Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Uchambuzi/Analysis: Bajeti ya Madeni

with 20 comments

Bajeti ya Mwaka huu 2012/2013 ni Bajeti ya Madeni

Serikali inapendekeza Bajeti ya TZS 15 trilioni(USD 8.75 Billion) katika mwaka 2012/13. Uchambuzi wa vitabu vya Bajeti unaonesha kwamba mafungu ya juu 5 kwenye Bajeti ni Kama ifuatavyo;

1    Huduma kwa Deni la Taifa          Tshs 2.7 trilioni(USD 1.69 Billion)
2    Wizara ya Ujenzi.                          Tshs 1 trilioni (USD 625 Million)
3    Wizara ya Ulinzi                          Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)
4    Wizara ya Elimu                              Tshs 721 bilioni (USD 451 Million)
5    Wizara ya Nishati na Madini    Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)
 TOTAL                                        TZS 5.982 Trilioni(USD 3.74 Billlion)
Chanzo: Vitabu vya Bajeti kwa Wabunge

Jumla ya mafungu haya ni sawa na asilimia 40% ya Bajeti. Kwa hiyo asilimia 40% ya Bajeti yote imepangwa kwa mafungu 5 tu. Fungu lenye kiwango kikubwa zaidi ya Bajeti kuliko vyote ni fungu 22 ambalo ni malipo kwa Deni la  Taifa. Pia sehemu kubwa ya fedha zilizotengwa kwa Ujenzi na Nishati ni madeni kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya miaka ya nyuma.

Hii yaweza kuwa Bajeti ya kulipa madeni zaidi kuliko Bajeti ya kuchochea maendeleo. Bajeti hii pia yaweza pia kuwa ni Bajeti ya kukopa maana jumla ya TZS 5.1 trilioni(USD 3.19 Billion) zitachukuliwa kama mikopo kwa Serikali. Mikopo ya kibiashara ambayo ni mikopo ghali sana itachukuliwa kwa wingi zaidi kuliko mwaka wa fedha uliopita.

Wabunge wanapaswa kufanya uchambuzi zaidi wa Bajeti ya mwaka huu inayopendekezwa na Serikali. Kuna haja kubwa sana ya kuharakisha kuanzishwa kwa Ofisi ya Bajeti katika Bunge na Kamati ya Bunge ya Bajeti ili kuweza kufuatilia kwa karibu, kuchunguza na kutoa taarifa kwa wabunge ili kuwezesha kuboresha Bajeti.

Misamaha yote ya Kodi na Madeni yote ambayo Serikali inaingia inabidi sasa ithibitishwe na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi ili kuongeza udhibiti na usimamizi wa Misamaha ya Kodi na pia Deni la Taifa.

20 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. kaka ki ukwel hayo madeni ni meng sana

  lambarty andreson

  June 7, 2012 at 12:10 PM

 2. Watanzania tuamke na kujihoji je bajeti hii ikipitishwa itakusaidiaje kujikwamua na kudhibiti mfumuko wa bei.

  Robson

  June 7, 2012 at 12:18 PM

 3. This is ridiculous..tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Deni la taifa limeongezeka mara mbili in one year and yet there’s no positive impact on the budget. NAKUUNGA MKONO kuwe na special audit kwenye akaunti ya deni la taifa,hapo kuna uozo umejificha mkubwa.

  Yudatade Sylvester

  June 7, 2012 at 12:18 PM

 4. Haistahili kulaumiana kwa serikali kupanga Bajeti kubwa kwa ajili ya Kulipia Madeni kwani, fedha zilizokopwa zilitumika kwa ajili ya Maendeleo ya Watanzania hivyo tusipoanza kulipa sasa, itakuja kutugarimu baadae kutokana na deni kuwa na riba kubwa.

  Dennis MpendaMungu

  June 7, 2012 at 12:19 PM

 5. Ni wazi kwamba kunatakiwa kuwepo uchambuzi makini wa bajeti kutoka kamati ya bunge,kama haipo kamati ni muhimu iundwe kwa7bu bajeti hii hailingani na mapato yanayokusanywa na isitoshe katika uandaaji lazima kuna uchochoro, naamini hailingani na rasilimali za taifa.Hivyo wabunge 2nawaomba muwe makini kwa7bu wananchi ha2ridhiki na kiwango hiki kidogo mno.

  HENRY SUMARI

  June 7, 2012 at 12:33 PM

 6. hivi tunaweza kumaliza deni kweli kwa hali hii inaonesha kiasi cha kukopa ni kikubwa kuliko cha kulipa so deni linaongezeka hii nchi miaka mitano ijao itauzwa tutakuwa wakimbizi kwenye nchi yetu nyie wenye madaraka ndio wakutukomboa maana sio wananchi wote wanajua haya.

  lukuni

  June 7, 2012 at 12:42 PM

 7. KAMANDA BIG UP SANA KWA VIPAUMBELE VYAKO:NA JARIBU KUTILIA MKAZO RELI YA TABORA -MPANDA NA TABORA-KIGOMA MAANA ITAJIBU SUALA LA USAFIRI MAENEO HAYO FIKIRIA HAKUNA BARABARA INAYOUNGANISHA KALIUA NA MPANDA PIA ITATOA FURSA 2089 ZA AJIRA YAANI WAHASIBU,MAINJINIA,MAKAGO,MAMANTILIE,MADUKA NA BODABODA LAKINI PIA SHIRIKA LA RELI LIMILIKIWE NA SERIKALI NA SIYO MUWEKEZAJI KWASABABU HAKUNA MUWEKEZAJI ANAYEPENDA KUONA TZ INAPANUA UCHUMI WAKE MAANA USAFISHAJI NI NGUZO MUHIMU KATIKA KUINUA UCHUMI.PILI, DENI LA TAIFA LICHUNGUZWE IKIWEZEKANA WEKENI UTARATIBU WA RAIS KUKOPA LAZIMA BUNGE LIPITISHE MAAMUZI HAYO KWA KUZINGATI SABABU ZA KUKOPA NA UTARATIBU WA MATUMIZI YA PESA HIYO.ALL
  ZE BEST KAMANDA

  PAUL JINERY

  June 7, 2012 at 12:57 PM

 8. me naona kabla yakuanza kusoma budget mpya mawaziri waseme budget hiliyopita wamefanikiwa kiasi gani kwenye malengo yao waliojiwekea na nn sababu hiliyofanya washindwe kufikia malengo hilitujui kma ni serikali imeshindwa kupeleka hela kwa wakati au ni watendaji wanzembe maana me naanza kupata mashaka kuwa tunaweza tukawa tunasomewa budget ya figure in reality hakuna fedha ambazo zinapelekwa sehemu husika kwa wakati mh. tunaomba ufutilie hili swala maaana kunambunge mmoja last time alikuwa hanacomplain kwamba fedha azipelekwi kwa wakati nahata zikifika haziwi zile zilizohainishwa kwenye budget it means zinaenda pungufu thats why wanashindwa kufikia malengo haya ni maneno ya mbunge wa bahi omary badwel kwenye budget hiliyopita.
  hebu tujiulize ndugu zangu last budget magufuli alipewa fungu kubwa sana pamoja na kawambwa sasa walifikia malengo kwa asilimia ngapi kabla hatujawapa fedha nyingine hii itasaidia kuona ufanisi wa matumizi ya fedha zetu halafu hile budget ya ndugu yangu wa mega Walt imefikia wapi na mpango wake wa dharula maana nasikia tena taifa litaingia kwenye mgao nataka kufahamu nani ambae amefanikiwa katk kuongeza mega walt kwenye grid ya taifa nssf, aggreko, nawenzake wamefikia wapi maana miradi hiilikuwa mingi sana.

  honoli mlandali

  June 7, 2012 at 12:58 PM

 9. Mambo yanazidi kuwa magumu

  Emily eliuta

  June 7, 2012 at 2:29 PM

 10. So now’ mkiwa kama wabunge na wazalendo wa hii nchi pia mnatuwakilisha sisi basi fanyen mwezalo kuokoa jahaxi, tafaadhal

  Emily eliuta

  June 7, 2012 at 2:36 PM

 11. Kwa bajeti hii umasikin unaweza kupungua

  Amos ngoli

  June 7, 2012 at 2:47 PM

 12. kweli kabisa hayo mapendekezo ni muhimu sana, ukizingatia watakaokamuliwa na deni linazii kuwa kubwa miaka nenda tax payers ni wananchi ningependa kujua serikali hii tangu ingje madarakani imekopa kiasi gani?na imerudisha kiai gani, hii mikopo ya kibiashara ambayo ina interests kubwa sana kwa kweli ni mzigo mkubwa sana kwa taifa,sasa ni wakati wa chadema kujikita strategicallly zaidi ktk uchumi kuwaelimisha wananchi jinsi chama tawala kinavyoendesh uchumi wake kukopa sana,matumizi makubwa yasio na tija yanavyozidi kuitumbukiza nchi na uhuru wetu hatarini kama sio kuiweka rehani.Kampeni ziwe zaidi ktk uchumi.

  ..

  david rugemarila

  June 7, 2012 at 3:22 PM

 13. Wabunge kumbukeni nyie ni wawakilishi wa wananchi tunaomba muamue mambo kwa busara yaani pumba na mchele vitenganishwe! Keep up Zitto kwa kutupa taarifa za maendele6 ya nchi yetu.

  Susan

  June 7, 2012 at 8:22 PM

 14. Mh.Tunashukuru kwa kutuelewesha juu ya mwenendo wa bajeti 2012/13. Hilo deni la Taifa linatisha, mbona haliishi?Serikali ifanye mikakati kuhakikisha kuwa uzalishaji unakua na kuuza bidhaa kwa wingi nje kuliko kuagiza bidhaa nyingi kutoka nje kwa gharama za juu.Ili uzalishaji bidhaa uweze kuwa wa tija ni lazima viwanda ambavyo vimelala vifufuliwe ili vianze uzalishaji na kukuza uchumi wa nchi.Kufufuliwa kwa viwanda kutawawezesha wananchi wengi kupata masoko ya mazao yao kama vile pamba,mkonge,miwa,kahawa na mahindi ambalo ni zao linalozalishwa sasa kwa wingi hapa nchini na kulifanya kuongeza kipato kwa wakulima n.k.

  Barabara mbovu ni chanzo kikubwa cha kukwamisha maendeleo ya wananchi vijijini kwa maana ya kwamba wakulima huko vijijini wananashindwa kusafirisha mazao yao kuyatoa huko mashambani mpaka maeneo ya masoko.Jambo hili huwafanya wakulima waibiwe na walanguzi wachache kwa bei ndogo wakati wanauza kwa bei kubwa tena bila kulipa kodi.Hivyo iwapo miundombinu ikiboreshwa vijijini na kupatikana nishati basi umasikini Tanzania itakuwa historia

  Jospide Majaba

  June 7, 2012 at 9:52 PM

 15. Je kuna haja ya kuongeza hayo au inatakiwa tuongeze tuu ukali ili kuongeza uwajibikaji katika serikali na mashirika yake ya umma? Ninafikiri kuongeza chombo kingine pale bungeni ni kuongeza urasimu ambao mara nyingi gharama yake ni kupoteza muda mrefu ktk kushughulikia jambo. So Zito mi nafikiri tuendelee kufanya uchambuzi na kupiga kelele ktk uozo wa serikali ili hatimae watanzania wote tupate mwamko. Mwamko utasaidia ufuatiliaji kufanyika ktk ngazi ya halmashauri zetu kupitia madiwani wa kila kata.

  Onesmo John

  June 8, 2012 at 11:13 AM

 16. Hali hii inaonyesha jinsi Serikali isivyo kusanya kodi vizuri, ina maana mapato ni madogo kuliko matumizi. TRA ifanye kazi yake ipasavyo, na kila Wizara yenye mamlaka ya kuiingizia serikali mapato ifanye hivyo kama ilivyoelekezwa.
  Pia matumizi mengine yasiyo ya lazima yaepukwe, mfano utakuta mtu anapelekwa mahakamani na escort ya magari matano huyo ni mtu mmoja tena hata hajaonyesha dalili yoyote ya kukimbia lakini ukipiga gharama inayotumika ni nyingi, hivyo viongozi wote wajaribu kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.
  Haitasaidia kusema maV8 yasinunuliwe wakati yapo magari mengine ya serikali pia yanatumiwa hovyo.
  Pia ina kera Tanzania kuomba omba misaada hivi hatuwezi kujisimamia wenyewe? matokeo yake tunatoa hata vitu vyetu kama vile Marekani ilivyopewa anga bure jamani Tanzania i dont know where are we going. Imagine tumeruhusu mtu akae kwenye anga letu muda atakaojisikia without asking hivi akitugeuka si anatupiga na kutumaliza kwa dakika?
  Mh. Zito tusaidieni hata mkipewa vyeo vikubwa visiwazibe midomo ila msisahau kusali maana mh! yahitaji maombi mazito ya ulinzi otherwise mh!

  Nice M

  June 8, 2012 at 2:38 PM

 17. kimsingi sishangai ukubwa wa deni nikizingatia historia ya taifa letu tangu miaka ya 80 kwenda mbele. nina mashaka na bajeti hiyo kuwa safari hii itamtoa vipi mkulima wa alizeti kule mudida singida au mkulima wa mihogo kule umatengoni songea, infact sioni kuwa atapita vipi kwa hii bajeti. wafanyakazi nao wataishia na maisha yale yale ya kufanyiwa promotion ya kukopa katika mabenki na bayport , maisha yatazidi kuwa magumu, mmachinga asitegemee kitu hapo,labda kidogo wenye biashara za kueleweka,kila kukicha tunaambiwa tufunge mikanda,imefikia mwisho hatuwezi tena.ni muda wa kutafakari upya.

  issa khatibu

  June 11, 2012 at 7:02 AM

 18. hii bajeti hana nia kabisa ya kumtetea mnyonge

  Emil

  June 15, 2012 at 6:09 PM

 19. Kwa sasa sitachangia kuhusu bajeti, ila nachukua nafasi hii kumpongeza aliyeanzisha blog hii kamanda wetu Ndugu Zitto Kabwe. Nawapongeza pia wadau wote wanaotumia blog hii katika kubadilishana mawazo juu ya mustakabali wa maisha yao katika nchi yao. Tukiweza kuwashawishi marafiki zetu walau hata kumi tu kujiunga na mtandao huu, ni dhahiri kuwa tutakuwa tumefanikiwa kutoa elimu kwa watanzania walio wengi kupitia mijadala mbalimbali tutakayokuwa tunafanya humu.

  Asanteni na Mungu awabariki nyote.

  Onesphor Mbuya

  June 15, 2012 at 11:44 PM

 20. Serikali mbovu,viongozi wabovu!mikataba mibovu!mipango mibovu! Tunaitaji mabadiliko!

  Yegoo

  December 28, 2012 at 9:27 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: