Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Maelezo ya Bajeti Kivuli

with 3 comments

Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.

  MAPATO

SHILINGI MILIONI

A Mapato ya ndani

 

11,889,078

  i)mapato ya kodi (TRA)

10,232,539

 

  ii)Mapato yasiyo ya kodi

1,163,533

 

B Mapato ya Halmashauri

493,006

 

 Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.

Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.

Kabwe Zuberi Zitto,Mb

Waziri wa Fedha na Uchumi Kivuli

19.06.2012

 

Zitto akiwasili Bungeni kwa ajili ya kwenda kuwasilisha bajeti ya upinzani

 

Zitto akiwasilisha hotuba ya bajeti kivuli

Advertisements

Written by zittokabwe

June 19, 2012 at 4:50 PM

Posted in Uncategorized

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Mmesameheka, lakini mara nyengine pateni muda wa kuhariri ili msitoe “mwanya wa mashambulizi”.

  HAMISI

  June 19, 2012 at 4:56 PM

 2. Jitahidini kuwamakini sana maana hilo nidio na mkumbuke kuwa kibaya huvuma zaidi kuliko kizuri.

  Enock

  June 19, 2012 at 5:54 PM

 3. wakati mwingine tuoneshe umakini kama chama chetu baba. Ila watanzania ni waelewa na tunaelewa error na fraud usijali kabisa baba.

  tari

  June 22, 2012 at 5:38 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: