Statement: Vurugu za #Zanzibar
1 .Vurugu za Zanzibar ni ‘unwanted distractions’ katika mchakato wa kuandika katiba mpya.
2. Hakuna namna vitendo hivyo vinaweza kuhalalishwa na kutetewa lakini ni matokeo ya muda mrefu ya ‘superficial attempts at dealing against group with ulterior motives.
3. Rais Ali MohamedShein aunde kikosi kazi maalum kwa ajili ya kudhibiti vurugu hizo,na kuanza mzungumzo na pande zote.Hiki sio kitendo cha kudharau kabisa.
4. Muungano wetu ni sacred na tumetoka mbali kushindwa sasa kuulinda, ‘not when we are so close at having an everlasting formula’.
5. Waliochoma nyumba za ibada wasakwe na kufikishwa mbele ya sheria mara moja. Tusiruhusu hata kidogo wapuuzi wachache kutuingiza katika vurugu za kidini ili kufikia malengo yao ya kisiasa.
6. Zanzibar Political leaders and public opinion makers must engage the Zanzibaris into a serious and objective dialogue about the future of Zanzibar within or outside the Union.
Written by zittokabwe
May 27, 2012 at 6:12 PM
Posted in Zanzibar
13 Responses
Subscribe to comments with RSS.
Naungana 100% na mapendekezo yako
Lyimo
May 27, 2012 at 6:53 PM
Ni kweli,hili ni kundi la wahuni wachache.Serikali lazima iwe kali kukomesha vurugu hizi.
David V
May 27, 2012 at 7:16 PM
RAISI wa Zanzibar aunde kikosi kazi kwa haraka na cha watu makini kuchunguza hili,maana linataka kutupeleka kwenye udini
Dickson Minde
May 27, 2012 at 8:20 PM
Thanks Zitto. (I am not being disrespectifull for addressing you in your first name). I know where we are coming from, for the Zanzibar revolution occured a few day afer my arrival for my first time/job. Our leaders who signed the Union documents must be turning in their graves. Am sure none of them expexcted 50 years later their of springs would riot, calling for religious bigotry, etc. All Tanzanians should spek out against such happenings.
Dominico KABYEMERA
Dominico Kabyemera
May 27, 2012 at 11:12 PM
Nakubaliana na wewe muheshimiwa…hakuna lakini hapa. Hili ni tendo la ugaidi
Tengo Kilumanga (@tengo_k)
May 27, 2012 at 11:02 PM
Hawa watu wasifumbiwe macho hata kidogo ingekuwa wakristo ndio watendaji wa huo uupuzi ingekuwa tayari wameshachukua hatua kali lakini lakini kwa sababu ni wao serekali bado inakwenda taratibu
mashel
May 28, 2012 at 8:13 AM
Nakushukuru kuona zanzibar kuwa kunahitajika maongozi ya mustakbal wa kitaifa ! kwa utafiti wangu mdogo wa ilmu nakwambia zaid ya 66.6 % hawataki muungano!
Abousalah
May 28, 2012 at 1:25 PM
HAYA
Abousalah
May 28, 2012 at 1:56 PM
Lakini kwa nini wazanzibar wasiachiwe nchi yao.we mheshimiwa ulidai katiba mpya bcs haikufanyika kura ya maoni basi hata muungano ni hivo hivyo ni mawazo ya watu wachache wapeni wa znz nafasi ya kura ya maoni kama wanautaka au la
Mfaume
May 28, 2012 at 2:39 PM
Suala ambalo ni la msingi kabisa ni kama hao walioandamana walikuwa wanatoa fikra za Wazanzibar wengi? Maandamano yanaweza kufanywa na watu 1,000 kati ya watu milioni 20 yakaonekana yanawakilisha watu wengi kumbe ni tone katika bahari.
Mimi kwa uzoefu wangu wote nilionao naona tatizo la Muungano sio uwepo wake bali namna ulivyofumwa. Hilo linaweza kuwa tatizo la kibahati mbaya la kihistoria. Ilikuwa ni wakati muafaka kwa sasa kwa ndugu zetu wa Zanzibar na wa hapa bara kujadili kwa kina matatizo ya muungano na kutoa maoni ya namna muungano unavyopaswa kuwa au ulivyopaswa kuwa. Kwa mujibu wa Sheria ya Mapitio ya Katiba hilo limepewa nafasi wazi ya kujadiliwa. Kinachokatazwa katika sheria hiyo ni kujadili uwepo au kutokuwepo kwa Muungano. Katazo hilo kwa maoni yangu ni la msingi na labda lazima tukizingatia kwamba mchakato wa utungwaji wa katiba mpya unafanyika ndani ya Katiba iliyopo. Katiba iliyopo itazikwa baada ya kutungwa na kusainiwa kwa Katiba mpya.
Kwa mujibu wa Katiba ya sasa Tanzania ni Jamhuri ya Muungano wa Zanzibar na iliyokuwa Tanganyika. Tukianza kujadili uwepo au kutokuwepo kwa dola ya Tanzania kama jamhuri ya muungano maana yake hatujadili juu ya utungwaji wa katiba mpya ya Tanzania bali Katiba ya nchi nyingine ambayo itazaliwa baada ya kuandikwa kwa katiba hiyo mpya. Tungetaka kujadili uwepo au kutokuwepo kwa muungano tungeanza kwanza kulijadili hilo na mjadala wa katiba mpya ungertegemeana na hatima ya mjadala wa kuwepo au kutokuwepo kwa muungano. Kama bahati mbaya matakwa ya wengi ingekuwa ni kutokuwepo muungano tungekuwa labla na mchakato wa kutunga katiba ya Tanganyika na ndugu zetu Zanzibar wangekuwa na mchakato kama huo.
Naungana na mheshimiwa Kabwe kwamba muungano ni lulu ya Tanzania. Tunauona hauna maana leo kwa mana upo. Kama bahati mbaya usingekuwapo ndio tungeona makali yake. Ingekuwa na athari kubwa kwa raia wa Tanzania waliofanya makazi yao ya kudumu na shughuli zao kuwa Zanzibar wakati asili yao ni bara na kinyume chake. Ina maana kwamba mzanzibari anayefanya shughuli zake za kimaisha Namanga kesho angeamka na hadhi ya raia wa kigeni anayeishi Dar Es Salaam. Hali kadhalika kwa ndugu yangu mbembe wa ujiji anayefanya shughuli zake za kimaisha huko Kisiwa Nduwi.
George Jinasa
May 28, 2012 at 5:47 PM
Hata tukitetea muungano ni bure ina bidi watu waelimishwe kinagaubaga kwanini tumo kwenye muungano, na yote hujikita katika haki za uraia ambazo zimejikita kimuungano. kwa kufanya hivyo our masses are conquerable
justin mabele
May 29, 2012 at 1:12 PM
Mimi nilikua naona ktk mtizamo wangu wamawazo kwa hakuna haja kuwang’ang’ania ktk muungano maana wao wananchi yao.
Reubeni Mabula
May 30, 2012 at 1:04 PM
Kimsingi zanzibar na Tanganyika sio suala la muungano tena. Muungano uikuwa ni kipindi hicho wakati unaanzishwa.Lakini kwa sasa tunachozungumzia ni Undugu baina ya watanzania waishio Unguja,Pemba,Mafia na Tanzania bara.Ukizungumzia mtu kama mmakonde katika muungano huu ameokea bara lakini huku ni wengi sana wanaendesha maisha yao tangu miaka mingi sana halikadhalika wapo wasukuma, wanyaturu mpaka watu kutoka kigoma wapo huku na Ukiangalia kuna watu wengi sana kutoka pemba na Unguja waishio Bara ukiwauliza suala la muungano watakueleza wao hawaendi popote. Je hiyo Zanzibar ni ya nani wa kumuachia? Mimi nadhani suala sio kuwaachia Zanzibar yao,hao ni wahuni ambao ukichunguza ni vijana ambao hata umri wao hauzidi miaka 30. Tuilinde nchi yetu isije ikawa ndio mwanya wa maadui kupitia huko.
Mgooh
June 1, 2012 at 12:04 AM