Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Benki Kuu: Hazina ya Taifa imekauka?

with 35 comments

 Zitto Kabwe, Mb.

Benki Kuu ya Taifa lolote ndio taasisi pekee yenye takwimu zote nyeti na za uhakika zinazohusu uchumi wa Taifa hilo. Katika tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania eneo la Machapisho kuna Taarifa nyeti sana mbili, Mapitio ya Uchumi ya Mwezi (Monthly Economic Review) inayotoka kila Mwezi katika Mwaka na Mapitio ya Uchumi ya Robo Mwaka (Quarterly Economic Bulletin). Taarifa hizi hutoa taarifa kuhusu masuala yote muhimu yanayohusu Uchumi wa Jamhuri ya Muungano na Uchumi wa Zanzibar ikiwemo taarifa za Mfumuko wa Bei, Mapato na Matumizi ya Serikali, Mwenendo wa Biashara ya Kimataifa na Deni la Taifa.

Ukienda kwenye tovuti ya Benki Kuu leo utakuta Taarifa hizi. Lakini Taarifa hizi zimeishia Desemba mwaka 2011 zikitaarifu masuala ya Uchumi ya Mwezi Novemba na robo ya mwaka inayoishia Desemba. Ukitaka kujua Bajeti ya Serikali na mwenendo wake hutapata taarifa za sasa bali za Mwezi Novemba mwaka 2011, miezi sita nyuma. Huu sio utendaji uliotukuka. Hii ni kuficha taarifa kwa wananchi. Taarifa zinafichwa ili iwe nini? Nani anafaidika na kufichwa kwa taarifa muhimu kama hizi?

Kuna tetesi kwamba Hazina ya Taifa (Hifadhi ya Fedha za kigeni – foreign reserve) inakauka, kwamba tuna hifadhi ya kuagiza bidhaa nje kwa mwezi mmoja tu. Niliposikia tetesi hizi sikuamini. Nilipoenda katika tovuti ya Benki Kuu ili kuweza kuwa na habari rasmi (authoritative) nimekuta takwimu za Novemba 2011.

Takwimu ya Mfumuko wa Bei iliyoko kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania ni ya mwezi Novemba mwaka 2011!

Ukitaka kujua mwenendo wa Bajeti ya Serikali kama makusanyo ya Kodi na Matumizi utapata Taarifa ya Mwezi Novemba mwaka 2011.

Ukitaka kujua manunuzi ya Mafuta (fuel imports) kwa miezi 3 ya mwanzo ya mwaka 2012 ili kuweza kuona namna Umeme wa dharura umeathiri urari wetu wa Biashara ya Nje hupati taarifa hiyo katika tovuti ya Benki Kuu.

Taarifa zinafichwa.

Ndio. Zinafichwa tena makusudi maana taarifa hizi zipo Benki Kuu. Huu ni uzembe maana Nchi inawalipa wafanyakazi wa Benki Kuu mishahara minono ili wafanye kazi hizi. Benki Kuu pia imetoa zabuni kwa Kampuni Binafsi kuchapisha Taarifa hizi. Kama Taarifa hazitoki kwa wakati ni wizi. Wizi ambao haupaswi kufumbiwa macho.

Benki Kuu ya Tanzania ipo miezi Sita nyuma. Aibu kubwa sana.

Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano akihakikishia mataifa duniani kuhusu uwazi Serikalini (#OGP), Taasisi kubwa kama Benki Kuu inaficha Taarifa ambazo ni nyeti kwa wananchi na muhimu kwa wafuatiliaji wa sera za Serikali. Rais wa nchi anaongea Buluu, Gavana wa Benki Kuu anasimamia Kijani!

Inaudhi na kukera sana kwenda kwenye tovuti ya Benki Kuu na kukuta taarifa za miezi Sita iliyopita. Benki Kuu hamstahili kuitwa Benki Kuu, labda benki kuu kuu. Rekebisheni jambo hili haraka sana maana kuficha taarifa kwa Umma ni ufisadi. Haki ya kupata taarifa ni haki ya msingi katika Katiba yetu.  Hatutaki kushtukizwa na kuambiwa Hazina ya Taifa imekauka.

Prof. Ndulu hakikisha Taarifa ya Mapitio ya Uchumi wa kila Mwezi imewekwa kwenye tovuti kwa muda mwafaka. Ifikapo mwisho wa Wiki inayoanzia Jumatatu Mei 14, tovuti ya Benki Kuu iwe na Taarifa za miezi yote (Desemba, Januari, Februari, Machi na Aprili). Taarifa hizi ni muhimu ili nasi tutekeleze majukumu yetu ya Kikatiba kama Wabunge, Mawaziri vivuli na Wananchi wa Tanzania.

35 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Tunashukuru sana kama zito kuwa unatufichulia hawa mafisadi upuuzi wanaoufanya kwa mali za uma

  phinias robart

  May 13, 2012 at 1:49 PM

  • BOT ni taasisi. Bila shaka ina mahali katika utawala wa nchi inapowajibika. Taarifa yoyote muhimu, isipowekwa mahaliinapotakiwa kuwepo haina maana haipo.Yawezekana ipo mahali pengine. Tuidai.Tunaidai kwa sababu tunataka kuitumia kutafakali na kuchambua mwenendo wa uchumi wetu. Who knowns? Yawezekana ni nzuri. Lakini hata ikiwa nzuri pia tuijue ili tuwapongeze watenda kazi. Lakini pia ikiwa mbaya dawa sio kuificha kwa maana mficha maradhi kilio humuumbua lakini pia mficha uch hazai.
   Ikiwa wataalamu wa kuanda taarifa hii hawakuiandaa, maana yake hawawajibiki kwa kazi waliyoajiwa kwayo. Wanapaswa kuwajibishwa kwa kosa hili. Uwajibikaji sio kwa mawaziri tu, ni kwa kila mtumishi wa umma.Kama hawawajibiki anayewasimamia anapaswa kuwajibika.
   Nisingependa sana kuamini kuwa taarifa inafichwa kwa sababu hakuna mantiki ya kufanya hivyo. Uchumi wa Taifa sio wa Prof. Ndulu au wa Raisi Kikwete, ni wa Watanzania wote. Mtu akificha kwa kudhani kuwa ni wake binafsi atakuwa amepotoka. Uchumi haujengwi na mtu mmoja au kikundi cha watu fulani tu unajengwa na watanzania wote hivyo ni busara wote waujua kupitia takwimu hizi ili wasaidie kuujenga kwa kutoa mawazo mbadala.Ikiwa fikra za Raisi au Gavana zimefikia ukomo, haziwezi tene kutusaidia, wapo wasomi wengi tu, watatoa mawazo ya kusaidiana na mabovu yaliyopo ili kuleta ufanisi zaidi. Baadaye uchumi ukikuwa utanufaisha wote wakiwemo wabovu.
   Nilikwisha sema kuwa Raisi Kikwete si muwazi kama watu wanavyotaka kupotoshwa na yeye mwenyewe, ni msiri ila akibanwa ni mwoga. Abanwa kwa hoja. Ataeleza takwimu hizo ziko wapi. Lakini sio aeleze tu takwimu ziko wapi lakini atuambie piakwa nini alikuwa haonyeshi kwa wakati huku watumishi wa kitengo wakiendelea kupata mishahara yao kama kawaida pamoja na marupurupu bila kukosa. Kinachosikitisha zaidi wameaajiri Consultancy wa kufanya kazi hiyo, sasa hao wataalamu wa BOT wanafanya nini?

   a

   May 14, 2012 at 12:10 PM

 2. Unajua sasa nadhani ni wakati serikali ijipange kila sekta sio kwa mawaziri tu au wakuu wa mikoa au wilaya na wakurugenzi bali mfumo mzima wa utekelezaji wa majukumu yake. Taasisi nyingi za kitaifa hazifanyi kazi kwa maslahi ya mtanzania bali kwaaji ya wakubwa wachache wenye kuficha mazambi yao kwa mwamvuli wa uongozi.Mh. Zitto unasimamia kamati ya bunge kuhusu mashirika ya umma nadhani mnahaja ya kuangalia utendaji wa haya mashirika upya!

  Mollel

  May 13, 2012 at 1:51 PM

 3. tunakupongeza sana kamanda wetu daima tukopamoja nawe

  Daudi masayi

  May 13, 2012 at 2:20 PM

 4. Waswahili wanasema ukweli unauma lakini na wananchi nasi tunataka kuona benki kuu wanatuwekea ukweli hata kama wataumia. Hizo taarifa ni muhimu mno tunakutakia kila la heri kwa kuwastua wafanyakazi wawajibike. Lakini kesho na keshokutwa nani atakuwa mtetezi wa sisi wanyonge? Jamani tuamke wote wakati ni huu wa mapambano. Asanteni na siku njema.

  Mahoza

  May 13, 2012 at 2:42 PM

 5. Mh.Zitto suala zito kama hili tunakuomba wewe na chama chako mliweke hadharani ili hata watanzania wasio na access ya mtandao wa internet waweze kufahamishwa

  Juma

  May 13, 2012 at 3:35 PM

 6. tatizo bot wanaajiriana kwa kujuana sana hawacheki saana qualification chamsingi unamjua nani na wapi. wapo kweli wenye sifa lkn pia ambao hawana sifa na wanaajiriwa huko wapo. kingene kwenye katiba mpya raisi asimchague gavana wa bot kwani atmlinda raisi na chama chake kwa vyovyote vile. BOT ni chombo muhimu sana kwa sera na maendeleo ya taifa lolote lile duniani.

  allen

  May 13, 2012 at 4:12 PM

 7. Asante sana kaka Zitto kwa umakini wako mkubwa, nani angejua yote haya,mweee!

  Simon Mwambagi

  May 13, 2012 at 4:45 PM

  • Hakika ni lazima watanzania wanaofuatilia masuala mbalimbali yanayohusu uchumi wa taifa letu ni muhimu kujua nini kinaendelea kwa kipata taarifa kwa wakati. taarifa zilizochelewa thamani yake inakuwa ndogo. Nakupongeza bro Zitto kwa taarifa hizi. mie mwenyewe nasoma mipango ya maendeleo hivyo umenifungua kichwa ili kila mwezi nifuatiliaa hali zikoje katika uchumi wa taifa letu. Inshaallah Allah akuongezee nguvu,busara na hekima katika kupigania haki za wanyonge.

   Hassan Kahungo

   May 13, 2012 at 10:03 PM

 8. Safi sn.. Kwanin usigombee Uraisi?

  Batondekwa kalegele

  May 13, 2012 at 5:15 PM

 9. Safi sana Zitto lazima tuwa wajibishe hawa wezi kula mishahala ya bure wakati hawa tekelezi majukumu yao ya muhimu.

  Salum

  May 13, 2012 at 6:02 PM

 10. That’s real shame and it’s make people untrustworthy with government Omg no comments on this but atlast you have seen this mr Mp

  Collins

  May 13, 2012 at 6:18 PM

 11. kwanza nianze na kuku pongeza kwa kazi nzuri unayo ifanya haya yote ninge yajuajehaya yote sintochoka kuingia kwenye mtando.

  Theofy kagete

  May 13, 2012 at 8:16 PM

 12. Hakika hili ni jambo la kuhuzunisha na linatia mashaka na kuacha maswali mengi kwa wananchi wa kawaida wa taifa hili. Mimi siamini kama taasisi hii inaweza kuwa na ujasiri wa kutoweka taarifa hizi muhimu pasipo baraka ya kiongozi wa juu wa taifa letu.

  Kama sivyo kwa nini hajawawajibisha watendaji wa taasisi hii kubwa na muhimu wa taifa letu. Taifa lolote linlaloendeshwa kwa usiri mkubwa bila shaka lina mambo ya kuficha na hivi sivyo namna ya kuendesha utawala bora. Hivi takwimu za kwamba Tanzania ni kinara wa utawala bora anachapisha nani? Wapi ambapo tumekidhi utawala bora?

  Thadei Maternus Mapunda

  May 13, 2012 at 8:48 PM

 13. […] kabwe na majibu ya mwigulu wa ccm MJADALA WA HAZINA YA TAIFA ZITTO KABWE VS MWIGULU NCHEMBA Benki Kuu: Hazina ya Taifa imekauka?by zittokabwe Benki Kuu ya Taifa lolote ndio taasisi pekee yenye takwimu zote nyeti na za […]

 14. Jamani nchi imekwisha saa ya ukombozi ni sasa, isipoondoka ccm maendeleo tutayasikia kwa masikio

  Bakari hassan

  May 13, 2012 at 10:55 PM

  • asante sana kakaZitto kwa mapendekezo yako na mungu Akubariki na akujalie afya njema

   tonny

   May 14, 2012 at 8:06 AM

 15. Tatizo sio bank kuu yetu kabsa kwani yetu haiwezi ikawa sawa na ya uingerza.
  Ukiangalia ya almost yote ndo hayo hayo especially England,Greece,portugal, Italy na nk.
  Problem kubwa hapa ni wOrld bank,IMF, America na allies wake. The issue hapa ni new world order ndo Iko in actions. Nchi ziwe brokeass ziwe dependent ile the issue iwe implemented. Huku

  Amin

  May 14, 2012 at 12:08 AM

 16. Mh! Inauma sana, ila muda sasa umewadia tutajua nani m-babe kati yao na sisi.

  Musa lionga

  May 14, 2012 at 12:20 AM

 17. Banki kuu ya TAnzania ndo hivyo. Mi nadhani sio kulaumu kwa kuangalia dunia Iko vipi?
  Tu angelie hio dunia ya kwanza mwanzo ndo tupate sababu ya kulaumu.
  Ni lazima Tujue underlying cause inayosababisha haya yote.na sio kuangalia immediate tu afu uje na lawama. Kamwe solution haitopatikana
  The British banking crisis continues
  As the British banking crisis continues, this episode of The Big Story explores the latest bad news from the banking industry for the ordinary British people.

  Britain’s banking industry is in crisis. Lloyds and RBS were bailed out by the British taxpayers at a cost of billions – with that cost that continues to rise.

  The new figures of billions in losses coupled with bonuses will be a bitter pill to swallow for the millions who had to use their hard-earned tax dollars to bail out a system many saw as bankrupted.

  Now with billions hemorrhaging from Lloyds and RBS and thousands of backroom jobs facing the chop, when will the Coalition stand up and challenge the financial service industry?

  As Britain faces a double-dip recession, low growth figures point to little good news on the horizon, what will the banking sector have to do to face real reform from a government which seems enamored with financial sector?

  During the program, the UK government’s inaction will be examined and the alternatives for a system which seems fundamentally unsustainable. It also asks if the 2008 crash scenario could happen again and what reform changes are needed.Naomba tusome hii habari

  Amin

  May 14, 2012 at 1:22 AM

 18. huyu ndo chadema nzima,wengine wote vilaza,HUYU NI KIONGOZI,HAIJALISHI CHAMA ANACHOTOKA,HUYU NI RAISI WANGU WA BAADAYE,THANK YOU MR PRESIDENT

  sagana

  May 14, 2012 at 9:39 AM

 19. […] my statement here in Kiswahili. https://zittokabwe.wordpress.com/2012/05/13/benki-kuu-hazina-ya-taifa-imekauka/. Find a comment to my statement in English at Swahili Street here. […]

 20. Kwa kweli ni wajibu wetu kufatilia kwa ukaribu utekelezaji wa sera za serikali hasa kwenye upande wa uchumi. Tunaoumia ni wananchi maskini. Mh. Zitto endelea kutupa ukweli.

  musa

  May 14, 2012 at 11:21 AM

 21. Ni aibu kwa taasisi nyeti kama BOT kufanya kazi kienyeji hivyo kama sio kuficha kimakusudi. Huwezi amini mfuko wa bei ulivyofika leo. Waweke aibu yao hadharani. Sidhani ni kosa l webmasters wao, kuna hila. Mbona zile za ‘Exchange rates’ wana update kila siku?

  Timbuktu

  May 14, 2012 at 11:30 AM

 22. Big up kwa ufuatiliaji huo na kuwakumbusha BOT wajibu wao mkuu

  David Bassu

  May 14, 2012 at 11:37 AM

  • Mh. Zito naiheshimu na kuvutiwa na michango yako, lakini kwa hili naona kidogo nafasi uliolipa sio.
   Bahati nzuri suala hili limekuja wakati ambapo namalizia utafiti wangu juu ya utendaji wa taasisi hii nyeti kabisa katika nchi yeyote duniani.
   Kwanza ninachoweza kusema Benki Kuu unkiacha vyuo vikuu vya UDSM, Mzumbe na Sokoine ndio Taasisi iliosheheni Kundi kubwa la wanataaluma wa viwango vya juu kabisa wakiwemo mdaktari wa kitaaluma (PHD’S) zinazokaribia 20.

   Taasisi hii vile vile imejenga heshima kubwa ndani na nje ya nchi kwa kutoa wataalamu mbali mbali kwa kuazimwa au kwa kupelekwa moja kwa moja . Viongozi kadhaa wa Taasisi za fedha ni zao la Taasisi hii wakiwemo Dr. charles Kimei (CRDB), Charles Singili (Azania), P. Noni (TIB), R.Bade aliekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Barclays na wengine wengi hasa wataalamu na maafisa wa ngazi za juu.

   Katika utafiti wangu nimegundua kwamba Benki Kuu pamoja na wataalamu vile vile imezalisha wanasiasa mahiri sana miongoni mwao Ni Bw. Edwin Mtei,Bw. Daniel Yona,Bw.Siraju Kaboyonga,Bw. James Lembeli,Bi. Vicky Kamata, Bw. Freeman Mbowe,Bw. Mwigulu Nchemba , Bw. Charles Kitwanga, Bw. William Mgimwa, Bw. Bob Nyanga Makani na wengine wengi sana.

   Kabla ya kuanza utafiti wangu sikujuwa kwamba taasisi hii inamajukumu mazito sana, hivyo nilijaribu kuipitia Sheria yake ya mwaka 2006 na kujaribu angalau kuowanisha na hali halisi , nimegundua kwamba wataalamu hawa wanayo haki ya kuenziwa na kulindwa vile vile majukumu yao ni nyeti , muhimu na yanatija kubwa kwa uchumi wa Taifa.Mfano unapozungumzia Akiba ya fedha za kigeni ni eneo moja tu kati ya mengi ambapo unaweza kuona utaalamu na umahiri wa wataalamu wetu hawa katika kutafuta masoko bora ya uwekezaji wa fedha usiku na mchana na hatimae kutunisha mfuko huo wa Nchi.

   Nimepitia Balance Sheet ya Taasisi hii kwa mwaka wa Fedha uliopita na kugundua mchango Mkubwa kwa maana ya gawiwo kwa serikali na kumbu kumbu zinaonyesha haijatokea katika historia.

   Utafiti wangu ulishangazwa pia kuona Taasisi hii pia ni miongoni mwa zile ambazo wafanyakazi wake wanahama kwa wingi kwenda kutafuta maisha mazuri zaidi katika taasisi mbali mbali za nje na ndani ya nchi , nimegunduwa kwamba wapo wafanyakazi waliohamia vyuo na Taasisi za elimu ya juu kama wakufunzi na watafiti wapo waliotimkia kwenye mashirika ya Kimataifa na wengine wengi wameazimwa kwenye Taasisi za Kiserikali na Kimataifa.Matukio hayo yamejenga Taswira kwamba taasisi hii kweli ina mafao mazuri lakini sio kwamba bora saana kuliko taasis nyengine zilizopo tunapozungumzia maslahi.Lakini kwa upande mwengine niliona kuna umuhimu Mkubwa kuwashauri wanasiasa wasizitumie Taasisi zenye majukumu ya aina hii kama njia za kuinuwa majina yao lakini katika njia ambayo inabeza na kukebehi ufanisi uliopatikana katika masuala ya msingi kwa kutumia kasoro ndogo ndogo zilizopo.

   Mayunga

   May 14, 2012 at 3:59 PM

 23. Hongera kaka kwa kufichua uozo huu cjui hii itaendeshwa hivi mpaka lini na sijui kama hawa viongoz wetu wana uchungu na nchi yao pamoja na wananchi wanaowaongoza hakika hili linanipa mashaka kidogo juu na aina ya utendaji wao.

  straton

  May 14, 2012 at 12:21 PM

 24. jamani hiii ni Benkik kuu kuu kuu jamani, watendaji wote wako chali wameuchapa usingizi na mvua na baridi kama hii. LKN tunawaambia wajifunike vizuri hayo habranketi yao maana sie akina mbu tupo tunawachunga, AIBU YA MWAKA YA TAIFA. Mh. kazi yako ni njema sana, Mungu akubariki na akutie nguvu akuepushe na woga, piga kazi mimi niko nyuma yako nafuata mwelekeo wako, naamin pia Mungu atakusaidia.

  lucy

  May 14, 2012 at 12:55 PM

 25. Tunaitaji vijana kama Zitto, niwepesi wakufutilia mambo na hapo BOT ni taasisi nyeti mnoo wanatakiwa vijana active. i appreciate u much bro!

  Raphael

  May 14, 2012 at 3:32 PM

 26. hao ndo walewale wameweka taaluma zao rehani ili kuokoa serikari iliokwama.

  kabolile

  May 14, 2012 at 8:26 PM

 27. kaka endelea kuzungusha gurudumu la M4C na safari naitakia baraka na neema tele. kazi zenu na ziheshimiwe mbele za Mwenye Enzi Mungu na hizi ni harakati mpya za ukombozi wa sasa

  Sakaya

  May 14, 2012 at 9:53 PM

 28. Hakika umenifumbua macho.Asante na endelea kutuelimisha

  Gelarld simfukwe

  May 15, 2012 at 9:24 AM

 29. Ni kweli bwana z.kabwe ni jambo jema umefanya vyema kuwaambia ukweli, sio wanajazana mule bot wanafanya utumbo na mkulo wao, ni haki ye2 wananchi watufahamishe tujue, sio wanaweka taarifa kuukuu baada ya ya kuweka upcoming events info services news updated , na thaman ya pesa na uchumi vinazid kudorola nchi imewash!nda waseme, ahsante

  Japhet kyando

  May 16, 2012 at 7:47 AM

 30. Nimefurahi sana kwa jinsi unavyokua mwepesi wa kufuatilia mambo mengi ambayo ni nyeti sana kwa maendeleo ya taifa letu,haswa swala zima la gesi asilia na petroleum kwa jinsi lilivyo wekwa kinamna ya kuficha ufisadi kua ni swala la muungano ama ni jambo liliko kwenye mambo ya muungano wakati waanga wa nishati hizo hawanufaiki chochote asilani.
  Hakikkisha jambo hilo linapata ufumbuzi katika bunge lijalo nina kuaminia bro…. Bwana awe nawe,nitakuombea kweli.maana uwezi jua kua Mungu alikuchagua kua mwenyeti wa bunge wa kamati ya maswala ya mashirika ya umma kwa ajili hii ili taifa letu liondikane na umaskini na mfumo dume wa utawala wa kifisadi unaongozwa na watu wachache wasio wazalendo.

  Pili nashukuru kupata kujua kua swala la kupata taarifa za shughuli za benk kuu ni jambo muhim kwa swala zima la maendeleo ya kiuchumi katika nchi yetu..wabane baba tupata kujua haki zetu za msingi……
  SONGA MBELEEEEE………….

  ELIAS

  May 29, 2012 at 12:26 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: