CHADEMA USA TOUR
Kesho Jumapili tarehe 27 Mei mwaka 2012 nitakutana na Watanzania wanachama na wapenzi wa CHADEMA wanaoishi Marekani. Mkutano utafanyika katika Jimbo la Maryland kama ilivyokwisha tangazwa hapo awali.
Katika mkutano huu wa kwanza na wa aina yake tutazindua uandikishaji wa wanachama wa CHADEMA kwa Watanzania wanaoishi Marekani. Pia tutazungumza masuala mbalimbali yanayohusu nchi yetu. Masuala ya kwanini nchi yetu haiondokani na umasikini licha ya utajiri wa rasilimali uliopo nchini, masuala ya namna gani tunajiandaa na uchumi wa gesi asilia na nafasi ya Watanzania waishio nje katika maendeleo ya Taifa.
Tutazungumza kuhusu uandikaji wa Katiba mpya na namna haki za Watanzania wanaoishi nje zitakavyoingia kwenye Katiba ikiwemo haki ya kupiga kura na hata haki ya kuwa na Uraia wa pili.
Ninapenda kuwakaribisha katika mkutano huu muhimu sana. Njooni tuzungumze. Njooni tujadiliane. Wasiliana na viongozi wa chadema Marekani kwa maelekezo zaidi.
—
ZZK
Songa mbele kamanda Mbowe Waeleze ukweli. Tuko pamoja katika kupigania Haki ya Mtanzania.
Jacob Msangi
May 26, 2012 at 11:03 AM
Hi, please float the idea of a diasporea bond.
The Great!
May 26, 2012 at 12:03 PM
Nakutakia kila la kheri na CDM izidi songa mbele. Watanzania tunaona juhudi zenu, hivi sasa yale magamba yanadondoka yenyewe yaking’aza magwanda…!! Hadi kufikia 2015 tutashudia mlundikano wa magamba yakiuzwa kwenye mitumba. (Tz Magharibi).
Stanley Phiri
May 27, 2012 at 12:54 AM
safi sana ndugu zitto na viongozi wote wa chadema kwa kupambana kuweka huru ndani na nje ya nchi,tupo pamoja
Dickson Minde
May 27, 2012 at 11:35 AM
Kaka Zitto kwa kweli wewe ni tegemeo la kizazi hiki, ni dira na Mwanga wa vijana si tu wapenda siasa bali wote wanapata nguvu ya uthubutu katika sehemu zao! God bless you na pia nakutakia kila lakheri!
Paxman
May 27, 2012 at 11:39 AM
Hongera sana kwa kuongea nao kitaifa zaidi
Hansen Nasli
May 28, 2012 at 3:02 AM
jamani wazalendo wa nchi hii tunawatakia safari njema mungu wetu awtangulie katika kufikisha habari njema kwa watanzania wenzetu waishio marekani nyie ni wa kombozi wetu hongereni sanaaaaaaaaaaaaaa
RICKY KABEZI
May 28, 2012 at 1:31 PM
Ni mfumo wa uongozi ndo maana tunawatuma nyinyi wawakilishi wetu, hivyo basi mnapokua mkifanya yote haya mjue kua tuko nyuma yenu, nyinyi mbele sisi nyuma. Pamoja sana katika kulijenga taifa letu pamoja, never loose hope.TOGETHER AS ONE!!!!!!!!!!!!!!!
GEOFREY ABOKE
May 30, 2012 at 10:13 AM
Jaani huku mtwara mmbo bado sio mazuri abisa coz mwamko wa ksias ndio tatizo
andreabarnabas
June 1, 2012 at 12:08 PM
We wish CDM na viongozi wake all the best katika kuikomboa tanzania na watanzania kwa ujumla, naomba CDM ifanye kila liwezekanalo mfike na Morogoro vijijini jamani tunataka mabadiliko, tusaidieni
Joyce John
June 4, 2012 at 12:56 PM
California mutakuja lini,nataka uwanachama.
Erick miky
July 17, 2012 at 7:44 AM
Ninataka kutoa salute kwa mtiririko mzuri wa sera na vision ynu ya taifa ambayo watanzania wanahamu nayo kipekee mm ni mfuasi mzuri xana wa hekima na busara za kijana john mnyka ni kijana anayefaa ktk ngaz za juu za chama .nawakilisha ahsanteni.
Emanuel p mushi
October 8, 2012 at 2:35 PM