononi nchi itakuwaje? Mkianguka ghafla huko Bungeni mtakwenda wapi i.e kabla ya kupanda hizo ndege zenu kwenda India, SA, UK????

   Lilian

   June 27, 2012 at 2:32 PM

   • unaakili mkuu

    mortone

    June 28, 2012 at 11:05 AM

  • Daahh. huu ni unyama wa hali ya juu lazima serikali iwajibike, hata katka nomarmal situation mtu akiumizwa wa kwanza kukamatwa ni yule aliyekuwa na ugonvi nae so kwa hili swala ni lazima serikali iwe answerable, inauma ctaki kuamini kama vtendo hvi vya kinyama vyaweza kutokea Tz

   Happy

   June 27, 2012 at 4:29 PM

  • FOOL HUJUI UNACHOKISEMA

   MAPPY

   June 27, 2012 at 4:58 PM

  • Jamii lazima itambue kuwa madaktari hawadai maslahi yao tu bali pia maslahi ya afya ya watanzania wasioweza kwenda kutibiwa nje.Tusiishabikie serikali ya aina yoyote ile ambayo inaonesha wazi kutokuguswa na hali hii.nasema hivi kama mtanzania mwenye uchungu na nchi hii inayoangamia kila kukicha kwa sababu ya upuuzi wa watu wachache.Leo mmempiga Mtaalamu kama huyu kesho mimi kabwela mtaniacha salaama?ukweli lazima ujulikane tu.haiwezekani watu wajichukulie sheria mkononi na kuangamiza roho za watanzania.mmempiga doctor huyu leo sasa subiri tuone nani atawatibu watanzania ambao wangetibiwa naye.
   Zitto nakuheshimu sana.pia wewe ni mmoja wa wale ambao hula kura zangu kila uchaguzi,fuatilieni hadi ieleweke.

   katyega

   June 28, 2012 at 10:32 AM

  • Dear Tanzanian Doctors

   As much as we are all aware of the miserable and pitiful state of affairs that is your working environment and compensation I still feel that it is my duty as a citizen to let you know that what you are doing by striking is wrong both from the point of your hypocratic oath as well as from a moral point of view. you all have a a unique and very important role to play in society as the care takers of the nation’s collective health you also need to bear in mind that most of your patients are the poor and underpriviledged who stuggle éveryday just to put food on the table and are unable to afford private healthcare services. In as much as we understand that the government’s lack of concern for your plight has led you to believe that the only way to get your due is by striking I must ask you to consider the consequences of your actions for the real victims who will pay the price for your actions are the poor who have nothing to do with your plight and are by far the most prone to potentially fatal but treatable diseases. Even if the government were to finally address all your demands it is not worth the loss of a single life that could have been saved but wasnt as a result of the course of action you have taken. the course of action you have chosen will not buy you favour with the general public in the long run as more and more people suffer and die as a result of your actions…while it is hard I implore you all to return to your work stations and keep fighting and making your demands known to the public and the government this will demonstrate to the general public (whose tax shillings put most of you through medical school) that you genuinly care for those you have sworn to treat and will make them your advocates in your struggle to get what you deserve. but if you continue down the path you have chosen you will soon find the sympathy that you now enjoy turn to hostile rage and contempt for your entire profession which may take a long time to repair.
   every one is entitled to decent working conditions and fair pay for an honest days work…but it is also important to go about getting what you deserve in a manner that does not make collateral damage of innocent people.
   Sincerley
   A concerned citizen!

   • There you are brother Eric!!! The problem with our exparties of now is, they are the same time politicians who are ready to risk the lives of wananchi for political gains. We are so unfortunate!!

    Moh'd

    June 29, 2012 at 7:46 AM

   • Duuuu kaka Eric wew kwa comments ni noma.! yaani aka kaparagraph ungekatafutia lugha sahihi(according to mrisho Mpoto… fikra sahih huja kwa lugha sahih.. though its still debatable to which is the right language then..) i think your remarks could be enough to finalize the whole discussion.. coz the reality will still remain that due to potentiality of this proffession.. the government incurs a very high costs to prepare these Health Engineers… and the source of income is mainly through the taxes that are paid either directly or indirectly by these dying people at the hospitals.. it could be better for them to think on other side in hummanitarian way..! Sawa kazi yenu ni ngumu kila mtu anajua kwamba kuanzia kusomea mpaka mtu anapoingia kazini…., eeeehh.. thats the reality.. si ndomana mko wachache.. afazali cku hz vilivokuja na hiv vya private ndio nasikia mnagraduate kama 700 kwa mwaka, wakat kwa cozi nyingine ni kama 0.0003 ya ya graduands.. eeehe kwani teachers, accountants, lawyers, hali ikoje? nani asiyejua kuwa nyie ni wachache sana n sometimes mnalazimika kuwawaacha wake zenu usiku wa manane peke yao home kwenda kuattend emmergency cases hospitali.. lakini si ndio alichokisema kaka Eric kuwa mlishakula viapo as what the soldiers do… kinachobakia apo ni kuingia vitani tu.. haya mengine si yanasovika tu ndani ya safari..! kwani mwanao akikudai ada ya shule utamlipa hapohapo.. si utakaa ujipange kwanza.. nyie mngeipa serikali atleast enough time(atleast for even a year..!) to set the budget according to ur complaints.. wakat na nyie mkiangalia hali halisi ya kiuchumi ambayo ni results ya hiz sera zetu mbovu zinazotucost..! MAONI YANGU NI HAYO TU JAMANI.. MADR. NUSURUNI TAIFA BWANA.. TUTAONGEA MENGI NA BLABLAA ZA KILA AINA NA KILA MTU ATAKUJA KWA MBWEMBWE ZAKE NYIIINGI TALKING THE SAME THING.. WAKATI SERIKALI YENYEW BADO NI HII HII… WHAT WILL BE THE CONCLUSION THEN..!

    Mtoto wa Mwalim

    July 2, 2012 at 12:01 PM

 2. Nahisi hata hao madaktari wenzake ambao wanamtibu inabidi wachunguzwe kwa makini katika wakati kama huu sababu hofu yangu ni kwamba isije kuwa tayari system ishaandaa Dokta feki ili akammalizie pale pale kitandani ama apigwe slow poison ya kuharibu kila system nzima ya mwili wake..

  Likati Thomas

  June 27, 2012 at 12:29 PM

 3. Ni kweli kabsa hata mimi naunga mkono hoja hii kwa kua haiwezekani kitendo kama hicho kitokee ktk kipindi hiki cha mgomo. Serikali ieleze kwa kina kuhusiana na suala hilo

  Cesar

  June 27, 2012 at 12:31 PM

 4. Nimesoma kwa makini na kuelewa nilikua nakuandika lakini naona wewe upo updated zaidi.Maswali ni mengi kuliko tunavyoweza kuichukulia Mh. Tujiulize prime minister alikua anamaanisha nini kwenye kujibu mwongozo wa Mh. ZAMBI leo asubuhi?

  Rohan Sandagila

  June 27, 2012 at 12:35 PM

 5. naomba serikali itoe tamko kwa hili tuache siasa kwenye masuala ya msingi

  PASKAL

  June 27, 2012 at 12:35 PM

 6. Hii ni hatari kubwa sana…! Kama ndiyo hivyo, tuanzishe mgomo na maandamano nchi nzima….!

  Apen

  June 27, 2012 at 12:35 PM

 7. Hakika nimesikitishwasana kukitendohicho chakinyama,nawaomba viongozi wanaojua wajibuwao katika kumtetea mwanamchi na kulitumikia taifalake asilifumbie macho sualahili,ninamini hizininjama binafsi zakuta kuwafanya wanamnchi wasiweze kutetea hakizao zamsingi ilakamwe hamtoweza kwani watanzania waleo siowale waenzizile na mkaemkijua lenyemwanzo halikosikuwa namwisho Mungu yuko hamtupi mjawake.

  leonard shaban

  June 27, 2012 at 12:35 PM

 8. Sasa tunakoenda ni kubaya kabisa, limetokea hili muda mbaya maana baadhi yetu hatutaacha kuhisi ni vitisho vya Serikali yetu.
  Wanadhani hii itasaidia? Kama wamehusika kwa namna yoyote wajue suala la namna hii huwa halinyamazishi, ila litaibua mengine, wakumbuke nchi zenye mapinduzi walianza hivi hivi watu wakaamua kuanza kukatana masikio.
  Watanzania si wajinga hata kidogo, tuna mantain amani na tunaamini bado kuna uwezekano wa kupata haki zetu.
  HUU SI MUDA WA KUNYAMAZISHANA, wacha watu wadai haki zao, si mnapamba masikioni? Imekuaje kwa hili?

  Zahira

  June 27, 2012 at 12:35 PM

 9. Inatisha! Tumefika huku?

  Bob

  June 27, 2012 at 12:36 PM

 10. Hapana hatujafika huko uchunguz ufanyike haraka….. Kutatua matatizo kwa style ya namna hiyo hapana tunaiomba serikali ifanyie kazi haraka saana uchunguzi wa kuumizwa kwa Dr. Ulimboka

  Edward Jidamva

  June 27, 2012 at 12:36 PM

  • unataka serikali ijifanyie uchunguzi yenyewe? hapo serikali inahusika moja kwa moja hakuna mjadala zaidi. this is not fair.

   BEST NGAO

   June 27, 2012 at 7:36 PM

  • Edward, sasa si wakati wa kurushiana maneno na kupoteza muda. Binafsi nawasihi wataalamu wenzangu kuwa serious na mambo haya na kufikilia mpango wa muda mrefu jinsi ya kutatua matatizo yetu wenyewe kupitia vyama vyetu vya wafanyakazi vyote nchini. Si jambo la busara kuiomba serikali kufanya uchunguzi dhidi ya kiongozi wa madakitari kwani tayari wana mgogoro nao. Mapendekezo yangu: Mosi. Immediate plan ni kwa vyama vya wafanyakazi kuziomba nchi wahisani kuleta wataalamu wachunguzi kuchunguza swala hili la Dr. Ulimboka na matokeo yatakuwa valid. Pili. Long term plan ni kwa vyama vyote vya wafanyakazi kwa umoja wao kuungana na ku-train wataalamu wa kuchunguza mambo kama haya na inapotokea ni kiasi tu cha kufanya uchunguzi sisi wenyewe na kupata valid and reliable information. Naomba jambo hili liwe fundisho kwa vyama vya wafanyakazi kujipanga kuwatetea na kuwalinda wanachama wake. Mwisho namuombea Dr. Ulimboka apone haraka na kuendeleza ndoto zake, AMINA.

   zittokabwe

   June 28, 2012 at 10:14 AM

 11. This is realy disappointing and shocking! Our future is uncertain if this the trend!

  Lekumok

  June 27, 2012 at 12:37 PM

 12. Kwa kwel ni hatar na serikal lazima ieleze umma wa watanzania nin kimetokea tena wakat wazir mkuu kesho anataka kutoa tamko kuhusu mgomo au………………….

  Nacbu

  June 27, 2012 at 12:42 PM

 13. Kwa hakika ni habari za ajabu na za kusikitisha sana kutokea kwa kiongozi wa wataalam wetu wa afya! Hii ndio “provocation” halisi kwa madaktari wote nchini! Naamini kwamba hao walofananya kitendo hicho ni wawakilishi wa taasisi fulani inayopingana na madai ya madaktari hao. Huo sio utaratibu wenye maana yeyote katika ki[indi hiki cha mgogoro, bali ni ujinga na ukosefu wa hoja katika kuelekea kutatua mgogoro huo. Kama mwananchi; naitaka serikali yangu ikomeshe hali hii mara moja la sivyo italeta vinyongo na chuki zitakazo ibomoa jamii nzima siku za karibuni.

  Kalasinga

  June 27, 2012 at 12:42 PM

 14. Dah …huu ni uhuni serekali lazima iwajibike juu ya hili ….na sisi wananchi lazima tuamke …

  Ibra

  June 27, 2012 at 12:48 PM

 15. Serkari yetu ni ya kibepari nafiki huyu kikwete kweli dhaifu pamoja na serkali yake mambo hayo ya udhaifu yanazidi kudhiilika sasaiv ila hawajui kwamba siku wanchi watapo choshwa na uchafu wanaoufanya hata s
  jui watakimbilia wapi

  phinias robart

  June 27, 2012 at 12:49 PM

  • wewe phinias ndo mwenye mawazo dhaifu, unadhani kikwete ni mpuuzi kama wewe… ipi cku utatafuta rais kama huyu hutompata… fikiria kabla hujaandika utumbo wako hapa we mpumbavu!

   Hola Kipapa

   June 28, 2012 at 3:13 PM

 16. maskini ! so sad binadamu wabaya but walofanya hivyo wakae na kujua damu ya mtu haiendi bure

  Mummie Ksummer

  June 27, 2012 at 12:51 PM

  • Kiundwe chombo huru kuchunguza hili suala la Dr. Ulimboka, ni ukweli uliowazi serikali inahuka.Swali je watawamaliza wotee? very sad

   Chado

   June 27, 2012 at 1:01 PM

 17. Real it is SAD, VERY SAD………

  Kweka

  June 27, 2012 at 12:59 PM

 18. napata tabu kuzungumza juu ya kilicho tokea lakini si njia sahihi ya kutatua migogoro katika taifa letu tunao jiita lenye amani lakini MUDA UTAZUNGUMZA TU.

  MTANZANIA MZALENDO

  June 27, 2012 at 12:59 PM

 19. Ni kweli tukio la kuhuzunisha saana hili! Jamani tusifike hapo ndg watanzania haileti maana kumdhuru Daktari wetu ambaye Leo mnafanyia unyama kama huu lakini kesho unaumwa wewe au mmoja wa familia yako na yeye ndio anaokoa maisha yako au ya mgonjwa wako! Wacheni mgomo ushughulikiwe kimgomo mgomo na si kufanya mambo kama haya!

  Merinah Mneo

  June 27, 2012 at 1:01 PM

 20. Tuache siasa kwenye mambo ya msingi hapa lazima serikali uhusike kwa namna moja au nyingine.

  Allan Shemahimbo

  June 27, 2012 at 1:04 PM

  • serikali iliangalie jambo hili kwa makini kwani ni kitendo kibaya sana itoe tamko mapewa ili wananchi wasiifikirie serikali yao vibaya juu ya hali hii

   mwanae

   June 27, 2012 at 7:35 PM

 21. Mimi naishangaa huu utawala na Serikali yetu…inaone kana kunasectar wana haki ya kudai haki zao nawengine awanaa haki..wabunge wakilalamika kidogo tuu wanasikilizwa..lakini walimu walikuwa wanadai haki yao awajasikilizwa mmbaka Rais kaingilia…Lazima Serikali iwajibike kwaili na inapendeza iyo kesho Waziri mkuu atuambie kwanini ili limetokea na mngongoro utaisha lini

  Jafari Mindu

  June 27, 2012 at 1:04 PM

  • Serikari haitowasikiliza wanainchi wake kwa sababu tupo tuu kama wajinga, imeshazoea tunaongea na hatuwajibiki, Imeshazoea kutudanganya watanzania maneno mengii kuanzia raisi wake mpaka raia wake utekelezaji mbovu. Its in our blood. Congo burundi, Kenya na Rwanda vitu kama hivi ni kawaida sanaa sasa je serikali itaruhusu vipi hivi vitu viingie tanzania, kama waliofanya hivi wataachiwa basi wengine nao wataiga.

   Flora

   June 27, 2012 at 1:38 PM

  • Kwa kweli kuna kila sababu ya kulifuatilia suala hili kwa undani hadi ukweli ubainike. Haiwezekani litokee swala zito kiasi hiki tena kwa kipindi ambacho serikali haiko sawa na watu wake. Hizi ni njama za serikali kuzima moto uliowashwa na madaktar dhidi yao. Na pia tutaomba serikali itueleze kwa kina kama uchunguzi ukufanyika na kubaini kuwa inahusika kwamba kama hizi ndo njia za kutatua migogoro kati yao na jamii au la! Inasikitisha sana, inahuzunisha sana na pia inakatisha tamaa kuona watanzania wenzetu wakuimizwa na kuteswa sababu tu ya kudai kilicho chao. Mimi na watanzania wenzangu tunaendelea kumuombea kwa Mungu ili apone mapema na arudi kwenye harakati za kudai haki si kwake tu na pia kwa madaktari wengine.

   Gaudence Mtui

   June 27, 2012 at 3:29 PM

 22. dah! Kweli hii ndo Tz ye2 polen familia ya Dr. Ulimboka na wote waloguswa na hl jambo la kusikitisha hv ni kweli kwamba viongoz wa serikali ye2 tukufu wameshindwa kutatu matatizo ya watanzania kwa njia ya democrasia wameamua kutumia udictata wanaharati wa kutetea haki za binadam wko wap jaman.

  August Kiria

  June 27, 2012 at 1:06 PM

 23. Natafuta haki yangu,kwa mtu ninaye mjua na kwa wakati huohuo nitekwe wakati naitafuta kaki yangu, je ni mshutumu nani zaid ya Mdeni wangu?? Serikali itupe ukweli wa jambo hili…

  Watson Mwanku

  June 27, 2012 at 1:13 PM

 24. Hakika tunakoelekea ni kubaya sana, haya mambo yalikuwepo toka utawala wa Nyerere na kwa kuwa watanzania walikuwa hawana uwezo wa kuhoji watawala wameendelea kujidai kuwa nchi nyetu ni ya amani na utulivu kitu ambacho siyo kweli bali woga wa watanzania. Kwa karne hii hawataweza kuwafunga watu kutetea haki zao kwa kutumia njia hii kwani mtanzania wa leo siyo wa kipindi cha Nyerere. Naomba tuungane katika kulikomesha hili ikiwezekana viogozi wetu akina zitto na wengine watuongoze kufanya maandamano nchi nzima ili serikali itambue kuwa tumechukizwa sana na uonevu huu…..SOLIDARITY 4REVER.

  Ndagije Chobaliko

  June 27, 2012 at 1:16 PM

 25. Duups very sad news

  salma

  June 27, 2012 at 1:17 PM

 26. kwa namna yoyote si jambo linalotoa picha nzuri, ni lazima serikali waeleze vizuri jambo hili!

  criss

  June 27, 2012 at 1:18 PM

 27. “Siku zote ng’ombe haoni umuhimu wa mkia wake mpaka pale unapokatika” Hii Serikali (ng’ombe) inatia Kichefuchefu kabisa. Haiingii akilini kumfanyia kitendo kibaya na cha kikatili Dr. Ulimboka! Mweusi amekosa nini kuteswa na kunyanyaswa katika ardhi yake?

  Mapogo, AD

  June 27, 2012 at 1:26 PM

 28. nimesoma vizur hyo habari na kuilewa kiongoz “ninaomba huyo mwakilish uliyem2ma a2saidie kufatilia kwa umakim na mwisho mungu awasaidie na kufanya kazi kwa usawa.

  Alistides anacleth

  June 27, 2012 at 1:27 PM

 29. Inabidi madaktari wajitahidi kumpa huduma kwa haraka ili kurejesha hali yake ya uzima na vilevile serikali ifuatilie ni nani amehusika na ukatili huo na sheria ichukue mkondo wake

  Ibin nassor

  June 27, 2012 at 1:37 PM

 30. Inasikitisha zaidi ya maelezo.

  AUDAX MUPERASOKA

  June 27, 2012 at 1:37 PM

 31. serikali lazima itakuwa ina husika kutekwa kwa dr uli,mungu atamjalia afya njema soon

  sam kaliro

  June 27, 2012 at 1:41 PM

 32. Inauma sana kama Tanzania tumefikia huko,rakini tusishangae sana kwani daima hakuna haki kwa wanjonge katika Tanzania,kama ipo iko kwenye makaratasi na kwa wenjenazo.Shida ni kwamba watu wanafanya siasa kwenye mambo ya msingi

  Kimasa Francis

  June 27, 2012 at 1:48 PM

 33. serikar iko wap, mkomboz wetu ninan?. kama vip bas tujiongoze wenyewe! peoples power!!!!

  steven patrick

  June 27, 2012 at 1:49 PM

 34. Mungu atuhurumie sote.ila tuelekeako ni kubaya zaidi mungu amtetee Dr. ulimboka na kumponya haraka.Daima penye haki husimama na kuonekana,tuache itikadi ze2 na tuitetee nchi ye2.

  Edna crawford

  June 27, 2012 at 1:49 PM

 35. Ndugu Zitto,sisi jicho letu lipo kwako na jopo lako.Tunaomba utusaidie kupambana na serikali hii dhalimu kwa sababu wewe ushapewa mice na tayari upo jukwani.MUNGU MPONYESHE DKT WETU ULIMBOKA.

  Fumbo

  June 27, 2012 at 1:49 PM

 36. truely this is an injuary to all! Inauma sana bado serikali inawajibu wa kutekeleza madai yao, na pia kuwajibika kwa hili la daktari, na pia sasa kwa hali hii tuelimishe watanzania wenzetu kwa tanzania sio nchi ya kidemokrasia bali ni nchi ya mabavu au nilipi sahihi…?..inawezekana kufanya vyo ni kujaribu kuwafunga midomo wengine kama walimu ambao wako mbioni kugoma je ndio njia sahihi…..? Ni dhairi maana ya democratic state inapote nkuibuka dictator ship state!!

  mkilanya

  June 27, 2012 at 1:50 PM

 37. Nimeamini Tanzania hakuna amani ila kiini macho tu. Nahisi huko tunakoelekea ni kubaya na vita yaweza kutokea maana hizi dalili sio njema. Serikali haiwezi kukosa lawama katika hili. Ukiona watawala wanatumia uhuni kutatua tatizo lililopo ndio utawala wao unafika kikomo.

  Kitungamirwa

  June 27, 2012 at 2:00 PM

 38. Kiukwel hii ni nchi huru na taasis zinaohaki kueleza na kudai staiki zao

  inauma nchi yetu kufikia huko na serikari inapaswa kabisa kujibu lawama hizi nawanaohucka kuchukuliwa hatua

  Betson Brighton

  June 27, 2012 at 2:02 PM

 39. kama tumeshafika hapa sasa waziri mwenye dhama ajiuzulu na uchunguzi wa haraka ufanyike.Tanzania imekuwa nchi ya kidikteta? na ikowapi amani tunayohubiri kwamba tunayo na tunajivunia?.na hiyo kesho anayosema waziri mkuu alikuwa anasubiri hili litokee?.nimechukia sana na kama ningekuwa na dhamana ningechukua hatua kali sana tena haraka.badala ya kuzungumza na madaktari kupata suhuhisho la madai yao tunaanza mambo ya ajabu kabisa.hatuwezi kupata suluhu kwa njia hizi na udhaifu unajionesha wazi hapa.

  onari chinguile

  June 27, 2012 at 2:03 PM

 40. NIMESIKITISHWA SANA NA HII TABIA KATIKA NCHI YETU,NINGEOMBA MADAKTARI PMJ NA VIONGOZI WATETEA HAKI WASICHOKE KUFATILIA KWA KARIBU HILI SWALA..MUNGU NAOMBA UMJALIE AFYA Dr.steven NA WEWE NDIO UNAEJUA UTAWAADHIBU VP WATU KAMA HAWA WASIOPENDA KUWAONA WATETEA HAKI.

  MiddyJunior

  June 27, 2012 at 2:05 PM

 41. Ni jambo la kusikitisha sn kama hali imeanza kuwa hvyo,hata hvyo shujaa mmoja anapopata kuna mashujaa wengine wengi wanazaliwa,so mapambano yataendelea daima,ndio sababu huwa tunasema serikari inaleta siasa hata katika uhai wa watu,never heard waziri,mbunge wa chama tawala katekwa nyala,but only other political parties au watu wanaotetea maslah ya taifa!Tunaitaji mabadiliko!

  Makamba

  June 27, 2012 at 2:05 PM

 42. Serikali imefikia hatua ya kuwageuka watendaji wake wa kazi kwa sababu ya maslahi binafsi? kudai haki imekuwa ni tatizo? wapi amani mnayoitangaza kila leo. najua tutayaweza yote katika yeye atutiaye nguvu. Get Well Soon Dr Ulimboka!

  ibrahim kessy

  June 27, 2012 at 2:10 PM

 43. Ni kitendo cha kinyama na si cha kukivumilia hata kidogo kwa nchi changa kama yetu ambayo inamatatizo mengi hivyo wale wanaoibuka na kuja haki muhimu kuanza kukandamizwa na kuumizwa kwa kiasi hichi…. Hapa naona sasa Mkwara wa Pm ni dhahiri kuwa LIWALO NA LIWE ni kushindwa kutoa maamuzi ya busara na kutisha watu. Hakika Kitendo hichi ni wazi kuwa kama madaktari na Wananchi kwa pamoja hawataungana kukemea hili litawasumbua Watanzania kwa Watu wachache kuwaamuulia wanyonge kwa chochote kile.

  Joside

  June 27, 2012 at 2:12 PM

 44. whoever did this is a devil,be it a natural or legal person,get well soon doctor.

  Kabondo

  June 27, 2012 at 2:22 PM

 45. Chozi lahaki likimwagika ndoijulikane wokovu unakaribia…….nna shaka nahawa viongoz wetu ikiwa uwezo wakufikil unagota nakuona njia iliyo halali nikuumiza ili wengine wapate kutulia, naamini hawajazima bali ndokwanza wamewasha. Na hii itawakosti sana

  shabir mohamed

  June 27, 2012 at 2:23 PM

 46. Ni kweli naunga mkono swala la madaktari wanaomuattend wachunguzwe isije tokea tatzo jingne kw dr.ulimboka.

  Pizzo

  June 27, 2012 at 2:29 PM

 47. Hii ndo tanzania bwana viongoz wanaposhndwa kutatua kero za watu kwa njia moja bas wanatafuta nyngne pole yake daktar wetu tuko pamoja nae

  Swebe nsobi

  June 27, 2012 at 2:29 PM

 48. Mimi naskitika sana maana serikali yetu imezoea kutatua matatizo kwa njia ya zimamoto pale inapokosa majibu hiki kilicho mpata Dkt Ulimboka ndicho kilichompata kumbenea,marehem chacha wangwe alipo taka kutoa taalifa bungeni kwamba ameona na Balali kule marekan akina Kolimba Mh Sokoine vifo vyao ni vya kutatanisha sasa tuliowapa mamlaka wamekuwa madkiteta sasa kazi kwetu 2015

  Colesco athanas

  June 27, 2012 at 2:47 PM

 49. Swali langu mi nahoji kwann madaktari wameudumie yeye wakati wamegoma? Mwacheni naye aonje machungu wanayopata wagonjwa kwa kuendeleza mgomo wao.

  Mdau

  June 27, 2012 at 2:48 PM

 50. “Anayeingia madarakani kwa kuchafua wenzake magazetini, anaweza kutumia mtutu kuhalalisha utawala wake” – Frederick Sumaye 2005. — Naanza kushawishika kuamini alichowahi kusema Waziri Mkuu mstaafu.

  Moussa Beneali

  June 27, 2012 at 2:52 PM

 51. Dr.Ulimboka

  mwizarubi

  June 27, 2012 at 2:56 PM

 52. Hakika Mungu atawalaani Kikwete pamoja na jopo lake, wajue tu kuwa ipo siku Haya yote wanayoyafanya yatawarudia. Wakumbuke ya Gaddaf, Sadam, Osni Mubarak

  DENISIKI MALIPO

  June 27, 2012 at 2:57 PM

 53. Kaka tuko nyuma yenu kuhakikisha tunaondoa madkiteta ndani ya nchi hii. Wameshindwa kutatua matatizo badala yake wanataka waue hii serikali mungu airehemu.

  Joseph mahona

  June 27, 2012 at 2:59 PM

 54. Hakika ni inaumaa sana na Wananchi Tuko Pamoja na mpambanaji HYU tunamwombea Mungu ampe nguvu

  tumsifu

  June 27, 2012 at 3:00 PM

 55. Hali hii ni mbaya sana. Kwa namna yeyote ile hawezi kuwa mwingine zaidi ya serikali kuhusika katika kitendo hiki. Kufanya hivi ni kuongeza chuki kwa wananchii na madaktari na kuongeza chuki kwa serikali. I hate this system of the govenment. Dhaifu Dhaifu sana.

  malova

  June 27, 2012 at 3:01 PM

 56. Inatisha, inasikitisha na inatia uchungu sana. Serikali bila kutueleza kwa usahihi juu ya hili
  itakuwa inajipalia makaa ya moto!

  Ango's Ango

  June 27, 2012 at 3:01 PM

 57. UHUNI . . . . .NI UHUNI…………

  UHUNI,.....NI UHUNI......

  June 27, 2012 at 3:04 PM

  • kwakwel nipo pamoja nawatanzania wanao tuhumu serikal mana tunapoendea tutamaliza wenyewe,kwann watanzania tucbadilike 2015.

   tumu allyyak

   June 27, 2012 at 7:56 PM

 58. Tanzania ndipo tunapofeli,,hatueshimu na kuthamini professionals,,nahisi tunaelekea ktk mapinduzi halisi,,,sorry doc

  Mutoka

  June 27, 2012 at 3:07 PM

 59. Nasikitika kusema hawa watu wa ccm na serikali yao wameanza kufilisika kimawazo na kimtazamo, kwani wameshindwa hata kutatua hoja za msingi za kikundi kidogo sana cha watumishi wa umma wanaofanya kazi ngumu na katika mazingira magumu na badala yake wanatumioa njia za kihuni na za kutishiana uhai kama wao wataishi milele au watatawala milele..Tunajua hizi ni mbinu chafu za serikali za kugandamiza fikra za kimaendeleo kwa kupandikiza fikra za uoga. Nakwambia hili hatutaliacha lipite hivi hivi tutalijibu kwa kishindo kukuu! “No need to complicate life because it is not permanent”

  evancekomu

  June 27, 2012 at 3:09 PM

 60. Kama matatizo yanamalizwa kwa njia kama hizo za kuteka watu serikali hii imekwisha, na mafisadi watekwe kama hivyo tumalize ufisadi. Usemi wa mnyika kumbe kweli !!!!!!!!!

  Bakari hassan

  June 27, 2012 at 3:12 PM

 61. ktk hili naanza kupata mtazamo mpya tofauti na niliokuwa nao mwanzo kuhusiana na nia dhabiti ya serikali ktk hili. wazir mkuu kwa namna moja au nyingne ana mambo ya kujibu hapa,naanza kupata mashaka sana kwa style hii kweli tunaelekea wap? hawa madaktari kumbe wana mambo ya mzing zaid ya propaganda zinazoenezwa na watu wasio na uelewa.

  daniel

  June 27, 2012 at 3:13 PM

 62. daaah hali hii haikubaliki hata kidogo,na hii inadhihilisha kuwa serikali yetu huwachukia wasema kweli na wanaodai haki zao.

  kinyaga yustino

  June 27, 2012 at 3:16 PM

 63. Hii sasa ni hatali na mengine yote fanyeni, rakini huku uzalendo utatushinda!!

  IDD ISMAILY

  June 27, 2012 at 3:16 PM

 64. Mimi naomba niwe tofauti na watu wengi waliochangia tena kwa hisia kali. Madaktari wanafanya kama alivyofanyiwa Dk. Ulimboka. Unapogoma kumhudumia mgonjwa mahtuti wakati ni kazi uliyosomea na umekula kiapo kuitekeleza unatofauti gani na wauaji wengine. Unapokuwa na madaktari wanaogoma mara 3 kwa mwaka ni nguvukazi kiasi gani inayopotea kwa uzembe huo? Sitaki kuamini kuwa mgomo pekee ndio utawatekelezea madai yao. kwa ufupi madaktari wameichezea sana serikali kiasi cha kuishika ndevu. Waliomfanyia hivyo huyo Dr. wanatoa fundisho la kumkumbusha huyo Dr. ahisi maumivu wanayoyapata wagonjwa kisha alinganishe na gharama za kutelekezwa na madaktari. Tunapotoa maoni tusiongozwe na hisia, jazba na mihemko ya nafsi. Tuongozwe na fikra za kiuchambuzi na tuwashauri madaktari waache kubishana na serikali kwa mtaji wa kuwaumiza wagonjwa na kuwasababishia vifo na pengine ulemavu wa kudumu. Nipo tayari kukosolewa. Huo ndio mtazamo wangu.

  Gidion Mwaki

  June 27, 2012 at 3:18 PM

  • Wewe nawe uwezo wa kufikiria ni mdogo sana tena sana, na inaonyesha ni kiasi hufuatilii mambo ya kijamii nchini na nje ya mipaka ya Tanzania. Unajua ni watu wangapi wanakufa kwa sababu ya kukosa vifaa mahospitalini, hiyo inayoripotiwa ni kiduchu ukilinganisha na vifo ambavyo havilipotiwi kutokana na upungufu wa dawa mahospitalini, vifaa na hata ICU kukosa oxygen? unajua mazingira hatarishi wanayofanyia kazi madaktari? Je, madaktari wa Tanzania ni kwanza kugoma? je unajua ni mara ngapi madaktari wamegoma nchini Nigeria kwa mwaka huu pekee kwa mfano? Ukiwa na mawazo ya kijinga bora uyajadili na watu vijiweni na nyumbani kwenu kuliko kuyaleta kwenye mtandao ambako watu wenye upeo wanasoma comments mbalimbali.

   Hujui utokako na wala uendako.

   Pole sana Dr. Ulimboka, wakati wa ukombozi kutoka mikono wa wakoloni weusi ni sasa.

   Kyoreye Chacha

   June 27, 2012 at 4:14 PM

   • dah!…jamaa ume mjibu kwa busara sana!…huyo ni chizi tena kakurapuka ku “comment” hana alijualo kuhusu hii serikali ya kifisadi!..tena kajisahau kua ye mwenyewe kaongozwa na hisia kuchangia :”negativity” kuhusu hilo!…ye hajui hilo “may be” kuna ndugu yake kashiriki katika hilo ndo mana hana uchungu! kwakua ukiwazungumzia hata hao madaktari pia ni watanzania!…ila nao wanajali mac lahi yao!… na ya watanzania kwa pamoja!….ila huyo chizi hajui hilo!!!…..hajui watumishi wa serikali wanavyo fanya kazi kwenye mazingira hatarishi na magumu!,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,na bado ikitoka ya madaktari!….. ita fuata ya waalimu!

    pole saana Dr. Ulimboka, Steve!

    INSHAALLAH!….M/mungu atakuponya!

    Mohamed Juma

    June 28, 2012 at 8:34 AM

   • Kaka nadhani hujui ‘The PR of Demand’ Madaktari wako vitani wanapambana na serikali silaha yao ni wagonjwa pekee. sasa kwa kuwa kivita si vizuri na haikubaliki kimataifa kuwatumia wagonjwa kama silaha wao wakachomekea masuala ya vifaa na mazingira duni ya kazi. Swali kwanini hili lije leo wakati wa kudai maslahi yao (kama walivyoanza wakati wa mgogoro wa ma-interns). Kila hoja niitoayo ina falsafa yake. Hawa wanakupumbaza mtu kama wewe asiye mchambuzi wa matini na matukio yakilinganishwa na hali halisi ya wakati husika. Hata hivyo nakushukuru kwa kujaribu kuonyesha hisia zako. Kumbuka mawazo yako sio msahafu na si lazima yaungwe mkono. Mimi niko tofauti na mawazo yako. Na hayo ndo maarifa.

    Gidion Mwaki

    June 28, 2012 at 4:44 PM

   • Jamani hebu tujiulize kwanza ni kitu gani madaktari wanakipigania, hapa mi ninachokiona wao wanapigania maslahi yao binafsi. kama ni vifaa na madawa je vifaa na dawa wanazozitumia leo kumtibu Dr. Ulimboka wamevitoa wapi? Pia je huo mgomo wao anaye umia hapa ni nani? Tunaoumia hapa ni sisi walala hoi ambao hatuwezi kumudu gharama kubwa za matibabu kwenye hospitali binafsi coz vigogo wote wanatibiwa nje. Hebu vuta picha…unampeleka baba yako au mama yako muhimbili halafu anafia mapokezi eti kwa sababu tu ya mgomo wa madaktari wanoshinikiza walipwe over 3mil shs.. Vyovyote iwavyo but hii njia waliyochagua kudai maslahi yao mimi siiungi mkono. TUACHE SIASA NA ROHO ZA WATU.

    khaundinkhotse

    June 30, 2012 at 12:32 AM

  • Enjoy kwa muda huu ila ukombozi ukiingia utabaki na maumivu kama alonayo Dr Ulimboka@Gidion Mwaki

   Kyoreye Chacha

   June 27, 2012 at 4:19 PM

  • hivi ungekuwa ww unaambiwa kufanya kazi kwa mshahara kidogo, na mazingira hatarishi kwa afya yako ungekubali usiwe mbinafsi madactari wana familia zinazowategemea km ww na wabunge acha ujinga huo
   atu

   esther

   June 28, 2012 at 8:36 AM

 65. Mungu ni mwema na anajibu maombi sisi sisi sisis watanzania baba yetu nani?

  john kisawa

  June 27, 2012 at 3:19 PM

 66. Udaigi wa Haki za Watanzania umefikia ktk hatua hizi? Ni nani mwenye Mamlaka ya kuwatesa wengine hata kujaribu kutaka kuwauwa ili yeye aendelee kuthaminika kwa wengine kwammba anaweza kuongoza na kutekeleza? Daima Mungu wa Utukufu, atasimama ktk kuwaumbua watu hawa.

  Dennis MpendaMungu

  June 27, 2012 at 3:20 PM

  • Jamani yani kweli serikali yetu imefikia huku hii ni hatari sana maana badala ya kutatua matatizo yaliyopo wanazidi kuongeza matatizo. Tunakuomba sana kaka Zitto hili swala ulivalie njuga maana huu ni unyanyasaji sana ukizingatia hao Madaktari wenyewe wanasoma kwashida hiyo miaka 5 yote halafu na mishahara yao pia waipate kwa mateso kama haya jamani.

   Aisha

   June 27, 2012 at 3:41 PM

 67. Hili siyo jambo la kutokea hapa Tanzania!

  Emmanuel Mziray

  June 27, 2012 at 3:32 PM

 68. Ukweli hauwezi kujificha kwani kama tumefikia hapa! Hii ni ishara kuwa Serikali iliyopo madarakani sasa imeshindwa kuendesha nchi kwa njia ya mjadala na maridhiano. Hivyo inachokiona sasa ni kutumia mabavu kupitia mwamvuli wa usalama wa Taifa. Tafakalini watanzania.

  Simon Wamiwa

  June 27, 2012 at 3:35 PM

 69. Siasa zimezidim kila mahala hata huko Mahospitalini tubadilike

  Mario Mutayoba

  June 27, 2012 at 3:44 PM

 70. Inaonyesha nijinsi gani serekali yetu inatuendesha kidikteta na kutotujali ss wananchi. Namwomba mungu akili za watanzania ziwe kama za walibya

  Festo jackson

  June 27, 2012 at 3:50 PM

 71. tunapoelekea ni kama MISRI, Inavyoonekana huo msitu wa PANDE umeshatumika sana kuwaadhibu wale wanaoitwa MAADUI wa SERIKALI, Watanzania tufumbue MACHO watatumaliza…!!!!!

  japhet kade

  June 27, 2012 at 3:55 PM

 72. CHADEMA itisheni mkutano wa hadhara kwa swala hilo mana inaonekana bungeni limeshindika!
  Tupo pamoja nanyi M4C!

  kalova

  June 27, 2012 at 3:59 PM

 73. wanajifanya kufuata utawala wa sheria ilihali raia zake tena wenye influence kwa jamii kunyanyasika hivi. imeniuma imeniskitisha na itaendelea kuniuma!

  kabanga kasulu

  June 27, 2012 at 4:05 PM

 74. Serikali lazima ilaumiwe kwa hili kwa sababu ingekuwa madaktari wamepewa haki zao wasingegoma

  Upendo

  June 27, 2012 at 4:12 PM

 75. baraza huru la usalama wa Taifa ndiyo jibu sahihi kwa matatizo kama hayo.Ushauri wa kihuni kama huu ni kiburi cha watawala kuwa wakuu wa nyombo vya usalama.baraza hilo liteuliwe na rais.liwe na mamlaka ya kumuita na kumhoji mtu yeyote kuanzia Rais ua mtu yeyote.

  mbogolo mlekwa

  June 27, 2012 at 4:15 PM

 76. Hii inasikitisha na inaonesha jinsi gani serikali hii inavyozidi kuchanganyikiwa na uongozi wake haiwezekani jambo kama hili litokeee kipindi kama hiki cha mgomo wa madaktatri tena akitokea kwenye kwenye chombo cha habari kusisitiza mgomo,lifanyiwe kazi na vyombo huru ili ukweli ufahamike.

  Mlyambongo

  June 27, 2012 at 4:23 PM

 77. Duh! naigopa serikali ya TZ! inatupeleka wapi hii nchi jamani? kwanini lakini? siamini kama serikali sikivu inayojali watu wake kama wanavyojinadi- inaweza kufanya vitendo vya kinyama kama hivi!!! ukweli hii inatisha sana na sijui kama hatujakaribia kuomba hifadhi nchi za jirani.Baba yetu JK Nyerere ulituacha kama yatima tunakukumbuka. Serikali imekuwa kama ya kijasusi!! tunaenda wapi sasa? mmmmh choka mbaya!!!!!!!

  Bugumba Msumba

  June 27, 2012 at 4:24 PM

 78. Hii ni kuonesha dhahiri kuwa serikali hii sio sikivu wanadhani Watanzania wa miaka ya 70 ndio wa leo wakiimbiwa NYERERE AJENGA NCHI baasi kila kitu kinakwenda sawa hakuna kuhojiwa nawaomba Wabunge wa upinzani kesho wamtake Waziri Mkuu kwenye masuali ya papo kwa papo atoe majibu yaliyokwenda shule ni kipi kinachoendelea

  ISSA

  June 27, 2012 at 4:25 PM

 79. Kwa hili serikali yetu tukufu ya chama dhaifu imeingia choo cha KIKE

  Sir

  June 27, 2012 at 4:31 PM

 80. Serikali ni CCM, jamani hawatufai tena kwa nini wakae kimya muda wote niliwasikiliza madaktari ilikuwa chanel 10 juzi walikuwa wanasema vitu vya msingi sana ila sijasikia majibu ya serikali nadhani ndo wamejibu kistaili hiyo.

  Justine

  June 27, 2012 at 4:36 PM

 81. CCM NA KIKWETE ACHENI KUWA NA ROHO YA KINYAMA,KWANZA WE KIKWETE NCHI IMEKUSHINDA SASA,AKIFA ULIMBOKA DAMU YAKE ITAAMBATANA NA NYIE.

  rehema hassani

  June 27, 2012 at 4:36 PM

 82. Kwa kweli ni habari za kusikitisha. Hao waliohusika na kutekwa kwa Dr. Ulimboka, wasakwe na wapelekwe mbele ya Sheria. Ninachelea kusema kuwa kuna mkono wa serikali, kutokana na sakata lililopo la madaktari kugoma. Hivyo naomba vyombo vya dola, vichukue hatua ili kubaini waliohusika. Kwa vyovyote wapo.

  Godwin Muganyizi

  June 27, 2012 at 4:37 PM

  • sintokawia kusema pana mkono wa serikali hapa.tunaagiza sheria ichukue mkondo wake kwa hawa waliotumwa kufanya unyama huu kwa watu wa umuhimu kama huyu dr,.kinyume na hapo tunawaomba wanaharakati na wanademocrasia kuitisha maandamano nchi mzima kwa masuala ya kinyama kama haya.

   edo lema.

   June 27, 2012 at 5:13 PM

 83. Madaktari wewe makini sana ili aliyehusika na tukio la kwanza dhidi ya Dr. Steven Ulimboka anaweza kummalizia kwasababu kutupwa Msitu wa Mbwe pande ni kwamba walijua ameshakufa.

  Namwene

  June 27, 2012 at 4:47 PM

 84. Sehemu ya kupatia umaarufu imejitokeza,bahati mbaya Ulimboka alitaka umaarufu kupitia Watanzania tena Wagonjwa,jiulizeni yule anayesababisha ajali kwa bahati mbaya barabarani hufanywa nini na wananchi wenye hasira kali,seuze huyu anayechochea tena kwa makusudi.Ujinga wenu ni kwamba Serikali ina mkono kwenye hilo mbona hamlikabidhi jeshi la polisi kadhia hiii.SITAKI KUAMINI KUWA WALE WALOSEMA NCHI HAITATAWALIKA NDO WANAOCHOCHEA MIGOMO HII ILHALI WAO WAKIPANDISHWA NDEGE KWENDA NJE KWA MATIBABU REF:ZITTO KABWE KUPELEKWA INDIA.

  aida

  June 27, 2012 at 4:53 PM

  • Wewe unadhani unaakili lakini unashida kabisa wewe! Tena nyie watu ndio mnaopotosha idadi kubwa ya watu! Umaarufu kweli can you think of that kama mtu mzima? Ama humu pia kuna watoto nini? Poor you!

   James

   June 28, 2012 at 2:08 AM

   • James wewe ndo mtoto, hayo aliyoandika Aida ni upande wa pili wa sarafu. Sio mnaegemea upande mmoja tu. Balance your thinking people. Madaktari wanagomaje kwa mtaji wa wagonjwa? Na je nani anahakika kuwa ni serikali imefanya hivyo? Je huyo dogo, hana maadui wengine zaidi ya serikali? Yeye ni malaika kwa kiasi gani hata asiwe na adui chini ya jua? Maswali haya nani anayajibu katika uchangiaji wetu? Tunapelekwa pelekwa na hisia tu kana kwamba tuna uchuuuungu sana na kuumizwa kwa dogo huyo. Agh!!! Rubish!!

    Gidion Mwaki

    June 29, 2012 at 5:24 PM

  • Lakin ngoja na mim niungane na wew wanaekuita mtoto cjui matuc gan mengine.. huyu jamaa usikute wala shuruba yake serikali haihusiki kabisaaa, sema tu mazingira na kauli ya bosi wa serikali mjengoni kule ndio utata.. mim nnachokijua kwa sis walevi mazingira ya bar or club you can do and talk anything bila kujua the ultimate impact to the surrounding society.. sasa pale Leaders si wote tunakuwaga out of minds.. hasahasa tukishakuwa safi baada ya kupata mambo yetu yalee.. sio siri uchungu wa kifo cha marehem mama yangu mzazi(mungu amrehemu..) alofia kwenye kituo cha afya matamba baada ya kukosekana drip za kuongeza maji, huwa naupata zaidi nikiwa tungi.. samahan mawadau lets try to be rational thinkers na tujaribu kuvuta subira.. CHA MSINGI TUMUOMBEE DR. ULIMBOKA APONE HARAKA, ILI AFICHUE AKIWA KWENYE MENTAL HEALT STATE.. KAMA MNAVYOITA WENYEW.. WHAT WAS REALLY HIDDEN IN THE DACKNESS..! MI NAONA KAMA TUMEKUWA WOTE KAMA MACHIZI KWA KUWORK UNDER ASSUMPTIONS… KAMA SERIKALI KWELI WANGEHUSIKA SI WANGEUA KABISA AS HOW THEY DID TO KOLIMBA AND OTHERS.. KAMA ALIVOTUHAKIKISHIA MP. WA VUNJO ENZI ZIILLEEEE ALIPOGOMEA MIC BUNGENI..! sema2 wengi hum ni wanafik and they only think in myopic way.. POLITICS..!

   Mtoto wa Mwalim

   July 2, 2012 at 12:43 PM

 85. Conspiracy…. GOD IS GOOD,HE WIL BE OK

  Mary marie

  June 27, 2012 at 4:54 PM

 86. I don’t believe this is happening in our country, thorough investigation should be done to gv answers for what has happened and the people responsible for this must be taken to the court of law

  Albert

  June 27, 2012 at 4:56 PM

 87. sasa hii ndo amani tunayojivunia,mwisho wao umefika lazima watuachie nchi yetu kwani wanatunyonya kuliko wakoloni walivyo tunyonya.

  simon kessy

  June 27, 2012 at 5:03 PM

 88. Wewe kigosi better keep your mouth shut, the government must ell us, why now! kwa nini huyu mtu hakuvamiwa siku ingine! why now when kuna strike ya madaktari, hatuwezi kwenda hivi, either watuue wote au watimize tunachokihitaji km watanzania.
  Acheni siasa, na kumbuka hakuna siasa bila uhai, madaktari wanapigania uhai wa mamilioni ya watanzania, nyinyi wengine na saiasa zenu uchwara mnapigania magari ya gharama na kuvuja pesa za umma, shame on you. I believe in God, he will stand on us, and Dr Ulimboka, get well soon. Life goes on na mapambano yanaendelea.

  James Dickson Auson

  June 27, 2012 at 5:04 PM

 89. ni habari za kusikitisha, serekali inalaumiwa kwa swala hili. kwani itokee kipindi ambacho wapo kwenye mgomo means kuna mtu ana husika na mtandao huo. Tumuombee apone then itajulikana ni nani alaumiwe.

  Neema Thomas

  June 27, 2012 at 5:10 PM

 90. Je serikali inaweza kufanya hivyo, sie walala hoi je tunaweza? Au ndo syria imehamia tanzania? Yote tisa kumi dk ulimboka anaweza kutufumbua mawazo na mtazamo wetu kwa serikali na mzozo uliopo

  Emmanuel Mayaya

  June 27, 2012 at 5:13 PM

  • hekima na busara zitumike kutatua suala hili badala ya nguvu. Uongozi ni dhamana ya muda, kesho atakaa mwingine atayewapeleka mahakamani wote wanaotumia madaraka vibaya. inauma sana kwa unyama aliofanyiwa Dr.

   MK

   June 27, 2012 at 5:38 PM

 91. Jambo kama hilo mengi yapo, huenda ikawa si serikali kama wengi wanavyodhani! huenda ni yeye mwenyewe kasababisha hilo, inawezekana tayari alishakubaliana na serikali kutoa tamko kuwa hakuna mgomo tena, sasa madaktari wenzake ndio wamemfanyika kitendo hicho kwa kuona kuwa amewasaliti. Tukio kama hilo jaribuni kuangalia pande zote tatu za sarafu, si kulaumu serikali tu.

  Tes

  June 27, 2012 at 5:22 PM

 92. Hii inafanana na yale yaliyomkuta Dr. Mwakiyembe and soon utaona jinsi ishu nzima itakavyopotoshwa na kuwekwa kapuni, real there is a deep secret behind this. Tumuombee Dr Ulimboka apone ili aeleza jinsi tukio zima lilivyokuwa.

  ju li us

  June 27, 2012 at 5:29 PM

 93. Dah!inasikitisha sana,kweli tumefika huku?!!

  Anitha

  June 27, 2012 at 5:48 PM

 94. TUACHIE CHOMBO HUSIKA KUFANYA UCHUNGUZI . UNAJUA VIJANA LAZIMA MFAHAAMU HATUA ILIYOPO SASA ULIMBOKA NI LULU LKN C WOTE WANAONA LULU YAKE . KTK SWALA HILI KILA MTU ANATAZAMA KWA JICHO LA TATU NA MAADUI WAKE WANATUMIA FULSA HIHI . LKINI ZITO WANGAPI WAMEKUBWA NA MATATIZO ILA WEWE UMELIONA HILI .

  MBAYUWAYU WA MCHANA

  June 27, 2012 at 6:17 PM

  • UCHUNGUZI UPI? WA NINI? ILI IWEJE? ALIKUFA PROFESA MWAIKUSA IPO WAPI TAARIFA YA WALIOKAMATWA, IPO WAPI TAARIFA YA WALIOMWAGIA TINDIKALI KUBENEA, IPO WAPI TAARIFA YA KADA WA CHADEMA PALE ARUMERU, VIPI YULE MWENYEKITI WA CCM PALE RUNGWE, MWAKYEMBE JE! ACHENI UJINGA WATANZANIA WE HAVE NOTHING TO LOOSE, RWANDA BAADA YA KUCHAPANA MIKONO LEO WANAENDELEA, WANAJUA HATHARI YA DAMU, WE HAVE TO PASS THAT WAY TO HARMONY THIS COUNTRY, PEOPLE ARE AFRAIDING OF DEATH, WHAT IS DEATH THEN “WHETHER WE FIGHT OR NOT AS HUMAN BEING WE ARE BOND TO DIE, SASA NI LIPI BORA TO DIE LIKE AN ANIMAL UNATESEKA AU UFE UKIACHA MAISHA MEMA KWA VIZAZI VYAKO ELFU VIJAVYO…TZ STAND UP! NIPO TAYARI I NEED SUPPORT..NAANDIKA NINALIA MIMI…AHH

   mwanamapinduzi halisi

   June 27, 2012 at 10:58 PM

   • Acheni ubwege! nani kasema kumwaga damu ndio kusafisha nchii,,,, Acheni ubinafsi, Tutumie njia nyingine kuishinikiza Serikali kuboresha mahitaji wa madaktari, lakini si kupitia ViFO vya Wananchi wasio na hatia…kila mtanzania anathamani sana na hakuna mbadala wa mtu..Au nyie ndo mnatibiwa nj’e ya Nchi.

    Jeff

    July 2, 2012 at 11:08 AM

 95. Habari nimeiipokea kwa masikitiko makubwa Tanzania ni nchi ya amani na utawala wa kisheria sasa mambo haya ya kutekana nyara kuumizana hadi mtu kufikia mahututi.

  Abbas

  June 27, 2012 at 7:49 PM

 96. KWANI NANI HAJUI KUWA WANAOWALIPA MISHAHARA MADAKTARI NI WATANZANIA, NA KIMSINGI NDIO AMBAO LEO WANAPEWA ADHABU YA BILA CHUKI NA VIBARUA WAO? KAMA ULIMBOKA NA WENGINE TUKIWEMO SISI TUNAOWALIPA TUNAAMINI HAKUNA MTAZANIA UKIACHA FISADI NDIYE ANAYEPATA KIASI CHA KUTOSHA, HIVYO INGEKUWA BUSARA KUGOMA KUWATIBU WABUNGE WENYE KUJIPENDELEA MAPOSHO KIBAO NA AMBACHO NDIO CHOMBO PEKEE KTK KUTUNGA SHERIA NA KUPITISHA BAJETI

  Mwasimba Simon

  June 27, 2012 at 7:53 PM

 97. kama kubenea

  joe

  June 27, 2012 at 7:54 PM

 98. 2015 movement 4 change. freedom is coming tomorrow!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  steven

  June 27, 2012 at 7:59 PM

 99. siku zote serikali inayotisha watu inaogopa kivuli chake. Kwa hali hii, ni suala la muda tu. PUNDA HALAZIMISHWI KUNYWA MAJI.
  HIVI TUKIWALAZIMISHA MADAKTARI KUTOA TIBA, WATATIBU KWA KUFUATA MAADILI YA KAZI?
  SERIKALI INAJIDANGANYA KWA HILI,
  HIVI HAO WALIOAMUA KUTEKELEZA UNYAMA HUU HAWAKUJARIBU KUANGALIA IMPACT YAKE KWETU WATANZANIA?
  KAMA NI SERIKALI BASI IMEJIVUNJIA HADHI KWETU KWA KUKOSA UAMINIFU.
  KITENDO CHA MADAKTARI KUGOMA KISINGEFIKA HAPA BUT NI KUTOKANA NA UJANJA UJANJA UNAOFANYWA NA SRIKALI KUPIGA DANADANA HUSUSANI WASHAURI KATIKA HILI HAWAISHAURI VIZURI SRIKALI.
  HUU NI UDHALIMU KATIKA NCHI YA KIDEMOKRASIA, JE SERIKALI YA NCHI HIYO TUIITEJE? WATENDAJI WAKE TUWAITEJE? VYOMBO VYAKE VYA DOLA NAVYO?
  YOU CAN NOT SOLVE THE PROBLEM ON THE WAY IT IS CREATED.
  MADAKTARI WANAGOMA KWA KUTOPATA STAHILI NA HAKI WAKIWA KAZINI, SRIKALI INAYOTAKIWA KUTOA HAKI HIYO INAGOMA.
  NINI TUTARAJIE?

  HII NI HATARI SANA

  June 27, 2012 at 8:58 PM

 100. Nadhani tunaongozwa na nchi ambayo viongozi wake hawana akili ila wana hasira na “Hasira hasara”/Kwa serikali yenye viongozi timamu halikuwa jambo la kumfanyia mtu tena kiongozi wa mgomo kwenye jambo ambalo serikali imeshindwa kulitatua mezani,Swala la mgomo kwangu mimi ni swala la msingi si kwa Madaktari tuu hadi wananchi wa kawaida/Sawa wengine wanawalaumu madaktari lakini; ni bora kugoma, kuliko kukaa hospitalini na mgonjwa kufia mikononi mwa dokta,wakati angeweza kumponya kama kungekuwa na vitendea kazi.Inauma sana hasa serikali inaposhindwa kutekeleza at least jambo moja la msingi kama hili/

  theswagga

  June 27, 2012 at 9:13 PM

 101. hili jambo si la kukurupuka na kulitazama kwa sura moja tu, kumekua na uzushi mwingi sasa hivi na pia njama kibao zakuchafuana mfano mdogo ni suala la Simbachawene. hapa kuna taswira nyingi mojawapo ni huenda ni wabaya wake waliokua wanamuwinda kitambo sasa wamepata timing nzuri, huenda pia ikawa ni wananchi waliochoshwa na misimamo yake ya migomo na wanaomchukulia vibaya.tusikimbilie moja kwa moja tu na kuituhumu serikali. kama mwanasheria na msimi naliona hili jambo katika taswira nyingi sana. Muhim ni kuwaachia polisi waendelee na uchunguzi huku tukisubiria hali yake iwe sawa tupate maelezo yake ya awali.

  Ally

  June 27, 2012 at 9:29 PM

  • Ahsante kwa kutupa upande wa pili wa jinsi ya kuliangalia jambo hili bwana Ally. Huu ndo ukomavu wa fikra. Tusiwe wavivu kufikiri na kuumiza vichwa. Tunakimbilia kuonyesha hisia tu. Sawa si vizuri kumtendea mtu kama alivyotendewa huyo Dr. lakini tusielekeze lawama sehemu moja kana kwamba tuna uhakika na msingi wa lawama zetu.

   Gidion Mwaki

   June 28, 2012 at 6:35 PM

 102. Masuala haya yanhitaji busara zaidi, kwani serikali inapowadanganya wananchi inakuwa inasaidia zaidi kuongeza vuguvugu la mageuzi ya kifikra kwa watu wake. kumjeruhi daktari na kutishia kumuua ni suala tashtiti lenye kuleta maswali mengi kwa jamii. Serikali itimize uhalisia wa maisha ya watumishi wake ione kama watumishi hao wataendelea au kuwa na mawazo ya mgomo.
  Habari za kupeana ahadi kisha wanazifukia ilikuwa ni enzi ile ya miaka ya sabini sio sasa. Watu wanafuatilia na kuona nini kinafanyika. Kumuua mtu mmoja ni sawa na kuchochea moto wa vurugu nchini. Suala hili Halihitaji akili nyingi kutambua kuwa muhusika kwa hili ni serikali, wengi wanatoa maoni yao, wanaleta kujuana katika mjadala ili waonekane wamaana sana kwa serikali, nyie ndio mtakufa kama mbwa koko. Kila mtu atazame suala hili kwa umakini zaidi ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu.
  Mwarabu aliwauza babu na bibi zetu katika masoko ya utumwa na serikali inatutumikisha kama walivyofanya waarabu kisha inatubeza na kututaka tuone kuwa hiyo ni haki yetu na tuache kulalamika. Wanapojitokeza watu wakujitoa muhanga kama Dr. Ulimboka linakuja suala la kutishiwa amani na maisha yao kuwa hatarini, huu ni aina ya uhuni ambao hauna budi kuepukwa.
  Ukianza kuhesabu ni wengi wamekufa kwaajili ya haki za msingi wanazozidai kwa serikali. Endeleeni kutufanyia vitendo vyote kadri mpendavyo ila siku yake ipo mtapata anguko kama la Mfalme Edipodo.
  Inasikitisha, inauma na kukera sana.
  Ulishasikia kesi ya Ngedere unampelekea Nyani aichunguze na kuitolea hukumu hivi ni vichekesho mnaotaka serikali hii ifanye uchunguzi. Uchunguzi wa nini na inajua imefanya nini?
  Labda mseme iwasaidie nyie mlio upande wake kuwafurahisha, kwa kuwakamata watu kujiosha uso na kuwafungulia kesi kwa niaba ya serikali.

  Mwl. Emanuel

  June 27, 2012 at 9:35 PM

 103. Kitendo hicho ni cha kinyama na cha hujuma,chamsingi wapewe haki zao na sio kuendeleze siasa

  Bakari

  June 27, 2012 at 9:41 PM

 104. mimi wananchi wa tanzania mnanikera sana yani kuna miwatu inachangia pumba mpaka unatamani ulitie kwenzi linyamaze..WITO WANGU KWA MADAKTARI NI KUWA IMETOSHA, IMETOSHA KUSIKIA UCHUNGUZI UNAENDELEA KILA SIKU, INGIENI MTAANI KESHO MTUTAFTIE SABABU TULIANZISHE, NINA HAMU YA KUMTOA MTU CHINI YA KARAVATI KAMA MZEE ILIVYOKUWA KWA GADDAF, ITS TIME TO RISE AND REVENGE, “OUR REVENGE WILL BE A LAUGHTER OF OUR CHILDREN” REVOLUTION IS NOT AN APPLE THAT FALLS WHEN IT IS RIPE, WE HAVE TO MAKE IT FALL…i mean what am writing, it a time to time to wait, i’m ready to take my Gun.

  mwanamapinduzi halisi

  June 27, 2012 at 10:46 PM

 105. waliofanya hiki kitendo cha kinyama watambue kwamba hii siyo njia sahihi ya kutatua tatizo,labda waseme wanahairisha tatizo and the time will come soon.Get well soon Dr.Ulimboka tuko pamoja.

  Prisca

  June 27, 2012 at 10:52 PM

 106. HIVI HAO WANAOSEMA KUWA ETI HILI SIO LA KWANZA, KWA HIYO NDIO TUENDELEE KUBALIKI UHUNI HUU? KTK HILI LILETWE JOPO LA KIMATAIFA KUJA KUCHUNGUZA TUKIO HILI, MAANA NI MGOGORO KATI YA MA DAKTARI NA SERIKALI, LAZIMA TUME ITOKE NJE YA NCHI NDIYO HAKI ITATENDEKA, LABDA HIYO TUME MWENYEKITI WAKE AWE MH. MWAKIYEMBE.

  Peter Mheta

  June 27, 2012 at 11:22 PM

 107. Looh!Kitendo alichofanyiwa Dr.Uli.ni cha kinyama.Sitaki kuamini kwamba kinafanyika Tanzania Kisiwa cha AMANI!

  Bulaya M.J.Mwambilu

  June 28, 2012 at 12:24 AM

 108. Tunakila sababu ya kukataa amani hii ya Tanzania mana imekuwa ya kupumbaza kama unga wa ndele wa bibi kilembwe.Amani bila justices is nothing.wake up Tanzanians ,we’re not free at all.

  azimio

  June 28, 2012 at 12:36 AM

 109. nnacho cctza jaman apo alipolazwa dr kuwen makin anaweza akamaliziwa hapo apo, na mckubali kuja ndg wajamaa tofaut na wanaojulikana kumwona tafadhali inch hii isha kuwa ya kigaid na kidikteta

  beny

  June 28, 2012 at 1:16 AM

 110. nnacho cctza jaman apo alipolazwa dr kuwen makin anaweza akamaliziwa hapo apo, na mckubali kuja ndg wajamaa tofaut na wanaojulikana kumwona tafadhali inch hii isha kuwa ya kigaid na kidikteta ‘wazir mkuu kasema kesho anakuja na jibu juu ya mgomo wa madaktar mi naic jibu ndo hili 2sha jibiwa

  beny

  June 28, 2012 at 1:33 AM

 111. Hayo ndo matokeo ya kauli za kidhaifu………… POTELEA MBALI .LIWALO NA LIWE………………..

  Filbert Renath

  June 28, 2012 at 5:29 AM

 112. nivema uchunguzi ukafanywa. Majibu tusitue kirahisi kwa kuanza kumshuku nani kahusika hatupaswi kudhani tu wa tanzania tubadilike mtakuwa mnaa cha hisia zinatawala akili zenu.tukio limetokea tayari ni vema tukafanya ushirikiane ifike tujifunze kupitia matukio na historia za ndani ya nchi na nje ya nchi. Katika kipindi hichi kibaya halafu unatia moto kwa petroli wht you espect.. Wengi wamekufa kwa mateso ya namna hiyo na kubaki siri kwa vinara kama ulimboka. mungu amsaidie.

  mohamedi mkonde

  June 28, 2012 at 5:56 AM

 113. JAMANI TUTAFIKA ? NIMEONA PICHA YA HUYO DAKTARI KWENYE VYOMBO VYA HABARI – EH INATISHA NA KUSIKITISHA MNO MNO! Hata hivyo TUSISHABIKIE VISASI ….. TUONGOZWE NA BUSARA! YUKO ALIYELIAMBIA BUNGE “LIWALO NA LIWE!” HAIKUPITA SIKU WALA MUDA TUKAYASIKIA HAYA YAKUTISHA ……… JE NI KWELI MZEE WETU LIWALO NA LIWE? Pamoja na yote; wote tunahitaji kuongozwa na busara zaidi kuanzia sasa, tusichochee moto unaowaka ndugu zangu ….. amani imeanza kutoweka wenzangu watanzania …….. tuwe watulivu na vyombo vyote vya usalama, sheria na vya kijamii kila kimoja kitumie busara ya juu kabisa inayoambatana na uvumilivu, ustahimilivu, usamehevu! KWA AKILI NDOGO ZA CHINI HILI HALIVUMILIKI ……… LAKINI KWA HEKIMA NA BUSARA HAKUNA KISICHOWEZEKANA! Mungi ibariki Tanzania na watu wake!

  Laurent

  June 28, 2012 at 7:03 AM

 114. Kwa kweli hali hii inatisha. Ni kweli Mh Zito unavosema serikali INAWAJIBIKA kueleza kilichotokea ni kwasababu ya mambo mawili. Moja ni wajibu wa serikjali kuhakikisha usalama kwa raia wote, pili ni mgogoro baina ya serikali na madaktari. Je waliamua kumjeruhi Dr steven ili aache kuwqasumbua? Lakini mbona yeye ni mjumbe tu? Je ni watanzania wengine wamechukizwa labda kutokana na ndugu/jamaa zao kuugulia pasipokutibiwa na hivyo kuamua kumwonjesha na yeye maumivu? SIJUI ila uchunguzi wa kina unahitajika na taarifa sahihi kutolewa bila kuegemea upande wowote…

  Goodluck Savutu

  June 28, 2012 at 7:53 AM

 115. Na kwa nini waziri mkuu alisema liwalo na liwe , kwa mimi hii inamaana alibariki mapambano holela katika suala hili , ni vema serikali itueleze ukweli, hii hali haikubaliki , ni wangapi waliothiriwa na mfumo huu ambao taarifa zao bado hazijulikani , inatisha sana. M4c now

  deogratias

  June 28, 2012 at 8:34 AM

 116. Swala la kugoma na kuanzisha vurugu kwa nchi nzima hilo sio sawa..!mi nadhani sasa ni muda muafaka kwa serikali kuonyesha haswa makucha yake ya uongozi wa kutumia mabavu kuliko kujifanya kuwa eti ni serikali yenye kuthamini na kuheshimu haki za raia kumbe sivyo..:dr ULIMBOKA alisimama nyuma ya wale wanaotetea huduma bora na hali nzuri katika hospital zetu ili hao wagojwa tutakaowapeleka huko mahosptalin wapate huduma inayokidhi vigezo vyote vya afya..!sasa serikali inatumia mfumo wa njia za panya kutaka kuwaaminisha watanzania kuwa eti madaktari wanadai mishahara mikubwa kumbe hiyo ni hali ya kimjadala na wala haikuwa kwa ajili ya matumbo ya madaktari ila ni kwa watanzania woote..!acheni madaktari watutetee jamani maana hospital zetu zimekua na matabaka na laiti kama kipato chako ni kidogo basi ujue ugumu na kuyumbishwa kwa matibabu kutakuhusu tu..!pia nawaomba madaktri kuwaonea huruma sasa watanzania wale ambao ni wagonjwa huko mahospitalin na kuwajibika nao ili kile wanachokidai kionekane kuwa na manufaa na faida kwa wote..na pia madaktari wakumbuke kuwa kwa sasa hii vita sio ya kwao peke yao bali ni watanzania wote kwa ujumja na wapo nyuma yao kwa kukubaliana na hoja zao za msingi kwa maslahi ya taifa letu..!”TANZANIA KWANZA::”

  Calvin mtey

  June 28, 2012 at 8:56 AM

 117. KAMA KUNA MAANA YA KUMCHUKIA DR. ULIMBOKA NI UJINGA MTUPU, KWA MAANA YEYE HAJIWAKILISHI KAMA YEYE ILA ANAWAKILISHA MADAKTARI. HAYA NI MATOKEO YA KUKOSA HEKIMA. MAANA UKWELI NI KWAMBA UONGOZI UNAHITAJI HEKIMA ZAIDI NA SIO NGUVU. UKIWA KAMA KIONGOZI LAZIMA UJIULIZE KWANINI UPO HAPO NA KWA NIHABA YA NANI NA KWANINI WEWE. MPE MUNGU NAFASI NA UTAFANIKIWA KWA KILA ULITENDALO MAANA HATA SULEIMANI ALIOMBA HEKIMA KWA MUNGU ILI AWAONGOZE WATU.

  Chacha

  June 28, 2012 at 9:10 AM

  • THIS IS TRUE, HAKUNA HAJA YA KUMCHUKIA MTU ALIYEPEWA DHAMANA NA WENZAKE ILI AWAONGOZE B’CAUSE HAJIWAKILISHI MWENYEWE ILA ANSIMAMA KWA AJILI YA WALIOMPA DHAMANA HIYO. HII NI DALILI KUWA SERIKALI ZETU ZIMEZOEA MAMBO KAMA HAYA YALIYOFANYWA KWA DR ULIMBOKA, I THINK THEY HAVE TO CHANGE THEIR TECHNIQUES; NI ZA KIPUUZI HADI WATOTO WADOGO WANAJUA?MMH, SERIKALI LAZIMA IWAJIBIKE !”YOU KNOW IT”! KWA MPANGO HUU, VYOMBO VYA USALAMA VYA NCHI VINAHITAJI MAPINDUZI KABISA!

   JOHN

   June 28, 2012 at 10:22 AM

 118. Jamani kwa nn lakini watu hawana utu, kama hao waliompiga Dr. Ulimboka, tegemeo lao lilikuwa kumuua ila mungu ni mwema Dr. bado yupo. Ila mungu atawafichua wale wote waliofanya unyama huo. Hata sisi watanzania tumeumia sana hivyo katika kila imani tutaingia katika sala na Mungu atampa nguvu ya kuweza kuwatibu watanzania. Eeee Mungu tunaomba unyooshe mkono wako kwa wale madaktari wanao mtibia Dr. Ulimboka uponyaji wako ukafanye miujiza na wote wapate kukutukuza, Amina

  Catherine

  June 28, 2012 at 10:11 AM

 119. This is terrible. Hurting to the extent that a normal person just cant take lightly. Serikali izungumze upesi kuhusu ukweli wa jambo hili. Na sijui watafanya nini kutuhakikishia kwamba hawahusiki! Wasitake damu yetu imwagike kabla ya wakati wake. The government is badly hurting us ila bado tulikuwa na uvumilivu kidogo. BUT TO DO THIS….. IFANYE HARAKA IZUNGUMZE. Alivyo kuwa mwepesi kusema “liwalo na liwe” awe mwepesi tena kulisafisha hili.

  Nyangoe

  June 28, 2012 at 10:23 AM

  • unajua, unaweza kumlazimisha punda kwenda kisimani, lakini kamwe huwezi kumlazimisha kunywa maji, ni kweli madaktari watarudi kazini lakini hawatatoa huduma stahiki, serikali iwe makini,inauma sana kitendo alichofanyiwa ulimboka, naungana na wapenda amani wote kumuombea afya njema, time will tell

   malago mary j

   July 1, 2012 at 12:10 AM

 120. Kwa uelewa wangu mdogo, ‘AMANI’ ni tunda la ‘HAKI’. Hatuwezi kusema kuwa tuna amani endapo haki za msingi haziwezi kupatikana. Je, ni kweli kwamba amani haitopatikana ila kwa ncha ya upanga? Vitisho hivi mpaka lini? Je, watatishiwa wangapi? Unaweza kumnyamazisha mtu na si fikra au mitazamo. Kwa hili umma unahitaji majibu sahihi toka kwa serikali yenye haki na wajibu wa kulinda raia na mali zao na si vinginevyo.

  Kisinda

  June 28, 2012 at 10:35 AM

 121. kwa kweli utawara huu haujawahi kutokea. God have mercy on us. ni hatari sana

  Mena

  June 28, 2012 at 1:44 PM

  • wote wan makosa hatuwezi kuilaumu serikali moja kwa moja hapa tuache siasa tuangalie kwanza, hw many people die, kwa ajili ya mgomo wa madaktari alafu tujue kabisa kwamba wanaokufa pale ni masikini sio viongozi na sio CCM wala CHADEMA RAIA WOTE WENYE ITIKADI KISIASA NA WASIO NA ITIKADI ZA KISIASA WATOTO NA WAZEE then wewe sio daktari wa serikali unashabikia vitendo ya kwamba madaktari wa serikali wagome ambao wanatibia masikini alafu raia wasichukue hatua my uncle amekufa siku tatu baaada ya mgomo pale muhi2, TUULIZANE DR ULIMBOKA NI DAKTARI WA HOSPITALI GANI?

   MPIGANIA HAKI

   June 28, 2012 at 6:37 PM

   • Safi. Mawazo mazuri. Huu ndo ukomavu japo wengine hawataki kuelewa.

    Gidion Mwaki

    June 29, 2012 at 5:34 PM

 122. Tumsifu Yesu kristu kwani yeye ndiye aliyemfanya Dr Ulimboka tumsikie japo kwa shida kwani angekufa Watanzania tusingelijua chanzo cha matatizo, na kwahili tukio Watanzania wote tuandamane hadi ikulu na ikiwezekana Mh. Rais Kikwete kutetea hoja ama maelezo ya waziri wake mkuu(Pinda) kuwa LIWALO NA LIWE KATIKA MGOMO WA MADAKTARI.

  Innocent Minja

  June 28, 2012 at 2:45 PM

 123. tatizo la watanzania ni mawazo mafupi, hivi mnavokurupuka na kuilaumu serikali yenu mshafanya uchunguzi mkaujua ukweli au mnaota tu??? hata watu wenye wanajiita wasomi bado tu wanapapatika kama wajinga… fanyeni uchunguzi then toeni lawama… dr. ulimboka tunamuurumia kapwata na tatizo hilo tunampa pole lakini mnafahamu ni nani yuko behind this au kwakua yeye ni kiongozi wa madokta na madocta wanabifu na serikali ndio mnajisemea tuhovyooo?// lipi jema kwenu? serikali ipi ilikua nzuri kwenu? ya nyerere iliyo wajaza ujinga au ya kikwete aliowatoa shimoni… AMKENI..ACHENI LAWAMA ZA KTOTO..

  Hola Kipapa

  June 28, 2012 at 3:33 PM

 124. INAUMAAA JAMAAN UDICTETA TAYARI USHAINGIA TZ ONA HAHA WARZ MKUU NILITEGEMEA AHUUZUNIKE YEE NDO ANASEMA LIWALO NA Liwe? injurI real an injury to one is an to all

  mando wasp

  June 28, 2012 at 3:43 PM

 125. NADHANI KUNA HAJA YA WATANZANIA KUIWAJIBISHA SERIKALI KWA KILA WALIFANYALO, KWANI NI SUALA LA AIBU SANA KUPUUZIA MADAI YA MSINGI YA MADAKTARI

  KORIWAWA

  June 28, 2012 at 6:02 PM

 126. Enyi mafisadi wapuuzi mmefikia hatua ya kufisadi hata uhai wa raia wema?asasi za kimataifa za haki za binadamu(AMNEST) ingilieni swala hili ikiwezekana wawekeeni vikwazo kutibiwa kwenye nchi zenu wafe kama maskini wanavyokufa coz wanatumia hela za maskini kupanda ndege kila kukicha na kuwauwa wanaodai haki zao.mtatuuwa na kutunyanyasa mpaka lini enyi wadhalimu?

  Grace

  June 28, 2012 at 9:58 PM

 127. kweli hii ni noma,ni sawa na kumkabidhi fisi bucha alafu useme eti linda,hivi tangu lini mtu aliefanya kosa akaambiwa kulichunguza kosa lake?TAYARI DR.AMESEMA AMEPIGIWA SIM NA USALAMA WA RAIA,Jina kapuni,akachukuliwa na wenzake kuachwa huru,TENA HATUA ZIANZE KUCHUKULIA KUANZIA YULE ALIE MUITA PEMBENI KUONGEANAE,SASA IWEJE hao hao tena wapewe kuchunguza,je inaleta maana?nukuu pale alipoojiwa na wale human rights,mi naona wazo alilotoa mr.zitto ni la msingi sana waletwe wataalamu kutoka nje ili wafanye hiyo kazi ya uchunguzi na sio kujidanganya kwa kulipana ela za uchunguzi angali watu tunazidi kuumia hali inazidi kuwa mbaya tz,maisha ni magumu sana NA HATUJUI HATMA YETU WATANZANIA.KESHO YETU NI NINI? NCHI YETU SASA INAKWENDA WAPI?

  mamatina

  June 29, 2012 at 1:53 AM

 128. NI UKWELI USIOPINGIKA KABISA SEHEMU YOYOTE DUNIANI WANAPOTOKEA WATU WA KUDAI NA KUIPINGA SERIKALI WATU HAWA HUFANYIWA VITENDO VIBAYA IKIWEMO KUTESWA,NA HATA KUUAWA! TUNAMKUMBUKA VZR MWL NYERERE AU NELSON MANDELA NA WENGINE KATIKA HARAKATI ZA KUDAI UHURU? TATIZO WATANZANIA WENGI HAWAJUI HISTORIA NDO MAANA WENGI WANAJIROPOKEA TU NADHANI UMEPATA PICHA! LIKINI IKUMBUKWE KUWA KAMA NI SERIKALI AU NI WAHUNI BASI WATAHUKUMIWA VIVYO HIVYO KAMA WALIVYOMFANYIA DR ULIMBOKA.TUNAMUOMBA MUNGU AMPONYE HARAKA MUNGU IBARIKI TZ,MUNGU MBARIKI DR ULIMBOKA NA MUNGU UWABARIKI MADAKTARI WOTE! SOLIDARITY FOREVER!

  john juma.

  June 29, 2012 at 4:38 PM

 129. Mie bado naona ipo haja hasa ya kutumia vyombo vya kimataifa kuchunguza hasa nini dhamira ya kweli ya wale wote waliohusika na tukio hili bila kujali cheo cha mtu. Kila mmoja baada ya uchunguzi ripoti imwagwe hadharani na mkondo wa sheria uchukue hatua yake. Tuliona nchi kama korea wakati fulani rais wao alishtakiwa na kufungwa jela. Hili likishaeleweka vyeo vya watu viwekwe pembeni.

  Mwl. Emanuel

  June 29, 2012 at 6:27 PM

 130. Jambo jingine kaka Zitto hebu tusaidie kwa kina madai ya msingi ya madaktari kwani watu wengi hatuelewe na tunapotoshwa na kupotoshana.
  Ungetuwekea bayana kisha hawa wanaojadili idadi ya watu wanaokufa waone je madai haya ni ya msingi au hayana msingi? Nimejaribu kufuatilia kwa Serikali inasema tu madai yao tunayashiughulikia laikini haiweki wazi ni yapi? Je hayo waliyoyashughulikia ni kwa kiwango gani? Tunaochangia tutaangalia je kuna uhalali gani na uzito wa haya ni upi? Ni tuwe na mwelekeo upi sasa?

  Mwl. Emanuel

  June 29, 2012 at 6:31 PM

  • Daktari ni kama wakala wa government katika kutatua matatizo ya kiafya ya watanzania,kama Daktari hatawezeshwa na government kiukamilifu katika kutatua matatizo ya wagonjwa basi ana haki ya kurudi kwa aliemtuma(serikali) na kama wasipoelewana ana haki ya kuachakufanya kazi ili kuishinikiza impatie vifaa na mahitaji muhimu ya kutibu watanzania::Watanzania tunajukumu la kuungana na wahudumu wote wa afya kuiambia serikali ambayo inawajibika kwetu directly…Hata madaktari wakirudi kazini bado wagonjwa wataendelea kufa kwa kukosa (madawa,oxygenated machines na vifaa vinginevyo)….Madaktari wengi waliogoma wameshasaidia na kutibu wagonjwa kwa muda mrefu iweje leo waonwe wasaliti?? siamini kama mabadiliko huja kirahisi we have to take risk smtimes for the betterment of our new generations..hakuna daktar anayependa kuona mtu akifa,daktari amesomea kutibu na sio kuua..Watanzania tuelewekuwa tuna haki ya kudai Hali nzuri za mazingira ya kazi kwa Madaktar wetu,waalimu,wanasheria na wanataaluma wengine ili tuweze kupewa huduma nzuri nailo litakuja pale tutakapoamua kuiambia serikali na kuiajibisha pale itakaposhindwa…tusiongozwe na emotions maana hazitasaidia..madai ya madaktr,waalimu na wanataaluma nyingine ni ya muda mrefu na yanatekelezeka na niwajibu wa serikali yetu kutekeleza kwa kuwa inawajibika kwetu..kumbuka madaktari ni mawakala tu

   phai

   June 30, 2012 at 11:33 AM

 131. mi naamini ulimboka kapigwa na wale wanaofanya kuwa vitendo vya vurugu ni msingi wa hoja zao ili wapate cha kukosoa serikali.. enzi za nyerere watu hawa walinunua bidhaa na kuzificha ili serikali ionekani haiwahudumii raia. zitto sio msahafu ambao una ukweli daima.. maneno yake yanatia shaka… nakumbuka lema baada ya kuchoka kupiga watu kwa siri alithubutu kutaka ufungwe mlango wa bunge ili wapige watu live.. zitto kama anapenda amani mbona hakukosoa.? anajua kinachoendelea asituzuge..

  mickey

  June 30, 2012 at 8:38 AM

  • Brother Mickey unakaribia kuufichua ukweli. Na kuna watu wanakurupuka tu humu kutoa hukumu ambazo hazina utafiti!! Naomba waache siasa za uzushi!!

   Moh'd

   July 2, 2012 at 12:05 PM

 132. Serikali yetu ni madicteta wakitaka wanifuate. sitto komaa mwakani wewe utakuwa kiongozi wetu

  Marine steveni

  June 30, 2012 at 9:11 AM

 133. its not democracy our goverment must be responsible for that issue

  scolla

  June 30, 2012 at 9:25 AM

 134. Hapa lazima serikali inyoshe maelezo kwani namna tukio lilivyotokea,na mazingira yanaigusa mojakwa moja ingawa si hukum kuwa serikali imehusika,lakini mazingira ndiyo yanafanya wananchi wasiwe na imani na serikali.Tunachoomba tumehuru iundwe na kufanya kazi bila kuingiliwa.Kama mtu ukidai haki yako unageuka kuwa adui basi tufanye nini sasa ili tupate haki zetuuuu? hili halikubaliki kabisa.Tunataka haki itendeke katika kufanya upelelezi.

  Robert Mwambozi

  June 30, 2012 at 7:34 PM

 135. Majibu ya nani mtesaji-muuwaji, mwenye busara hahitaji kuudhani wala kuuliza. Kiburi cha Chinjachinja huyu kitakumaliza kupitia vifo vyo wagonjwa ambao sasa hawapati matibabu. We need paradigm shift!

  mama harakati

  June 30, 2012 at 10:49 PM

 136. jamani tuache ushabiki madaktari wana madai ya msingi tambueni wengi wao vijana wamesoma kwa mkopo hivyo wana madeni na mazingira ya kazi is worse…FIKILIA DAKTARI ANAPOKEA MAJERUI WA AJARI WAKATI MWINGINE WALE WAZALENDO HUTOA PESA ZAO WALAU KUWAPATIA CHAKULA

  ABBY

  July 1, 2012 at 12:05 AM

  • Hospitali gani hiyo Dr. anatoa pesa yake? Huku ndiko tunakosema kukurupuka na kudanganyana. Kama hamna cha kuchangia humu mtandaoni bora mnyamaze, msitutie machungu zaidi sisi wenye wagonjwa hospitalini lakini hawajaonwa na Dr. kwa wiki 5 achilia mbali kuhudumiwa. Hapo ni Muhimbili Dr. ni mungu, haonekani mpaka muwe na appointment pembeni huko ndo amuone mgonjwa wako. Inasikitisha sana.

   Gidion Mwaki

   July 2, 2012 at 2:38 PM

   • Gid,wewe ndiye unadhani kuwa hukurupuki?unafikiri madaktari hawasomi kwa mikopo vyuoni?wewe ndiye unadanganywa na unaleta hisia zako kuwa madaktari ndo wamemwachaniza mgonjwa,unadhani kama hospitali zingekuwa na vifaa vya kumtibia wote sisi makabwela tungejazana muhimbili?nadhani matatizo hayo aliyonayo mgojwa wako na wagonjwa wengine yangeishia hospitali za kawaida tu.kuna kila haki ya madokta kudai serikali kuboresha mazingira ya kazi.ukitaka kujua nenda ward ya wazazi uone mama zetu wanavyolala chini.hivi kweli unadhani serikali haina hela ya kununua vitanda vya wagonjwa au kujenga jengo la kulaza wagonjwa muhimbili?unamkumbuka maige amepora pesa kiasi gani na sasa serikali haifanyi juhudi zozote kurudisha pesa hizo zinunue vitanda?wachache wanatumia ujinga wenu kupora mali na kujinufaisha huku wakisahau mambo ya msingi.unajua kuna madiwani wangapi tanzania na wameongezewa posho kiasi gani na kwa kazi ipi kubwa kuliko wafanyayo madaktari hata wasisikilizwe?unajua ni kiasi gani mawaziri wanalipwa?hela ya rada iliyorudishwa toka uingereza isingeweza kununua vifaa vya tiba na unadhani imetumika vipi wakati serikali haikuwa na tegemeo la kipata?baada ya kuipata hela hiyo kwa nini haikufumba macho na kuiingiza katika kuboresha hospitali zetu?mimi nadhani unapaswa ukae chini uitafakali serikali yako kwanza kabla ya kuwalaumu madaktali ambao wamekuwa wavumilivu toka tupate uhuru hadi hii leo wagome ujue wamezidiwa.siasa isikupotoshe ndugu,unajua watu wanaweza kukushangaa sana brother.

    mortone

    July 2, 2012 at 3:03 PM

  • abby hebu tuhakikishie jinsi ambavyo tunalipa hizo fedha za mikopo coz mi sioni km nalipa!….acheni utani jamani watu wanakufa na wengine wanapata vilema vya maisha coz ya huu upuuzi wa madaktari kugoma. 7 mill wanazohitaji hawa madaktari si waende huko zinakopatikana. wanaoteseka ni ndugu zetu na masikini wenzetu..

   khaundinkhotse

   July 2, 2012 at 11:48 PM

 137. Busara na utulivu ni muhimu sana ktk kutatua mgogoro huu baina ya serikali na madaktari

  jimmy c

  July 2, 2012 at 7:42 PM

 138. Jamani ndugu zangu! nafikiri hamjaelewa madai ya madaktari. jaribuni kutafuta ukweli ndiyo mtaona ukweli ulivyo. msione kuwa ni hela tu ndiyo madaktari wana ng’ang’ania la hasha!!, Kuna vitendea kazi ambavyo ndiyo muhimu kuliko vyote. Si wengi wenu mnaona kuwa utaambiwa uende hospitali nyingine ambayo ina vyombo upime halafu umletee daktari majibu aweze kukuandikia dawa stahili ya ugonjwa wako? Haya ma trilioni ndiyo daktari anayapigania ili wananchi waweze kusaidika. Msichukuliwe na mawimbi ya siasa but look at the reality!!!!!! hakuna haja ya Daktari kukuandia dawa isiyolingana na ugonjwa wako. Msaidieni afanye uchunguzi wa kina kwenye ugonjwa ndiyo akupe dawa halisi. hata yeye anaona uchungu sana. Wote ni binaadamu na nafikiri wanajue mengi yanotendeka kuliko mie na wewe. Mimi nawapongeza kwani kila jambo la kheri lina madhara na faida zake. Hivyo tumwombe mungu yaishe salama. Kwa kauli ya Rais ni mbaya na nafikiri awe mtu mwenye hekima kuliko mabavu. Yeye kama kiongozi asingetoa kauli kama hiyo!!!!! Ati Asiye taka na ajiondoe mwenyewe!!!!!!!!!! Hakuna sababu ya kuandikiana na kujibu Barua. Kwa hakika wanao mpa advise wanampatosha!!!!! Nimasikitiko makubwa sana. Hebu tu atueleze hizo hela za kuajiri madaktari wengine atazitoa wapi kwani kuajiri Dr from anywhere, Tanzania itlipa maradufu. Hivi ni nyumba ngapi anazowalipia madkatari? Nafikiri huu ni ufinyu wa fikra. Ushauri wangu ni kuwa tusilaumu madaktari kabla ya kujua ukweli wa jambo. Pia naomba Serikali itamke wazi madai yote ya madaktari na yapi yaliyotekelezwa. Ni kweli tunavyosema kuwa madaktari walikula kiapo Je Kiapo cha kukaa bila ya kuwatendea haki watanzania? wana wapigania watanzani na siyo maslahi yao pekee. Lini mtu akaenda shamba bila ya Jembe. Msituletee sera ambazo hazina maandlizi ie Kilimo. Huna shamba, kwani yamepewa matajiri/ wawekezaji. Maji hakuna, vifaa hakuna, ie tractor and yet unataka kilimo? kila leo walioiba kuku ndiyo makafara Hahahhahaaaaaaa!!!!!! walibobea wanatesa na vijisenti vyao. hata wakiugua wanapelekwa nje. Jamani nafikiri tuone kuwa sasa hakuna jipya tunaloweza kupata. Tuamke na tuone kuwa tumechelewa sana. Mie siyo mshabiki wa chama lakini tunasikia na tunaona. Poleni sana madktari na Walimu wote. Tumwombee mungu Dr Uli na tumtakie maisha marefu. Wenye nchi tumieni hekima!!!!!!!

  Pili nawaomba wabunge muendapo mbungeni msianze malumbano kama Alivyofanya Eng. Manyanya!!!!! Tumia Busara dada!!!! Ni kweli wewe ni msomi lakini ulikuwa huna haja ya kusema wewe ni msomi. Unatupozea muda wa bunge! nawapongeza vyama vya upinzani kwani mnyoyafanya ni mema na Mungu awabariki na kuwalinda.

  Lilian K

  July 3, 2012 at 2:07 PM

 139. ni suala la kuwepo tume huru kuchunguza sakata hili,kwani hadi sasa kila kitu kinachozungumzwa ni hisia tu,tusubirini tuone na kusikia then tutapata pa kuanzia,muhimu tumuombee Dk. Ulimboka apone nafikiri atakuwa na mengi sana ya kutueleza watanzania na dunia kwa ujumla

  Francis

  July 9, 2012 at 1:00 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: